Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

DK. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WAWILI (UJERUMANI NA CHINA) OFISI KWAKE MJINI DODOMA LEO KUHUSU MAENDELEO YA UHIFADHI NA UTALII NCHINI

0
0
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akisalimiana na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Wächter ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika kuendeleza Uhifadhi na Utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Wächter (kushoto) ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika kuendeleza Uhifadhi na Utalii nchini. 
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Wächter (katikati) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika kuendeleza Uhifadhi na Utalii nchini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa China nchini, Bi. Wang Ke ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo amemuomba kushirikiana na Wizara yake kuweka mkakati wa pamoja wa kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipokea zawadi ya taswira la Ua la Taifa la China kutoka kwa Balozi wa nchi hiyo nchini, Bi. Wang Ke ofisini kwake mjini Dodoma leo. Amemuomba balozi huyo kushirikiana na Wizara yake kuweka mkakati wa pamoja wa kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Balozi wa China nchini, Bi. Wang Ke alipotembelewa na balozi huyo ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo amemuomba kushirikiana na Wizara yake kuweka mkakati wa pamoja wa kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China.  (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii).

Wafanyakazi HESLB waaswa kuwa wabunifu

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amewataka wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuongeza ubunifu ili kuondokana na changamoto wanazokutana nazo.

Prof. Mdoe amesema hayo leo (Jumatatu, Novemba 13, 2017) alipokua akiongea na Menejimenti ya HESLB katika ziara aliyoifanya katika makao makuu ya HESLB jijini Dar es Salaam.

“Pamoja na mafanikio mnayoyapata hasa katika ukusanyaji wa mikopo lakini bado kuna changamoto…zikiwemo za malalamiko ya vigezo vya utoaji mikopo ambavyo mnahitaji kuwa wabunifu kwa kuwashirikisha wadau,” amesema kiongozi huyo katika ziara yake ya kikazi.

Kwa mujibu wa Prof. Mdoe, nia ya Serikali ni kuona malalamiko yote ya wadau yanatafutiwa ufumbuzi kwa haraka, na ili hilo litimizwe ni muhimu kwa wafayakazi wa taasisi za umma kuwa wabunifu zaidi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akiongea na menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). Keshoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu Prof. Sylvia Temu na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru. (Picha na HESLB) 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). Keshoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu Prof. Sylvia Temu. (Picha na HESLB) 
Baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya Bodi ya Mikopo katika mkutano na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ambaye amefanya ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). (Picha na HESLB) .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TUME YA UCHAGUZI YAKUTANA NA VYAMA VYA SIASA KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO

0
0
Hussein Makame-NEC.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistolces Kaijage amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili ya Uchaguzi.

Jaji Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa NEC na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kuelekea Uchaguzi mdogo wa madiniwa.Alisema iwapo ukiukwaji au uvunjaji wa Maadili  hayo utatokea, Chama au Mgombea awasilishe malalamiko hayo mbele ya Kamati husika ili ishughulikiwe kisheria.

Aliwakumbusha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 53 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Tume inayo mamlaka ya kuruhusu kuwepo kwa Kampeni za Uchaguzi katika maeneo ya Uchaguzi na siyo Mikutano ya Vyama vya Siasa. Hivyo, kampeni hizo zifanyike kwenye Kata husika na inategemewa kuwa Mikutano ya Kampeni italenga kuwashawishi, kwa namna ya kistaarabu, wananchi wa Kata husika ili wamchague Mgombea anayefanyiwa kampeni. 

