Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

TFDA YAWANOA WASINDIKAJI WA CHAKULA MKOANI GEITA

$
0
0

Na,Joel Maduka,Geita.

Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA imewakutanisha wajasiriamali wanaosindika chakula mkoani Geita na kutoa mafunzo yatakayowasaidia kutengeneza vyakula vinavyokidhi viwango vya usalama na vitakavyoweza kukuza soko la ndani na nje.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa usalama wa chakula makao makuu ya TFDA Bw Lazaro Mwambole alisema tafiti walizofanya zimebaini kuwa wengi wenye viwanda vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazotengeneza na hawajui kanuni za usindikizaji.

“Mgeni Rasmi taifiti ambazo zilifanyika mwaka 2016 zilionekana kuwa wamiliki wengi wa viwanda vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazozitengeneza hali ambayo imesababisha kutokufanya kwa ubora zaidi usindikaji wao”Alisema Mwambole.

Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita Bw Emily Kasaga amewaasa wafanyabiashara kuhakikisha wanarutubisha vyakula ili view salama na vyenye ubora kwa kuwa afya ya watumiaji iko mikononi mwao.Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Bi Fatma Hassan na Bw Edward Geni wamesema mafunzo hayo yamewafungulia mwanga zaidi kwa kuwa wengi walikuwa wakifanya kazi hizo bila kujua kamawanakosea. 
Kaimu Mkurugenzi usalama wa chakula makao makuu ya TFDA Bw Lazaro Mwambole akiendelea kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa kusindika chakula Mkoani Geita. 
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo ambao wanashughulika na usindikaji wa vyakula wakifuatilia mafunzo kwa umakini. 
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo ambao wanashughulika na usindikaji wa vyakula wakifuatilia mafunzo kwa umakini. 
Kaimu Mkurugenzi usalama wa chakula makao makuu ya TFDA Bw Lazaro Mwambole akielezea dhumuni na malengo ya mafunzo hayo wakati alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi. 
Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa idara ya uchumi na uzalishaji,Bw Emily Kasaga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wafanyabiashara wa kusindika vyakula kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya mji wa Geita. 
Baadhi ya washiriki mkoani Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasimi na watumishi wa SIDO na TFDA.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU MKURUGENZI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE YA BUNGE LA CHINA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mhe. CAO Weizhou alipofika Wizarani tarehe 06 Desemba, 2017. Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na China. Pia Mhe. Dkt. Kolimba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali inayotoa kwa Tanzania hususan katika sekta ya ujenzi wa miundombinu. 
Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou wakifuatilia mazungumzo. Wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke. 
Sehemu nyingine ya Ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou. 
Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Bi. Justa Nyange, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Charles Faini, Katibu wa Naibu Waziri, na Bw. Halmesh Lunyumbu, Afisa Mambo ya Nje 
Mhe. Dkt. Kolimba akiagana na Mhe. CAO mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 
Picha ya pamoja 

WAKULIMA wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mpunga wilayani Kakonko mkoani Kigoma waaswa kuongeza ufanisi kwa zao la mpunga

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WAKULIMA wa Sikimu ya Umwagiliaji ya Mpunga Katika vijiji vya Katengera na Ruhiti Wilayani Kakonko, wametakiwa kuongeza ufanisi kwa zao la Mpunga ilikuzalisha mazao ya kutosha kutokana na zao hilo kuwa zao la biashara kwa Wilaya hiyo na serikali kwa kushirikiana na wawekezaji wamewekeza fedha nyingi ilikuinua uchumi wa Wananchi hao.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, wakati akikabidhi vifaa vya upaliliaji kwa kikundi cha upaliliaji vyenye thamani ya shilini 12,700,000 vilivyo tolewa na shirika LINK vitakavyotumika Kupalilia Katika Mashamba ya Mpunga katika sikimu ya Katengera na Ruhiti lengo ikiwa ni kuwaongezea kipato Wanawake wanaojishughulisha na upaliliaji pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuongeza uzalishaji.

