Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

ASYA IDAROUS KHAMSIN KUFUNIKA SHEREHE ZA UHURU OAKLAND

0
0
Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka 2017 Mama wa mitindo maarufu hapa Tanzania kama Asya Idarous Khamsin, ambaye kwa sasa makazi yake ni nchini Marekani.  Ifikapo December 9th 2017  ataiwakilisha Tanzania kwa kuonyesha mitindo yake kwenye sherehe za uhuru Oakland Carlifonia.

Hivyo tukiwa kama Watanzania ni jambo la kujivunia maana Tasnia ya mitindo imekuwa ni moja kati ya vyanzo vizuri vya kuitangaza nchi yetu. Tunapaswa kuonyesha ushirikiano kwa wabunifu (Designers)  wetu wanao jituma kama Mama yetu Asya Idarous Khamsin na wengineo.

Ukiguswa unaombwa kusambaza ujumbe huu kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wanao penda Fashion  Asante.


KATIBU WA CCM CHA MAPINDUZI MKOA WA RUVUMA AHAPA KUPAMBANA NA WANARUSHWA

0
0

Katibu wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa RUVUMA AMINA IMBO amehapa kuwashukulia hatua kali wanachama wa chama hicho wanaojihusisha na utoaji rushwa wakati wa uchaguzi  ,amesehayo wakati wa kuwachagua viongozi wa chama hicho katika ukumbi wa shule ya WASICHANA SONGEA habari kamili hii hapa video yake.

BASHE ATEMBELEA GEREZA LA WILAYA YA NZEGA,ABAINI MSONGAMANO MKUBWA WA WAFUNGWA,AJITOLEA KUWALIPIA FAINI WOTE WALIOFUNGWA KWA MAKOSA MADOGO

0
0
  Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe amepata wasaa wa kutembelea gereza la Wilaya ya Nzega, ambapo ameongea na Mkuu wa Magereza Bw. Anatory Kyuza  na baadae kujionea msongamano mkubwa wa wafungwa katika gereza hilo.

Aidha, Mhe. Bashe amewalipia wafungwa wote waliokuwa wamefungwa kifungo cha makosa madogo hasa yale ya kushindwa kulipa Faini za kuanzia shilingi elfu Hamsini (50,000) mpaka shilingi  Laki tatu(300,000)  ili kusaidia kupunguza msongamano wa wafungwa katika gereza hilo.

Pia, Mhe. Bashe* alitembelea  shamba la magereza ambapo alikubaliana pamoja na Mkuu wa Magereza kuweka nguvu kwenye kilimo cha Muhogo ambapo Serikali imetoa mbegu bora kwa ajili ya kilimo hicho wilayani Nzega.

Gereza la Nzega limejengwa mwaka 1923 na lina uwezo wa kuhifadhi wafungwa 50 tu lakini sasa linahudumia wafungwa na mahabusu takribani 200.

Kwa upande mwingine, Ili  kuboresha makazi ya askari wa Jeshi la Magereza wilayani Nzega Mhe. Bashe  ameamua kuchangia jumla ya  mifuko ya Saruji 100 na matofali 10,000.  
  Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe amepata wasaa wa kutembelea gereza la Wilaya ya Nzega ambapo ameongea na Mkuu wa Magereza Bw. Anatory Kyuza  na baadae kujionea msongamano mkubwa wa wafungwa katika gereza hilo.
Mhe. Bashe pia alipata wasaa wa kutembelea  shamba la magereza ambapo alikubaliana pamoja na Mkuu wa Magereza kuweka nguvu kwenye kilimo cha Muhogo ambapo Serikali imetoa mbegu bora kwa ajili ya kilimo hicho wilayani Nzega.

WATUMISHI WA UMMA WAKUMBUSHWA UWAJIBIKAJI WENYE TIJA KATIKA MAENEO YAO YA KAZI

0
0
Na Robert Hokororo, Kishapu DC

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Kakunda amewakumbusha watumishi wa umma uwajibika wenye tija katika maeneo yao ya kazi huku akisisitiza kila idara ina umuhimu wake.

Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mh. Kakunda alisistiza kwa kusema mtumishi anapaswa kuyajua vyema majukumu yake anayopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Alisema lazima uthibitishe kuwa unatimiza majukumu yako kwa kutekeleza maagizo yote yanayotolewa pamoja na miongozo yote inayokuwepo, sera, programu za nchi pamoja na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali. 

“Mtumishi lazima ujue kila kitu ‘at a finger tip’ kilichopo katika dawati lake, Mkurugenzi nae anapaswa kujua kila kitu kinachohusu Halmashauri yake. Kama mtu hujui makujumu yako ina maana hata ukienda likizo pengo lako halionekani,” alisema.

Aliwakumbusha wahasibu hasa katika utunzaji nyaraka za mahesabu na wagavi kutimiza wajibu wao kwa umakini kuepuka hoja huku akionya atakayezalisha hoja atajibu yeye mwenyewe kama ambavyo sheria ilivyopitshwa mwaka jana na si Halmashauri kama ilivyozoeleka 

Naibu Waziri pia aliwatasisitiza wahandisi waache mazpea ya kukaa ofisini na kusubiri ripo bali watoke wakague miradi wenyewe na kutembea na nyaraka zinazohusu miradi hiyo badala ya kumuachia Afisa Mipango mwenyewe.

Awali akizungumza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela aliwataka watumishi kujenga utaratibu wa kutembelea wananchi kujua kero zao badala ya kukaa ofisini kusubiri wawafuate.

Alisema kuwa lengo la viongozi wa mkoa ni kumkumbusha kila mtumishi kwenye halmashauri yake anafanya kazi kwa weledi na kutekeleza taratibu na sheria za utumishi wa umma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. George Kakunda akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara yake. Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akitoa neno wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba akifungua kikao kwa ajili ya Mhheshimiwa Naibu Waziri kuzungumza na watumishi. 
Watumishi wa Halmashauri ya Kishapu na viongozi mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.
Naibu Waziri TAMISEMI, Mh. George Kakunda akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kishapu.

KATIBU WA BUNGE AIPONGEZA NHIF

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga (kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Ushauri wa Kiufundi wa Mfuko huo, Aifena Mramba wakati akimueleza jambo.
Na Mwandishi Wetu

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Stephen Kagaigai ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kazi kubwa inayofanya na kwa ushirikiano inayotoa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Bunge.

Amesema NHIF ni taasisi ambayo imekuwa tegemeo kwa afya za Watanzania hivyo akatoa rai kwa wanachama wote na watumishi kuhakikisha wanaulinda Mfuko huo ili uweze kuimarika na kutoa huduma zaidi kwa vizazi na vizazi.

Hayo aliyasema Dar es Salaam jana wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu na baadhi ya Maofisa wa Mfuko waliohudhuria uzinduzi wa Michezo ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. “Huu Mfuko kwa kweli umekuwa ni msaada sana kwetu, nawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayoifanya na kipekee nitoe pongezi zangu kwa namna mnavyoshirikiana na Bunge letu katika kuhakikisha huduma tunapata kama inavyotakiwa,” alisema Bw. Kagaigai.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Konga alisema kuwa Mfuko utaendelea kuboresha na kuimarisha huduma zake ili kila Mwananchi ajivunie uwepo wa Mfuko huu kwa kuwa ni njia bora ya kupunguza gharama za matibabu.

Alisema kuwa Mfuko umeshiriki kikamilifu katika mashindano hayo ya michezo kwa kuhakikisha huduma za awali za matibabu pamoja na vipimo kwa wabunge vinapatikana wakati wote wa michezo.

