Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Kipindi cha Miaka miwili ya JPM madarakani, sehemu ya Pili.


SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU UFANYAJI KILIMO BORA CHA MBOGAMBOGA

$
0
0
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO, DODOMA

Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuweza kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga katika maeneo sahihi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Aweso wakati akijibu swali la Mhe. Zainabu Amiri kuhusu Mpango wa Serikali wa kuwapatia maji safi na salama wakulima hao wa mbogamboga.

Mhe. Aweso amesema kuwa Wizara ya Maji kwa kuzingatia umuhimu wa afya za wananchi inaendelea kutoa miongozo na ushauri kuhusu maji yanayofaa kwa matumizi ya binadamu na kwa shughuli za uchumi.

" Katika kuhakikisha wananchi wanalima mbogamboga katika maeneo sahihi, Serikali iliunda kikosi kazi kwa kushirikisha maafisa wa Baraza la Mazingira la Taifa(NEMC) ambapo kilitembelea baadhi ya mito ya Dar es salaam na kugundua uchafuzi mkubwa wa mazingira unaosababishwa na utiririshaji wa majitaka kutoka majumbani na kwenye viwanda ambapo maji hayo kuwa na kemikali zisizofaa kwa matumizi ya kilimo cha mbogamboga kwa mfano mto Msimbazi" amesema Mhe. Aweso.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema kuwa, Serikali inawataka wananchi kuacha kulima mbogamboga katika maeneo hayo yenye uchafuzi kwa kuwa maji hayo yana athari kwa afya.Vilevile amesema kuwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) inaendelea kupima maji ya mito hiyo na kutoa taarifa za hali ya maji hayo.

Mbali na hayo, Mhe. Aweso ameshauri Halmashauri za Manispaa katika Jiji la Dar es Salaam kutunga na kusimamia Sheria ndogo kwa ajili ya kudhibiti uchafuzi wa maji ya mito hiyo.


 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Aweso

MHASIBU TAKUKURU, GODFFREY GUGAI APANDISHWA KIZIMBANI NA KUSOMEWA MASHTAKA 43

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA, BALOZI WA OMAN PAMOJA NA BALOZI WA CHINI NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa mazungumzo,Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke ambaye alimtembelea Makamu wa Rais kwa mazungumzo ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Oman nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe.Wang Ke ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha,Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Mhe.Wang Ke mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA NOVEMBA 16, 2017

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza mkutano wa tisa wa kikao cha nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya wabunge wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu  leo mjini Dodoma unapofanyika mkutano wa tisa wa kikao cha nane.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa mkutano wa tisa wa  kikao cha nane  cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dk.Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Mbunge wa Karagwe(CCM) Mhe.Innocent Bashungwa wakati wa mkutano wa tisa wa kikao cha nane  cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Picha zote na Daudi Manongi - MAELEZO,DODOMA.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MALIASILI KAMILISHENI ZOEZI LA UWEKEJI ALAMA MAENEO YA HIFADHI-MAJALIWA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kukamilisha zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika maeneo yote ya hifadhi ifikapo Desemba 30, 2017.

Agizo hilo limekuja baada ya kuwepo kwa migogoro ya mipaka kati ya wananchi na hifadhi ambapo baadhi ya wananchi wanaendesha shughuli za kijamii ndani ya hifadhi.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Novemba 16, 2017) wakati akijibu swali la mbunge wa Ulyankulu, Bw. John Kadutu wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma.

Bw. Kadutu alitaka kujua hatua zilizofikiwa na Serikali katika uwekaji wa alama za mipaka katika maeneo mbalimbali ya hifadhi ili kuwaondolea wananchi usumbufu.

“Wizara ifanye mapitio ya maeneo yote ya hifadhi ambayo bado hayajawekewa alama za mipaka na kukamilisha zoezi hilo ifikapo tarehe 30, Desemba, 2017.”

Pia Waziri Mkuu amewataka wananchi wote wanaoishi maeneo ya karibu na hifadhi hizo au hata ndani watoe ushirikiano kwa wataalamu ili kuweza kukamilisha zoezi hilo kwa wakati.

