Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109609 articles
Browse latest View live

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AMZAWADIA MILIONI MOJA ASKARI WA KIKE KWA UTENDAJI KAZI MZURI KAZINI

0
0
Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa ametowa zawadi ya utendaji kazi mzuri kwa askari wa Jeshi hilo Sajini Anna Akuny wa Gereza la Wanawake Segereza leo Desemba 5, 2017 katika Makao Makuu ya Magereza Jijini Dar es Salaam.
Askari huyo Sajini Anna amekabidhiwa Sh. milioni moja (1,000,000) na Kamishna Jenerali wa Magereza kutokana na kuonesha utendaji wake mzuri pamoja na nidhamu kazini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa amemtaka askari huyo kutokubweteka na mafanikio hayo bali iwe chachu ya kufanya kazi kwa bidii zaidi.
Jenerali Malewa ametoa wito kwa Maafisa na Askari wa Jeshi hilo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo inayotolewa mara kwa mara na Uongozi wa Jeshi hilo.
Hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari huyo imehudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, DCP. Augustine Mboje pamoja na Mkuu wa Gereza Segerea, ACP. Godfrey Kavishe.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akimkabidhi zawadi ya Sh. Milioni moja(1,000,000) askari wa kike Sajini wa Magereza, Anna Akuny(katikati)  kutokana na utendaji wake mzuri kazini aliouonesha katika Gereza la Wanawake Segerea(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza  Segerea, ACP. Godfrey Kavishe.
Askari wa Kike Sajini Anna Akuny(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) mara baada ya kumkabidhi zawadi ya utendaji kazi mzuri kazini. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu.

CHALAMILA MWENYEKITI MPYA WA CCM MKOA WA IRINGA, SALIM ABRI "ASAS" ACHUKUA UJUMBE WA (NEC) TAIFA KWA KISHINDO

0
0
MS1
Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila akitoa hotuba yake ya kwanza kuwashukuru wapiga kura mara baada ya kushinda uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa leo akiwashinda wapinzani wake wawili Bw. Evance Balama na Salim Abri ambaye amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC mkoa wa Iringa.
MS2
Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila akitoa hotuba yake ya kwanza kuwashukuru wapiga kura na kuelezea Dira na Mwelekeo wa Uongozi wake mara baada ya kushinda uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, katikati ni Salim Abri ambaye amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mkoa wa Iringa na kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi huo Mh. Januari Makamba.
AS
Bw. Salim Abri Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mkoa wa Iringa katika uchaguzi huo akiwashukuru wapiga kura mara baada ya kutangazwa mshindi kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi huo Mh. Januari Makamba na kulia ni Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila
1
Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila kulia na Bw. Salim Abri Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mkoa wa Iringa wakiwashukuru wana CCM mkoa wa Iringa kwa kuwaamini na kuwapa ridhaa ya kukiongoza chama hicho.
2
Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila kuli na Bw. Salim Abri Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa washindi katika uchaguzi huo.
3
Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila na Bw. Salim Abri Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC mkoa wa Iringa wakiwa wakii.furahi paoja na wapiga kura mara baada ya kutangazwa washindi.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KITULO, MAARUFU KAMA BUSTANI YA MUNGU

0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy wakiangalia maua ya asili ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi ya Taifa ya Kitulo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama 'BUSTANI YA MUNGU'.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy (kulia) na baadhi ya viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo wakiangalia maua ya asili ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kitulo, Pius Mzimbe wakiangalia maporomoko ya maji ya Mwakipembo ambayo ni kivutio cha utalii ndani ya hifadhi ya Kitulo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Pamoja na kivutio hicho hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama 'BUSTANI YA MUNGU'..
Muonekano mwanana wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo. Hifadhi hii ina aina zaidi ya 350 za maua huku aina 35 yakiwa ndwele na hupatikana katika hifadhi hiyo pekee duniani. Vivutio vingine vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ni Maporomoko ya maji, ndege aina mbalimbali ambao wengine huama kutoka ulaya wakati wa baridi, wanyamapori aina Swala, Mbega na Nsya. Hata hivyo katika kutimiza mkakati wa Wizara kuboresha vivutio vya utalii, hifadhi hiyo ipo katika maandalizi ya kuanzisha makazi ya Pundamilia na wanyama wengine. Awamu ya kwanza ya kuhamisha pundamiliz 25 kutoka hifadhi ya taifa ya mikumi inatarajiwa kukamilika mwishoni mw mwaka huu. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama 'BUSTANI YA MUNGU'.
Aina mojawapo ya ua ambalo hupatikana katika hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii).

