Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AZINDUA HOTELI YA FANTASY MSALATO, MJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Hoteli ya Fantasy iliyojegwa katika Kata ya Msalato, Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Mhe. Mussa Hassan Mussa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Amani, Zanzibar na ayefuatia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula . Wengine katika picha kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony Mavunde na Mbunge wa Kijitoupele, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiweka Jiwe la msingi la Ujenzi wa Awamu ya pili ya Hoteli ya Fantasy iliyopo Msalato, Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Mhe. Mussa Hassan Mussa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Amani, Zanzibar na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony Mavunde
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akipanda Mti mara baada ya kuzindua Hoteli ya Fantasy iliyojegwa katika Kata ya Msalato, Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza wakati alipokwenda kuzindua Hoteli ya Fantasy iliyojegwa katika Kata ya Msalato, Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Mhe. Mussa Hassan Mussa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Amani, Zanzibar. Wengine katika picha kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde na anayefuatia ni Mbunge wa Kijitoupele, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha.


PICHA NA BUNGE

RC MAHENGE ATOA NENO KWA WATUMISHI DODOMA

$
0
0
Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge amewataka watumishi wa Umma na Taasisi mbalimbali kwenye Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuwahudumia Wananchi kikamilifu na kwa uadilifu wakitambua kuwa sasa Mkoa wa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.

Aidha amesema yapo baadhi ya maeneo Mkoa bado haufanyi vizuri hususani katika sekta ya elimu ambapo hali ya ufaulu hairidhishi.

Akiwa wilayani Mpwapwa katika ziara yake ya kutembelea wilaya za Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kujitambulisha Dkt. Mahenge amesema eneo la Elimu ya Msingi na Sekondari hali ya ufaulu hairidhishi ambapo Mkoa umeshika nafasi ya 24 kati ya Mikoa 26 kwenye matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017, Wakati kwa upande wa Matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya Sekondari kidato cha nne mwaka 2016 Mkoa ulikuwa wa 19 kati ya Mikoa 26.

Amesema viongozi hao wanayodhamana kubwa kwa Wanadodoma kwenye masuala yote ya maendeleo kama vile Elimu, Afya, Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kutumia fursa ya kuwa jirani na Serikali katika kusukuma mbele masuala ya Maendeleo kwenye Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akikagua kitalu cha miche ya Mikorosho ambayo itaanza kugaiwa bure kwa wananchi kwa lengo la kuipanda na kukuza kilimo cha zao la korosho wilayani Mpwapwa
Sehemu ya Kitalu cha Miche ya Mikorosho kilichopo eneo la Magereza Mpwapwa, jumla ya tani sita (6) za mbegu bora za mikorosho zimeoteshwa kwa lengo la kugawa bure miche ya mikorosho kwa wananchi kuipanda na kukuza kilimo cha zao hilo Wilayani Mpwapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge namna miti ya mikorosho ilivyozaa korosho kwenye shamba darasa la Magereza Mpwapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha kukamua mbegu za alizeti na usindikaji mafuta ya alizeti cha mjasiriamali Ndg. Sangito Akyoo. 


MAHAFALI YA TISA YA KIDATO CHA NNE KOM SEKONDARI 2017 YAFANA

$
0
0
Shule ya Sekondari Kom iliyopo mjini Shinyanga leo Jumamosi Novemba 11,2017 imefanya mahafali ya 9 ya kidato cha nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2006. 

Mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya kidato cha nne mwaka 2017 yaliyohudhuriwa na wazazi na wageni mbalimbali alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.

Akizungumza katika mahafali hayo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema mabadiliko yoyote yanaletwa na ushirikiano hivyo kupitia ushirikiano.lisema shule hiyo imekuwa maarufu nchini kutokana na elimu bora inayotoa na kutokana na hali hiyo imeupatia sifa mkoa wa Shinyanga.

