Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 202 | 203 | (Page 204) | 205 | 206 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Rais wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya ISACA tawi la Tanzania, Boniface Kanemba akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu semina inayohusu usalama wa matumizi ya mitandao ya kompyuta ‘Cyber Defence East Africa 2013 itakayofanyika Julai 28 mjini Morogoro.  Kulia ni, Ofisa Mtendaji  wa Norway Registers Development (NRD), kwa nchi za Afrika Mashariki, Sebastian Marondo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

  ISACA Tanzania chapter pamoja na NRD East Africa wameandaa semina inayohusu usalama wa matumizi ya kompyuta na  mitandao yake katika nyanja zote. Semina hii ijulikanayo kama Cyber Defense East Africa 2013 itakayofanyika Tar 28 -30 mwezi wa nane pale nashera hoteli Morogoro. Mafunzo haya ambayo yatafunguliwa na naibu waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh January Makamba yamelenga kwa kina kutoa mafunzo kwa waatalamu wa TECHNOHAMA haswa wale wanaohusika na usalama wa mitandao hiyo. 
  Mafunzo haya ambayo yatawahusisha wataalumu wa makampuni ya usalama  wa mitandao kutoka pande  mbali mbali za dunia yakiwemo makampuni kutoka nchi za ulaya, America na Africa Kusini, FireEye, Fortinet, Lumension, IBM Q1Labs, Qualys, AccessData na Balabit wataongea kwa kina wanachokifanya katika ulinzi na usalama wa mitandao na teknolojia wanazozitengeneza za kudhibiti uhalifu wa mitandao
  Vile vile, wataalamu hao wataonyesha kwa vitendo mambo mbali mbali yanayofanyika wakati wa kufanya  wizi wa mitandao, na  washiriki wa semina hii watashiriki kwa vitendo hivyo ambayo vimelenga kutoa ufahamu zaidi juu ya kile kinachotokea kwenye mtandao  haswa kwa matumizi mabaya kama wizi. Kila mshiriki atajionea kwa macho yake jinsi wizi wa mtandao unavyoandaliwa na kufanyika katika maeneo mbali mbali yakiwemo katika mabeki, serikali, makampuni ya simu na mengineyo na hivyo kuongeza ufahamu wa jinsi ya kudhibiti uhalifu.

  Mafunzo haya ni kwa ajili ya wadau mbalimbali kutoka secta zote za uma na binafsi na pia kutoka nchi zote tano za Afrika Mashariki, yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burudi. 

  Hii ni kutokana na nchi hizi kuwa na changamoto sawa la ongezeko la wizi wa mitandao na matumizi mabaya ya mitandao  katika miaka ya hivi karibuni. Mfano, tafiti iliyofanywa na kampuni ya Deloitte mwaka 2012 inaonyesha kuwa mabeki ya kibiashara kwenye nchi za Africa Mashariki yanapoteza takribani zaidi ya Tsh Bil 80 kutokana na wizi wa mitandao kwa mwaka kiasi ambacho bado kinasadikiwa kuwa kinaweza kuwa ni zaidi ya hapo ikizikatia kuwa matukio mengi huwa haya ripotiwi hivyo kutokuwa na idada kamili ya fedha zote.

  Hali kadhalika matumizi ya M-pesa nayo yameongezeka kwa kasi na hivyo kuongeza matukio ya wizi unaohusiana na miamala yake. 
  Mbali na wizi wa fedha, makampuni mengi binafsi, umma pamoja na serikali yanapoteza taarifa nyingi sana zikiwemo zile binafsi na nyaraka muhimu za matumizi ya ofisini bila kujua. Taarifa hizo ambazo huchukuliwa kwa kutumia teknolojia ya wizi wa mitandao huishia mikononi mwa wahalifu ambao wanazipembua na kujua siri mbali mbali za makampuni, zikiwemo taarifa za fedha, mipango mikakati kimasoko, utawala na kadhalika.
  Ndg waandishi wa habari, tumechukua jukumu hii tukijua kabisa serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu kwa kila mtanzania, ni lazima makampuni na mashirika binafsi tuungane kwa pamoja kuilinda na kuijenga nchi yetu huu ukiwa ni mpango unaoenda sambamba na malengo ya millennia haswa lengo namba 8 “Developing a global partnership for development” lengo ninalosisitiza matumizi zaidi ya mitandao na kuhimiza serikali kushirikiana na secta binafsi kuendeleza  mpango wa maendeleo.