Mkuu huyo aliwaagiza wakulima hao kuongeza uzalishaji kutokana na serikali kwa kushirikiana na Wafadhiri wametatua changamoto ya vifaa vya kupalilia vilivyo kuwa vikisababisha kupata mazao machache na kuwataka kulima misimu miwili na kila hekali moja kuzalisha gunia 40 hadi 45 tofauti na kipindi ambacho walikuwa hawana nyenzo hizo.

" niwaombe wakulima wote kulima marambili katika sikimu hii sikimu hii ni ya umwagiliaji kwahiyo maana ya kumwagilia lazima mlime na kiangazi, serikali imeweka fedha nyingi sana katika sikimu hii lazima mjitahidi kuzalisha ilituweze kupata viwanda vya kukoboa mpunga na kuinua uchumi wa wanakakonko kwa yeyote atakae shindwa kulima marambili tutachukua shamba lake na tuwagawie wawekezaji iliwaweze kuwekeza zaidi na kupata mazao ya kutosha", alisema Ndagala.

Hata hivyo Ndagala aliwaagiza Wakulima hao kuzingatia maelekezo ya mabwana shamba katika uwekaji wa mbolea, pamoja na kuzingatia Muda wa kupalilia ilimuweza kuongeza uzalishaji na kupata mazao yenye ubora.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akishiriki kupalilia zao la Mpunga katika shamba la WAKULIMA wa Sikimu ya Umwagiliaji ya Mpunga Katika vijiji vya Katengera na Ruhiti Wilayani Kakonko
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi vifaa vya upaliliaji kwa kikundi cha upaliliaji vyenye thamani ya shilini 12,700,000 vilivyo tolewa na shirika LINK vitakavyotumika Kupalilia Katika Mashamba ya Mpunga katika sikimu ya Katengera na Ruhiti lengo ikiwa ni kuwaongezea kipato Wanawake wanaojishughulisha na upaliliaji pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuongeza uzalishaji.


BULEMBO AWATAKA WANA CCM KIGOMA KUWA WAMOJA NA KUHAKIKISHA MAJIMBO YOTE YALIYOKO UPINZANI YANAREJESHWA.

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel -Kigoma.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, ambae pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma,Abdallah Burembo amewaagiza Viongozi wapya wa Chama hicho Mkoani Kigoma kuhakikisha Wanayarudisha majimbo ya Kigoma mjini na Kakonko na kata zote zilizochukuliwa na upinzani .

Aidha amewataka kufanya kazi ya chama ya kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi kwa kuwatuma kazi Viongozi wa serikali, na kuwakagua kama Wanatekeleza pamoja na kuwaacha Wabunge kufanya wajibu wao na kuacha Makundi makundi katika siasa kwa kuwaweka Wana CCM pamoja ilikuhakikisha ushindi wa majimbo yote kigoma .

Wito huo ameutoa  jana, baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Mkoa katika Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Kumchagua Mwenyekiti wa Mkoa , Mjumbe wa baraza kuu taifa NEC na wajumbe wa halmashauri kuu ya Mkoa, ambapo Burembo aliwapa pole viongozi hao waliochaguliwa kwakuwa Wanakazi kubwa ya kuhakikisha Majimbo yanayotawaliwa na chama tawala yaendelea kuwepo na kuyarudisha yale yote yaliyo chini ya upinzani pamoja na kata zote.

Hata hivyo katika uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa ilichukuliwa na Amandusi Nzamba aliewashinda wenzake watano kwa kura 371 akifatiwa na Hamis Betese kura 249 akifuata aliekuwa mwenyekiti wa zamani Amani Kabour 97, Philipo Tabhiliho kura mbili na Antony Mpozemenya tisa,pamoja na nafasi ya Mjumbe wa baraza kuu taifa ilichukuliwa na Kilumbe Ngenda alie shinda kwa kura 426 kati ya Wagombea wenzake Asha Baraka na Atanasi dyoya.

