Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO NOVEMBA 16,2017


NAIBU MEYA MANISPAA YA ILALA OMARY KUMBILAMOTO AONGOZA KAMATI YA FEDHA NA UTAWAL KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kamati ya Fedha na Utawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ,imefanikiwa kutekeleza asilimia 98 ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokusudiwa kutekeleza katika awamu ya kwanza ya mwaka fedha wa 2017/2018 katika kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba kutumia Sh bilioni 1.2 kati ya Sh bilioni 2.5 zilizotakiwa kutumika.

Hayo yamesemwa leo na Mchumi wa manispaa hiyo Ando Mwankuga baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kujionea kile walichopanga, kuwa kimetekelezwa kwa ufanisi, na baadhi ya miradi imekamilika na mingine ikiendelea kutekelezwa kikamilifu.

Amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo, kuna changamoto mbalimbali ambapo miradi mingi inaanzishwa lakini haikamiliki kwa wakati,miradi hiyo hufanyika kutokana na vyanzo mbali mbali vya fedha za ndani na ruzuku ya serikali na kukuta mradi ni mkubwa kuliko kiwango cha fedha,kilichopo,pia amewaomba madiwani kupitisha bajeti kulingana na miradi ili kutatua changamoto ya miradi kutofanikiwa. 
Mchumi wa manispaa ya ilala (katikati) Ando Mwankunga akizungumza walipofanya ziara katika ujenzi ofisi ya kata Mvuleni ambapo inaendelea kujengwa.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Enock Segesela,(kulia) akielezea jambo.
Hii ndiyo ofisi ya kata ya Mvuleni inayoendelea kujengwa, ambapo ina chumba cha Mwenyekiti,ofisi ya chumba cha mtendaji kata,ukumbi wa mikutano,choo,pamoja na stoo ya kuifadhi vitu.
Naibu Meya katika Manispaa ya ilala (kushoto) Omary Kumbilamoto pamoja na diwani wa kata ya segerea Edwin Mwakatobe wakikagua Kisima cha maji katika kata ya segerea.

MAHAFALI DUCE YAFANA, PROF MUKANDALA AWAAGA RASMI WANA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewatunukia wahitimu 1443 wa ngazi mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es salaam (DUCE) kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Katika mahafali hayo Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete aliwatunukia wahitimu hao sambamba na kutoa zawadi kwa wanafunzi nane waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.

Rais wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam, Prof William Anangiyse amesema kuwa jumla ya wahitimu 1371 wametunukiwa digrii za awali katika fani mbalimbali na Wahitimu 72 ni wa ngazi ya stashahada ya uzamili katika elimu  (PGDE) na kutimiza idadi ya 1443.

Prof Anangisye amesema kuwa jumla ya 928 ni wanaume na 515 ni wanawake huku wahitimu 1015 wakitunukiwa digrii ya elimu ya jamii na ualimu (B.A.Ed), , 233 ni wahitimu wa Sayansi na Ualimu ( B.Sc.Ed), wahitimu 72 ni Elimu katika sayansi (B.Ed.Science) na Elimu katika elimu ya Jamii ( B.Ed.Arts) ni wahitimu 51.
Mbali na hilo, Mwenyekiti wa bodi ya Usimamizi ya Chuo Kikuu Kishirikishi  Cha Elimu Dar es Saalam, Prof. Rwekaza Mukandala kwenye mahafali ya 10 ya chuo hicho amewaaga rasmi wanajumuiya wa Chuo Kikuu Kishirikishi  baada ya kumaliza muda wake wa mwaka mmoja alioongezewa na Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwenhe mahafali ya mwaka jana.