Waziri Mkuu amesema wananchi wanaoshi katika maeneo yaliyoko ndani ya hifhadhi wawaache wataalamu wakamilishe zoezi hilo na baada ya kukamisha Serikali itafanya mapitio na kisha kutoa maamuzi kwa manufaa ya Taifa.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema sheria namba moja ya Ajira za Wageni ya mwaka 2015 inaruhusu utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni kwa muda wa miaka miwili.  “Hata hivyo vinaweza kuongezwa kulingana na mahitaji hadi kufikia vipindi viwili.”

Hata hivyo, Serikali imewapa masharti wageni wanaoomba vibali vya kufanya kazi nchini kuandaa mpango wa kuwarithisha ujuzi Watanzania ili kuchukua nafasi za wageni hao mara baada ya muda wa vibali vyao kumalizika.

Pia Serikali inayataka makampuni yote uwekezaji kutoa kipaumbele cha ajira kwa Watanzania kwa kuwa kwa sasa tunao Wataalamu wa kutosha katika fani mbalimbal

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kuteuliwa Bw. Abdallah Bulembo aliyetaka kufahamu wageni wanaokuja kufanya kazi nchini wanaruhusiwa kufanya kazi kwa muda gani.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, NOVEMBA 16, 2017.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA LEO BUNGE MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma  Novemba 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Aldersgate ya mjini Babati ambao walitembelea Bunge Mjini Dodoma kwa lengo la kujifunza Novemba 16, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na walimu  na  wananfunzi wa shule ya Sekondari ya Ibuaga wilayani Kongwa ambao walitembelea Bunge kwa mwaliko wa Mbunge wao Spika wa Bunge, Job Ndugai Novemba 16, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM wa mkoa wa Dodoma kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Novemba 16, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wananchuo wa Chuo Kikuu cha Saint John cha mjini Dodoma kwenye viwanja vya Bunge Mini Dodoma Novemba 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO AWASAA WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI ABIRIA KUACHANA NA MTAZAMO WA MGOMO

$
0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditie amewataka wamiliki  na wadau wa vyombo vya usafirishaji wa abiria hapa nchini kuacha azma yao ya kufanya mgomo ifikapo Desemba Mosi, mwaka huu na badala yake wampe nafasi ili aweze kushughulikia malalamiko yao.

Naibu Waziri huyo alitoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam jana wakati alipokuwa akizungumza katika mkutano wa dharula wa wanachama wa Taboa na vyama vingine kama Uwamadar, Darcoboa, Tati na Tatoa ambao ulikuwa ukijadili kanuni za usafirishaji hapa nchini zilizotolewa na SUMATRA.

Nditie aliwataka wamiliki hao kumpa muda ili aweze kuzipitia kanuni hizo na kuona kama zinamapungufu ili aweze kuwalisiliana na Sumatra waangalie namna ya kurekebisha kwa kuwa kanuni zinaweza kurekebishwa.

Aidha alikiri kuwepo kwa penati nyingi kwenye kanuni hizo na kwamba kutokana na kanuni hizo hakuna mmiliki ambaye anaweza kubaki salama iwapo kanuni hizo zitaanza kutekelezwa.

“Nimepitia tu  kwa haraka kanuni hizo na nimegundua kuna panati 57ambazo hata iweje mmiliki yoyote hapa nchini hawezi kuzikwepa ni lazima tu atakumbana nazo endapo kanuni hizo zitaanza kutekelezwa,”amesema.

Amesema serikali haina lengo la kuwakomoa wadau wa usafirishaji kwa kuwa wao wamekuwa wakiingiza fedha nyingi sana na hivyo ipo haja ya kushirikiana nao ili nao waweze kupata faida.

Wakizungumza katika mkutano huo, wamiliki hao walisema kuwa iwapo sheria hiyo itaanza kutumika usafirishaji utakuwa mgumu na kwamba wamiliki hao hawana mgogoro na serikali lakini kutokana na suala hilo hawataweza kutoa huduma hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya usafirishaji ya Ibraline, Ibrahimu Shayo amesema kuwa wamiliki wote walikubaliana kwamba sheria na kanuni hizo zikianza kutumika basi watapaki magari yao majumbani na ni bora magari hayo wayafugie kuku.