WAZIRI MWAKYEMBE AWATAKA WATANZANIA KUWA WAZALENDO

0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe   amezungumza  na wasanii wa tasnia mbalimbali hapa nchini akiwataka kuendeleza  na kuutangaza uzalendo wetu unaoendana na maadili yetu, ikiwa kauli mbiu ni nchi yangu kwanza.
Waziri huyo amesema hayo  jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa uwanja wa taifa  akiwahimiza Wasanii hao ambao ni kioo cha jamii kuwa na  mchango mkubwa  katika kuijenga nchi yetu. "Waandishi wa habari pia ni miongoni mwa mashujaa wetu waliotufikisha hapa tulipo" amesema waziri Mwakyembe.
Aidha Waziri  Mwakyembe  asema kuwa siku ya Ijumaa 8, Desemba mwaka huu  Dodoma kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kampeni ya uzalendo kwanza kwa nchi yangu ambapo uzinduzi huo  utahudhuruwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa ni mzalendo wa kwanza katika ujenzi wa taifa letu
 Naibu waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo Juliana Shonza  amesikitishwa na baadhi ya wasanii ambao ni vioo vya jamii hapa nchini kutokuwa na maadili ya kizalendo kwa kutumia vibaya vyombo vya mawasiliano  kwa kupiga picha zisizofaa na kutuma kwenye mitandao ya kijamii,Na amewataka kuwa  mabalozi wazuri katika  kutangaza uzalendo kwanza Hapa nchini
Hata hivyo naibu  huyo  ametoa pongezi za dhati kwa  Mrisho mpoto akiwa mzalendo alietoa wazo hilo na wasanii wenzake, Na amesema kuwa  wizara imeipa uzito kampeni hii na kuamua kuwa inde mkoani kwaajili ya uzinduzi huo.
Vile vile pia naibu Shoza  amempongeza mwanamashumbwi Ibrahim class kwa kuwa mzalendo kwa kuwa bingwa wa 3 barani Afrika na   asie na mpinzani  nchini Tanzania na kumkabidhi hundi ya shilingi milioni 18 laki 2 na 40 elfu
Nae bondia Ibrahimu class  amemalizia kwa kusema kuwa mazoezi na kujiamini ndio kinachomfanya afanye vizuri katika mashindano yake ya ndani na  nnje ya nchi na ametoa shukrani zake za dhati kwa watanzaia kwa kumuunga mkono katika mapambano yake.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa katika mkutano huo kuhusu uzinduzi wa uzalendo kwanza utakaofanyika tarehe 8, Desemba mwaka huu mkoani Dodoma.
Naibu waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza  akizungumza na wageni waalikwa kuhusu uvunjifu wa maadili ya kizalendo unaofanywa na baadhi ya wasanii hapa nchi Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  uwanja wa Taifa.
Naibu waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza  akimkabidhi bondia Ibrahimu Class  hundi ya shilingi milioni 18,240,000 na kumpa pongezi kwa kuweza kutetea ubingwa wake.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe  akimpa pongezi  mwanamasumbwi wa Tanzania Ibrahim Class kwa kazi nzuri anayoifanya na kuwa mzalendo hapa nchini.
Mwanamasumbwi  Ibrahim Class akizungumza na wageni waalikwa kuhusu mafanikio yake katika mashindano yake kwa ujumla na kuwapongeza watanzania kwa kumuunga mkomo.

Wasanii mbalimbali  hapa nchini waliojitokeza katika kuhudhuria mkutano huo  leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  uwanja wa taifa

MAGAZETI YA JUMATANO LEO DECEMBER 6, 2017

MPINA ABARIKI NARCO KUVUNJA MKATABA WA MWEKEZAJI MZEMBE KATIKA RANCHI YA KAGOMA

0
0
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  ameridhia  maamuzi ya Kampuni ya Ranchi za NARCO kuvunja mkataba baina ya mwekezaji Agri Vision Global Ltd na serikali  katika  Ranchi ya Kagoma  mkoani Kagera na kuamuru aondoka mara moja baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha miaka mitano.

Waziri Mpina ametoa maelekezo  hayo jana  alipotembelea Ranchi ya Kagoma kuangalia shughuli mbalimbali  katika Ranchi hiyo ambapo ametoa siku saba kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo na badala yake Serikali kupitia NARCO kuendelea kusimamia shughuli za mifugo katika Ranchi hiyo.

“Ninakuagiza  Mkuu wa Wilaya  kuanzia sasa  hakikisha unaimarisha ulinzi katika ranchi hii katika kipindi cha kukabidhi Ranchi baina ya Serikali na Mwekezaji  ili kusitokee hujuma zozote” alisisitiza Mpina

Alitaja baadhi ya mambo ambayo hayakutekelezwa na mwekezaji huyo kuwa ni pamoja na  kujenga  machinjio ya nyama,  kujenga kiwanda, kutoa gawio la shilingi bilioni tatu kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano, kutoa shilingi 2672 kwa hekta moja kama tozo la ardhi na kushindwa kuendeleza miundombinu ya NARCO waliyoikuta wakati  wanaingia mikataba hiyo miaka mitano iliyopita.

Waziri Mpina  amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa  Philemoni Wambura  kuhakikisha kwamba ndani ya siku saba anamleta Meneja katika Ranchi hiyo kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za ranchi hiyo na kuhakikisha kuwa inafanya kazi zake kisasa.

Aidha Mpina ametoa siku saba  kwa   Uongozi wa NARCO kuhakikisha kuwa imefanya tathmini  ya hasara zilizosababishwa na mwekezaji huyo ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yake  ili aweze kuilipa Serikali ikiwa ni pamoja na shilingi bilioni kumi na tano kama  gawio la miaka mitano iliyokaa ambalo amesema halijawahi kulipwa hata shilingi moja.

“Sasa tumeamua kuchukua hatua na tutaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wawekezaji wasiowaaminifu wanaotaka kuihujumu serikali katika sekta hizi za mifugo na Uvuvi” alihoji Mpina

Alionya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba wanauwezo wa kuwekeza katika vitalu  ili wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa. Aliongeza kwamba  Serikali imegundua  baadhi ya wawekezaji wanaopewa vitalu wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani  na kujipatia faida wakati  Serikali haipati chochote.

