Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

DKT NCHIMBI ASHAURI WAHADZABE WAPEWE AJIRA ZA MUDA KUPITIA TASAF

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ameshauri Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) uanzishe kazi za ajira za muda, kwa walengwa wa Mpango huo kutoka jamii ya Wahadzabe waliopo Wilayani Mkalama ili uwasaidie kuinua uchumi wao.

Dkt Nchimbi ametoa ushauri huo mara baada ya kutembela kijiji cha Singa Wilayani Mkalama na kuona bwawa litakalotumika kuhifandhi maji ya mvua kwa ajili ya shughuli mbalimbali lililojengwa na walengwa wa Tasaf Kijijini hapo kisha kutembelea kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza Wilayani humo aliposhuhudia malipo ya walengwa wa kihadzabe wa Mpango wa Tasaf.

Ameeleza kuwa jamii ya wahadzabe hawana mradi unaohusisha kazi za ajira za muda ambazo zimekuwa zikisaidia katika kuongeza kipato, kuwafundisha thamani ya kazi pamoja na kutekeleza miradi ambayo imekuwa ikisaidia jamii nzima kama vile mabwawa na barabara.

“Nashauri TASAF kabla ya msimu huu wa mvua kuisha muwaletee na hawa wahadzabe mradi wa ajira za muda kama ambavyo walengwa wa vijiji vingine wamekuwa wakifanya kazi hizo na zimekuwa zikichangia maendeleo kwa vijiji vyao”, ameeleza na kuongeza kuwa,

“Miradi ya ajira za muda zitawafundisha Wahadzabe kujituma kufanya kazi ambazo zinachangia maendeleo ya jamii huku kazi hizi zikiwa kama darasa la wao kujifunza kwa vitendo kuwa kama anaweza kwa mfano kushiriki kujenga bwawa basi anaweza kufanya jambo kubwa katika familia au maisha yake”, amesisitiza Dkt Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na Wahadzabe waliokuwa wakijiandaa kupokea fedha kutoka Mpango wa Tasaf katika kijiji cha Munguli Wilayani Mkalama, Dkt Nchimbi amewatahadharisha kutofanya matumizi mabaya ya fedha hizo.
Walengwa wa Tasaf wa kijiji cha Singa Wilayani Mkalama wakimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (hayupo pichani) alipowatembelea kushuhudia ujenzi wa bwawa walilolijenga katika mpango wa ajira za muda za Tasaf.
Bwawa lililopo katika kijiji cha Singa Wilayani Mkalama lililojengwa na walengwa 246 wa Tasaf katika mpango wa ajira za muda, bwawa hilo linaujazo wa mita 5777.6 ambalo litasaidia upatikanaji wa maji na uanzishwaji wa kilimo cha umwagiliaji, Dkt Nchimbi ameagiza halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kuweka miundombinu ya kunyweshea maji mifugo kutoka katika bwawa hilo.


MIAKA 56 YA UHURU:RAIS MAGUFULI AELEZA MAFANIKIO YA SERIKALI.

WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO

$
0
0
Na Said Mwinshehe, Globu ya Jamiii

MTOTO wa kwanza wa mwanamuziki Nguza Vicking, Nguza Mbangu amesema Mungu ameonyesha ukuu wake na kuifanya familia yao iliyokuwa kwenye kilio cha muda mrefu sasa kuwa kwenye shangwe. 

 Nguza ambaye kwa sasa anajulikana kwa jina la Nabii Michael amesema hayo leo jijini Dar es Salaam nje ya gereza la Ukonga ambalo baba yake mzee Nguza alikuwa akitumikia kifungo cha maisha kabla ya Rais Dk. John Magufuli kumuachia kwa msamaha wa Rais baada ya kutangaza kusamehe wafunga 8157 akiwamo mwanamuziki huyo na mwanaye Papii Kocha.

Nguza Mbangu amesema kilichotokea ni mapenzi ya Mungu kwa kuonesha ukuu wake huku akimshukuru Rais kwa kutoa msamaha huo, amesema familia itatoa tamko rasmi baada ya Rais kumtoa mzee wao kifungoni.  

 "Tutatoa tamko la familia kwa kilichotokea ila niseme tunamshukuru Mungu kwa kuonesha ukuu wake. Pia tunamshukuru Rais kwa uamuzi wake" amesema. 

