Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110120 articles
Browse latest View live

VIJANA WA ZANZIBARA NA TANZANIA BARA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM KUANGALIA FURSA ZILIZOPO NCHINI

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

VIJANA wa Zanzibar na Tanzania Bara wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuliletea taifa maendeleo.

Katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark vijana hao wapatao 14 kwa niaba ya wenzao walijadiliana mambo mbalimbali na kuangalia fursa za maendeleo zilizopo nchini.

Kwa ujumla fursa zilizokuwa zimeangaliwa katika maeneo mbalimbali na wazo hilo limekuja baada ya baadhi yao kutembea nchi nzima Tanzania Visiwani na Tanzania Bara na kuziona hivyo wakaona ni vema kuunganisha nguvu ya pamoja kwa kuwashirikisha wenzao na kuona waanzie wapi.

"Tumetembea nchi nzima na kuona fursa mbalimbali tukaona ni vizuri vijana wa Zanzibar na Tanzania Bara tukutane tujadiliane na tuone ni fursa zipi tuzifanyie kazi kwa manufaa yetu kama vijana na taifa kwa ujumla" alisema mmoja wa vijana hao ambaye hakupenda kuingia kiundani zaidi kwa kuwa mchakato wa jambo hilo ndio kwanza upo jikoni.

Vijana kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuzifanyia kazi kwa ajili ya kulitetea taifa maendeleo. Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark jijini Dar es Salaam.
Majadiliano yakiendelea.
Msisitizo katika majadiliano hayo.


MEYA MWITA AHUDHURIA MKUTANO WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA ULIOANDALIWA NA UMOJA WA MATAIFA MJINI ADDIS ABABA

$
0
0
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameondoka Jijini hapa jana jioni kuelekea Addis Ababa, kuhudhuria mkutano wa kujadili changamoto zinazo wakabili viongozi wa serikali za mitaa.

Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Umoja wa Mataifa ambapo unalengo la kujadili na kutoa majibu ya changamoto ambazo wanakutana nazo viongozi wa serikali za mitaa wakiwepo Mameya wote.

Miongoni mwa changamoto ambazo zitajadiliwa katika mkutamo huo pamoja na mambo mengine ni suala la bajeti katika halmashauri na ukusaji wa mapato.Mbali na Mameya ,mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutoka Nchi mbalimbali.

Aidha Meya Mwita atazungumza na mkutano huo kuelezea changamoto zilizopo katika jiji la Dar es Salaam , namna ambavyo kwa asilimia kadhaa wameweza kuzitatua.Aidha katika mkutano huo ataeleza pia mafanikio yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam kupitia sekta mbalimbali za Maendeleo.

” Katika mkutano huo hatuta kuwa jiji la Dar es Salaam pekee ,ni Nchi mbalimbali Duniani zitakuwepo, tutajadili changamoto zinazo tukabili kwenye halmshauri zetu, mafanikio,lakini pia kujengeana uwezo kwenye utendaji kazi” alisema Meya Mwita.

Imetolewa leo Desemba 11

Na Christina Mwagala , Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji

Watanzania Changamkieni Fursa ya kujiandikisha kushiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya International Africa Festival Tubingen 2018 Ujerumani

Mahojiano na Saidi Kanda - sehemu ya 3

$
0
0
Sehemu ya 3 ya mazungumzo yetu na mwanamuziki mpiga ngoma na muziki wa jadi- Saidi Kanda anaelezea baadhi ya wanamuziki aliyofanya nao kazi. Na nini kajifunza au atafundisha kutokana na hilo?

WATOTO SITA WENYE MATATIZO YA MOYO WAENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s  Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka  watoto sita (6) wenye umri wa mwaka mmoja hadi  miaka kumi na tatu  nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto, wauguzi pamoja na wazazi wao wameondoka alfajiri ya jana tarehe  10/12/12. Baada ya matibabu ya watoto kukamilika  Maafisa Wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.

Taasisi  yetu inatibu magonjwa mbalimbali ya moyo kwa watoto  kupitia  wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini humo kwa ajili ya matibabu.

Tunaushirikiano mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. Licha ya Maafisa Wauguzi wawili kubaki nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo pia tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita   na wauguzi wawili ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu.Aidha Daktari wetu mmoja bado anaendelea na masomo nchini humo.

Hili ni kundi la tano  la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH)  ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo  ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Imetolewa na :

Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
11/12/2017.

KILIO CHENU NIMEKISIKIA MIMI MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA MABADILIKO, APONGEZWA NA WADAU WA UTALII - DK. KIGWANGALLA

$
0
0


Na Hamza Temba, Arusha
..............................................................
Wadau wa Utalii Jijini Arusha wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa kukubali kuyafanyia kazi mapendekezo yao ya kuwaingiza wajasiriamali wadogo katika utoaji wa huduma za kusafirisha watalii nchini.


Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo wakati akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini humo.


Chambulo alisema kwa muda mrefu sasa kanuni zinazotumika zinamtaka mfanyabiashara ya usafirishaji watalii awe na magari matatu kwa kiwango cha chini ikiwa ni pamoja na kulipia ada ya leseni ya Dola za Kimarekani 2,000 sawa na wafanyabiashara wengine matajiri jambo ambalo limekuwa likiwabagua wafanyabiashara wadogo.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki. 

“Tunakupongeza sana Mhe. Waziri kwa kutupa angalao hilo moja, tuliomba mwenye kagari kamoja nae aruhusiwe na apewe leseni walau ya dola 200 ili afanye biashara kidogo kidogo mwishowe atanunua gari tano na kuendelea, tunataka sisi Watanzania wote tufaidike na rasilimali zetu,” alisema Chambulo.


Awali akiwasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya utalii, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu alisema kwa upande wa watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo wenye gari moja hadi magari matatu watatakiwa kulipa ada ya leseni ya dola za Kimarekani 200.


Kwa upande wa wafanyabiashara wenye magari kuanzia manne hadi kumi alisema imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 2,000, wenye magari 11 hadi 50 Dola za Kimarekani 3,000, magari 51 hadi 100 Dola za Kimarekani 10,000 na magari 100 na kuendelea Dola za Kimarekani 15,000.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu (kushoto).

Kwa upande wa wafanyabiashara ambao sio Watanzania wenye magari 10 hadi 30 imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 10,000, magari 31 hadi 100 Dola za Kimarekani 15,000 na magari 101 na kuendelea Dola za Kimarekani 20,000.


Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la kuwasilishwa kwa mapendekezo hayo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya utalii kwa wadau ni kuweka ushirikishwaji na makubaliano ya pamoja ya kutekeleza kanuni hizo.


Alisema sehemu kubwa ya mapendekezo hayo imezingatia maombi na maoni ya wadau hao ambayo yaliwasilishwa kwake awali. “Kilio chenu nimekisikia mimi mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko, lengo kubwa la mapendekezo haya ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo wenye gari moja waweze kuingia kwenye biashara hii ya utalii pamoja na kuongeza mapato ya Serikali na jamii kwa ujumla,” alisema Dk. Kigwangalla.

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mkutano huo.

Katika hatua nyingine amewaagiza watalaamu ndani ya Wizara yake kuhakikisha wanakamilisha kanuni hizo mpya ndani ya mwa mwaka huu ili utekelezaji wake uanze mapema mwakani, 2018.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

HOTUBA YA RAIS DKT.MAGUFULI KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA 9 WA UVCCM DODOMA

SERIKALI NA UMOJA WA MATAIFA ZAUNGANA NA MRADI WA DUNIA WA XPRIZE ILI KUWAPATIA WATOTO 2,400 ZANA YA KITEKNOLOJIA YA ELIMU

$
0
0
 WILAYA YA MUHEZA, TANGA, TANZANIA – Katika sherehe zilizofanyika katika kijiji kimoja huko mkoani Tanga, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaligawa tableti zilizowekewa mfumo wa elimu kwa watoto. Tableti hizo ziligawiwa kama sehemu ya mradi wa majaribio wa miezi 15 chini ya Global Learning XPRIZE, ambao ni mradi wa miaka mitano uliotokana na mashindano duniani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 15.

Mradi huu wa dunia unatoa changamoto kwa timu za wabunifu kubuni na kuandaa zana- wazi za kiteknolojia ili kuwawezesha watoto walio na fursa ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Kama sehemu ya majaribio, zaidi ya watoto 2,400 kutoka katika vijiji 167 katika wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Mkinga, Muheza, na Pangani watapewa tableti mpya ya aina ya Google Pixel C, zilizotolewa kwa hisani ya Google. Tableti hizo zimewekewa mifumo ya elimu kutoka kwa washindi watano wa mwisho wa Global Learning XPRIZE. Washindi hawa walichaguliwa kutoka katika timu 198 na paneli ya majaji 11 wa kujitegemea na walio wataalamu na kutangazwa mwezi September, 2017 wakati wa wiki ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

“Teknolojia hii inayowawezesha watoto kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu pasipo msaada wa mwalimu, ni ubunifu wa kiwango cha juu kabisa,” alisema Mayasa Hashim ambaye ni Afisa Elimu Mkoa wa Tanga. “Msaada huu utaleta matokeo mazuri katika kuwakomboa watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu ili kwamba na wao wajifunze stadi hizi.”

Tableti hizo ziligawiwa na WFP kwa sababu shirika hili linasimamia uendeshaji wa kitengo cha lojistiki na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) cha majaribio katika mazingira halisi. Jukumu lake ni pamoja na kuingiza zana hiyo ya kiteknolojia katika tableti, kuanzisha vituo vya kuwekea umeme unaotokana na jua kwenye tableti hizo vijijini na kusimamia matengenezo, marekebisho na kutoa tableti mpya katika kipindi chote cha majaribio ya ugani.

