Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

Wananchi kuhudumiwa BURE Bugando Jijini Mwanza

0
0
Na George Binagi.

Wananchi jijini Mwanza wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kwenye “Kongamano la Watoa Tiba kwa Vitendo”, litakalofanyika kwenye viwanja vya Hospitali ya Kanda Bugando jijini Mwanza kuanzia jumatano Novemba 29 hadi ijumaa Disemba Mosi mwaka huu, ili kupata huduma ya ushauri kuhusiana na matatizo mbalimbali ikiwemo magonjwa.

Hata hivyo huduma hiyo itatolewa kwa wananchi siku moja tu ambayo ni jumatano Novemba 29, ambapo watahudumiwa bure kuanzia majira ya asubuhi.

Akizungumza na BMG, Mratibu wa kongamano hilo Dr.Joyce Karawa amesema wananchi watapata huduma ya ushauri nasaha bure kuhusiana na mitindo ya kimaisha inayopelekee ulemavu wa kimwili na kiakili na pia namna ya kujiepusha.

“Tunatarajia kuwa na wataalaumu wa afya kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, hospitali ya Rufaa KCMC, hospitali ya magonjwa ya akili Mirembe pamoja na nyinginezo hivyo tunawasihi wananchi kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hiyo bure”. Amesema Dr.Karawa.

Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Watoa Tiba kwa Vitendo Tanzania (Tanzanian Occupational Therapists Association-TOTA), likiwa na kauli mbiu ihimizayo “Kutanua Wigo wa Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Kujenga Uhuru wa Kujitegemea” ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA MELI YA HOSPITALI YA CHINA, AAGANA NA KUSHUKURU WANAMAJI NA MADATARI WALIOKUJA NAYO

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la wanamaji wa Meli ya Hospitali ya China alipotembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017 kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la wanamaji na wanaanga wa Meli ya Hospitali ya China alipotembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017 kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la wanamaji wa Meli ya Hospitali ya China alipotembelea leo Jumapili Novemba 26, 2017 kuwashukuru na kuwaaga baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali na Kiongozi Mkuu wa Meli ya Hospitali ya China Kamanda Guan Bailin   alipoitembele aleo Jumapili Novemba 26, 2017  kuwashukuru na kuwaaga wanamaji na madaktari waliokuja nayo baada ya kutoa huduma kwa wananchi kwa takriban juma zima katika bandari ya Dar es salaam.

WATOTO 20 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA

0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) ya nchini Israel wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa watoto 20 wenye matatizo ya Moyo.

Upasuaji huo ambao unatumia mtambo wa Cathlab umefanyika katika kambi maalum ya matibabu iliyoanza tarehe 23/11/2017 na kumalizika kesho tarehe 27/11/2017. Matibabu yaliyofanyika ni ya kuziba matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo.

Katika kambi hii tunatarajia kufanya uchunguzi wa moyo kwa watoto 100 kati ya hao watoto 60 ambao watakuwa na matatizo makubwa watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua mwakani na watoto 40 watatibiwa hapa nchini.

Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 25 tunaamini hadi kambi itakapomalizika watoto wote hawa watakuwa wamepata matibabu. Watoto 20 waliopata matibabu wengine wameruhusiwa na waliobaki hali zao zinaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika.

Tangu mwaka 2015 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ilianza kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart- SACH) ya nchini Israel ambapo hadi sasa jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na Taasisi hii.

Tunawashukuru sana wenzetu hawa wa SACH kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma ya matibabu bure kwa watoto wenye matatizo ya moyo. Watoto waliotibiwa wamepona na wale ambao walikuwa wanafunzi wanaendelea na masomo yao.

VIJANA WASOMI WATAKIWA KUMSAIDIA RAIS MAGUFULI KULILETEA TAIFA MAENDELEO

0
0

Na Dotto Mwaibale

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila amewataka Vijana wasomi na wanataalumu nchini kumsaidia Rais Dk.John Magufuli kuliletea Taifa maendeleo.

Ndabila ametoa mwito huo jijini Dar es Salaam jana wakati akiwahutubia wasomi wanataaluma katika kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark lenye lengo kwa wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla.

"Ninyi wasomi mmesomeshwa kwa ajili ya kuwatumia wananchi na taifa msaidieni Rais wetu John Magufuli kuliletea taifa la Tanzania na kanisa maendeleo kwani hakuna mtu mwingine tunaye mtegemea zaidi yenu" alisema Askofu Ndabila.