  Tunaomba kutumia fursa hii kuishukuru serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wanatupatia kila mara.
   Pia tunamshukuru Mshimiwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kutoa muda wake kufungua Mafunzo haya.

  Pia tutumie fursa hii kuwahamasisha wadau wote wa TECHNOHAMA kutoka serikali, kwenye Mabenki,Mashirika ya umma na yale ya binafisi na hata mtu mmoja mmoja kujitoa kwa kina kushiriki fursa hii ya mafunzo ya kimataaifa ya usalama wa mitandao.

  Nafasi ziko wazi, unaweza kujiandikisha kwenye mitandao yetu au kwa kupiga simu kama inavyoonekana hapa chini.

  0 0


  Na Swahili TV
  Mhe. Balozi Liberata Mulamula ametoa kauli ya kuwaunganisha watanzania wote, amesema kamwe hatoruhusu tofauti na makundi katika jamii za kitanzania. Ameyazungumza hayo katika papo kwa hapo ya Swahili TV.

  0 0

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo amefungua mafunzo ya awali kwa mawakili wapya wa serikali wapato 33 kwenye hoteli ya giraffe, Dar-es-salaam. Mambo aliyotilia mkazo ni kuepuka vitendo vya rushwa, kuwatumikia watanzania wa tabaka zote, kufanya kazi kwa juhudi na kutambua ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali sio sehemu ya kufanikisha maslahi binafsi.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awali kwa mawakili wapya wa serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt Eeliezer Feleshi na kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Abdulrahman Mdimu
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali(kushoto) Jaji Frederick M. Werema na Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Eliezer M. Feleshi wakibalishana mawazo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awali kwa mawakili wapya wa serikali
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (katikati waliokaa) kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mawakili wapya wa serikali. Picha na Abuu Kimario

  0 0


  0 0
 • 07/23/13--01:40: --none--


 • 0 0

  Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida wakiwa katika majadiliano ya kuipitia Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo hivi karibuni.
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, Bw. Frederick Kabendwe akwasilisha maoni ya Wajumbe hao kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika Wilayani humo hivi karibuni.
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Shinyanga, Bi Caroline Shayo akitoa maoni yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya katika eneo la kuhusu Maadili ya Viongozi wa Umma katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo hivi karibuni.
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Bi. Jackline Moshi akichangia hoja wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Mkutano uliofanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw. Charles Wakuling’anga akiwasilisha maoni ya kundi lake lililojadili eneo la haki za Binadamu katika Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika Halmashauri hiyo hivi karibuni.

  0 0

  IMG_0093
  Mshauri Mwelekezi masuala ya utawala bora Bw. Wilbert Kitima akiendesha mafunzo kwa washiriki wa Redio Jamii yaliyofanyika mjini Kayanza, wilayani Karagwe mkoa wa Kagera na kumalizika mwishoni mwa Juma. Kushoto ni Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu
  IMG_0549
  Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin akizungumzia mahitaji muhimu kiuwezeshaji utoaji wa taarifa na kufafanua kuwa mradi huo utasaidia kutoa fursa kwa jamii kujadili masuala ya maendeleo kupitia redio za kijamii hivyo kuwezesha na kurahisisha upatikanaji wa habari kupitia redio hizo.
  IMG_0477
  Mkurugenzi wa Radio Jamii visiwani Zanzibar Hamad Shapandu (aliyesimama) akiwasilisha changamoto zinazoikabili kituo chake kwenye kikao cha kitaifa cha kujadili mradi wa Sida kutathmini kazi za mwaka uliopita kuona mafanikio yaliopatikana, kuzichanganua kero zilizojitokeza katika utekelezaji na mpango kazi kwa mwaka ujao kwa Afisa Mipango Taifa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin (aliyeketi) wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
  IMG_0528
  Usia Nkhoma Ledama kutoka Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akitoa somo kwa viongozi wa redio jamii kuhusu umuhimu wa kuwepo uwazi wa taarifa na habari zao katika mitandao ya kijamii ili kuongeza ufanisi na soko la kazi zao kujulikana Kimataifa na kuongeza nafasi ya kujipatia matangazo katika redio zao za kijamii.


