Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

DODOMA SEKONDARI MABINGWA WAPYA WA MASHINDANO YA MCHEZO WA BASEBALL NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) Katikati aliyeshika gongo la Mchezo wa "Baseball" akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Chama cha mchezo wa Baseball na Softball Tanzania na wafadhili wa Chama hicho kutoka klabu ya Rotary ya Osaka Kaskazini nchini Japan. Siku ya tarehe 1Disemba, 2017 mashindano ya mwaka huu yalipo funguliwa rasmi. Timu ya Dodoma Secondari ndiyo mabingwa wapya nchini Tanzania.

MAAGIZO YA WAZIRI MHAGAMA KWA PROGRAMU YA MIVARF KUOGEZA THAMANI YA BIASHARA ZA MIFUGO WILAYANI LONGIDO

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi,  Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama ameielekeza Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), kuongeza Thamani Biashara za Mifugo wilayani Longido kwa kutatua  kero zote  za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo.

Mhagama ametoa maagizo hayo baada ya kukagua  Soko la kimkakati lililojengwa na Serikali kupitia Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF). Soko hilo litawanufaisha wananchi wapatao 14,2000  wa wilayani Longido ambapo asilimia 95 ni wafugaji na wanaojishughulisha na biashara za mifugo.

Soko  hilo la kimkakati ambalo halijafunguliwa rasmi , tayari halmashauri ya wilaya hiyo imeweza kukusanya mapato ya kiasi cha shilingi milioni 106 kwa mwaka  2016/2017 ambapo kwa makusanyo hayo yamewezesha halmashauri hiyo kuvunja rekodi ya miaka kumi iliyopita kwa kukusanya shilingi bilioni 1.3 kwa mara ya kwanza  kwani awali mapato yake yalikuwa chini ya bilioni moja. Aidha umuhimu wa soko hiloumejidhihirisha pale Halmashauri ilivyoweza mwezi Novemba kutoa asilimia 10ya mapato yake kwa wananwake na Vijana ikiwa nikwa asilimia5 kwakilakundi na hii ikiwa nimara ya kwanza kwa Halmashauri hiyo kuweza kutekeleza hilotangu kuanzishwa kwake.


MIVARF;  ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini  iliyobuniwa  na serikali ya Tanzania  kwa  kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaanai (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).   Programu hii inatekelezwa  katika mikoa 29 ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani  tangu mwaka 2011.

MSAADA UNAHITAJIKA KWA MTOTO MLEMAVU ANAYEKULA KWA MIRIJA MIAKA MINNE SASA

$
0
0
Na Wankyo Gati, ARUSHA

Mkazi wa Mtaa wa Jamhuri kata ya Daraja Mbili Halmashauri ya Arusha Mjini Mkoani hapa, Asha Hussein amewaomba Wananchi kumsadia Fedha za Matibabu na kujikimu kimaisha kutokana na tatizo la Ugonjwa wa Utindio wa Ubongo aliyepata Mtoto wake Abul Hussein (6).

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao , Mama Mzazi wa Mtoto huyo, alisema kuwa Mtoto wake kwa kipindi cha Miaka Minne tangu kuzali kwake amekuwa akitumia Mirija ya mipira wakati wa kula chakula kutokana na hali ya Ugonjwa inayomkabili kwa sasa.
Aliongeza kuwa anawaomba Watanzania kunisaidia ili niweze kupata Matibatu ya Mtoto sababu hali yake ni Mbaya sana nayakuuzunisha, suala la uchumi ni ngumu hata kupata Fedha za kumshughulikia katika Matibabu limekuwa ni shida kwa kweli”

Akizungumzia hali ya Ugonjwa kwa Masikitiko, Mama wa Mtoto huyo, alisema kuwa kwa kipindi cha miaka Minne Mtoto wake amekuwa akiishi ya kulishwa chakula kwa kutumia mirija, hali inayosababisha kutapika kila Mara na wakati mwingine damu umtoka kutokana na mipira hiyo kukaa tumboni kwa muda mrefu. Alisema kuwa Mtoto huyo alipozaliwa alibainika kuwa alikuwa na tatizo la kukakamaa na kutokuona vizuri ambapo alisema kitaalamu tatizo hilo, linaitwa tatizo la utindio wa ubongo.