“Sisi kama serikali tunajivunia uwepo wa shule hii katika mazingira yetu kwani inatutangaza, tupo tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto zinazojitokeza ili kusukuma gurudumu la maendeleo”,alieleza Matiro.“Tupo tayari kuhakikisha kuwa tunashirikiana na sekta binafsi na milango yetu ipo wazi na panapotokea changamoto msisite kutufikia”,alisema.
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe wakati wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kom.Kulia ni mwenyekiti wa bodi ya shule Peter Kugulu,kushoto ni mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom,Jackton Koyi 
Wahitimu wakiingia ukumbini 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimlisha keki mhitimu wa kidato cha nne Dickson Nyansika .
Wanafunzi wakiimba shairi 

WIZARA YA AFYA YAWATAKA WANAWAKE KUPIMA AFYA ZAO ILI KUPAMBANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Neema Rusibamayira amesema kuwa anafurahishwa na jitihada zinazofanywa  na taasisi zisizo za kiserikali kwa kuhakikisha wanapambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy mwalimu, Dkt Neema amesisitiza elimu juu ya masuala ya afya kwa akina mama kuweza kupata elimu zaidi kwani wao ndo waathirika wakuu wa ugonjwa wa kisukari.

Akitoa rai hiyo baada ya matembezi hayo yaliyoanzia Muhimbili mpaka viwanja vya Mnazi mmoja vikihusisha wadau mbalimbali, Dkt Neema amesema elimu juu ya masuala ya magonjwa yasiyoambukizi yatasaidia kupunguza kwa ongezeko la wagonjwa wa kisukari pia wananchi wawe na kawaida ya kupima afya zao mara kwa mara.

Matembezi hayo yameenda na kauli mbiu ya mwanamke na kisukari pia wadau walioweza kushirikiana kwa pamoja ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), TANCDA, LIONS Club na TDA ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani yakienda na kauli mbiu ya mwanamke na kisukari.
 Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Neema Rusibamayira akizungumza baada ya matembezi ya hisani ya kuhamasisha wananchi kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani na mwaka huu yakienda na kauli mbiu ya Mwanamke na kisukari.
 Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Benard Konga akizungumza baada ya matembezi ya hisani ya kuhamasisha wananchi kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani na mwaka huu yakienda na kauli mbiu ya Mwanamke na kisukari. 

Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Neema Rusibamayira(wa kwanza kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Benard Konga alipowasilia katika viwanja vya Mnazi baada ya matembezi ya hisani ya kuhamasisha wananchi kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani na mwaka huu yakienda na kauli mbiu ya Mwanamke na kisukari.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA JUMAPILI LEO NOVEMBA 12,2017

“Marufuku kuuza mbolea tofauti na bei elekezi,” – RC Wangabo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameagiza kukamatwa kwa wafanyabiashara wote wanaouza wanaouza pembejeo kwa zaidi ya bei elekezi iliyotolewa rasmi na serikali kwani kufanya hivyo ni kukiuka utaratibu uliowekwa na serikali kwaajili ya kuwanufaisha wakulima.

Amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya maduka katika Manispaa ya Sumbawanga wanauza mbolea kwa bei isiyo halali na hivyo tayari ameshaagiza vyombo vya dola viwashughulikie watu hao haraka iwezekanavyo.

“Ni marufuku kwa wauzaji wa pembejeo kuuza mbolea kwa bei ambayo ni nje ya bei elekezi, msako mkali utafanyika kwa halmashauri zote kuhakikisha kuwa bei elekezi ndio inayotumika na kuwabaini wale wote wanaouza kinyume na bei hii elekezi,” Alisisitiza.

Ameongeza kuwa bei hizo zinatofautiana kati ya Halmashauri na Halmashauri na kwa Manispaa ya Sumbawanga bei elekezi kwa mbolea ya kupandia (DAP) ni shilingi 55,427 na ya kukuzia (Urea) ni 42,848. Halmashauri ya Nkasi mbolea ya kupandia (DAP) ni shilingi 55,961 na ya kukuzia (Urea) ni 43382. Halmashauri ya Kalambo mbolea ya kupandia (DAP) ni shilingi 57,022 na ya kukuzia (Urea) ni 44,443 na Sumbawanga Vijijini mbolea ya kupandia (DAP) ni shilingi 56,808 na ya kukuzia (Urea) ni 44229.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.

TAARIFA KWA UMMA

Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400

$
0
0
NAIBU Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewahamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini na kufanikisha kupata vifaa vya ujenzi wa mradi wa awamu ya kwanza wa nyumba za Polisi Mikoa ya Pemba, Zanzibar.