Amesema kuwa asilimia 95 ya biashara ya usafirishaji hawatoi fedha mifukoni mwao, isipokuwa wamekuwa wakipata mikopo toka kwenye taasisi za fedha ambazo zimekuwa zikitoza riba kubwa na huku kanuni pia zikiwabana.

Nae,  Mjumbe wa Taboa kutoka mkoni Mwanza, Anuary Said alisema kuwa SUMATRA ni wasaliti sana na wamekuwa wakiwadhalau sana wadau wa usafirishaji kwa muda mrefu sana na haoni kama kuna umuhimu wa kuwepo kwa chombo  hicho.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Atashasta Nditie akizungumza na vyama vya wamiliki wa vyombo vya abiria  jijini Dar es Salaam.

WATENDAJI TOENI USHIRIKIANO WA KUWEZESHA KUKAMILIKA KWA MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM (DMDP) – WAZIRI JAFFO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo amewataka watendaji wa Manispaa ya Temeke kutoa ushirikiano ili kuwezesha kukamilika kwa mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) na watendaji watakaoshindwa kutoa ushirikiano huo watashughulikiwa.
Akizungumza leo wakati uzinduzi wa jengo la ofisi na Maabara za mradi  wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) lililojengwa katika Manispaa ya Temeke, Jaffo amesema mradi huo utawezesha manispaa ya Temeke kuwa ya sura mpya na kuwa mfano kwa jiji la Dar es Salaam.
Amesema mradi utawezesha kujengwa kwa barabara na mifereji na hivyo kupunguza msongamano wa magari.
Amesema mradi huo ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) utatekelezwa katika jiji zima la Dar es Salaam katika kupanga mji kuwa na makazi bora yenye huduma zinazoendana na makazi hayo.
“Temeke mmekuwa na  bahati ya kuwa ya kwanza kutekeleza mradi huu, shirikianeni kuifanya Temeke kuwa ya kisasa kwa kuondoa Temeke  iliyokuwepo zamani isiyokuwa na miundombinu rafiki kwa makazi ya wananchi,” amesema.
Mratibu wa mradi huo katika manispaa ya Temeke, Edward Simon amesema Shilingi bilioni 265 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi barabara na mifereji. Amesema jumla ya kilometa 91 za barabara za ndani zitajengwa kwenye manispaa hiyo.
Amesema mradi huo ukikamilika utawezesha barabara kupitika na kupunguza mafuriko kutokana na kutengenezwa mifereji.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akizungumza na katika uzinduzi wa jengo la ofisi na Maabara za mradi  wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akikabidhiwa  mfano ufunguo wa jengo la mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP)  kutoka kwa Mratibu wa Miradi, Devis Shemangali unaofadhiliwa  na Banki ya Dunia  leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Vanessa Mdee Releases Bounce!

$
0
0
With Money Mondays in the pipeline – there’s no stopping VeeMoney. With 3 Pan-African features released within the past fortnight (IMARA – Frederic Gassita (Gabon), Vitamin U – Roberto (Zambia) and Cassper Nyovest’s Baby Girl (South Africa) which features VeeMoney in the visual as a special appearance). Vanessa continues to reign over the continent with her slew of chart toppers and now this brand new Boy is Mine inspired collabo with two of the baddest vocalists out of Tanzania – Maua Sama and TommyFlava. Bounce samples Wayne Wonder’s Bounce Along and will have you doing exactly that as we gear up for her December album release. 

 Bounce is produced at BKej Studios (Tanzania) by Breezy, with sultry visuals shot by Justin Campos to accompany this immediate smash. Enjoy Bounce!

Kubeza dhana ya Viwanda ni Mtazamo Finyu na Uliopitwa na Wakati-Waziri Jenista Mhagama

Mhariri Mtendaji wa TSN Afurahishwa na Jarida la Nchi Yetu

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi nakala ya Jarida la Nchi Yetu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz alipotembelea Ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Jarida hilo nit oleo maalum la mwezi Novemba ambalo limeangazia miaka miwili ya uongozi wa Rais Dkt, John Pombe Magufuli.Picha na: MAELEZO

taarifa kwa umma

BALOZI WA CHINA AAHIDI KUCHIMBA KISIMA DODOMA

$
0
0

Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Makao Makuu

Balozi wa China hapa nchini Mhe.Wang Ke ameahidi Serikali yake itatoa msaada wa kugharamia mradi wa uchimbaji kisima kimoja cha maji na miundombinu ya usambazaji wa huduma hiyo kwenye moja ya kijiji cha Mkoa wa Dodoma.