Askofu Ndabila aliwataka wasomi hao waende kwa wananchi wakawanoe na kuweza kuwiva kisawasawa ili waendenane na kasi ya maendeleo anayoihitaji Rais Magufuli.
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Amina Sanga akitoa mada kwenye kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark jijini Dar es Salaam jana lenye lengo wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla.
Vijana wasomi wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.

RAIS DKT MAGUFULI AVAMIA BANDARINI LEO NA KUKUTA MADUDU

0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo toka viongozi wa Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi na TRA kuhusiana na magari ya wagonjwa 53 yaliyofichwa katika kona moja ya Bandari ya Dar es salaam huku wamiliki wake wakiwa hawajulikani alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua sehemu ya magari zaidi ya 6000 yaliyopo bandari ya Dar es salaam mengine yakiwa hapo kwa miaka zaidi ya kumi bila kuchukuliwa na wenye nayo alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo kuhusu magari zaidi ya 50 ya Jeshi la Polisi yaliyopo bandarini toka mwaka 2015 kwa sababu ya kutolipiwa  ushuru alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017

PICHA NA IKULU

PICHA ZA MATUKIO KATIKA KAMBI YA MATIBABU NA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO KWENYE TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA KUSHIRIKIANA NA SAVE CHILD’S HEART-SACH YA NCHINI ISRAEL

0
0
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel Katharina Schmitt akiangali jinsi moyo wa mtoto unavyofanya kazi (Echocardiogram) kwenye kambi ya matibabu na upimaji wa moyo kwa watoto inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Afisa Muuguzi wa JKCI Pal Bhadreshwara na kushoto ni mama wa mtoto.
Mama Judy Shore kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel akielezea jinsi Taasisi hiyo inavyotoa huduma za matibabu ya moyo kwa watoto na mafunzo kwa wafanyakazi wa kada ya afya hapa nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia kambi ya matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization) inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo hadi sasa jumla ya watoto 20 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na hali zao zinaendelea vizuri.Kulia ni Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kutoka JKCI Peter Kisenge.
Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akiongea na waandishi wa Habari kuhusu uhusiano wa Taasisi hiyo na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart- SACH) ya nchini Israel ambapo hadi sasa jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji wa moyo bure nchini Israel. Kulia ni Simon Fisher na kushoto ni Mama Judy Shore wote kutoka SACH.
Watoto wakicheza wakati wakisubiri kwenda kufanyiwa kipimo kinachoangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiogram) katika kambi ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel. Jumla ya watoto 100 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi kati ya hao 60 ambao watakuwa na matatizo makubwa watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu na 40 watatibiwa hapa nchini.

Picha na JKCI

SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU

0
0

Na Ismail Ngayonga- MAELEZO

SERIKALI ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la nchi hiyo (JICA) imesema itaendelea kuisadia miradi mikubwa ya maendeleo nchini ikiwemo barabara ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Hayo yamesemwa mwishoni wa wiki Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida wakati wa utoaji tuzo ya heshima ya Rais wa JICA kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale.

Balozi Yoshida alisema tangu mwaka 1980, JICA imekuwa mshirika wa karibu wa maendeleo na Serikali ya Tanzania ikiwemo kuunga mkono juhudi za kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi kupitia ufadhili wa miradi ya kipaumbele kwa ikiwemo barabara.

Aliongeza kuwa utoaji wa Tuzo ya Rais wa JICA kwa Mhandisi Mfugale imedhirisha imani ya Serikali ya Japan kwa Tanzania katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa JICA, na kuahidi kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi wa Mataifa hayo.

“Misaada ya JICA nchini unajumuisha misaada bila masharti, misaada ya kiufundi, kufadhili miradi kwenye maeneo ya vipaumbele kwa serikali hususan katika sekta za kilimo, miundombinu ya barabara, maji, nishati, utawala na afya” alisema Balozi Yoshida.
Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshinda (kushoto) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
PIX1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa kupewa Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshinda (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa mara baada ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akionyesha Tuzo ya Rais wa JICA katika hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshinda, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Toshio Nagase.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MHANDISI MFUGALE APEWA TUZO YA RAIS WA JICA KWA KUTHAMINI MCHANGO WAKE

MILIONI 500 KUOKOLEWA KATIKA MATIBABU YA WATOTO WENYE UGONJWA WA MOYO

CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA KUANZA KUTOA MAFUNZO MAALUM KWA WATOA HUDUMA ZA UTALII NCHINI KUANZIA KESHO

0
0
 Na Hamza Temba-WMU

Katika kutimiza azma ya Serikali kuboresha huduma za ukarimu kwenye sekta ya utalii nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imekichagua Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro kwa ajili kutoa mafunzo maalum kwa waongoza watalii nchini. 

Mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kesho (Jumatatu) chuoni hapo yatakuwa kwenye mfumo wa kujiendeleza na yamelenga kuwawezesha watoa huduma katika sekta hiyo kupata sifa za kusajiliwa na kupewa leseni ya kuendelea kutoa huduma hiyo kwa mujibu ya sheria ya utalii Na. 11 ya mwaka 2008 kifungu cha 48.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga katika mahafali ya 53 ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa chuo hicho katika kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashada kwenye Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii.

"Katika kutambua utaalamu na uzoefu wa chuo chenu, Wizara yangu imeichagua Mweka kutoa mafunzo yatakayowawezesha waongoza watalii nchini kupata sifa ya kusajiliwa (cheti) na kupewa leseni," alisema Naibu Waziri Hasunga.

"Nimefurahi kusikia kuwa  mmeshajipanga tayari kuanza kutoa mafunzo hayo baada ya kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo na kuainisha mapungufu kwenye taaluma, ujuzi na mitazamo pamoja na kuandaa mtaala wa mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka, Brightone Mbilinyi kuhusu mafunzo ya silaha yanavyotolewa chuoni hapo katika mahafali ya 53 ya chuo hicho yaliyofanyika jana katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Zaidi ya asilimia 60 ya mafunzo chuoni hapo hutolewa kwa vitendo. Wengine Pichani ni Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada (wa pili kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho (wa nne kulia).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Leonard Mgamba kuhusu mafunzo ya taaluma ya wanyamapori yanavyofanywa kwa vitendo chuoni hapo. Wengine pichani ni Balozi wa Nigeria nchini, Sahabi Dada (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Harun Mbogo (kushoto) na Mtenaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiwa ndani ya handaki linalotumika kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa kozi mbalimbali chuoni hapo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akikagua gwaride la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Astashahada na Stashada katika taaluma za usimamizi wa wanyamapori na utalii katika mahafali ya 53 yaliyofanyika chuoni hapo jana katika Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Zaidi ya asilimia 60 ya mafunzo chuoni hapo hutolewa kwa vitendo na wahitimu 224 wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Hotuba ya Naibu Waziri Mhe Anthony Mavunde wakati wa mbio za AIDS TRUST FUND MARATHON-Novemba 25, 2017

RAIS DKT MAGUFULI ATAKA VIONGOZI SERIKALINI KUIGA MFANO WA RC MAKONDA

TAARIFA KUTOKA Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar

0
0

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

WIZARA YA HABARI UTALII UTAMADUNI NA MICHEZO

Tel: 0255 24 2237325/0255 24 2237313                        Idara ya Habari Maelezo
Fax: 0255 24 2237314P.O. Box 2754
maelezozanzibar@hotmail.com,  maelezozanzibar@gmail.com                                                  

Gazeti la Mwananchi la toleo Nam. 6330 la Jumapili Novemba 26, 2017 habari yake kuu inasema  “Butiku: Katiba Z’bar inataka Umoja wa Kitaifa, isipuuzwe”.
Taarifa hii haikuzingatia weledi, imejiegemeza katika ushabiki.
Ukweli ni kwamba hakuna katiba iliyopuuzwa  Zanzibar kama anavyodai Bwana Joseph Butiku. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeundwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 inaeleza bayana muundo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Tunamshauri Mzee Butiku akasome vizuri Katiba ya Zanzibar. Nafasi ya Makamu wa kwanza wa Rais ipo, haijafutwa. Sehemu ya Pili ya Katiba kifungu cha 39 kinazungumzia Makamu wawili wa Rais Zanzibar.
Katika kifungu cha 39 A (1) cha Katiba ya Zanzibar kinazungumzia kuachwa wazi kwa nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
Kifungu hicho kinasema;
Endapo, Ndani ya siku Saba mara baada ya Rais kushika madaraka, Chama kinachostahiki kutoa Makamu wa Kwanza wa Rais, kitashindwa kuwasilisha kwa Rais jina la uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais, Rais bila ya kujali masharti ya kifungu cha 39(1) na (3) cha Katiba, atawacha wazi nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kuteua Makamu wa Pili wa Rais.
Tunamshauri Mzee Butiku asome kwa umakini Kifungu cha 42(A) na vifungu vyengine vya Katiba ya Zanzibar.