Mradi huo umeanza katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba ambapo nyumba kumi na mbili zinatarajiwa kujengwa ili kufanikisha askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi ndani ya mikoa hiyo waweze kuishi katika nyumba za jeshi pamoja na kupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba za makazi ya polisi hao, pia mradi huo utajenga nyumba katika mikoa mipya nchini pamoja na makao ya nchi Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, katika Bandari ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba, jana, Mhandisi Masauni alisema, ujenzi wa nyumba hizo utakua ni wa hatua ya awali, lakini mipango mbalimbali itaendelea kuwezesha nyumba nyingi zaidi kujengwa katika eneo hilo ili kuhakikisha baadhi ya askari wanaoishi nje ya kambi za polisi waweze kuishi kambini ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

“Leo nimewakabidhi wakuu wa mikoa hawa vifaa vya ujenzi ambavyo ni mifuko ya saruji, nondo, ndoo za rangi na mabati ili waweze kusimamia zoezi hili la ujenzi wa nyumba za askari wetu kwa umakini mkubwa,” alisema Masauni na kuongeza;
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto) mabati yaliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya Meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, nondo zilizochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, mifuko ya saruji iliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani mara baada ya meli hiyo kuwasili na mizigo hiyo kutoka jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Pemba pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada kukabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi wa nyumba za polisi katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni alisema wadau wamemchangia shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 12 za Jeshi la Polisi ili kukabiliana na ukosefu wa nyumba za polisi katika mikoa hiyo. Awamu ya ujenzi wa nyumba hizo ni ya kwanza, na awamu ya pili itakua mikoa ya mipya nchini ambayo ni Geita, Simiyu, Katavi na Songwe. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Mwajuma Majid Abdalla, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.


MHANDISI MTIGUMWE ATEMBELEA KITUO CHA UKAGUZI WA MAZAO MPAKA WA HOLILI NA TARAKEA

$
0
0
Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe Leo Novemba 11, 2017 ametembelea Vituo vya ukaguzi wa mazao vilivyopo Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ili kujionea ufanisi wa utendaji kazi sambamba na kubaini Changamoto zinazowakabili ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa ushuru.

Katika ziara hiyo ya kikazi Mhandisi Mtigumwe ametembelea Kituo cha HOLILI na TARAKEA ambavyo vipo upande wa Tanzania ikiwa ni mpakani mwa Tanzania na Kenya.HOLILI ni moja ya mpaka kati ya Tanzania na Kenya ambalo upo umbali wa takribani Kilomita 25 Kutokea Himo Njiapanda huku Mpaka wa TARAKEA ukiwa umbali wa Takribani Kilomita 58 kutokea Himo Njiapanda.

Miongoni mwa Changamoto alizozibaini katika ziara hiyo kwenye Vituo vya ukaguzi wa Kilimo kwenye hivyo mipaka miwili ni pamoja na uduni wa vifaa vya kufanya kazi za Kiofisi, Kutokuwa na vifaa vya kufanya kazi ya kupimia Sampuli ya mazao katika Maabara ya Holili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mtigumwe amewataka watumishi wanaosimamia ukaguzi wa mazao kutojihusisha na vitendo vya upokeaji Rushwa kwani kwa mtumishi atakayebainika kufanya hivyo sheria zitachukuliwa haraka dhidi yake ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Mpaka huo wa TARAKEA una jumla ya Njia za panya 250 kutokea Mpaka wa Hororiri mpaka kufikia mpaka wa Namanga.Aidha, Alisema serikali inaendelea na juhudi mbalimbali za kuzikabili Njia za panya zote ili kubaini kila aina ya uhalifu unaofanywa ikiwemo magendo yanayopitishwa kinyemela.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya..
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisikiliza maelezo ya utendaji kazi katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA.

RC Wangabo asisitiza Unyenyekevu, Uadilifu na Uwajibikaji kwa watumishi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesisitiza Uwajibikaji, na kujituma kwa watumishi wote wa serikali mkoani humo ili kuweza kupeleka mbele gurudumu la maendeleo na kuwatumikia wananchi ambao wapo ili waweze kuhudumiwa na watumishi.

