Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA, AENDESHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akizungumza na  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird leo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akimsindikiza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017.
w4, w5 na w6:  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawari  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017.

PICHA NA IKULU

WADAU WALAMBA NONDOZZZ JIJINI DAR LEO

$
0
0
WANAFUNZI 28 wamehitimu shahada za uzamili Utawala wa Biashara na Biashara Kimataifa katika chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma , Utafiti na Ushauri, Dk. Imanuel Mzava amesema shahada ya uzamili wa Utawala wa Biashara na Biashara Kimataifa inatolewa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Biashara ya Kimataifa ya nchini India (Indian Institute of Foreign Trade)

Amesema kuwa shahada hiyo ilinza kutolewa mwaka 2000 na hadi kufikia leo, wanafunzi 600 wamehitimu katika kozi hiyo na wameendelea kupokea wanafunzi wengine wengi.

Mzava amesema kuwa kuanzishwa kwa shahada hiyo nchini kwa ushirikiano wa Taasisi ya India kumewapunguzia gharama wahitaji wa shahada hiyo ambapo walitakiwa wakasome nchini India lakini elimu hiyo hapa hapa nchini kupitia Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Pichani juu ni baadhi ya wanafunzi hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kulamba nondozz zao, leo katika chuo cha IFM jijini Dar es salaam.
 Mdau Alimwene ambaye pia ni mfanyabiashara akiwa na wahitimu wenzake kabla ya kulamba nondozz hizo.
 Mdau Alimwenye akilamba Nondozz yako na hapa akikabidhiwa na Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma , Utafiti na Ushauri, Dk. Imanuel Mzava. 
 Dada Levina Kato wa Mamlaka ya Bandari pia alikuwa ni mmoja wa waliolamba nondozz.
 Mary Massawe pia kutoka Bandari
 Mdau Morgard Lumbanga 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BOHARI YA DAWA (MSD) YAPONGEZWA KWA USAMBAZAJI WA DAWA NCHINI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD), imepongezwa kwa kushinda tenda ya kununua dawa Jumuhiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

Pongezi hizo zimetolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Profesa Lawrence Mseru wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na timu yake wakati wakiwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto walizonazo za upatikanaji wa dawa na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.

"Kwanza tunawapongezeni MSD kwa kufikia hatua ya kununua dawa katika Jumuhiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) hii ni hatua ya kujivunia kama nchi" alisema Profesa Mseru.

Mseru aliongeza kuwa licha ya kuwepo changamoto ndogo ndogo MSD imejitahidi katika huduma ya usambazaji wa dawa hapa nchini hivyo akaomba ushirikiano baina yao uendelee kudumishwa ili kutoa huduma nzuri zaidi ya kuwahudumia wananchi ukizingatia kuwa taasisi hizo zote zinafanya kazi ya Serikali.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI),Respicious Lwezimula alisema kazi kubwa inayofanywa na MSD inapaswa kuungwa mkono kwa kununua dawa na vifaa tiba.

"Tuna kila sababu ya kuwaunga mkono hawa wenzetu kwa kununua vifaa tiba na dawa kutoka kwao badala ya kununua kwenye maduka ya watu binafsi kikubwa tunawaomba bei yao iwe tofauti kidogo" alisema Lwezimula.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amani Malima alisema suala la manunuzi ya dawa na vifaa tiba linachangamoto kubwa lakini MSD wamesaidia sana kuzipunguza kutokana na ushirikiano wanaofanya baina yao na wateja wao hawana budi kupongezwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI) katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto walizonazo za upatikanaji wa dawa na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja katika ziara iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI), Respicious Lwezimula (kulia), akizungumza katika kikao hicho.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (wa tatu kushoto), akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika ziara hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UMOJA SWITCH YAHAMASISHA KUBADILI KADI