Mkuu wa Chuo Dkt Kikwete aliweza kutoa zawadi kwa wahitimu nane waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho pamoja na Emanuel Safari Dadi aliyefanya vizuri kwa ujumla na kumpongeza kwa juhudi kubwa alizozifanya katika kipindi chake cha masomo.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepiga picha na mhitimu Emanuel Safari Dadi aliyefanya vizuri katika mitihani yake yote na kupata GPA 5.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu  Dar es Salaam Peter Ngumbulu (Kulia), Rais wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam Prof William Anangyse, Mlau wa Chuo Kikuu Kishirikishi Cha Elimu Dar es Salaam Prof. Martha Qorro na wajumbe wengine katika mahafali ya 10 yaliyofanyika jana Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa zawadi kwa wahitimu nane waliofanya vizuri kwenye mitihani yao. Chini akiwa amepiga nao picha ya pamoja.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunukia wahitimu wa ngazi mbalimbali katika mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam yaliyofanyika jana Jijinj Dar es Salaam.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HIFADHI YA MAMLAKA YA NGORONGORO

$
0
0

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Tanga wakiingia kwenye hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro tayari kuanza ziara ya siku kumi ya mafunzo 
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Ngorongoro,Walter Mairo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kabla ya kuanza ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi wakati wa ziara yao ya siku kumi.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo,Samweli Nsyuka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la mchanga ambalo limekuwa likihama mara kwa mara 
Waandishi wa habari,Mbaruku Yusuph wa gazeti la Tanzania Daima na Mbonea Hermani wa Star TV wakiangalia eneo la ambalo limegunduliwa fuvu la binadamu wa kwanza wakati wa ziara hiyo.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo,Samweli Nsyuka kulia akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Jumba hilo la Makumbusho .Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

DEATH ANNOUNCEMENT

MDAHALO WA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE WAFANYIKA CHUO KIKUU CHA MZUMBE

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika Mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyika Novemba 15 2017 chuoni hapo mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyoika katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mdahalo wa Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UFANYE NINI UKIGUNDUA UMENUNUA ARDHI ILIYOWEKWA REHANI BILA KUJUA ?.

$
0
0

Na Bashir Yakub.

Umenunua kiwanja au nyumba. Aliyekuuzia amekuhahakikishia kuwa kiwanja/nyumba hiyo iko salama na haina mgogoro wowote. Mbali na mgogoro pia amekuhakikishia kuwa kiwanja/nyumba hiyo hajaiweka rehani popote ili kuchukua mkopo. 

Amekuhakikishia kuwa mpaka wakati unanunua kiwanja/nyumba hiyo, ni kuwa iko salama na haijashikiliwa na benki au taasisi yoyote ya fedha kwa ajili ya mkopo.

Au pengine hukuuliza kabisa kama kuna deni lolote, umejikuta tu umenunua bila kuuliza swali kama hilo. Baadae sasa ndio unagundua kuwa kiwanja/nyumba uliyonunua kuna taasisi moja ya fedha ambapo aliyekuuuzia alichukua mkopo na kuiweka dhamana/rehani na bado hajamalizia mkopo huo. 

Taasisi hiyo inakuonesha nyaraka halali za kushikilia kiwanja/nyumba hiyo kama dhamana muda mrefu hata kabla wewe hujanunua. Na kwa bahati mbaya aliyekuuzia hujui tena alipo au bahati nzuri unajua alipo.

Lakini hata ukijua alipo, tayari umeishanunua na hela ulishampa na kila kitu kilikwishakamilika. Nini kinakusaidia kukutoa katika hali hii ambayo sasa unaelekea kuingia katika mgogoro mkubwa wenye sura ya hasara. 

Sheria namba 4 ya 199, Sheria ya ardhi itatupatia majibu ya jambo hili.

1.UNUNUZI WA AINA HIYO UNAVYOTAMBULIKA KISHERIA.

Ununuzi wa aina hiyo unatambulika kama aina ya ununuzi ambao unaingilia haki ya mtoa mkopo. Kifungu cha 69(1) cha sheria hiyo kinauita ununuzi huo kama ununuzi unaolenga kupora/kuharibu(defeat) haki ya mtoa mkopo. 
Mtoa mkopo hapa ni benki au taasisi nyingine ya fedha iliyotoa mkopo. 
Kwahiyo kujikuta umenunua eneo lenye mazingira ya namna hiyo hadhi yake ni kama ilivyoelezwa hapa juu.


TATU MZUKA YAMPONGEZA BI. BUJINGINYA KUTOKA NGARA KWA KUSHINDA MILIONI 50.

$
0
0
Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera ameibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika jumapili.

Bi Bujinginya, mama wa watoto wawili ambaye anaungana na washindi milioni 130 wa Tatumzuka amesafirishwa kwa ndege kutoka Ngara kuja Dar es Salaam ili kuchukua pesa yake ya ushindi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Mikocheni.