Awali,  akipewa ripoti ya maendeleo ya mifugo na uvuvi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Deodatus Kinawiro mbaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, alisema kutokana na oparesheni za uvuvi haramu zinazoendelea wilaya ya ngara imekamata tani 6 za samaki zilizokuwa zikipelekwa katika nchi ya burundi .


 Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  akiwa na viongozi wa Mkoa wa Kagera wa Serikali mara baada ya kuwasili jana kukagua shughuli za mifugo katika Ranchi za Mifugo zilizopo mkoani hapo jana.
 Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina(mwenye Kofia )akitoa maelezo  ya kwa mkuu wa Wilaya ya Richard Lugango kuboresha ulinzi katika Ranchi ya Kagoma baada ya kumuamuru mwekezaji  katika Ranchi hiyo kuondoka mara moja baada ya kushindwa kutekeleza mkataba baina yake na Serikali hapo jana.   
 Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  akipima urefu wa bwawa la maji ya kunyeshea mifugo katika Ranchi ya Kagoma mkoani Bukoba ambapo aliamuru mwekezaji  Agri Vision Global Ltd katika   kuondoka mara moja baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha miaka mitano hapo jana.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina  akikagua eneo la ranchi ya Kagoma kuangalia  hali halisi ya uwekezaji wa shamba la mifugo hapo jana.

KIVULINI YAFANYA KIKAO CHA WANA MABADILIKO MRADI WA USAWA WA KIJINSIA

0
0
Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto,Shirika la Kivulini limefanya kikao cha wana mabadiliko kwa ajili ya kufanya tathmini na mrejesho wa shughuli za mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana unaotekelezwa halmashauri wilaya mbili za Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga. 

Kikao hicho kilichokutanisha wana mabadiliko 65 kutoka vijiji vitano vya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Shinyanga Vijijini) ambavyo ni Nyida,Nsalala,Butini,Nduguti na Welezo kimefanyika leo Disemba 5,2017 katika Ukumbi wa mikutano wa Empire Hotel mjini Shinyanga. 

Akizungumza katika kikao hicho, Afisa mwandamizi wa mradi huo, Bi. Eunice Mayengela alisema lengo la kikao hicho ni kujadili mafanikio na changamoto ambazo wana mabadiliko wanakutana nazo kwenye maeneo yao katika kutekeleza mradi. 

Mayengela alisema suala ya ukatili dhidi ya wanawake ni la jamii nzima hivyo panahitajika ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatoweka katika jamii. 

“Lazima tushirikiane kwa pamoja kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,wana mabadiliko,serikali na wadau wengine tunapaswa kuungana ili tuwe na nguvu ya pamoja”,aliongeza Mayengela. 

Mayengela alitumia fursa hiyo kuwataka wanawake kuacha uoga wanapofanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kubakwa na badala yake watoe taarifa kwenye vyombo vya sheria ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii. 

Naye afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja aliwataka wanawake kupaza sauti wanapofanyiwa ukatili. 

“Akina mama pazeni sauti,fuateni sheria,msiwahurumie sana hawa wanaume,nanyi wanaume acheni mila na desturi zilizopitwa na wakati,wapeni urithi wa mali ikiwemo ardhi wake zenu,hata kupigana katika ndoa nako kumeshapitwa na wakati”,alieleza Mhoja. 

Mhoja pia alikemea tabia ya akina baba kuwapa ujauzito watoto badala ya kuwaacha wasome kwa ajili ya kuwasaidia katika maisha yao. Mhoja aliwataka wana mabadiliko kutumia vyema fursa waliyopewa na shirika la Kivulini ambalo limekuwa likiwapatia ujuzi na mbinu mbalimbali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kwa upande wao washiriki wa kikao hicho walisema wamekuwa wakitoa elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia kwa jamii,kutatua migogoro ya ndoa na ardhi.
Wana mabadiliko wakimsikiliza afisa mradi wa usawa wa Kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana kutoka Shirika la Kivulini, Eunice Mayengela.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja akizungumza katika kikao hicho ambapo aliitaka jamii kubadilika na kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati zinazogandamiza wanawake na watoto.
Wana mabadiliko wakiwa ukumbini.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Masili Mhoja akisisitiza umuhimu wa wanandoa kupendana kama njia mojawapo ya kukabiliana na ukatili katika familia. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA HUDUMA ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imezindua mwongozo wa huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya tiba ikiwemo zahanati, vituo vya afya na hospitali ikiwa ni katika kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya  kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iitwayo NIPO TAYARI.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Sekta Ofisi ya Rais Tamisemi, Dkt. Andrew Komba amesema uzinduzi wa mwongozo huo ni katika kueleka awamu ya pili ya kampeni ya NIPO TAYARI itakayozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais,Mhe. Samia Suluhu Hassan ifikapo Desemba 7 mjini Dodoma.

“Mwongozo huo utasimamia na kutekeleza shughuli zinazohusiana na mazingira na umelenga katika kutoa maelezo stahiki namna ambavyo vituo vya afya, ikiwemo ngazi za chini mpaka juu ili maelekezo hayo yaweze kutumika katika upangaji wa mipango na uandaaji wa bajeti zitakazotumika,” amesema Dkt. Komba. Aidha Dkt. Komba amesema kuwa watanzania tunatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira pamoja kutumia vyoo bora ili kuweza kudumisha afya njema kwa maendeleo ya Tanzania.