Kwaupande wake daktari bingwa Julius Msuya wa magonjwa ya kina mama na watoto kutoka hospitali ya St Thomas Mkoani Arusha alisema kuwa hali hiyo inatokana na uchelewaji wa mama kujifungua ambapo husababisha kukosekana kwa hewa ya oksijeni katika ubongo wa mtoto na hivyo kupelekea kupata matatizo mbalimbali ikiwemo kutokukomaa kwa viungo vyake sanjari na kupata tatizo la utindio wa ubongo.

Msuya alisema kuwa wakati wakujifungu kwa kinamama ikitokea kama kachelewa ndiyo matatizo kama hayo, yanamtokea Mtoto na kumsababishia Madhara Makubwa . Amina Salum ni Jirani, na yeye alitoa angalizo kwa wanawake na watoa huduma wote wa hospitali hapa, Nchini kuwa makini ili kuepusha upatikanaji wa watoto wa aina kama ya Abdul.

Alieleza kuwa Kumekuwepo na ongezeko la watoto wa aina hiyo katika jamii hali ambayo imekuwa ikizua taharuki katika familia na wengine kuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina badala yake wakina mama wajawazito wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya suala hilo.

WANAHABARI WAFUNDWA JUU YA UMUHIMU WA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI NA KUPIGANIA HAKI ZA WATOTO

$
0
0
Mwanaharakati wa Haki za Watoto nchini na Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative , Rebeca Gyumi  akizungumza na Wahariri na Waandishi waandamizi wa Vyombo mbalimbali vya Habari juu ya haki za Mtoto na   vita dhidi ya Ndoa za Utotoni zinazoendelea nchini.
 Mtaalamu wa kupigania Haki za Watoto kutoka Taasisi ya Save The Children, Neema Bwaira akizungumza na Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo Mbalimbali vya Habari hapa nchini wakati wa Semina juu ya haki za Mtoto Jijini Dar es Salaam
 Mtaalamu wa Masuala ya Haki za Watoto kutoka nchini Thailand anayefanya kazi na Taasisi ya Save The Children nchini, Yui Mutomol  akitoa Elimu kwa Waandishi wa Habari waandamizi na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari Jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya Waandishi Waandamizi na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa Makini wakati wa semina ju ya haki za Mtoto iliyoandaliwa na Taisisi ya Save The Children Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Waandishi Waandamizi  na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya habari waliohudhuria  Semina juu ya haki za mtoto iliyoandaliwa na Tasisi ya Save The Children nchini

TIB CORPORATE BENKI YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MATIBABU KWA ZAHANATI YA MSONGOLA- ILALA

$
0
0
Benki ya TIB imetoa msaada wa vitanda viwili pamoja na mashine ya kupumulia kwa mtoto mwenye tatizo la kupumua katika zahanati ya Msongola , Ilala jijini Dar es Dar es Salaam.
Akizungumza baada kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo amesema kuwa benki inaguswa na afya za wananchi pamoja na watoto.
Amesema kuwa benki itaendelea kutoa msaada mbalimbali kwa ajili ya wananchi wake ambao ndio mtaji wa benki pale wanapopata huduma bora za afya.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema msaada huo ni muhumu katika zahanati ya Msongola na kuwata benki hiyo kuendelea kuunga mkono zahanti katika kuweza kutoa huduma bora.
Amesema serikali ina mambo mengi pale panapotokea wadau wanajitolea wanakuwa wameisaidia serikali katika kutatua changamoto  na kuweza kuendelea kutoa huduma nyingine sehemu zenye changamoto.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo(kulia) akimkabidhi vifaa vya matibabu Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema  kwa niaba ya Zahanati ya Msongola vyenye thamani ya shilingi milioni saba (7) walizochanga wafanyakazi wa benki hiyo ili kusaidia wakina mama wanaojifungua katika Zahanati hiyo. Kushoto ni Mbunge wa Ukonga,  Mwita Waitara.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari, wafanyakazi wa TIB Corporate Benki, Wauguzi na wananchi wa Msongola mara baada ya TIB Corporate Benki kukabidihi msaada wa vifaa vya matibabu kwenye Zahanati ya Msongola leo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Benki, Edward Lymo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu benki hiyo inavyorudisha fadhila kwa wananchi kwa kusaidia kwenye masuala ya kijamii ikiwemo na msaada walioutoa kwenye Zahanati ya Msongola.
Baadhi vifaa vilivyotolewa na TIB Corporate Benki kwenye Zahanati ya Msongola leo jijini Dar es Salaam.