Baada ya kushinda mara chache katika droo ya kila saa, alipata msukumo wa kuendelea kucheza bila kukata tamaa. "Baada ya kuishi kwa kutafuta pesa ya mlo kila mwezi na miezi mingine bila pesa, Kiukweli sikujua itakavyokuwa ikifika Januari. Nimefurahi sana kwamba sasa naweza kutembea kwa kujiamini tena baada ya ushindi huu’ alikiri Bi Bujinginya.

Pia katika tukio la kukabidhi zawadi kwa mshindi alikuwepo Bwana Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.Dhamira ya Tatu Mzuka ya kubadilisha maisha ya watu haijabadilika ambapo zimebaki siku chache ili ichezeshwe droo kubwa ya Supa Mzuka jackpot ya milioni 150 jumapili ijayo. Tarehe 19 Novemba saa 3:30 usiku Mtanzania mmoja ataondoka na kitita cha milioni 150.

"Kila mtu ambaye umecheza tangu Tatumzuka izinduliwe na kutumia kuanzia shilingi 500 tu kupitia MPESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY, umeingia katika droo hii ambapo unaweza kujishindia milioni 150," alielezea mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba.

Bi Mutahaba aliwahimiza watanzania kuendelea kucheza, akisisitiza kwamba bado washiriki hawajachelewa kujiwekea nafasi ya ushindi huo wa kihistoria.
Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi Bi.
Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera alieibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika mwishoni mwa wiki
Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi,Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.

BCX YATOA ELIMU YA MATUMIZI YA KADI YAKE YA UHURU PAY KWA ABIRIA WA KIVUKONI NA TEGETA-NYUKI

$
0
0

Wakala wa Kampuni ya BCX, Neema Urassa (katikati) akitoa Elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam eneo la Feri walipotembelea banda lao lililokuwa likitoa huduma za mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo ya nauli uliozinduliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya usafiri wa Daladala.
Wakala wa Kampuni ya Business Connexion (BCX), akiwakabishi vipeperushi wakazi wa Tegeta Nyuki, ambavyo vinatoa maelezo kuhusu huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na BCX hivi karibuni jijini Dar es salaam.

Msimamizi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo ya nauli katika usafiri wa Daladala kwa kutumia Kadi au Stika unaotolewa na Kampuni ya BCX, Andrew Wayayu (watatu kushoto) akizungumza na Dereva na kondakta walipokuwa wakitoa elimu kuhusu mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo ya nauli katika usafiri wa Daladala.

OPEC YAIPATIA TASAF DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 12 KUTEKELEZA MRADI WA KUPUNGUZA UMASKINI AWAMU YA TATU

$
0
0

NA ESTOM SANGA-TASAF.

Umoja wa nchi zinazozalisha Mafuta kwa wingi OPEC- umeupatia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kiasi cha Dola za kimarekani milioni 12 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kupunguza Umasikini Awamu ya Tatu katika mikoa ya Njombe na Arusha.

Akifungua kikao kazi cha mradi wa kupunguza Umasikini awamu ya tatu (TPRP III ) kwa wasimamizi wa halmashauri za wilaya za mikoa ya Njombe na Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga, amesema kiasi hicho cha fedha kimetolewa ili kuendeleza miradi ya wananchi kwa jamii zenye upungufu wa huduma za jamii ,uhaba wa kipato na kujiongezea kipato.

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na mkurugenzi wa miradi wa TASAF,Bwana Amadeus Kamagenge, bwana Mwamanga amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa fedha hizo zinazowanufaisha walengwa na kusaidia kufanikisha mkakati wa serikali wa kupambana na umasikini nchini.

Aidha Bwana Mwamanga amesema takribani miradi 407 iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji baada ya kupatiwa fedha na kuwaagiza watendaji hao wa halmashauri kuongeza kasi ya kuibua miradi mingine kwenye maeneo yao ili kusaidia jitihada za serikali za kusogeza huduma za kijamii hususani elimu na afya karibu zaidi na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

Bwana Mwamanga pia ametoa wito maalumu kwa viongozi wa halmashauri za wilaya katika mikoa ya Njombe na Arusha kuendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao hususani ile inayohitaji mchango wa jamii husika ili miradi hiyo iweze kuwa endelevu na yenye manufaa kwa wananchi.