Naye mwanamuziki maarufu King Kikii aliyekuwa nje ya gereza hilo baada ya kupata taarifa za kuachiwa Nguza Viking amesema kuwa kilio cha muda mrefu ambacho watanzania wamelia tangu Nguza Viking awe jela hatimaye imekuwa shangwe. Amesema  baada ya tamko hilo Nguza Viking amepigwa butwaa kwani haamin kama yupo huru lakini furaha imechukua nafasi yake.

Wakati huohuo mtoto wa kike wa Nguza Viking, Monica amesema anamshukuru Rais Mguful kwa kumtoa jela baba yake na kuongeza sasa furaha imerejea nyumbani. 

Nje ya gereza la Ukonga mashabiki wa mwanamuziki huyo wamejitokeza kwa wingi ili kumuona baada ya kuwa huru. Mara kadhaa baadhi ya askari magereza walizuia watu kusimama nje ya gereza hilo lakini watu waliamua kupiga kambi kuanzia saa saba mchana hadi jioni hii.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi wakati akiwasili kuongoza  sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na Mama Mwanamema Shein kwenye sherehe hizo
 Marais Wastaafu Mhe Benjamin Mkapa na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Viongozi mbalimbali katika Jukwaa kuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017. Picha na Ikulu

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amekagua ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu-NBS mjini Dodoma na kutoa wito kwa wakandarasi wanaojenga miundombinu mbalimbali yakiwemo majengo kutumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Amesema hayo baada ya kushuhudia mkandarasi anayejenga jengo hilo Hainan International Ltd ya China, akitumia vifaa mbalimbali vya ujenzi vinavyopatikana hapa nchini zikiwemo mbao na vifaa vya umeme, hatua ambayo amesema inachangia kuwaongezea kipato wananchi.

Akizungumzia ujenzi huo, Dkt. Mpango amesema jengo hilo litatumika ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwakuwa litatumika kuchakata takwimu mbalimbali zitakazotumika katika kutunga sera na mipango mbalimbali ya kuendeleza nchi.

“Huwezi kupanga mipango yoyote bila kuwa na takwimu nzuri na bora, hapa ndipo vile “vichwa” vyetu vya takwimu nchini vitachakata takwimu hizo ndipo zitumike katika kutunga sera bora kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu” Alisistiza Dkt. Mpango
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), akitoa maelekezo wakati alipokagua ujenzi wa Jengo la ghorofa 5 la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa na kushoto kwake ni Mhandisi Mshauri Bw. Abdulkarim Msuya.
 Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya (kulia) akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
 Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa, (wa tano kulia) mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

THBUB yampongeza Rais kwa kuwafutia watu 61 adhabu ya kifo

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga kwa niaba ya Tume na Wafanyakazi wote wa THBUB anachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kufuta adhabu ya kifo kwa watu 61 waliokuwa magereza mbalimbali nchini, wakisubiri utekelezaji wa adhabu ya kifo dhidi yao.

Tume inampongeza sana Mhe. Rais kwa uamuzi wake huo kwani unaendana na Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Na. 62/149 la tarehe 18 Desemba 2007 linalozitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuta au kusimamisha utekelezaji wa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala.

Tume inatambua kwamba, kama alivyosema Mhe. Rais, msamaha huu haufuti adhabu ya kifo katika sheria za nchini.

Hivyo, kutokana na mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 130(1) (g), Tume inapenda kuchukua nafasi hii kuishauri Serikali kuona uwezekano wa kufuta adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala, ili iendane na Azimio la Umoja wa Mataifa  lililotajwa hapo juu.

Pia, Tume inaisihi Serikali, hususan Idara yake ya Ustawi wa Jamii kuwasaidia, na Wananchi kwa ujumla kuwapokea, wale wote waliopewa msamaha ili waweza kuendelea na maisha yao kama raia wema katika jamii.

Imetolewa na:
(SIGNED)
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Desemba 9, 2017

MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 56 YA UHURU WA TANZANIA BARA, TAREHE 9 DISEMBA, 2017

$
0
0
Katika kuadhimisha Miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe      9 Disemba, 2017 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-


(i)           Wafungwa wote wapunguziwe moja ya sita (1/6) ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58, isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2(i – xxi).


(ii)         Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, Kifua kikuu (TB) na Saratani (Cancer) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa hawa wathibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


(iii)       Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi.  Umri huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


(iv)        Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.


(v)          Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability). Ulemavu huo uthibitishwe na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


2.      Aidha, Msamaha wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-


(i)                Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa au kwa makosa ya kujaribu kuua (attempt to murder).


(ii)              Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.


(iii)            Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.


(iv)             Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile cocaine, heroin, bhangi n.k.


(v)               Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na uombaji na upokeaji au utoaji rushwa.