“Tumeshirikiana na Ofisi ya Bunge kuhakikisha afya za waheshimiwa wabunge zinakuwa imara wakati wote wa michezo na huduma zitatolewa kwa wabunge wote bila kujali nchi aliyotoka kwa kuwa sote tunaunganishwa na Jumuiya hii ya Afrika Mashariki,” alisema Bw. Konga

Alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wananchi watakaofika katika Uwanja wa Taifa kutembelea banda la Mfuko ambalo watapata elimu mbalimbali juu ya huduma zinazotolewa na Mfuko.
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga baada ya uzinduzi wa mashindano ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu Bw. Bernard Konga akisalimiana na wabunge wanaoshiriki nashindano hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga akizungumza na baadhi ya wabunge.

Mahojiano Saidi Kanda - sehemu ya 2- NGOMA

0
0
Kwa kuanzia kama hujawahi kumsikia Saidi Kanda sikiliza wimbo maarufu "Nasikitika " wa Remmy Ongala. Hizo ngoma kali zinapigwa na nguli huyu mzawa wa Bagamoyo. Mwezi huu, Desemba 2017, Saidi Kanda yuko safarini Kenya na Tanzania kushughulikia muziki yake. Anahesabiwa kati ya wapiga ngoma stadi ulimwenguni. Alitunukiwa tuzo ya kwanza ya shirika maarufu la WOMAD - mwaka 1989. Sehemu ya pili ya mazungumzo na Mwanamuziki huyu wa Jadi- Mpiga ngoma mkali - Saidi Kanda- mkazi Uingereza- anazungumzia THAMANI ya Ngoma na vyombo vyetu asilia.

WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WATAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI

0
0
Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini wamesisitizwa kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kusaidiwa. Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa wito huo hivi karibuni Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, kwenye mkutano wake na Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Dhahabu na Vito (Green Garnet) wa Namungo wilayani humo.

  Nyongo alisema dhamira ya Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo kuwa na uchimbaji wenye manufaa kwao na Taifa kwa ujumla na ili kufikia dhamira hiyo ni vyema wakajiunga kwenye vikundi. "Mkijiunga kwenye vikundi itakua ni rahisi kuwafikia kwa pamoja na kuwapatia misaada mbalimbali yenye tija kwenye shughuli zenu," alisema.

Alisisitiza kwamba umoja ni nguvu, na ili mchimbaji awe na uwezo na nguvu kwenye utekelezaji wa majukumu yake inabidi afanye kazi akiwa ndani ya umoja na wenzake. Alisema pale ambapo wachimbaji watakua wamejiunga kwenye vikundi, itakua rahisi hata kwa Taasisi za kifedha kuweza kuwafikia na kuwasaidia ikiwemo kuwapatia elimu ya fedha na vilevile mikopo.

"Nimekuja hapa kuzungumza nanyi ili kubaini changamoto zinazowakabili kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi, na pia ninawaasa mhakikishe mnajiunga kwenye vikundi," alisema. Aliongeza kwamba Serikali ingependa kuona Wachimbaji Wadogo wa Madini wanafanikiwa kufikia kwenye uchimbaji wa Kati na baadaye kuwa Wachimbaji Wakubwa.

Aidha, Wachimbaji hao walimuomba Naibu Waziri Nyongo kuendelea kuwatembelea mara kwa mara ili kuelewa changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi kila inapobidi. Baada ya kuzungumza na wachimbaji hao, Naibu Waziri Nyongo alitembelea Mgodi wa Dhahabu unaomilikiwa na Kampuni ya Germin Exploration ya Namungo huko Ruangwa na kukagua shughuli zinazofanywa na mgodi huo.

Vilevile alitembelea mradi wa kuchimba Madini ya Kinywe (Graphite) wa Kampuni ya PACCO GEMS LTD iliyopo katika vijiji vya Mtondo na Nanjaru wilayani humo ambapo aliahidi kuwasaidia kumaliza tatizo la upatikanaji wa hati ya umiliki wa ardhi wanayohitaji ili mradi uweze kuanza mara moja.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza alipotembelea Mgodi unaomilikiwa na Kampuni ya Germin Exploration.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akipata maelezo ya Mradi wa kuchimba Madini ya Kinywe (Graphite) wa Kampuni ya PACCO GEMS LTD iliyopo katika kijiji cha Mtondo na Nanjaru wilayani humo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alipotembelea na kuzungumza na Wachimbaji kwenye Miradi ya kuchimba Madini ya Dhahabu na Kinywe Wilayani Ruangwa.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akipata maelezo ya Mradi wa kuchimba Madini ya Kinywe (Graphite) wa Kampuni ya PACCO GEMS LTD iliyopo katika kijiji cha Mtondo na Nanjaru wilayani humo.