” Kwa mujibu wa kipengele cha 2.1. (c) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 tunategemea kila Chama cha Siasa kiendelee kufanya Kampeni kwa mujibu wa ratiba. Kampeni zote zinatakiwa kuanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni” alisema Jaji Kaijage. 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa kwenye mkutano wa Tume na vyama hivyo ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Novemba 26, 2017. Mkutano huo umeliofanyika leo jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Jaji  Mst. Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Ramadhani akitoa mada kwa viongozi wa vyama vya siasa wakati Tume ilipokutana na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam leo. 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (wa tatu kulia) akiwa meza kuu na Makamu Mwenyekiti Jaji Mst. Hamid Mahmoud Hamid( wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani )wa pili kulia), Makamishna wa NEC Jaji Mst. Marry Longway na Asina Omari na kulia ni Mwakilishi wa Mkuuu wa Jeshi la Polisi (IGP), kwenye mkutano wa Tume na vyama vya siasa uliofanyika Dar es Salaam jijini leo.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage kwenye mkutano wa Tume na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

JUKWAA LA AFYA LA DICOTA LAFANA, GREENBELT, MARYLAND

0
0

Meza kuu kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Mhe. Wilson Masilingi, Naibu Waziri wa afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman,Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, Balozi Anisa  Mbega, Bi.Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) !, Bwn. Assenga kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. wakifuatilia jukwaa la afya lililoandaliwa na DICOTA katika kuwakutanisha wadau wote nje na ndani ya Marekani sekta ya afya kuwatambua na kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika sekta hiyo nchini Tanzania. Jukwaa la afya lilifanyika siku ya Jumamosi Novemba 11, 2017 Martins Crosswind Greenbelt, Maryland nchini Marekani. Picha naVijimambo Blog na Kwanza Production
Bwn. Lunda Asmani akiwakaribisha wadau wote na kufungua jukwaa la afya.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akisoma hotuba yake kwenye kongamano la Afya lililofanyika siku ya Jumamosi Nov 11, 2017 Greenbelt, Maryaland nchini Marekani. Katika hotuba hiyo aliwashukuru DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo la wadau wa afya kwa kuthamini kazi kubwa inayofanywa na wadau hao na jitihada binafsi zinazofanywa kwa kusaidia ndungu zao nyumbani Tanzania pia alisema Rais Dkt John Pombe Magufuli anatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora kwa nchi yao.
Balozi wa African Union nchini Marekani, Mhe.Arikana Chihombori Quao akichangia kwenye jukwaa hilo na kueleza changamoto nyingi nchi za Afrika inazopata katika sekta hiyo kutokana na miundo mbinu kuwa duni na sababu kubwa inachangiwa na wakoloni walivyoligawa bara la Afrika na kuwa nchi mbalimbali kwa kuogopa nguvu ya Afrika na utajiri wake usije ukaongoza Dunia.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman akiwashukuru Diaspora kwa mchango mkubwa kwa sekta ya afya Zanzibar na baadae kutoa salamu za Rais wa Zanzibar Mhe. Dr Ali Mohamed Shein kwa kutoa shukurani zake na kuthamini mchango mkubwa wa Diaspora hasa katika sekta ya Afya.

WAZIRI MPINA ATOLEA UFAFANUZI UCHOMAJI WA VIFARANGA

SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI

0
0

Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma

Serikali imerejesha hati ya  Kiwanja Namba 9331 kilichopo kitalu namba 91 Msalato Dodoma kwa mmiliki wake halisi Bw. Sagaf Omari na Bi Madina Hassan ambao ni wamiliki halali wa kiwanja hicho kilichouzwa kwa Bw. Lucas Mlay  wa Jijini Dar es Salaam kwa shilingi milioni 35  kwa njia zisizo halali.


Akizungumza wakati akimkabidhi hati hiyo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa kiwanja hicho  chenye ukubwa wa takribani hekta mbili na nusu kiliuzwa bila mmiliki halali wa kiwanja hicho kuwa na taarifa kupitia kwa wanasheria wasio waaminifu waliosaidia kutaka kufanikisha wizi wa kiwanja hicho.



“Niwatahadharishe Mawakili wote na wanasheria ambao wanashirikiana na watu wasio waaminifu kutaka kudhulumu viwanja vya wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawachukuliwa hatua kali za kisheria na kwa kuanza tutaanza na hawa mawakili waliofanikisha mchezo huu wakumdhulumu mama huyu na mume wake kiwanja chao wanachomiliki kihalali” Alisisitiza Lukuvi



Akifafanua Waziri Lukuvi amesema kuwa Wizara yake imejiridhisha kuwa nyaraka zilizowasilishwa ili kubadilisha umiliki wa kiwanja hicho ni za kughushi na  wamiliki halali wa kiwanja hawakuwa na taarifa kuhusu kuuzwa kwa kiwanja chao hadi walipopata taarifa kwa majirani na kuamua kuchukua hatua kwa kuwasilisha malalamiko yao katika Ofisi yake.