(vi)             Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo (robbery with violence, armed robbery and attempted robbery).


(vii)           Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali (fire arms, ammunitions and explosives).


(viii)         Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti, ukatili kwa watoto au kujaribu kutenda makosa hayo.


(ix)            Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.


(x)              Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari na pikipiki, uharibifu wa miundombinu au kujaribu kutenda makosa hayo.


(xi)            Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole (Act. No. 25/1994) na Sheria ya Huduma kwa Jamii (Act. No. 6/2002).


(xii)          Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao na kuhujumu uchumi.


(xiii)        Wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo na Msamaha wa Mhe. Rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.


(xiv)         Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo.


(xv)           Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, kupoka na kufanya biashara ya binadamu (Human Trafficking).


(xvi)         Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.


(xvii)       Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na nyara za Serikali na ujangili (poachers).


(xviii)     Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya wizi/ubadhirifu wa fedha za Serikali.


(xix)         Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali.


(xx)           Wafungwa walioingia gerezani baada ya tarehe 30/10/2017.


(xxi)         Wafungwa waliowahi kufungwa gerezani.


3.      Wafungwa 8,157 watafaidika na msamaha huu ambapo 1,828 wataachiliwa huru tarehe 9 Disemba, 2017 na 6,329 watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu. Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mujibu wa  Ibara ya  45(1) (d) ya  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa  Mamlaka  Rais wa Jamhuri ya Muungano    wa Tanzania  kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kufuta adhabu yote. 

Kwa kutumia Mamlaka aliyo nayo amewasamehe wafungwa  wengine 63  kati yao wafungwa 61 ni wale waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa, waliokuwa na  umri mkubwa  na waliokaa gerezani muda mrefu. Na pia amewasamehe wafungwa wengine wawili waliokuwa wakitumikia kifungo cha maisha ambao ni  Nguza Viking(BABU SEA) na Johnson Nguza. Hivyo kwa ujumla amewasamehe wafungwa 8220.


imetolewa na

Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu)



KATIBU MKUU

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
09/12/2017

BABU SEYA, PAPII KOCHA WATOKA GEREZANI JIONI HII

$
0
0
Mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) pamoja na Mwanaye Papii Kocha wakipunga mikono muda huu baada ya kutoka katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam wakokuwa wanatumikia kifungo cha maisha na sasa wameachiwa huru kwa msamaha wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alioutoa leo huko Mjini Dodoma kulikofanyika Maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Babu Seya na Mwanawe ni sehemu ya wafungwa 8157 walipata msamaha wa Rais.
Babu Seya akitoka gerezani jioni hii.
Baadhi ya mashabiki wa wanamuzi wakiwa nje ya gereza la Ukonga Dar es Salaam wakimsubiri mwanamuziki Nguza Viking na mtoto wake Papi Kocha waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela na sasa wamepata msamaha. Picha na Said Mwinshehe, Globu ya Jamii.

SALAMU ZA MIAKA 56 YA UHURU KUTOKA PSPF

GAZETI LAKO PENDWA LA KISWAHILI LA HABARI LEO LABISHA HODI RWANDA KWA KISHINDO

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MKUTANO MKUU WA TISA WA UWT

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi waliochaguliwa kuongoza kwa kuzingatia Katiba, Kanuni za UWT, CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

Makamu wa Rais aliwasihi viongozi hao kuvunja makundi ya kampeni nwaliyokuwa nayo na kujenga Umoja na Mshikamano ndani ya Jumuiya na Chama.Makamu wa Rais alisisitiza kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na kwa uzalendo “Kushinda kuwa Kiongozi haina maana unajua yote, tuwe tayari kukosoana lakini tusisingiziane”

Makamu wa Rais aliwakumbusha Viongozi hao kuhakikisha Jumuiya inashiriki kikamilifu katika kuandaa mazingira mazuri ya ushindi wa CCM katika chaguzi za Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020.Makamu wa Rais alisema Viongozi waliochaguliwa wanajukumu kubwa la kujenga Jumuiya imara kwa kuitoa hapo ilipo na kuipeleka mbele ikiwa na kuongeza wanachama wapya kutoka katika makundi mbali mbali.

Mkutano Mkuu wa Tisa wa UWT ulifunguliwa jana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kufungwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo ulifanyika uchaguzi na Mhe. Gaudensia Kabaka alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake Tanzania na Bi. Thuwayba Kisasi alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akihutubia wakati wa kufunga mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka baada ya kutangazwa mshindi katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akimpongeza Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akiwapungia mkono wajumbe wakati wa kufunga mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka akihutuba baada ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea waliogombea nafasi ya Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

SERIKALI KUFANYA MAPITIO YA MIRADI YA MAJI KUANZIA MWAKA

$
0
0

Serikali imewaagiza Wahandisi wa maji kuhakikisha wanasimamia miradi ya sekta ya maji nchini inayozingatia thamani ya shilingi na yenye kuleta tija kwa Watanzania.