Balozi Wang Ke alimuahidi msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge leo alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma, ambapo alimtaka Dkt. Mahenge kutumia timu ya Watalaalamu wa Maji wa Mkoa kufanya usanifu na makadirio ya bajeti ya mradi huo na kuiwasilisha Ofisi za Ubalozi wa China kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi.Aidha, Balozi Wang Ke ameelezea kuwa Uongozi wa Mkoa utaainisha ni kijiji kipi ambacho kitapewa fursa ya kupatiwa mradi huo.

Kwa upande wake, Dk. Mahenge ameishukuru Serikali ya China kupitia kwa Balozi Wang Ke kwa ajili ya mradi huo na amebainisha kuwa mradi huo pia unaweza ukatumika kuwasaidia vijana kwenye kijiji kitachopewa mradi kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Dkt. Mahenge amemwelezea Balozi Wang Ke kuwa amefanya ziara kwenye Wilaya za Mkoa wa Dodoma na amejionea namna ambavyo wananchi wanahitaji kubwa la maji na hivyo mradi huo umekuja wakati muafaka kabisa.

Katika mazungumzo ya Viongozi hao, mradi huo utahusisha Utafiti wa uwezekano wa kupata maji chini ya Ardhi, Uchimbaji wa Kisima kirefu, ununuzi wa mashine ya kuvuta na kusukumia maji, ujenzi wa Miundombinu ya kusambazia maji, Tenki la kuhifadhia maji na vituo vya wananchi kuchotea maji.
Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge ambapo aliahidi kutoa msaada wa kuchimba kisima kimoja cha maji Mkoani Dodoma.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na Balozi wa China Mheshimiwa Wang Ke (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika mazungumzo yao, kushoto ni Katibu Tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge na kulia ni Afisa kutoka Ubalozi wa China.

Wananchi Watakiwa Kutumia Mvua Kwa Shughuli za Uzalishaji

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Serikali imewataka Viongozi na wananchi wote kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha nchini kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu leo Mjini Dodoma, wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu tahadhari kwa umma kuhusu mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Mhe. Ikupa amesema kuwa, mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania ilitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba mpaka Desemba 2017 kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua.

Aidha, ameongeza kuwa kutokana na taarifa hiyo serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ilielekeza Wizara na mamlaka za Serikali za Mitaa kuchukua hatua stahiki kwa kutumia mvua hizo kwa shughuli za uzalishaji mali pamoja na na kuchukua hatua za tahadhari kwa madhara yanayoweza kujitokeza.

“Kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya kijiji na mitaa zinatakiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 na kanuni za usimamizi wa maafa za mwaka 2017 ya kuchukua hatua za kuzuia, kupunguza madhara na kujiandaa kukabiliana na maafa endapo yatatokea,” amesema Mhe. Ikupa.


KAMATI YA BUNGE YA MAADILI YAMHOJI MHE. KUBENEA MJINI DODOMA

$
0
0
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.

Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. 

Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika leo baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe. 

Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi.

“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.
Mwenyekiti Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe. Almasi Athuman Maige (Mb), akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichokutana kumhoji Mhe. Saed Kubenea (Mb) kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea alifika mbele ya Kamati hiyo leo ikiwa ni mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano yake yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea (Mb) akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea amefika mbele ya Kamati hiyo leo kwa mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano hayo yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.PICHA NA BUNGE

Wakulima 206 Wapata Mafunzo Ya kilimo Cha Chai kutoka NOSC

$
0
0

KUTOKANA na ushirikishwaji wa wakulima wadogo katika zao la chai kupitia Kampuni ya Kuhudumia Wakulima Wadogo Njombe (NOSC), viongozi wa Mkoa wa Njombe wanajivunia mafanikio yaliyopatikana katika kilimo cha chai kilichosaidia kuinua kipato cha wakulima wadogo na kuongeza fedha za kigeni.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Njombe, Bwana Lameck Noah kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Bw. Christopher Ole Sendeka mkoani hapa jana katika mahafali ya mwaka mmoja kuhusiana na mafunzo ya kilimo cha chai kilichohusisha wakulima zaidi ya 206.