MKUCHIKA APONGEZA MCHANGO WA TASAF KATIKA KUPAMBANA NA UMASIKINI NCHINI.

0
0
NA ESTOM SANGA- DODOMA

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa George Huruma Mkuchika amesema serikali itaendelea kuunga mkono mchango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kutatua kero zinazowakabili wananchi katika kupambana na umasikini ili vita hiyo iwe endelevu .

Mheshimiwa Mkuchika amesema jambo muhimu kwa TASAF ni kuhakikisha kuwa walengwa wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wanafikiwa na kunufaika na huduma za mfuko huo huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili mema katika utendaji kazi wa wadau wote wanaohusika na utekelezaji wa Mpango huo .

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF zilizowasilishwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga mjini Dodoma, Waziri Mkuchika ameuagiza uongozi wa TASAF kuhakikisha kuwa unawatumia kikamilifu Maafisa maendeleo ya Jamii walioko katika maeneo mbalimbali nchini kuhamasisha shughuli za maendeleo na kupambana na umasikini.

“tunao maafisa maaendeleo ya Jamii nchini kote,lakini nina wasiwasi na namna wanavyotumiwa katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,naagiza TASAF mtumie vizuri hazina hiyo ya wataalamu katika utendaji kazi wenu” ameagiza Waziri Mkuchika.

Aidha Waziri huyo ameitaka menejimenti ya TASAF kuhakikisha kuwa inaandaa mipango thabiti katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kipindi kirefu huku akisisitiza kuwa walengwa wa Mpango huo wanapaswa kuwekewa mazingira yatakayowawezesha kujitegemea hata baada ya kuondolewa kwenye shughuli za Mpango.

Akitoa taarifa ya utekelezaji,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mfuko huo umeendelea kuwajengea msingi wa kujitegemea walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini nchini kote,kazi ambayo amesema imefanyika kwa mafanikio makubwa.

Walengwa wengi hivi sasa wameweza kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwenye maeneo yao huku akitaja mafanikio makubwa katika utekelezaji wa masharti ya elimu na afya kwa walengwa jambo ambalo amesema linaendelea kusaidia juhudi za serikali za kupambana na adua ujinga na maradhi.

“Kumekuwa na mwitikio mkubwa katika kuwapeleka watoto kutoka kaya masikini kupata elimu na huduma za afya, kwani hayo ni miongoni mwa masharti ya Mpango, na hyo kwetu ni mafanikio makubwa” amesisitiza Bwana Mwamanga.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mfuko huo kwa sasa unakabiliwa na changamoto ya kufikia takribani asilimia 30 ya vijiji ambavyo havikufikiwa katika awamu inayokaribia kukamilika, hivyo jitihada zaidi zinafanywa ili kupata fedha za kukamilisha vijiji hivyo katika awamu itakayofuata.
 Mheshimiwa Mckuchika akitazama nakala za vipeperushi,taarifa na majarida yenye taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF,Ofisi kwake mjini Dodoma. 
 Waziri Mkuchika (aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na Utumishi wa Umma ,baada ya kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF ofisini kwake mjini Dodoma, aliyevaa Kaunda suti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Mhe. George Mkuchika (aliyevaa tai nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislau Mwamanga,ofisi kwa Waziri mjini Dodoma.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 13.11.2017