SOMA ZAIDI HAPA

BALOZI WA KUWAIT NCHINI AL-NAJEM AMKABIDHI DIWANI WA VIGWAZA VIFAA VYA WENYE ULEMAVU NA MABESENI YA AKINAMAMA WAJAWAZITO

$
0
0
Balozi wa Kuwait nchini ,Mhe.Jasem Al- Najem akizungumza na baadhi ya wananchi wa Vigwaza kwenye zahanati ya Vigwaza Chalinze Bagamoyo Mkoani Pwani baada ya kumkabidhi diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani vifaa vya watu wenye ulemavu na mabeseni 100 yenye vifaa vya uzazi vyote vikiwa na thamani ya mil.17.5.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Balozi wa Kuwait nchini ,Mhe.Jasem Al- Najem wa kwanza kushoto akikabidhi vifaa vya watu wenye ulemavu na mabeseni 100 yenye vifaa vya uzazi vyote vikiwa na thamani ya mil.17.5, Kwa diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani wa pili kutoka kulia.

Na Mwamvua Mwinyi,Vigwaza.

Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jasem Al- Najem amemkabidhi diwani wa kata ya Vigwaza, jimbo la Chalinze Bagamoyo mkoani Pwani, Mohsin Bharwani vifaa vya watu wenye ulemavu na mabeseni 100 yenye vifaa vya uzazi vyote vikiwa na thamani ya mil.17.5. Kati ya fedha hiyo kiasi cha sh. mil 13 ni gharama ya vifaa vya watu wenye ulemavu ikiwemo magongo 20, fimbo za wenye ulemavu 10, fimbo za walemavu wa macho 10, miwani 20, mafuta ya wenye ulemavu wa ngozi na viti vya kubebea wagonjwa kwa watu wazima 20 na kwa watoto kumi.

Pamoja na hilo, sh mil 4.5 ni gharama ya mabeseni 100 yenye vifaa vya akinamama wajawazito kabla na baada ya kujifungua. Akipokea vifaa hivyo, kwenye zahanati ya Vigwaza, diwani wa kata ya Vigwaza Bharwani alimshukuru balozi wa Kuwait nchini Al-Najem na kusema ni balozi wa mfano na anastahili kuigwa.

Alieleza wamekuwa wakishuhudia misaada mingi ikielekezwa mijini lakini balozi huyo amefika kijijini kwa watu wenye shida na wanaohitaji misaada kama hiyo.

KANISA BOTSWANA LAUOMBEA UONGOZI WA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Uongozi wa serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania inayoongozwa na Dr. John Pombe Magufuli ni mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika kwa kuwa umekuwa makini kutumia vizuri rasilimali za nchi kwa manufaa ya watu wake.

Viongozi wengi wa kiafrika wamekuwa wakitumia vibaya rasilimali za nchi zao kwa kujilimbikizia mali huku wananchi wakibaki kuwa masikini wa kutupa. Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Dr. Magufuli unapambana na wanaofuja mali za uma pamoja na kuepuka sherehe na mikutano isiyo ya lazima ili kuokoa pesa kwa ajili ya kuendesha miradi ya maendeleo.

Hayo yalisemwa na Rev. Dr. Celestino Chishimba alipokuwa akiongoza sala maalumu ya kuadhimisha uhuru wa Tanzania iliyofanyika jumapili iliyopita kwenye kanisa la Anglican Holy Cross Cathedral jijini Gaborone nchini Botswana.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya watanzania waishio nchini Botswana wakiongozwa na viongozi wa chama cha watanzania chini Botswana. Viongozi waliohudhuria ni Mwenyekiti, Bw. Nieman Kissasi, Makamu Mwenyekiti Bi Rehema Mselle Kalabamu, Katibu Bi Magret Tibesigwa na Mweka fedha Msaidizi Bi Haika Marandu. Historia fupi ya Tanzania ilitolewa na Eng. Ben Rugumyamheto.

Sherehe za kuadhimisha uhuru wa Tanzania zilihitimishwa na hafla iliyoandaliwa na Chama cha Watanzania nchini Botswana (ATB). Hafla hii ilifanyika kwenye kumbi za mikutano za Maharaja Gaborone juzi jumamosi. Mgeni rasmi kwenye hafla hii alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini anayehudumu pia Botswana, Mh. Silvester Ambokile.

Wageni wengine waliohudhuria sherehe hizi ni pamoja na Bw. Richard Lupembe kutoka ubalozi wa Tanzania uliopo Pretoria Afrika Kusini na mwenyekiti wa Chama cha Waganda nchini Botswana Bw. Jonathan Beesigomwe aliyeuwakilisha umoja wa wana Africa Mashariki nchini Botswana.