Kwa upande wake Mratibu wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi ya Mazingira, Anyitike Mwakitalima amesema kuwa kampeni hiyo inalenga kuwahamisha wananchi kuweza kutumia vyoo bora na mpaka kufikia Juni 2021 kaya zote nchini ziwe zinatumia vyoo. “Kutokana  na kulegalega  katika baadhi ya maeneo, waligundua kwamba kisababishi kimojawapo ilikuwa ni ukosefu wa mwongozo wa taifa ambao wadau na serikali ingeutumia kusimamia usafi wa mazingira kwahyo kampeni hii itahakikisha mpaka kufikia 2025 kaya zote zinatumia vyoo vilivyo bora” alisema Bw. Anyitike.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango kutoka Shirika la Water Aid, Abel Duganga amesema kutokana na kukosekana kwa mwongozo huo unaopima hali ya maji nchini utendaji wa serikali na wadau ulikuwa ukisuasua,  lakini sasa utawezesha kuwa na vigezo vinavyofanana katika kupima na kuwa na takwimu sahihi.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Sekta (DSC) Dkt. Andrew Komba ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha usafi wa Mazingira Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Stephen Kiberiti akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Andrew Komba wa pili kutoka kushoto katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya.
Wadau wa masuala ya Afya na Usafi wa mazingira wakifuatilia kwa ukaribu taarifa kutoka kwa mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) katika mkutano wa ufunguzi wa Mwongozo wa Taifa wa Huduma za maji na usafi wa mazingira katika vituo vya Afya uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.


GAMBO AWAASA WATAALAM WA UGAVI NA UNUNUZI KUZINGATIA UADILIFU KATIKA KAZI ZAO

0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewaasa wataalam wa ununuzi na ugavi kuzingatia maadili katika kazi zao za kila siku ili kuleta ufanisi katika maeneo wanayotumikia. Bwana Gambo ameyasema hayo wakati akifunga kongamano la nane la wataalam wa ununuzi na ugavi lililofanyika mkoani Arusha kwa muda wa siku mbili.

Awali mwenyekiti wa PSPTB Sr. Dr. Hellen Bandiyo amemhakikishia mkuu huyo wa mkoa kwamba wao kama wataalam wa ununuzi wanao mchango mkubwa sana katika kuhakikisha malengo ya serikali ya awamu ya tano ya kuelekea uchumi wa viwanda yanafanikiwa.

“Ni jukumu la wagavi kuzingatia maadili katika maeneo ambayo tumeaminiwa ili kumsaida rais wetu Dr. Magufuli kuweza kuifikisha nchi yetu katika uchumi wa viwanda, na sisi kama wataalam wan chi hii ni lazima tujione tuna deni katika ustawi wa chi yetu” alisema Dr. Bandiyo.

Gambo aliwaasa wataalamu hao kuhakikisha wanazingatia weledi na kuitumia taaluma yao vizuri kwa ustawi wa taasisi zilizowaajiri, “Taaluma ya ugavi na ununuzi ni zaidi ya kwenda dukani na kununua, inakwenda mbali zaidi ya hapo inahitaji weledi na uadilifu ili kuleta matokeo chanya katika maeneo yetu ya kazi kwa ustawi mzuri wa taifa letu” Mhe Gambo alisema.

Aidha moja kati ya changamoto alizozipokea Mkuu wa Mkoa ni pamoja na baadhi ya waajiri kuwatumia wataalam wa manunuzi ambao hawajasajiliwa na bodi hiyo ambapo Mhe Gamboa amewataka kwa kuanzia wawasilishe orodha ya waajiri hao waliopo mkoani kwake ili aone namna ya kuwashughulikia kwa kua kufanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu za nchi yetu.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza na wadau katika kongamano la nane la wataalam wa ugavi na ununuzi lililofanyika jijini Arusha wa muda wa siku mbili.
Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dr. Hellen Bandiyo akizungumza katika kongamano la nane la wataalam wa ununuzi na ugavi lililohitimishwa jijini Arusha.
Mhe Gambo akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa kongamano la nane la wataalam wa ugavi na ununuzi.

BOHARI YA DAWA (MSD) YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KATI 2017-2020

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa pili kulia), Mganga Mkuu wa Serikali, Mohamed Kambi Bakari ( kulia) wakisaini hati ya mkataba maalumu wa utendaji kazi (Performance Contract) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ( kulia). Wengine wanao shuhudia tukio hilo ni Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daud Msasi na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Ilangwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akimkabidhi hata hizo za mkataba Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akikata utepe kuashiria uzinduzi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akihutubia kwenye uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD)imezindua Mpango Mkakati wa Kati 2017 – 2020 ili kuongeza kasi ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini. 

Akizindua mpango mkakati huo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya ameipongeza MSD kwa kuandaa upya mpango huo ambao wamejikosoa na kuboresha maeneo muhimu ili kuendana na vipaumbele vya serikali na mahitaji ya wananchi wa Tanzania, hususan vituo vya Afya vya Umma.

