Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

RC MAHENGE: SITAKI KUSIKIA TATIZO LA UPUNGUFU WA CHAKULA WALA NJAA DODOMA

$
0
0

Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amesema Mkoa wa Dodoma hauna sababu zozote za kukumbwa na tatizo la upungufu wa Chakula wala Njaa kwa wananchi wake kwa kuwa unazo fursa za kutosha za kuzalisha mazao ya chakula yanayotosheleza mahitaji ya Mkoa.

Aidha amesema mkoa huo una fursa za kuzalisha mazao ya biashara yatakayoweza kuwainua kiuchumi wa mwananchi na Mkoa kwa ujumla.

Dk. Mahenge ameyasema hayo mwishoni mwa wiki akiwa katika ziara Wilayani Kongwa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Wilaya za Mkoa wa Dodoma.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu huyo amewataka Viongozi na wataalamu kuwasimamia wananchi kupanda mazao yanayotumia maji kidogo na kustawi kwa ufanisi Mkoani Dodoma kama Mtama, Uwele, Muhogo, Alizeti na Sasa zao la Korosho lililothibitika kustawi vizuri kwenye Ardhi ya Dodoma.

Aidha amewataka viongozi na Wataalamu wa kilimo wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanawaelimisha na kuwasimamia wananchi kutekeleza mkakati wa kilimo wa Mkoa unaolenga kuzalisha chakula cha kutosheleza mahitaji ya Mkoa, kwa kuachana na kilimo cha mazoea badala yake unasisitiza kilimo cha maarifa, na cha kisasa.

Amewatoa hofu wananchi kuwa zao la mtama mbali na kutumika kama chakula lakini lina soko la uhakika kwa ajili ya viwanda vya kutengeneza vinywaji hivyo hata kama mwananchi hataki kula mtama anaweza kuuza na akanunua chakula anachokitaka mwenyewe lengo likiwa kuwa na uhakika wa chakula.

Amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi kwa kuanzisha kampeni ya kuondoa njaa wilayani Kongwa (ONJAKO) na kuzitaka Wilaya nyingine kuiga mfano huo.

Awali, akielezea Kampeni ya ONJAKO Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwenye wilaya hiyo kila kaya, pamoja na mazao mengine ni lazima kulima heka mbili (2) za mtama kwa ajili ya chakula na endapo kaya yoyote itakayokaidi muhusika atalazimika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini (50) na endapo atashindwa basi adhabu ya kifungo cha miezi mitatu (3) itamkabili, Lengo likiwa kuhakikisha kila kaya inazalisha chakula cha kutosheleza mahitaji yake.

Kadhalika, Dk.Mahenge amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Rehema Madenge kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Dodoma kuhakikisha kila Wilaya ina ainisha mahitaji ya vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya elimu ili vifaa hivyo vinunuliwe kwa mfumo wa pamoja moja kwa moja kutoka Viwandani baada ya kupata idhini ya Wizara ya Kisekta lengo likiwa kupunguza gharama za vifaa.
 
Amepiga marufuku tabia za viongozi na Wakuu wa Idara kwenye Wilaya kukaa tu ofisini na kuwataka waweke ratiba ya mara kwa mara ya kutembelea shule kufanya ukaguzi ili kubaini changamoto halisi zinazo kabili hali ya utoaji elimu na kuzitafutia majibu ya kudumu, pia ametaka Wilaya ziwape walimu ushirikiano unaohitajika ili waweze kutekeleza jukumu la kuwafundisha watoto kwa ufanisi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua mradi wa maji ya chemichemi kwenye kijiji cha Kongwa Maji
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na ujumbe alioambatana nao wakikagua mashine ya kusukumia maji kwenye mradi wa maji ya chemichemi kijijini Kongwa Maji
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Suguta Wilayani Kongwa.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akiwasalimia Watoto wenye Ulemavu wa Viungo na matatizo ya akili wanaotibiwa kwenye kituo cha Watoto cha Mlali Kongwa.


BREAKING NYUZZZZZ.....: MUIGIZAJI WA FILAMU ELIZABETH MICHAEL "LULU" AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA

$
0
0
 Muigizaji wa Filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa ni mwenye huzuni sana wakati akiwa katika Mahakama Kuu Dar es salaam kabla ya kusomewa hukumu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili jela. 