WACHIMBAJI WADOGO NYARUGUSU WAJITOLEA KUJENGA MADARASA

0
0
NA CONSOLATA EVARIST,GEITA.
Wachimbaji wadogo kwenye Kata ya Nyarugusu na Serikali ya kijjiji na kata  hiyo wameshirikiana kuchangia ujenzi wa madarasa manne na ofisi 2 za walimu kwenye Shule ya Msingi Tologo iliyoezuliwa na upepo na kubaki darasa moja.
Akizungumza na mkuu wa wilaya ya Geita , wakati alipokwenda kujionea shughuli na jitihada ambazo zinafanywa na wachimbaji wadogo za kuboresha miundo mbinu ya elimu,Bw Evarist Pascal alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa hali ambayo ilisababisha wanafunzi kusomea madarasa ambayo yalikuwa yameezuliwa na mvua walionelea ni vyema wakichangia ujenzi huo hili  watoto wapate sehemu nzuri ya kujisomea.
Hata hivyo ameendelea kutaja kuwa ujenzi wa madarasa hayo pamoja na ofisi za walimu umegharimu kiasi cha  Sh, Milioni 56.
Aidha ameendelea kusema kuwa  kitongoji cha Tologo kinakabiliwa na upungufu wa zahanati ya mama na mtoto kwa kuwa ipo zahanati moja ya Boko ambayo imeelemewa na kwamba ili kuchangia ujenzi huo wametengeneza madirisha 11 na kufyatua matofali elfu 3
Kutokana na juhudi ambazo wamezifanya Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewapongeza wachimbaji hao na ameahidi kushirikiana nao ili kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo .
Madarasa ya shule ya msingi ya  Tologo ambayo yamejengwa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.
Evarist Pascal  ambaye ni mchimbaji mdogo akitoa maelezo kwa mkuu wa Wilayaya Geita(ambaye yupo katikati)shughuli za ujenzi na ghalama ambazo zimetumika kujenga madarasa hayo.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akishukuru kwa kazi ambayo imefanywa na wachimbaji wadogo wa kata ya Nyarugusu Wilayani humo.

Madarasa ya shule ya msingi ya  Tologo ambayo yamejengwa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.

Diwani wa Kata ya Nyarugusu,Swalehe Juma akielezea na kuonesha darasa ambalo bado halijakamilika.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl,Herman Kapufi pamoja na viongozi wa kijiji na kata na wachimbaji wakitoka kwenye eneo la shule.




MAGAZETI YA JUMANNE LEO NOVEMBA 14,2017

Dua ya mama Hidayat bint msemo kufanyika Muslim Resource Centre Red lane, Coventry, UK

0
0
Kufuatia kifo cha mama yetu mpenzi Hidaya bint Msemo ambae ni mama yake mzazi sheikh Ahmad Muhammad Suleiman (Mashaka) na ni mama yake mkuu Sheikh Ally bin Asili, tunawaomba ndugu zetu tujumuike pamoja kwa ajili ya kumuombea dua mama yetu Allah amfanyie wepesi ktk safari yake. Dua ambayo itajumuisha kina baba na kina mama, itafanyika siku ya Jumamosi sawa na tarehe 18/11/2017 saa kumi jioni kwenye ukumbi wa:
Muslim Resource Centre
Red lane, Coventry
CV6 5EE
United Kingdom
Shughuli itaanza baada ya swala ya maghribi ambayo inaswaliwa saa kumi na robo. Ni muhimu kufika kwa wakati.
Kwa mawasiliano na maelezo Zaidi wasiliana na 
Sheikh Ali Asili,  07397565541
Sheikh Muhammad Hassan, 07438566797
Kufika kwako ndio mafanikio ya shughuli yetu. 
Nyote mnakaribishwa.
والله ولي التوفيق

WAZIRI KALEMANI AKUTANA NA WAWEKEZAJI UMEME WA SUMAKU

0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amekutana na wawekezaji wenye nia ya kuzalisha umeme nchini kwa kutumia teknolojia mpya ya sumaku. Alikutana na wawekezaji hao Novemba 13, mwaka huu Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.
Baada ya kuzungumza na Waziri, wawekezaji hao kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited ya Ujerumani, walifanya majadiliano na wataalam wa nishati kutoka wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Wawekezaji hao walitakiwa kuwasilisha Andiko la Awali (concept note) la Mradi wao ili lipitiwe na kujadiliwa na wataalam husika, kabla ya kuendelea na hatua nyingine stahiki za uwekezaji nchini. 
 Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika kikao na wawekezaji kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited ya Ujerumani (kulia). Kushoto ni maafisa wa Wizara, TANESCO, REA na EWURA.

