Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya wazinduliwa leo mjini Dodoma

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba ambaye pia ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,akizungumza mapema leo mjini Dodoma mbele ya Wadau mbalimbali wa mambo ya Afya,ikiwa ni sehemu ya kuelekea kilele cha uzinduzi wa kampeni ya Unawaji Mikono kwa vituo vya Afya itakayojulikana kwa jina la NIPO TAYARI awamu ya pili,Ambapo katika uzinduzi wa kampeni hiyo itakayozinduliwa rasmi Desemba 7,2017 mkoani Dodoma,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Makamu wa Rais Mama samia Suluh Hassan
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba ambaye pia ni mgeni rasmi akikata utepe kuzindua  Jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma,uzinduzi wa jarida hilo ni sehemu ya kuelekea kilele cha uzinduzi wa kampeni ya Unawaji Mikono kwa vituo vya Afya itakayojulikana kwa jina la NIPO TAYARI awamu ya pili,Ambapo katika uzinduzi wa kampeni hiyo itakayozinduliwa rasmi Desemba 7,2017 mkoani Dodoma,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Makamu wa Rais Mama samia Suluh Hassan.
Mratibu wa Kampeni ya Usafi wa mazingira-wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Anyitike Mwakitalima akizungumza jambo mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo,mapema leo mjini Dodoma,kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa jarida  lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa Njombe,Dkt Buru Mwamasage jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba akimkabidhi Afisa Afya mkoa wa Dodoma,Edward Ganja jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), DktAndrew Komba akimkabidhi Mkurugenzi wa Mipango kutoka shirika la WaterAid -Tanzania Bwa.Abel Dugange  jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa jarida lenye Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira katika vituo vya afya,mapema leo mjini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMATI YA UN KUTETEA HAKI ZA MSINGI ZA WAPALESTINA YAKUTANA NA BALOZI MAHIGA

0
0
Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (wa pili kulia) na wajumbe wengine wa kamati hiyo wakimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (wa kwanza kushoto) kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea.
Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour (katikati) akisaini kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli kabla ya kumkabidhi Balozi Augustino Maiga.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo na Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina alipokutana nayo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour

Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) jijini Dar es Salaam.

MBUNGE VITI MAALUM IRINGA ROSE TWEVE AIBUKA MSHINDI WA PILI MBIO ZA MITA 100 NA 200

0
0
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Rose Tweve (kushoto)  ni Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko baada ya kumaliza mbio katika mashindano ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa  Riadha yaliyoshirikisha wabunge kutoka Kenya na Uganda

Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Iringa Mhe Rose Tweve ameibeba timu ya riadha ya Wabunge wa Tanzania baada ya kuibuka mshindi wa pili wa mbio za mita 100 na 200.

Katika mbio zingine Josepha Komba mbunge wa viti Maalum Tanga aliibuka mshindi wa kwenye mbio za  mita 1500.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Rose Tweve kazini sambamba na Mbunge Zubeda sakura.

Mashindano ya Wabunge ya nane kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yamezidi kuwa na sura mpya kila siku kwa timu zote kujiandaa ili waweze kuibuka na ushindi.

Rose amesema kuwa amefurahi kuweza kushika nafasi ya pili kwenye mbio za mitaa 100 na za mita 200 kwani anaamini mwaka unaofuata atafanya mazoezi kwa sana na kufanya vizuri zaidi.

Amesema kuwa  Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mkoa wenye wanamichezo tegemeo katika timu ya Bunge la Tanzania.

Takribani wabunge  nane wa mkoa wa Iringa wanashiriki kwenye michezo mbali mbali ambao ni Kocha wa timu ya soka ambaye pia mshiriki wa mchezo wa kutembea kwa kasi Walk-race Venance Mwamoto (Kilolo), Mahmoud Mgimwa ( riadha na kuvuta kamba), Menard Kigola (riadha/Kuvuta kamba), Ritha Kabati (netball/volleyball),
Godfrey Mgimwa a.k.a Neymar (soka) ,Rose Tweve (Riadha), Cosato Chumi a.k.a Gazza (soka) na Mchungaji Peter Msigwa-kiungo mshambuliaji (soka)
Wabunge wakifurahi pamoja baada ya kumaliza mbio na wakipongezwa na wabunge wengine.
Mbunge wa Viti Maalum Iringa Rose Tweve akiwa katika pozi kabla ya kuanza kwa mbio.

