Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 204 | 205 | (Page 206) | 207 | 208 | .... | 3285 | newer

  0 0

  TAASISI ya Aisha Sururu, imetoa msaada wa baiskeli maalum kwa mtoto mlemavu, Saada Hamis Hamad (14), ambaye ni mshindi wa kwanza, kundi maalum, katika mashindano ya kuhifadhi Quran Tukufu, kitaifa.

  Saada ambaye mikono na miguu yake imelemaa, alikabidhiwa baiskeli hiyo juzi jioni, na mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aisha Sururu, ambapo alisema ina mahitaji muhimu kwa mtu mwenye ulemavu, ikiwemo sehemu ya kujisaidia.

  Akizungumza mara baada ya kupokea baiskeli hiyo, aliishukuru taasisi kwa kumsaidia kwa mambo mengi, ikiwemo kuibua kipaji chake cha kuhifadhi Quran na kumsafirisha kwa mara ya kwanza.

  Alisema tangu apate akili, amekuwa akijisaidia kwa tabu bila staha na kwamba kupitia baiskeli hiyo, itamsaidia mambo mengi ikiwemo kuzunguka maeneo mbalimbali, ambapo hapo awali alishindwa kwani ili kutoka sehemu moja kwenda nyingine ilikuwa lazima abebwe.

  "Kabla ya hapo nilikuwa nipo tu nyumbani, sikuwahi kupelekwa shule wala kutoka nje ya mji wangu, lakini nashukuru nimejifunza mengi na nimepata msaada huu,"aliongeza Saada.

  Mtoto huyo, ambaye ni mkazi wa Mamoja, Pemba, alisema kuwa, ana ndugu zake wanne, ambao wawili kati yao ni walemavu kama yeye isipokuwa kaka yake wa kwanza ambaye alizaliwa akiwa mzima wa viungo.

  Aisha, ambaye pia ni diwani wa viti maalum Ilala, aliwataka wahisani wengine kujitokeza na kununua baiskeli mbili kwa ajili ya ndugu zake Saada hasa mdogo wake ambaye anasoma chekechekea.

  "Mdogo wake amekuwa akibebwa kwa ajili ya kupelekwa shule na kuridishwa nyumbani, hivyo baiskeli hiyo itapunguza adha na kumsaidia kuhudhuria masomo bila wasiwasi,"aliongeza.

  0 0


  0 0
 • 07/24/13--11:30: Article 6


 • 0 0


  0 0

  Kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars) kikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda jioni ya leo,tayari kwa mtanange wa marudiano na timu ya Taifa ya nchi hiyo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii.
   Kikosi cha Taifa Stars kikiwa uwanja wa ndege wa Mwanza kikisubiri usafiri kilikutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye naye alitua hapo kwa muda akielekea Bukoba kwa ziara ya siku sita mkoani Kagera
   Rais Kikwete akisalimiana na wachezaji wa Taifa Stars jijini Mwanza
   Rais Kikwete akiwatakia Taifa Stars kila la heri katika mchezo wao wa marudiano

  0 0
 • 07/24/13--12:16: tangazo la msiba London
 • Familia ya Mr. A Alfaghee inasikitika kutangaza kifo cha binti yao mpendwa MAIMUNA FATMA KARUMBA kilichotokea jana London UK.
   Ukiwa kama ndugu, jamaa na rafiki mchango wako wa dhati unahitajika ili kufanikisha maziko ya Binti Yetu Mpendwa, Ambayo Yamepangwa Kufanyika IJUMAA TAREHE 26 July 2013. 
  Gharama za maziko ni £3000 tunaomba chochote ulichonacho ilikufanikisha maziko haya. Michango yote inwekee kwenye account ya
    MR A ALFAGHEE
  Sort 09-01-27
  Account Number 11832254
  Santander.
  Asanteni Kwa Ushirikiano Wenu
  R.I.P MAIMUNA FATMA KARUMBA

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba leo Julai 24, 2013.
  Rais Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi mbali mbali wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( Kaunda suti nyeusi) akiagana na Mkuu wa Gereza la Wilaya, Mrakibu wa Magereza, Kamanda Mbilinyi mapema leo Julai 24, 2013 alipopita kukagua Gereza la Wilaya la Geita kabla ya kuendelea na safari yake Mkoani Kagera kushiriki Maadhimisho ya Sherehe za Mashujaa zitakazofanyika kesho tarehe 25 Julai, 2013 katika Kambi ya Jeshi ya Kaboya(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).