 Mwekezaji kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited ya Ujerumani, Colin Cloete akiwasilisha mapendekezo ya kuzalisha umeme kwa teknolojia mpya ya sumaku, mbele ya Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani na wataalam wa sekta hiyo kutoka Wizarani, TANESCO, REA na EWURA.
 Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani (kushoto), akifafanua jambo kwa wawekezaji kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited, wakati wa kikao baina yao kilichofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani akiagana na wawekezaji kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited, waliofika wizarani kuwasilisha mapendekezo ya kuwekeza nchini kwa kuzalisha umeme unaotumia teknolojia mpya ya sumaku. 

INTRODUCING NEW SINGLE "NIMEMUELEWA" BY NAS B

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba na Balozi wa China nchini Mhe. WANG Ke wakifuarahia jambo walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Mjini Dodoma.Naibu Waziri amemuhakikishia Mhe.Balozi WANG Ke kuwa Wizara na Serikali wataendelea kudumisha uhusiano wa kahistoria uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China. Pia Mhe. Dkt. Kolimba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa kufadhili miradi mbalimbali hapa nchini 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba na Balozi wa China nchini Mhe. WANG Ke wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo 

2018 SADC SECONDARY SCHOOL ESSAY COMPETITION

0
0




N:B All applicants are requested to send their applications to the following address:
    
         Permanent Secretary
         Ministry of Education,  Science and Technology
         Block 10,
         College of Business Studies and Law,
         University of Dodoma,
         P.O.Box 10
         DODOMA


Bodi ya DAWASCO yaridhishwa na uwekezaji sekta ya Maji

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco , Mhadisi Cyprian Luhemeja akifafanua jambo wakati wa ziara ya kikazi ya bodi mpya ya Dawasco katika mitambo mikubwa ya uzalishaji na usamabazaji Maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu iliyopo Mkoani pwani.

Bodi mpya ya Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), imeridhishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika sekta ya Maji ya kuhakikisha kuwa hadi kufikia 2020 tatizo la Maji linakwisha kabisa katika Miji mbalimbali nchini hususani katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kutokana na mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu juu na Ruvu chini kuwa ya Kisasa na yenye uwezo mkubwa wa kuhudumia mikoa hiyo.

Bodi hiyo mpya ya DAWASCO imeshuhudia uwekezaji mkubwa kwenye miradi hiyo, na kuridhishwa na kazi inayofanywa na shirika hilo mara baada ya kutembelea mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu iliyopo Mlandizi, Pamoja na Bagamoyo Mkoani Pwani, ambapo lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea namna ambavyo serikali imejikita katika kuhakikisha inamaliza tatizo la Maji lililopo nchini na linamtua mama ndoo ya Maji Kichwani.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya DAWASCO, Prof. Tolly Mbwete amepongeza jitihada zilizofanywa na serikali za kuwekeza katika sekta ya Maji, pia wameridhishwa na kazi kubwa zinazofanywa na DAWASCO pamoja na DAWASA za kuhakikisha wakazi wote wa Dar es salaam na Pwani wanapata huduma bora ya Majisafi hasa wale ambao bado maeneo yao hayajafikiwa na miundombinu ya huduma ya Majisafi.
 "Tumeona kazi kubwa na nzuri inayofanywa na DAWASCO na DAWASA, tumejionea namna ambavyo serikali imewekeza katika sekta hii ya Maji, na namna ambavyo kazi kubwa ya kutibu, kusafisha na kusafirisha Maji inavyofanyika hadi hatua ya kumfikia mlaji, hakika sio kazi nyepesi, inahitaji nguvu na kujituma zaidi ili watu wote waweze kupata huduma bora” alisema Prof. Mbwete. Pia, wajumbe wengine wa bodi hiyo,Wamefurahishwa na namna ambavyo taasisi hizo zinavyofanya kazi ya uzalishaji na utibuji Maji kwa ufanisi na utaalamu wa hali ya juu.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema kuwa ziara ya bodi ya DAWASCO imekuja wakati mwafaka ambapo Shirika hilo lipo katika kupambana pamoja na kumaliza tatizo la upotevu wa Maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani. Aidha, ameeleza kuwa maeneo mengi ambayo yalikuwa na changamoto ya huduma ya Majisafi kwa sasa yanapata huduma hiyo, hasa katika maeneo ambayo yapo pembezoni mwa barabara ya Morogoro kuanzia Mbezi, Kimara, Ubungo pamoja na maeneo mengi ya Tabata kwa sasa wanapata huduma ya Majisafi, hasa baada ya kukamilika kwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu.