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ambao pamoja na mambo mengine unajenga miundombinu hususani ile inayolenga moja kwa moja kaya za walengwa wa Mpango kwa kuongeza kasi ya kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi. 
 Mkurugenzi wa miradi wa TASAF ,Bw. Amadeus Kamagenge (aliyesimama) akifungua kikao kazi cha Mradi wa kupunguza Umasikini awamu ya Tatu,katika ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam.,Kulia kwake ni Mkurugenzi wa fedha, Bi. Chiku Thabiti,kushoto kwake ni meneja wa miradi ya miundombinu wa TASAF Mhandisi Elisifa Kinasha. 
 Meneja wa miradi ya miundombinu wa TASAF,Mhandisi  Elisifa Kinasha (aliyesimama) akitoa maelezo ya kikao kazi cha Mradi wa kupunguza umasikini awamu ya tatu kwa wasimamizi wa halmashauri za wilaya za mikoa ya Arusha na Njombe yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam.

 Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha mradi wa kupunguza  umasikini awamu ya tatu (TPRP) kwa wasimamizi wa halmashauri za wilaya za mikoa ya Arusha na Njombe.Kikao kazi hicho kinafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam.

 Washiriki wa kikao kazi cha mradi wa kupunguza  umasikini awamu ya tatu (TPRP) kwa wasimamizi wa halmashauri za wilaya za mikoa ya Arusha na Njombe wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi hicho  kinachofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za makao makuu ya TASAF jijini Dar es salaam.

RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAHAFALI YA 10 YA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU (DUCE) CHA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, (pichani juu), ameongoza mahafali ya kumi (10), ya Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE)cha Chuo kikuu Dar es salaam kwenye viwanja vya chuo hicho, Chang’ombe jijini Dar es Salaam jana Novemba 15, 2017.

Katika mahafali hayo zaidi ya wanachuo 1,443 waliochukua mafunzo ya Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED), Shahada ya Elimu ya Sayansi na Elimu, (Bsc) na Shahada ya Elimu (BED), pamoja na wahitimu waliojiendeleza (Post graduate), 

walitunukiwa shahada ya kwanza, ambapo mwanachuo Dadi Omary Safari, alipewa tuzo ya kuwa mwanachuo bora zaidi kitaaluma.
Dkt. Kikwete akitangaza kuwatunuku shahada baadhi ya wanachuo hao. 
Baadhi ya wanachuo wakisubiri kutunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Dkt. Kikwete, akiteta jambo na Profesa Mukandala.
Dkt. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wahitimu, Amisa Hassan, na baba mdogo wa muhitimu huyo, Khalfan Said.


RC WA TANGA MARTINE SHIGELLA AZINDUA RASMI TAWI LA BENKI YA NMB MKATA WILAYANI HANDENI

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh.Martine Shigella leo amezindua rasmi tawi la NMB benki lililopo Kata ya Mkata Wilayani Handeni na kuwataka wakazi wa maeneo ya jirani kuacha kuhifadhi fedha nyumbani. 

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ufunguzi wa tawi hilo la kibenki ni fursa kubwa kwa wakazi wa Mkata na maeneo ya jirani kwani huduma za kifedha zimesogezwa karibu na ni chachu ya ukuaji wa maendeleo na uchumi wa Mkata.

Aliongeza kuwa Mkata ni eneo lenye mzunguko mkubwa wa kifedha kutokana na kuwa na wafanyabiashara mbalimbali, wakulima, wafugaji,wafanyabiashara wa matunda na biashara nyingine hivyo wanategemea kwa kiasi kikubwa huduma ya benki katika utunzaji wa fedha na usalama wao.

Mh. Shigella alisema kuwa NMB Benki imesaidia sana wananchi kwa kutoa mikopo na misaaada mingine ya kijamii hivyo ni vyema kuitumia benki hiyo kwani kwa kufanya biashara na NMB ni kufanya biashara na serikali kwa sababu kwa upande mwingine NMB ni Serikali ambapo fedha zinazowekwa ndizo zinazorudi kwenye jamii kwa mtindo wa mishahara, ujenzi wa miundo mbinu na huduma nyingine za kijamii.