KAMISHNA SURURU, AIPONGEZA UHAMIAJI KASKAZINI UNGUJA KUSOGEZA HUDUMA NDANI YA JAMII

$
0
0
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kati kati), akiwatoa hofu Watendaji wa Mamalaka ya Vitambulisho vya TAifa (NIDA) kwamba kuanzia mwezi January 2018, Idara ya Uhamiaji Zanzbar imejipanga kushughulikia maombi ya Vitambulisho vya Taifa kwa Raia wote watakaofika katika Ofisi yao iliyopo Kinduni, Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja, badala ya kufuata huduma Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini iliyopo Kivunge. Hatua hiyo ni utekelezaji wa Ahadi za Serikali kufikisha huduma karibu na Wananchi. Aliyasema hayo wakati alipotembelea Ofisi hizo wakati wa ziara ya kikazi katika Wilayani humo tarehe 05 - 06 Disemba, 2017.
Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, amewapongeza watendaji wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa kusogeza huduma za Uhamiaji karibu na Jamii inayowazunguka. Alitoa pongezi hizo leo alipotembelea Vituo Maalum “Detached Points” vilivyopo ndani ya maeneo ya Kendwa na Nungwi, Shehia za Nungwi - Banda Kuu, Mnarani na Kiungani, Wilaya ya Kaskazini “A” na Fukwe za Kiwengwa, Pongwe na Pwani mchangani, Shehia za Kiwengwa, Moga na Pongwe kwa Wilaya ya Kaskazini “B” alipofanya ziara ya kikazi katika Wilayani hizo tarehe 05 – 06 Disemba, 2017.

Mkoa wa Kaskazini Unguja ni kitovu cha shughuli za Biashara na Uwekezaji katika sekta ya Utalii, hali inayosababisha kuwavuta wageni wengi kutoka Mataifa mbali mbali Duniani kutembelea maeneo hayo kwa madhumuni tofauti. “katika Mkoa huu Idara yetu ina kazi kubwa ya kuhudumia wageni wanaoingia na kuishi ndani ya Mkoa huu, kwani ni Mkoa ambao huwavuta wageni wanaokuja kutembea na kupumzika kwenye fukwe nadhifu, kuna wanaokuja kwa kuwekeza na wale wanaokuja kufanyakazi na biashara mbali mbali za Utalii, hali ambayo huibua changamoto nyingi za Kiuhamiaji” alisema Kamishna Sururu.

Kutokana na muingiliano huo wa wageni wa makundi tofauti, Idara ya Uhamiaji yenye dhamana ya kuhakikisha wageni wote wanaoingia na kuishi nchini wanafanya hivyo kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Uhamiaji, ina mchango mkubwa katika kuimarisha Ulinzi, Uchumi na Utamaduni wa watu wa Zanzibar. Kuanzishwa kwa Vituo maalum kwenye maeneo hayo ni mapinduzi makubwa katika Udhibiti na Usimamizi wa wageni wanaoingia na kuishi Zanzibar kinyume cha Sheria.
“Kwa kweli Nimefarijika sana kuona jinsi mlivyojipanga kuweza kuyafikia maeneo yote yenye changamoto za uwepo wa baadhi ya wageni wanaojipenyeza na kuishi nchini bila ya Kufuata Sheria za Uhamiaji. Uwepo wa Vituo hivi naamini ni muarobaini wa kuondoa kabisa tatizo la Uhamiaji haramu” Alisema Kamishna Sururu na kuongeza “Hatuzuwii wageni kuja kutembea, hatuzuwii wageni kufanyakazi ama kuwekeza nchini kwetu bali tunataka wageni wote waingie na kuishi nchini kwa kuheshimu Sheria za Nchi yetu, kwa kufanya hivyo tutaweza kufikia ile adhma njema ya serikali kufungua milango ya Biashara na Uwekezaji katika sekta ya Utalii kwa manufaa makubwa bila ya kuathiri Jamii na Tamaduni zetu”.