  0 0
 • 07/24/13--13:09: Article 0


 • 0 0


  0 0

  IMG_0620
  Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya Wilayani Karagwe Mwl. Emmanuel Muganyizi kuhusiana na umuhimu wa wanfunzi wa shule yake kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa na faida zake.
  IMG_0638
  Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Ndama na kuwapa hamasa ya kuwa walezi wazuri wa vilabu hivyo vitavyoanzishwa shuleni hapo ikiwa ni kama somo la ziada kwa wanafunzi wao ili wasipate muda wa kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
  IMG_0672
  Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na vijana wa shule za sekondari Ndama wilayani Karagwe mkoani Kagera, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa (UN Club) vinavyoanzishwa mashuleni kwa kuwa kwanza vitawasaidia kujitambua.

  Amewaambia kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu hivyo mashuleni kujiunga kwa wingi zaidi na kutawawezesha kujifunza shughuli za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.

  Bi. Usia pia amewafafanulia vijana kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya kazi za kujitolea.


  0 0

  Lifelong Learning for Career Professionals
  Would you like to sharpen your career skills, increase your professionalism (and marketability) and learn about the latest trends, technologies, and strategies? If so, Virginia International University's School of Continuing Education and Workforce Development (SCE) is just for you! Our SCE programs provide just-in-time training for career professionals with real-world do-it-now application.
  Would you like to increase your English language communication skills? Computer skills? Business skills? Leadership ability? Are you a teacher, health care provider, business professional, IT professional, call center representative, or simply a person who is looking to switch careers or excel in the one you already have? 

  Would you be interested in coming to the Washington, D.C. metropolitan area for short-term educational programs at Virginia International University's modern campus that run for two days, two weeks, or two months? Would you like to find a program that can arrange your hotel accommodations, transportation, meals, and even optional sightseeing for you during your visit? If so, Virginia International University's SCE programs are just for you!
  Welcome to Virginia International University's School of Continuing Education and Workforce Development (SCE). Read on to learn more about our lifelong learning programs for career professionals just like you!

  0 0

  Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika leo Mkoani Morogoro.

  0 0

  Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader akitoa shukrani zake kwa uongozi na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo.
  Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akiwashukuru wawakilishi kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa kutambua mchango wa TTCL katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani alipotembelea Nchini Tanzania.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
  Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dtk. Kamugisha Kazaura akibadilishana mawazo na Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
  Uongozi wa TTCL pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini katika picha ya pamoja.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba mapema leo asubuhi.Kushoto ni Jaji Mkuu,Mhe. Mohamed Chande Othman.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya ukaguzi wa Jengo hilo mara baada ya kulizindua rasmi leo asubuhi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Kikwete (katikati) , Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman wa pili kushoto, Jaji Mkuu wa Zanzibar,Mhe. Othman Makungu (wa Tatu ), Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu (wa pili kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Gad Mjemmas,kulia,Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Mathias Chikawe (wa pili kushoto)na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Ltn Mstaafu, Fabian Massawe wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama Bukoba Mara baada ya uzinduzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. (Picha na Mary Gwera,Mahakama ya Tanzania)
  Muonekano wa jengo la Mahakama Kuu Bukoba lililozinduliwa na rais.

  0 0


  0 0
 • 07/25/13--05:20: SWAHILI TV MTAANI KUNANI
 • Na Alex Kassuwi
  Kwa wanakijiji wenzangu, miaka 30 iliyopita nisingeliweza kuamini ninayo yaona na kuishi hivi sasa. Kwa kifupi tuliona wakija kijijini kama mapadri, wataalamu wa mashirika toka nje ama walimu.

   Nilijenga imani kila mzungu ni msomi na tajiri. Nilipohamia ughaibuni nimekuta ni tofauti sana, wapo wazungu wengi mbumbumbu na wanabangaiza tu.

