Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

JUKWAA LA UTU WA MTOTO LAWAJENGEA UWEZO MABINTI KUPAMBANA NA VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YAO


TAHADHARI

$
0
0
 Daraja linalounganisha Ulongoni na Gongo la Mboto, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam linaweza kukatika wakati wowote kama linqvyoonekana mapema leo,kufuatia mvua zilizonyesha na kuhamisha tuta la upande mmoja na kusababisha magari kushindwa kupita.Picha na Nyakasagani Masenza.

NHIF YAMPONGEZA RAIS DKT. MAGUFULI

TAARIFA KUHUSU UBORESHAJI WA MITAMBO YA KIBENKI

Watu 6 Mbaroni Kwa Kukutwa na Nyaya za Umeme Mali ya TANESCO

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 07/11/2017 huko maeneo ya Tegeta IPTL lilifanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T. 897 ARF aina ya FUSSO likiwa limebeba nyaya za umeme Roller/Drum 05 zikiwa ndani ya gari hilo.

Aidha dereva wa gari hilo aliwaelekeza askari watuhumiwa wenzake na baada ya upekuzi zilikamatwa Roller/drum 02, mashine ya kupaka, rangi na makopo Mmatatu (3)matupu ya rangi yaliyotumika kubadilisha uhalisia wa Roller/drum, zote zilikutwa kwa mtu aitwaye ZAWAKO KASIBA na mke wake, mkazi wa IPTL Tegeta na watuhumiwa wengine wanne.

Watuhumiwa wote wamekamatwa na mawasiliano yalifanyika na Shirika la umeme (TANESCO) na walifika kuzitambua nyaya hizo na kugundua kuwa ni mali za Shirika ambazo ni DRUM 07 zikiwa na mita 21,000 zenye thamani ya Tsh Milioni 70.7

Jumla ya watuhumiwa sita wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo akiwemo mwanamke mmoja.

Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaotuhumiwa kuhujumu miundo mbinu ya TANESCO.

WATEJA WA VODACOM NA TECNO WALETEWA PHANTOM 8 MSIMU WA SIKUKUU

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu (kushoto) na Mkuu wa maduka ya rejareja wa kampuni hiyo, Brigita Stephan (kulia) wakimsikiliza Afisa Mawasiliano wa Tecno, Eric Mkomoye akiongea na waandishi wa habari na kuwaonesha simu aina ya Tecno Phantom 8, Wakati wa uzinduzi wa simu hiyo kwa kushirikiana na  Vodacom ambapo simu hiyo inaambatana na ofa ya kifurushi cha 5GB, SMS 300 pamoja na dakika 300 kwenda mitandao yote na  inapatikana katika maduka yote ya kampuni hizo kwa bei nafuu.
 Mkuu wa matukio wa Tecno,Anuj Khosua(kushoto) Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Jacquiline Materu(wapili kushoto)na Mkuu wa maduka ya rejareja wa Vodacom, Brigita Stephan pamoja na Afisa Mawasiliano wa Tecno, Eric Mkomoye wakionesha simu aina ya Tecno Phantom 8, Wakati wa uzinduzi wa simu hizo  kwa kushirikiana na  Vodacom ambapo simu hizo zinaambatana na ofa ya kifurushi cha 5GB, SMS 300 pamoja na dakika 300 kwenda mitandao yote na  inapatikana katika maduka yote ya kampuni hizo kwa bei nafuu.
 Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Jacquiline Materu(kushoto) na Afisa Mawasiliano wa Tecno,Eric Mkomoye,wakimpongeza mwaandishi wa habari baada ya kubahatika kushinda simu aina ya Tecno Phantom 8, Wakati wa uzinduzi wa simu hizo  kwa kushirikiana na  Vodacom ambapo simu hizo zinaambatana na ofa ya kifurushi cha 5GB, SMS 300 pamoja na dakika 300 kwenda mitandao yote na  inapatikana katika maduka yote ya kampuni hizo kwa bei nafuu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Tecno wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa simu aina ya Tecno Phantom 8 ambapo simu hizo zinaambatana na ofa ya kifurushi cha 5GB, SMS 300 pamoja na dakika 300 kwenda mitandao yote na  inapatikana katika maduka yote ya kampuni hizo kwa bei nafuu.

