Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 203 | 204 | (Page 205) | 206 | 207 | .... | 3286 | newer

  0 0


  The Duchess of Cambridge safely delivered a son, weighing 8lbs 60z, yesterday evening (4.24 pm UK time) in the presence of her husband, Prince William, the Duke of Cambridge.

  Their Royal Highnesses, Charles the Prince of Wales and Duchess of Cornwall were delighted with the news of the birth of the Prince’s first grandchild. The Prince of Wales said: “Both my wife and I are overjoyed at the arrival of my first grandchild. It is an incredible special moment for William and Catherine and we are so thrilled for them on the birth of their baby boy”
  Her Royal Highness and her child, who becomes third in succession line, are both doing well and remained in hospital overnight.
  Their Royal Highnesses Prince William and Kate, the Duchess of Cambridge, have asked well wishers around the world who wish to celebrate the royal birth by giving gifts  to give these to underprivileged children and mothers. This reflects the UK’s commitment to ensuring all mothers and children around the world have access to good maternal and newborn health care.
  DFID (UK AID) is providing essential medicines to ensure health care to mother and child.
  _______________________________________________________
  If anyone wishes to send personal messages of congratulations, these can be posted to the @ClarenceHouse Twitter account. Clarence House and Buckingham Palace will also be updating content on The Duke and Duchess’s official website, and on the British Monarchy Facebook page as more information becomes available. The name of the child is expected to 
  be made public within the next two weeks.

  For more information, please contact:
  Victor Mlunde
  Political Advisor and Acting Press Officer
  British High Commission
  Dar es Salaam
  Tel: +255 (0) 22 229 0234 
  Mob: +255 (0)714 289428 
  Email: victor.mlunde@fco.gov.uk

