Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

New Opportunities In The East African Crude Oil Pipeline(EACOP)

$
0
0
This is a series of articles focusing on the proposed Uganda-Tanzania crude oil pipeline project. My intention is to provide you all the necessary information so we  help the public to effectively involve in this prestigious project.

A lot of people commented on that post. And I  would like to express my sincere gratitude for those who took their precious time to leave their comment on the post.
So in today’s article, I will outline more opportunities that are in dire demand in the proposed East African Crude Oil pipeline project.
Let face them:
1.Pipes and Connection
2.Pipeline Equipment
3.Logistic and Transportation services
4.Pipeline Coating
5.Civil engineering Services
6.Pipe Inspection
7.Audit and Insurance Services
8.IT and Telecommunication services
9.Medical Services
10.Food and accommodation services
11. Training
12. Human resources services
If your business offers some of the services and product mentioned in the list, then you have opportunities to work with East African Crude Oil Pipeline (EACOP)
And if you wondering how to get involved In The East African Crude Oil pipeline project. I have written the entire articles that will give you steps by steps instruction on how to participate in the project. Click the link to read the article.How To Participate In Uganda-Tanzania Crude Oil Pipeline Project

I hope this help. If you have question or suggestion, please reach   tome via Hussein.boffu@tanzaniapetroleum.com. I read all the email.

UJIO WA BAADHI YA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA WAVUTIWA NA FURSA ZA UWEKEZAJI PWANI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo,akizungumza jambo kuhusu masuala ya uwekezaji baada ya kutembelewa na baadhi ya wawakilishi wa makampuni ya uwekezaji kutoka nchini China.

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

WAWAKILISHI wa makampuni ya uwekezaji toka nchini China ,waliofika mkoani Pwani kuangalia fursa za uwekezaji, wamefurahishwa na kuvutiwa na fursa nyingi walizoziona na kuonyesha nia ya kuwekeza. Aidha wameeleza watatuma wataalamu wao watakaojua wawekeze kwenye sekta gani kati ya maeneo na sekta waliyoonyeshwa ili kujiletea manufaa.

Wakizungumza baada ya kumtembelea mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo walieleza, baada ya kuonyeshwa maeneo hayo ya uwekezaji kwa njia ya video ,wameguswa na kufurahishwa kuwekeza mkoani hapo. Mmoja wa wawakilishi wa wawekezaji hao, Liv Ming aliipongeza nchi ya Tanzania kwa ushirikiano na mahusiano yake na nchi yao ,tangu enzi za marais Julius Nyerere na Mao Tse Sung.

“Tumejionea fursa nyingi za kiuwekezaji na tutatuma wataalamu wetu kuja kuangalia na kutupa ushauri tuwekeze kwenye eneo gani kwani tumeona uwekezaji kwenye sekta ya umeme, vipuri vya magari na uhifadhi wa mazao-kilimo,” alisema Ming.
Ming alieleza kuwa,wameona maeneo mbalimbali kwa njia ya video ambayo wanaweza kuwekeza na wataendelea kufanya mawasiliano na mkoa kwa ajili ya masuala ya uwekezaji wa viwanda kwenye sekta mbalimbali.

“Tumevutiwa na mambo mengi pia kuna baadhi ya makampuni ya wenzetu kutoka China wamewekeza viwanda zaidi ya miaka 20 hivyo tutaendelea kuhamasisha wenzetu nao waje kuwekeza,” alisema Ming.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,ujio wa wageni hao ni faraja kwa mkoa huo na Taifa kijumla kwani itasaidia azma ya serikali ya kuwa nchi ya viwanda. Alielezea ,mkoa utaendelea kuhamasisha wawekezaji wa nje na ndani ya nchi ili wawekeze kwenye sekta mbalimbali zilizopo. Mhandisi Ndikilo,alisema wamejipanga kuwa ukanda wa viwanda kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya nchi ya viwanda na uchumi wa kati.

Ujio wa wawekezaji hao ni kufuatia ziara ya wiki mbili iliyofanywa na timu ya baadhi ya viongozi mkoa wa Pwani wakiwemo viongozi na wataalamu waliokwenda kujifunza uhamasishaji na masuala ya uwekezaji nchini China mwezi Oktoba mwaka huu .