MHISPANIA AWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA KUTUMIA BAISKELI.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

MPANDA milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal ameweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.

Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.

Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa ,za Mlima Kilimanjaro,Arusha na Saadan inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,

Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anaeleza hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Prof. Elisante Aagiza Kiwanda cha Viuadudu Kujitangaza

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel akiongoza kikao alipokutana na uongozi wa kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) katika ziara yake ya kikazi jana Wilayani Kibaha. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Ramson Mwilangali.
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kuzazilisha Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) Bw. Samwel Mziray akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya kiwanda hicho wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto) jana Wilayani Kibaha. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Joseph Rwegasira Bushweishaija
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel Profesa Elisante Ole Gabriel akisikiliza maelezo kuhusu dawa za kuulia mazalia ya mbu toka kwa Meneja wa Uzalishaji katika kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) Mhandisi Aggrey Ndunguru alipotembelea katika kiwanda hicho jana Wilayani Kibaha. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji Prof. Joseph Rwegasira Bushweishaija .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel akisoma maelezo katika chupa ndogo ya dawa za kuulia mazalia ya mbu alipotembelea kiwanda cha kuzalisha dawa hizo cha Tanzania Biotech Production Limited kilichopo Kibaha Mkoani Pwani jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Ramson Mwilangali na Mhandisi Aggrey Ndunguru.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Elisante Ole Gabriel akikagua mitambo ya kuzalishia bacteria ambayo hutumika katika kiwanda cha Uzalishaji wa Viuadudu (Tanzania Biotech Production Limited) wakati wa ziara yake jana Wilayani Kibaha mkoani Pwani. Kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho Mhandisi Aggrey Ndunguru.


SPIKA JOB NDUGAI AZUNGUMZA NA WABUNGE WALIOSHIRIKI MAFUNZO NCHINI CHINA.

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi nchini China katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea zawadi aliyopewa na Chuo Kikuu cha Guangdong  kilichopo Jijini Guangzhou China, wakati wa ziara ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China, zawadi hiyo ilikabidhiwa na kiongozi wa Msafara , Mheshimiwa. Augustino Masele (kushoto) na wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi nchini China katika tukio lililofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) wakati wa kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Msafara, Mheshimiwa Augustino Masele (kushoto) iliyotoka Chuo Kikuu cha Guangdong  kilichopo Jijini Guangzhou China, wakati wa ziara ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China, katika tukio lililofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (watatu kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji wao wa kazi nchini China katika tukio lililofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)​

DC NYASA AITUPIA LAWAMA TBA KWA KUKWAMISHA UJENZI WA OFISI YA MKURUGENZI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya NYASA ISABELA CHILUMBA amemwomba mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME kuhakikisha anaingilia kati ujenzi wa nyumba yake ,ofisi ya mkurungenzi baada ya kuonekana TBA kushindwa kuifanya kazi kwa wakati huku TBA wakida kuwa maji ndiyo tatizo licha ya kuzungukwa na ziwa Nyasa.

SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) SASA LAFIKILIA KUJA NA UTALII KWA BODA BODA NA BAJAJI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litafikiria matumizi ya Boda boda na Bajaji kwa wageni watakao hitaji kutembelea Hifadhi zake endapo yatajitokeza maombi ya kutosha kuhusu matumizi ya vyombo hivyo.

Hatua hiyo inatokana na bidhaa mpya ya Utalii wa kutumia Baiskeli iliyoanzishwa hivi karibuni katika Hifadhi za Taifa za Mlima Kilimanjaro na Arusha kuanza kuwa kivutio kwa watalii kutoka nchi mbalimbali walioanza kufanya utalii wa Baiskeli.

Miongoni mwa watali hao ni pamoja na mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal aliyeweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.

Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal aakiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia walipoianza safari ya kuelekea kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru mara baada ya kufanikiwa kufika huku akiendesha baiskeli . 
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto) na Ramon Abecia (Kulia) katika kilele cha Uhuru walipoanda kwa kutumia baiskeli .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya wageni hao kushuka baada ya kufanikiwa kufika kilele cha uHuru kwa kutumia Baiskeli.

Mkutano Wa COP 23, Utatoa Suluhisho La Kukabiliana Na Changamoto Ya Mabadiliko Ya Tabia Ya Nchi-Meya Mwita

$
0
0
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa mkutano wa COP 23 ambao Mameya na watendaji wakuu wa majiji na miji mbalimbali duniani utatoa suluhisho la pamoja la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi katika miji yao.

Akiwa Nchini Ujerumani , Meya Mwita emesema kuwa mkutano huo utakuwa mahususi kwa jiji la Dar es asalaam kupata suluhisho na kuhakikisha kuwa wanakabiliana ipasavyo na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo janga la mafuriko ambalo limekuwa ni tatizo sugu jijini hapa.

Mkutano huo unaofanyika sambamba na Mkutano wa 23 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, COP 23 inahusu miji na Taasisi zenye uhusiano na ubia na miji ya Ujerumani katika utekekezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko hayo inayofadhiliwa na Nchi hiyo.

Mkutano huo wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi umeandaliwa na Taasisi ya Engagement Global ya Ujerumani kwa miji washirika kutoka nchi mbalimbali duniani ambapo umeanza jana alasiri mjini Bonn nchini Ujerumani.

Kutoka Tanzania miji mingine inayoshiriki katika mkutano huo ni Jiji la Mwanza, Manispaa ya Zanzibar na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. 

Hata hivyo mkutano huo utaendelea hadi Novemba 11, mwaka huu ambapo jiji la Dar es Salaam linashiriki katika likiwa na ujumbe wake unao ongozwa na Mstahiki Meya Jiji hilo Mwita pamoja na Mkurugenzi Sipora Liana.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye koti jeusi , Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana wa kwanza kulia wakijadiliana jambo na ujumbe wa jiji la Hamburg katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia ya Nchini unaoendelea Nchini Ujerumani.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye koti jeusi ,akiwa na Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana wakipata chai baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya mkuanomhuo.

MSHTAKIWA SETHI AIOMBA MAHAKAMA IMRUHUSU KWENDA KUPATIWA MATIBABU YA PUTO LAKE NCHINI AFRIKA KUSINI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mshtakiwa Harbinder Singh Sethi,ameoimba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumruhusu kwenda kupatiwa matibabu ya puto lake lililoisha muda nchini Afrika Kusini kwa daktari wake maalumu kwa madai ya kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemueleza kuwa hawawezi kufanya upasuaji huo.

Maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo na wakili wake, Joseph Sungwa leo Novemba 10/2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakati shauri hilo linalomkabili Sethi na James Rugemarila lilipopelekwa kwa kutajwa na Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter na Leonard Swai kudai upelelezi haujakamilika.

Katika kesi hiyo, Sethi na James Burchard Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Akiwasilisha maombi hayo, wakili Sungwa alidai alielezwa na mteja wake kwamba baada ya kufanyiwa vipimo na Muhimbili, walimweleza hawana ujuzi wa kumfanyia upasuaji wa puto.hilo na endapo litaendelea kubaki mwilini mwake linaweza kupasuka muda wowote na kuzalisha sumu ambayo litaatarisha maisha yake na njia pekee iliyobakia ni kwa mshtakiwa Sethi kumuona daktari wake anayeishi Afrika Kusini.

“Ili mshtakiwa aweze kuja mahakamani kuudhuria kesi yake na hatimae kuweza kujitetea, tunaomba kama inawezekana aende kumuona daktari wake ambaye anaishi Afrika Kusini kwa matibabu”, alidai Sungwa.

Ombi hilo lilipingwa vikali na wakili wa serikali,Swai akidai Muhimbili haijashindwa kumfanyia upasuaji wa puto mshitakiwa huyo, bali anajicheleweshwa mwenyewe kutokana na kutaka uwepo wa daktari wake wa Afrika Kusini.