MWILI WA MWANAFUNZI WA SCOLASTICA ALIYEUAWA WAAGWA MKOANI KILIMANJARO, WENGI WAJITOKEZA KUUSINDIKIZA

0
0
Msafara wa Magari ya waombolezaji na lililobeba mwili wa marehemu Humphrey Makundi ukipita eneo la Marangu mtoni wakati ukitoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuelekea kanisa la KKKT Usharika wa Mamba Kwa Makundi wilaya ya Moshi.
marehemu Humphrey Makundi alikuwa ni Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo ambaye inadaiwa alipotea katika mazingira tatanishi Novemba 6, na baadaye mwili wake ukaokotwa kando ya mto Ghona ambao uko umbali wa mita 300 kutoka shuleni hapo, na mwili wake kudaiwa kuzikwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mjini, mkoani Kilimanjaro. 

Mwili huo ulifukuliwa baada ya siku kadhaa kwa amri ya Mahakama ili kufanyiwa uchunguzi na kubainika ni mtoto huyo.
 

Ibada ya kumuombea marehemu Humphrey Makundi imefanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Kwa Makundi .
Ndugu ,Jamaa na Marafiki wakipita mbele ya jeneza kutoa Heshima zao za mwisho katka kanisa la KKKT Usharika wa Kwa Makundi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Humphrey Makundi.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimfariji Baba mzazi wa Humphrey,Bw Jackson Makundi.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akitoa heshima za mwisho katika ibada ya marehemu Humphrey Makundi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKALA YA SHERIA: UTARATIBU UNAOSTAHILI KUFUATWA KABLA YA KUFUTIWA UMILIKI WA ARDHI

0
0
Na Bashir Yakub.

Yafaa kujua utaratibu unaotakiwa kufuatwa kabla ya kufutiwa hati miliki ya ardhi (nyumba/kiwanja). Unapojua utaratibu huu ndipo unapojua kama ulionewa au hapana. Na kuonewa ni pamoja na kukiuka utaratibu. Na kukiuka taratibu yoyote ya kisheria kunabatilisha mchakato wa kufutwa kwa hati yako na kutakiwa kurudishiwa eneo lako au fidia.

Makala yaliyopita tulieleza mambo ambayo ukifanya unahesabika kukiuka masharti ya umiliki wa ardhi na ni hapo unapoweza kufutiwa umiliki. Leo tuangalie utaratibu wa kufuta umiliki ikiwa imethibitika kuwa tayari umekiuka masharti hayo. Sheria namba 4 ya 1999 , Sheria Ya ardhi imeeleza utaratibu wa kufuta umiliki wa ardhi.

UTARATIBU.
1.Ni lazima uwe umekiuka masharti au moja ya masharti uliyopewa wakati unakabidhiwa ardhi/hati kwa mujibu wa kifungu cha 48 ( 1) cha Sheria ya ardhi. Usikubali kufutiwa umiliki ikiwa hujakiuka sharti/masharti ya umiliki uliyopewa, labda iwe vinginevyo.

2. Baada ya kuwa umekiuka masharti yafaa upewe taarifa maalum( notice) kwa mujibu wa kifungu 48(2). Ni taarifa inayoeleza masharti ya umiliki uliyokiuka na onyo la kufutiwa umiliki. Taarifa hiyo ni ya siku 90(miezi mitatu). Taarifa hiyo utapewa wewe mmiliki na kila mwenye maslahi katika ardhi hiyo mf, mpangaji, mrehani nk. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI 

RC MAKONDA, ABUBAKAR BAKHRESA WATEULIWA KAMATI YA MAANDALIZI YA FAINALI AFCON U-17

0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Bakhresa Limited, Abubakar Bakhresa wameteuliwa kwenye Kamati za Maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) mwaka 2019 nchini.