Maeneo hayo muhimu ni pamoja na Kujitegemea kifedha, kuuhuisha Mnyororo wa Ugavi, Kuboresha mfumo wa Tehama, Matumizi yenye tija ya Rasilimali Watu, Utawala na Ushirikishwaji wadau.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya ameingia mkataba maalumu wa utendaji kazi (Performance Contract)na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu ili kuhakikisha utekelezwaji wa haraka wa Mpango mkakati uliozinduliwa.

Aidha katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema atahakikisha Mpango Mkakati 2017-2020 unatekelezwa ambapo kila Mkurugenzi na Mameneja wa MSD wameingia mikataba inayopimika ya utendaji kazi. 

Bwanakunu aliongeza kuwa ufuatiliaji wa utendaji utafanywa kupitia Ofisi maalumu ya kusimamia utekelezaji wa mikakati ya MSD(Strategic Management Office)Tayari kila Mkurugenzi na mameneja wa MSD wamesaini mkataba kutekeleza Mpango Mkakati huo wa Kati.

SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO YA WANAWAKE

0
0
Serikali imesaini Mkataba wa makubaliano wa Miradi ya Wanawake Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women). Akitia saini Mkataba huo kwa niaba ya Serikali Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa Mkataba huo unahusu Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Wanawake Watanzania.

Bibi Sihaba Nkinga ameongeza kuwa Mkataba huo umeainisha maeneo ya ushirikiano ambayo ni Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW),Kufanya Mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000, Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/2021).

Aidha Bibi Sihaba Nkinga amesisitiza kuwa Mkataba huo utasaidia kuendeleza jitihada za Serikali ya Tanzania na Wadau mbalimbali katika kufikia Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. “ Makubaliano haya yatasaidia sana katika kusaidia juhudi za Serikali na Wadau kumuwezesha wanawake wa Tanzania kujikwamua kiuchumi na kufikia usawa wa kijinsia”alisema Bibi. Sihaba.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UN Women - Tanzania, Bibi Hodan Addou amesema kuwa pamoja na jitihada zilizofanyika kati ya Shirika hilo na Serikali katika kuwaletea Maendeleo Wanawake, jitihada zingine zitakazofanyika ni kusaidia juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania za kuongeza Ushiriki wa Wanawake katika Uongozi na kutoa maamuzi kwenye ngazi zote.

“Tunaahidi kushirikiana naSerikali katika kumuinua na kumuendeleza mwanamke wa Kitanzania katika kujikwamua kiuchumi” alisema Bibi Hodan. Mkataba huo wa Mwaka mmoja (2017/2018) unalenga kumuwezesha mwanamke wa kitanzania kujiajiri, kujitegemea na hivyo kujikwamua kiuchumi kwa kujiongezea kipato binafsi, familia na taifa kwa ujumla.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Bibi. Hodan Addou (kulia) wakitia saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya Wanawake utakaodumu kwa kipindi cha Mwaka mmoja (2017/2018) katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Desemba 05, 2017.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Bibi. Hodan Addou (kulia) wakikabidhiana Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Miradi ya Wanawake utakaodumu kwa kipindi cha Mwaka mmoja (2017/2018) katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Desemba 05,2017.

ASILIMIA 62 YA MRADI WA DAWASA WA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI UMEKAMILIKA: WAZIRI KAMWELE

0
0
 Waziri wa Maji na Umwagilkiaji, Mhandisi Isack Kamwele, (katikati), Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), Mhandisi Romanus Mwang'ingo, (kulia), na Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS Limited ya India wakionyesha furaha wakati Mheshimiwa Waziri na ujumbe wake walipotembelea moja ya maeneo ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji jijini Dar es Salaam na Pwani, kwenye ujenzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji la Makongo, Desemba 5, 2017
 Waziri Mahandisi Kamwele, (kulia), Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mwang'ingo, (wakwanza kushoto) na wataalamu wengine,m wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja, wakati Mheshimiwa Waziri alipotembelea mradi wa ujenzi wa tenki Makongo juu.
 Waziri Mhandisi Kamwele, (Kushoto), akifurahia jambo na Meneja Uhusiano na Jamii wa DAWASA, Bi. Neli Msuya, wakati Waziri alipotembelea eneo la utandazaji mabomba huko Malamba Mawili.
Mhandisi Kamwele, akiongozana na wafanyakazi wanaofanya kazi ya kutandaza mabomba huko Malamba Mawili.

KANGI LUGOLA AITAKA KAMPUNI YA MADINI YA NYARUGUSU KUWALIPA FIDIA WANANCHI

0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola ,akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita wakikagua eneo ambalo lilipasuka na kupeleka maji ya sumu kwenye maeneo ya mashamba ya wananchi. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola akiangalia baadhi eneo ambalo limepasuka. (PICHA NA JOEL MADUKA)

Ekari 270 za mashamba ya wakulima kwenye kijiji cha Ziwani Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita zimeathiriwa na Sumu iliyotoka kwenye Bwawa la kuhifadhia Kemikali lililopasuka kingo zake na maji kusambaa kwenye mashamba hayo.

Hali hiyo imemlazimu Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bw Kangi Lugola kuitaka kampuni ya Madini ya Nyarugusu inayohusika na suala hilo kuwalipa fidia wananchi 57 ambao mazao yao yameathirika.