Na Karama Kenyunko
Leo Novemba 13, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imemuhukumu msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael "Lulu" kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba

Hukumu hiyo imesomwa na Jaji Sam Rumanyika ambaye amesema, ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka na wazee wa baraza waliotoa maoni yao kuwa kweli mshtakiwa Lulu aliuwa bila ya kukusudia.

Lulu ametiwa hatiani chini ya kifungu cha sheria Namba 195 cha cha mwenendo wa mashtaka ya jinai.
Lulu akiwa Mahakamani mapema leo kabla ya kusomewa hukumu yake.

MBIO ZA TIGO DODOMA HALF MARATHON ZAFANA

$
0
0
 Wafanyakazi wa Tigo walioshiriki katika mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon wakiwa na bango linalosema 'Tumekusoma' kabla ya kuanza kwa mbio hizo ndefu jijini Dodoma leo. Tumekusoma ni kampeni mpya ya Tigo inayolenga kuwapa wateja wake urahisi wa kutumia huduma za simu pamoja na faida zaidi za bonasi kila watakapotumia namba mpya ya *147*00# kununua muda wa maongezi, bando, data na kufanya miamala ya fedha.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na medali na vyeti walivyotunukiwa kwa kushiriki mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana.
Naongoza kwa mfano na vitendo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dr Hamisi Kigwangala akimalizamio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana. Mhe Dr. Kigwangala alishiriki katika mbio za kilometa 21.
Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon (wanaume), Dickson Allan wa Mara akipokea zawadi zake za ushindi kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana SHoza baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijino Dodoma jana.

Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii.

$
0
0
Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Utalii wameombwa kumpa ushirikiano Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deograsius Mdamu, ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Wizara hiyo , Bi. Uzeeli Kiangi katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu mwanzoni mwa mwezi Julai kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma akiwa ameitumikia Wizara kwa kushika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33.

Akizungumza katika hafla hiyo alisema ‘’ Watumishi ni kiungo muhimu katika kumsaidia Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutekeleza majukumu yake, ni matumaini yangu kuwa mtampa ushirikiano katika hili’’

Amesema kupitia ushirikiano huo utasaidia kupelekea Wizara kutimiza azma ya kufikia watalii milioni 8 na fedha za kigeni dola bilioni 20 kila mwaka kufikia mwaka 2025.Aidha, Bi.Kiangi aliwataka watumishi kuzingatia miiko ya kazi zao kwa kutojihusisha na vitendo vya kupokea rushwa wanapotimiza majukumu yao, la sivyo serikali hii ya awamu ya tano haitawaacha salama.

‘’Wakati wa utumishi wangu nilijitahidi kukwepa kupokea rushwa kwa kuwa sikujua huyu anayetaka kunihonga katumwa na nani na kwanini anipe rushwa wakati natimiza majukumu yangu jihadharini na watoa rushwa’’ alisisitiza
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye picha ya pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (katikati) katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu na Afisa Utalii Domina Moshi (kushoto)
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (kulia) akiwa na Afisa Utalii Mwandamizi, Martin Mrema (katikati) wakiwa wanatabasamu huku wameshika kwa pamoja moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya Bi. Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu. 
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (Kulia) akiwa na Afisa Utalii Domina Moshi (katikati) wakiwa wanatabasamu huku Bi. Kiangi akiwa ameshika kwa moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha yake aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.

NAIBU SPIKA ACHANGISHA MILIONI 150 KWA AJILI YA HOSPITALI YA WILAYA YA NMTUMBO

$
0
0
Shilingi milioni 150 zimeshangishwa ikiwa fedha taslimu na ahadi kwa ajili kujenga chumba cha upasuaji na wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya namtumbo mkoani ruvuma.