  0 0

  IMG_0093
  Mshauri Mwelekezi masuala ya utawala bora Bw. Wilbert Kitima akiendesha mafunzo kwa washiriki wa Redio Jamii yaliyofanyika mjini Kayanza, wilayani Karagwe mkoa wa Kagera na kumalizika mwishoni mwa Juma. Kushoto ni Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu
  IMG_0549
  Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin akizungumzia mahitaji muhimu kiuwezeshaji utoaji wa taarifa na kufafanua kuwa mradi huo utasaidia kutoa fursa kwa jamii kujadili masuala ya maendeleo kupitia redio za kijamii hivyo kuwezesha na kurahisisha upatikanaji wa habari kupitia redio hizo.
  IMG_0477
  Mkurugenzi wa Radio Jamii visiwani Zanzibar Hamad Shapandu (aliyesimama) akiwasilisha changamoto zinazoikabili kituo chake kwenye kikao cha kitaifa cha kujadili mradi wa Sida kutathmini kazi za mwaka uliopita kuona mafanikio yaliopatikana, kuzichanganua kero zilizojitokeza katika utekelezaji na mpango kazi kwa mwaka ujao kwa Afisa Mipango Taifa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin (aliyeketi) wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
  IMG_0528
  Usia Nkhoma Ledama kutoka Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akitoa somo kwa viongozi wa redio jamii kuhusu umuhimu wa kuwepo uwazi wa taarifa na habari zao katika mitandao ya kijamii ili kuongeza ufanisi na soko la kazi zao kujulikana Kimataifa na kuongeza nafasi ya kujipatia matangazo katika redio zao za kijamii.
  IMG_0495
  Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu amesema kupitia mradi huo watendaji wa vyombo vya habari katika jamii wana nafasi kubwa ya kuhamasisha jamii katika mijadala ya maendeleo na kudumisha amani katika taifa. Kushoto aliyeketi ni Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin.
  IMG_0480
  Meneja wa Kituo cha redio ya Jamii FADECO ya Wilayani Karagwe Adeline Lweramula akitoa maoni namna ya kuboresha utekelezaji wa mradi wa SIDA unaofadhili mafunzo ya redio za Jamii wakati wa kikao cha kitaifa cha kujadili mradi wa huo kutathmini kazi za mwaka uliopita kuona mafanikio yaliopatikana, kuzichanganua kero zilizojitokeza katika utekelezaji na mpango kazi kwa mwaka ujao.
  Na.Mwandishi wetu-Karagwe.
  Watanzania wenye nafasi mbalimbali za kutoa huduma kwa jamii, wameshauriwa kuondoa tabia ya kuogopana na kuoneana haya katika utendaji wa majukumu yao, ili mchango wao usaidie katika utendaji wenye tija katika sekta wanazozisimamia.
  Akizungumza na mameneja na wajumbe wa bodi za redio za jamii Tanzania katika mkutano maalum wa wiki moja ulioandaliwa na Unesco wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera, Mshauri Mwelekezi masuala ya utawala bora Bw. Wilbert Kitima amesema kuwa maeneo mengi yamekosa ufanisi kwa kuwa na watendaji wasio na sifa.
  Amewaagiza watendaji hao kufanya kazi kwa kufuata sheria wakifahamu kuwa vituo wanavyosimamia ni vya jamii, hivyo havinabudi kuendeshwa ipasavyo, wakifahamu uajibikaji sio kufanya kazi tu za kiofisi bali matokeo mazuri ndio kigenzo cha ufanisi, badala ya kukumbatia nafasi zote za kiutendaji.
  Amefahamisha kuwa vyombo vya jamii vinakabiliwa na changamoto nyingi za kiutendaji kutokana na vianzio vya ukusanyaji wa mapato, hivyo hawanabudi kuwa wabunifu, waadilifu na waaminifu, wenye msimamo thabiti wa kusimamia kazi zao kwa maslahi ya jamii na kuacha tabia yakuishi kwa udalali ambayo haina maslahi katika kuziendesha redio zao na kufanya kila linalowezekana kuepusha majungu katika kuendesha vituo hivyo.
  Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu amesema pamoja na mafunzo ya ujasiriamali katika kuendesha vituo hivyo pia watawezeshwa kufanyakazi na washauri waelekezi wa serikali za mitaa na halmashauri za wilaya.
  Amesema kutafanyika uzinduzi wa ushirikiano wa redio FADECO na Shirika la simu la Airtel katika kufanyakazi kwa ushirikiano baada ya shirika hilo kuruhusu transmita ya redio Fadeco, kuwekwa katika mnara wa Airtel kuongeza wigo kwa wasikilizaji wa redio hiyo ambao walikuwa hawajapata huduma ya matangazo watanufaika baada ya matangazo kwenda mbali zaidi.
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Meneja wa Redio Fadeco Adeline Lweramula , pia kutafanyika uzinduzi wa mtandao wa taarifa za wanahabari watoto, wanaoandaa vipindi vya watoto na redio Fadeco chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la Unicef.
  Aidha kutafanyika uzinduzi wa kampeni ya mwaka mmoja kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa wilaya ya Karagwe.

  0 0


   Asikari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Rodney Ndunguru
  Aliye kaa katikati ni mama wa marehemu Rodney Ndunguru

   Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea  katika makaburi ya Mjimwema
   Umati wa watu uliojitokeza katika mazishi ya Rodney Ndunguru katika makaburi ya  mjimwema leo

   Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi
   Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka taji katika kaburi la mwanaye
  ---------------------------------------
  Na Cresensia Kapinga,Songea.

  SIMANZI ,Vilio,majonzi  vimetawala wakati wa mazishi ya askari wa Jeshi la Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere mkoani Morogoro ambapo mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwemo askari wa Jeshi la wananchi ambao walihudhuria mazishi yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.

  Katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na Paroko wa kanisa katoriki jimbo kuu la Songea parokia ya Mjimwema padre Noel Duwe ambaye wakati  akiendesha ibada ya mazishi aliwaonya Watanzania kutochezea amani  na kwamba utulivu walionao watanzania unahitajika kulindwa kwa namna ya aina yeyote na si vinginevyo.

  Padre Due alisema kuwa kwa wale wote wanaotaka kuchezea amani na utulivu tulionao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa kuwa watanzania hatujazoea vurugu wala umwagaji wa damu jambo ambalo lilionekana kuvuta hisia kwa watu waliofika kuomboleza msiba hu.