$
0
0
Umoja Switch inianzishwa miaka zaidi ya kumi iliyopita ili kuwezesha benki ndogo na za kati kuweza kupata huduma za ATM. Kupitia Umoja Switch benki zaidi ya 27 zinawezesha wateja wao kupata huduma kwenye ATM zaidi ya 250 bara na visiwani.Ili kuongeza usalama na pia kutua fursa ya kuongeza bidhaa zaidi, Umoja Switch ilianza mkakati wa kuhamisha wateja kutoka kwenye kadi za zamani zenye ufito (magnetic stripe) kwenda kwenye kadi mpya za kisasa na zenye usalama wa juu (Chip). 
 Zoezi hili ambalo linaishia mwezi huu wa Disemba mwishoni.Ili kuwazawadia wateja wake hususani wale wenye kadi zenye Chip, Umoja switch imeanzisha droo kubwa inayowezesha wateja kushinda fedha wanazotoa kwenye ATM maradufu,shilingi milioni moja,simu za mikononi au T-shirts za Umoja. Droo hii ni kwa wateja wenye kadi mpya ambao wanatumia ATM za Umoja popote Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja Danfold Mbilinyi alisema “ Lengo kuu la umoja ni kusogeza huduma za kibenki kwa Watanzania wengi zaidi popote Tanzania. Tunafurahi kuwa tumeweza kufika maeneo mengi Nchini na bado tunalenga kuongeza kasi ya ubunifu na usogezaji wa huduma zetu.
Kuboresha ubora wa kadi zetu ili kuongeza usalama na pia kutoa fursa zaidi ya ubunifu ni ishara tosha kuwa Umoja Switch inalenga kuwa msharika madhubuti wa Maendeleo ya Tanzania hususani sekta ya kifedha. Tunawakaribisha wateja wetu na hata ambao si wateja wetu kubadilish kadi au kufungua akaunti kwenye benki yeyote mshirika ili nao washinde kwenye droo hii kubwa“.

SERIKALI KUBORESHA KIVUTIO CHA UTALII CHA ENEO LA BARABARA YA LAMI INAYOPITA JUU ZAIDI KUTOKA USAWA WA BAHARI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akiongozwa na Meneja wa shamba la Miti Kawetire, Arnorld Shoo kukagua moja ya eneo katika shamba hilo ilipopita barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari wakati wa zaira yake ya kikazi jana mkoani Mbeya. Alisema Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.
Bofya kitufe cha PLAY kuangalia VIDEO

Na Hamza Temba, Mbeya
........................................................
Serikali imesema itaboresha mazingira ya kivutio cha utalii cha barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi kutoka usawa wa bahari kuliko barabara zote nchini ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii na kuongeza idadi ya watalii na mapato.


Hayo yameelezwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga baada ya kutembelea shamba la miti la Kawetire wilayani Mbeya na kujionea sehemu ya barabara ya lami inayopita katikati ya shamba hilo katika mlima Kawetire kwenye safu za milima ya Mbeya.


Eneo hilo la barabara hiyo ambayo hupitisha magari kutoka Jijini Mbeya kwenda katika Wilaya ya Chunya na Mikoa ya Singida na Tabora lina urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari katika Latitude 08’ 35 S na Longitude 33’ 25 E.


“Hatutaki ule utalii wa kutegemea wanyamapori pekee, hii sasa ni sehemu ya aina nyingine ya utalii ambayo ni lazima tuiboreshe tuweke kibao kizuri tuweke mazingira mazuri pamoja na kukitangaza ili watanzania na watalii kutoka nje waweze kutembelea hapa,” alisema Hasunga.


Alisema ili kufikia lengo liliwekwa na Serikali la kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni mbili mwaka 2020 na milioni 8 mwaka 2025 vivutio vyote vya utalii vilivyopo nchini vitatambuliwa, kuimarishwa na kuviwekea miundombinu itakayowavutia watalii kuvitembelea.


Aidha aliuagiza uongozi wa shamba hilo kushirikiana na wakala wa huduma za barabara –Tanroads katika kuboresha mazingira yanayozunguka eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka bango la kisasa la kutambulisha eneo hilo, kujenga bustani na maeneo rafiki ya kupumzikia kwa ajili ya kuwavutia watalii kutembelea eneo hilo na kupiga picha.


Mbali na kivutio hicho aliuagiza uongozi wa shamba hilo kutobomoa majengo ya kale yaliyotumiwa na wakoloni katika shamba hilo na badala yake yatumike kwenye utalii wa mambo ya kale sambamba na utalii wa misitu ya kupandwa inayopatikana pia katika shamba hilo.


Hata hivyo alisema kupitia mradi wa REGROW wa kuendeleza utalii kanda ya kusini Serikali imepokea mkopo wa masharti nafuu wa dola za Kimarekani milioni 150 sawa za zaidi ya bilioni 340 za kitanzania kutoka benki ya dunia kwa ajili ya kusaidia kuboresha miundombinu ya vivutio vya ukanda huo.


Kwa upande wake Meneja wa shamba hilo, Arnorld Shoo alisema eneo hilo la barabara limekuwa ni kivutio cha kipekee cha utalii katika shamba hilo ambapo pia hupata mapato kupitia watu na vikundi mbalimbali ikiwemo wanakwaya na wanafunzi ambao hufika eneo hilo kwa ajili ya kupiga picha za kumbukumbu.  