Mh. Balozi aliwapongeza wana jumuia ya watanzania nchini Botswana kwa kudumisha umoja na ushirikiano miongoni mwao kwani ni mfano wa kuigwa kusini mwa Afrika. Aliwasihi watanzania kukumbuka kuwekeza nyumbani Tanzania hasa wakati huu ambapo nchi yetu inahamasisha uwekezaji kwenye kilimo, elimu na viwanda.
Waumini waliohudhuria ibada maalumu ya kuiombea Tanzani wakimsikilisha Padre Chishimba alipokuwa akielezea kuhusu uongozi wa Tanzania wakati alipokuwa akihubiri.
Baadhi ya watanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania.
Padre Dr. Chishimba na Bw. Kissasi wakikata keki maalumu iliyoandaliwa ya kuadhimisha uhuru wa Tanzania. Wanaoshuhidia zoezi hilo ni Bi Rehema kalamabu na Eng. Ben Rugumyamheto
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini anayehudumu pia Botswana, Mh. Silvester Ambokile akiwahutubia watanzania waliohuduria hafla ya kuadhimisha uhuru juzi jumamosi kwenye kumbi za Maharaja jijini Gaborone.

WAZIRI MPINA AFUTA TOZO ZOTE ZA MIFUGO ZISIZOZINGATIA SHERIA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akisoma stakabadhi ya malipo ya sh 50,000 kwa kila ng’ombe kinyume cha sheria aliyotozwa mfugaji wa Kijiji cha Handa, Tulway Bombo ambapo Waziri Mpina alitangaza kufuta maamuzi hayo na kuamuru wafugaji hao kurudishiwa fedha zao.

Na John Mapepele

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amefuta tozo ya faini ya shilingi elfu hamsini kwa kila Ng’ombe mmoja na ameuagiza Uongozi wa Wilaya ya Singida kuwarudishia mara moja fedha wafugaji wote walizotozwa faini kinyume cha Sheria katika zoezi la kukamata mifugo linaloendelea katika Hifadhi ya Msitu wa Jamii wa Mgori.

Waziri Mpina ametoa maelekezo hayo leo alipotembelea eneo la Hifadhi ya Msitu wa Jamii wa Mgori, kwenye Kijiji cha Handa na kuwaagiza Wakuu wa Mikoa ya Singida na Dodoma kupitia kwa Wakuu wa Wilaya ya Singida na Chemba kushirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo kufika katika eneo hilo kabla ya tarehe15/12/2017 kushughulikia mipaka baina eneo la Singida na Handa kwa upande wa Wilaya ya Chemba na migogoro ya wafugaji inayoendelea.

“Kama Waziri mwenye dhamana ya kushughulikia Sekta ya Mifugo na Uvuvi nchini sipo tayari kuvunja Sheria kwa kuwakumbatia wahalifu wanaokiuka Sheria za nchi kwenye Sekta ya Mifugo na Uvuvi, lakini pia wahalifu wanatakiwa kutozwa faini kulingana na Sheria na taratibu zilizowekwa. Utozaji wa faini ambao hauzingatii hili ni uvunjaji wa Sheria “ alisisitiza Mpina.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Handa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma baada ya kufika kijijini hapo kisha kuamuru wafugaji waliokamatiwa mifugo yao na kutozwa faini ya sh 50,000 kila ng’ombe warudishiwe kiasi cha sh. 30,000 kutokana na faini hiyo kutozwa kinyume cha sheria.

Waziri Mpina alisema utozaji wa faini wa shilingi 50,000/= toka shilingi 20,000/= za awali kwa kila Ng’ombe aliyekamatwa na shilingi 25,000/= kwa Mbuzi toka shilingi 5,000/= za awali haukubaliki na kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Singida, Elias Tarimo kurudisha shilingi 30,000/= kwa kila Ng’ombe ambazo zimetozwa bila kufuata Sheria yoyote.

Baadhi ya wafugaji waliofika katika kijiji cha Handa kulalamikia tozo ya shilingi 50,000 kwa kila Ng’ombe mmoja walizotozwa na Halimashauri ya Wilaya ya Singida ni pamoja na Jerumani Waline aliyetozwa jumla ya shilingi 2,500,000/=, kwa idadi ya mifugo 66, Mabula Mwala aliyetozwa shilingi 1,950,000/= kwa idadi ya mifugo 45, Joel Tahan aliyetozwa jumla ya shilingi 1,000,000/= kwa idadi ya mifugo 31, Elizabeth Hamisi aliyetozwa shilingi 1,050,000/= kwa idadi ya mifugo 34,na Elizabethi Nyambi aliyetozwa jumla ya shilingi 350,000/= kwa idadi ya mifugo 8.