Amesema kuwa bila ya uadilifu katika matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo zinazotolewa na serikali katika halmashauri hakutakuwa na maendeleo lengwa jambo litakaoiingizia serikali hasara na kurudi nyuma kimaendeleo.

Ameyasisitiza hayo alipokutana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi katika ziara yake ya siku mbili iliyolenga kutembelea miradi mbalimbali ya halmashauri pamoja na kujitambulisha kwa watumishi na makundi mbalimbali ya wananchi katika wilaya.

“Jambo ninalosisitiza la kwanza ni uwajibikaji, kila mtumishi wa serikali anatakiwa kuwajibika kufanya kazi kwa bidii na kujituma, kwani serikali hutoa pesa nyingi za miradi ya maendeleo hivyo tusipokuwa waadilifu na kufanya kazi kwa bidi rasilimali zetu tutazipoteza, tunataka thamani ya fedha ionekane huko kwenye utekelezaji wa miradi hiyo,” Alisisitiza.

Pamoja na hayo RC Wangabo amewataka watumishi hao kuwa wanyeyekevu wanapokuwa wanawahudumia wananchi na kutotumia vyeo vyao kuwanyanyasa wananchi hao kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakiogopa kuingia kwenye ofisi za kiserikali ili kutatuliwa changamoto na matatizo yanayowakumba kutoka katika maeneo yao.

Amesema kwa kufanya hivyo kutaipa sifa serikali na pia kujiwekea akiba ya uaminifu kwa wananchi wanaopewa huduma hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wngabo akisalimiana na Afisa Kilimo Wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Samel Kamwea alipofika tayari kwa kuanza ziara yake ya kwanza kuzunhgukia halmashauri Mkoani humo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wngabo akisalimiana na Afisa Kilimo Wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Samel Kamwea alipofika tayari kwa kuanza ziara yake ya kwanza kuzunhgukia halmashauri Mkoani humo. 

HESLB yatangaza wanafunzi wengine 1,775 wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo, Yafungua dirisha la rufaa hadi Novemba 19

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha nyingine yenye wanafunzi 1,775 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 31,353.

Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo, Awamu ya Pili (11,481), Awamu ya Tatu (7,901). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumapili, Novemba 12, 2017) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, orodha kamili ya wanafunzi hao inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na pia imetumwa kwa vyuo husika leo ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.

“Tumekua tukifanyia kazi orodha za udahili ambazo tumekuwa tukipokea, na kila tunapokamilisha, tunatoa orodha za wanafunzi waliopangiwa mikopo ambao wana sifa – leo tumetoa hao 1,775,” amesema Bw. Badru.

Bw. Badru, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari pia amekumbusha kuwa kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018. Fedha hizo, shilingi 427.54, ni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 122,623 wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea na masomo.

Kufunguliwa kwa dirisha la rufaa

Wakati huohuo, HESLB imetangaza kufungua dirisha la rufaa kuanzia kesho, Jumatatu, Novemba 13, 2017 hadi Novemba 19, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili.  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa HESLB, lengo la HESLB ni kuhakikisha wanatangaza orodha ya majina ya waombaji mikopo waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo au kabla ya tarehe 30 Novemba mwaka huu.

“Tunatoa wito kwa uongozi wa vyuo vyote kupokea maombi ya rufaa za wanafuzi na kuwasilisha kwa Bodi ya Mikopo kabla ya Novemba 22, 2017 ili kuiwezesha Bodi kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo Novemba 30, 2017,” amesema Bw. Badru katika taarifa yake.

Maelezo ya kina kuhusu utaratibu wa kuwasilisha rufaa yatatolewa kupitia tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).

"JAMBO MTOTO"

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsalimia Mtoto Ivan Bosco (miezi7) akiwa katika Viwanja vya Bunge na Mama yake Mariam Zablon kutoka Bukombe Mkoani Geita walipotembelea bungeni Dodoma Novemba 10, 2017 kujionea shughuli za Bunge.

Zaidi ya wanafunzi 3000 wa vyuo vikuu kunufaika na mradi wa ”Mobile for change”

$
0
0
Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwajengea uwezo wanavyuo katika nyanja za Uongozi, kibiashara, maisha ya kawaida na masuala ya kifedha kwa njia ya mtandao”Banking on Mobile for Change in Universities Project”, kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Green Hope itakayosimamia mafunzo na Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Thomas Yohana.