“Mitambo hii ya Ruvu juu na Chini ina hudumia sehemu kubwa ya Jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa Pwani, hivyo kutokana na upanuzi uliofanyika katika mitambo hii maeneo mengi sasa yanapata huduma Majisafi ya kutosha na hata yale maeneo yaliyokuwa na changamoto kutokana na miinuko, sasa yanapata huduma”. alisema Mhandisi Luhemeja.

Bodi ya DAWASCO iliyozinduliwa mapema na Mh Waziri wa Maji ,Mh Isack Kamwele mapema wiki hii imekuwa ni bodi ya Tano tangu shirika hilo kuanza majukumu yake ya kuzalisha na kusambaza Maji katika Mkoa wa Dar es salaam pamoja na miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani pwani ambapo itakuwa chini ya Mwenyekiti wake Profesa Tolly Mbwete..

VIT University strengthens ties with SUZA

0
0

The VIT University of Vellore, India and the State University of Zanzibar (SUZA) have taken a major step in furthering their ties through the collective signing of two addenda to the Agreements of Cooperation on the Bachelor Programme in Multimedia and Animation and Bachelor Programme in Computer Science.  This event was held at Tunguu Campus on Monday 13th November, 2017.
Dr. Govindasamy Viswanathan, the Founder and Chancellor of VIT University who signed the Agreements on behalf of his university has expressed his institution’s readiness and determination in maintaining concrete relations with SUZA. 
 Prof. Rai and Dr. Viswanathan sign addenda to the Agreements of Cooperation being witnessed by other officials and students.
 Dr. Viswanathan who was accompanied by Dr. C. Vijaykumar, the VIT University Director of International Relations said that the cooperation between the two institutions will benefit students, lecturers and officials of both universities.

 “India and Africa have so much in common and Zanzibar being part of this continent is one of the representatives, so let’s work together, as there are so many things we can benefit from each other if we collaborate,” Dr. Viswanathan insisted.
In his remarks, Prof. Rai emphasised the need for the ties; he said that it is essential for SUZA to highlight its challenges so as to be able to tackle them through collaborative efforts and viable educational programmes. “We have recently merged with other higher learning institutions of Zanzibar, the issue to proud of, so we need to use this partnership in building our capacity so as to improve the quality of education,” he added.

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE WASIOJIWEZA NA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA MKOANI SHINYANGA

0
0
 Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria Agnes Mgeyekwa akiongea na Wazee pamoja na wafanyakazi wa makazi ya wazee wasiojiweza ya Kolandoto yaliyopo katika manispaa ya Shinyanga wakati Tume ilipotembelea makazi hayo ikiwa ni sehemu ya Utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania.
 Sehemu ya wazee wa Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Kolandoto yaliopo katika Manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza katibu Msaidzi Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Agnes Mgeyekwa.
 Mkuu wa Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga Bi. Sophia Kang’ombe akisisitiza jambo wakati Tume ya Kurekebisha Sheria ilipotembelea makazi hayo wakati wa utafiti wa Mfumo wa Kisheria wa Huduma za Ustawi wa Jamii nchini.
 Mhadhiri Msaidizi kutoka chuo cha Ustawi wa Jamii Bw. Paul Mwangosi akizungumza wakati Tume ya Kurekebisha Sheria ilipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza  ya Kolandoto.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MCHEZO WA GOLF NCHINI