  Aidha Padri Due alimfagilia waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano Mizengo Pinda kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa kuwa jeshi la Polisi lihakikishe kuwa linawadhibiti watu wanaoleta fujo kwa kupiga na kwamba kauli yenye agizo hilo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote badala ya kuibeza kwa kuwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakidharau vyombo vya Dola  wakizani kuwa serikali haipo.
   
  Kwa upande wake  Kaimu wa Brigedi ya kanda ya kusini Kanari George Msongole alieleza kuwa taarifa ya kifo cha Rodney ilipokelewa muda mfupi baada ya kifo chake na kuwa Jeshi la wananachi linaungana  na familia ya marehemu katika majonzi na msiba mzito.

  Kwa upande wake msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amesema kuwa  familia imepata pengo kubwa kwa kuondokewa na kijana wao ,na ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuisaidia  ili waweze kujengewa nyumba ambayo itwasaidia kwa kuishi mama yake mzazi na mjane.
   
  Alisema kuwa Rodney Ndunguru amefariki akiwa na miaka takribani miaka saba kazini na akiwa na umri wa miaka 28 ambapo kimsingi kifo chake kimeacha pengo kubwa katika famila kwani katika uhai wake ilikuwa farja kwa ndugu na jamaa.
   
  Rodney Ndungu amezikwa saa 10:45 jioni kwenye makaburi ya mjimwema ambako mamia ya wakazi ya mkoa wa Ruvuma walihudhulia akiwemo mwakilishi wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu ambaye ni katibu tawala ya wilaya ya songea Joseph Kapinga na kwamba mazishi yaliendeshwa kijeshi ambapo askari wote walikuwa wamevaa sare huku wakifunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao. 


  habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com

  0 0

  On Friday night, NTV's Larry Madowo hosted Tanzanian NBA player Hasheem Thabeet, 7ft. 3inch. who also happens to be the tallest active NBA player, on the trend. Hasheem is touring the Kenya, and part of his stay there took him to Laiser Hill academy, his old school. Hasheem made the entire studio personnel at NTV to look like midgets. 

  0 0

  Familia ya Mzee Shilatu wa Mbagala wanasikitika kutangaza kifo cha Baba yao Mpendwa JOHN SHILATU kilichotokea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 23/07/2013 saa 10 jioni kutokana na shinikizo la damu.
  Habari ziwafikie Ndugu, Jamaa, Marafiki, Viongozi, Wanasiasa wote wanaomfahamu vyema Marehemu popote pale walipo.
  Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwa Marehemu Mbagala. Kwa mawasiliano zaidi juu ya msiba piga simu namba 0717 488622
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
  Amen!!