Zaidi ya wanafunzi 3000 wa vyuo vikuu wataanza kunufaika na mradi wa”Mobile banking for change”kupitia taasisi ya maendeleo ya jamii ya Vodacom Tanzania Foundation ikishirikiana na shirika la Green hope.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana wakati wa uzinduzi wa program hiyo,Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald alisema mradi wao utatumika kuwajengea wanafunzi uwezo katika ujuzi wa nidhamu ya fedha,stadi za maisha na uongozi bora.

Sandra alisema wanafunzi watakaofaidika ni takriban 3000 kutoka vyuo vya mtakatifu Agustino (SAUT), Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo kikuu cha Dar-es-salaam(UDSM).
Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Thomas Yohana akielezea manufaa watakayo yapata wanafunzi kupitia mpango wa kuwajengea uwezo wanavyuo katika nyanja za Uongozi, kibiashara, maisha ya kawaida na masuala ya kifedha kwa njia ya mtandao”Banking on Mobile for Change in Universities Project”, uliozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na Vodacom Tanzania Foundation, kushoto ni Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania mkoani Mwanza Victoria Chale.

“Mafunzo yetu yanalenga kunufaisha wanawake 2,100 sawa na asilimia 70 huku wanaume 900 sawa na asilimia 30 ambao watakaopatikana katika vyuo husika,” Sandra alisema.

Hata hivyo, meneja huyo alisema mafunzo hayo yataanza mwezi huu na kuisha April 2018 na yatafundishwa kwa njia ya semina pamoja na midahalo.

Sandra alisema baada ya mafunzo hayo wanafunzi watakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na  stadi za maisha,ongezeko la kudhibiti matumizi ya fedha zao pamoja na kujiwekea akiba.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Green Hope ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo,Martin Lusenga alisema baada ya mafunzo hayo wanafunzi watakuwa na uhakika wa kuweza kujitunzia kipato chao.

“Lengo letu sisi ni kuhakikisha kwamba kizazi hiki kinapata fursa ya kupanua wigo ya masuala mbali mbali ikiwemo kujiajiri hata baada ya masomo,” alisema.

Mmoja ya washiriki kutoka chuo cha SAUT, Thomas Yohana alisema anawaomba wanafunzi wenzake wahakikishe wanashiriki mafunzo hayo kwa wingi ili kujifunza maswala mbali mbali kwa manufaa yao ya baadaye.

“Ni mara chache sana kupatikana kwa fursa kama hii, hivyo basi niwashauri wanafunzi wenzangu kujitokeza mara tu nafasi kama hizi zinapokuwa zimetoka,” alisema Yohana.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) ,wakimsikiliza Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald mwishoni mwa wiki baada ya kuzindua mpango wa kuwajengea uwezo wanavyuo katika nyanja za Uongozi, kibiashara, maisha ya kawaida na masuala ya kifedha kwa njia ya mtandao”Banking on Mobile for Change in Universities Project”.

Maadhimisho ya Siku ya Jumuiaya ya Wahandisi wa mitambo ya Mawasiliano, Uongozaji na Ufuatiliaji Miennendo ya Ndege Tanzania yafanyika jijini Dar

$
0
0
Kaimu MkurugenziMkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Vallery Chamullungu akizindua siku ya Jumuiya ya Wahandisi wa Mitambo ya Mawasiiano , Uongozaji ndege na ufuatiliaji miendendo ya Ndege Tanzania (ATSEP), wengine ni Emanuel Mikongoti Mhandisi wa mitambo ya kuongozea Anga (katikati), na Obed Dabana Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uongozaji ndege na huduma za ufundi.
Rais wa Jumuiya ya Wahandishi wa Mitambo ya Mawasiliano, Uongozaji na Ufuatiliaji Mienendo ya Ndege Tanzania(TASEA)Emanuel Mikongoti akiongea wakati wa ufunguzi wa Siku ya maadhimisho ya jumuiya ya wahandisi wa mitambo ya mawasiliano, uongozaji na ufuatiiaji mienendo ya ndege duniani yaliyoadhimishwa jijini Dar es salaam.Wa pili kushoto ni kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Vallery Chamulungu, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uongozaji ndege na Huduma Obed Dabana na Katibu Mtendaji wa TATSEA Lucy Msuya.
Washiriki wa maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Wahandisi wa Mitambo ya Mawasiliano, Uongozaji na Ufuatiliaji Mienendo ya Ndege Duniani wakiwa katika Picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Vallery Chamullungu ,Maadhimisho hayo yamefanyika jijini Dar es salaam.