  Ushauri kwa dada zangu wanaowinda kuolewa na wazungu "kila king'aacho sio dhahabu"

     Kwa matukio ya Swahili TV mtaani kunani tembelea www.swahilitv.blogspot.com

  0 0


  Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini,Jerry Silaa akizungumza machache wakati wa kufungua rasmi mkutano huo leo,kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Richard Kasesela akizungumza wakati akiwasilisha mada yake ya namna ya kupata leseni ya uwekezaji kwenye jamii hapa nchini.wakati wa Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Dar es Salaam.Katika Mada yake hiyo,Pia Kasesela amesisitiza umuhimu wa Wawekezaji kuwa karibu na Jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na kujenga makazi ya kudumu katika maeneo ya migodi yao.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Richard Kasesela akiendelea kuwasilisha mada yake ya namna ya kupata leseni ya kuweza uwekezaji kwenye jamii hapa nchini.wakati wa Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Dar es Salaam.
  Mhadhiri na Kiongozi wa Wanafunzi wa Kituo cha Mafunzo ya Takwimu Afrika Mashariki,Dkt. Camillus Kassala akiwasilisha mada yake iliyokuwa inahusu uwezekano wa Serikali za Mitaa zinavyoweza kushiriki kwenye Miradi Mikubwa wakati wa Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini unaoendelea leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Dar es Salaam.
  Wadau mbali mbali wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini unaoendelea leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Dar es Salaam.


  0 0

  Benki ya  Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika  kuhimiza maendeleo endelevu ya  ardhi  ili kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo.

  Ripoti ya Benki hiyo iliyotolewa Julai 22, 2013  imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika ina karibu nusu ya eneo la ardhi nzuri  ambayo haijaendelezwa kwa kilimo, bara hilo limeshindwa  kuiendeleza ardhi hiyoinayokadiriwa kuwa hekta milioni 202 kujikwamua katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi,kuongeza nafasi za kazi na kulleta mafanikio kwa jumla.

  Ripoti hiyo inayoitwa  “Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,”  inaeleza kuwa  nchi za Afrika najamii zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya chakula na kubadilisha  taratibu za usimamizi na umiliki  wa ardhi katika mwongo ujao.Afrika,

  Ripoti hiyo imeeleza, ina kiwango kikukbwa cha umaskini ambapo asilimia 47.5 ya watu wake wana kipato chini ya  dola za Marekani $1.25 kwa siku.. 
   
  “Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,”  anasema  Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.


  “Kuboresha usimamiaji wa ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi  zaidi kwa waafrika , wakiwemo wanawake ambao ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika ambao wanakwazwa  kumiliki ardhi na sheria za kimila..Hali hii haikubaliki na lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.” 
   
  Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.  Hata hivyo kumekuwa na matumaini ya maboresho  chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi za   Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na Uganda ambapo  mpango wa kutumia  ardhi kwa mafanikio ya pamoja  unaweza kuleta mapinduzi  ya  uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na  kuondoa umaskini wa kutupea Afrika..  
   
  Mpango wa kuleta mabadiliko  
   
  Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake  katika kipindi cha muongo ujao kwa::  
     · Kuwa na mabadiliko  na uwekezaji kurasimisha ardhi  na  maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi.     · Kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa  na kujengwa  bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya  watu asilimila 60 barani Afrika.  .    · Kukabiliana na udhaifu wa utawala na rushwa katika mfumo wa usimamizi wa ardhi katika nchi za Afrika ambao  kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya wananchi walio maskini.    · Serikali za Afrika kuwa na dhamira  ya kisiasa  kuhimiza  mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. . 
   
  Ripoti  hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu  nchi za Afrika  na  washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha  dola za Marekani bilioni 4.5  katika kipindi cha miaka 10 kuleta mabadiliko ya sera na uwekezaji

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Musoma Vijijini waliokutana kujadili Rasimu ya Katiba. Mkutano huo ulifanyika wilayani Musoma.
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro Prof. James Mdee akitoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba katika mkutano uliofanyika mjini Moshi hivi karibuni.
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro Bi. Elingao Mshanga akitoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba katika mkutano uliofanyika mjini Moshi juzi.
  Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu akiongea na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Katiba la wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wakati wa mkutano wa kujadili Rasimu ya Katiba. Mkutano huo ulifanyika wilani Kalambo hivi karibuni.

older | 1 | .... | 204 | 205 | (Page 206) | 207 | 208 | .... | 3285 | newer