IDARA YA UTALII YAMTAKIA MAISHA MAPYA ALIYEKUWA MKURUGENZI MSAIDIZI WA IDARA YA UTALII, BI.UZEELI KIANGI BAADA YA KUSTAAFU KWA MUJIBU WA SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akimkabidhi moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma.
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akiwa na Afisa Utalii, Nina Kisando (katikati) wakiwa wanatabasamu huku wakionesha moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya Bi. Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii wakimsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma.
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi ( wa pili kushoto) akisindikizwa na baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii mara baada ya hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MWAKYEMBE:WATANZANIA JITOKEZI KUMSHANGILIA BONDIA WETU IBRAHIM CLASS

$
0
0
Na Anitha Jonas WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kumshangilia bondia Ibrahim Class katika pambano lake la kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia kutoka Afrika ya Kusini  Koos  Sibiya.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa wito huo jana  jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake bondia  kwa pambano litakalofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017.

“Bondia huyo anauwezo mkubwa na amekwisha kushinda mara mbili kwa Afrika na kwa mkanda huu wa kugombea ubingwa wa dunia nimeona ni vyema akapigania hapa nchini ili watanzania waweze kuona uwezo wake na pamoja na kumongezea ari ya kupambana kwa ajili ya watanzania walikuja kumuunga mkono,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea  kuzungumza katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alisema  atasimamia mchezo wa ngumi na kuhakikisha unarudisha heshima yake kama ilivyokuwa zamani kwa kuhakikisha anadhibiti wapiganaji wanaokwenda kwenye mapambano na kununuliwa huku wakililetea sifa mbaya taifa ya kutumika kupandisha watu madaraja.

Kwa upande wa Bondia Ibrahim Class wa nchini aliwahakikishia watanzania kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha anauchukua ubingwa huo na mkanda huo kubaki nchini huku akiwataka watanzania kuja kujionea wenyewe namna atakavyopambana na kuonyesha uwezo wake.

“ Nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa  waje kujionea wenyewe jinsi gani nitakavyo mpiga huyo mwafrika kusini na kuchukua mkanda nimejiandaa vizuri na mazoezi ninayofanya niyakiwango cha juu,”alisema bondia Class.
Pamoja na hayo nae Rais wa TPBC Bw.Chaurembo Palasea aliongeza kuwa mchezo wa ngumi umekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ulingo kwa ajili ya kufanyia mazoezi kwani hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa sekta ya mchezo wa ngumi. 

Halikadhalika Waziri Mwakyembe  amesema kuwa serikali itaanzisha bodi itakayosimamia sekta ya ngumi kwa lengo la kuondoa kukosekana kwa dira ya usimamizi wa sekta ya ngumi nchini.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia) akitoa wito kwa watanazania  kujitokeza kwa wingi uwanja wa uhuru tarehe 25/11/2017 kushangilia pambano la bondia Ibrahim Class (kushoto)  wanchini akitetea ubingwa wa dunia uzito wa kati na bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini leo jijini Dar es Salaam alipomtembelea bondia huyo  kambini  Joe Gym  Kawe. yake ya mazoezi .
 Bondia Ibrahim Class (kulia) akifanya mazoezi na Mwalimu Msaidizi Bw.Kelvin Magembe (kushoto) kuonyesha uwezo wake mbele ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia)alipomtembelea kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano litakalofanyika kati yake na Bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017 Uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.

 Bondia Ibrahim Class (kulia) akimkabidhi  zawadi ya tisheti yenye jina lake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) alipomtembelea bondia huyo  kambini Joe Gym  Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano la tarehe 25/11/2017 katika uwanja wa uhuru na bodia wa Afrika ya Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati leo jijini Dar es Salaam.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungungumza na Mbunge wa Urambo Tabora, Magreth Sitta, nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Joseph Ngonyani(Maji Marefu) nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena, nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KAMA YALIVYONASWA NA KAMERA YETU

$
0
0
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa wamebeba shehena ya Mzigo wa ndizi kwa ajil iya kupeleka Kigamboni kama walivyokutwa na mpiga picha wetu kando kando wa barabara ya kuelekea katika kivuko cha Kigamboni eneo la Kivukoni Dar es Salaam leo.
Wasukuma Mkokoteni wakisaidia kusukuma Mzigo wa vyombo mbalimbali kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika barabara ya Kivukoni jijini Dar es Salaam leo.