Akizungumza kwa niaba ya wafugaji bwana Jerumani Waline, amesema changamoto kubwa kwa sasa ni kuainishwa kwa mipaka ya Kijiji cha Handa na Hifadhi ya Msitu wa jamii wa Mgori na eneo la kunyeshea maji mifugo ambapo alimuomba Waziri kulishughulikia suala hilo. Waziri Mpina ameiagiza Halmashauri ya Singida kupitia mara moja tozo hizo na kuzipeleka kwenye Mamlaka husika ili zipitishwe na kuanza kutumika kwa taratibu zinazokubalika kisheria.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza kwa makini Mkazi wa Kijiji cha Handa wilayani Chemba, Jumanne Sadick kuhusu tatizo la mpaka kati ya Pori la Hifadhi ya Swagaswaga na Mgori ambapo Waziri Mpina aliagiza ifikapo Disemba 15 mwaka huu Katibu Mkuu Mifugo na viongozi wa Mkoa wa Singida na Dodoma kufika eneo hilo ili kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

Pia amezitaka Halimashauri zote nchini kutojiingiza katika mtego wa kutoza faini ambazo hazipo kisheria kwa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria na kuagiza kuwa kuanzia sasa Halimashauri zote zinatakiwa kutoa taarifa kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pindi zinapotaka kuendesha operesheni za mifugo ili kuwa na ufahamu wa pamoja baina ya Wizara na wadau wengine hali ambayo itasaidia kuboresha operesheni hizo na kuondoa migongano isiyo ya lazima.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

NAIBU WAZIRI MHANDISI MANYANYA ATEMBELEA MAONESHO YA PILI YA VIWANDA JIJINI DAR

$
0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya ametembelea maonesho ya pili ya Viwanda vya Tanzania na kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwanda vya Tanzania.
 Pia Naibu waziri amehudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa Viwanda vya nchini uliojadili changamoto mbalimbali za uwekezaji na ufanyaji biashara nchini na kuwahakikishia wawekezaji wote wakubwa na wadogo kushirikiana na serikali katika kusema wapi wanakwamishwa ili juhudi za haraka zifanyike pale mwekezaji anapopata tatizo.
 Naibu Waziri amesema serikali inatambua umuhimu wao katika nchi hii na kuwaomba kufanya kazi kwa bidii na tija pia kulipa kodi ili kusaidia haraka maendeleo ya nchi.
Aidha Mhe. Waziri amezungumza na Waandishi wa habari na kueleza jinsi alivyojionea maonesho haya ambayo yamekuwa mfano kwa nchi yetu kwa kuwaleta pamoja wafanyabiashara na wawekezaji wote.

UZINDUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA MKOA WA GEITA

$
0
0
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita aliyevaa koti la rangi ya dhambarau na miwani akipata maelezo juu ya matumizi ya kamera za barabarani kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Geita, Mkaguzi wa Polisi Mark Thomas Masawe wakati wa ukaguzi wa mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama mkoani humu.
ofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Hagai Ruben akitoa maelezo kuhusu ukataji wa leseni za usafirishaji kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani iliyofanyika kimkoa katika Mji Mdogo wa Katoro Geita.
Wataalam wa Jeshi la Zima Moto na Wokozi Mkoa wa Geita wakiwaeleza wajumbe wa Baraza la Usalama barabarani la Mkoa wa Geita juu ya matumizi mbalimbali ya mitungi yenye Gesi ya kuzima moto wakati wajumbe hao walipotembelea banda la kikosi hicho.
Emmanuel Chacha mtaalam kutoka Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu ya Geita (GGML) akitoa maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya wokozi katika maeneo ya migodi kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na wajumbe wa baraza la Usalama barabarani .

VIDEO: TTB YAMKABIDHI BENDERA BALOZI WA UTALII NCHINI MAREKANI

TUNAZO RASILIMALI NYINGI LAKINI BADO KUNA HALMASHAURI ZINALALAMIKA HAKUNA MAPATO: DKT NCHIMBI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amezitaka halmashauri za Mkoa wa Singida kuacha kulalamika kukosa mapato bali watumie vizuri rasilimali nyingi zilizopo, ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuongeza mapato yao.  Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akifungua mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida. 

Amesema Mkoa una fursa nyingi katika sekta ya kilimo, utalii, ufugaji, madini na uvuvi ambazo bado hazijatumiwa vizuri na halmashauri katika kukuza uchumi wa viwanda kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Singida. 

“Singida ina zalisha Vitunguu vingi na bora nchini, ina zalisha viazi zitani vingi na vyenye ubora, singida pia ni mzalishaji mkubwa wa alizeti na mafuta ya alizeti huku tukiwa na viwanda zaidi a 120 vya kusindika mafuta ya alizeti, katika sekta ya utalii tuna vivuti vngi ikiwemo bwawa la kuongelea ‘swimming pool’ lililojengwa na mjerumani na lipo katikati ya pori lakini vyote hivi hatujavitumia vizuri,” amesisitiza Dkt Nchimbi.