"Tutawapima viongozi mliochaguliwa pamoja na viongozi wa serikali kutokana na ushindi tutakao upata hatuwezi kishindwa katika uchaguzi wakati Dc upo Mkurugenzi Upo na Mkuu wa Mkoa upo, serikali ni ya chama cha mapinduzi waliopo chini ya serikali wanaitumikoa serikali na kutekeleza ilani yetu kama kuna mtendaji au mkurugenzi hafuati utekelezaji wa ilani tutawatoa tuambieni wanao sababisha sisi tushindwe kuaminika hatuwezi kukubari tuyakose majimbo haya tunayataka kwa gharama yoyote ile", alisema Mwenyekiti wa jumuia ya Wazazi.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NHIF YAKUTANA NA WATOA HUDUMA WAKE WA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku moja na Watoa Huduma wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kupeana mrejesho wa huduma kwa wanachama, uliofanyika kwenye Ukumbi wa GEPF, jijini Dar es salaam leo.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umekutana na Watoa Huduma wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kupeana mrejesho wa huduma kwa wanachama lakini pia kujadili mambo mbalimbali yatayofanikisha kuboresha huduma za matibabu.

Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam kikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda ambaye amewataka watoa huduma kuhakikisha wanawahudumia vizuri wanachama wa Mfuko ili kuondokana na malalamiko yasiyo ya lazıma.

“Wanachama wetu wanapofika huko kwenu wahudumieni vizuri ili waone thamani ya fedora zao walizochangia lakini pia waone umuhimu wa kuendelea kuwa wanachama….tambueni mdomo ni sumu kubwa hakikisheni mnautumia vizuri” alisema Mama Anne Makinda.

Kwa  upande wa wagon huduma ambar waliwakilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Grace Magembe, aliupongeza Mfuko kwa jitihada mbalimbali ambazo umekuwa ukifanya kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa na wanachama wanahudumiwa kwa kiwango kikubwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku moja na Watoa Huduma wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kupeana mrejesho wa huduma kwa wanachama, uliofanyika kwenye Ukumbi wa GEPF, jijini Dar es salaam leo.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe akitoa salamu za watoa huduma katika mkutano huo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Angela Mziray akitoa muongozo wa Mkutano huo.

MICHUZI TV: WAFANYAKAZI TICTS WALIVYOUNGANA NA FAMILIA ZAO KUSHEHEREKEA FAMILY DAY

TAASISI YA HER INITIATIVE 'PANDA' WATOA SEMINA SHAWISHI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MWANZA

$
0
0
Desemba 2, 2017 katika chuo kikuu cha Mt. Augustine (SAUTI) Mwanza kulifanyika tamasha la uvumbuzi, ujasiriamali na kazi kwa wasichana lijulikanalo kama PANDA. Tamasha hilo ambalo huandaliwa kila mwaka na taasisi ya wasichana iitwayo Her initiative, inayojikita katika kumsaidia msichana kuweza kusimamia maswala yake binafsi, kifedha, kielimu, na kumpa uelewa msichana katika Nyanja mbali mbali za ujasiriamali wakiwa vyuoni. 

Kwa mara ya kwanza taasisi hiyo (her initiative) iliamua kufanya tamasha hilo jijini Mwanza ikiwa ni msimu wa nne kufanyika tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo, huku dhamira ya msimu wake huu wanne ilikua ni Uvumbuzi kwenye kila idara. 

Tamasha hilo lilihudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 800 kutoka vyuo vikuu na Taasisi za elimu mbali mbali zilizopo jijini Mwanza ikiwemo CBE, CUHAS na Mzumbe. Wasemaji wakuu katika tamasha hilo kwa mwaka huu walikuwa ni Benjamin Fernandes Mtanzania wa kwanza kupata nafasi ya kusoma Vyuo vikuu bora marekani vijulikanavo kama STANFORD GRADUATE SCHOOL OF BUSINESS na HAVARD KENNEDY SCHOOL OF GOVERNMENT na pia kufanya kazi katika foundation kubwa ya kimataifa ijulikanayo kama Bill and Melinda Gates. Ambaye aliongelea Uvumbuzi katika nafasi za kimataifa. 

Idris Sultan mshindi wa BBA, mchekeshaji , mtangazaji na Balozi wa Global Peace. Ambaye aliongelea maswala ya uvumbuzi katika Sanaa na kipaji na kushirikisha story yake binafsi ya mafanikio. 