KAMISHNA JENERALI MALEWA APOKEA UTAMBULISHO WA MMWALIMU WA JUDO MAKAO MAKUU YA MAGEREZA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dk. Juma Ali Malewa amepokea utambulisho wa Mwalimu wa Judo Shozy Yogi aliyekuja kumtembelea Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 December 2017.

Mwalimu Shozy Yogi alifika Makao Makuu ya Magereza akiambatana na kiongozi wa Japan International Cooperation Mr. Tsujimoto Makoto, Mkuu Msaidizi wa Kikosi Maalum cha kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM), Mrakibu Alli Uwesu na Msaidizi wa Mwalimu, Warder Oscarius.

Kamishna Jenerali Malewa aliupokea ugeni huo na kufanyanao mazungumzo ya jinsi mwalimu huyo ataendesha mafunzo hayo kwenye kambi ya KMKGM. Mwalimu Shozy Yogi aliwasili toka tarehe 17 November,2017 na amefika hapa Tanzania kwa mafunzo ya muda mrefu ya mchezo wa Judo kwenye kambi ya Kikosi Maalu cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dk. Juma Malewa akimsikiliza Kiongozi wa Japan Internation Cooperation (JICA) Mr. Tsujimoto Makoto alipomtembelea ofisini kwake.
Mwalimu wa mchezo wa Judo toka Japan, Shozy Yogi(Kushoto) akimsikiliza Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya Magereza. Kulia kwake ni kiongozi JICA ambaye amemleta Tanzania.
Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa(wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu Shozy Yogi(mwenye shati jeupe), Mr. Tsujimoto Makoto (mwenye suti nyeusi), Kamishna wa Utawala na Fedha(wa tatu kushoto). Wengine ni Mrakibu Mwandamizi Matilda Mlawa (wa kwanza kushoto), Mrakibu Alli Uwesu na Wdr Oscarius.
Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa akiagana na Mwalimu wa Judo Shozy Yogi ofisini kwake baada ya kufanya nae mazungumzo.

DKT SHEIN AHUDHURIA MAZISHI YA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI SERIKALI ZANZIBAR OTHMAN BAKARI LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na wakijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar katika Sala ya Kuuombea Mwili wa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikali Zanzibar Marehemu Othman Bakari dua ikisomwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Masjid Shurba kidingochekundu Zanzibar na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe .(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Othman Bakari, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikali Zanzibar, maziko hayo yamefanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.(Picha na Ikulu),

BREAKING NYUZZZZ: ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MANYARA, JOEL BENDERA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamiii hivi punde inaeleza kuwa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera amefikwa na mauti leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua. 

Taarifa zaidi zitawafikia baadaye.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA USAFI AWAMU YA PILI KESHO MKOANI DODOMA

$
0
0

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mwakilishi wa shirika la DFID nchini Tanzania Elizabeth Arthur wakikagua vyoo bora vinavyotumika na Wanafunzi wa shule ya Msingi  Humekwa,wilayani Chamwino mapema leo,ambapo Mh.Ummy amekagua usafi wa Mazingira pamoja na vyoo bora,
ikiwa ni sehemu ya kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira iliyobeba ujumbe wa 'NIPO TAYARI' , ambapo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.PICHA NA MICHUZIJR-DODOMA
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mwakilishi wa shirika la DFID nchini Tanzania Elizabeth Arthur wakikagua vyoo bora vinavyotumika na Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Humekwa,wilayani Chamwino mapema leo,ambapo Mh.Ummy amekagua usafi wa Mazingira pamoja na vyoo bora,
ikiwa ni sehemu ya kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira iliyobeba ujumbe wa 'NIPO TAYARI' , ambapo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Mwakilishi wa shirika la DFID nchini Tanzania Elizabeth Arthur wakiangalia  namna Kibuyu Chilizi kinavyosaidia kuepukana na magonjwa ya matumbo,kuhara pamoja na kipindupindu