  0 0

  Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Mwanza 
   Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amewataka Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Nchini kuzingatia Taratibu za kazi za kila siku katika Uendeshaji wa Magereza(Prisons Routine). 
   Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja ameyasema hayo leo wakati wa Ziara yake ya Kikazi katika Magereza Mkoani Mwanza alipokuwa akiongea katika Baraza la Makamanda na Askari wa Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza na Gereza Butimba, Mwanza. 
   Pia Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa Makamanda na Askari watakao tenda kazi zao kwa ufanisi unaopimika watapandishwa vyeo ili kuwaongezea molari zaidi ya kazi ambapo amewataka wajitahidi zaidi kutenda kazi zao kwa weledi katika maeneo yao ya kazi. 
   Aidha amewatadhalisha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Nchini kuacha mara moja tabia ya kutumia nguvu kazi ya Wafungwa katika shughuli binafsi kinyume na taratibu za Uendeshaji wa Jeshi la Magereza. 
   "Tutaendelea kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na Askari watakaothibitika kutumia vibaya nguvu kazi ya Wafungwa kwa maslahi yao binafsi". Alisisitiza Kamanda Minja. 
   Kamishna Jenerali Minja pia amezungumzia mafanikio mbalimbali yaliyofanyika ndani ya Jeshi la Magereza tangu ateuliwe na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza.
  Ametaja mafanikio hayo katika Jeshi ni pamoja na kukamilika kwa Karakana ya kutengeneza Magari katika Gereza Kuu Ukonga, Usajili wa Namba mpya za Magari ya Jeshi la Magereza, Kuanzishwa kwa Huduma za Maduka yanayouza bidhaa zisizo na Tozo la Kodi(Duty Free Shops) katika Mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma pia ujenzi unaendelea katika Mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro. 
   Mafanikio mengine ni pamoja na kukamilika kwa Jengo la gorofa kwa ajili ya makazi ya askari wa Magereza Mkoani Iringa, upanuzi wa Zoezi la Usafirishaji wa Mahabusu kutoka gerezani kwenda Mahakamani katika Mikoa ya Pwani, Arusha na Mkoa wa Dodoma ambapo zoezi linaendelea vizuri bila matatizo yeyote. 
   Kwa upande wao Maafisa na Askari wa Mkoa wa Mwanza wamempongeza Kamishna Jenerali kufanya Ziara yake Mkoani Mwanza ili kuweza kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili pamoja na kusikiliza shida mbalimbali za Maafisa na Askari. 
   "Tunampongeza sana Kamishna Jenerali Minja kwa uamuzi wake wa kuja hapa Magereza Mkoani Mwanza hasa kuja kuzungumza na sisi Askari wa Magereza Mkoa wa Mwanza tunaimani kubwa shida zetu zitapatiwa ufumbuzi kwa wakati kama ilivyokatika Utendaji wake wa kazi kuwa wa kasi na viwango". Alisikika Askari Mmoja wa Gereza Butimba, Mwanza. 
   Hii ni mara ya kwanza kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja kufanya Ziara yake ya kikazi tangu ateuliwe rasmi tarehe 25 Septemba, 2012 kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
   Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(Kaunda suti nyeusi) akimtambulisha Mhe. Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe kwa Wakuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga na Mkoa wa Mara baada ya kuwasili mapema asubuhi  katika Uwanja wa ndege wa Mwanza tayari kwa Ziara ya Kikazi katika Magereza Mkoani Mwanza leo

   Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(aliyepo kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo( aliyepo kulia) mapema leo Julai 23, 2013 alipofika ofisini kwake kuweka sahihi katika Kitabu cha Wageni(mwenye shati jeupe) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiangalia Mashine Maalum ya kupimia Magonjwa mbalimbali wakati alipomtembelea Zahanati ya Gereza Butimba mapema leo Julai 23, 2013, anayeelezea ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Mariam Lumuli ambaye ni Mtaalam wa Maabara wa Zahanati hiyo. 
  Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

  0 0

  ASKARI WA JESHI LA ULINZI WAKISAIDIA KUONDOA MAJERUHI  KATIKA ENEO LA AJALI ILIYOTOKEA LEO ENEO LA MWANAKWEREKWE BAADA YA GARI MOJA  MSAFARA WA MAZISHI KUPINDUKA KARIBU NA SOKO KUU LA MWANAKWEREKWE UMBALI WA MITA MIA 300 KUTOKA MAKABURI YA MWANAKWEREKWE WALIKOZIKWA WANAJESHI WALIOUAWA DARFUR.
   MAJERUHI ZAIDI WAKIONDOLEWA ENEO LA AJALI KUPELEKWA HOSPITALI

  GARI LILILOPATA AJALI. 

  0 0

  Habari ya kazi ndugu zangu.

  Ninayo furaha kuwajulisha ya kwamba sasa kazi zangu zote za muziki zitakuwa zinapatikana kwenye mitandao yote ya kununua nyimbo za wasanii duniani. Tayari nishasambaza Album yangu ya kwanza " Pwaa The Album" na singles zingine kama "Hmmm", na "Mambo" kwenye mitandao ifuatayo:

   iTunes, Amazon MP3, Spotify, Google Play, Xbox Music, Deezer, Rhapsody, Simfy, MySpace Music, Nokia, Wimp, Sony Music Unlimited,Napster, Verve Life, Media net, Shazam,eMusic, iHeartRadio, Muve Music, and Rdio.


  kwa wale mliokosa nafasi ya kujipatia nakala za album yangu ya kwanza, hii ni fursa kwenu kujipatia Album hiyo kupitia mitandao hii kwa bei nafuu sana. Tupeane support ili tukuze muziki wetu.

  kwa sasa namalizia kurekodi album yangu ya pili ambayo ipo kwenye mahadhi ya kimataifa zaidi na punde ikikamilika  ntaanza kuachia single moja moja kupitia mitandao hii, mitandao ya simu kwa njia ya RBT na  pamoja na wa "The Kleek" chini ya mkataba wangu mpya na Universal Music Group.