Rose Ndauka mjasiriamali na mshindi wa kike wa tuzo za uigizaji , muanzilishi wa Ndauka Advert na mmiliki wa Connexion House of Beauty  Dar es salaam alieongelea Uvumbuzi kwenye Sanaa, biashara. 

“Muamko huu wa wanafunzi wengi zaidi ya 700 inaonyesha jinsi gani  vijana wa sasa walivo na nia ya kutaka mafanikio na kujifunza njia mbali mbali za ujasiriamali na uvumbuzi naamini kupitia wazungumzaji wa leo vijana hakika watakua wamebadilishwa kifkra. Tumeona umuhimu wa tamasha hili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hivyo tunategemea kufanya Zaidi na mikoa mingine “  Alisema mwenyekiti wa taasisi hii ya Her initiative Maureen Richard. 

Panda 2017 Mwanza imedhaminiwa na TECNO mobile Tanzania, Jembe FM na Michuzi Blog.
  Mchekeshaji na Mshindi wa Big Brother Afrika 2014,Idrisa Sultan akizungumza leo katika semina ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza.
Msemaji na Muhamasishaji katika fursa za kimataifa, Benjamin Fernandes akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya jijini Mwanza kwaajili ya kuwavutia kwa njia mbalimbali kutokana na aliyoyapitia katika maisha ya shule pamoja na maisha ya Kawaida.Pia amewashauri wanafunzi hao wa vyuo vikuu vya jijini Mwanzakusoma kwa bidii pamoja na kuwa wavumilivu kwenye vikwazo mbalimbali wanavyokutana navyo. Hayo yamesemwa katika semina fupi ya kuwashawishi iliyoandaliwa na Taasisi ya her initiative Present PANDA iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza.
 Msanii wa Bongo Muvi na Mjasiriamali na mshawishi katika upande wa sanaa, Rose Ndauka akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza katika semina iliyofanyika leo katika chuo kikuu cha Makatifu Agustino jijini humo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Her Initiative - PANDA, Moureen Richard akizungumza na katika semina ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Mwanza iliyofanyika katika Darasa la M12 katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino jijini Mwanza.
Baadhi ya wananfunzi wa vyuo vikuu vya jijini Mwanza wakiwasikiliza watoa maada katika semina iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Augustino jijini Dar es Salaam.

MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MPYA WA CHINA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke, wakati balozi huyo alipomtembelea Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania. Katikati ni msaidizi wa Balozi huyo, Liang Lin.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke, wakati balozi huyo alipokua anafafanua jambo katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika ofisi ya Naibu Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walikubaliana kuendeleza ushirikiano zaidi kati ya China na Tanzania. Katikati ni msaidizi wa Balozi huyo, Liang Lin.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha ofisini kwake, Balozi mpya wa China nchini, Wang Ke (katikati), wakati balozi huyo alipomtembelea Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania. Kushoto ni msaidizi wa Balozi huyo, Liang Lin. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SERA MPYA YA UJENZI KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Ujenzi, Bi. Elizabeth Tagora, akifungua rasmi warsha ya siku moja, ya wadau wa ujenzi, kujadili mapitio ya Sera mpya ya Ujenzi, mjini Dodoma.
Mwezeshaji wa mapitio ya Sera mpya ya Ujenzi, Bw. Cyril Batalia akifafanua jambo kwa wadau wa sekta ya ujenzi,wakati wa warsha ya kujadili na kuboresha sera hiyo, mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Ujenzi, Bi. Elizabeth Tagora (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya Ujenzi mara baada ya kujadili mapitio ya Sera mpya ya Ujenzi, mjini Dodoma.

Lisu kunogesha tamasha la uamsho dar

$
0
0
Na Salesi Malula

Mwimbaji John lisu anatarajia kunogesha Kongamano kubwa la Uamsho linalotarajia kutikisa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake ambapo mhubiri maarufu kutoka Sweden mwinjilisti Johanes Amritizer anatarajiwa kuwa mnenaji mkuu wa kongamano hilo la uamsho ambalo waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wanatarajia kunogesha tamasha hilo.