MHANDISI MTIGUMWE AITAKA BODI YA KAHAWA KUONGEZA UZALISHAJI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua kiwanda kidogo cha uzalishaji wa kahawa katika Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili Ofisi hizo kwa ziara ya kikazi.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameitaka Bodi ya Kahawa ambayo ni Taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kusimamia sekta ya Kahawa nchini kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa Kahawa nchini kwani  Kahawa ni miongoni mwa mazao ya kipaumbele.

Mhandisi Mtigumwe ametoa Rai hiyo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa Mara baada ya kutembelea Ofisi za Bodi hiyo zilizopo Mtaa wa Railway, Kata ya Mawenzi Katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Alisema kuwa Mwaka 2011 wadau waliandaa na kupitisha mkakati wa miaka 10 wa maendeleo ya Kahawa ambayo lengo kuu ilikuwa ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia Tani 80,000 Mwaka 2017 na Tani 100,000 Mwaka 2021 lengo ambalo halijafikia na bado uzalishaji ni mdogo hivyo kuongeza uzalishaji linapaswa kuwa jambo la haraka iwezekanavyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akikagua namna Kahawa inavyohifadhiwa tayari kwa kuingia sokoni.

Katibu Mkuu Alimuelekeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa Kahawa na uhamasishaji Masoko Kufanya Utafiti ili kubaini nini chanzo cha uzalishaji mdogo wa Kahawa iwapo wananchi kutotunza vizuri kahawa yao, Hali ya hewa na udongo au mbegu sio nzuri zinazotumika.

Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inajipanga kwa kampeni kubwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kufahamu umuhimu wa kulima kwa wingi mazao ya Chakula na Biashara ikiwemo zao la Kahawa.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo, Alisema miongoni mwa sababu ambazo huchangia uzalishaji mdogo katika mazao mbalimbali nchini huwa ni pamoja na Wananchi kuchanganya mazao wakati wa kupanda jambo ambalo sio rafiki sana katika Kilimo, sambamba na Kutoacha nafasi kati ya mche na mche.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza na wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazo.

Mhandisi Mtigumwe aliitaka Bodi ya Kahawa Kufanya Utafiti wa maeneo ambayo Kahawa inastawi kwa wingi ili kuongeza sehemu za kuzalisha Kahawa kufikia uzalishaji wa kiwango kikubwa tofauti na ilivyo hivi sasa.

Hata hivyo amesema kuwa atazishughulikia haraka iwezekanavyo Changamoto za Uzalishaji, Changamoto za Ubora, Changamoto za Masoko sambamba na Changamoto za Sekta.

Majukumu ya Bodi ya Kahawa ni pamoja na usimamizi wa sheria namba 23 ya marekebisho yake ya Mwaka 2009 na kanuni za Kahawa 2013 sambamba na kuratibu Majukumu shirikishi (Shared Functions) Baina ya serikali na wadau.
Muonjaji katika Maabara ya Kahawa Bi Regina Mushi Daud akiendelea na majukumu yake katika maabara ya Kahawa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu/Mkurugenzi wa Ubora wa kahawa na uhamasishaji masoko Kutoka Bodi ya Kahawa akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe namna wanunuzi wanavyokabiliana katika ununuzi wa Kahawa
Picha ya pamoja wafanyakazi wa Bodi ya Kahawa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.

VIJANA 120 KUTOKA NCHI MBALIMBALI BARANI AFRIKA KUHUDHURIA KONGAMANO LA VIJANA NA UONGOZI JIJINI DAR

$
0
0
JUMLA ya vijana 120 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, wanatarajiwa kuhudhuria kongamano la vijana viongozi, litakalofanyika kuanzia Novemba 15 hadi 17 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo lililoandaliwa na kuratibiwa na Shirika la Open Society Initiative For Eastern Africa(OSIEA) kwa kushirikiana na Shirika la Mulika Tanzania, litawakutanisha vijana hao na kuweza kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana wa bara la Afrika huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Waleavu, Antony Mavunde.
 