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa ameongoza na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Vumilia Nyamonga,Mganga Mkuu wa Mkoa hospitali ya Dodoma Dkt James Charles pamoja na Mwakilishi wa shirika la DFID nchini Tanzania Elizabeth Arthur wakitoka kukagua mazingira ya usafi wa zahanati ya kijiji Humekwa
wilayani Chamwino mapema leo,ambapo Mh.Ummy amekagua usafi wa Mazingira pamoja na vyoo bora,ikiwa ni sehemu ya kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira iliyobeba ujumbe wa 'NIPO TAYARI' , ambapo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza mapema leo mbele ya Wanakijiji cha Humekwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma,na baadae kujibu kero kadhaa za wananchi huo kuhusiana sekta ya Afya katika kijiji hicho na kufanya ukaguzi wa Usafi wa Mazingira na Vyoo bora ikiwa ni sehemu ya kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira iliyobeba ujumbe wa 'NIPO TAYARI' , ambapo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
 

Mwakilishi wa shirika la DFID nchini Tanzania Elizabeth Arthur,ambao pia ni baadhi ya Wafadhiri wa Mazingira na Usafi katika sehemu mbalimbali hapa nchini,akiwasalimia baadhi wa wanakijiji cha Humekwa wilayani Chamwino,waliofika kwenye mkutano wa hadhara,ambapo mgeni rasmi alikuwa WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alifika katika kijiji hicho kukagua Usafi wa Mazingira na Vyoo bora kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya usafi wa Mazingira iliyobeba ujumbe wa 'NIPO TAYARI' , ambapo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.Pichani kulia ni Mganga Mkuu hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dkt James Charles pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe.Vumilia Nyamonga.

Mmoja wa Wanafunzi wa shule ya Msingi Humekwa,katika kijiji cha Humekwa wilayani Chamwino akinawa mikono kwa kutumia maji ya kibuyu chilizi pamoja sabuni mara baada ya kutoka chooni,kuepuka kuambukizwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo Kipindupindu.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AKAGUA MAKAZI YA MAKAMU WA RAIS

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maelezo ya ujenzi kutoka kwa Msanifu Majengo, Edward Kayombo (kulia) wakati alipoenda kukagua ofisi na makazi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma Desemba 6, 2017 wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TBA-Dodoma, Steven Simba (kushoto) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Maimuna Tarishi, na wapili kushoto ni Waziri wa Nchi Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan pindi atakapohamia Dodoma.

Waziri Mkuu amefanya ukaguzi huo leo mchana (Jumatano, Desemba 6, 2017) katika eneo la Kilimani, mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Waziri wa Nchi (OWM) anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana, Bibi Jenista Mhagama alisema Kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma kilibaini kuwa mahali alipokuwa akiishi awali siyo sahihi kwa ajili ya makazi ya kudumu ya Mhe. Makamu wa Rais.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo ya mpangilio wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Msanifu Majengo, Edward Kayombo (kulia) wakati alipokwenda kukagua ofisi hiyo mjini Dodoma Desemba 6, 2017 (katikati) ni Waziri wa Nchi Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.

“Pale palikuwa panafaa kwa ajili ya ziara za kikazi alipokuwa akija Dodoma, kwa hiyo tumeamua tufanye ukarabati hapa, ili aweze kuishi kwa viwango vinavyostahili.”

Alisema kazi ya matengenezo kwenye makazi yake itagharimu sh. bilioni 1.5 wakati kazi ya kutenganisha ofisi za watumishi na wasaidizi wa Makamu wa Rais itagharimu sh. milioni 680.

Waziri Mkuu pia alikagua matengenezo ya Ofisi inayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais ambayo itakuwa eneo la Ndejengwa.
Wakati huohuo, Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dodoma, Bw. Steven Simba ambaye anasimamia ujenzi huo, alimweleza Waziri Mkuu wanataraji kuwa kazi hiyo itakamilika kabla ya Desemba 30, mwaka huu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ukarabati wa makazi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma Desemba 6, 2017.

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI WA BODI SITA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi sita za taasisi za Serikali baada ya wenyeviti waliokuwepo kumaliza muda wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 06 Desemba, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kwanza Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Monica Ngenzi Mbega kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko kuanzia tarehe 30 Novemba, 2017.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Egid Beatus Mubofu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuanzia tarehe 01 Desemba, 2017.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Abiud Kaswamila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kuanzia tarehe 01 Desemba, 2017.