CCM IRINGA WAPIGA KURA KUCHAGUA UONGOZI MPYA LEO

0
0
Mjumbe wa NEC Mh. Januari Makamba akizungumza na kutoa utaratibu wa wagombea na wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa unaofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa leo Chama cha mapinduzi kimekuwa na chaguzi za ngazi mbalimbali kuchagua viongozi watakaokwenda kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano tutawaletea taarifa zaidi kuhusu matokeo ya uchaguzi huo. 
Wagombea wa nafasi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika uchaguzi hu.
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NEWS ALERT: WANAFUNZI 2,679 WAPATA MIKOPO YA TZS 9.6 BILIONI KUPITIA RUFAA

0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Disemba 5, 2017) imetangaza orodha yenye wanafunzi 2,679 ambao wamepata mikopo ya elimu ya juu yenye thamani ya TZS 9.6 bilioni kufuatia kukamilika kwa uchambuzi wa rufaa zilizowasilishwa na wanafunzi hao.
Kati ya wanafunzi hao, 1,847 ni wa mwaka wa kwanza ambao mikopo yao ina thamani ya TZS 6.84 bilioni na wengine 832 ni wale wanaoendelea na masomo lakini hawakuwa na mikopo katika miaka iliyopita. Wanafunzi hao wanaoendelea na masomo wamepata mikopo yenye thamani ya TZS 2.76 bilioni.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema orodha ya wanafunzi hao na fedha zao zimetumwa katika vyuo walipo wanafunzi hao hivi sasa.
“Hatua hii inafanya jumla ya wanafunzi 33,200 wa mwaka wa kwanza kuwa wamepangiwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya TZS 108 bilioni kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hadi sasa,” amesema Badru na kufafanua kuwa Serikali imetenga jumla ya TZS 427.54 bilioni kwa ajili ya mikopo hiyo kwa mwaka 2017/2018.
HESLB ilifungua dirisha la rufaa kwa siku saba kuanzia tarehe 13 Novemba, 2017 hadi tarehe 19 Novemba, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawakuwa wameridhika na upangaji wa mikopo na kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili.
Wanafunzi waliohamishiwa mikopo yao
Wakati huohuo, Badru amesema HESLB imeanza kuhamisha mikopo iliyokuwa imeelekezwa katika vyuo tofauti na waliko kwa sasa. Mikopo ya wanafunzi 590 wa mwaka wa kwanza yenye thamani ya TZS 1.78 bilioni ambayo awali ilikuwa imepelekwa katika vyuo tofauti na walipo wanafunzi imehamishwa.
“Wanafunzi hao waliohamishiwa mikopo yao ni wale ambao walipangiwa mikopo na kupelekewa fedha zao katika vyuo ambavyo walipata udahili awali, ila baadaye wakaamua kujiunga na vyuo vingine ambavyo nako walipata udahili,” amesema na kuongeza kuwa orodha kamili ya wanafunzi hao pamoja na fedha za wanafunzi hao zimetumwa katika vyuo walipo hivi sasa.
Bodi ya Mikopo inaendelea kupokea orodha za wanafunzi waliosajiliwa katika vyuo mbalimbali na wale wenye mikopo, fedha zao zitahamishiwa katika vyuo walipo katika awamu zijazo.
Mikopo kwa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu
Katika hatua nyingine, Bodi ya Mikopo imesema jumla ya wanafunzi 45 wa shahada za uzamili na uzamivu ambao ni wanataaluma na waajiriwa wa vyuo mbalimbali nchini wamepata mikopo yenye thamani ya TZS 441.4 milioni katika mwaka wa masomo 2017/2018.
Badru amesema leo kuwa mikopo hiyo hutolewa na HESLB kwa wanataaluma hao ili kuvijengea vyuo uwezo wa kitaaluma chini ya makubaliano kati ya Bodi ya Mikopo na vyuo hivyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Abdullah Ibrahim Al-Suwaidi wa pili kutoka (kushoto) aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Balozi Zuhura Bundala wa kwanza (kulia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Abdullah Ibrahim Al-Suwaidi aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Total Momar Nguer mara baada ya kuwasili Ikulu pamoja na ujumbe wake. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kampuni ya Total Momar Nguer mara baada ya kamaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya Total Momar Nguer wa tatu kutoka (kushoto ) aliyeambatana na ujumbe wake mara baada ya kamaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage pamoja na Balozi Zuhura Bundala wa kwanza (kulia). PICHA NA IKULU.