Akiongea katika ziara yake mkoani Arusha katika wilaya ya Longido Mhe. Joseph George Kakunda, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, amesema kumekuwepo na ufujaji wa fedha za katika Miradi ya maji nchini na mara nyingi imekuwa sio endelevu na yenye kuleta hasara kubwa kwa Taifa.

“Wahandisi hakikisheni mnasimamia utekelezaji wa miradi ya maji kwa thamani ya shilingi, wale wote wanaojenga miradi hiyo muwasimamie vizuri, fedha tunazozikopa hakikisheni mnazitumia vizuri, acheni kupokea rushwa, nataka kuona Wahandisi wanajenga mradi kwa maslai ya watu wa Longido ili kuondoa kero za maji, zingatieni taratibu, kanuni na sheria ili tupate tunachostahili” 

Mhe. Kakunda amewataka Watendaji na Wahandisi kufanya mapitio ya miradi ya maji nchini ili kuona miradi iliyotekelezwa kwa halali na pia ili iliyotekelezwa kwa wizi ionekane. “haiwezekani tangu tuanzishe Programu ya Maji Vijijini tumekwisha tumia zaidi ya shilingi trilioni 1.6lakini bado kila sehemu kuna shida ya majikwa nini kila mradi una maisha yake kama miaka 10, 15, 20, 25 hili haliwezekani, hatuwezi kwenda namna hiyo, mimi nitapendekekeza tufanya mapitio ya miradi yote ya maji iliyojengwa hasa kuanzia mwaka 2008. Kwanini watu wa kawaida wanajenga mradi mkubwa kutoka kwenye chanzo hadi hapa”

Akiwa kijijini Elondeka, Mhe. Kakunda amepongeza hatua zilizofikiwa za Mradi wa maji unaotekelezwa na Mradi wa Tabia nchi (DCFP)ambao umegharimu kidogo cha fedha shilingi milioni 36 na kushauri wananchi kuulinda siku zote. Pia alikagua mradi wa maji unaotekelezwa na Halmashauri ya wilaya Longido ambao bado haujakamilika.

Akisoma taarifa ya mradi mbelel ya Mheshimiwa Naibu Waziri Kakunda, Mtesigwa Missana ambaye ni Afisa Tarafa Longido amesema kuongezeka kwa kutotabilika kwa tabia ya hali ya hewa yanazidisha changamoto kama vile kubadilisha mtindo wa maisha ya wananchi.

Aidha, Mhe. Kakunda amewaasa wananchi kuulinda mradi wao waliouchagua wenyewe, “toeni ushirikiano kwa mradi huu kwa sababu mmeuchagua wenyewe, lindeni sana mradi huu ili uweze kuhudumia ninyi wenyewe na mifugo, mradi huu una faida kwenu ninyi, mifugo na wanyama wa porini”
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Arusha, wilaya ya Longido, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Haki kazi Catalyst wa mjini Arusha
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akitoa maelekezo kwa watendaji wa maji katika mradi wa maji wilayani Longido
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akikagua mradi wa maji wilayani Longido
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akipanda kwenye tanki la maji linalojengwa katika mradi wa maji wilayani Longido
Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Joseph G.Kakunda akipiga picha na akina mama na watoto wakati waziara yake ya kukagua mradi wa maji wilayani Longido.

Majina ya Wanajeshi 14 walifariki huko nchini Congo

$
0
0
1.Pte Mwichumu 12 kj 
2.Pte Hali Haji Ussi band coy 
3.Pte Hamad Mzee Kamna 12 kj 
4.Deogratius Kamili 101 
5.Juma Mossi 11 kj 
6.Paschal Misingo 11 kj 
7.Idd Abdala SMV 
8.Cpl Issa Khamis 111 
9.Pte Shaziri Nyandonde 83kj 
10.Pte Hamad Haji Bakari 101 
11.Sgt Makame Abdalah 101 
12.Pte Nassor Daud 12 kj 
13.Pte Saleh Said Mahembano 302 
14.Pte Vuai Mohammed 12 kj 

HATUNAO MPAKA SASA

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO DECEMBER 10,2017

MWENYEKITI WA CCM, RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA TISA WA UVCCM MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM , Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM) kabla ya kufungua mkutano wao wa Tisa unaofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM , Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ndg. Abdulrahman Kinana, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa pamoja Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa, Mboni Mhita wakiimba moja ya nyimbo za Chama hicho, kabla ya kufungua mkutano wa Tisa wa UVCCM unaofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM , Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ndg. Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa Tisa wa UVCCM unaofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo. Katikati ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akifuatiwa na Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wajumbe wa mkutano tisa wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho unaofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM , Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteja jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa, Mboni Mhita.
Wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM) kabla ya kufungua mkutano wao wa Tisa unaofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo.