Nne, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Esther Hellen Jason kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuanzia tarehe 01 Desemba, 2017.

Tano, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Kenneth Mdadila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi ya kifedha ya Self Microfinance Fund Limited kuanzia tarehe 01 Desemba, 2017. 

Sita, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Titus Mlengeya Dismas Kamani kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania kuanzia tarehe 06 Desemba, 2017.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Desemba, 2017

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ALIA NA MAKAMPUNI YALIYO NDANI YA UWANJA WA NDEGE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM

KILI STARS KUIKABILI Z’BAR HEROES BALOZI WETU NCHINI KENYA DKT PINDI CHANA AKISHUHUDIA

$
0
0
Na Alfred Lucas wa TFF, Machakos
Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kesho Alhamis Desemba 7, 2017 inatupa karata yake ya pili kwenye michuano ya CECAFA dhidi ya Zanzibar Heroes ya Zanzibar kwenye mchezo wa kwanza utakaoanza saa 8.00 mchana kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos.
Mchezo huo unatarajiwa kushuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Pindi Hazara Chana ambaye anaiwakilisha nchi katika Kenya. Kuelekea mchezo huo, Kilimanjaro Stars imefanya mazoezi yake ya mwisho leo Desemba 6, mwaka huu asubuhi kwenye Uwanja wa Machakos Academy chini ya Kocha mkuu Ammy Ninje.
Kocha Ninje amesema maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Zanzibar yamekamilika na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Libya. Mbarak Yusuph ndio mchezaji pekee atakayekosekana kutokana na kusumbuliwa na mejeraha ya misuli lakini Kocha Ninje amesema ana washambuliaji wanne ambao atawatumia kuziba nafasi hiyo ya Mbarak.
Nahodha Himid Mao amesema mechi hiyo itakuwa ngumu lakini wako tayari kupambana kupata matokeo ya ushindi kwakuwa kila mmoja wao ana morali kubwa na nia ya kupata ushindi. Amesema kikubwa watatakiwa kutulia na akili zao kuzielekeza uwanjani kuhakikisha Kilimanajro Stars inabeba pointi zote 3.
Kilimanjaro Stars inashuka kwenye mchezo wa kesho ikiwa na pointi moja katika Kundi hilo la A ambalo linaongoza na Kenya wenye pointi 4 wakifuatiwa na Zanzibar wenye pointi 3, Libya wenyewe wana pointi 2 wakati Rwanda wanaburuza mkia wakiwa hawana pointi wakifungwa kwenye michezo yake yote miwili iliyochezwa.
Timu hizo za Kundi A zinaingia Uwanjani hiyo kesho zikiwa kwenye nafasi tofauti wakati Kilimanjaro Stars ikikamata nafasi ya nne ikiwa na pointi moja iliyoipata kwa kutoka suluhu bila kufungana na Libya,Zanzibar Heroes wao wapo kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi tatu baada ya kushinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Rwanda.
Timu nyingine kwenye Kundi hilo mbali ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes ni Libya na Rwanda ni wenyeji Kenya “Harambee Stars”. Kundi B lenyewe linacheza mechi zake huko Kakamega likiwa na timu za Uganda, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.
Mshambuliaji  Ibrahim Ajib akiruka viunzi wakati mazoezi  ya mwisho kabla ya kupambana na Zanzibar Heroes  kwenye Uwanja wa Machakos Academy chini ya Kocha mkuu Ammy Ninje.
Jonas Mkute (Kushoto) akipambana na Hamisi Abdallah (kulia) huku Shiza Kichuya akijiandaa kutoa msaada wakati wa mazoezi 
 Mshambuliaji Elias Maguli katikati ya mazoezi  ya mwisho kabla ya kupambana na Zanzibar Heroes  kwenye Uwanja wa Machakos Academy chini ya Kocha mkuu Ammy Ninje.
Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakiwa katika mazoezi  ya mwisho kabla ya kupambana na Zanzibar Heroes  kwenye Uwanja wa Machakos Academy chini ya Kocha mkuu Ammy Ninje.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 06.12.2017