Akizungumza na waandiishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Ofisa Program Msaidizi wa OSIEA, Adam Antony, alisema kogamano hilo ni mara ya pili kufanyika baada ya lile la mara ya kwanza kufanyika mwaka jana na kushirikisha nchi za Afrika Mashariki pekee.

Antony alisema katika mkutano huo,vijana hao watakaohudhuria ni pamaoja na wale ambao tayari wameshaanzisha biashara  na miradi mbalimbali huku wengi wakiwa kutoka nchini Tanzania.

“Pia tunategemea kuwa na vijana ambao walishawahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali zao  ambao wataweza kutoa shuhuda  mbalimbali za namna walivyoweza kufanikiwa katika kazi zao kama moja ya kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa vijana ambao ni viongozi kwa sasa,”alisema Ofisa huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mulika Tanzania, Hussein Melele, alisema mada zitakazozungumziwa katika kongamano hilo ni pamoja na nafasi ya vijana kufikia Afrika tuitakayo(Agenda 2063), vijana kushirikishwa katika ngazi za maamuzi kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.

Jingine ni kujadili masuala ya rasilimali zinazopatikana Afrika na namna zinavyoweza kuwasaidia vijana katika kujiletea maendeleo kwa mmojammoja na jamii kwa ujumla.

Matarajio baada ya kufanyika kwa kongamano hilo, Melele alisema ni kutokana na kongamano hilo kuwakutanisha vijana viongozi na wadau wa maendeleo , mashirika ya kitaifa, mabalozi na wanataaluma ni wazi kwamba baadaye  wataweza kuwaonesha njia ya namna gani wataweza kufanya nao kazi pamoja.

“Aidha kongamano hili litakuwa ni daraja kwa vijana hawa kuweza kutatua changamoto katika sekta mbalimbali hususani zinazowahusu vijana wenyewe ikiwemo za afya, ajira, uongozi, elimu, biashara na mengineyo,”alibainisha Mkurugenzi huyo.

ANSAF YAISHAURI SERIKALI KUONGEZA MAAFISA UGANI KWENYE HALMASHAURI

$
0
0
NA KAROLI VINSENT
SERIKALI imeshauriwa kuwaongeza Maafisa Ugani kwenye halmashauri mbalimbali nchini ili waweza kumsaidia  Mkulima  aweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi .
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo (ANSAF), Audax Rukongwe wakati wa mkutano uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Kilimo kujadili kuhusu huduma za Ugani kwa kulima ili ziendane na shughuli ya Viwanda hapa nchini.

Amesema  kitendo cha sasa cha kumtumia Afisa Mgani mmoja katika Kijiji kimoja  ni kitendo ambacho hakiwezekani katika kumsaidia Mkulima.
“Afisa Ugani katika Kijini Kimoja, ni kitu hakiwezekani,maana leo tunasema tuna kijiji kimoja na kesho tukawa na vijiji ishirini hivyo itashindikana kwa afisa Ugani huyu kufanya kazi kwenye vijiji vyote, ni vema serikali ikaliangalia hili”Amesema Rukongwe.

Amesema  kutokana na hali ilivyo ya uchache wa Maafisa Ugani kunahaja ya sekta binafsi kuwekeza kwenye utoaji wa Huduma ya  Ugani kwa Wakulima  ili iwe rahisi kwa Mkulima kusaidika.


“Sasa kuna haja sekta binafsi kuwekeza kwenye kutoa huduma ya Ugani  kwa wakulima ili waweze kulipia kwa kiasi husika cha fedha, kwa mfano kwa wale wakulima wafugaji kama Ngome anaumwa Nyumbani hanahaja ya kumsubili aje Afisa Ugani bali anamtafuta Afisa ugani  wa Sekta Binafsi anampa hela anamsadia “Amesema Rukongwe. 
Kwa Upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokine (SUA)Dk Sizya Lugeye ambaye ni miongoni wa wadau hao katika mkutano huo, ameishauri serikali kuhakikisha wanawaongezea nguvu za maafisa Ugani waliopo ikiwemo kuwapata fedha pamoja vitendea kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanizi zaidi katika kuwahudumia wakulima.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la wadau wa Kilimo, Audax Rukongwe akizungumza na Waandishi wa habari leo wakati wa Mkutano wa wadau wa Kilimo ili kujadilia masuala mbalimbali yanahusu Kilimo.