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) na Meneja wa shamba la Miti Kawetire, Arnorld Shoo wakiangalia bango linaloonesha eneo katika shamba hilo ilipopita barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari wakati wa zaira yake ya kikazi jana mkoani Mbeya. Alisema Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.

MAGAZETI YA JUMANNE LEO DECEMBER 5,2017

HDIF YAFUNGUA RASMI MASHINDANO YA MWISHO YA MAWAZO CHALLENGE

$
0
0
 Kiongozi msaidizi wa HDIF  Joseph Manirakiza akifungua rasmi mshindani hayo ya mwisho kwa timu 12 za  madkatari wanafunzi wanaoshindanishwa ili kupata timu 10 zitakazo pata seed fund toka HDIF.
 Timu ya Afya Plus iliyoa huruma ya kufanya vipimo vya urefu uzito BP na Kisukari katika eneo la tuko.
 Baadhi ya tiny zilizofika fainali toka mchakato huu ulipoanza na mawazo zaidi ya 350 mpaka kufikia 12 zilizoingia fainali.

MADEREVA WAACHE KUENDESHA VYOMBO VYA MOTO BILA YA TAALUMA WALA LESENI - RC NDIKILO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani Mkoani hapo, iliyozinduliwa na kufanyika viwanja vya Mailmoja, Kibaha.
Kaimu kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Pwani, Salum Morimori akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani Mkoani hapo, iliyofanyika viwanja vya Mailmoja, Kibaha. (picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MKUU wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo, amewaasa baadhi ya madereva kuacha kujiingiza kwenye biashara ya usafiri wa vyombo vya moto ikiwemo bodaboda bila kwenda kwenye mafunzo ya udereva na kupata leseni kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria za usalama barabarani. Amesema wapo baadhi ya madereva wanaoendesha vyombo hivyo kwa kujifunza kwa wenzao kwa masaa kisha kuingia barabarani suala ambalo ni kuhatarisha maisha ya abiria wanaowabeba.

Akizindua wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani humo katika viwanja vya Mailmoja, mhandisi Ndikilo alisema ajali nyingi husababishwa na makosa ya kibinadamu. Alisema kati ya makosa hayo ni pamoja na yanayosababishwa kwa makusudi na madereva hao ikiwemo kuendesha huku wakiwa hawana leseni. Mhandisi Ndikilo alieleza kuwa, pia kuendesha wakiwa wametumia vileo ,kupishana pasipo tahadhali (overtaking),uchovu wa kuendesha masafa marefu na kuendesha vyombo vibovu.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

RC Wangabo aiagiza SUWASA kuwakatia maji wenye madeni na wao kulipa deni la Milioni 348 wanalodaiwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo ameiagiza Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA) kuwakatia maji wateja wenye madeni sugu ili waweze kulipa madeni yao wanayodaiwa na taasisi mbalimbali za serikali nchini. Amesema kuwa uendeshaji wa Mamlaka hiyo utaendelea kuwa mgumu endapo wataendelea kuwafumbia macho wateja wanaowadai na kushauri kuanza kuangalia namna ya kutumia kadi za “pre- paid” (malipo ya kabla) katika huduma hiyo ya maji ili kuzuia madeni yatokanayo na malipo baada ya matumizi.

“lazima muwabane walipe madeni, ni kama umeme kama mtu halipi Kata, na huku kata maji, kama umewekwa utaratibu basi uheshiumiwe huo utaratibu, nimesikia kwenye taafifa hapo kwamba kuna upungufu wa fedha makudsanyo madogo na matumizi makubwa na wakati huo huo mna madeni makubwa na watu hawalipi, kata,” Mh. Wangabo alisisitiza.

Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara yake ya kwanza kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA) ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo pamoja na kuufahamu kwa kina mradi wa Maji safi na usafi wa mazingira katika miji saba nchini Sumbawanga ikiwemo, chini ya MDG – Initiative unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na Serikali ya Ujerumani wenye thamani ya Bilioni 31. Aidha ameendelea kuwasisitiza Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Manispaa pamoja na vyombo vya usalama kuhakikisha vyanzo vya maji vinahifadhiwa na kupiga marufuku wale wote wanaofanya shughuli za kibinaadamu katika vyanzo vya maji na kuwachukulia hatua wale wanaokiuka sheria hiyo ya mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa SUWASA Hamis Makala amesema Mamlaka hiyo inadai taasisi za kiserikali Shilingi Milion 69 na pia inadai watu binafsi shilingi milioni 250 huku Mamlaka hiyo ikiwa inadaiwa shilingi milioni 100.6, na kuongeza kuwa miongoni mwa changamoto wanazozipata ni kukauka kwa vyanzo vya maji.