Ubalozi wa Norway waipatia UN Tanzania dola milioni 5.1 ili kufanikisha UNDAP II

$
0
0
Ubalozi wa Norway nchini umeipatia msaada wa dola bilioni 5.1 Umoja wa Mataifa Tanzania ili kusaidia kufanikisha Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).Makubaliano hayo yamesainiwa na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez katika ofisi za ubalozi wa Norway uliopo jijini Dar es Salaam.Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi Kaarstad alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo inatolewa na Norway ili kufanikisha mpango wa UNDAP II ambapo kwasasa imefika dola milioni 10.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali na UN katika mpango huo.
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa Umoja wa Mataifa Tanzania. (Picha zote na Rabi Hume)

"Lengo la msaada huu ni kuwasaidia wakimbizi waliopo Kigoma na kwa wananchi wa Kigoma kwa ujumla, makubaliano mapya tuliyosaini leo yanalenga maeneo yaliyokusudia. Kusaidia kilimo ili kuwezesha kuwepo chakula cha kutosha kwa ajili ya wakimbizi na wananchi wanaozunguka hayo maeneo ya kambi,"Sehemu nyingine ambayo msaaada huu unalenga, ni kusaidia ni kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto. Matumaini yetu msaada huu utafungua milango kwa washirika wengine wa maendeleo kuchangia ili kufanikisha mapango huu," alisemaNaye Rodriguez aliushukuru Ubalozi wa Norway kwa msaada waliowapatia na kwa serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao inautoa kwa Umoja wa Mataifa ili kufanikisha mpango huo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumza kuhusu msaada ambao wameupokea kutoka Ubalozi wa Norway.  

Rodgriguez alisema msaada huo utatumika kama ulivyopangwa kwa wakimbizi na wananchi waliopo mkoa wa Kigoma kwa kuhakikisha kunakuwa na chakula cha kutosha kwa wakimbizi wote wanaokadiriwa kufikia 340,000, lakini pia kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia kwa watu wote."Kwa miongo mingi, Norway imeendelea kuwa mshirika wa kuaminika kwa Tanzania na Umoja wa mataifa. Kwa kuweka mkazo katika mahitaji ya wanawake na watoto walio hatarini, rasilimali hizi zitatoa mchango muhimu katika kukidhi mahitaji ya wenye uhitaji mkubwa kama ilivyoelezwa katika Malengo ya Dunia." alisema Rodriguez.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad wakisaini makubaliano ambayo yatawezesha Norway kuongeza dola milioni 5.1 katika makubaliano ya Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).

MPINA AMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI ALIYESHIRIKI UTOROSHAJI WA KILO 2500 ZA SAMAKI KWENDA BURUNDI ZENYE THAMANI YA SHILINGI 20,850,000.00

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yohana Budeba kumsimamisha kazi mara moja Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Ayoub Ngoma kwa tuhuma za kushiriki katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= hapo jana.

Akizungumza katika ofisi ya Kitengo hicho iliyopo mjini Kagera, Mpina alisema mnamo tarehe 03/12/2017 majira ya Saa 03:00 asubuhi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara ilikamata gari lenye namba za uasajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter likiwa limepakia samaki zenye uzito wa kilo 2,000 aina ya Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato kwenye mpaka wa Murusagamba wilayani Ngara.

“Katika kipindi cha uongozi wangu, tayari nimesha waagiza Makatibu Wakuu waliopo katika Wizara yangu kutembea na barua zilizozosainiwa za kusimamisha kazi watumishi wote wanaohujumu jitihada za Serikali ibaki kujaza jina tu. Kwa sasa hatuna hata nusu dakika ya uvumilivu kwa watu kama hawa, tutawaondoa mara moja.” Alisisitiza Mpina

Aidha, Waziri alisema Afisa huyo na Dereva wa gari hilo bwana Ayuob Sanga wanashikiliwa na polisi kwa hatua za kisheria kwa kuhusika na tukio hilo, na kuongeza kwamba samaki hawa walikuwa wakitoroshwa kwenda nje ya nchi bila ya kufuata Sheria ya Uvuvi Na 22 ya 2003 na taratibu mbalimbali za usafirishaji wa samaki na mazao yake nje ya nchi.