”wananchi muweke utaratibu wa kuhifadhi fedha zenu kwenye benki badala ya kuzikumbatia ndani hali inayopelekea kuhatarisha usalma wa maisha yenu, NMB imefungua tawi kuwapunguzia kufuata huduma za benki mbali, tumieni fursa hii kupata mikopo ili kukuza uchumi wenu na Taifa kwa ujumla” Alisema Mkuu wa Mkoa.

Aidha amewataka NMB Benki kujiandaa na fursa za miradi mikubwa ya Bomba la mafuta,Viwanda,Madini, Kilimo na Ufugaji iliyopo Wilayani Handeni na Mkoa wa Tanga ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi wote kwa kuongeza matawi mengi ili kuepusha wananachi kuzunguka na fedha mifukoni.
​Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martine Shigella kushoto na Mkurugenzi wa NMB Benki Bi. Ineke Bismeka wakifungua kibao cha ufunguzi wa Tawi hilo​.
Mkuu wa Mkoa Tanga,Mh. Martin Shigela akizungumza na wananchi wa Mkata wakati wa ufunguzi wa Tawi la NMB
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akishukuru uongozi wa NMB kwa kuona umuhimu na kufungua Tawi eneo la Mkata.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA




TAARIFA YA AJALI YA NDEGE YA COASTAL AVIATION ILIYOTOKEA JANA

$
0
0

Baadhi ya Wananchi wakishuhudia ajali katika eneo la Empakai ilipotokea ajali ya ndege ya Coastal Aviation jana mkoani Arusha,ambapo katika ajali hiyo imethibitishwa kuwa watu 11 walipoteza maisha

TAKUKURU KILIMANJARO YAMSHIKILIA DAKTARI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA,MAWENZI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)mkoani Kilimanjaro,imemtia mbaroni Daktari wa Hospital ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi akituhumiwa kudai na kupokea rushwa ya shilingi 150,000.

Daktari huyo,Deogratias Godfrey Urio,alikamatwa jana katika mji mdogo wa Himo kwenye baa maarufu ya Mombasa High Way baada ya kuwekewa mtego na makachero wa takukuru mkoani Kilimanjaro.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Kilimanjaro(RBC),Holle Makungu imesema kuwa kukamatwa kwa daktari huyo kunatokana na malalamiko ya ndugu wa mgonjwa aliyekuwa akipigwa dana dana kupatiwa huduma ya upasuaji katika hospital hiyo.

Makungu ameeleza katika taarifa yake kuwa,mgonjwa huyo alikuwa akihitaji kufanyiwa upasuaji wa uvimbe katika kizazi chake tangu oktoba mwaka huu baada ya kufanyiwa vipimo kwenye hospital hiyo na kubainika kuwepo kwa uvimbe.

Lakini licha ya kubainika kuwepo na uvimbe huo,mgonjwa huyo hakuweza kupata tiba haraka baada ya kuelezwa na daktari huyo kuwa hawezi kufanyiwa upasuaji huo hadi hapo atakapotoa fedha hizo.


CHUO CHA KODI KUFANYA MAHAFALI YA KUMI JUMAMOSI NOVEMBA 18 2017

$
0
0
Chuo cha Kodi kitafanya mahafali ya Kumi Jumamosi tarehe 18 Novemba 2017 katika ukumbi wa chuo cha Kodi ambapo Mgeni rasmi katika mahafali hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Katika mahafali hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango atatunuku vyeti, stashahada na shahada kwa wahitimu 520 ambao wamefuzu masomo yao mwaka 2016/2017 na kusathili kutunukiwa vyeti.

Dkt. Mpango pia atatoa zawadi mbalimbali kwa wahitimu 12 waliofanya vizuri zaidi katika masomo ikiwa ni utaratibu ambao chuo kimejiwekea ili kutambua jitihada nzuri ambazo zimefanywa na wanafunzi hao pamoja na kuwashajihisha wanafunzi wanaoendelea na masomo kufanya vizuri zaidi katika masomo. 