Katika safari hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa ambapo waliweza kuzungumza na makampuni 106 huku 30 kukubali kuja mkoani Pwani kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji na hatimae kuwekeza.

NBC NA SANLAM WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) akisaini mkataba wa ushirikiano katika ya NBC na Kampuni ya Bima ya Sanlam, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka na kushoto kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman.  Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake ndani ya matawi ya NBC nchini kote Waliosisima kutoka kushoto ni, Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. 

 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Tanzania, Manasseh Kawoloka (kushoto) na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Tanzania, Khamis Suleman (kulia), wakifurahi baada ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano. Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uenezaji Biashara na Masoko wa Sanlam General, Jabir, Kigoda, Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Benjamin Nkaka na Meneja Mkuu Bima Binafsi wa Sanlam Life, Wilson Mnzava. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi (katikati), akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano katika ya benki hiyo na Kampuni ya Bima ya Sanlam. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General, Manasseh Kawoloka na kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life, Khamis Suleiman. Ushirikiano kati ya NBC na Sanlam utawawezesha wateja kupata huduma za kibenki pamoja na huduma za bima za bidhaa zake katika matawi ya NBC nchini kote.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TANGAZO MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU WA TANZANIA BARA

RC Wangabo Ameitaka Manispaa Ya Sumbawanga kuboresha Masoko

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameitaka Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha wanaboresha mazingira ya masoko yaliyopo kwenye Manispaa hiyo ili wananchi waweze kupata huduma kwenye maeneo hayo bila ya kulazimika kufika katikati ya mji kupata huduma hiyo.

Amesema kuwa wakuu wa idara katika Manispaa hawanabudi kuhakikisha wanashuka kuwafuata wananchi na wafanyabiashara wa masoko hayo na kusikiliza kero zao na kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya masoko hayo ikiwemo majengo, usafi wa mazingira na vyoo.

“Nimeambiwa changamoto nyingi sana na wafanyabiashara wa soko la sabasaba na wamekuwa wakifanya biashara zao kwenye mazingira machafu hali ambayo haizoeleki na haifai kuendelea kuwepo, hivyo manispaa lazima iweke kambi kusikiliza kero zao na kuzitatua, kwani lipo kwenye uwezo wao,” Mh. Wangabo alisisitiza.

Aidha, ameitaka manispaa hiyo kuhakikisha usalama wa biashara za wafanyabiashara hao unaimarika ili kupunguza malalamiko yao na kuongeza kuwa atahakikisha malalamiko hayo yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Matola katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa samaki wa soko la Sabasaba katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wafanyabiashara wa soko la OTC Kizwite katika Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akinunua bidhaa alipotembelea Soko la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea Soko la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.



TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu na ajali za barabarani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii sheria za usalama barabarani. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya kifo kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 26.11.2017 majira ya saa 10:00 Asubuhi huko Maeneo ya Kadege, Kata ya Forest, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Gari yenye namba za usajili T.913 BEW aina ya Toyota Ipsum iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye MUGANIZI RAPHAEL [34] Mkazi wa Simike iligongana na gari yenye namba za usajili T.204 CSZ/T.670 BEZ aina ya Scania Lory ikiendeshwa na HOSEA S/O MWASHAMBWA [28] Mkazi wa Uyole na kusababisha kifo kwa dereva wa Gari yenye namba za usajili T.913 BEW Toyota Ipsum.

Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa gari yenye namba za usajili T.913 BEW Toyota Ipsum hasa ukizingatia eneo hilo ni lenye mteremko mkali. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. Dereva wa lori alikimbia mara baada ya ajali na juhudi za kumtafuta zinaendelea. Upelelezi unaendelea.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama. Hata hivyo Kumekuwa na matukio 02 ya mauaji kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 25.11.2017 majira ya saa 22:06 usiku huko katika Kijiji cha Ipwizi, Kata ya Mjele, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MINZA PAUL [25] Mkazi wa Ipwizi alifariki dunia baada ya kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aliyefahamika kwa jina SHILONDI MAKWENGE ambaye alitoroka baada ya tukio.

NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA KITUO CHA UTOTOLESHAJI VIFARANGA VYA SAMAKI WILAYA YA MKURANGA

$
0
0

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akimsikiliza kwa makini mmiliki wa Jan's Aqua Centre Johnson Noni anayejishughulisha na ufugaji wa samaki aina ya sato katika kijiji cha Kisayanu kata ya Mbezi Wilaya ya Mkuranga, ikiwa ni katika ziara ya naibu waziri.

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega amefanya ziara katika vijiji vinne vya kata ya Mbezi na kufurahishwa na hatua kubwa waliyofikia kwenye ujenzi wa zahanati za kijiji sambamba na bwawa la Samaki lenye uwezo wa kutengeneza vifaranga milioni 2 kwa mwezi mmoja.

Akiwa katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega aliweza kufahamu namna utotoshaji wa mayai ya samaki unavyofanyika ikiwemo changamoto wanazokutana nazo wafugaji wa samaki hao.

Ulega amesema, mpaka sasa kuna maeneo makubwa matatu nchini yanayofanya utotoshaji wa vifaranga ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ni Mkuranga pekee  ila kuna Kibirizi Kigoma, Naliendele Mtwara na Kinguruwira Morogoro na amechukua changamoto ya kodi ya ongezeko la thamani  kama suala la kwanza kabisa na kama wizara watalisamia kwa ukubwa wake.
Mmiliki wa eneo hilo linalopatikana katika kata ya Kisayani lijulikanalo kama Jan'S Aqua Centre , Johnson Noni amesema za ufugaji huo wa samaki aina ya sati kuwa ni kubwa sana hasa katika upatikanaji wa chakula cha samaki kwa sababu ya kodi kuwa juu.

Noni amedai kuwa, samaki wanatumia sana Vyakula vya Protein ambapo ni dagaa, soya ila ukiangalia vyakula hvyo viko juu sana ingawa serikali wametoa kodi katika mbegu za soya ila virutubisho vinavyotengenezea chakula cha mifugo bado kipo juu.

Ameeleza kuwa uwezo wa bwawa lake linaweza kutoa vifaranga milioni mbili kwa mwezi kwa ajili ya kuviuza kwa watu wengine wanaotaka kufuga samaki na zaidi pia wana uwezo wa kuacha samaki wakue na kuwauza kwa wateja kwa ajili ya kitoweo.

Kwenye Ziara hiyo, Naibu Waziri alitembelea kijiji cha Ngalambe, Mwazenga na Miyekela na kujionea namba ujenzi wa Zahanati za vijiji hivyo zimefikia katika hatua gani ya ujenzi pamoja na kuwapatia fedha na mifuko ya saruji.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akikagua baadhi ya maeneo ya ufugaji wa samaki aina ya sato yanayomilikiwa na Johnsona Noni.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akikabidhi mifuko ya Saruji kwa wanakijiji wa Miyekela kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Zahanati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Ujenzi Abdalla Ulega akisalimiana na wakina mama wa kijiji cha Mwanzenga wakati wa ziara yake katika kata ya Mbezi wilaya ya Mkuranga.
Picha zote na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii.

WAANDISHI WA KIGOMA WAFUNDWA JINSI YA KURIPOTI KUHUSU WAKIMBIZI NA UMAKINI DHIDI YA CHANGAMOTO YA UWEPO WA SHERIA MPYA YA HABARI.

$
0
0


Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya siku mbili kuhusu kuripoti habari za wakimbizi na umakini dhidi ya changamoto ya uwepo wa sheria mpya ya habari mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa(UN)na kuratibiwa na MISATAN Tanzania.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka kushoto ni Mhariri mtendaji wa Guardian Jesse Kwayu (kushoto)James Marenga Wakili kutoka mahakama kuu.
Afisa uhusiano na mawasiliano,Ofisi ya mratibu mkazi mashirika ya umoja wa mataifa(UN)Didi Nafisa akitoa mada kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)juu mradi wa pamoja wa Kigoma unaofanywa na mashirika 16 ya umoja wa mataifa katika kambi za wakimbizi zilizopo Mkoani humo.
Baadhi washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kwa makini toka kwa mwezeshaji Jesse Kwayu(hayupo pichani). 
Kaimu Mkurugenzi MISATAN Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZINAZOHUSU SEKTA YA FEDHA NA BIASHARA