Dkt Nchimbi ameongeza kuwa halmashauri zinapaswa kutotumia mafunzo hayo kulalamika bali mafunzo hayo yawajengee uwezo wa kutambua wapi kuna pengo katika maendeleo ya jamii na kisha kuanisha fursa na mikakati ya kuzitumia fursa hizo kuziba pengo hilo. Aidha amewataka kutumia fursa ya malengo na mitazamo waliyonayo ambayo inaweza kuleta maendeleo pamoja na kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa kubaini na kuitumia ajenda ya fursa na vikwazo katika maendeleo kwa ngazi zote. 

Dkt Nchimbi amesema matarajio yake ni kuona kila mshiriki wa mafunzo hayo ana mabadiliko ya tabia katika utendaji wake ambapo mabadiliko hayo yanaweza kupimika aidha kwa macho au viashiria vingine. Ameongeza kuwa matarajio ya mengine ni kuwa na Singida mpya yenye takwimu sahihi za bidhaa zote zinazozalishwa Mkoani Singida ili kuzitumia takwimu hizo katika kupanga mikakati ya maendeleo pamoja na kutangaza fursa zote zilizopo Mkoani hapa. 

Dkt Nchimbi ameeleza kuwa mafunzo hayo wamepatiwa ili kutatua changamoto zilizopo na endapo kutaendelea kuwepo kwa changamoto hizo katika sekta mbalimbali ikiwemo za kilimo, afya, maji, elimu, barabara na utawala bora basi tumi nzima ya fursa na vikwazo itakuwa imeshindwa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi mapema leo akifungua mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida, kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Lutambi.
Naibu Mshauri Mkuu, Maendeleo ya Mfumo wa Mafunzo wa Mpango Shirikishi Jamii kutoka shirika la JICA Naoyuki Shintani akiwa na Mtaalam wa mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo O&OD kutoka OR-TAMISEMI Silas Salamaluku wakijadilia jambo wakati wa mafunzo kwa watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba Linno Mwageni na baadhi ya watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.
Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola na Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dkt. Mpamila Madale wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka baadhi ya watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.

Mwenyekiti Mpya wa UVCCM apatikana mjini Dodoma leo

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa UVCCM Kheri James, nje ya Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma Desemba 11, 2017 (katikati) ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MATOKEO UCHAGUZI UVCCM TAIFA 2017

1. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Tanzania 2017-2022 ni Ndugu Kheri Denice James.

2. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti... 

Kura halali 565 
Thabia Mwita 286 (Mshindi)
Rashid Mohamed Rashid 282 

#MatokeoUchaguziUVCCM

3. Wajumbe wa NEC kutoka Tanzania Bara.. 

Sophia Kizigo 
Musa Mwakitinya 
Keisha 

#MatokeoUchaguziUVCCM

4. Wajumbe 2 kwenda Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka Zanzibar.. 

Abdallaghari Idrisa Juma 
Maryam Mohamed Khamis 

#MatokeoUchaguziUVCCM

5. Wawakilishi kutoka Tanzania Bara kwenda Baraza kuu UVCCM Taifa nafasi 3.. 

Rose Manumba 
John Katarahiya 
Secky Katuga

#MatokeoUchaguziUVCCM

6. Wawakilishi kutoka Zanzibar kwenda Baraza kuu UVCCM Taifa 

Nasra haji 
Abdallah Rajabu

#MatokeoUchaguziUVCCM

7. Mshindi nafasi ya Uwakilishi kutoka Vijana kwenda Jumuiya ya Wazazi ni AMIR MKALIPA
 #MatokeoUchaguziUVCCM

8. Mshindi nafasi ya Uwakilishi Vijana kwenda UWT ni DOTO NYIRENDA

IGP SIRRO AKAGUA NA KUSHIRIKI MAZOEZI YA UKAKAMAVU NA ASKARI WA MKOA WA TABORA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu toka kulia leo asubuhi alishiriki mazoezi ya utayari na kuwatia hamasa Askari wa Mkoa wa Tabora, katika ziara yake ya siku moja mkoani humo, hatua hiyo ni kutokana na kuwataka askari wa Jeshi la Polisi kuwa na utayari wakati wote.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiwa amembeba Joshua mtoto wa muumini wa kanisa la Siroham mkoani Tabora kabla ya uzinduzi wa zahanati ya Polisi iliyojengwa kwa hisani ya kanisa hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wa tatu kutoka kushoto akiangalia mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi akiwa katika mazoezi ya utayari kupita juu ya kamba mkoani Tabora leo. Picha na Jeshi la Polisi.