“Hadi Novemba mwaka 2017, SUWASA inadaiwa Milioni 100.6 kutoka kwa wadaiwa wake, mgawanyo wa madeni ni; Madawa ya Maji Shilingi Milioni 14.5, TRA Shilingi Milioni 13, EWURA Shilingi Milioni 6.8, Fidia Shilingi Milioni 32, TANESCO Shilingi Milioni 17, Mita za Maji Shilingi milioni 6, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Shilingi Milioni 11 kwaajili ya hati miliki,” Makala alifafanua.

Halikadhalika Makala alisema kuwa deni hilo limekuwa kubwa zaidi baada ya mkandarasi Herkin Builders kudai Shilingi Milioni 247.6 kama riba ya kucheleweshewa malipo ya kujenga mradi wa dharura wa maji safi Sumbawanga kati ya mwaka 2009 hadi March 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kaunda suti ya Blu) akitaka ufafanuzi wa mchoro wa mradi wa maji taka unaotumika katika Manispaa ya Sumbawanga kutoka kwa Mkurugenzi wa SUWASA Hamis Makala (Kushoto) alipofanya ziara katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA).
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akitaka ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi wa SUWASA Hamis Makala (Kulia) wa namna maji machafu yanavyobadilishwa na kuwa safi ili kuendelea kutumika alipofanya ziara katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA).
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (katikati) wakitembelea mradi wa maji taka yanayobadilishwa na kuwa safi ili kuendelea kutumika. katika eneo hilo lenye ekari zaidi ya 100 lililopo Manispaa ya Sumbawanga alipofanya ziara katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA).
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyenyoosha kidole) akitaka maelezo kutoka kwa mmoja wa wataalamu wanaoendesha mitambo ya kusafishia maji ili na hatimae kuwafikia wananchi alipofanya ziara katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA).
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo pamoja na viongozi wengine wakiendelea kukagua mradi wa maji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA).

HEINEKEN® LAUNCHES AMSTEL BEER IN THE TANZANIAN MARKET

$
0
0
General Manager for Heineken East Africa, Mr. Uche Unigwe (second from left) with various stakeholders during the official launch of Amstel lager in Tanzania.

HEINEKEN Tanzania today officially announced the launch of premium beer brand AMSTEL into the Tanzanian market. Speaking at the launch event in Dar Es Salaam, HEINEKEN East Africa General Manager Uche Unigwe said the introduction of AMSTEL was advised by the growing demand by Tanzanians for a different brand of quality beer in the market.

“The decision to introduce AMSTEL into the Tanzanian market is informed by our research that shows our target consumer enjoys a classier lifestyle in their everyday pursuit of attainable luxuries”. “This provided a great opportunity for us to expand our portfolio of products thus we brought in AMSTEL to meet this demand”, he said
Uche noted “Premium domestic beer drinkers now have the option of socializing without sacrifice with a beer that instils the confidence of a premium brand choice without losing taste or image.” The distinctive, golden AMSTEL beer with its mildly bitter taste and excellent quality has become well known around the world, beyond the borders of its native Netherlands. Today AMSTEL is available in over 100 countries. We proudly welcome this new gem to the Tanzanian market.

This entry by AMSTEL will add momentum in transforming HEINEKEN East Africa’s existing business across the country by extending its footprint, increasing scale and further strengthening its brand portfolio” said Michael Mbungu, Country Manager HEINEKEN Tanzania. He added, “AMSTEL is a winning proposition for retailers and on-premise operators as it offers an imported alternative to their domestic premium beer selection.

HEINEKEN TANZANIA, through the AMSTEL Brand will also participate in a series of in-country partnerships and events to further cement AMSTEL’s winning proposition. Additionally, we are the official sponsors of the Europa League and we plan on bringing the momentum of the beautiful game to the region, as you are aware the Europa League is growing”, he added.

With a brand heritage that spans way over a century, AMSTEL aims to encourage consumers to enjoy their drink and at the same time advocates responsible drinking. Amstel is available at retail outlets countrywide where Kenyans will get to experience it in a 330ml bottle and a 500ml can.