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akielezea masuala mbali mbali ambayo yamejadiliwa na Mawaziri wa Tanzania Bara pamoja Visiwani.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akiongoza kikao cha  Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed aboud Mohamed na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. 
 Baadhi ya Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mbali mbali zinazohusu Muungano zinajadiliwa.
 Baadhi ya Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mabli mbali zinazohusu Muungano zinajadiliwa.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

WANAUME WATAKIWA KUWA CHACHU YA MABADILIKO KATIKA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NCHINI

$
0
0
 Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia, Theodosia Mhulo kutoka WLAC Akifungua maadhimisho hayo katika ofisi za REDESO zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo alitoa wito kwa wana harakati na Wadau kwa ujumla kuanza kuwatumia Wanaume kama chachu ya mabadiliko katika vita ya ukatili wa Kijinsia nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya REDESO, Abeid Kasazi akizungumza kabla ya kumakaribisha mgeni rasmi kufungua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani kote, yaliyofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo zilizopo kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Mshauri kutoka  REDESO, Brigitha  Sedekia akitoa somo juu ya ukatili wa kijinsia  kwa watu waliofika katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliokuwa wamekaa Meza kuu wakati wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani wakishiriki kuimba kwa pamoja
 Kundi la Muziki la Wakimbizi linalojulikana kwa jina la Bana ba Zambe wakitoa Burudani wakati wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani
 Sehemu ya wageni waalikwa walioshiriki katika Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani

WAZIRI MKUU AKABIDHI KOMBE KWA TIMU YA AFISI KUU ZANZIBAR

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Afisi Kuu Zanzibar.Bwana Vuai Jecha baada ya timu yake kuibuka mshindi kwakuifunga timu ya Kwahani mabao 3 kwa 1. katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Aman Zanzibar. Novemba 25/2017. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mwenye nguo nyeupe akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Afisi Kuu Zanzibar. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

ULIPOFIKIA UJENZI WA JENGO LA ABIRIA (TERMINAL III) UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM

CHUO KIKUU MZUMBE KUTUNUKU SHAHADA MBALIMBALI KWA WAHITIMU 3461

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi ya Mbeya Desemba 8 na Chuo cha Kampasi ya Dar es Salaam Desemba 22. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya mahafali hayo, Dk. Mrisho Malipula na katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Mrisho Malipula, akitoa ufafanuzi juu ya mahafali hayo.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, akitoa ufafanuzi juu ya mkutano wa Baraza la Masajili 'Convocation' utakaofanyika Novemba 29, 2017 Kampasi Kuu Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.


Morogoro, Tanzania-Novemba 27


MAHAFALI ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe yanatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 30, 2017, jumla ya wahitimu 3,461 katika mwaka wa masomo 2016/2017 wanatarajiwa kutunukiwa shahada, stashahada na astashahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas samatta, kati ya wahitimu hao ni

*Shahada ya Uzamivu (PhD) ni 4 (0.12%)

*Shahada za Umahiri (Masters) ni 1,005 (29.04%)

*Shahada za Kwanza (Bachelors) ni 2,063 (59.61%)

*Stashahada (Diploma) ni 191 (5.52%)

*Astashahada (Certificate) ni 198 (5.72%).


Kati ya wahitimu wote waliohitimu Kampasi Kuu ni 2,119 (61.23%).

Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe Mbeya ni 734 (21.21) na Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe Dae es Salaam ni 608 (17.57%).

Mahafali hayo yanatarajiwa kufanyika Kampasi Kuu Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi Mbeya Desemba 8 2017 na Chuo cha Kampasi Dar es Salaam Desemba 22 2017.

Mahafali hayo yatatanguliwa na mkutano wa 17 wa baraza la Masajili Çonvocation' utakaofanyika Novemba 29 2017 katika ukumbi wa mihadhara wa Fanon, uliopo kampasi Kuu. Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe kuanzia mwaka 2002 na wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Maendeleo (IDM) wanakaribishwa kuhudhuria mkutano huo.

Mjadala mahususi na nafasi ya wahitimu na wanachuo katika kuchangia maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe utafanyika.