  Asanteni sana na hii hapa ni link ya 
  kupata nyimbo zangu zote kupitia iTunes.


  0 0

   Mdau Leonora wilson ndesanjo akipozi baada ya kula nondozzz ya
  BA Hons Human Resource Management Chuo kikuu cja  Glamorgan University,  Cardiff UK
   Leonora akiwa na rafiki yake Sim Joseph baada ya kula nondozzz pamoja
  Leonora akiwa na baba na mama
    Kushoto ni ndugu yake Donald ambaye naye kala no nondozzz hivi  karibuni wa pili ni mama mzazi Florence Wa tatu Leonora mwenyewe na wa nne ni Baba Wilson Ndesanjo
  Kulia Bw. Ian Banks mume wa mama yake mdogo Leonora wa nne Diane May akiwa na watoto wake Adrian Na Raell na wa pili na watatu ni Bw. na Bi. Wilson Ndesanjo na wa tano Leonora na rafiki yake Sim Joseph wa Uk waliokula nondozzz pamoja na familia yake

  0 0
 • 07/24/13--00:29: TANGAZO
 • Natafuta fundi cherehani mwenye uzoefu wa kushona nguo za kike vizuri na kiume kidogo.

  Sifa
  • Awe hajaoa wala kuolewa
  • Uwezo wa kuisimamia Biashara hiyo mwenyewe bila mtu nyuma yake
  • Awe tayari kufanya kazi Miswe Mlandizi ambako ndo kituo cha kazi
  • Mzoefu zaidi kwenye nguo za kike new fashion.
  • Awe tayari kuanza kazi maramoja.
  Mambo mengine; Atapata malazi na chakula atakapoanza kazi hadi Biashara ikikaa vizuri atajitegemea. Preferred wadada kulingana na nature ya Mazingira ya kazi.
  Wasiliana nami kwa namba za simu hapo chini.
  0754 840487 na 0653 264 566 au inbox me at  agape_nchimbi@yahoo.com
  Mdau

  Nauza printer heavy duty machine aina ya Minolta 350Di ipo katika hali nzuri kabisa na mara ya mwisho nimetoa kopi 34,000 ndani ya siku tatu bila matatizo. Naiuza kwa sababu naleta mali mpya Yaani machine mpya, nabadilisha vitendea kazi vyote kwenye ofisi yangu hivyo hivi naviuza kupisha nafasi kwa vifaa vipya. In any case nauza hata kama scraper. Lazima vitoke, bei maelewano tu. Machine hii ilinunuliwa Netherlands kwa maana hiyo ni original brand.
  Tafadhali kwa mawasiliano zaidi  nipigie kwa namba hizi     0754 840487 na 0653 264 566 au  inbox me at  agape_nchimbi@yahoo.com
  Mdau

  0 0

  JESHI la polisi mkoani Ruvuma kwa mara nyingine limefanikiwa kukamata nyara za serikali katika wilaya ya Tunduru tukio ambalo limetokea Julai 21 mwaka huu majira ya saa 11:40 alfajiri lililotanguliwa na tukio jingine lililotokea Juni 26 mwaka huu ambapo jumla ya meno 18 ya tembo yalikamatwa wilayani humo kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na idara ya wanyamapori pamoja na wananchi wanaotoa taarifa za siri kwa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama.

  Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amesema kuwa sik hiyo ya tukio askari polisi waliokuwa doria walifanya upekuzi kwenye mabasi yaliyokuwa yakianza safari alfajiri katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Tunduru ambapo katika basi moja lenye namba za usajili T315ABS aina ya Scania mali ya kampuni ya WAHIDA walifanikiwa kukamata sanduku moja likiwa na nguo pamoja na vipande 21 vya meno ya tembo .

