Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

WASHINDI WA DROO YA TATU WA PROMOSHENI YA ZALI LA MWANASPOTI WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

$
0
0
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Huldermary Munisi(kushoto) akimkabidhi Fadhili Mahiche zawadi ya Pikipiki mara baada ya kuibuka msindi wa droo ya tatu ya Zali la Mwanaspoti inayoendelea nchini.Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika tamasha lililofanyika Viwanja vya Toto tundu Tabata Dar es Salaam.

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited(MCL), kupitia kampeni maalumu ya kazeti lake nguli la michezo la Mwanaspoti katika promosheni ya Zali la Mwanaspoti imekabidhi zawadi za washindi wa droo ya tatu wakati wa tamasha kubwa lililofanyika Viwanja vya Toto Tundu Tabata.

Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Tiketi ya kwenda kushuhudia Ligi Kuu ya Wingereza Ulaya ,Pikipiki moja, Tv 2, nchi 32, zikiwa na vingamuzi vyake vikiwa vimeunganishwa na kifurushi cha mwezi mzima pamoja na simu 2(Smartphone).
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Huldermary Munisi(kulia) akimkabidhi Gogfrey Mpiluka zawadi ya Simu ya mkononi(Smartphone) mara baada ya kuibuka msindi wa droo ya tatu ya Zali la Mwanaspoti inayoendelea nchini.Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika tamasha lililofanyika Viwanja vya Toto tundu Tabata Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Huldermary Munisi(kushoto) akimkabidhi Salvatory Mtenga zawadi ya TV nchi 32, ikiwa na king’amuzi cha Azamu kikiwa kimelipiwa mwezi mzima mara baada ya kuibuka msindi wa droo ya tatu ya Zali la Mwanaspoti inayoendelea nchini.Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika tamasha lililofanyika Viwanja vya Toto tundu Tabata Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Huldermary Munisi(kushoto) akimkabidhi Joyce Eosmsiles zawadi ya Simu ya mkononi(Smartphone) mara baada ya kuibuka msindi wa droo ya tatu ya Zali la Mwanaspoti inayoendelea nchini.Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika tamasha lililofanyika Viwanja vya Toto tundu Tabata Dar es Salaam. 

IGP SIRRO AFANYA ZIARA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati), akiwa ameongozana na kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kipolisi Kinondoni (ASP) Solomoni Mwangamilo (Kulia), alipofanya ziara bandari ya Dar es salaam kukagua magari 31 ya Jeshi hilo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. John Pombe Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akimsikiliza kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kipolisi Kinondoni (ASP) Solomoni Mwangamilo (Kulia), alipofanya ziara bandari ya Dar es salaam kukagua magari 31 ya Jeshi hilo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. John Pombe Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi, kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa.

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA ALIPOFIKA KUJITAMBULISHA LEO IKULU.

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akikabidhiwa Kijarida cha Mahakama Kuu Tanzania na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Profesa Ibrahim Hamis Juma alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Profesa Ibrahim Hamis  Juma alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, akiwa amefuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Profesa Ibrahim Hamis Juma, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha leo.27-11-2017. (Picha na Ikulu)

SPIKA JOB NDUGAI AONGOZA MAWAZIRI, WABUNGE NA VIONGOZI MBALI MBALI KATIKA MAZISHI YA ALIEKUWA MBUNGE WA SONGEA MJINI MAREHEMU MHE. LEONIDAS GAMA

$
0
0

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza Mawaziri, Wabunge pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika Mtaa wa Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.



Viongozi mbali mbali waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Wanafamilia waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini marehemu Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Viongozi mbali mbali waliofika kuuaga mwili wa aliekuwa Mbunge wa Songea Mjini Mhe. Leonidas Tutubert Gama katika tukio lililofanyika leo katika makaburi ya Likuyufusi Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri Mahiga akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni alipomtembea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba 2017.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Italia. Pia wamejadili mikakati ya kuboresha ushirikiano katika sekta ya elimu hususan elimu ya ufundi, miundombinu, utalii, biashara na uwekezaji. 
Mazungumzo ya Kiendelea. 

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AAGIZA MKANDARASI WA REA KUHAKIKISHA UMEME UNAWAKA KISIJU NA MKAMBA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameagiza mkandarasi anayesimamia Mradi wa  umeme wa vijijini REA mkoa wa Pwani kufikia Ijumaa aweze kuhakikisha nyumba 14 za Kijiji cha Kisiju ziwe tayari zimeshaingia umeme pamoja mkandarasi kuweka transfoma zilizoharibika haraka sana kwenye Kijiji cha Kizapara Mkamba.