  0 0
 • 07/23/13--02:13: Vacancy at Oxfam in Tanzania

 • 0 0
 • 07/23/13--02:27: --none--


 • 0 0

  Benki ya NMB imefadhili semina kubwa iliyohusisha maafisa maendeleo wa vijana kutoka nchi nzima.Semina hii ambayo ilikua ni ya siku mbili ilifanyika katika kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Mhe. Dkt.Fenera Mukangara ambae ni Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo alizindua rasmi semina hii na kuishukuru Benki ya NMB kwa ufadhili mkubwa ambao wamejitolea ili kufanikisha semina. Dhumuni la semina ni kujadili maendeleo ya vijana kuanzia ngazi ya halmashauri,kuimarisha utendaji kazi kwa vijana wa mikoa na wilaya.

  Mhe. Dkt. Fenera Mukangara ambaye ni Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo akiongea na maafisa maendeleo ya vijana nchini wakati wa uzinduzi wa semina ya siku mbili

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.

  Meneja wa NMB Mikopo Midogo Midogo Bw. Mashaga Changarawe akielezea huduma mbali mbali zitolewazo na Benki ya NMB zikiwemo akaunti pamoja na mikopo mbalimbali kwa wajasiliamali

  Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akizungumzia jinsi ambavyo Benki ya NMB kwa kupitia huduma zake kwa wajasiliamali inavyosaidia kuongeza ajira kwa vijana nchini

  Sehemu ya washiriki wa semina hiyo.

  Erick Shigongo nae alitoa mada kuhusiana mafanikio na kujitambua katika ajira.

  0 0

  Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema kikosi chake kimejiandaa kuikabili Uganda kwenye mechi ya marudiano ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) itakayochezwa Jumamosi jijini Kampala.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Kim amesema tangu kikosi chake kimeingia kambini Julai 14 mwaka huu, wachezaji wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mazoezi na wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo.

  “Uganda ni timu bora kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Mechi itakuwa ngumu, tunaamini tunakwenda kufanya vizuri. Tayari tunayo mikakati kwa ajili ya mechi hiyo, tunakwenda kuikamilisha Kampala,” amesema Kim.

  Hata hivyo, Kim amesema licha ya mwitikio mzuri wa wachezaji kwenye mazoezi lakini wanakabiliwa na changamoto ya wengi wa wachezaji kuwa wamefunga wakati wachezaji wanapokuwa kambini wanatakiwa kula, kunywa na kupumzika.

  “Hiki ni kipindi kigumu kwa mpira wa miguu, na suala la kufunga ni la kiimani ambapo hatuwezi kuwazuia wachezaji kufunga. Karibu nusu ya wachezaji wanafunga, hii ni changamoto ambayo tunaiheshimu,” amesema Kim na kuongeza kuwa ni wazi kikosi chake cha kwanza kitakuwa na mabadiliko baada ya beki Shomari Kapombe kwenda kwenye majaribio nchini Uholanzi.

  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaondoka Mwanza kesho (Julai 24 mwaka huu) saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir na kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 8.15 mchana.

  Wachezaji waliomo kwenye msafara huo ni makipa Juma Kaseja, Mwadini Ali na Ali Mustafa. Mabeki ni Aggrey Morris, David Luhende, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir Haroub na Vincent Barnabas.