  Amesema kuwa vipande hivyo vya meno ya tembo vilikuwa na uzito wa kilogramu 34.45 na thamani yake ikiwa ni dola za kimarekani 189,475 sawa na fedha za kitanzania shilingi 30,316,000na mkia mmoja wa tembo na walipoendelea kufuatilia katika mizigo hiyo walibaini kuwepo kwa tiketi moja ya kusafiria abiria ikiwa na namba zilizofutwafutwa na walipofuatilia kwenye kitabu cha tiketi waligundua kuwa tiketi hiyo ilikuwa imesajiliwa kwa jina moja tu.

  Na askari walipoendelea kufuatilia ilionekana abiria mwenye tiketi hiyo na mizigo hiyo iliyotiliwa mashaka aliamua kuitelekeza mizigo yake baada ya kuwaona askari polisi wakiwa kwenye upekuzi wa mabasi na hivyo mtu huyo hakuweza kufahamika na jitihada za polisi kwa kushirikiana na wananchi za kumtafuta zinaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani .

  Aidha kamanda Nsimeki ameendelea kuwaomba wananchi na raia wema kuendelea kutoa ushirikiano mwema kwa jeshi la polisi katika harakati za kuzuia biashara hiyo haramu inayoendelea kuhujumu uchumi wa taifa.

  Katika tukio jingine lililotokea katika kijiji cha Langiro wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kamanda Nsimeki amesema tukio hilo lililotokea Julai 22 mwaka huu majira ya saa 7 usiku ambapo mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Peter Kapinga(19) aliuawa baada ya kupigwa na mti kichwani na watuhumiwa wa tukio hilo ni Ingo Kapinga na Elias Kapinga ambapo chanzo niugomvi uliotokea kwenye disko na ugomvi wao huo ulisababisha kifo kwa sababu ya wivu wa kimapenzi ulioanzia kwenye muziki huo amba baada ya tukio hilo mtuhumiwa mmoja Inigo Kapinga alitoroka na mwenzake Elias Kapinga(14) alikamtwa na anahojiwa na polisikuhusina na tukio hilo.

  0 0

  Mdau Sara Ali Aboud akitembea kwa madaha kwenye stage mara baada ya kulamba Nondoz yake ya BSc in Mathematics (Financial IT ),katika Chuo Kikuu cha Brunell University nchini Uingereza.
  Mdau wa Globu ya Jamii,Sara Aboud (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na mama yake mzazi Bi Mariam Kilumanga (Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake UK -TAWA) na mdogo wake Samie Aboud wote wakiwa ni wenye furaha sana baada ya Sara kulamba Nondozz yake hiyo.
  Mdau Sara Ali akiwa katika pozi na anti yake,Bi Mariam Mungula a.k.a Katibu CCM UK / TAWA UK .
  Siku isingekamilika iwapo Mdau Sara Ali asingepata picha Ukumbusho na Mkuu wa Chuo "Vice Chancellor " wa Brunell University.

  GLOBU YA JAMII INAMPA HONGERA SANA MDAU SARA ABOUD KWA KUKAMILISHA MASOMO YAKE HAYO, NA HONGERA SANA KWA MZAZI WA SARA KWA KAZI NZURI YA KUMSOMESHA BINTI ILI AJE KUWA MSAADA MKUBWA KWA TAIFA LETU HAPO  BAADAE.

  0 0
 • 07/24/13--01:42: --none--


 • 0 0

  Naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (hawapo pichani) alipotembelea mamlaka hiyo.
  Mkurugenzi mpya wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeje akisoma taarifa kwa naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge alipotembelea mamlaka hiyo.
  Meneja fedha na utawala wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akijitambulisha kwa naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge hayupo pichani wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.
  Afisa mapato wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) brucevictor Sangawe kijitambulisha kwa naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge hayupo pichani wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa mamlaka hiyo.
  Wafanyakazi wa mamlaka ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakifuatilia hotuba ya naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge alipotembelea mamlaka hiyo.
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge alipotembelea mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA).Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

  0 0

  Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akihakiki namba ya mmoja ya washindi watano wa Sh Milioni Mbili wa promosheni ya Cheka Plus kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.Promosheni hiyo inaendeshwa kila mwezi na Vodacom.
  Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akimshuhudia Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akiongea na mmoja wa washindi wa Promosheni ya Cheka Plus ambapo washindi watano walijishindia shilingi milioni mbilimbili kila mmoja kupitia Promosheni hiyo kubwa ya mwezi.