Aidha Baraza la Masajili linaendelea kuwahamasisha wahitimu wote wa Chuo Kikuu Mzumbe na wadau wengine kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa hosteli ya wanachuo wa kike kupitia 'Çonvocation Fundraising Account'namba 01o150209448900 iliyopo Benki ya CRDB, Tawi la Mzumbe.

DKT SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA CHINA NCHINI, PIA AAGANA NA MABALOZI WAOIWAKILISHA TANZANIA KATIKA NCHI ZA MISRI NA ZAMBIA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke, alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar na kwa mazungumzo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar Dk Shein Ikulu leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kulia kwa Balozi huyi ni Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi zake, Zanzibar Balozi Xie Xiuowu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha Nchi za Zambia na Misri, kulia Balozi wa Tanzania Nchini Misri Mhe. Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor na Balozi wa Zambia Mhe Abrahaman Kaniki, walipofika Ikulu Zanzibar kumuaga Rais wa Zanzibar leo. (Picha na Ikulu)

Zabuni Mradi wa Umeme wa Stiegler’s yafunguliwa

$
0
0
Zabuni ya Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha Umeme kiasi cha MW 2100 kwa kutumia maporomoko ya maji katika Mto Rufiji (Stiegler's Gorge) imefunguliwa leo tarehe 27/11/2017 ambapo Kampuni 81 zilijitokeza kununua nyaraka za Zabuni hizo na kampuni Nne ndizo zilizorudisha nyaraka za zabuni husika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ugavi ya Wizara ya Nishati, Armon Macachayo wakati wa kikao cha Zabuni hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam.

Macachayo alisema kuwa baada ya ufunguaji wa Zabuni husika, Zoezi linalofuta ni kufanyika kwa tathmini ili kupata Kampuni moja itakayokidhi vigezo vya kukabidhiwa mradi. Zabuni hiyo ilitangazwa tarehe 30 Agosti, 2017 ambapo Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, ilialika Taasisi Binafsi na Kampuni zenye uwezo kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza kuomba zabuni husika.

Akitoa taarifa za kutangazwa kwa Zabuni husika mwezi Agosti, 2017, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alisema kuwa Mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga mradi huo ni yule atakayeridhia kujenga mradi husika kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi na kusema kuwa kukamilika kwa mradi husika kutasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme nchini.

Inatarajiwa kuwa, baada ya zoezi la tathmini na majadiliano ya mkataba wa ujenzi kukamilika, mwanzoni mwa mwezi Januari mshindi wa zabuni hiyo atakabidhiwa Mradi ili kuweza kuanza kazi ya ujenzi wa mradi mara moja.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alishukuru kampuni zote zilizojitokeza kununua zabuni husika na kuwakaribisha kuwekeza katika miradi mingine ya uzalishaji Umeme.
Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga akishuhudia ufunguaji wa Zabuni ya Ujenzi wa mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge (MW 2100) uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi, Wizara ya Nishati, Armon Macachayo na wengine ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na watendaji kutoka Kampuni mbalimbali.
Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na watendaji kutoka kampuni mbalimbali zilizonunua zabuni ya Mradi wa Umeme wa Stiegler’s Gorge wakiwa katika kikao cha ufunguaji wa Zabuni hizo jijini Dar es Salaam.

Tamasha la Vodacom Pinduapindia lafana jijini Mwanza

$
0
0
Msanii wa muziki wa Singeli Manfongo, akitumbuiza kwenye viwanja vya Magomeni-Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, wakati wa Tamasha la Pinduapindia lililoandaliwa na Vodacom Tanzania PLC,kwajili ya kuwaelimisha wateja wao kuhusiana na kifurushi cha pinduapindua.
Msanii wa muziki kizazi kipya Young Killer,akitumbuiza kwenye viwanja vya Magomeni-Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, wakati wa Tamasha la Pinduapindia lililoandaliwa na Vodacom Tanzania PLC,kwajili ya kuwaelimisha wateja wao kuhusiana na kifurushi cha pinduapindua.

JAPAN YAONYESHA NIA KUIJENGA DODOMA KWA MIUNDOMBINU YA KISASA

$
0
0
SHIRIKA la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) limesema liko tayari kushirikiana na Serikali kujenga miundombinu ya kisasa ya usafiri, Nishati ya umeme, maji na usafi wa mazingira katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma. Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Bw. Hiroshi Kato wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Jijini Dar es Salaam.