Imetolewa na :-
Dk. Juma Mohammed Salum
KNY
Mkurugenzi
Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar
Zanzibar
26, Novemba, 2017

CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA KUANZA KUTOA MAFUNZO MAALUM KWA WATOA HUDUMA ZA UTALII NCHINI

0
0
Na Hamza Temba-WMU
Katika kutimiza azma ya Serikali kuboresha huduma za ukarimu kwenye sekta ya utalii nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imekichagua Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro kwa ajili kutoa mafunzo maalum kwa waongoza watalii nchini. 
Mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kesho (Jumatatu) chuoni hapo yatakuwa kwenye mfumo wa kujiendeleza na yamelenga kuwawezesha watoa huduma katika sekta hiyo kupata sifa za kusajiliwa na kupewa leseni ya kuendelea kutoa huduma hiyo kwa mujibu ya sheria ya utalii Na. 11 ya mwaka 2008 kifungu cha 48.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga katika mahafali ya 53 ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa chuo hicho katika kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashada kwenye Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii.
"Katika kutambua utaalamu na uzoefu wa chuo chenu, Wizara yangu imeichagua Mweka kutoa mafunzo yatakayowawezesha waongoza watalii nchini kupata sifa ya kusajiliwa (cheti) na kupewa leseni," alisema Naibu Waziri Hasunga.
"Nimefurahi kusikia kuwa  mmeshajipanga tayari kuanza kutoa mafunzo hayo baada ya kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo na kuainisha mapungufu kwenye taaluma, ujuzi na mitazamo pamoja na kuandaa mtaala wa mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka, Brightone Mbilinyi kuhusu mafunzo ya silaha yanavyotolewa chuoni hapo katika mahafali ya 53 ya chuo hicho yaliyofanyika jana katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Zaidi ya asilimia 60 ya mafunzo chuoni hapo hutolewa kwa vitendo. Wengine Pichani ni Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Sahabi Dada (wa pili kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho (wa nne kulia).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka, Leonard Mgamba kuhusu mafunzo ya taaluma ya wanyamapori yanavyofanywa kwa vitendo chuoni hapo. Wengine pichani ni Balozi wa Nigeria nchini, Sahabi Dada (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Harun Mbogo (kushoto) na Mtenaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiwa ndani ya handaki linalotumika kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa kozi mbalimbali chuoni hapo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akikagua gwaride la wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka muda mfupi kabla ya kuwatunuku vyeti wahitimu 224 wa kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Astashahada na Stashada katika taaluma za usimamizi wa wanyamapori na utalii katika mahafali ya 53 yaliyofanyika chuoni hapo jana katika Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Zaidi ya asilimia 60 ya mafunzo chuoni hapo hutolewa kwa vitendo na wahitimu 224 wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti. 
Naibu Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akimtunuku cheti mmoja ya wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori, katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka wakati wa mahafali ya 53 yaliyofanyika jana chuoni hapo katika Wilaya ya Moshi Mkoani Kiliamanjaro. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho. Jumla ya wahitimu 224 wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti. 
 Naibu Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akitoa tamko la kuwatunuku kozi mbalimbali wananfunzi 224 wa chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka katika mahafali ya 53 ya chuo hicho ambacho yamefanyika jana mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Prof. Faustin Bee (wa tatu kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

BancABC yashirikiana na Kitengo cha Dharura Cha Muhimbili kutoa bima ya afya kwa watoto

0
0
BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imeshirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kutoa huduma ya bima ya afya itakayofaidisha watoto 100 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia mradi mpya wa afya wa Muhimbili uliozinduliwa leo.

Akizindua mpango huo wa Afya wa Muhimbili Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliishukuru BancABC kwa kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili katika suala hilo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa watoto.