Kongamano hilo kubwa linatarajia kuunganisha maelfu ya waumini pamoja na waimbaji  kutoka madhehebu mbalimbali katika masuala ya Injili ambapo waandaaji wakuu ni Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (Victory Christian Centre Tabernacle Mbezi A Jijini Dar es salaam).

Katika mahojiano maalumu, Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies  Of God – VVCT  Dkt. Huruma Nkone ambaye ndiye mwenyeji wa kongamano hilo la uamsho alisema wameandaa tukio hilo wakiamini kuwa uzoefu mkubwa wa mnenaji katika medani ya masuala injili utakua msaada mkubwa sana kwa jamii ya watu wote bila kujali utofauti wa imani na madhehebu yao kwani kuna hekima za kipekee ambazo mwiinjilisti Johanes ambaye anaheshimika sana ndani na nje ya Tanzania ataziachilia kwa wote ambao watahudhuria kongamano hili ambalo kwetu kama kanisa tunajivunia sana kwa kupewa heshima ya kipekee.

“Natoa wito kwa watu wote wa jiji la Dar es salaam kutokosa kongamano hili la kipekee ambapo pia kutakua na maombi maalumu kwa washiriki wote na kuna Baraka za kipekee ambazo mtumishi huyu anaweza kuziachilia na ni fursa ya kipekee kuhudumiwa na mtumishi huyu wa kimataifa alisistiza.

Alisema maandalizi yote yamekamilika kongamano litaanza tarehe 8-10 december 2017 kuanzia saa 10:30 jioni katika kanisa la Victory Christian Centre, lililopo Mbezi Beach A, Mwai Kibaki road, kilimani close

 waimbaji mbalimbali maarufu kama John Lisu, Rivers of Joy Internartional, sarah Ndosi, ,na Samuel yonah,na DGC Kwaya.  

SHEREHE ZA UVISHWAJI PETE WAKINA MAMA WALEZI WA SOS YAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuwasalimia wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar hafla iliofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Rais wa SOS Duniani Father Siddhartha Kaul mara baada ya kuwasili katika Kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguja katika Sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar.katikati ni Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Shadya Mohammed Suleiman.

Wakina mama walezi 18 wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar waliovishwa Pete katika sherehe zilizofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.
Duniani Father Siddhartha Kaul akitoa hotuba yake kuhusianana lengo la kuwekwa vituo vya kulelea watoto SOS Duniani katika sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar hafla iliofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kushoto akimvisha Pete ya SOS Mama mlezi wa SOS Fatma Suleiman Haji anaelea Watoto Nyumba Namba Nne katika sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar hafla iliofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein wanne kutoka kulia akiwa na Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Shadya Mohammed Suleiman katika Picha ya pamoja na Wakina mama walezi waliovishwa Pete katika sherehe ya Uvishwaji Pete wakinamama wa SOS Tanzania Bara na Zanzibar hafla iliofanyika katika kiwanja cha SOS Mombasa Wilaya ya Magharibi B Unguj.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

SHULE YA SEKONDARI IWAWA MKOANI NJOMBE YANUFAIKA NA KOMPYUTA 10 TOKA VODACOM TANZANIA FOUNDATION

$
0
0
Meneja wa Vodacom Tanzania PLC,Mkoa wa Njombe,Benedict Kitogwa(kushoto)akiwasisitiza walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Iwawa iliyopo mkoani humo kuzitumia vizuri na kuzitunza kompyuta 10 zilizotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation shuleni hapo jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Mkoa wa Njombe,Besta Chaula(kushoto)akipokea moja ya kompyuta kati ya 10 toka kwa Meneja wa Vodacom Tanzania PLC wa Mkoa huo,Benedict Kitogwa msaada huo ulitolewa na Vodacom Tanzania Foundation jana.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Iwawa Mkoa wa Njombe wakionyesha baadhi ya kompyuta kati ya 10 walizopewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation jana,Anaeshuhudia kulia ni Meneja wa Vodacom Tanzania PLC,Mkoani humo,Benedict Kitogwa.