NUNUA LUKU KWA NJIA ULIYOZOEA BAADA YA MAREKEBISHO SASA MAMBO POA

$
0
0
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) 

Tunawataarifu Wateja wetu kuwa, hivi sasa mifumo ya LUKU inapatikana katika njia zote za manunuzi.

Wateja mnaweza kufanya manunuzi kwa kutumia njia zote.

Asanteni kwa ushirikiano wenu.


Mitandao ya Kijamii 


Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu 
Desemba 10, 2017

SALAMU ZA MIAKA 56 YA UHURU KUTOKA PSPF

NAIBU WAZIRI TAMISEMI,JOSEPH KAKUNDA AFURAHISHWA NA MIRADI YA KUWAWEZESHA WANANCHI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda(kushoto) akipanda ngazi kukagua mradi wa maji wilayani Longido,akiwa na Mkuu wa wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,Godfrey Chongolo. 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Longido(wa pili kulia) wakimsikiliza Mhandisi wa Maji wilayani Longido,Ramadhani Musiba(kushoto) utekelezaji wa miradi ya maji. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda akipanda ngazi kukagua mradi wa maji kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa wilayani Longido. 
Ujumbe wa Naibu Waziri wa Tamisemi,Joseph Kakunda pamoja na maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Longodo wakikagua moja ya miradi ya kuwawezesha wananchi kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi. 
Mhe Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakijumuika na wananchi kuimba wimbo wa kufurahia mradi wa maji.

Na Mwandishi Wetu,Arusha

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda amepongeza ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa katika mpango wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi katika wilaya za Longido,Monduli na Ngorongoro.

Mradi huo unaosimamiwa kwa pamoja na Ofisi ya Rais-Tamisemi,taasisi ya kimataifa ya maendeleo na mazingira(IIED) na Haki Kazi Catalyst unatarajiwa kuwanufaisha wananchi walio katika wilaya hizo tatu.

Akiwa katika Kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa alipongeza hatua iliyofikiwa ya kuwawezesha wananchi kupata maji safi kwaajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na mifugo yao ikizingatiwa wilaya ya Longido asilimia 95 ya wakazi wake ni wafugaji.

Amesema mkandarasi amekua mzalendo kwa kujenga miundombinu ya maji tenki pamoja eneo la kunyweshea mifugo kwa thamani ya Sh 36 milioni na kuonya wakandarasi wasio na uzalendo wanatekeleza miradi kwa gharama kubwa lakini inakua haina ufanisi.

Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo amesema wilaya yake ipo jumla ya miradi 14 inayofadhiliwa na IIED kwa lengo la kuwawezesha wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Naye Flora Assey ambaye ni mratibu wa mradi huo kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema lengo la mradi huo ni kuweka mfumo utakaowezesha upimaji wa kiutendaji katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Jiji la Dar es Salaam lapata tuzo kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka

$
0
0
JIJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017 kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.

Katika tuzo hiyo mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka huu. Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo na Jiji la New York nchini Marekani na Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo jijini hapa.

Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (wa pili kulia mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine huko Chicago nchini Marekani wakiwa wameshika tuzo zao.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies.

RAIS DKT. MAGUFULI ATIA SAINI NYARAKA ZA MSAMAHA WA WAFUNGWA 63 AMBAPO 61 WALIKUWA WAMEHUKUMIWA KUNYONGWA NA MAJINA MAWILI (2) YA WAFUNGWA WALIOKUWA WAMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini Nyaraka zenye majina ya Wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili ya Familia ya Nguza Viking (Babu Seya), na Johnson Nguza waliopata msahama wa Rais, katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiyahakiki kwa kuyasoma majina ya Wafungwa 63 waliopata msahama wa Rais kabla ya kutia saini Nyaraka hizo za Msamaha katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa akishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa mara baada ya kutia saini majina ya wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili ya Wafungwa Nguza Viking(Babu Seya), na Johnson Nguza waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images