Alisema mradi huo wa Muhimbili kushirikiana na BancABC unaendea sambamba kabisa na malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma ya Afya kwa uhakika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani watoto ndio moja ya makundi ambayo huathirika sana wasipopatiwa huduma za Afya za uhakika.

“Natoa wito kwa wazazi watumie fursa hii iliyotolewa na BancABC kwa ushirikiano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwafungulia watoto wao akaunti BancABC ili kuhakikisha watoto wao wanapata huduma kwa uhakika muda wowote bila ya ulazima wa kuwa na fedha tasilimu pale mtoto anapougua,” alisema.

Alitoa wito pia kwa watoa huduma za kifedha nchini pamoja na mashirika mengine kuhakikisha yanaiga mfano huo wa BancABC kwani wizara yake iko tayarikushirikiana na taasisi ambazo ziko tayari kuimaisha huduma katika sekta ya afya hasa upande wa utoaji huduma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu akikabidhi moja ya kadi za bima kwa watoto zaidi ya 100 wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa na ushirikiano baina ya Kitengo cha magonjwa ya dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na BancABC Tanzania.

Baadhi wa watoto wanufaika na kadi za bima wakiwa na walezi wao wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu

Baadhi ya wafanyakazi wa Kitengo cha magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi100 ya ambao ni mayatima
Baadhi ya wafanyakazi BancABC Tanzania wakifuatilia kwa umakini hotuba  ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima kwa watoto zaidi100 ya ambao ni mayatima.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Kilele cha Tigo Fiesta 2017 chahitimishwa kwa burudani ya kukata na shoka jijini Dar Es Salaam

0
0

Msanii Madee kushoto akiwa na Janjaroo na TundaMan kwa pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia jana.

Ommy Dimpozi akiwa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana

Alikiba akiwa na kundi lake wakitumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta liliofanya hitimisho lake usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.

Vanessa Mdee akiwa na dansa wake wakitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika usiku wa jana  viwanja vya leaders.

Mwanamziki Mkongwa wa BongoFleva Afande sele akiwa  katika jukwaaa la Tigo fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaaam.

Maua Sama akiwa na kundi lake akitumbuiza katika kilele cha Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

KASI YA UTEKELEZAJI YA MIRADI YA MAJI HALMASHAURI YA ITIGI INARIDHISHA

0
0
Utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Itigi umeonekana kuwa wenye kasi inayoridhisha licha ya halmashauri hiyo kuanzishwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kaimu Kaibu Tawala Mkoa wa Singia Buhacha Baltazari Kichinda ametoa tathmini hiyo wakati wa kikao na wataalamu wa halmashauri hiyo ambapo wamejadili mikakati ya kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji.

Kichinda amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa haina wasiwasi kuhusu halmashauri kutekeleza na kusimamia miradi ya maji huku matarajio yakiwa ni ifikapo Juni 2018, asilimia ya upatikanaji wa maji ipande kutoka asilimia 34 za sasa hadi kufikia lengo la mkoa la asilimia 72.

“Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri mnaonyesha dhahiri mmejitosa kuwapunguzia wananchi adha ya kutafuta maji huku wakiacha kwa muda shughuli zao za uzalishaji mali, nina imani mtafikia asilimia 72 hata kabla ya Juni 2018 kwakuwa fedha mnazo na pia mnafanya usimamizi wa karibu wa miradi”, amesisitiza Kichinda.
Ukarabati katika bwawa la Itagata lililoko halmashauri ya Itigi ukiendela, kukamilika kwa bwawa hilo kutasaidia usambazaji wa maji kwa vijiji jirani pamoja na kuwezesha skimu ya umwagiliaji katika kijiji cha Itagata.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Singida na hata halmashauri ya Itigi haina mito inayotiririsha maji mwaka mzima hivyo kusababisha uhaba wa upatikanaji wa maji katika kipindi cha kiangazi huku wananachi wakitegemea mabwawa na visima ambavyo vinatakiwa kujengwa na serikali.

“Kipidi cha Kiangazi kwakweli utawahurumia wananchi wanavyosumbuka kutafuta maji, wanatumia muda mwingi huko na kujikuta wana muda kidogo wa kuzalisha mali, hali hii haipendezi na nina imani pia viongozi wa Itigi hili haliwapendezi ndio maana mmeweka nia ya dhati kulitatua ili wananchi wapate muda mwingi wa kuzalisha kwaajili ya maendeleo ya Mkoa na taifa letu”, amefafanua Kichinda.