Awali Bw Lugola aliagiza muwekezaji huyo akamatwe kutokana na kile alichodai kuwa ni uvunjifu wa sheria za utunzaji wa mazingira mgodini hapo na kwamba uongozi wa mgodi huo ulimzuia Afisa Mazingira wa Wilaya ya Geita Bi Hellen Eustace kutekeleza majukumu yake baada ya kufika mgodini hapo kukagua namna wanavyozingatia utunzaji mazingira

Bw Kangi alisema Mwekezaji haruhusiwi kuendelea na shughuli anazozifanya na kufunga mgodi huo hadi watakapotekeleza mambo waliyoelekezwa

Mkurugenzi wa Nyarugusu Mine Company Bw Fred Masanja amesema kusimamishwa kwa shughuli zao kunaweza kuathiri ytendaji wao kwa kuwa Tani Laki moja na 20 hawataweza kuzizalisha na hivyo watapata hasara ya zaidi ya Sh Milioni 600 hadi 700. Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola akizungumza na wananchi ambao mashamba yao yameathirika kutoka na sumu ambayo imeeharibu mazao yao pamoja na viumbe hai. 

UNESCO LAUNCHES A CAMPAIGN WITH THE MAASAI IN NGORONGORO TO REDUCE FEMALE GENITAL MUTILATION

0
0
UNESCO, in close collaboration with the Ngorongoro District Council and the Council of Masaai traditional leaders, will conduct a large campaign to intensify efforts to address Female Genital Mutilation (FGM)in Ngorongoro, particularly during the FGM high season of December 2017 when girls go home from school and parents take the opportunity to circumcise them. The session is a continuation of a similar campaign held in June 2017 where trained campaigners managed to rescue four girls who were in the verge of being mutilated in Ngorongoro district. 

The December campaign will consist of three clusters: 1.A School-Based Campaign, targeting students, teachers, and school-parent committees in 28 schools (4 secondary); 2.A Community-Based campaign, targeting mostly parents and caretakers in 29 selected villages in Loliondo division through parent/caretakers village/sub-village sensitization meetings. 

3.A Public Campaign through the Loliondo FCommunity Radiwhere a series of programmes will be broadcasted engaging community leaders, law enforcers, medical officials, religious leaders, former ngaribas (circumcisers) and young people. Expected to reach around 70,000 people, the campaign will kick-off with a 2-day orientation workshop in Wasso on 5 and 6December 2017. The workshop will bring together 65 campaigners and facilitators composed by district and ward officials, Maasai spiritual leaders and Maasai leaders to guide them on how best to deliver key messages to the targeted populationas well as organize for sheltering girls in need. In the Maasai community, the practice of female genital mutilation is deeply rooted in cultural practices and customary beliefs, part of the ritual passing from childhood to adulthood. According to district health statistics, in 2015, 90% (1,375) of the1693 Maasai women who gave birth at health facilities were circumcised. 

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015/16 indicates that Arusha ranks third nationally on the regions where FGMis practised, with a41% prevalence, right after Manyara and Dodoma. Since 2015, UNESCO has been collaborating with government and traditional leadersin Ngorongoro district to strengthen the capacities of community-based structures to address sexual and reproductive health related issues including FGM & early marriage, facing girls and young women, as well as promoting girls education with a particular focus on school retention. Using the socio-cultural approach, UNESCO’s initiatives has gained community support and achieved notable impact including change of mind-set of some traditional leaders and more than 30 Ngaribas who are now strong advocates against the practice.

Maelezo ya awali (PH) katika kesi inayomkabili Afisa Msaidizi wa Forodha wa TRA kusomwa Januari 11, 2018

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Maelezo ya awali (PH) dhidi ya Afisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi anayekabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo la kukutwa akimiliki magari 19,  mali isiyolingana na kipato chake yatasomwa Januari 11, 2018.

Jenipher alipaswa kusomewa maelezo hayo ya awali leo lakini Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter alieleza mahakama ni hapo kuwa bado hawajamaliza kuiandaa. Na kuomba ipangwe tarehe nyingine

Hakimu Huruma Shaidi anayesikiliza kesi hiyo ameahirisha hadi Januari 11, mwakani  itaanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa  kati ya Machi 21,2016 na Juni 30,2016  jijini Dar es Salaam  akiwa  mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19.

Nagari hayo ni   Toyota RAV4, Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Viz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota Wish na  Toyota Mark X.

Mengine ni Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown,  Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry yote yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na kipato chake halali.

Pia anadaiwa kikutwa akiishi maisha ya kifahari  yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.

WATAALAM SEKTA YA MADINI WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO GGM

0
0
Wataalam kutoka Taasisi za Serikali zinazohusika na Sekta ya Madini ndani na nje ya nchi pamoja na Wakufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Mkufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI), Colleen Crystal (kulia) akizungumza na wataalam wa Madini wa Tanzania na nje ya Tanzania wakati walipofanya ziara ya mafunzo katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) .
Wataalam wa Madini wa Tanzania na nje ya nchi wakiangalia eneo ambalo uoteshaji wa miti umefanyika baada ya uchimbaji madini kukamilika lengo likiwa ni kuhifadhi mazingira mara baada ya shughuli za uchimbaji madini kukamilika katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) .
Mkufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI), Colleen Crystal (kushoto) akizungumza na Wataalam wa Madini wa Tanzania na nje ya Tanzania wakati walipofanya ziara ya mafunzo katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) .