YALIYOJIRI BUNGENI MJINI DODOMA LEO NOVEMBA 10,2017

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Azzan Zungu akiingia bungeni tayari kuongoza Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Wabunge wakiwa wamesimama wakati wa dua ya kuiombea nchi na bunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Capt(Mst) George Mkuchika akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati  wa Mkutano wa Tisa wa kikao cha nne cha Bunge hilo leo Mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso akijibu hoja  mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akijibu hoja  mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Hamisi Kigwangalla akijibu hoja  mbalimbali ya wabunge wakati wa Mkutano wa tisa wa  kikao cha nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania leo Mjini  Dodoma.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mahakama yatupilia mbali maombi ya matunzo ya mtoto dhidi ya Mwanamuziki Diamond Platnum

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya Mwanamuzi Diamond Platnum.

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 10/2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa mahakama hiyo.

Hakimu Devotha alitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika kutokana na msanii Diamond kuwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto.

Katika pingamizi lililowasilishwa na Diamond mahakamani hapo anadai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.

Awali Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine alikuwa anaomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond. Mwanamitindo huyo alifungua kesi hiyo mahakamani hapo akiiomba mambo mbalimbali likiwemo la matunzo ya mtoto waliozaa na msanii huyo.

Katika kesi hiyo, Hamisa anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi. Hamisa alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Kupitia hati hiyo ya madai, mwanamitindo huyo anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Hata hivyo, Diamond aliwasilisha hati ya majibu kinzani akipinga maombi hayo ya Diamond akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi sh. milioni tano kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

RC RUVUMA AMEPIGA MARAFUKU KUMWITA MWANAFUNZI WAKIKE BABY

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewataka wafunzi wakike waliopo mashuleni kuacha mara moja tabia ya kukubali kuitwa mababy hayo yamesemwa katika ziara yake ya siku moja katika shule ya NASULI iliyopo wilayani NAMTUMBO mkoani habari kamili hii hapa video yake

WAGONJWA 15 WAFANYIWA UPASUAJI WA KUPANDIKIZA MISHIPA YA DAMU KATIKA MOYO NA KUREKEBISHA MSHIPA MKUBWA WA DAMU KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU.

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India wamefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa wagonjwa 15 katika kambi maalum ya upasuaji ya siku sita inayomalizika kesho.

Upasuaji wa moyo unaofanyika katika kambi hii ambayo imeanza Jumatatu tarehe 8/11/2017 hadi Jumamosi tarehe 11/11/2017 ni ya upasuaji wa kufungua kifua kwa watu wazima. Upasuaji uliofanyika ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting), na kubadili milango miwili hadi mitatu ya moyo (Valve Replacement).

Kwa mara ya kwanza hapa nchini tumefanya upasuaji wa kurekebisa mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic Aneurysm Repair).

Tulifanya upasuaji kwa wagonjwa watatu kwa siku, wote hawa wanaendelea vizuri na wataruhusiwa pindi afya zao zitakapoimarika. Baadhi yao ambao tumewafanyia upasuaji jana na juzi wako katika chumba cha uangalizi maalum na wengine wako wodini wameshaanza kufanya mazoezi.

Kama wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nje ya nchi Serikali ingelipia zaidi ya milioni 405 kwani gharama za mgonjwa mmoja kwenda kutibiwa nje ya nchi ni zaidi ya milioni 27. Gharama za matibabu haya hapa nchini kwa wagonjwa 15 ni milioni 225 (milioni 15 kwa mgonjwa mmoja).

Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri. Tunawashauri wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati.
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi Roberth Mallya na kushoto ni Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi Anjela Muhozya akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee Ali Ascar Beliranwalwa. 
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi Roberth Mallya na kushoto ni Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi Anjela Muhozya akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee Ali Ascar Beliranwalwa. 
Mkutano wa waandishi wa Habari ukiendelea  kuhusu kambi maalum ya upasuaji ambayo imefanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete  (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya Mjini Mumbai nchini India ambapo wagonjwa 15 wamefanyiwa upasuaji. Upasuaji uliofanyika  ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting), kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve Replacement) na kurekebisha mshipa mkubwa unaotoa damu kwenye moyo kwenda sehemu zote za mwili (Aortic Aneurysm Repair). 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi wakati alipomtembelea Waziri mkuu ofisini kwake mjini Dodoma leo Novemba 10/2017 kwa mazungumzo ya kikazi.Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera Bunge,Kazi Ajira,Vijana na Walemavu Jenista Mhagama.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfafanulia jambo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara Joyce Sokombi.(chadema) wakati wa Majadiliano ya Mapendekezo ya Mpango  wa Taifa wa Fedha kwa Mwaka 2018/2019 bungeni Dodoma leo Novemba 10/2017.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Martha Mlata (CCM) wakati wa Majadiliano ya Mapendekezo ya Mpango  wa Taifa wa Fedha kwa Mwaka 2018/2019 bungeni Dodoma leo Novemba 10/2017.

WAZAZI WAASWA KUWASOMESHA WATOTO WA KIKE

$
0
0
NA DENIS MLOWE, IRINGA

WAZAZI na Walezi wameaswa kuwasomesha watoto wa kike na kuachana na fikra potofu kuwa kumsomesha mtoto wa kike ni kupoteza rasilimali fedha kwani maisha ya sasa bila elimu ni changamoto kubwa kwa mtoto wa kike.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kenneth Komba kutoka Idara ya Elimu mkoa wa Iringa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Spring Valley iliyopo Mkoani Iringa.

Alisema kuwa mtoto wa kike akipatiwa elimu kuna uwezekano mkubwa kwa taifa kuwa na maendeleo kutokana na kuwajibika kwao katika maisha ya kila siku hivyo wazazi na walezi ni muhimu kuwasomesha watoto wa kike kwa lengo la kuendeleza ndoto walizonazo.

Alisema kuwa jukumu la kusomesha elimu ya msingi hadi sekondari ni la serikali lakini wazazi na walezi wanaosomesha shuleni hapo ni kuisaidia serikali hivyo ipo tayari kupokea changomoto zote katika shule hiyo na kushirikiana kuzitatua.

Komba aliipongeza shule ya sekondari Spring Valley kwa kuwa moja ya shule zinazofanya vizuri mkoani hapa kielimu na tabia kwani ni moja ya shule ambazo idara ya elimu haipati malalamiko ya mara kwa mara kutoka shuleni hapo.
 Wanafunzi wa shule ya wasichana ya Spring valley wakicheza muziki katika sherehe za kumaliza kidato cha nne
 wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Springa Valley wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Spring Valley iliyoko katika manispaa ya Iringa wakiwa katika mafunzo ya vitendo shuleni hapo.

WARSHA YA WANACHAMA WA UMOJA WA POSTA AFRIKA KWA NCHI ZINAZOZUNGUMZA KIINGEREZA YAFANYIKA JIJINI ARUSHA NOVEMBA 6 HADI 8, 2017

$
0
0
WARSHA ya Kimataifa ya wanachama wa Umoja wa Posta Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza, imefanyika jijini Arusha, Tanzania ikizishirikisha nchi mbalimbali barani Afrika.

Katika warsha hiyo, ijulikanayo kama ‘operational readness for e-commerce,’ ilianza Novemba 6 na kumalizika Novemba 8, 2017, Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete, aliwataka kuwa na utayari wa kibishara ili waweze kuendana na mabadiliko ya tekinolojia.

"Tukiongeza ubunifu wa kufanyakazi kwa mbinu za kisasa kwa kutumia huduma za intaneti, wateja wengi watavutiwa na kuendelea kuwepo kwenye soko na kuweza kukabiliana na ushindani wa kibishara." Alisema.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete, akizungumza wakati akiifungua warsha ya kimataifa ya wanachama wa Umoja wa Posta Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza, ilioanza jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Mount Meru, Novemba 6 na kumalizika Novemba 8, 2017.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta duniani (UPU), Bi. Loilinda Dieme, akizungumza katika warsha hiyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Bw. Younous Djibrine, akizungumza katika warsha hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo Kwiyukwa akizungumza katika warsha hiyo.

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images