Naye Mhandisi wa Maji Mkoa wa Singida Lydia Joseph amesema endapo halmahauri hiyo itasimamia kwa umakini na haraka kukamilika kwa miradi ya Itigi mijini, Kitaraka na Aghondi itasaidia ongezeko la upatikanaji wa maji kwa asilimia 20.
Wataalamu kutoka halmashauri na Mkao wakijadiliana baadhi ya mambo huku wakishuhudia ukarabati wa bwawa la Itagata utakaosaidia kusambaza maji katika vijiji jirani na kuwezesha kilimo cha umwaigiliaji.

Kwa upande wake Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Itigi Evaristo Mgaya amesema halmashauri hiyo inatekeleza miradi ya maji katika vijiji vya Rungwa, Ipande, Sanjaranda, Itigi, Kitaraka na Aghondi huku kukiwa na mradi wa visima 16 vya ‘windmill’ katika vijiji 12.

Mgaya ameeleza kuwa miradi hiyo itakamilika ndani ya kipindi cha mwaka huu wa fedha yaani kabla ya Juni 2018 hivyo kuongeza upatikanaji wa maji kwa zaidi ya asilimia 72.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi Luhende Pius Shija amesema wamewajibika sana kuboresha upatikanaji wa huduma za maji ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi.

Luhende amesema licha ya kuendelea kutekeleza miradi iliyoko kwenye bajeti pia yeye na wataalamu wa idara ya maji wameongeza jitihada kwa  kuwasilisha maombi mengine ya kuonezewa fedha za miradi ya maji ambapo tayari wamekubaliwa hali itayaongeza zaidi upatikanaji wa maji.
Kaimu Kaibu Tawala Mkoa wa Singia Buhacha Baltazari Kichinda akikagua ukarabati wa bwawa la Itagata lililoko halmashauri ya Wilaya ya Itigi, kukamilika kwa bwawa hilo kutasaidia usambazaji wa maji kwa vijiji jirani pamoja na kuwezesha skimu ya umwagiliaji katika kijiji cha Itagata.
Mhandisi wa maji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Emaeli Songaeli pamoja na wataalamu wa halmashauri ya Itigi wafuatilia kwa umakini Kikao cha ufuatiliaji wa miradi ya maji katika halmashauri hiyo.

Mahojiano Maalum na Mpiga Muziki Stadi- Saidi Kanda- Sehemu ya 1

0
0
Mwaka 1989 shirika maarufu la muziki Uingereza , WOMAD, lilimtunuku Mtanzania Saidi Kanda tuzo la Mpiga Ngoma wa Kimataifa wa Mwaka duniani. Kuanzia hapo mzawa huyu wa Bagamoyo aliyezaliwa 1962, anahesabika mpiga ngoma wa nne kiufundi ulimwenguni chini ya magwiji hatari kama Airto Morreira (Brazil) na Changuito (Cuba) ... Baada ya kusakata vituz na wanamuziki mbalimbali akiwemo marehemu Remmy Ongala, Kofi Olomide na msanii maarufu wa kimataifa, Grace Jones; leo Kanda anaongoza kikosi chake kikali cha "Mvula Mandondo" kutangaza albam yake ya kwanza, "Ambush".... KWA SIMU TOKA LONDON inawaletea sehemu ya kwanza ya Sura Tano za mahojiano kumtathmini mtunzi huyu anayetetea (na kuhusudisha ), sana muziki wa kiasili wa Kitanzania nje na ndani ya Afrika Mashariki.

Kilele cha Tigo Fiesta 2017 chahitimishwa kwa burudani ya kukata na shoka jijini Dar

0
0

Alikiba akiwa na kundi lake wakitumbuiza katika jukwaa la Tigo fiesta liliofanya hitimisho lake usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.

Msanii Madee kushoto akiwa na Janjaroo na TundaMan kwa pamoja kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam usiku wa kuamkia jana. 
Ommy Dimpozi akiwa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia jana.

Mwanamziki Mkongwa wa BongoFleva Afande sele akiwa katika jukwaaa la Tigo fiesta usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaaam.

Wasanii Kassim Mganga na Jux wakishirikiana kuimba pamoja kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam juzi.  

MAGAZETI YA JUMATATU LEO NOVEMBA 27,2017

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

Latest Images