SERIKALI YASAINI MIKATABA MINNE YA UJENZI WA BARABARA

$
0
0
Serikali imesaini mikataba minne na kampuni nne za ujenzi wa barabara yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 702 kwa ujenzi wa kilomita 402. Tukio hilo la kusaini mikataba hiyo limeshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Mandeleo ya Afrika (AfDB), MarieHellen Minja, wabunge ambao miradi hiyo ya Barabara itapita majimboni mwao, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na wakandarasi walioshinda zabuni.

Akizungumzia utiaji saini huo, Waziri Mbarawa amesema fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tabora (Usesula)- Koga hadi Mpanda yenye urefu wa kilomita 335 na kilomita 67 kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma. Waziri Mbarawa amesema ujenzi wa barabara hizo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na ahadi za Rais John Pombe Magufuli wakati wa kampeni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)Bi. MarieHellen Minja, wakishuhudia tukio la utiaji saini wa mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402) lililofanyika leo jijini Dar es salaam.

Aidha, Waziri Mbarawa ametumia nafasi hiyo kuwataka wakandarasi walioshinda zabuni kujenga barabara zenye ubora na viwango kwa kuzingatia muda wa ujenzi. Profesa Mbarawa ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuona ujenzi wa barabara hiyo unakamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

"Naomba TANROADS msimamie ujenzi wa barabara yenye ubora kwani wakandarasi wengi ni wajanja na ikitokea mtu ameharibu asipewe nafasi kabisa ya ujenzi wa barabara hapa nchini," amesema Waziri Mbarawa. Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa wakandarasi waliopewa kazi wametokana na uchambuzi mkubwa uliofanyika kati ya wakandarasi 129 waliojitokeza mwaka 2016 kuomba zabuni za ujenzi wa barabara hizo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini, Mhandisi Patrick Mfugale, akibadilishana nyaraka za mkataba mara baada ya kusaini na Mkandarasi wa Kampuni ya Jiangxi Geo Bw. Chen Xianghua leo jijini Dar es salaam, atakayejenga barabara ya Usesula hadi Komanga km 108.

Mhandisi Mfugale amefafanua kuwa ili kurahisisha ujenzi wa barabara hizo wamegawa kwa wakandarasi wanne ambapo barabara ya Usesula hadi Komanga kilomita 108 itajengwa na Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering Group Corporation Limited ya China kwa gharama ya zaidi ya Sh.Bilioni 158 na itajengwa kwa miezi 36.

"Komanga hadi Kasinde kilomita 108 itajengwa na Mkandarasi Kampuni ya China Wu Yi Co. Limited kwa zaidi ya sh.billioni 140 na Kasinde hadi Mpanda kilomita 105 Mkandarasi Kampuni ya China Railway Seventh Group Co.Ltd kwa sh. Bilioni 133," amesema Mhandisi Mfugale. Mhandisi Mfugale ameongeza kuwa barabara ya Mbinga hadi Mbamba Bay kilomita 67 inajengwa na Mkandarasi China Henan International Corporation Group Co.Ltd (Chico) kwa sh. Bilioni 129.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipokea zawadi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kama ishara ya shukrani kwa ajili ya ujenzi wa barabara jimboni kwake, mara baada ya kushuhudia tukio la utiaji saini mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay (kilomita 402) lililofanyika leo jijini Dar es salaam.

Amesema TANROADS imejipanga kusimamia ujenzi huo kwa kufuata viwango vinavyohitajika vya ujenzi wa barabara nchini. Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bi. Minja amesema ofisi yake itaendelea kutoa mchango kwa serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini pale watakapo hitajika.

Bi. Minja amesema kuwa matarajio ya AfDB ni kuona Tanzania inapata maendeleo kwa haraka na njia rahisi ni kupitia miundombinu. Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye barabara ya Tabora hadi Mpanda inapita jimboni kwake ambapo amesema kuwa ujenzi huo utafungua fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, amesema barabara hiyo itakuwa kiungo muhimu kati ya Tanzania, Msumbiji na Malawi. Amesema kuwa Nyasa ina vivutio vingi vya utalii hivyo ujio wa barabara hizo utakuwa njia rahisi ya kuwafikisha watalii eneo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Bi. MarieHellen Minja, mara baada ya kushuhudia tukio la utiaji saini wa mikataba minne ya mradi wa ujenzi wa barabara za Tabora – Koga- Mpanda na Mbinga – Mbaba Bay zenye jumla ya (kilomita 402), jijini Dar es Salaam.

bei mpya ya mafuta Zanzibar kwa mwezi wa Disemba kuanzia kesho

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi masuala ya wateja wa Mamlaka ya udhibitiwa huduma wa nishati na maji(ZURA) Mussa Ramadhani Haji akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini Maisara Zanzibar.(Picha na Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar.)

MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Zanzibar (ZURA) imetoa taarifa juu ya bei mpya ya mafuta itakayoanza kutumika rasmi kuanzia kesho Jumanne tarehe 12-12-2017. Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara, Kaimu Mkurugenzi masuala ya wateja, Mussa Ramadhani Haji  alisema kuwa bei hizo Zura imepanga kufuatia mambo yafuatayo;-

Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations) katika mwezi wa Novemba 2017 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa Disemba 2017.