Afisa Mfawidhi wa Kanda wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Gabrieli Mageni alimweleza Waziri Mpina baadhi ya taratibu zilizokiukwa kuwa ni pamoja na samaki hao kutopaswa kuvuliwa kwa kuwa walikuwa wakubwa zaidi ya sentimeta 85 na wadogo chini ya sentimeta 50, msafirishaji kutokuwa na kibali cha kusafirisha mazao ya uvuvi, kutolipia ushuru na mrabaha wa Serikali, kutokuwa na cheti cha afya pamoja na leseni ya kuuza mazao ya uvuvi nje ya nchi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina (mwenye miwani) akiangalia maboksi ya samaki aina ya Migebuka yenye kilo 240 yaliyokamatwa katika kituo kikuu cha basi cha mjini Kagera hapo jana.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina(mwenye miwani ) akitoa tamko la kumsimamisha kazi mara moja Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera bwana Ayoub Ngoma kwa tuhuma za kushiriki katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530 kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= hapo jana.
. Moja ya boti inayotumika kwenye doria katika ziwa Viktoria na Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera.

Kamati ya UN kutetea haki za Wapalestina yazungumza na Waziri Dk. Mwakyembea

$
0
0
KAMATI maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina imekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa mazungumzo maalum walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waziri Dk. Mwakyembe, Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck alisema michezo inaumuhimu mkubwa kwa jamii kwani ni kiungo kinachotumika kujenga mshikamano na kudumisha amani kwa mataifa mbalimbali na jamii kwa ujumla.

Aliwahimiza wanahabari nchini kuendelea kuandika habari za Palestina kiusahihi ili kuielimisha jamii juu ya suala hilo na pia kupaza sauti na hatimaye suluhu kupatikana eneo hilo, aliwataka vijana kupenda kusoma historia za maeneo anuai ikiwemo mvutano kati ya Palestina na Israeli kwa ajili ya kujijengea uelewa wa mambo duniani.

Kwa upande wake Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour akizungumza na waziri alitoa ombi la mechi ya kirafiki kimataifa kati ya Tanzania na Palestina kudumisha zaidi uhusiano uliopo pande mbili. Kamati hiyo ilipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu katika mdahalo, asasi za kiraia na Jukwaa la Wahariri.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akikabidhiwa kitabu cha picha na historia ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli alipotembelewa na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisalimiana na Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour (wa pili kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.

Jaffo:Stawavumilia wakurugenzi na wenyeviti wa kamati za fedha ambao hawatatoa fedha za maendeleo

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo amesema hatawavumilia wakurugenzi na wenyeviti wa kamati za fedha ambao hawatatoa fedha za maendeleo zinazotokana na mapato ya ndani ya halmashauri kulingana na bajeti zao.

Alitoa onyo hilo wakati akifungua kongamano la siku mbili la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

Jafo alisema wakurugenzi na wenyeviti hao wataondolewa katika nafasi zao endapo watashindwa kutoa fedha hizo ikiwa ni pamoja na asilimia tano za mapato ya ndani kwa vikundi vya vijana na wanawake.

“Wakarugenzi watakaoshindwa kutoa fedha katika mapato yao ya ndani hawatatosha katika kipindi cha utawala huu, umeipanga katika bajeti , umekusanya halafu vijana na akina mama hujawapelekea asilimia tano za mapato ya ndani, basi mkurugenzi utakuwa hutoshi”

 .WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo akizungumza katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtenda wa Wajibu, Lodovick Utouh akizungumza juu madhumuni ya mkutano huo kwa wenyeviti wa halmashauri, Mameya na Wakurugenzi juu ya upangaji mikakati ya kuhudumia wananchi katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Wajibu, Yona Kilaghane akizungumza juu maazimizio na utekelezaji wa wajibu maombi ya WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sulemani Jafo katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu, Hadson Kamoga akizungumza na waandishi wa habari juu utekelezaji wa maazimio yatakayotokana na kongamano hilo katika kongamano la siku mbili  la wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri juu ya uwajibikaji mamlaka za serikali za mitaa linalolenga kujadili nafasi ya mamlaka hizo katika kutekeleza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
 Sehemu wenyeviti wa halmashauri, Mameya na Wakurugenzi

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO DECEMBER 7,2017

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images