Akiwa ameambatana na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega, Naibu Waziri Wa Nishati ameyasema hayo mbele ya wananchi wa kata ya Kisiju na Mkamba na kuahidi kuwa ifikapo siku ya Ijumaa ataenda  kuhakikisha kama kweli nyumba hizo zitakuwa zimeshaingia umeme na kuwaka.

Naibu Waziri wa Nishati amemtaka mkandarasi ahakikishe transfoma hizo mpaka siku ya Ijumaa ziwe zimeshafungwa kuanzia kesho huku akiwaagiza Shirika La Umeme Nchini Tanesco pamoja na REA kuhakikisha matatizo hayo yanamalizika.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye ni Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega katika kata ya Kisiju  wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa umeme wa vijijini REA kwenye Kata ya Kisiju na Mkamba na kuagiza Mkandarasi anayesimamia mradi huo kuhakikisha Ijumaa umeme unawaka kwenye vijiji hivyo.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wanakijiji wa Kisiju wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miundo mbinu ya mradi wa umeme wa vijijini REA na kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi na kumuagiza mkandarasi kuhakikisha umeme unawaka kufikia siku ya ijumaa kwa kata ya Kisiju na Mkamba.

Subira amesema kuwa, umeme huo wa REA hatua ya tatu  takribani vijini 25 vya wilaya ya Mkuranga vimeingia kwenye mradi huo na kiujumla vitakuwa vijiji 43, na serikali imedhamiria kuanzia 2017 hadi 2021 vijiji vyote 7873 vyote viwe vimepelekewa umeme.

Mbunge wa Mkuranga Ulega, amesema wananchi wa baadhi ya vijiji vya Mkuranga walikwamisha mchakato wa kupatikana kwa umeme wa REA kwa kudai fidia ya maeneo yao yaliyotakiwa kupita mradi huo.

"Umeme wa REA ambao ni wenye gharama nafuu zaidi umekwamishwa kwa kipindi kirefu na wananchi wenyewe kwani wengi wao walikuwa wanadai fidia ya maeneo yaliyotakiwa kupita mradi huo," amesema Ulega.

Ulega amesema kuwa, mradi huo wenye manufaa makubwa kwa wananchi wavijijini ulikwamishwa na wao wenyewe kwa takribani miaka miwili na kufikia wengine kuamua kulipa fidia kwa wanakijiji waliokataa mradi huo kupita kwenye maeneo yao.

Naibu waziri wa Nishati aliweza kutembelea kijiji cha Kisiju na Mkamba na kujionea namna mradi wa REA ulipofikia pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi katika kupata umeme huo.

Takribani Bilioni 469 kwa fedha za ndani na bilioni 30 kwa fedha za nje zimetengewa kwa ajili ya Wizara ya Nishati kuhakikisha umeme unafika katika Vijiji vyote na ifikapo June 2019 kwa awamu ya kwanza vijiji takribani 3559 vitakuwa vimeshapata umeme wa uhakika
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na wananchi wa kata ya Kisiju wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkranga Abdallah Ulega akizungumza na wanakijiji wa Kiparaza kata ya Mkamba wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ya ukaguzi wa mradi wa umeme vijijini REA kwenye kata za Kisiju na Mkamba.

Naibu waziri wa Nishati Subira Mgula akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdalaah Ulega wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundo mbinu ya mradi wa umeme wa vijijini REA  katika kata za Kisiju na Mkamba. Picha zote na Emmanuel Masaka.

KIPINDI CHA DIRA YA DUNIA JUMATATU

KUZINGATIA MAADILI NA KUPIGA VITA RUSHWA NDIO MSINGI MKUU WA MAENDELEO YA TAIFA LETU

$
0
0


Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) akimkabidhi nyaraka kuhusu maadili mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI Bi. Janeth Mishinga wakati wa uzinduzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa nchini.
Sehemu ya washiriki waliohudhuria ufunguzi wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani S. Jafo (Mb) 
Baadhi ya wanafunzi waliowawakilisha wenzao wakati wa Klabu za Maadili wakati wa wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Hazina Ndogo.

Tanesco yakanusha Taarifa ya uzushi inayosambaa katika mitandao ya kijamii

$
0
0
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  linakanusha Taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikiwataka Wateja kununua Umeme kwa wingi kutokana na zoezi linaloendelea la kubomoa Ofisi za Makao makuu ya TANESCO  hivyo kupelekea  kuathirika kwa mfumo wake wa LUKU.