“Katika mkoa wetu tulijiwekea utaratibu kuwa kila mkulima alime mazao ya aina mbili ya chakula na biashara, kwa upande wa chai tatizo lilikuwa ni aina ya miche, ilikua inachukua muda mrefu kukua lakini tunaishukuru NOSC imetuletea mice inayokua kwa miezi 12 mkulima anaanza kupata majani mabichi ya chai,” alisema Bw. Noah.

Alibainisha kuwa elimu hiyo ina maana kubwa kwa mkoa wake kwa sababu itawasaidia kulima kisasa na kuwaongezea kipato wananchi wa mkoa huo, lakini pia viwanda vitapata malighafi hiyo muhimu kwa ajili ya soko la ndani na nje.

“Tunafahamu chai inapendwa na mataifa ya magharibi, zao hili lina fedha nyingi za kigeni. Soko la chai lipo na tunawahakikishia wakulima serikali inahangaika kupata mnada wa chai katika ukanda huu badala ya kufanyika Mombasa nchini Kenya.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah(wapili kushoto) akikabidhi cheti bwana Thiemo Msewa(kulia) katika hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima wa chai(farmer field school) mkoani humo yaliyoratibiwa na Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakulima katika kilimo cha chai na mazao mengine. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NOSC, Bwana Filbert Kavia. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Ruth Msafiri 
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah akizungumza jambo wakati wa hafla hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima wa chai(farmer field school) mkoani humo yaliyoratibiwa na Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wakulima katika kilimo cha chai na mazao mengine. 
Operation Director wa Wood foundation Tanzania Bwana Mathew Ng’enda(watatu kushoto) akishangilia mara baada ya wakulima kuwasilisha mada mbalimbali juu ya elimu ya kilimo cha chai (farmer field school) waliyoipata kutoka Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo Njombe(NOSC). Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Njombe Bwana Lameck Noah. na watatu kulia ni Mkurugenzi mkuu wa NOSC Bwana Filbert Kavia. 

GAVANA WA BENKI KUU ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA

$
0
0
Na: Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika tarehe 20 Novemba, 2017 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya amesema maadhimisho hayo yanayoratibiwa na ofisi hiyo kwa niaba ya Serikali, yana lengo la kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa Tasnia ya Takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii Barani Afrika.

Ruyobya amesema kuwa kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora”

“Kaulimbiu hii inalenga kuweka mkazo katika matumizi ya Takwimu za Uchumi kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wote nchini na Afrika kwa ujumla”, amebainisha Ruyobya.

Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw, Irenius Ruyobya akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 20 Novemba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtakwimu Mwandamizi wa ofisi hiyo Bw. Philemon Mwenda.
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw, Irenius Ruyobya alipokuwa akizungumza kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 2o Novemba jijini Dar es Salaam.
Picha na MAELEZO

WABUNGE VINARA WA JINSIA WAPATIWA SEMINA NA WAWEZESHAJI KUTOKA TGNP MTANDAO

$
0
0
Vinara wa jinsia katika mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019 na Muongozo wa Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia semina iliyokuwa inahusu mpango kazi wa kurasimisha masuala ya jinsia katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ilifanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma, semina iliyokuwa inawezeshwa na wawezeshaji kutoka TGNP Mtandao
Mwenzeshaji kutoka TGNP Mtandao Ndg. Geofrey Chambua akizungumza na vinara wa jinsia katika mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019 na Muongozo wa Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika semina iliyokuwa inahusu mpango kazi wa kurasimisha masuala ya jinsia katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ilifanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania( TWPG), Mhe Magreth Sitta (kushoto) akizungumza wakati wa semina kwa vinara wa jinsia katika mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019 na Muongozo wa Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa inahusu mpango kazi wa kurasimisha masuala ya jinsia katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ilifanyika leo katika hoteli ya Morena Mjini Dodoma, semina iliyokuwa inawezeshwa na wawezeshaji kutoka TGNP Mtandao

PICHA NA OFISI YA BUNGE

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 16.11.2017

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images