KAMPUNI YA STAR MEDIA (T) LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA UNAIDS KATIKA UTOAJI WA ELIMU NA MATANGAZO KUPITIA KAMPUNI HIYO.

0
0
Kampuni ya Star Media (T) Ltd  imefikia makubaliano na shirika la kimataifa la kupambana na Ukimwi (UNAIDS) katika utoaji wa elimu na matangazo kupitia kampuni hiyo ili kuhakikisha ifikapo 2030 gonjwa la UKIMWI linatokomezwa .
Makubaliano hayo baina ya Kampuni ya Star Media (T) Ltd na UNAIDS yametiliwa saini leo  jijini Dar es Salaam  katika ofisi za Ubalozi wa China na kuhudhuriwa na Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong, wawakilishi wa UNAIDS, Mkurugenzi wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko  pamoja na wawakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Startimes na UNAIDS zimefikia makubaliano ya pamoja  ili kuhakikisha wanafikia lengo la kutokomeza UKIMWI katika ukanda wa Afrika ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Star Media (T) Ltd, Wang Xiaobo amesema Startimes na UNAIDS zitashirikiana pamoja katika kutoa taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Ukimwi ili kupunguza unyanyapaa na kutengwa miongoni mwa waathirika wa virusi vya ugonjwa huo, katika maeneo mbalimbali ambayo kampuni ya startimes tayari inarusha matangazo yake.

 " Tutahamasisha kupima, kulinda na kumaliza unyanyapaa, ugonjwa wa Ukimwi ni adui mkubwa kote duniani na sisi kama startimes tunajisikia fahari kuungana na UNAIDS katika mapambano haya” amesema Wang.
Mkurugenzi wa Startimes Tanzania, Wang Xiaobo pamoja na Mkurugenzi na Mwakilishi wa shirika la kimataifa la kupambana na Ukimwi (UNAIDS) nchini Tanzania,  Dkt.Leopold Zekeng(kulia) wakitiliana sahihi ya makubaliano ili kuhakikisha wanafikia lengo la kutokomeza UKIMWI katika ukanda wa Afrika ifikapo mwaka 2030. Katikati ni Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong.
Mkurugenzi wa Startimes Tanzania, Wang Xiaobo pamoja na Mkurugenzi akipeana mkono na Mwakilishi wa shirika la kimataifa la kupambana na Ukimwi (UNAIDS) nchini Tanzania,  Dkt.Leopold Zekeng(kushoto) mara baada ya kumaliza kutiliana sahihi. Katikati ni Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong.
 Kaimu Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Gou Haodong(katikati) akizungumza na wadau wa Ukikwi pamoja na waandishi wa habari kuhusu kuhusu mchango wa China katika kupambana na gonjwa la Ukimwi nchini Tanzania.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AMZAWADIA MILIONI MOJA ASKARI WA KIKE KWA UTENDAJI KAZI MZURI KAZINI, JIJINI DAR

0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akimkabidhi zawadi ya Sh. Milioni moja(1,000,000) askari wa kike Sajini wa Magereza, Anna Akuny(katikati) kutokana na utendaji wake mzuri kazini aliouonesha katika Gereza la Wanawake Segerea(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Segerea, ACP. Godfrey Kavishe.
Askari wa Kike Sajini Anna Akuny(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) mara baada ya kumkabidhi zawadi ya utendaji kazi mzuri kazini. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Makao Makuu.

Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa ametowa zawadi ya utendaji kazi mzuri kwa askari wa Jeshi hilo Sajini Anna Akuny wa Gereza la Wanawake Segereza leo Desemba 5, 2017 katika Makao Makuu ya Magereza Jijini Dar es Salaam. Askari huyo Sajini Anna amekabidhiwa Sh. milioni moja (1,000,000) na Kamishna Jenerali wa Magereza kutokana na kuonesha utendaji wake mzuri pamoja na nidhamu kazini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa amemtaka askari huyo kutokubweteka na mafanikio hayo bali iwe chachu ya kufanya kazi kwa bidii zaidi. Jenerali Malewa ametoa wito kwa Maafisa na Askari wa Jeshi hilo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo inayotolewa mara kwa mara na Uongozi wa Jeshi hilo.

Hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari huyo imehudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, DCP. Augustine Mboje pamoja na Mkuu wa Gereza Segerea, ACP. Godfrey Kavishe.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO AFANYA ZIARA KATIKA MAMLAKA YA MAWASILIANO NCHINI (TCRA)

0
0
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akisalimiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) alipofanya ziara katika ofisi hizo ili kujitambulisha na kukagua huduma mbalimbali wanazozitoa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa TCRA kuhusu vifaa vya mawasiliano vilivyotumika zamani alipotembelea makumbusho ya Mamlaka hiyo katika ziara ya kujitambulisha na kukagua huduma ya mawasiliano.
  Picha ya pamoja na wafanyakazi wa TCRA

CREDIT SCORING TEAM FROM GROUP CREDIT AGRICOLE OF MOROCCO VISITS TADB

0
0

By Our Reporter,

Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) has received a delegation from Group Credit Agricole of Morocco (GCAM) who will be in country for 11 days mission, from 4th-15th December 2017.

The purpose of this visit is to facilitate TADB to develop Credit Scoring System to be used in scoring small holder’s farmer’s projects as well as implementing the operationalization of the signed MoU that intends to promote productive investments in the agriculture sector and development of agro-industrial value chain in Tanzania and Morocco.

According to the TADB Management, these objectives will be achieved through promotion of financing and support systems, especially for smallholder’s farmers.The delegation from GCAM led by Director of Engineering and Agro business, Mr. Jalal Bouchama, other members include Chief of Agroindustry Department, Mrs. Sanae Benmali, Director of Credit Information System, Mr. Abdessamad Danguir and Ms. Sara Nachid, IT Developer.

TADB and GCAM signed a memorandum of Understanding (MoU) in October 2016.TADB becomes first financial institution in Tanzania to get assistance from GCAM, which aim to enhance agricultural activities and to stabilize rural populations by improving their living standards.

Since its creation, Crédit Agricole of Morocco has committed to agriculture and socio-economic development in rural areas by working in co-ordination with the Moroccan government to to support the agricultural and rural development in Morocco.
TADB Acting Managing Director, Mr. Augustino Matutu Chacha (with red tie) briefs a delegation from Group Credit Agricole of Morocco on the roles and mandates of TADB. The delegation is in the country for 11 days mission.
TADB Acting Managing Director, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) insists something when he meets with delegation from Group Credit Agricole of Morocco. Right is TADB’s Director of Finance and ICT, Mr. Severin Ndaskoi.
A delegation from Group Credit Agricole of Morocco attentively listens to TADB Acting Managing Director, Mr. Augustino Matutu Chacha (not in picture).
Head of delegation from Group Credit Agricole of Morocco, Mr. Jalal Bouchama (left) who is a Director of Engineering and Agro business hints the role of GCAM on agriculture and socio-economic development in Morocco. Right is Mr. Samuel Mshote from TADB.
TADB Management members speak during the discussion with delegation from Group Credit Agricole of Morocco.