Tunaomba Wateja wetu wapuuze taarifa hiyo, kwani TANESCO kama ilivyobainisha katika taarifa ya awali , huduma zote za umeme ikiwemo ya manunuzi ya LUKU zitaendelea kama kawaida .

Tutaendelea kutoa taarifa kila inapohitajika.

Tafadhali usisogelee, usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: -

Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz 

Mitandao ya Kijamii 
www.facebook/tanescoyetultd 

twitter.com/tanescoyetu 

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu 
Novemba 27, 2017

WADAU WA NGUVU WATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI KATIKA UONGOZI WA BIASHARA CHUO KIKUU CHA ESAMI ARUSHA

$
0
0

Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) ,Florian Mutabazi akipokea Cheti chake kutoka kwa Waziri wa Elimu wa Malawi,Bright Msaka baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA) Chuo Kikuu cha Eastern and Southern African Management Institute(ESAMI) kilichopo jijini Arusha katika mahafali yaliyofanyika chuoni hapo,wahitimu wametoka nchi 32 barani Afrika.Picha na Filbert Rweyemamu 
Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Florian Mutabazi akiwa mwenye furaha baada ya baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA) 
Mdau wa blog za kijamii ,Yotham Ndembeka ambaye ni mtumishi katika Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha akipongezwa na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Eastern and Southern African Management Institute(ESAMI)kilichopo jijini Arusha,Profesa Bonard Mwape baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA). 
Afisa Habari katika Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),Florian Mutabazi(kushoto) akifurahia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Utawala na Fedha,Jesca Eriyo. 
Picha ya pamoja ya uongozi wa taasisi ya ESAMI. 
Mtumishi Mwandamizi katika Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Grace Mbaruku(kulia) akifurahia baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara(MBA). 

MASAUNI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI NYUMBA MPYA ZA ASKARI POLISI MKOANI MARA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia),akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara,Adam Malima (watatu kulia) na viongozi wengine, baada ya kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara, kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari hao
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano, kukagua nyumba za askari polisi na familia zao zilizopo kata ya Mukonde, Mkoani Mara, Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, baada ya kukagua nyumba za askari polisi na familia zao zilizopo kata ya Mukonde, Mkoani Mara,wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano.Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara kwa Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
Familia za askari wanaotarajiwa kuhamia katika nyumba mpya zilizopo katika eneo la Mukonde, wakimsikiliza Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati alipotembelea kuona maendeleo ya mradi huo ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani Mara. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Zabuni Mradi wa Umeme wa Stiegler’s yafunguliwa

$
0
0
Zabuni ya Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha Umeme kiasi cha MW 2100 kwa kutumia maporomoko ya maji katika Mto Rufiji (Stiegler's Gorge) imefunguliwa leo tarehe 27/11/2017 ambapo Kampuni 81 zilijitokeza kununua nyaraka za Zabuni hizo na kampuni Nne ndizo zilizorudisha nyaraka za zabuni husika. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ugavi ya Wizara ya Nishati, Armon Macachayo wakati wa kikao cha Zabuni hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam.Macachayo alisema kuwa baada ya ufunguaji wa Zabuni husika, Zoezi linalofuta ni kufanyika kwa tathmini ili kupata Kampuni moja itakayokidhi vigezo vya kukabidhiwa mradi.

Zabuni hiyo ilitangazwa tarehe 30 Agosti, 2017 ambapo Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, ilialika Taasisi Binafsi na Kampuni zenye uwezo kutoka ndani na nje ya nchi kujitokeza kuomba zabuni husika.

Akitoa taarifa za kutangazwa kwa Zabuni husika mwezi Agosti, 2017, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alisema kuwa Mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga mradi huo ni yule atakayeridhia kujenga mradi husika kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi na kusema kuwa kukamilika kwa mradi husika kutasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme nchini.

Inatarajiwa kuwa, baada ya zoezi la tathmini na majadiliano ya mkataba wa ujenzi kukamilika, mwanzoni mwa mwezi Januari mshindi wa zabuni hiyo atakabidhiwa Mradi ili kuweza kuanza kazi ya ujenzi wa mradi mara moja.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alishukuru kampuni zote zilizojitokeza kununua zabuni husika na kuwakaribisha kuwekeza katika miradi mingine ya uzalishaji Umeme.
 Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia kwa waliokaa) akishuhudia ufunguaji wa Zabuni ya Ujenzi wa mradi wa Umeme wa  Stiegler’s Gorge (MW 2100) uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Katikati  ni  Mkurugenzi wa Idara  ya Manunuzi, Wizara ya Nishati, Armon Macachayo na wengine ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na watendaji  kutoka Kampuni mbalimbali. 

Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na watendaji kutoka kampuni mbalimbali zilizonunua zabuni ya Mradi wa Umeme wa Stiegler’s  Gorge wakiwa katika kikao cha ufunguaji wa Zabuni hizo jijini Dar es Salaam.

MTAA KWA MTAA NDANI YA CHUNYA

MAGAZETI YA JUMANNE LEO NOVEMBA 28,2017

MAKAMU WA RAIS AWASILI NAIROBI KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS UHURU KENYATTA LEO

$
0
0


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Robinson Githae na Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Hazara Chana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha wageni katika chumba cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya.

1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Robinson Githae baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya asubuhi hii ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika leo katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. 

Picha na Ikulu


HALMASHAURI ZAAGIZWA KUHAKIKISHA WANAHAMASISHA WANACHI KUWA NA VYOO BORA PAMOJA NA KUVITUMIA

$
0
0
Na,Jumbe Ismailly SINGIDA Nov,28,2017 Magonjwa 

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Joseph Kakundi amewaagiza Maafisa afya wa ngazi zote katika Halmashauri,Hospitalini,Kata na vijiji kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kuwa na vyoo bora kwenye kaya zao pamoja na kuvitumia ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza miongoni mwa jamii.

Naibu Wazziri huyo alitoa agizo hilo alipokuwa akifungua mkutano wa siku tano wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania unaofanyika katika Hoteli ya Katala Beach mjini Singida.

Kwa mujibu wa Kakundi akizungumzia kwa upande wa shule za msingi na sekondari alibainisha kuwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa kila wanafunzi 20 wa kike kutumia tundu moja na kwa wanafunzi 25 wa kiume watumie pia tundu moja,kiwango ambacho hakitoshelezi kutokana na idadi ya matundu yaliyopo katika shule hizo.

“Kwa hiyo lazima walimu wasimamie ili matundu yaliyopo yatumike kikamilifu japokuwa kuna upungufu na tunahitaji hela nyingi sana ili tuweze kufikia viwango vya kitaifa,lakini pale penye upungufu ni lazima tusimamie wanafunzi watumie vile vyoo vizuri”alisisitiza Naibu waziri huyo.

Hata hivyo Naibu Waziri Kakundi alisisitiza kwamba shule yeyote ile isiyokuwa na matundu ya vyoo,shule hiyo haitaruhusiwa kuendelea kutoa huduma kwa wananzi na badala yake serikali haitasita kuifunga mara moja na kuelekezaa kwamba ni lazima pawe na njia zingine za dharura za kuwasaidia wanafunzi hao kwenda kujisaidia.

Akitoa taarifa fupi kwa Naibu Waziri huyo,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Selemani Manyata alisema kwamba takribani asilimia 4 ya wananchi wa Mkoa wa Singida ambao ni sawa na wananchi 11,000 hawana kabisa vyoo bora na asilimia 48 ya wananchi wana vyoo vya muda hali ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji yanayoleta magonjwa ambayo matibabu yake ni gharama kubwa.

“Sisi kama Chama cha Afya ya Jamii Tanzania kuanzia haya magonjwa yanayoweza kuzuilika na kama malengo ya Mileniamu yanavyosema kwamba tupunguze kiwango hicho”alifafanua.Aidha Mganga Mkuu huyo aliweka bayana apia kwamba kutokana na idadi kubwa ya kaya ambazo hazina vyoo wanaendelea kuhamasisha Halmashauri ili wananchi waweze kutumia vyoo.

Hata hivyo Dk.Manyata alitoa mfano kwamba inakadiriwa kuwa mtu mmoja hujisaidia kinyesi kisichopungua uzito wa gramu 250 na kwa mwaka mtu mmoja hujisaidia kinyesi chenye uzito wa kilo 90 kwa siku kinachoenda kwenye vyanzo vya maji.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Afya ya Jamii Tanzania,Dk Mashombo Mkamba alizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliananazzo kuwa ni pamoja na kuelewa na watu kukubali na wawe tayari kupima afya zao kwani mpaka sasa bado watu ni wagumu sana kupima afya zao,labda akishauriwa kupima malaria na siyo ugonjwa mwingine.
 baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku tano wa wanachama wa Afya ya jamii Tanzania wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wa Katala Beach mjini Singida wakiendelea na mkutano wao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)