Wakati Makonda, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Abubakar Bakhresa ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Usafiri na Malazi.
Uteuzi huo umefanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais wake, Wallace Karia na Makonda atasaidiwa na Makamu Mwenyekiti, Yusuph Singo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Michezo, Wajumbe Sunday Kayuni, Leslie Liunda, Nassoro Idrissa ‘Father’, Mohamed Kiganja ambaye ni Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Mhandisi Davis Shemangale.
Bakhresa atakuwa chini ya Mwenyekiti Mhandisi Ladislaus Matindi na Wajumbe Aziz Abood, Ahmed Mgoyi, Ahmed Shabiby, Dk. Maige Mwakasege Mwasimba na Shebe Machumani.

TFF pia imeunda Kamati ya Masoko na Habari chini ya Mwenyekiti, Kelvin Twissa na Wajumbe Mwandishi wa Habari za Michezo na Katibu wa zamani wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas, Dk. Omari Swaleh wa  Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mkurugenzi wa AMG Group Iman Kajula na Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando.
Kamati nyingine ni ya Fedha na Mipango itakayokuwa chini ya Mwenyekiti, Doto James na Wajumbe Mohamed Dewji, Dk. Seif Muba, Bernard Lubogo, Paul Bilabaye, Jacquelline Woiso na Cornel Barnabas.

Kamati ya Uratibu Utalii itakuwa chini ya Mwenyekiti, Dk Khamis Kigwangala na Wajumbe , Allan Kijazi Devotha Mdachi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke, Hoyce Temu, Leah Kihumbi ambaye ni Mkurugenzi wa Sanaa na Makamu Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani.

Kamati ya Itifaki, Mwenyekiti ni Mndolwa Yusuph ambaye ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Wajumbe Filbert Bayi, Mkurugenzi Uwanja wa Ndege JNIA, Happiness Luangisa, Alex Makoye Nkenyenge na Alhaji Idd Mshangama.
Kamati ya Tiba na Udhibiti wa Dawa za Kusisimua Misuli itakuwa chini ya Mwenyekiti, Profesa Lawrence Museru, Dk. Paul Marealle, Dk. Edmund Ndalama, Dk. Christina Luambano, Daktari Mkuu wa Hospitali ya Temeke na Hiiti Sillo.
Kamati ya Sheria na Taratibu Mwenyekiti ni William Erio na Wajumbe Dk. Damas Ndumbaro, Edwin Kidifu, Ally Mayai na Khalid Abeid.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mwenyekiti ni  IGP Simon Siro na Wajumbe Michael Wambura, CP. Andengenye wa Zimamoto, CP. Lazaro Mambosasa wa Polisi Kanda Maalum ya Dar-es-Salaam, Mkuu wa Askari wa Usalama Barabarani, TISS na Jonas Mahanga.
Kamati ya Rasilimali Watu itakuwa chini ya Mwenyekiti Dk. Francis Michael, Allan Kijazi, Wane Mkisi, Juliana Yassoda na Gerald Mwanilwa.

Kamati hizo ndogo zitakuwa chini ya Kamati Kuu inayoongozwa na Mwenyekiti Dk. Harrison Mwakyembe (MP); Makamu Mwenyekiti wa Leodegar Tenga na Mtendaji Mkuu wa Kamati hiyo ni Henry B. Tandau.

IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UDHIBITI WA VIASHIRIA HATARISHI MAHALA PA KAZI

0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bw. Maercel Katemba akifungua Mafunzo ya Mfumo wa Udhibiti wa Viashiria Hatarishi Mahala pa Kazi kwa watumishi wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii yanayofanyika katika katika Ukumbi wa VETA mkoani Dodoma, tarehe 4 Desemba, 2017.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bibi Mchome akitoa neno la utangulizi kwa washiriki wa Mafunzo ya Mfumo wa Udhibiti wa Viashiria Hatarishi Mahala pa kazi yanayoendelea ukumbi wa VETA mkoani Dodoma.
Mwezeshaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Udhibiti wa Viashiria Hatarishi Bw. Dickson Rusage akielezea mwitikio chanya uliooneshwa na Wizara/ Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kutekeleza Mfumo huo miongoni mwa Wizara zilizoanza utekelezaji wake.

BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA

0
0
Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo lake katika bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali. Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.

Mshindi wa fainali alijishindia shilingi milioni moja taslimu pamoja na pikipiki wakati mshindi wa pili akipata shilingi laki tano na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi laki tatu.

Akizungumza baada ya fainali, Bonnah alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwisho wa mwaka ili kuinua michezo jimboni hapo na kusema mshindi wa mwaka huu atapata nafasi ya kwenda Dodoma kushindana na timu ya wabunge.
Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda Kimanga kabla ya mchezo wa fainali.
Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa katika picha ya pamoja na EFM jogging club

Mbunge Bonnah Kaluwa akionyesha umahiri wa kupiga danadana akitazamwa na wachezaji wa zamani wa Taifa Stars.

Usiku wa Kitendawili kufufua upya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk John Pombe Magufuli anataraji kuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ utakaofanyika Ijumaa hii Disemba 8, 2017 kupitia ‘Usiku Wa Kitendawili’ mjini Dodoma.

akizungumza na Waandishi wa habari Msanii  wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi cha Sanaa cha Mpoto Theatre Gallery na wadau wa sanaa za Ubunifu ndio wataouratibu usiku huo wa Kitendawili kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Sanaa utamaduni na Michezo.

Usiku wa Kitendawili ulianzishwa baada ya msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kuachia wimbo ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo na kuanzisha mjadala kuhusu uzalendo.

Akiongea na wadau wa sanaa katika Maandalizi ya Kampeni hiyo ya Kitaifa itayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere, Mrisho Mpoto amesema kampeni hiyo ina lengo la kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza ndani ya Taifa letu.

Alisema mambo ambayo yatayozingatiwa katika kampeni hiyo ni pamoja na kudhubiti na hatimaye kukomesha kabisa mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa Umma, kuongezeka kwa tuhuma za rushwa, kuibuka ufisadi, ubadhilifu wa mali za Umma pamoja kuongeza hari ya kufanya kazi na Uzalendo.

“Usiku wa Kitendawili utatumika kama jukwaa la kuwaleta pamoja watanzania pamoja na viongozi wao ili kukumbushana kuhusu wajibu na kujadili mustakabali wa Taifa. Kutakuwa na vivutio mbalimbali pamoja na wimbo maalumu kutoka kwa wasanii maalumu Mwaka Huu,” alisema Mpoto.

Aliongeza,”Tumekuja kuunadi Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ kwasababu tunaamini Uzalendo na Utaifa lazima uwepo ili kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili kuunga mkono juhudi za Raisi Dkt. John Pombe Magufuli za kujenga Taifa lenye Uzalendo, Utu, Weledi na Uadilifu uliotukuka. Mimi ni mzalendo ndio maana hata kwenye hizi harakati nipo toka nimetoa wimbo wangu wa kwanza, ukiangalia nyimbo zangu zote ni za kuonganisha jamiii 120 za watanzani,”

 “Naamini kwenye kufanya kazi ambayo itawafanya watanzania pamoja na kizazi kijacho kitambue kuna watu ambao walifanya kazi kubwa kwenye hili taifa, kuacha alama ambazo haziwezi kufutika katika maisha ya historia ya nchi hii, kwa sababu hivi vyote ambavyo vinaenda kufanywa ni kufufua upya na kuiweka pamoja mitazamo ya watanzania ili kujenga Taifa la Wazalendo na Wachapakazi kuiga nyayo zilizoachwa na hayati Baba wa Taifa,” alifafanua zaidi.