WAZIRI JENISTA AKAGUA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA UHURU WA TANZANIA BARA

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikagua maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri leo Mjini Dodoma.
Onesho kutoka katika Kikundi cha Komando wakionesha umahiri wao katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri leo Mjini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri leo Mjini Dodoma.
Gwaride la Mkoloni kutoka Jeshi la Polisi likionesha umahiri wake ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri leo Mjini Dodoma.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wanaoongoza misafara ya Viongozi wakionesha umahiri wao katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo Mjini Dodoma.
Halaiki ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakiunda umbo lililoonesha ramani ya Tanzania wakati wa maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri leo Mjini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bibi Rehema Madenge akimueleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa maandalizi ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Jamhuri leo Mjini Dodoma.Picha zote na Beatrice Lyimo, MAELEZO, DODOMA

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEWA NA BALOZI WA UJERUMANI

0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dkt. Detlef Waechter kwenye ofisi yake ndogo Jijini Dar es Salaam.Mazungumzo hayo yamelenga kuisaidia Tanzania kwenye sekta ya Afya
Waziri Ummy Mwalimu (kushoto) akimuelezea jambo Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dkt. Detlef Waechter kwenye ofisi yake ndogo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia,Wazee na watoto Ummy mwalimu (kushoto) akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dkt. Detlef Waechter kwenye ofisi yake ndogo Jijini Dar es Salaam.Mazungumzo hayo yamelenga kuisaidia Tanzania kwenye sekta ya Afya

RC Wangabo Ashauri Gereza La Mollo Kujikita kwenye Uzalishaji Wa Mbegu Za Mahindi Na kuuza

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amelishauri gereza la kilimo la Mollo kuona umuhimu wa kujikita kwenye uzalishaji wa mbegu ili kuuza na gereza hilo kuweza kujiendesha na kupambana na changamoto mbalimbali zilizopo katika gereza hilo.
Amesema kuwa katika mikoa ya nyanda za juu kumekuwa na shida ya uuzwaji wa mbegu feki na kupelekea malalamikomengi toka kwa wananchi lakini kwa kutumia nguvu kazi iliyopo katika gereza hilo wanaweza kupata soko hilo kama watajikita kwenye uzalishaji huo.

“Tumekuwa tunahangaika mbegu hapa kwa mikoa ya Rukwa na Katavi, tunaweza tukajikita kwenye gereza hili na kuzalisha mbegu kwa wingi kwaajili ya matumizi ya mkoa mzima na majirani, hivyo ndio vitu vya kufikiria, tunaweza kuzalisha mazao lakini hata mbegu pia,” Alisema.

Mh. Wangabo Ameyasema hayo alipofanya ziara katika gereza hilo lililopo kata ya Mollo, Manispaa ya Sumbawanga ili kujionea shughuli za kilimo za gereza hilo ambalo kwa mwaka huu wa mavuno limepata magunia ya mahindi 4058 na hulisha magereza matatu ya mikoa ya Rukwa na Katavi.

Nae mkuu wa gereza hilo ACP John Mwamgunda amesema kuwa gereza linalima mazao ya mahindi ya mbegu nay a chakula kati ya ekari 350 hadi 400 na maharage hulimwa kati ya ekari 20 hadi 30 na bustani ya mboga kati ya ekari 2 hadi 3 na kuwa mpaka sasa wana ziada ya magunia ya mahindi ya chakula 3263 ambayo yanaweza kuhimili hadi msimu ujao wa mavuno.