IDARA YA MAAFA YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MAAFA

$
0
0
Ofisi ya Waziri Mkuu imeendesha warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo inayohusu Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa masuala ya Menejimenti ya maafa nchini.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Novemba 12, 2017 Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.William Ngeleja alieleza kuwa warsha hiyo itawajengea uwezo wajumbe wa Kamati hususani katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Warsha hii ni muhimu kwa wajumbe wa kamati kwani itaongeza uelewa kuhusu sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 pamoja na dhana nzima ya Menejimenti ya Maafa".Akifanua mhe.Ngeleja amesema warsha hiyo itasaidia kuongeza tija katika utendaji wa kamati hasa katika kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya maafa.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwaeleza wajumbe kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini ili kujenga uwezo wa Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali pindi maafa yanapotokea hivyo warsha hii inatija kwa wajumbe wote.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe. William Ngeleja akitoa maelezo ya awali kuhusu utendaji kazi wa kamati hiyo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 bungeni Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uratibu wa Maafa na namna Serikali inavyojenga uwezo wa Idara hiyo ili kuongeza tija wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa .
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu Maafa Novemba 12, 2017 bungeni Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA 

KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI WAZUNGUMZA NA WATUMISHI WA KITUO CHA DAR ES SALAAM

$
0
0
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo waliopo katika kituo cha Dar es Salaam leo ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii na kufuata Sheria za Utumishi wa Umma.
  Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Bw. Nicholaus Willium akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo waliopo katika kituo cha Dar es Salaam leo ambapo amewataka kufanya kazi kwa kujituma na kwa ushirikiano.
Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akizungumza  wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara  ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo waliopo katika kituo cha Dar es Salaam leo Jijini Dar es Salaam .

"UWANJA WA NDEGE WA CHATO KUSAIDIA USAFAIRISHAJI WA BIDHAA ZA MADINI"-NAIBU WAZIRI NYONGO

BENKI YA KILIMO YATUPIA JICHO MIRADI YA KILIMO ZANZIBAR

$
0
0
 Katika jitihada za kuchagiza maendeleo ya kilimo Visiwani Zanzibar, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya ziara katika miradi mbalimbali ya kilimo visiwani humo.

Ziara hiyo imelenga kufanya utambuzi wa miradi ambayo ina uhitaji wa mikopo ya gharama nafuu hali itakayochochea kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima kama vile kujengewa uwezo juu ya uandaaji wa andiko la miradi ya Kilimo, upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba.

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) ambao walikuwa wenyeji wa TADB, Bw. Ussi Mohamed Juma (aliyesimama) akizungumza na ugeni huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya ZSTC Kinazini, Zanzibar. 

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi hiyo, Bibi Rehema Twalib, amesema kuwa TADB ikiwa chombo cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya  asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

“Ziara yetu hii inalenga katika kusaidia juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” alisema.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bibi Rosebud Kurwijila, Bibi Rehema Twalib, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao na uongozi wa ZSTC. 

Akizungumza na ugeni huo, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) ambao walikuwa wenyeji wa TADB, Bw. Ussi Mohamed Juma alisema ujio wa TADB visiwani humo kutasaidia wakulima wa  Zanzibar ambao kama walivyo wakulima wengine nchini kukosa mikopo ya gharama nafuu hali inayorudisha nyuma jitihada za wakulima hao.

Akaongeza kuwa lengo la TADB linasadifu majukumu ya kuanzisha kwa ZSTC ambayo yanalenga kuchagiza maendeleo katika mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika mazao ya ili kilimo hivyo kukuza, kuboresha ubora na kuongeza ushindani wa kupamba na bidhaa nyingine za kilimo katika soko la dunia.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (alyesimama) akifafanua kuhusu malengo ya TADB wakati wa mazungumzo yao na ZSTC. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya ZSTC Kinazini, Zanzibar. 

Bw. Juma akaahidi ZSTC kutumia ushirikiano huo na TADB katika kuwezesha maendeleo na kusaidia mabadiliko ya sekta ya kilimo visiwani humo.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa ujio wa TADB visiwani Zanzibar utasaidia kutatua tatizo la mitaji kwa wakulima kwani kwa sasa taasisi za nyingi za fedha zinaelekeza mikopo zaidi kwenye upande wa biashara na bidhaa.