  Kampuni ya Vodacom Tanzania imeendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwawezesha kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 10 kupitia promosheni ya 'Cheka Plus.'

  Kitita hicho cha Shilingi Milioni 10 kimenyakuliwa na washindi watano (5) ambapo kila mmoja amejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 2 kila mmoja kupitia Promosheni ya 'Cheka Plus' iliyofanyika tarehe 20 mwezi huu. 

  Washindi hao ni pamoja na; Musa Hussein Ellmy ambaye ni mkazi wa (Karatu - Arusha), Vumi Joshua Mteru (Kilimanjaro), Joseph Godfrey Kyando (Tunduma, Mbeya), Anatori Emmanuel Chogolo (Dar es Salaam), na Amina Joseph Mmbaga (Arusha).

  Meneja Uhusiano wa Umma wa Kampuni hiyo Bw. Matina Nkurlu, alisema kuwa zaidi ya wateja 6,000 wamefaidika na ofa hiyo kabambe inayoendelea hivi sasa nchi nzima ambapo zaidi ya Shilingi Milioni 100 zilikabidhiwa kwa wateja mbalimbali walioshinda kupitia Promosheni ya 'Cheka Plus.'

  Nkurlu alisema kuwa hadi hivi sasa, tayari wateja mbalimbali nchini wameweza kujishindia kiasi kinachofikia zaidi ya Shilingi milioni 100 "Tumekuwa tukipata washindi 100 kila siku ambapo wamekuwa wakijishindia shilingi 10,000 kila mmoja na washindi wengine 10 wakijinyakulia shilingi 50,000 kila siku, sambamba na droo kubwa ya mwezi ambapo katika washindi watano(5) kila mmoja wao amekuwa akijinyakulia kitita cha shilingi milioni mbili.

  Hivyo toka uzinduzi wa promosheni hii ya 'Cheka Plus,' wateja takribani 10 wameweza kujishindia kiasi cha shilingi milioni mbili mbili kila mwezi," alisema Nkurlu nakuongeza kuwa "promosheni hiyo bado inaendelea hivyo ninapenda kuwasihi wateja wa mtandao wa Vodacom kuendelea kufaidika na huduma zetu ikiwemo promosheni ya "Cheka Plus" na kuweza kujishindia zawadi kemkem sambamba na kuendelea kuwasiliana na wapendwa wao."

  Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa Promosheni ya 'Cheka Plus,' umewezesha wateja kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS), na kuperuzi kwenye mtandao wa intaneti bila hofu.

  Ili kuweza kujiunga na huduma ya Cheka Plus, wateja wanashauriwa kupiga *149*01 # na kuchagua kifurushi wanachokitaka. Promosheni ya Cheka Plus inawezesha wateja kutuma SMS na kupiga simu katika kiwango cha bei nafuu kabisa.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tano kutoka kushoto) akishiriki swala ya Magharibi na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wa Mkoani Arusha, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaongoza baadhi ya wananchi wa mkoani Arusha kuchukua futari, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiagana na wageni wao baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR.

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Cherrie Blair wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, mara baada ya kufanya mazungumzo yao.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na mgeni wake Mama Cherrie Blair, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza walipokutana leo kwenye ofisi za WAMA tarehe 23.7.2013 Mama Blair yupo nchini akifuatana na mumewe Tonny Blair katika ziara ya kikazi.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa nasaha zake baada kuwafuturisha viongozi wa serikali, madhehebu ya dini wa wilaya ya Mkuranga na wananchi wa kijiji cha Hoyoyo kilichoko karibu na Mkuranga katika Mkoa wa Pwani tarehe 23.7.2013.

  Na Anna Nkinda - Maelezo

  Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuhubiri amani katika majukwaa yao ili jamii ielewe umuhimu wa kuwepo kwa amani na kuendelea kuishi kwa upendo na ushirikiano.

  Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiwafuturisha wanakijiji cha Hoyoyo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

  Mama Kikwete alisema kuwa viongozi wa dini wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa waumini wao wanaelewa umuhimu wa amani katika nchi kwa kujenga mshikamano kama waasisi wa Tanzania walivyouanzisha .