General Manager for Heineken East Africa, Mr. Uche Unigwe (right) delivers keynote speech during the official launch of Amstel lager in Tanzania. Looking on is Country Manager for Heineken Tanzania Michael Mbungu.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 04.12.2017

Miss Universe Tanzania alalamikia matokeo ya mashindano ya kimataifa

$
0
0
Miss Universe Tanzania, Lilian Erica Maraure  amelalamikia hatua ya majaji ya kutomuingiza hata katika hatua ya16 bora ya fainali hizo richa ya kuongoza katika kura za mitandao.

Lilian ambaye ni mtangazaji wa TBC international, alisema hayo mara alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere alisema kuwa miaka yote, warembo wanaongoza katika kura za mitandao upata nafasi ya kuingia katika hatua ya fainali tofauti na mwaka wake.

Alisema kuwa ameshangazwa hatua ya majaji ya kuwaingiza katika hatua ya 16 bora warembo ambao kuwenye kura za mitandao hawafanya vizuri na kumuacha wewe.

“Natambua kuwa maamuzi ya majaji ni ya mwisho, lakini nahoji hatua iliyochukuliwa ya kuacha kuingia hatua ya 16 bora na hata kwenye fainali pamoja na kupigiwa kura nyingi sana na kuongoza,” alisema Lilian.

Katika mashindano hayo, Mrembo wa Afrika Kusini, Demi-Leigh Nel-Peters alitwaa taji hilo. Pamoja na matokeo hayo,Lilian alisema kuwa amepata uzoefu wa kutosha mbali ya kupata mikataba kadhaa ya kufanya maonyesho ya mavazi na ofa ya kusoma nchini Marekani.

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communication, Maria Sarungi ambaye pia ni mratibu wa Taifa wa mashindano hayo, alisema kuwa wanayachukulia matokeo hayo kama changamoto na kuangalia zaidi mashindano yajayo.

“Ni kweli kuwa matokeo yanashangaza, hatujawahi kulalamika katika mashindano ya nyuma, safari hii tulihamasisha wadau watupigie kura nyingi, lakini matokeo ndiyo kama yalivyokuwa,” alisema Maria.

Maria alisema kuwa  wanasubiri kuambiwa lini mrembo ataenda Marekani kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho ya mavazi na mkataba wa kusoma katika fani ambayo ataichagua.
Miss Universe Tanzania (kushoto) akizungumza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere. Anayefuatia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communication, Maria Sarungi na mwakilishi wa Shirika la Ndege la Ethiopia.

TBA YATHIBITISHA KUTUMIA BILIONI 10/- UJENZI WA HOSTELI ZA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM (UDSM)

WANANCHI MKOANI SIMIYU WATAKIWA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya taifa (NIDA) linaloendelea mkaoni humo. Wito huo umetolewa na Afisa Tawala Wilaya ya Bariadi ndg. Rutaihnwa Albert ambaye pia amewataka watendaji wa Kata pamoja na wasimamizi kuweka utaratibu mzuri wa wananchi Kusajiliwa pindi wanapofika kwenye vituo vya Usajili.

Aidha wananchi wametakiwa kufika kwenye vituo vya usajili wakiwa na nakala (photocopy) ya viambatisho vyao muhimu vinavyo hitajika kuwasajili ambavyo ni Cheti cha Kuzaliwa, Pasi ya Kusafiria (Passport), Vyeti vya Elimu ya Msingi na Sekondari, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha Bima ya Afya, Nambari ya Mlipa Kodi (TIN No.) na Kitambulisho cha Mpiga kura pamoja na kuzingatia taratibu za usajili pindi wanapokuwa kwenye vituo.

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa sasa linaendelea katika mikao 15(kumi na tano ya Tanzania) ambapo kwa mkoa wa Simiyu zoezi linaendelea kwa Kata za Senani, Mwamanenge na Ipililo.
Wananchi mkoani Simiyu wakiwa katika foleni kusubiri kuchukuliwa alama za kibaiolojia baada ya kukamilisha zoezi la kujaza fomu za maombi ya Kitambulisho cha Taifa.
Mwananchi wa kijiji cha Ditima akiwa katika meza ya Mwenyekiti wa Mtaa akisubiri fomu yake kukaguliwa na kusainiwa ili aweze kwenda kuchukuliwa alama za kibaiolojia zinazojumuisha kupigwa picha, kuweka saini na kuchukuliwa alama za viganja(finger print).
Mmoja wa wananchi akijaza fomu ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa wakati Mwenyekiti wa mtaa wa Ditima akichambua fomu walizojaza wananchi na kuwapatia ili wakashiriki katika hatua ya pili ya Usajili ikiwa ni kuchukuliwa alama za kibaiolojia.