Bw. Kato alisema kuwa mradi mwingine wanaotaka kuutekeleza katika mji wa Dodoma ni udhibiti wa taka ngumu na kwamba wanachosubiri ni Serikali kuainisha maeneo ya vipaumbele vilivyoko katika mpango mji wa Dodoma. Aidha Makamu huyo wa Rais wa JICA alisema kuwa Shirika lake litaendelea kusaidia eneo la kilimo hususan kilimo cha mpunga ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuwakomboa wakulima.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amelishukuru Shirika hilo kwa kuonesha nia ya kusaidia ujenzi wa mji wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya nchi. Alisema kuwa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuupanga mji wa Dodoma mapema ili kuondoa changamoto za msongamano wa huduma za jamii kwenye eneo moja kama ilivyo Jijini Dar es Salaam.

“Pamoja na umuhimu wa miundombinu ya maji, umeme, usafiri wa mjini, lakini pia tunataka tujenge mapema njia za juu (ring roads) ili kudhibiti msongamano wa magari” alisema Dkt. Mpango.

Aliongeza kuwa mradi mwingine wa kipaumbele katika mji huo ni ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo la Msalato, karibu kilometa 20 kutoka katikati ya mji huo ili kurahisisha usafiri kwa njia ya anga. Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazopata ufadhili mkubwa wa miradi mbalimbali ya maendeleo kutoka Japan kupitia Shirika hilo la Kimataifa la Maendeleo (JICA).

Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa barabara ya juu (fly over) katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam, upanuzi wa awamu ya kwanza ya barabara mpya ya Bagamoyo (Mwenge-Tegeta) na ufadhili mpya wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka Morocco hadi Mwenge.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase, pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa pili kulia) wakijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu, nishati, kilimo na maji, walipokutana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Hiroshi Kato (hayupo pichani) katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Elijah Mwandumbya akizungumzia mabadiliko ya Sheria ya Kodi yaliyofanywa hivi karibuni ambayo yanalenga kutoa misamaha ya kodi yenye tija kwa umma wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), wa nne kushoto na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali ya Japan, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

SERIKALI YAZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA KONDOMU

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega  akikata  utepe kushairia  uzinduzi wa mkakati wa kandomu kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba Mosi. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, serikali imezindua mkakati wa Taifa wa Kondomu na wiki ya maonyesho na Huduma ili kuhakikisha maambukizi dhidi ya ugonjwa huu yanapungua kwa kiasi kikubwa ama kumalizika kabisa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Adallah Ulega, amesema mkakati huu umetayarishwa kueleza vipaumbele vya kimkakati vinavyohitajika kupungiza maambukizi ya VVU, Magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa
 "Takwimu za matumizi ya kondomu kwa Tanzania ni asilimia 50, matumizi haya yako chini wakati kondomu zikitumiwa kwa usahihi na mara kwa mara zinauwezo wa kupunguza maambukizi ya VVU" amesema Ulega
 Amesema mkakati huo,  unakusudia kuongeza matumizi ya Kondomu kwa wanawake na wanaume kutoka 34% kwa wanawake na 40.5% kwa wanaume ya mwaka 2012 had I 55% kwa wote ifikapo mwaka 2018.  

Aidha amesema vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 watoe taarifa ya kutumia kondomu wakati wa ngono.
"kiwango kidogo cha matumizi ya kondomu kama njia ya kuzuia magonjwa ya ngono kinatishia kufikiwa kwa malengo ya muda mrefu ya nchi tuliyojiwekea hii ikiwa ni pamoja na malengo ya dunia ya sifuri Tatu ifikapo 2030 hasa ikizingatiwa kwamba kondomu zina uwezo wa kings kwa zaidi ya 80%.
Aidha amesema, pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali, Jamii bado inamchango mkubwa katika kupambana na magonjwa ya ngono na ukimwi.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko akieleza jinsi maambukizi ya VVU yalivyo kwa sasa amesema, takribani watu elfu 55 kwa mwaka wanamaambukizi mapya na kundi kubwa likiwa ni vijana.  kati ya hao asilimia 40 ya vijana wanamaambukizi mapya wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.