MAKAMU WA RAIS AWASILI NAIROBI KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI JWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS UHURU KENYATTA

Timu ya mpira wa miguu ya Albino United jijini Dar es Salaam yatembelea Mikumi

$
0
0
 Timu ya mpira wa miguu ya Albino United jijini Dar es Salaam majuzi ilipata fursa ya kutembelea hifadhi ya Mikumi na kujionea vivutio kibao vya kitalii katika ziara iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kama njia mojawapo ya kupromoti utalii wa ndani.
 Timu ya mpira wa miguu ya Albino United jijini Dar es Salaam majuzi ilipata fursa ya kutembelea hifadhi ya Mikumi na kujionea vivutio kibao vya kitalii katika ziara iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kama njia mojawapo ya kupromoti utalii wa ndani.
Timu ya mpira wa miguu ya Albino United jijini Dar es Salaam majuzi ilipata fursa ya kutembelea hifadhi ya Mikumi na kujionea vivutio kibao vya kitalii katika ziara iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kama njia mojawapo ya kupromoti utalii wa ndani.
Picha na Augustina Makoye wa TTB.

MKAZI WA DAR ES SALAAM ATUSUA MILIONI 15 ZA VODACOM TANZANIA

$
0
0
 Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania PLC,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Chiku Saleh(katikati)wakionyeshwa na  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu,namba ya simu ya mshindi  aliejishindia Tsh. Milioni 15/- Godwin Kasembe Mkazi wa kinondoni jijini Dar es Salaam wakati wa kuchezesha droo ya 17  ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno  “CHECK” au “VODA” kwenda namba15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akiongea kwenye simu na mmoja wa washindi wakati wa kuchezesha droo ya 17  ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno  “CHECK” au“VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu,kushoto ni Meneja huduma za Ziada na Tehama wa kampuni hiyo, Mathew Kampambe na Msimamizi mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Chiku Saleh.

Vijana Dar watunukiwa vyeti baada ya kuhitimi masomo ya ufundi kupitia VSOMO

$
0
0
 Mamlaka ya mafunzo ya ufundi VETA leo imekabidhi vyeti vya kuhitimu masomo ya ufundi stadi kwa vijana 8 wa mkoa wa Dar es saalam baada ya  kuhitimu masomo yao ya ufundi wa umeme wa majumbani pamoja na ufundi wa simu mara baada ya kumaliza kusoma kupitia aplikesheni  ya VSOMO na kuhitimu katika viwango vya VETA.
 Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es saalam , Bw. Habibu Bukko aliishukuru  Airtel kwa ushirikiano wake na VETA kupitia  Aplikesheni ya VSOMO ambapo imekuwa ikifaidisha wanafunzi walioko mbali na vyuo vya VETA kuweza kusoma VETA wakiwa popote, vilevile alipongeza vijana hao kwa kutumia simu zao za mkonononi vyema na kuhitimu masomo ya  ufundi
 Alisema jitihada hizi za Kufanikiwa kutoa Masomo ya Ufundi stadi kupitia Aplikesheni ya VSOMO zinaenda sambamba na mikakati iliyojiwekea VETA na  serikali  kwa ujumla katika kutanua wigo ili kutoa wa elimu ya Ufundi stadi hata kwa jamii ambayo bado haifikiwa na miundombinu ya vyuo vya VETA mahali walipo ili  nao kuwawezesha kushiriki maendeleo ya jamii.
“Hadi sasa tunao zaidi ya vijana takribani 54 waliohiti masomo yao kupitia VSOMO na kukabithiwa vyeti vyao. “nawapongeza kwa dhati vijana hawa kwa kuhitimu masomo yao leo. Pia tunao wanafunzi 25  wanasubiri kupangiwa masomo ya Vitendo ili  kuhitimu na kupata vyeti . Nitoe wito kwao kujiandaa vyema kuingia kwenye mafunzo ya viyendo laikini pia kwa watanzania hususani vijana kutumia fursa hii kujisomea masomo ya ufundi  kwa kupitia mfumo huu wa VSOMO wakiwa popote VETA itawahudumua” alisema  Bw. Bukko.
 Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko akikamkabidhi Cheti Mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kwa njia ya mtandao  Sunday Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA  na Kampuni ya Airtel Tanzaniam. Kushoto ni Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano.


 Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA  na Kampuni ya Airtel Tanzaniam. Kushoto ni Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano.
Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA  na Kampuni ya Airtel Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images