VIDEO: MAKALA MAALUM YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA 12 WA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII ULIOFANYIKA NOVEMBA 06-09,2017 DODOMA


MAJENGO YA MABWENI YA DKT MAGUFULI NI SALAMA - CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

WIZARA YA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA UFUNGAJI MIGODI

$
0
0
Wizara ya Madini kupitia Kitengo cha Mazingira kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa kutoka nchini Canada (CIRDI) wameanza kutoa mafunzo ya ufungaji wa migodi  kwa wataalam kutoka Taasisi za Serikali zinazosimamia Sekta ya Madini ndani na nje ya nchi. Mkuu wa Kitengo cha Mazingira katika Wizara ya Madini,   Gidion  Kasege amesema kuwa wataalam hao watapata mafunzo kuhusu ukokotoaji wa mahesabu ya gharama za ufungaji migodi, usimamizi wa maji migodini na jinsi ya kutengeneza sehemu ya kuhifadhia mabaki ya uchenjuaji (mining tailings).

Alisema kuwa, hii ni mara ya pili kwa Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa wataalam hao wa Madini na kwamba Awamu hii imeshiriksha nchi nyingine za Afrika ili wataalam hao waweze kubadilishana uzoefu na kujifunza mafanikio na changamoto ambazo nchi hizo zinapata katika shughuli za ufungaji wa migodi. Alieleza kuwa nchi zinazohudhuria mafunzo hayo ni Tanzania, Kenya, Namibia na Ethiopia, ambapo mafunzo yanatolewa kwa njia ya nadharia na vitendo katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita  (GGM) na Buzwagi uliopo mkoani Shinyanga.

Naye, Afisa katika Ofisi ya Madini mkoani Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu ameeleza kuwa kupitia mafunzo hayo wataalam wataongeza uelewa katika shughuli za usimamizi wa migodi nchini na hivyo kuhakikisha kuwa migodi inafuata taratibu zote zinazotakiwa wakati wa usitishaji wa shughuli zao nchini. Alisema kuwa kupitia changamoto ambazo nchi nyingine wamepata katika shughuli hizo za madini, itawasaidia kuwa makini zaidi wa utekelezaji wa shughuli hizo nchini.

Kwa upande wake, Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Madini, Innocent Makomba, alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wataalam kwani yanaongeza uelewa wa masuala yanayopaswa kutekelezwa kabla ya ufungaji wa migodi ikiwemo suala la kushirikisha jamii inayozunguka migodi kabla ya kufanyika kwa maamuzi.

" Tunajifunza kuwa ni muhimu kushirikisha jamii kwani  wao wanaweza kuamua kuwa maeneo ambayo uchimbaji umeshafanyika yatengenezwe kwa ajili ya kufanyia shughuli nyingine kama uvuvi, kilimo au hata kuwa makazi ya watu na kupitia mafunzo haya tumeona mifano ya jinsi nchi nyingine zilivyotekeleza suala hilo," alisema Makomba.

Vilevile, Makomba alisema kuwa mafunzo hayo yamewaongezea uelewa katika suala utengenezaji wa sehemu za kuhifadhia mabaki ya uchenjuaji (mining tailings) ili zisilete madhara kwa wananchi au mazingira.
Wataalam wa Madini kutoka Tanzania na Ethiopia wakifuatilia mafunzo ya ufungaji migodi yaliyokuwa yanatolewa na wakufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI).
Mkufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI), Colleen Crystal akitoa mafunzo kuhusu uhifadhi wa mabaki ya uchenjuaji (mining tailings) kwa wataalam wa Madini wa Tanzania na nje ya Tanzania.
Wataalam wa Madini kutoka nchini Tanzania wakifuatilia mafunzo ya ufungaji migodi yaliyokuwa yanatolewa na wakufunzi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya nchini Canada (CIRDI).

Wataalam wa Madini kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa katika mafunzo ya ufungaji migodi yaliyoratibiwa na Wizara ya Madini na Taasisi ya Kimataifa kutoka nchini Canada (CIRDI).

ILI KUPUNGUZA AJALI BARABARANI; MADEREVA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU HURIA SINGIDA

$
0
0
Madereva wa vyomo vya moto hasa bajaji na bodaboda wamewahimizwa kujiunga na chuo kikuu huria ili waweze kujiendeleza kielimu na kuboresha huduma zao, ambapo kwa kufanya hivyo watasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa wito huo juzi wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi cha Mjini Singida. 