Jumla ya anafunzi watakao tunukiwa vyeti, stashahada na shahada katika mahafali ya Kumi ya Chuo cha Kodi ni wahitimu 82 wa Cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki yaani the ‘East African Customs and Freight Forwarding Practising Certificate (EACFFPC). Wahitimu 39 wa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Basic Technician Certificate in Customs and Tax Management (CCTM). Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Diploma in Customs and Tax Management – (DCTM)’ wahitimu – 147, Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Bachelor of Customs and Tax Management (BCTM)’ Wahitimu – 134, ‘East African Community Postgraduate Certificate in Customs Administration (PGCCA)’ wahitimu 85 na Stashahada ya Uzamili katika Kodi yaani ‘Postgraduate Diploma in Taxation (PGDT) wahitimu - 33

Pamoja na kutunuku vyeti stashahada, na shahada kwa wahitimu, Mgeni Rasmi pia atatoa tuzo kwa wahadhiri wa Chuo cha Kodi waliofanya tafiti mbalimbali katika kipindi cha mwaka wa masomo wa 2016/2017 na kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na jarida la Chuo cha Kodi yaani ‘Journal of the Institute of Tax Administration’ (JITA).
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA,) Profesa Isaya Jairo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mahafali ya kumi ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika chuoni hapo Jumamosi Novemba 18 2017. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mkuu wa chuo, Oliver Njunwa. (Picha na Robert Okanda wa Okanda blogs) 
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Profesa Isaya Jairo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mahafali ya kumi ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika chuoni hapo Jumamosi Novemba 18 2017. Kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo (Utawala), Emmanuel Masalu na Afisa Uhusiano Mkuu wa chuo, Oliver Njunwa.

TAMKO LA MHE. UMMY MWALIMU KUHUSU WIKI YA KUZUIA USUGU WA VIMELEA DHIDI YA DAWA ZA ANTIBIOTIKI TAREHE 13- 19 NOVEMBA, 2017

BENKI YA KILIMO YATEMBELEA ENEO LA MRADI LA UMWAGILIAJI LA MWAMANYILI WILAYANI BUSEGA

$
0
0
Katika kutekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali ya kuchochea mapinduzi ya kilimo, Bodi ya wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetembelea eneo utakaofanyika mradi wa kilimo cha kisasa cha  umwagiliaji la Mwamanyili Wilayani Busega mkoani Simiyu.

Akizungumza lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa Benki ya Kilimo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwakwamua wakulima nchini kutoka katika kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha kibiashara ili waweze kujiongezea kipato.

Aliongeza kuwa Mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji ukianza kufanya kazi utatimiza malengo hayo ya Benki kwani utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuwainua wananchi Kiuchumi na kukabiliana na upungufu wa chakula wakulima watakaolima katika skimu hiyo.

“Benki ya Kilimo ipo tayari kuunga mkono miradi ya aina hii ambayo inalenga katika kuendeleza miundombinu muhimu ikiwemo ya uendelezaji wa skimu za umwagiliaji, usafirishaji, hifadhi ya mazao, usindikaji, pamoja na masoko ili kumuongezea mkulima kipato,” alisema.
 Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Eng. Tumbu akitoa maelekezo kwa ugeni kutoka TADB juu ya chanzo cha maji cha maji kitakachotumika katika mradi wa umwagiliaji wa Mwamanyili.
 Muonekano wa eneo likalotumika kwa ajili ya mradi wa kilimo umwagiliaji wa Mwamanyili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (aliyenyanyua mikono) akihimiza jambo wakati walipotembelea eneo likalotumika kwa ajili ya mradi wa kilimo umwagiliaji wa Mwamanyili.




VIONGOZI WA MRADI WA UTAFITI WA AFYA YA MALIASILI MAJINI, TRAHESA, WAKUTANA NA MAKAMU WA MKUU WA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO(SUA).

$
0
0
Makamu wa Mkuu wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, Prof Raphael Chibunda amewahakikishia viongozi wa mradi wa utafiti unaoshughulika na afya ya maliasili za majini, TRAHESA, kupewa kila aina ya msaada na SUA ili kufanikisha malengo yake kwa manufaa ya nchi husika na ulimwengu kwa jumla.

Hakikisho hilo limetolewa leo kufuatia viongozi wa mradi wa TRAHESA kumtembelea Makamu wa mkuu wa Chuo ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha rasmi baada ya uteuzi wa Prof. Chibunda mapema mwaka huu.