Pia thamani ya shillingi ya  Tanzania , gharama za usafiri , Bima na’ Premium ‘hadi Zanzibar  . Kodi za serikali  na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

Alisema bei za rejereja ya mafuta ya Petroli kwa mwezi wa Disemba, 2017 imepanda kwa shillingi (100) kwa lita kutoka shilling 2,130 Mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 2,230 kwa lita katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.5%.

Pia alisema bei ya rejereja ya mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Disemba , 2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shilling 2,280 kwa lita katika mwezi Novemba hadi shilling 2,190 kwa lita katika mwezi wa Disemba, 2017 sawa na  asilimia 4%.

Aidha alisema bei ya reja reja ya mafuta ya Taa kwa mwezi wa Disemb 2017 imepanda kwa shilling (80)  kwa lita kutoka shillingi 1.539 kwa lita katika mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 1,619 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.9%

Vilevile bei ya reja reja ya mafuta ya Banka kwa mwezi waDisemba,  2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shillingi 2,122 kwa lita katika mwezi wa Novemba, 2017 hadi shilling 2,032 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.4%.

WANANCHI WAASWA KUJENGA UZALENDO, KULINDA RASILIMALI ZA NCHI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akishiriki kupanda katika Shule ya Msingi Jeshini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru, huku baadhi ya makamanda, maofisa na wapiganaji wa Jwshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha Anga cha 601 KJ, walimu na wanafunzi wakishuhudia.
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi (Base Comender) Kanali Albert Joseph Kitumbo akipanda mti katika maadhimisho ya siku kuu ya Uhuru yaliyofanyika Shule ya Msingi Jeshini.
Mkuu wa Kikosi cha Anga cha 601 KJ cha Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Bryceson Msilu akipanda mti kwa kushirikiana na wanafunzi wa shule wa Shule ya Msingi Jeshini wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru iliyoadhishwa jijini Mwanza kwa kupanda miti.Nyuma ya mkuu huyo wa kikosi ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WANANCHI wa Mkoa wa Mwanza wametakiwa kujenga uzalendo kwa mkoa na taifa lao kwa kufanya kazi na kulinda rasilimali za nchi ziweze kuwanufaisha wao, vizazi vya sasa na vijavyo. Rai hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kwenye Maadhimisho ya Siku yaUhuru iliyoadhimishwa kwa kupanda miti katika Shule ya Msingi Jeshini iliyopo wilayani Ilemela .

“Tujiulize , mimi ni mzalendo kwa jamii na taifa langu ? Kufanya kazi ni uzalendo wa kutosha na unaongeza tija katika kuboresha uwezo, kuitikia na kushiriki shughuli za kijamii na hivyo kila mmoja awajibike kwa kujenga uzalendo kwa mkoa wetu na taifa laetu,”alisema Mongella.

Mkuu huyo wa mkoa alisema ulinzi wa rasilimali za nchi ili ziweze kunufaisha jamii ni uzalendohoji na kuhoji wananchi wangapi wametimiza wajibu wao kwa kuzilinda rasilimali hizo. Pia aliikumbusha jamii kupanda miti ili kutunza na kulinda mazingira na kuacha kukata miti ovyo, kuchimba mchanga, kupasua mawe na kufanya hivyo mazingira yanaharibika.

“Upandaji miti uwe endelevu na uwe sehemu ya utamaduni wetu, tusisubiri wakati wa sherehe ndio tupande miti.Tukifanya hivi watoto wetu watajua umuhimu wake na wataelewa maana ya misitu na rasilimali za misitu,”alisema Mongella na kushauri kila shule kupanda miti ya matunda ili wanafunzi wafaidike badala ya miti ya mbao pekee.

Akizungumza kwenya sherehe hizo, mwanamazingira wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Envalomental Convertion (TECO) John Masweta alishauri kupanda misitu mikubwa ya miti kwa ajili kumbukumbu ya Uhuru na kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na kuiomba serikali ya mkoa kufanya harambee ya kukusanya fedha za kuwezesha upandaji miti wa misitu hiyo.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jeshini Pelesia Manyama aliwataka wananchi wanaoishi jirani na shule hiyo kuacha kuchungia mifugo yao kwenye eneo lililopandwa miti.

Awali Mkuu wa Kikosi cha Anga 601 KJ Meja Bryceson Msilu alieleza kuwa ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kushirikiana na TECO wamepanda jumla ya miti 3,400 kuanzia Disemba mosi mwaka huu na wanatarajia kupanda miti 3,000 ya matunda katika maeneo mbalimbali ya taasisi za umma jijini Mwanza.
Viewing all 110120 articles
Browse latest View live




Latest Images