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAMA SALMA KIKWETE ATAKA MASHINDANO YA MABUNGE EAC KUDUMISHA UDUGU NA USHIRIKIANO

0
0
 Mbunge wa Bunge la Tanzania ambaye ni Mke wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikikwete akikagua timu ya Bunge la Tanzania iliyocheza na timu ya Bunge la Afrika Mashariki katika mashindano ya mabunge ya nchi za Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mama Salma alihimiza mashindano hayo kuwa kielelezo cha kudumisha udugu na ushirikiano wa nchi za jumuiya hiyo. 
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Mama Salma akikagua kikosi cha Bunge la Afrika Mashariki
 Kikosi cha timu ya Bunge la Tanzania
Kikosi cha timu ya Bunge la Afrika Mashariki

KILIMANJARO WAPONGEZWA KWA KUZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI

0
0
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua rasmi Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kilimanjaro huku Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto), Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira (wa pili kushoto) pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour (kulia) wakishuhudia tukio hilo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi.

MKOA wa Klimanjaro, umepongezwa kwa kuitikia agizo la Rais John Magufuli la kutaka kila mkoa ubainishe fursa za uwekezaji zilizopo na kuandaa mwongozo wa uwekezaji.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Joseph Kakunda katika hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Kilimanjaro uliondaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Akimwakilisha Waziri wa Nchi wa Ofisi hiyo Selemani Jafo, Naibu Waziri huyo alisema kwamba agizo la Rais ambalo limelenga kuweka mikakati mahsusi ya kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda.

Akitoa salamu za pongezi kwa Mkuu wa mkoa, Mh. Anna Mghwira Naibu Waziri Kakunda alisema wakati mkoa wa Kilimanjaro unatekeleza maagizo, serikali kuu nayo inaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ili kuvutia wawekezaji mbalimbali. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mh. Joseph Kakunda akitoa hotuba wakati wa kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro kwa niaba ya Waziri wa Nchi wa Ofisi hiyo, Mh. Selemani Jafo (hayupo pichani) kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la NSSF mjini Moshi, mkoani humo.

Akizungumzia Mwongozo huo Naibu Waziri alisema kwamba kazi ya kubaini fursa za uwekezaji katika miradi mbalimbali yenye faida siyo tu kwa wawekezaji pekee bali pia kwa taifa letu kupitia kodi na upatikanaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa kila eneo la nchi.

Alisema kazi iliyofanywa na mkoa huo ina maana kubwa kwa kuwa sasa inakuwa rahisi kwa wawekezaji wawe wa ndani au nje kujua namna ya kuwekeza katika mkoa wa Kilimnjaro kwa kuzingatia mahitaji yao na namna rasilimali watu na miundombinu ilivyo.

Alisema agizo la Rais la utengenezaji wa mwongozo unakwenda sanjari na ubainishaji na uandazi wa maeneo ya uwekezaji ili yanapotakiwa yapatikane hima. Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mh. Joseph Kakunda (katikati) kutoa hotuba ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa ufadhili wa UNDP katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Moshi. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha S. Amour. 

Aliutaka mkoa huo kuutangaza mwongozo wao kwani biashara ni matangazo katika maeneo mbalimbali ya kimataifa na ya wawekezaji katika masoko ya hisa kwa njia ya kielektroniki ili wavune utayari wao wa kukaribisha uwekezaji.

Kakunda alisema kwamba mkoa huo kwa asili unaweza kabisa kuvutia wawekezaji. Kinachostahili kufanywa kwa sasa ni kuhakikisha kauli mbiu ya Kilimanjaro ya Viwanda, inawezekana chukua hatua inatekelezwa kwa vitendo.

Akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Mh. Anna Mghwira alisema kwamba Mwongozo huo utafanyiwa kazi na matunda yake yataonekana wakati taifa linaelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Alisema mkoa huo una rasilimali za kutosha kuwezesha wawekezaji mbalimbali kutekeleza adhma ya kuwa na viwanda vidogo na vya kati vinavyotumia rasilimali kutoka mkoani.

Aliwashukuru wataalam wa ESRF waliwezesha kupatikana kwa muongozo huo na wafadhili ambao ni UNDP.

Naye Dk Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ambayo ndiyo ilipewa jukumu na Mkoa wa Kilimanjaro kufanya utafiti na uchambuzi wa kina ili kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa, aliupongeza mkoa wa Kilimanjaro kwa kuona umuhimu wa kuwa na mwongozo wa uwekezaji.

Aidha katika hotuba yake hiyo alisema kuwa taasisi yake ilitengeneza sehemu tatu za taarifa ambazo zote zililenga kutoa uwanda mpana kwa wawekezaji kuwa na taarifa muhimu za uwekezaji katika mkoa wa Kilimanjaro.
 Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Mbaga Kida akitoa taarifa kuhusu uandaaji wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Kilimanjaro ulioandaliwa na taasisi yake kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) katika hafla iliyofanyika mjini Moshi kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF. 


Alisema katika hotuba yake kwamba ESRF ilifanikiwa kuandaa ripoti tatu ambazo ni Ripoti ya Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials Report), Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities Report) pamoja na Mwongozo wa Uwekezaji ambao Mkoa umezindua rasmi leo.