“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara na bidhaa na kuwasahau wakulima na wasindikaji wa mazao, hivyo tunaamini TADB itasaidia kutatua changamoto hii,” alisema.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MPYA WA CHINA NCHINI TANZANIA

$
0
0
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi mpya wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Wang ke (kulia) alipotembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati) akizungumza na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto), Balozi mpya wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Wang ke (wa pili kushoto), pamoja na ugeni kutoka ubalozi wa China nchini Tanzania, katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Spika Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi mpya wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Wang ke (wa pili kushoto) katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Spika Mjini Dodoma, katikati ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na Wageni wengine ni wasaidizi wa Balozi kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania.
 Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akipokea zawadi toka kwa Balozi mpya wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Wang ke (kushoto) baada ya kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi Wang ke (kulia), Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kushoto) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Mchango wa Asasi za Kiraia kwenye Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi

$
0
0
                    Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Vijijini ADLG iliyopo Jijini Mwanza, Jimmy Luhende akichangia mada kwenye Mkutano wa Sekta ya Uziduaji 2017 uliofanyika Mjini Dodoma.

Novemba 02-03, 2017 ulifanyika Mkutano wa Sekta ya Uziduaji (Madini, Mafuta na Gesi) Mjini Dodoma ambapo miongoni mwa maazimio kwenye mkutano huo ni Asasi za Kiraia kushiriki ipasavyo katika kuhakikisha Taifa linanufaika na Rasilimali zake.

Ungana na BMG kujua yaliyojiri kwenye mkutano huo ulioandaliwa na muungano wa Asasi za Kiraia zinazoangazia masuala ya Utawala Bora kwenye sekta ya Uziduaji nchini HakiRasilimali. Tazama HAPA ufunguzi wa mkutano huo. Tazama HAPA hafla ya usiku baada ya mkutano huo. Mwanasheria Veronica Zano (kushoto) kutoka Zimbabwe akichangia mada kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Vijijini ADLG iliyopo Jijini Mwanza.

TABOA, UWADAR Wakanusha Taarifa ya Mgomo Inayosambaa Mitandaoni

$
0
0
Na.Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Chama cha Wamiliki wa Mabasi Yaendayo Mikoani (TABOA) na Umoja wa Wasafirishaji Abiria Jijini Dar es Salaam (UWADAR) wamekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao kuwa Novemba 14 mwaka huu watakuwa na mgomo wa kusitisha huduma za usafirishaji.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa UWADAR, Kismat Dhalla wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwa ajili ya kukanusha suala hilo.

Dhalla amesema kuwa taarifa hiyo iliandaliwa na vyama hivyo lakini ilishatolewa katika vyombo vya habari siku nyingi zilizopita hivyo kuna baadhi ya watu wameamua kuisambaza upya bila ridhaa ya wahusika.

“Ni kweli ile taarifa ni ya kwetu lakini tulishaitoa siku nyingi na mgomo huo haukufanyika kwa kuwa tuliahidiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kuwa itayafanyia kazi madai yetu”, alisema Dhalla.

Dhalla ameongeza kuwa tayari SUMATRA imeandaa mkutano na wadau ambao utafanyika mnamo Novemba 15 mwaka huu kwa ajili ya kujadili kuhusiana na baadhi ya Kanuni zilizotungwa katika Sheria hiyo ya SUMATRA.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa SUMATRA, Tumaini Silaa amesema kuwa lengo la SUMATRA ni kuhakikisha kuwa usafiri unapatikana muda wote na unamfaidisha msafiri na msafirishaji ndio maana mamlaka hiyo inajitahidi kuyamaliza malalamiko ya TABOA na UWADAR pindi yanapojitokeza.

“Sisi kama SUMATRA tunaona kuwa hakuna mgogoro kati yetu na wadau wa usafiri isipokuwa ni kutoelewa Kanuni ambazo zimepitishwa na Mhe. Waziri mwenye dhamana hivyo tutakapokutana katika mkutano huo tutaeleweshana kwani tunaamini kuwa kanuni zilizoandaliwa ziko vizuri”, alisema Bw.Silaa.

Amefafanua kuwa baadhi ya watu bado wanachanganya Kanuni za mwaka 2007 ambazo zimefutwa na kanuni hizi mpya lakini wanatakiwa kufahamu kuwa kanuni mpya zimeweka usawa kwa upande wa msafirishaji, abiria, dereva na kondakta.