  Viungo ni Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis Mcha, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni John Boko, Juma Luizio na Mrisho Ngasa.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Na Abdulaziz Video,Lindi

  Huku kukiwa na zaidi ya sh milioni 700 zikiwa zimeanza kutumika katika ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi ambapo zoezi la ujenzi wa kituo kipya cha mabasi wilayani humo kuanza kujengwa na kutumika katika maeneo ya uwanja wa ndege,Baadhi ya Abiria leo wametishia kugoma kutokana na Kuzuia tena uwepo wa kituo cha karibu na maeneo ya Mjini kutokana na Umbali uliopo na kituo hicho kipya.

  Hali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya baadhi ya Abiria kugomea kituo hicho kipya kutokana na Halmashauri ya Wilaya hiyo kushirikiana na Jeshi la Polisi kufuta kituo cha Tunduru na kuagiza wasafirishaji wote kutumia kituo cha Stesheni kuwa cha mwisho njiani kabla ya kufika kituo kikuu ambapo kuna umbali mrefu hali inayofanya Abiria wengi kunufaisha watoa huduma za bajaj na Bodaboda huku wengine wakitembea Umbali Mrefu kwa kukipita msituni.

  Akiongea na Mtandao huu Mwandishi wa Gazeti la Raia Mwema wilayani humo,Ahmaid Mmow alieleza kuwa hali hiyo imeleta kero kubwa kwa Abiria wanaosafiri kati ya Nachingwea,Masasi,Newala,Lindi na Dar es salam huku wengine wakisafiri wakiwa na shida mbalimbali za kijamii.

  Abiria wengi baada ya kuanza kwa stand mpya waliumia sana na umbali na msitu uliopo lakini Halmashauri ilipoanzisha kituo cha Tunduru ya Leo kidogo kilileta ahueni sasa sijui ni kwa nini wamekifuta hali inayofanya abiria wengi kulazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya km 5 hadi stand Mpya na stesheni.

   Hii inaumiza sana hasa wenye wagonjwa,Kufuatia hali hiyo Baadhi ya Mawakala wa Mabasi ya Abiria na Abiria wamedhamiria kuitisha maandamano ya kuhamasisha kutotumia kituo kipya kinachoendelea kujengwa hadi kitakapokamilika kutokana na kukosekana kwa baadhi ya huduma muhimu za kijamii ikiwemo mabanda ya kupumzikia Abiria.
  Basi zikiwa stendi


  0 0

   
  Picha ya pamoja mara baada ya  kuuzinduwa mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 bure jijini Mbeya,hafla hiyo inayoratibiwa na RITA,imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya.Mpango huo umefadhiriwa na mashirika mbalimbali likwemo shirika la UNICEF,DFTDA (iliyokuwa CIDA Canada zamani) pamoja na Shirika la Wafanyakazi la kujitolea (VSO).
   Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki akizindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya,kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini,Dkt.Norman Sigalla na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Ushauri RITA,Bwa.Vincent Mrisho na wageni mbambali wakilishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.Shughuli nzima inaratibiwa na RITA.
  Mgeni Rasmi,  Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki akimkabidhi mmoja wa akina mama aliyejitambulisha kwa jina la Fides Samson akikabidhiwa cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake mwenye umri chini ya miaka 5,mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya.Mpango huo umefadhiriwa na mashirika mbalimbali likwemo shirika la UNICEF,DFTDA (iliyokuwa CIDA Canada zamani) pamoja na Shirika la Wafanyakazi la kujitolea (VSO).
   Baadhi ya akina mama wakiwa na vyeti vya kuzawaliwa vya watoto wao wanye zaidi ya wiki mbili tangu kuzaliwa kwao,mara baada ya kabidhiwa leo na Mgeni Rasmi,  Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki mara baada ya kuuzindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 bure jijini Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,mkoani Mbeya.Mpango huo umefadhiriwa na mashirika mbalimbali likwemo shirika la UNICEF,DFTDA (iliyokuwa CIDA Canada zamani) pamoja na Shirika la Wafanyakazi la kujitolea (VSO).
   Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa katiba na Sheria,Mh, Angellah Kairuki akizungumza mbele ya wakazi wa mji wa Mbeya (hawapo pichani) mapema leo wakati alipokuwa akizindua mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya.
   Baadhi ya Wakazi wa jijini Mbeya wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Ruanda Nzovwe mapema leo wakati  wa uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili wa Vizazi  na vifo kupitia mkakati wa usajili wa watoto wa umri chini ya miaka 5 Mkoa wa Mbeya,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe,jijini Mbeya.
  PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0