Amesema masomo ya chuo kikuu huria humwezesha mtu kujiendelea kwa kupata elimu bora bila kuathiri shughuli zake za kila siku hasa za kujipatia kipato. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba akiimba na kikundi cha burudani huku Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akicheza katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya Singida Mjini.

“Dereva wa bodaboda, bajaji au mkazi yeyote mkoani kwetu, tusiridhike na elimu tuliyonayo, kumbukeni elimu haina mwisho. Hivyo tutumie chuo chetu hiki cha huria kujiendeleza kielimu. Tukiwa na wasomi wengi mkoa wetu kwa vyovyote   lengo la kuwa na uchumi wa kati na chini ya viwanda utalifikia kwa haraka”, amesema.

Dkt Nchimbi amwataka madereva wa vyombo vya moto kutii na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na sio tu kuendeshwa na kamera za barabarani.

“Baadhi  ya madereva wa vyombo vya moto, hawaheshimu kabisa sheria za usalama barabarani, wanaendeshwa na  kamera. Siku moja yupo dereva mmoja wa bodaboda alikuwa mbele yangu, huku akiandika ujumbe kwenye simu yake. Utamaduni huu haufai kwa sababu ni chanzo cha ajali”,amesema Dkt.Nchimbi. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wakazi wa Singida waliojitokeza katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya Singida Mjini.

Aidha amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba kusimamia zoezi la madereva wa bajaji na bodaboda kujiunga na Chuo kikuu Huria.

“Hebu angalia uwezekano wa kuanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya madereva hawa kujiendeleza kielimu. Tunataka ifike siku tuwe na madereva hawa wana diploma au digrii, kwa hili nina imani na wewe utaweza kuwasaidia vizuri”, amesema. 

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema atagharamia safari ya viongozi wa madhehebu ya dini kwa kutoa kiasi cha shilingi laki tano, kwenda kufanya sala maalum kwenye maeneo yaliyokidhiri  kwa vitendo vya ajali. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba akizungumza na wakazi wa Singida waliojitokeza katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya Singida Mjini.

“Karibu kila wilaya ina eneo ambalo ajali haziishi kutokea mara kwa mara. Nina imani Mungu hajanipa mkoa wenye maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajali. Nimekubaliana na viongozi  wangu wa madhehebu ya dini wataenda katika maeneo hayo, na kuomba Mungu atuondolee balaa la ajali za barabarani kwenye maeneo hayo” amesema. 

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amewaagiza viongozi wa madereva wa bodaboda na bajaji, kusimamia vema madereva hao ili wapunguze ajali za barabarani.  Mmoja kati ya wakazi wa Manispaa ya Singida, Njolo Kidimanda, amesema kuwa kuna haja  serikali kuongeza kiwango cha faini kwa madai kiwango kilichopo, hakiwaogopeshi kabisa  baadhi ya madereva. Aidha, Kidimanda ameshauri madereva kuwa mstari wa mbele katika kuchangia damu salama, ili kusaidia majeruhi wa ajali barabarani wenye hitaji la damu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, jumla ya watu 68 wamefariki kutokana na ajali za barabarani kati ya Januari hadi Oktoba mwaka huu. Idadi hiyo imeonyesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na ajali za  barabarani kwa kuwa katika kipindi hicho hicho mwaka jana, watu 152 walifariki.
Kikundi cha burudani wakionyesha ukakamavu katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya Singida Mjini.

VETA WAWATAKA WATANZANIA KUTILIA MKAZO MASOMO YA UFUNDI STADI

$
0
0

Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi stadi VETA Sitta Peter akizungumza na wanahabari kuhusiana na umuhimu wa watanzania kutilia mkazo masuala ya ufundi stadi kwani yana nafasi kubwa ya kujiajiri na kuacha kusubiri ajira kama fani zingine leo Jjini Dar es Salaam.

Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi stadi VETA imewataka watanzania kutilia mkazo masuala ya ufundi stadi kwani uhakika wa ajira ni mkubwa hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda.



Hayo yalisemwa leo wakati wa ziara ya msanii wa vichekesho MC Pilipili aliyekwenda kutembelea chuo hicho ikiwa ni chuo cha tano baada ya kutembelea vyuo vingine vinne tofauti.

Meneja wa Mahusiano wa VETA Sitta Peter amesema kuwa suala la ufundi stadi ni la watu wote na sio kundi maalumu kama watu wanavyodhania na kuliacha nyuma wakisahau kuwa hakuna maendeleo yanayoweza kuja pasipo kuwa na wataalamu wa ufundi.