Pia, kanuni hizo mpya bado hazijaanza kutumika mpaka pale SUMATRA itakapotoa elimu ili kila mmoja awe na uelewa na Sheria na Kanuni zake.

SHEKH NURDEEN KISHK AISOGEZA JAMII KARIBU KWA KUFUNGUA KISHK TV ONLINE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi wa taasisi ya AL Hikma Nurdeen Kishki amesema kuwa kwa sasa waumini wake pamoja na jamii inayozungumza  wanaweza kupata mawaida yake, hadhara, hotuba  na hadithi mbalimbali kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Shekh Kishk ameweka wazi akaunti zake za mitandao ya kijamii facebook, twitter , instagram sambamba na kufungua TV ya Online itakayokwenda kwa jina la Kishki Online Tv.

 Akizungumza wakati wa utambulisho wa akaunti hizo, Shekh Kishk amesema kuwa jamii iliyokuwa inamfuatilia kwa kipindi kirefu walikuwa wanalalamika kwa  kukosa mawaidha yake ambapo kwa kiasi kikubwa kinazidi kuwasogeza karibu nae.

“ Jamii inayonifuatilia ilikuwa inalalamika kila wakati wakisema kwanin Shekh haufungui mitandao ya kijamii na wengine walitaka kunifungulia ila sikuwa tayati, ila kuna baadhi ya watu walikuwa wanatumia mgongo wangu kufungua akaunti za facebook kwa kutumia jina langu na wakifanikiwa kwani walipata watu wengi kwa kipindi kifupi,”amesema Shekh Kishk.

Shekh Kishk amesema kuwa,  katika akaunti hizo watu wataweza kupata darasa mbalimbali za hadithi, mawaidha, hotuba, hadithi na kutakuwa na usomaji wa Quran katika sauti saba, mbali na hilo kutakuwa na video za mawaidha na hotuba ambazo anazitoa wakati  akiwa katika ziara za mikoani na hata nje ya nchi kwani amekuwa anatembea na watu wa habari kila mahala.

Amewatoa hofu watu kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii ndiyo inaweza kusababisha kufanya maovu ila ukiamua kuitumia vizuri inaweza kukuletea faida.

Kwa upande wa katibu wake anayejulikana kwa jina la Masawe, alisema kuwa kwa kipindi kirefu alikuwa anasumbuliwa na watu mbalimbali kwa nini Shekh Kishk hafungui akaunti za kijamii  ila baad aya kukaa naye na kushauriana tukaamua kufungua na katika muda wa saa 24 ameweza kupata marafiki 5000 na kuamua kuwa na page ya facebook.
 Shekhe Nurdeen Kishk akiwaonyesha waandishi wa habari jina analotumia katika mtandao wa kijamiiya facebook, twitter na instagram sambamba na Kishk Online Tv leo Jijini Dar es salaam.
 Shekh Nurdeen Kishk akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kufungua akaunti za mitandao ya kijamii facebook, twitter na instagram sambamba na Kishk Online Tv zilizotambulishwa rasmi leo.
Katibu wa Shekh Nurdeen Kishk akizungumza na waandishi kuhusu namna jamii ilivyokuwa inatamani kuona Shekh anakuwa na akaunti katika mitandao ya kijamii.

"IMEBUMA KATIKATI YA BARABARA"

$
0
0
Wasamalia wakiipiga kibega gari iliyokuwa imebuka katika makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma eneo la Ubungo, na kupelekea adha ya kupita kwa Mabasi ya Mwendo kasi.

HABARI KAMILI: Lulu kutumikia miaka miwili jela

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

Leo Novemba 13, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imemuhukumu msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Hukumu hiyo imesomwa na Jaji Sam Rumanyika ambaye amesema, ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka na wazee wa baraza waliotoa maoni yao kuwa kweli mshtakiwa Lulu aliuwa bila ya kukusudia.

Alisema  Aprili 12, 2012 ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Lulu kufikishwa Mahakamani ambapo alifikishwa katika mahakama ya mkoa wa Dar es Salaam, ambayo ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kujibu tuhuma za mauaji ya marehemu Kanumba. Lakini baadae baada ya kusota rumande kwa takribani miezi kumi, Lulu alibadilishiwa mashitaka na kushitakiwa kwa mauaji ya bila kukusudia, shtaka lililomuwezesha kuwa nje kwa dhamana hadi leo.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Rumanyika amesema, kesi hiyo imejikita katika ushahidi wa mazingira na kwamba mshtakiwa mwenyewe alikubali kwamba yeye ndio alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemeu Kanumba ambaye alikuwa ni mpenzi wake kwa miezi minne . Alisema ili kuthibitisha kesi hii ni watu wawili pekee ndio wenye uwezo huo ambao ni mshitakiwa na marehemu.