“Pamoja na kuwa na maeneo hayo vitendea kazi bado ni vichache na baadhi vilivyopo vimechakaa, hivyo tunahitaji kuongezewa vitendea kazi,” Alimalizia.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akisalimiana na maafisa magereza wa gereza la Kilimo Molo alipofanya ziara katika gereza hilo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) pamoja na Mkuu wa Gereza la Molo ACP John Mwamgunda wakikagua ujenzi wa Zahanati mpya ya kisasa itakayotumika kwaajili ya wananchi na magereza ambayo ipo eneo la magereza.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akijadiliana na Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali juu ya ujenzi wa Zahanati mpya ya magereza walipotembelea gereza hilo kujionea shughuli za kilimo zinazofanywa na gereza hilo pamoja na miradi mingine inayofanywa na gereza hilo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia), Mkuu wa Gereza la Molo ACP John Mwamgunda (katikati) na Katibu tawala wa Mkoa wa Rukwa Bernard Makali wakizungukia miradi iliyopo ndani ya eneo la gereza la kilimo la Molo lililopo kata ya Molo Manispaa ya Sumbawanga. 

WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA AWASILI MKOANI DODOMA LEO

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Dodoma wakati alipowasili   kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Desemba 5, 2017, baada ya safari ya Singida, Lindi na Dar es salaam.  Kulia kwake ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mekewe Mary  wakiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Benilith Mahenge wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Desemba 5, 2017. Mheshimiwa Majaliwa amerejea Dodoma  baada ya safari katika mikoa ya Singida, Lindi na Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KILI STARS YAJIFUA TAYARI TAYARI KUWAVAA NDUGU ZAO ZANZIBAR HEROS

0
0
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Ninje leo Jumanne Desemba 5, 2017 ameanza mazoezi maalumu ya kurekebisha upungufu wote uliojitokeza kwenye kikosi chake katika mchezo uliopita.
Stars Mazoezi ya kuruka
Kilimanjaro Stars, ilicheza mchezo wa kwanza dhidi ya Libya Jumapili Desemba 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kenyatta na matokeo yakawa sare tasa katika mfululizo wa mechi za michuano ya Cecafa.
Katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Machakos Academy leo asubuhi, Kocha Ninje ameanza kufanyia kazi namna ya kukaba wakati mpira unapokuwa kwa adui au timu inapopoteza mpira.
Stars Nelson Juma (kulia) na Kelvin Yondani (kulia) wakimzuga Shizza Kichuya.
Baada ya mazoezi hayo Kocha Ninje ameoneshwa kufurahishwa na namna wachezaji walivyoelewa na kufanya kile alichowaelekeza kukifanya ambapo amesema inaonesha dalili nzuri ya kumaliza tatizo hilo lililoonekana kwenye mchezo wa kwanza na Libya.
Katika mazoezi hayo pia walifanya mazoezi ya namna ya kufanya mashambulizi na kupandisha timu.
Stars_ Boniface Maganga (kushoto) akimkabili Amani Kaita (katika) huku Yohanna Mkomola akiwa tayari kutoa msaada.
Kesho wataendelea tena na mazoezi kujiandaa na mchezo unaofuata utakaochezwa Alhamis kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos dhidi ya timu ya Taifa ya Zanzibar.
Stars_ Elias Maguli (kushoto) akipiga hesabu za kumtoka Jonas Mkude
Kilimanjaro Stars ipo kundi A pamoja na timu za Rwanda, Zanzibar, Libya na wenyeji Kenya ambapo kabla ya michezo ya leo katika kundi hilo – Harambee Stars inaongoza kwa kupata pointi 3 katika mchezo wa mwanzo, wakifuatiwa na Libya na Kilimanjaro Stars wenye pointi 1 kila mmoja wakati Zanzibar na Rwanda wakiwa hawana pointi.