  “Katika shughuli yetu hii tumekusanyika watu wa dini mbalimbali wanaofunga mwezi huu na wengine mwezi mwingine lakini dua ni dua kupitia kwa mwanadamu yeyote Mwenyezi Mungu inamfikia, hivyo basi tuzidi kushikamana kwa kila jambo”.

  Aliendelea kusema kuwa amani inatafutwa kwa miaka mingi lakini inaweza kutoweka kwa muda mchache hivyo basi kila mtu hasa viongozi wa dini watumie muda wao kuhubiri umuhimu wa amani katika nchi na neno amani lisitoweke ndani ya vinywa vyao.

  Kwa upande wake Sheikhe Athuman Kinyozi alimshukuru Mama Kikwete kwa futari aliyoiandaa kwa ajili yao na kusema kuwa mtu anayejitoa kwa ajili ya kufuturisha wengine anapata thawabu kwa Mwenyezi Mungu.

  Sheikhe Kinyozi alisema kuwa kufanya kitendo cha kufuturisha si lazima uwe na uwezo mkubwa kifedha bali unaweza ukanunua hata tende au maji na kuwapa watu waliofunga kile ulichowapa kikiwa ni kitu cha kwanza kutia midomoni mwao utalipwa thawabu za funga ya wale wote uliowapa kitu walichokula.

  0 0

  Naibu waziri wa maji Dk Mahenge akiangalia na kupokea maelezo toka kwa wafanyakazi wa MUWSA katika chanzo cha maji cha Nsere mkoani Kilimanjaro.
  Chumba maalumu kwa ajili ya matibabu ya maji katika chanzo cha maji cha Nsere mkoani Kilimanjaro.
  Naibu waziri wa maji Dk Mahenge akiangalia na kupokea maelezo toka kwa wafanyakazi wa MUWSA katika mradi wa kisima cha maji kinachochimbwa katika eneo la Longuo manispaa ya Moshi.
  Mitambo ya kuchimbia kisima katika eneo la Longuo mradi unaosimamiwa na mamlaka ya maji sai na usafi wa mazingira mjini Moshi( MUWSA).Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

  0 0


  0 0

  President of the United Republic of Tanzania Dr. Jakaya Kikwete (third from left, 1st row), U.S. Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt (second from left, 1st row) and Peace Corps Country Director for Tanzania Elizabeth Omalley (left 2nd row) with a group of volunteer American health professionals who will provide medical and nursing training to Health Education Institutions in Tanzania under the U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) supported Global Health Service Partnership (GHSP) initiative when they paid him a courtesy call at the State House in Dar es Salaam on July 23, 2013. GHSP volunteers with expertise and vast experiences in general medicine, women's health, obstetrics and gynecology, pediatrics, anesthesiology, family medicine, cardiology, social sciences, nursing and midwifery will serve for one year as faculty members and service providers in Bugando Medical Centre - School of Nursing, Sengerema DDH/Teaching Hospital, Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), Mirembe School of Nursing , Mvumi DDH/Clinical Officers Training College, Baylor Pediatric Centre for Excellence in Mwanza and Mwananyamala/ICAP - TB, HIV and AIDS centre for Excellence.
  U.S Ambassador to Tanzania Alfonso E. Lenhardt (center) and Peace Corps Tanzania Country Director Elizabeth Omalley (fifth from left) with a group of American health professionals who will provide medical and nursing training to Health Education Institutions in Tanzania under the U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) supported Global Health Service Partnership (GHSP) initiative during a brief introductory meeting at the U.S. Embassy in Dar es Salaam. GHSP volunteers with expertise and vast experiences in general medicine, women's health, obstetrics and gynecology, pediatrics, anesthesiology, family medicine, cardiology, social sciences, nursing and midwifery will serve for one year as faculty members and service providers in Bugando Medical Centre - School of Nursing, Sengerema DDH/Teaching Hospital, Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), Mirembe School of Nursing , Mvumi DDH/Clinical Officers Training College, Baylor Pediatric Centre for Excellence in Mwanza and Mwananyamala/ICAP - TB, HIV and AIDS centre for Excellence.Photo courtesy of the American Embassy.

older | 1 | .... | 203 | 204 | (Page 205) | 206 | 207 | .... | 3286 | newer