Amesema kati ya hao asilimia 40,  asilimia 80 ni watoto wa kike.
Amesema matumizi ya kondomu yatasaidia sana maambukizi mapya ya VVU na kuwawezesha watu kuishi maisha mazuri huku wakiendesha shughuli zao.

Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yanatarajia kufanyika desemba Mosi mwaka huu, n kitaifa yatafanyikia jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa Rais, Samoa Suluhu Hassan.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akitembelea katika mabanda mbalimbali ya maonesho yaliyopo ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja leo Jijink Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kandomu kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba Mosi.
 Naibu Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akizungumza na taasisi mbalimbali katika uzinduzi wa mkakati wa kondomu uliofanyika leo kwenye Viwanja vyw Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Abdalla Ulega akielezewa namna ya kuvaa kondomu ya kiume na muelimishaji kuhusu matumizi sahihi ya kondomu kutoka T- Marc Tza Benjamin Salema alipotembelea mabanda yaliyopo ndani ya Viwanja vya Mnazi leo Jijini Dar es Salaam.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGA PESA KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akizungumza na wataalam, wanahabari na viongozi wa Wizara hiyo kutoka katika sekta ya Uvuvi, baada ya kuonyeshwa zana zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu, katika kanda ya Dar es Salaam.
baadhi ya zana zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu katika kanda ya Dar es Salaam.

Akiwa katika zoezi la kupongeza kikosi maalum kilichoanza oparesheni ya kupambana na uvuvi haramau katika bahari ya hindi leo, zoezi lililokwenda sambamba na kuonyeshwa vifaa vinavyotumika katika uvuvi haramu vilivyokamatwa katika zoezi hilo lilioanza mwezi Julai mwaka huu, Waziri wa mifugo na Uvuvi Mhe. Luahaga Mpana amezitaka halmashauri ambazo shughuli za uvuvi zinafanyika kutenga fedha ili kuweza kupambana na uvuvi haramu.

Mpina ambaye ameshangazwa na kitendo cha Halmashauri hizo kukusanya fedha za ushuru zitokanazo na shughuli na uvuvi na kujisahau kabisa kuingia katika zoezia la kupambana na uvuvi haramu kwa kutenga fedha hususan za kufanya doria.

Aidha, Mpina Amewataka viongozi wakuu wa Wizara yake, Katibu Mkuu Dkt. Yohana Budeba na Kaimu Mkurugenzi wa maeneleo ya Uvuvi Bw. Magese Bulayi kutembea na barua rasmi katika ziara zao za kikazi kwenye halmashauri husika zilizokuwa tayari kuwawajibisha watumishi wazembe katika zoezi zima la kupambana na uvuvi haramu.

“Mkurugenzi wa maendeleo ya uvuvi na katibu Mkuu,nawaagiza mtembee na barua zilizotayari kusimamisha au kufukuza kazi watumishi wazembe katika halmashauri, barua hizo zibaki wazi katika sehemu ya kujaza majina yao tuu, na ndani ya mwaka mmoja nataka tukomeshe kabisa uvuvi haramu. “ Alisisitiza Mpina.

Awali akieleza madhara ya matumizi ya kitoweo cha samaki waliyovuliwa kwa njia ya vilipuzi na mabomu, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yohana Budeba alisema kuwa samaki wanaovuliwa kwa njia hiyo huleta madhara makubwa kwa walaji ikiwa ni mapoja na magonjwa ya tumbo na Saratani

NYUNDOZZZ ZAANZA KUTEMBEZWA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI, UBUNGO JIJINI DAR

$
0
0
 Baadhi ya Mafundi wa Mabomba ya maji, wakiendelea na zoezi la kuhamisha mabomba katika tenki la maji nje ya Majengo ya Wizara ya Maji, Ubungo jijini Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya kubomoa majengo hayo ili kupisha ujenzi wa barabara za juu, kufuatia agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
 Fundi akikata moja ya Mabomba hayo.
 Ubomoaji ukiendelea katika majengo ya Wizara ya Maji, Ubungo jijini Dar es salaam leo.
 Matenki ya maji yakihamishwa kupisha bomoa bomoa.
 Baadhi ya majengo yakiwa yameshatembezewa nyundozzz.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images