ECOBANK YABORESHA MIUNDOMBINU YA MAJI SHULE YA MSINGI HANANASIFU JIJINI DAR

0
0
Shule ya Msingi Hananasifu, iliyopo katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeepukana na dhahama ya kuweza kupata magonjwa ya mlipuko kama vile Kipindupindu baada ya Ecobank kuboresha miuondombinu ya maji shuleni hapo.
Kifuatia uwekwaji wa miundombinu hiyo bora pia, Ecobank imeweka tanki maalumu ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa Huduma ya maji safi na salama  katika vyoo na maeneo mbali mbali shuleni hapo yenye uhitaji wa maji kwa wanafunzi na walimu.
Aidha benki hiyo imetoa vitabu pamoja na kukabidhi zawadi mbali mbali kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la sita walioshika nafasi ya kwanza hadi ya tatuu
Akizungumza wakati wa hafla ya kufungua Kisima hicho leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank, Mwanahiba Mzee amesema,  msaada huo utasaidia shule hiyo kupata maji safi na salama na dhamira yao kubwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu  nchini kwa kuboresha miundombinu.
"Tuliguswa sana baada ya kupewa taarifa kuwa shule hii inawanafunzi 728 lakini miundombinu ya maji imeziba na kubakia sehemu moja tu ambayo inatumiwa na shule nzima, vyoo havina maji na hivyo imekuwa changamoto ya kiafya kwa wanafunzi na walimu, tukaona in vyema kusaidia na kuokoa afya za watoto, amesem Mzee.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Aiddah Uisso amesema walikuwa wakikabiliwa na chanhamoto kubwa ya maji kwani kwa idadi kubwa ya wanafunzi waliopo shuleni hapo, huduma ya maji na salama ni muhimu sana.
" Kwa msaada wa maboresho ya miundombinu yaliyofanyika kwa sasa tunuhakika wa maji safi na salama kwa walimu na wanafunzi.  Vitabu  pamoja na zawadi vilivyotolewa kwa wanafunzi bora, kutaongeza hamasa kwao kufanya vizuri zaidi.
 Mkurugenzi wa Mtendaji Wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akikata utepe kuashiria kumaliza uwekaji wa miundombinu ya maji safi na salama kwa kukabidhi mabomba yaliyojengwa katika  shule ya Msingi Hananasifu, kulia mwenye nguo nyeusi ni Mwalimu Mkuu Wa Shule hiyo, Aida Uisso wakishuhudiwa na baadhi wa ya wafanyakazi wa benki hiyo, walimu na wanafunzi.
 Mkurugenzi wa Mtendaji Wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza na walimu pamoja na wafanyakazi wa Benki hiyo baada ya kumaliza uwekaji wa miundombinu bora na tanki maalumu la maji katika shule hiyo ili kurahisisha usambazaji na upatikanaji wa maji safi na salama shuleni hapo. Pembeni yake ni Afisa Elimu manispaa ya Kinondoni, Mikidadi Azizi akifuatiwa na Diwani wa kata ya Hananasifu, Ray Kimbita.
 Mkurugenzi wa Mtendaji Wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee (kulia) akikabidhi msaada wa vitabu vya kiada kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Hananasifu, Aida Uisso iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Hananasifu iliyopo katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, darasa la kwanza hadi la sita waliofanya vizuri katika mitihani yao wakiwa wameshikilia zawadi zao walizozawadia na Ecobank kwa ufaulu huo.

SERIKALI YATAKA UMILIKI WA HATI MOJA YA UMILIKI WA UWANJA WA NDEGE WA DAR ES SALAAM

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kuweka utaratibu kwa wamiliki wa viwanja ndani ya uwanja wa ndege kuondoa ili kuwa na hati moja ya uwanja kwa kumilikiwa na mamlaka hiyo.

Hayo aliyasema leo Naibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta  Nditiye wakati alipotembelea uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Kampuni mbili ambazo zina hati katika uwanja wa ndege ni Tanzanair pamoja na Puma Energy ambazo zilipata ardhi kwa taratibu.

Amesema Mamlaka ndiyo ndiye ina mamlaka ya kuwa na hati ya ardhi pasipokuwepo kwa kampuni kuwa hati ya umiliki ndani ya uwanja wa ndege.

Mhandisi Nditiye amesema nyumba  59 ambazo ziko katika uwanja wa ndege na zimekubali mamlaka ifanye utaratibu wa kutwaa eneo hilo.

Aidha ametaka TAA kuwa karibu kwa moja kwa moja na puma energy wakati wanachukua mafuta pamoja kuweka katika ndege ili serikali iweze kupata mgawo wake vizuri na sio kuendelea kuchukua takwimu.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Richard Mayongela amesema kuwa suala la umiliki wa hati watafatilia katika wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Amesema mameneja wote nchini wa uwanja wa ndege kuweka alama za mipaka na atakayeshindwa kufanya hivyo bora akapisha ili kuweza kuondokana na migogoro ya ardhi na wananchi.
 Naibu wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta  Nditiye akizungumza na Menejimenti ya viwanja wa ndege nchini (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius  Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Richard Mayongela akizungumza juu ya utekelezaji wa maagizo ya Naibu wa Waziri wakati alipotembelea uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta  Nditiye akipata maelezo kuwa Naibu Meneja wa Ghala la Mafuta la Puma Energy katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela  katika ghala la mafuta la Puma Energy wakati Naibu waziri alipofanya ziara katika uwanja wa mwalimu Julius Nyerere.
Sehemu kalakana ya Tanzanair katika uwanja wa ndege wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Viewing all 109609 articles
Browse latest View live




Latest Images