Mpoto amesema lengo kuu la maadhimisho hayo kuambatana na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa kuanzia mwaka 2018 ni kutumia jukwaa hilo kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kujenga na kuendeleza Utaifa.

Alisema baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo wiki hii huko Dodoma, itafanyika kwenye mikoa yote nchini na itasimamiwa na Kamati za Utamaduni chini ya Uwenyekiti wa Mkuu wa Mkoa na  Wilaya.

Introducing "Ni Yeye" (Official Video) Prince Meddy

Introducing "Mungu Ni Mungu Tu" Official Video by Christopher Mwahangila


ujenzi wa mradi wa maji Halmashauri ya Kondoa Mji waendelea vyema

0
0
Ujenzi wa tanki la maji katika mradi wa maji Kichangani ukiendelea katika Halmashauri ya Kondoa Mji
Mkandarasi wa mradi wa Kichangani akimwonyesha Mkurugenzi mabomba yaliyofika eneo la mradi mtaa wa Tura tayari kwa kutandazwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa Mji Khalifa Kondo mwenye kofia akipokea maelezo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa maji katika mtaa wa Kwapakacha.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa Mji Khalifa Kondo mwenye kofia akishuhudia wananchi wa mtaa wa Kwapakacha wakichota maji kwenye kisima wakisubili kuunganishiwa miundombinu ya maji katika maeneo yao.

MASHINDANO YA NANE YA MABUNGE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAENDELEA LEO UWANJA WA NDANI WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
 Wachezaji wa mpira wa wavu wa Tanzania (jezi ya bluu) na wachezaji wa mpira wa wavu wa Kenya (nyeupe) wakichuana ikiwa ni Muendelezo wa  Mashindano ya Nane ya Mabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoanza jana katika uwanja wa Taifa Mjini Dar es Salaam, Tanzania.
 Wachezaji wa mpira wa wavu wa Tanzania (jezi ya bluu) na wachezaji wa Kenya (nyeupe) wakijiandaa kwa ajili ya kuanza mchezo baina yao uliofanyika leo katika uwanja wa ndani wa Taifa, Tanzania  ikiwa ni Muendelezo wa  Mashindano ya Nane ya Mabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoanza jana katika uwanja wa Taifa Mjini Dar es Salaam, Tanzania.
 Wachezaji wa Timu ya mpira wa wavu wa Tanzania wakijadiliana wakati wa mapumziko wakati wa mchezo baina yao na kenya katika Muendelezo wa  Mashindano ya Nane ya Mabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoanza jana katika uwanja wa Taifa Mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Mashabiki wa Timu ya Tanzania wakishangilia wakati timu ya mpira wa wavu ya Tanzania ikicheza na timu ya mpira wa wavu ya Kenya leo katika uwanja wa ndani wa Taifa, Tanzania katika Muendelezo wa Mashindano ya Nane ya Mabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyoanza jana katika uwanja wa Taifa Mjini Dar es Salaam, Tanzania.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)​

WAKALA WA MAJENGO NCHINI (TBA) YATOA UFAFANUZI BAADA YAKUPATIKANA NYUFA KATIKA HOSTELI ZA CHUO KUKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM).

0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Baada yakuripotiwa kuwa na Nyufa kadhaa katika Jengo jipya la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zilizobuniwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), Desemba 3, 2017, TBA wamefanya ukaguzi katika Jengo hilo nakubaini kuwa nyufa hizo zimetokea kwenye 'Expansion Joint' iliyopo Block A.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga amesema kuwa kwa kawaida katika taaluma ya ubunifu wa majengo, Majengo mapana huwekewa nafasi (Expansion Joint) ambayo huyatenganisha na kuwa sehemu mbili au zaidi ili kuruhusu Jengo kupumua inapotokea kutitia kwa udongo, au kutanuka na kusinyaa kwa udongo kutokana na hali ya hewa.

Mhandisi Mwakalinga amesema 'Expansion Joint' ni sehemu ambayo iantarajiwa Nyufa kutokea, katika ubunifu wa Majengo hayo, amesema kuwa TBA ilizingatia hitaji hilo ambapo kila jengo  (Block) lina jumla ya Expansion Joint tatu (3).