‘’Kwa sababu hiyo, mshitakiwa anatakiwa kutoa maelezo ya kina yanayojitosheleza na akishindwa kufanya hivyo ataonekana kwamba yeye ndiye muuaji. Ushahidi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee endapo utaendelea kumnyooshea kidole mshitakiwa,’’ alisema Jaji Rumanyika.
Alisema maelezo aliyoyatoa mshitakiwa yanakidhi viwango na vigezo kwa kuwa alikubali kwamba walikuwa na mzozo na kupigwa. Alisema ‘’kwa maoni yangu kuanguka au kudondoka kwa mtu mmojawapo katika ugomvi atakuwa amesukumwa au kumkaba mwenzake.’’
Alisisitiza  kuwa mshitakiwa anajukumu la kutoa maelezo ya kutosha kuhusu tukio lililotokea na kwamba alijikanganya wakati akitoa utetezi wake.

 Alieleza  kuwa Lulu aliiambia mahakama marehemu Kanumba  alikuwa amelewa na desturi ya mlevi mara nyingine huanguka, lakini yeye alieleza kuwa aliburuzwa na kurudishwa chumbani hivyo kama alikuwa mlevi hakueleza kama wakati wanakimbizana alianguka.

Pia alisema maelezo yaliyotolewa na Josephine Mushumbuzi yanaacha maswali mengi kwa sababu hayana hadhi ya cheti cha daktari na kwamba Daktari Paplas Kagaiga ndiye aliyethibitishwa na mshitakiwa mwenyewe pamoja na mdogo wa marehemu, Seth kuwa ndiye daktari  wa familia na kwamba ndiye aliyepaswa kujua historia ya marehemu ikiwemo afya na maradhi. Hata hivyo, mshitakiwa kwa kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi alitazamiwa  ajue maradhi ya marehemu lakini kwenye utetezi wake hajaeleza.

Makumbusho ya Taifa yaandaa onesho la picha zilizopigwa miaka iliyopita

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Raia wa Denmark, Jesper Kirkanes wameandaa onesho la picha mbalimbali za maisha ya Watanzania zilizopigwa miaka 50 iliyopita.

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Profesa Audax Mabula amesema onesho hilo ni muhimu kwa watanzania kujikumbusha maisha ya miaka 50 iliyopita.

Amesema kuwa onesho hilo litafanyika Novemba 16 katika viwanja vya makumbusho ya Taifa ambalo litafunguliwa na Balozi wa Denmark nchini, Einar Jensen.Profesa Mabula amesema kuwa katika siku ya onesho hilo hakutakuwa na kiingilio katika kuangalia picha hizo pamoja na picha zingine zilizomo katika makumbusho ya taifa.

Aidha amesema kuwa onesho la picha hizo ni pamoja maisha na kazi zilizokuwa zinafanywa watanzania ambapo kwa sasa watanzania wanatakiwa kujua historia ya maisha ya miaka 50 iliyopita.

Amesema wakati uliopo wa sera ya viwanda ni funzo kutoka kwa watanzania ambao waliishi kwa kuweza kuendesha maisha yao kwa kujitengenezea vitu ambavyo walikuwa wakihitaji.Profesa Mabula amesema kuwa picha hizo zilipigwa mwanzoni mwa mwaka 1968 mpaka mwaka 1977 na zilipigwa na Raia wa Denmark, Jesper Kirkanes ambaye alikuja nchini kwa kazi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa , Audax Mabula akizungumza na waandishi habari juu ya onesho la picha zilizopigwa miaka 50 iliyopita litakalofanyika Novemba 16 mwaka huu katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa.
Raia wa Denmark, Jesper Kirkanes ambaye alipiga picha za maisha ya watanzania miaka 50 iliypita akizungumza na waandishi habari juu ya maana picha hizo leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images