Article 1

0
0
Na Shamimu Nyaki – WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania wote kujitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni ya kitaifa ya Uzalendo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 08 Desemba 2017 mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Wizara yake imeamua kuanzisha Kampeni ya Uzalendo ili kuwakumbusha watanzania kupenda,kujali na kuthamini nchi yao kwa kuenzi na kuupenda Utamaduni wa Taifa letu ambao ndio unaounganisha na kutambulisha watanzania.
“Uzalendo wetu umetikisika ni lazima sasa kuamka na kujua kuwa tuna jukumu la kuenzi Uzalendo tuliojengewa na Waasisi wa Taifa letu  wa kupenda nchi yetu na kudumisha Utamaduni wetu”Alisema Mhe. Waziri Mwakyembe.
Aidha amewataka watanzania pia kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha katika maisha ya kila siku kwa kuwa Lugha hiyo ndio inayotambulisha Mtanzania popote anapokuwa pamoja na kuheshimu alama zote za Taifa ikiwemo Bendera ambapo ameagiza matumizi sahihi ya Bendera hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza amesema Kampeni hiyo ni muhimu sana kwa Taifa letu kwakua inalenga kukumbusha jamii Utamaduni wetu ambao ndio unafanya jamii kuwa na uzalendo katika nyanja zote za maendeleo.
“Ili kufikia adhma ya Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda bila kuwa na uzalendo wa kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana.” Alisema Mhe. Juliana.
Mhe. Juliana ameongeza kuwa Wasanii wanahabari na wanamichezo wanajukumu kubwa sana la kuutangaza Kampeni hii lakini pia kuelimisha jamii maana ya Uzalendo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kutenda mambo mazuri yanayoendana na Utamaduni wa Tanzania kwa wao ni kioo cha jamii.
Naye msanii Mrisho Mpoto ameiahidi Serikali kushirikiana nayo katika kuelimisha jamii maana ya uzalendo kupitia sanaa yake ambapo amesema atashirikiana na wasanii wenzake kuandaa nyimbo zitakazowakumbusha watanzania umuhimu wa Uzalendo ili kuwa na Taifa lenye jamii inayotambua maana ya uzalendo kama ilivyokuwa enzi za mababu zetu.
Kampeni ya uzalendo yenye Kauli mbiu “UZALENDO NA UTAIFA,NCHI YANGU KWANZA” ina lengo la kurejesha hali ya watu kupenda nchi yao  kupinga mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa Umma,kuongezeka kwa tuhuma za rushwa,kuibuka kwa ufisadi,matumizi mabaya ya mamlaka na ubaguzi wa aina yeyote ambapo itakuwa inaadhimishwa kila mwaka.

Pix 1
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi (wapili kushoto) akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Mhe. Juliana
Pix 2
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Pix 3
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma leo Jijini Dar es Salaam.

Pix 5
Mjumbe wa kamati ya uzalendo Bw. Mrisho Mpoto (kulia) akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
Pix 6
Mwanamziki mkongwe nchini Bw. John Kitime (aliyesimama) akichangia wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Pix 7
Baadhi ya wadau wa sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Pix 8
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akimkabidhi mshindi wa shindano la Ubingwa wa Dunia uzito wa kati Bw. Ibrahim Class hundi ya shilingi milioni kumi na nane wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

Tigo na WorldRemit washuhudia ukuaji mkubwa katika huduma ya kuhamisha fedha katika akaunti za simu za mkononi Tanzania

0
0
Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit, Andrew Stewart akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni yake na Tigo Tanzania unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi kwenda kwa huduma ya Tigo Pesa. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed.
Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha za Simu za Mkononi wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Hussein Sayed akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni yake na Tigo Tanzania unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi kwenda kwa huduma ya Tigo Pesa. Kulia ni  Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit, Andrew Stewart.
Meneja Uhusiano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni ya Tigo na ile ya World Remit unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi kwenda Tigo Pesa. Kulia ni Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed na Andrew Stewart, Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit .

WorldRemit na Kampuni ya kidigitali Tigo Tanzania wameshuhudia ukuaji wa kasi wa huduma za kuhamisha fedha kwenda katika akaunti za fedha za simu za mkononi nchini Tanzania, taarifa zimebainisha.

Katika kipindi cha miaka miwili cha ushirikiano baina ya kampuni hizi, huduma ya Tigo imebainika kuwa ndiyo huduma ya kutuma fedha inayokuwa kwa kasi zaidi miongoni mwa washirika wa WorldRemit.