RC WANGABO ASIFU KIKUNDI CHA KINAMAMA KINACHOJISHUGHULISHA NA UJENZI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesifu kikundi cha kinamama wanaojishughulisha na kazi za ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi alipofanya ziara  kwenye ujenzi wa kituo cha afya Nkomolo wilayani humo.

Amesema kuwa serikali itaendelea kutoa ajira kwa vikundi mbalimbali kwa makundi yote ya wanawake na vijana wanaojishughulisha na ujenzi kutokana na kuwa na miradi mingi inayohitaji ujuzi wao na kuwaasa wanawake na vijana waige mfano huo ili waweze kujishughurisha kuliko kukaa vijiweni na kuendelea kuilaumu serikali.

“Nimependezwa na ujasiri wa hawa kina mama ambao sikutegemea kuwaona hapa, kwa namna wanavyofanya kazi nimefarijika sana, itabidi na wanawake wengine wanaokaa majumbani waige mfano wao kuliko kukaa tu na kusubiri kuletewa,” Alibainisha.

Ujenzi huo unaofanywa kwa mradi wa kuboresha vituo vya afya 172 nchini kwa fedha zilizotolewa na Wizara ya OR – TAMISEMI zilizochangwa na wadau wa maendeleo duniani wakiwemo benki ya dunia na wengineo.

Kwa upande wake mmoja wa wanawake hao Salome Sululu amethibitisha kuwa wamekuwa wakifaidika kwa kibarua hicho walichokipata na fedha wanazopatiwa kuwa zinawasaidia kujikimu katika familia na kuwawezesha kupata mitaji ya kujiendeleza kwenye kilimo na kusifu utaratibu wa serikali wa kuajiri vibarua wa maeneo husika bila ubaguzi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akipata maelezo kuoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hya Wilaya ya Nkasi Julius Kiondo.
Kinamama wakijishughulisha katika ujenzi wa kituo cha afya Nkomolo wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.

KAMPUNI YA TATU MZUKA IKISHIRIKIANA NA NAIBU WAZIRI MAVUNDE WAKABIDHI MATOFALI 3000 NA MIFUKO YA SARUJI 100 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ZA MSINGI MPYA ZA MBANDE NA MUUNGANO MKOANI DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde  mwishoni mwa wiki amekabidhi matofali 3000 na mifuko ya saruji 100 katika Kata ya Makutupora kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa Shule za Msingi Mpya za Mbande na Muungano Wilaya ya Dodoma mjini mkoani Dodoma.

Msaada huo alioukabidhi umetoka kwa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka  ambayo ilikabidhi zawadi kwa washindi katika droo ya michezo hiyo,Mavunde aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza zaidi ili kusaidia kuboresha Elimu nchini.
 
Waziri Mavunde alisema kuwa ujenzi wa shule hizo utasaidia kupunguza adha inayowapata wanafunzi kutembea umbali mrefu  wa zaidi ya kilomita 7 kufuata shule katika eneo la Veyula.
 "TATU MZUKA kwa ushirikiano na  Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh.  Anthony Mavunde  (Mbunge Dodoma Mjini) wakikabidhi  matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa mmoja wa viongozi katika kata ya Makutupora  kwa ajili ya ujenzi  wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande. Kwa ajili  ya ujenzi wa madarasa mawili  kila moja.
  "TATU MZUKA kwa ushirikiano na  Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh.  Anthony Mavunde  (Mbunge Dodoma Mjini) wakiwashukuru baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa kata ya Makutopora mara baada ya kukabidhi  matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi  wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoka kijiji cha Makutopora na Mbande kushuhudia tukio la makabidhiano ya matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande,iliyotolewa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka ikishirikiana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde.



MAGAZETI YA JUMATATU LEO NPVEMBA 13,2017

Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images