TAIFA CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 16 HADI 23 UWANJA WA NDANI WA TAIFA

$
0
0
Ikiwa zimesalia siku 10 kuelekea Mashindano ya Taifa Cup kwa timu za kikapu nchini, tayari timu zimeshawasilisha  maombi ya ushiriki wao.

Timu hizo kutoka sehemu mbalimbali nchini zimeweza kutuma maombi yao kwa timu za wanaake pamoja na wanaume.

Taifa cup confirmation
1. Mbeya Male and Female
2. Rukwa Male
3. Mtwara Male
4. Dream Team Male & Female
5. Dar City Male & Female
6. Dodoma Male & Female
7. Tabora Male & Female
8. Iringa Male & Female
9. Kusini Unguja Male
10. Mara Male
11. Shinyanga Male & Feml
12. Morogoro Male
13. Unguja Kaskazin Male & Female

14. Songwe Male
15. Arusha Male
16. Lindi Male
17. Singida Male
18. Tanga Male & Female
19. Manyara Male
20. Songea Male
21. Kighoma Male & Female

MKURUGENZI MANISPAA YA DODOMA AMALIZA HOFU YA WAFANYABIASHARA 2,500

$
0
0

NA RAMADHANI JUMA,OFISI YA MKURUGENZI

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amemaliza hofu ya kuhamishwa iliyokuwa imetanda kwa wafanyabiasha takribani 2,500 wa Soko la Sabasaba Mjini Dodoma baada ya kuwahakikishia kuwa wataendelea kufanya shughuli zao katika Soko hilo linalomilikiwa na Manispaa ya Dodoma na kwamba hakuna wa kuwahamisha.

Aliyasema hayo jana alipofanya ziara Sokoni hapo na kufanya mkutano na Wafanyabiashara hao ambao walimueleza Mkurungenzi huyo kuwa wamekuwa wakipata taarifa zisizo rasmi kuwa upo mpango wa wao kuhamishwa katika soko hilo hali inayowakosesha usingizi na kutojua hatma yao.

“Hakuna kuhama hapa ng’oo…Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ndiyo mmiliki wa Soko hili ambalo asili yake hapo awali lilikuwa eneo la Maonesho ya Sabasaba ambapo wadau mbalimbali walikuwa na vibanda vyao vya maenesho” alifafanua Kunambi huku akishangiliwa na wafayabiashara hao.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Kunambi alifuatana na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede.Wafanyabiashara hao waliishukuru Manispaa ya Dodoma baada ya viongozi hao kufika na kuzungumza nao katika wakati muafaka baada ya kufanya biashara zao kwa wasiwasi mkubwa kwa siku kadhaa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba (hawapo pichani) Mjini Dodoma jana ambapo aliwahakikishia kuwa hawatahamishwa katika soko hilo. 
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya DodomaJumanne Ngede akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Mjini Dodoma jana ambapo alifuatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi. 
Sehemu ya Wafanyabiashara ya Manispaa ya Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Mkurugenzi huyo na wafayabiashara wa soko hilo jana.

RAIS DKT MAGUFULI AWASILI DODOMA LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Desemba, 2017 amewasili Mkoani Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru zitakazofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi tarehe 09 Desemba, 2017. Katika Ikulu ya Chamwino, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge.

Akiwa Mkoani Dodoma Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) atafungua vikao vya Jumuiya za CCM na pia atakuwa mgeni rasmi katika shughuli mbalimbali za kiserikali. Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
07 Desemba, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Binilith Satano Mahenge alipowasili Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Novemba 7, 2017 tayari kwa shuguli mbalimbali za kikazi. PICHA NA IKULU.

MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA BAADHI YA MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU, MKUU WA MKOA WA ARUSHA NA KAMATI SHIRIKISHI YA JAMII KUHUSU UTATUZI WA MGOGOIRIO WA PORI TENGEFU LA LOLIONDO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) na Mkurugenzi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Pastoralist Women Council, Manda Ngoitika baada ya kikao kilichowahusisha baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Kamati Shirikishi ya Jamii kuhusu utatuzi wa Mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo kilichofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, mjini Dodoma Desemba 6, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kilichowahusisha baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Kamati Shirikishi ya Jamii kuhusu utatuzi wa Mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo kilichofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, mjini Dodoma Desemba 6, 2017.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

RAIS DKT MAGUFULI AWASILI DODOMA LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Binilith Satano Mahenge alipowasili Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Novemba 7, 2017 tayari kwa shuguli mbalimbali za kikazi. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU AFUNGUA JENGO LA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua ofisi ya Umoja wa Mataifa na kusema uamuzi huo ni hatua muhimu ya kuendeleza mchakato wa Serikali wa kuhamia Dodoma. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamsi, Desemba 7, 2017) wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa taasisi za Umoja wa Mataifa waliohudhuria hafla ya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Dodoma, katika eneo la Mlimwa, Manispaa ya Dodoma.
         
“Wote mtakubaliana nami kwamba uzinduzi wa ofisi hii ya Umoja wa Mataifa ni hatua muhimu sana ya kuendeleza mchakato wa Serikali wa kuhamia Dodoma. Pia, inafungua mlango mpya utakaowezesha ofisi zote za kibalozi na mashirika ya kimataifa kujenga ofisi zao hapa Dodoma na kuhamia mapema,” alisema.

Alisema anatambua kwamba kwamba wapo viongozi na watendaji wenye hofu ya kuhamia na kuanza maisha mapya Dodoma. “Baadhi ya watendaji wanaogopa changamoto za kuhamisha watoto wao na wenza wao ili kuanza maisha mapya. Napenda kuwatoa hofu kwamba Dodoma ni mahali pazuri pa kuishi na kuna fursa nyingi,” alisema.  Alisema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu iliyopo ya huduma za jamii na miundombinu ya barabara, maji, umeme na mawasiliano ili iwe bora zaidi. Alitumia fursa hiyo kuwasihi waombe maeneo ya ujenzi kwa ajili ya ofisi na makazi.

Aliushukuru Umoja wa Mataifa kwa kuiteua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazotekeleza mfumo mpya wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuungana na kutekeleza shughuli zake kwa pamoja kama familia moja ya Umoja wa Mataifa yaani “UN Delivering as One”.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema Umoja wa Mataifa unayo mashirika 50 na kwamba mashirika 23 kati ya hayo, yanafanya kazi zake hapa nchini. Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Manispaa ya Dodoma, watahakikisha kuwa mashirika hayo yanapatiwa viwanja vya kutosha ili kujenga ofisi zao mapema iwezekanavyo.

Mapema, Mwakilishi Mkazi wa UNDP na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania; Bw. Alvaro Rodriguez alisema wamefurahi kupata fursa ya kuwa taasisi ya kwanza ya  kimataifa kuwa na Ofisi yake kwenye makao makuu ya nchi hapa Dodoma


“Tumefurahi kujumuika kwa pamoja hapa Dodoma, lakini tunaahidi kuwa na sisi tutahamia kwa awamu kama ambavyo Serikali imekuwa ikifanya. Hili litategemea upatikanaji wa viwanja na majengo kwa ajili ya ofisi, kwa hiyo wafanyakazi wetu nao watahamia taratibu,” alisema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP. nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga.
Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mahariki, Dr. Augustine Mahiga akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi w UNDP Nchini uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi yake uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017.

KUELEKEA 9 DISEMBA.....

IN LOVING MEMORY OF MAMA ROSE SHOMARI

$
0
0
It has been 12 years since you departed from us, in this day a memory of a life so beautifully lived and a heart so deeply loved. We will always remember you and the lessons of life you gave us. 

May the Lord God hold you in Peace. In our hearts, you will always be remembered every day with the whole entire Shomari family your sons, daughters, grandsons, and granddaughters.

We thank God for your life, great advice, as a loving mother and a counselor. May the almighty Lord rest your soul in eternal Peace until we meet again.

Our hope comes from the Lord as he says he will wipe every tear from their eyes there will be no more death or mourning or crying or pain…Rev 21:4.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images