0
0
Na Lorietha Laurence- WHUSM, Arusha.
Serikali imeahidi kushirikiana kwa ukaribu na wadau wa mchezo wa Golf nchini katika kuhakikisha mchezo huo unafundishwa kuanzia ngazi ya chini ili kuandaa wachezaji bora wa kimataifa wataoiwakilisha nchi katika mashindano hayo duniani.
 Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akifunga mashindano ya Kili Golf Mkoani Arusha ambapo ameeleza kuwa mchezo huo ni wa muhimu  ukazingatiwa katika kukuza sekta ya michezo.
“Mchezo huu wa Golf ni mzuri sana kwa kuwa unakusanya watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaleta pamoja nami naahidi kuwa Wizara yangu itahakikisha inashirikiana kwa karibu na wadau wa Golf nchini ili kuukuza zaidi” amesema Mhe. Dkt. Mwakyembe.
Mhe. Dkt. Mwakyembe ameongoza kwa kuwataka washiriki wa mchezo huo kuwa mabalozi wazuri katika kuutangaza mchezo huo ndani na nje ya nchi na kuhamasisha vijana wengine kuwa na moyo wa kujifunza.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa amewasili katika Viwanja vya Kili Golf Jumapili Mkoani Arusha  kwa ajili ya kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf Kulia ni Katibu Wake Bw. Andrew Magombana na kushoto ni Bw. Chris Martin Makamu wa Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union).
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kili Golf Bw. Bastiaan Bruins (Kushoto) baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa  ajili ya kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf katikati ni  Makamu wa Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union) Bw. Chris Martin.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na waandaji wa mashindano ya Wazi ya Kili Golf Mkoani Arusha.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akitoa risala kwa washiriki wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf katika halfa ya kufunga mashindano hayo jana Mkoani Arusha.
 Mshiriki kutoka Kenya Bw. Edwin Mudanyi  akijiandaa kupiga mpira wakati wa fainali wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani Arusha ambapo  jumla ya washiriki 250 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Zambia, Afrika ya Kusini na Tanzania walishiriki.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe  akimpa mkono wa hongera mmoja wa washindi wa kwanza Bw. Victor Joseph kutoka Tanzania baada ya kumalizika kwa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani Arusha.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAKULIMA WA KANDA YA ZIWA KUFIKIWA KUPITIA KONGANE

0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo kwa wakulima wa kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla ili kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.

Dhamira hiyo imewekwa wazi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila wakati akitembelea miradi mbalimbali ya kilimo mkoani Mwanza hivi karibuni.

Bibi Kurwijila alisema kuwa katika kutekeleza mkakati wa kuwafikia wakulima wengi zaidi nchini Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imejipanga kutoa huduma kupitia kongane mpya nane (8) ili kuongeza tija kwa wakulima nchini.

“Kongane ni njia ya kimkakati ya kijiografia yenye kujikita katika shughuli za kilimo zinazohusiana, wasambazaji, na taasisi zinazohusishwa katika kujenga usawa wa moja kwa moja miongoni mwa wadau, hivyo ili kukidhi mahitaji ya wakulima nchini, benki ya kilimo itawafikia kupitia njia hii,” alisema.

Aliongeza kuwa kongane ya Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Geita na Simiyu itatoa fursa ya ushindani kwa njia endelevu ili kuchagiza uhusiano na ushirikiano katika uongezaji wa thamani hasa katika makundi mbalimbali ya minyororo ya thamani, pamoja na taasisi na mamlaka za udhibiti zinazosaidia sekta ya kilimo nchini.
 Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (kulia) akitoa maelezo juu ya uchakataji wa nyama kwenye Kiwanda hicho kwa ugeni kutoka Benki ya Kilimo. Ugeni huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kulia).
 Ugeni huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kushoto) wakiangalia namna ng’ombe anavyoandaliwa mara baada ya kuchinjwa.
 Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (wapili kushoto) akionesha soseji zilizokuwa katika hatua za ufungaji. Wanaomuangalia ni wageni kutoka Benki ya Kilimo.
 Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazosindikwa na Kiwanda cha Chobo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Joseph Mutashubilwa (wapili kulia) na Bw. Dome Malosha (kulia).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images