Peter amesema kuwa matumizi ya ufundi stadi yanasaidia mchango mkubwa sana katika kuinua uchumi, watu wanajiajiri na kuingizia pato taifa pasi na kusubiri kuajiriwa kama fani zingine zinavyokuwa.

"Kwa Tanzania na dunia nzima ufundi stadi soko lake linakuwa kutokana na uhitaji wa wataalamu kuelekea kwenye uchumi wa viwanda na fursa nyingi zinapatikana huko",amesema Peter.

MC Pilipili kwa upande wake amesema VETA wanafanya kazi kubwa sana ya kutoa mafunzo ya fani mbalimbali na amejionea hilo leo katoka vyuo vyote alivyotembelea.

Mc Pilipili aliweza kutembelea sehemu mbalimbali za chuo hicho na kupewa maelezo mbalimbali ya namna kazi za ufundi stadi zinavyoendeshwa.

Msanii wa Vichekesho MC Pilipili akipata maelezo mbalimbali ya namna mafunzo ya ufundi stadi yanavyoendeshwa na Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi VETA leo Jijini Dar es Salaam.

Msanii wa Vichekesho MC Pilipili akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake na kujionea namna Mafunzo ya ufundi stadi yanavyoendeshwa na Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi stadi VETA.


TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU OFISI ZA TBS ZINAZOHUSIKA NA UTOAJI MIZIGO BANDARINI

$
0
0
2017-12-05
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS)
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizotolewa kupitia mtandao wa kijamii (Jamii Forum) kuwa Shirika linadidimiza jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli zinazotaka Mamlaka zinazohusika na utoaji mizigo bandarini kufanya kazi masaa 24.
Shirika limetii agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kufanya kazi masaa 24 bandarini na bandari kavu ambako huduma za kutoa mizigo zinafanyika muda wote, hivyo maafisa wa TBS wanakuwepo muda wote na wateja wanahudumiwa kikamilifu. Pia namba za simu za maafisa wa TBS zimewekwa ubaoni ili kurahisisha utendaji wakati wote.
Pia kwa upande wa bidhaa za mafuta zinazotokana na petroli, sampuli huchukuliwa bandarini mara tu meli inapotia nanga na kupimwa muda huohuo na majibu yanapotoka  hurusiwa kushushwa au kurudishwa zilikotoka endapo zitakuwa zimefeli.
Hata hivyo ofisi zingine za TBS zinazohusika na utoaji mizigo bandarini zilizopo jengo la Diplomat, mtaa wa Mkwepu / Kaluta, Karibu na jengo la TTCL Makao Makuu, jijini Dar es Salaam, zinafanya kazi kuanzia saa 1.30 asubuhi mpaka saa 4.00 usiku, hii ni kuanzia siku za Jumatatu mpaka Ijumaa. Siku za jumamosi ofisi hufunguliwa saa 3.00 asubuhi mpaka saa 10.00 jioni. Endapo mteja atahitaji huduma baada ya muda tajwa, Shirika limeweka namba za simu ili kuwawezesha wateja kuendelea kupata huduma endapo kuna uhitaji.
Shirika linaomba radhi  kwa wateja kutokana usumbufu uliojitokeza siku Jumamosi ya tarehe 2 Desemba, 2017, kwani ofisi  za jengo la Diplomat zilifunguliwa saa 4.00  asubuhi badala ya saa 3.00 asubuhi. Hata hivyo wateja waliofika kuanzia muda huo walihudumiwa  kikamilifu na kuendelea na taratibu zingine za kutoa mizigo bandarini.

Shirika linaendelea na jitihada za kuboresha huduma zaidi kwa wateja, ikiwa ni pamoja na kuingia mkataba na benki ya NMB ili wateja waweze kupatiwa huduma za kibenki bandarini  hadi usiku. Pia kuanzia sasa ofisi  ya TBS katika jengo la Diplomat zitaanza kutoa huduma kuanzia saa 1.30  hadi saa 12.00 jioni  kwa siku za Jumamosi
Shirika litaendelea kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuhakikisha kwamba bandari zetu zinatoa huduma bora na zenye tija kwa taifa letu.
Kwa maelezo zaidi wasilianaj na:
Mkurugenzi mkuu
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
S.L.P. 9524, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2450298/2450206/2451763-6
Nukushi: +255 22 2450959

Hotline:0800 110 827

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images