Amesema mradi huo wa utafiti wa afya ya maliasili za majini wakiwemo samaki utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi washiriki pamoja na dunia kwa ujumla kwa vile hakujakuwepo kwa tafiti za kutosha za maliasili za majini katika nchi za mashariki na kusini mwa Afrika.

Kiongozi Mtafiti wa mradi wa TRAHESA Prof. Robins Mdegela akiongozana na maafisa kutoka nchi mfadhili Norway na nchi washiriki katika mradi za Kenya, Uganda, Zambia na mwenyeji Tanzania wapo katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, kwa kikao cha kawaida cha mradi kufuatia SUA kuchaguliwa kama nchi mwenyeji wa mradi tangu ulipoanzishwa mwaka 2014.

Prof. Mdegela amesema katika mradi huo wa utafiti wanajumuisha pia wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu kutoka nchi zinazoshiriki katika mradi na wanadhaminiwa kufanya tafiti mbalimbali kuhusiana na afya za maliasili za majini wakiwemo samaki na mimea majini.

RC Wangabo azihimiza Halmashauri kuongeza mashine za mapato kuongeza ukusanyaji

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewasifu wananchi wa kata ya Mtowisa, Tarafa ya Mtowisa, Wilayani Sumbawanga kwa kuonyesha mshikamano katika ujenzi wa shule ya Sekondari Vuma pamoja na ujenzi unaonendelea wa kituo cha polisi kitakachohudumia tarafa ya mtowisa.

Tarafa hiyo yenye kata 4 ina shule moja ya kidato cha tano na sita jambo alilosifu Mh. Wangabo kuwa imetimiza ilani cha Chama Tawala kwa kuwa na Shule moja ya aina hiyo kwa kila tarafa.

Amesema kuwa ataendelea kusisitiza kauli ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa maendeleo hayana vyama, hivyo alisisitiza wananchi hao kutobaguana kwa itikadi zao bali wahimizane katika kutatua changamoto na kuleta maendeleo katika tarafa yao.

“Mmenivuti mliponieleza kwamba mnashirikiana katika nyanja mbalimbali, kuna majengo yale ya shule mnashirikiana na jengo hili la polisi mnashirikiana ili kuhakikisha kwamba changamoto mbalimbali zilizopo ndani yenu mnazitatua, hili limenifurahisha na ningependa muendelee nalo, na umeoja na mshikamano uliopo muudumishe bila ya kujali vyama vyenu.” Alisifu.

Ameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha mtowisa, kata ya mtowisa Wilayani Sumbawanga katika ziara yake ya siku mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga yenye lengo la kutembelea miradi mbalimbali na kujitambulisha kwa wananchi.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya mtowisa Mh. Edgar Malini alisema kuwa wananchi wa mtowisa hawana tabu wa kutoa ushirikiano ili kujiletea maendeleo wenyewe isipokuwa wamekuwa na kilio cha muda mrefu kuhusu umeme na maji.
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule akitoa maelezo ya kumtambulisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kwa wananchi wa kijiji cha Zimba kata ya Mtowisa, Wilayani Sumbawanga. wakati walipofika kwenye kijiji hicho kuona kiwanda cha kukamulia alizeti. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kutoka kulia) akiuliza swali kwa mhandisi wa maji wa Wilaya Patrick Ndimbo (wa kwanza kushoto) wakati walipotembelea mradi wa maji wa kutumia umeme wa jua mji mdogo Laela Wilayani Sumbawanga wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.8. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akishiriki kutumia ala ya kigoda kuchekecha juu ya mtungi na kuzalisha sauti inayowezesha kuleta mlio kwaajili ya kunogesha nyimbo, Ni ala ya asili inayotumiaka katika ngoma za kitamaduni za Kifipa muda mfupi kabla ya kufanya mkutano na wananchi wa mji mdogo wa Laela. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimsalimia mmoja wa kinamama wa kikundi cha ngoma Laela Odila Maufi wakati alipokuwa akiingia katika viwanja vya shule ya Msingi Laela kwaajili ya Mkutano wa hadhara kujitambulisha kwa wananchi na kuongea nao.  
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images