Amesisitiza kuwa Nyufa zilizotokea katika Block A ziko kwenye Expansion Joint, kwa hiyo siyo kwa sababu ya upungufu wa ubunifu au ujenzi bali umetokea katika maeneo yaliyokusudiwa (Expansion Joint).

"Katika ukaguzi wa awali uliofanywa na wataalaamu wa TBA, ilionekana upande mmoja wa ile Expansion Joint, uko vizuri kwani ule uwazi umeonekana kufunikwa na kipande cha ubao bilo kujazwa udongo wa Saruji", amesema Mwakalinga.

"Upande wa pili wa ule uwazi ulijazwa kimakosa na udongo wa Saruji na kuondoa urahisi wa sehemu mbili za jengo kupumua. Upande wa pili wa uwazi uliojazwa udongo ndiyo unaonyesha dasari ya Nyufa zilizojotokeza, kutokana na ripu kwenye ukuta mzima wa sehemu ile kuungana na ule udongo ulioingia kwenye 'Expansion Joint'.

TBA imewatoa hofu watumiaji wote wa majengo hayo kwa kuwaambia kuwa ni salama kwa matumizi yaliyokusudiwa kutokana na kutokea kwa Nyufa za kawaida katika ujenzi wa Majengo na zimetokea sehemu iliyokusudiwa ambayo itafanyiwa marekebisho stahili. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala Majengo nchini (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Nyufa zilizotekea kwenye Jengo la Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Block A) ambazo zilibuniwa na TBA. Kulia ni Mhandisi Mkuu wa TBA, Eng. Jasper Lugemarila.

Mhandisi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Eng. Jasper Lugemarila akionesha baadhi ya Nyufa zilizopo katika Hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Block A).

Baadhi ya Nyufa zilizopo katika Jengo la Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Block A). Ambapo imeripotiwa kuwa ni Nyufa za kawaida na hazina madhara yoyote kwa matumizi.

WABUNGE TUMIENI MICHEZO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA EAC-MAJALIWA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bunge la Tanzania muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi dhidi ya timu ya Bunge ya Burundi alipofungua mashindano ya mabunge ya nchi za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo Desemba 4, 2017. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bunge la Burundi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi dhidi ya timu ya Bunge ya Tanzania alipofungua mashindano ya mabunge ya nchi za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo Desemba 4, 2017. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wabunge wanaoshiriki mashindano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wayatumie kuimarisha ushirikiano.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Desemba 4, 2017) wakati akifungua mechi ya mpira wa miguu iliyozikutanisha timu za Tanzania na Burundi kwenye Uwanja wa Taifa.

Mashindano hayo ya Nane ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yalifunguliwa jana (Jumapili, Desemba 3, 2017) na Spika wa Bunge Job Ndugai

Waziri Mkuu amesema nchi zote zinashiriki mashindano hayo ni  ndugu hivyo ni vema wakayatumia katika kuimarisha ushirikiano wa Mabunge ya Jumuiya hiyo.

Pia Waziri Mkuu amewataka wachezaji hao kuhakikisha kucheza mpira mzuri na wazingatie viwango vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema katika mashindano hayo kila timu inahitaji kupata ushindi, hivyo amewataka wanatumie vizuri ujuzi wao ili waibuke na ushindi.

Katika ufunguzi huo Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Akson, Katibu wa Bunge la Tanzania Stephen Kagaigai.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt.  Harrison Mwakyembe.

Katika mashindano hayo timu ya Tanzania imeibuka kidedea baada ya kushinda magoli matatu na Burundi ilipata magoli mawili.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, DESEMBA 4, 2017.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA 8 LA MWAKA LA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya Wahudhuriaji wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya awali ya Heaven  Moshono Arusha pamoja na walimu wao ambao walikuwa uwanja wa ndege wa Arusha wakati Makamu wa Rais anaondoka Arusha mara baada ya kufungua wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images