Huduma hii inawawezesha Watanzania katika zaidi ya nchi 50 kutuma fedha kwenda katika akaunti za fedha za simu za mikononi kwa haraka. Wamiliki wa akaunti za fedha za simu za mkononi pia wanakuwa na uwezo wa kutuma fedha ndani ya nchi, kununua muda wa maongezi, kulipia ankara au kutoa fedha taslimu kupitia mtandao mkubwa wa mawakala wa Tigo.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MHANDISI ISACK KAMWELE ATEMBELEA MIRADI YA DAWASA YA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI

0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, ameanza ziara ya siku mbili ya kukagua baadhi ya miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji  Safi na Maji Taka, (DAWASA), jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2017.
Katika siku yake ya kwanza ya ziara hiyo, Waziri alitembelea Mradi wa Uboreshaji Mfumo wa Usambazaji maji ambapo kazi zinazofanyika chini ya mradi huo ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji  yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3.0 hadi milioni 6.0, lakini pia ujenzi wa vituo vine(4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa 16 za kusukuma maji, ununuzi wa transfoma  na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji yatakayokuwa na urefu wa kilomita 477.
Mradi huu utanufaisha maeneo ya Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni , Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo,Kitopeni, Ukuni, Kerege, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa maji wa Ruvu Chini.
Aidha maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba,Mbezi, Makuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo yote haya hupata huduma kutoka Mtambo wa Ruvu Juu ambao ulizinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhurim ya Muungani wa Tanzania Juni 21, 2017.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, akiteremka kutoka juu ya tenki la maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo Desemba 5, 2017, wakati wa ziara yake ya siku mbili kukagua miradi ya maji inayoendeshwa na DAWASA

 Mhandisi Kamwele, mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo wakimsikiliza Mkandarasi, wapili kulia), na Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakitembelea eneo la ujenzi wa trenki la kuhifandia maji, Mabwepande nje kidogo ya jijji


 Mhe. Waziri Mhandisi Kamwele, (wapili kushoto), Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo wakimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India.

 Mhe. Waziri Kamwele, (kushoto), akifafanua jambo, wakati akipatiwa maelezo na Mkandarasi kutoka kampunin ya India ya WAPCOS, Mhandisi P.G. Rajani

Taswa SC kukipiga na Saleni FC ya Lugoba

0
0
Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC)  kesho  itacheza mechi maalum ya kirafiki dhidi ya timu ya Saleni FC  kwenye uwanja wa  Saleni, Lugoba.

Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10.00 jioni na imeandaliwa kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya timu hizo mbili.

Mwenyekiti wa Taswa SC Majuto Omary alisema kuwa  maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na timu ya waandishi itaondoka jijini saa 3.00 kuelekea Lugoba, Chalinze.

Majuto alisema kuwa wachezaji wote wa Taswa SC wanatakiwa kuwahi kufika ili kuondoka mapema na kuwahi shughuli nyingine zilizoandaliwa na wakazi wa Saleni kabla ya kuanza kwa mechi hiyo.

Alisema kuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo ambao mbali ya kudumisha ushirikiano, pia utatumika  kuangalia vipaji mbalimbali vya wachezaji wanaoishi katika eneo hilo.

“Tumejiandaa vizuri sana, na kudhihirisha hilo, tumeshinda mechi mbili mfululizo dhidi ya timu ya Polisi Kombaini ambao tuliwafunga mabao  5-0 na juzi tu tumewafunga Wabunge wa Jamhuri ya Muungano waTanzania  (Bunge SC) mabao 4-2, kwa kifupi tupo vizuri sana,” alisema Majuto.

Alifafanua kuwa baada ya mechi hiyo, timu yao itaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Shule ya Kisasa ya Kenton iliyopo Sinza Afrika Sana kwa maandalizi ya mechi na safari nyingine za nje ya mkoa.

Alisema kuwa Taswa SC Jumapili inatarajia kucheza mechi nyingine ya dhidi ya timu ya Kijitonyama Chipukizi Veterans, mchezo ambao umepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama.

Sherehe za Uhuru London 09 /12/2017 moto! Plus Official New Song Release "Itapendeza Sana" by Engine.

Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images