  Mwenge huo wa Uhuru umetembelea miradi 23 ya maendeleo na miradi 28 ya vikundi Mkoani Rukwa vyenye thamani ya fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni 3.4 ikiwa ni mchango wa Serikali kuu, Halmashauri, Wananchi na Wadau wengine wa maendeleo.
  Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukamilisha ratiba yake katika Wilaya hiyo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mkuu huyo wa Mkoa atasafiri kwa ndege kuukabidhi Mwenge huo Mkoani Tabora. 
   Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Juma Ali Simai akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi Mjini Sumbawanga tarehe 22 Julai 2013. Kulia ni Diwani wa kata ya katandala Ndugu Kisabwite na Mbunge Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kmanta akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani humo tarehe 20 Julai 2013.
  Mkuu wa Wilaya ya Kalambo machachari katika mbio za mwenge wa Uhuru Moshi Chang'a akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Kalambo tarehe 21 Julai 2013.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa na Naibu wake Mhe. Philipo Mulugo wametembelea Ofisi Mpya za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zilizopo Mwenge Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam.

   Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Kawambwa aliongozana na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo akiwemo Kaimu Katibu Mkuu Bw. Selestine Gesimba, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Prof. Sylvia Temu na Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Tarimo. 

  Akiwakaribisha katika Ofisi hizo Bw. George Nyatega, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, alisema sababu kuu ya kuhama Ofisi za awali ni kutokana na taasisi kuzidi kuwa kubwa na kwamba idadi ya wafanyakazi imeongezeka na hivyo ilitakiwa kupata ofisi kubwa ili kuboresha huduma kwa wadau wake.

   Mhe. Dkt. Kawambwa ameipongeza Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kwa hatua hiyo na pia kwa namna ambavyo imeboresha huduma katika miaka ya hivi karibuni. Aidha ameiagiza Menejimenti ya Bodi hiyo kutobweteka na mafanikio yaliyopatikana badala yake iendelee kutoa huduma kwa ufanisi na weledi mkubwa katika mwaka wa masomo unaokuja wa 2013/2014 ili kuepusha migogoro ya wanafunzi kuhusu mikopo. 

   Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Ofisi ya Makao Makuu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imehama kutoka Msasani Tirdo Complex, Dar es Salaam ilipokuwa awali tangu kuanzishwa kwake Julai 2005.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) na Naibu wake Mhe. Philipo Mulugo wakifuatilia Kwa umakini Taarifa ya Menejimenti ya Bodi ya Mikopo Iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Bw. George Nyatega (hayupo pichani).
  Mhe. Dkt. Kawambwa wa pili Kushoto akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Nyatega (aliyevaa koti la khaki) namna uchambuzi wa fomu za waombaji mikopo inavyofanyika, Pembeni aliyeshika Moja ya fomu za waombaji ni Naibu Waziri Mhe. Philipo Mulugo.
  KARIBU SANA MHESHIMIWA……….! Maneno yalisikika kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw. George Nyatega (Kulia), akimkaribisha Naibu Waziri Mhe. Mulugo katika viunga vya Ofisi mpya za Bodi hiyo zilizopo Mwenge-Barabara ya Sam Nujoma.
  Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Ikimkaribisha Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo (katikati) katika Ofisi Mpya za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zilizopo Mwenge Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika Hitma ya wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni,Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally iliyosomwa katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika kuwaswalia Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,na Cpl Mohammed Juma Ally ,mbele katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo,wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
  Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakibeba Jeneza la mwili wa Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,baada ya kuwasilim katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) na viongozi wengine walihudhuria katika mazishi ya Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia udungo katika Kaburi la Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,aliyezikwa leo Mwanakwerekwe Mjini Unguja, akiwa ni miongoni mwa wanajeshi wa jeshi la Ulinzi la Tanzania 7 waliouwawa hivi karibuni Nchini Sudan Jimbo la Daafur.
  Baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na Ndugu na Jamaa wa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally ,waliofurika katika viwanja vya makaburi ya Mwanakwerekwe,ambapo ndipo walipozikwa leo,mchana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na Vingozi na Waislamu,wakiangalia Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania,walipokuwa wakitoa hesha ya mwisho kwa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Mwanakwerekwe leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0


  0 0

  NA MIZA KONA / HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kulivunja Shirika la Utalii Zanzibar kutokana na changamoto zinazolikabili Shirika hilo hivi sasa.

  Akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2013/2014 huko katika Baraza la Wawakilishi Chukwani,Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema sababu kubwa ya kuvunjwa shirika hilo ni kushindwa kuhimili ushindani uliopo wa biashara ya sekta hiyo.

  Amesema kuwa taratibu za kulivunja rasmi Shirika la Utalii la Zanzibar zinatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao kuanzia sasa.

  Akizungumzia Shirika la Utangazaji Zanzibar(ZBC) amesema linatarajia kuweka vifaa vipya vya Studio pamoja na kununua gari moja ya kurushia matangazo ya moja kwa moja kutoka nje ya studio hasa katika sherehe na maadhimisho ya Kitaifa.

  Waziri Said Ali Mbarouk amesema lengo la Wizara ni kusimamia mazingira bora ya kazi ili kuliwezesha Shirika la ZBC kutoa huduma bora na zenye ufanisi.

  Akitoa maoni ya Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari Mwenyekiti wa kamati hiyo Mlinde Mbarouk Juma wameshauri watendaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar kubadilika kiutendaji. kufanyakazi kwa umakini zaidi na kuacha kufanyakazi kwa mazoea .

  “Kwa kuwa uendeshaji wa Mfumo wa Digital unahitaji umakini wa hali ya juu kwa kutokuwa makini tutakuja kulaumiana na kuona ni bora tungelibaki katika mfumo wa analogia”, alisema Mwenyekiti Mlinde.

  Aidha ameeleza kuwa Utalii ni chachu ya maendeleo katika nchi jirani, lakini bado Zanzibar haujapewa kipaumbele na kuwekewa mikakati na kuwanufaisha wananchi wengi.

  “Kamati inatoa rai kwamba dhana ya Utalii kwa wote itekelezwe kwa vitendo na wala sio maneno pamoja na kuwekwa sera na sheria ambazo zitapunguza gharama kwa wazawa.” Alisisitiza Mlinde.

  Wameishauri Wizara kujidhatiti katika kuutangaza Utalii wa Zanzibar kwani kufanya hivyo utaweza kuongeza soko katika mataifa mbali mbali na kuitangaza katika nchi za jirani.

  Katika kutekeleza majukumu yake Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo imeomba iidhinishiwe jumla ya shilingi 9,985,000,000 kwa kazi za kawaida na shilingi 510,000,000 kwa kazi za maendeleo.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwonesha mandhari mbalimbali Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe Tony Blair na mkewe Cherrie Blair alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.PICHA NA IKULU.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi na Bw. Manoj Kohli wa Airtel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Pamoja wa chama hicho alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Beatrice Singano, mmoja wa wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013. PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 202 | 203 | (Page 204) | 205 | 206 | .... | 3278 | newer