Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

JUMUIYA WAFANYABIAASHARA WA JAMHURI YA CONGO WAISHIO NCHINI WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUONDOA VIKWANZO KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais Jumuiya ya Wafanyabishara wa Congo nchini, Mukendi kabobu akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara katika bandari ya Dar es Salaam.


Jumuiya ya wafanyabiaashara wa jamhuri ya Congo waishio nchini wameeleza kuridhshwa na mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini ukiligansha na ilivyokua awali ambapo ilikua na changamoto mbalimbali.

Wakizungumza na waandishi kwa kutatua changamoto walizozilalamikia ikiwemo Urasimu wa utoaji wa mazigo bandarini ,Wamesema hapo nyuma kulikuwa na urasimu ulisababisha idadi kubwa ya wafanyabiashara wanaotoka nchini Congo kukacha kutumia bandari ya Dar es salaam.

Rais wa Jumuiya ya Wafanyabishara wa Congo nchini, Mukendi kabobu, amesema wanaipongeza serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais Dk.  John Pombe Magufuli kwa kuondoa vikwazo vya kibiashara katika uondoshaji wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.

Amesema kuwa wafanyabiashara wa Congo kila wakiwa na mambo ambayo yamekuwa kikwazo kwao yamekuwa yakitatuliwa na kufanya biashara kuwa nyepesi katika kupitishia bandari ya Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Jumuiya hiyo,John Kapeta amesema kuwa wa wafanyabiashara wanaotoka nchi ya Congo wanafanya biashara bila kikwazo kutokana na jitihada alizochukua Rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya uboreshaji wa huduma katika bandari ya Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wafanyabishara wa Congo nchini, John Kapeta akizungumza na waandishi habari juu ya urahisi wa kupata huduma katika bandari ya Dar es Salaam pale wanapotaka kuotoa mizigo mkutano ulifanyika jijjini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

COSTECH KUTUNGA SHERIA ITAKAYOSIMAMIA MASUALA YA UTAFITI NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeweka mapendekezo matano ya tafiti sambamba na kutunga sheria zitakazowapa muongozo watafiti pindi wanapotaka kufanya utafiti wa aina mbalimbali. 

Akizungumza leo katika siku ya mwisho ya maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa utafiti baina ya Tanzania na Sweden yaliyoanza jana, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dugushilu Mafunda amesema kuwa kwa sasa wamejikita katika mapendekezo matano ambayo yamegawanyika katika vipengele mbalimbali ambapo kupitia taasisi yao wanafanya tafiti hizo. 

Mafunda amesema kuwa, kuna tafiti nyingi sana zimeshafanyika ila zinashindwa kufanyiwa kazi kutokana na baadhi ya tafiti hizo kuhitaji miradi mikubwa kwenye kuiendesha. 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dugushili Mafunda akizungumzia namna taasisi yao ilivyoweza kusimamia tafiti mbalimbali na kushindwa kufanyiwa kazi ikiwa ni siku ya mwisho ya maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa masuala ya utafiti baina ya Tanzania na Sweden leo Jijini Dar es Salaam. 
"Tafiti nyingi tayari zimeshafanywa na kikubwa zaidi zaidi zimekuwa zinashindwa kuendelea kufanyiwa kazi kutokana na baadhi ya tafiti hizo kuhitaji miradi mikubwa ya uendeshaji, zaidi ni makampuni ya kujitokeza kwa ajili ya kusaidia kufanyika,"amesema Mafunda. 

COSTECH wamekuwa mstari wa mbele katika kusimamia tafiti mbalimbali zinazoendeshwa nchini huku wakiwa kwenye hatua za mwisho za kutunga sheria zitakazokuwa zinawataka watafiti kufuata maadili kwenye tafiti zao. 

Akieleza hayo Afisa mwandamizi wa Utafiti (COSTECH) Hildegalda Mushi amesema kuwa kuna taasisi nyingi kwa sasa zinafanya tafiti kwenye nyanja tofauti ila tumeamua kutunga muongozo huu kwa ajili ya kusaidia kusimamia maadili bora. 

"Muongozo huu ambao utakamilika Januari 2018 utaweza kusimamia ubora kwenye kulinda mazingira ya binadamu, wanyama na mifugo pia tafiti hizo zitakuwa kwa matakwa ya kitaifa na kimataifa,"amesema Hildegalda. 

Amesema tafiti zote haziwezi kufanyika mpaka waweze kupata kibali na iwapo mtafiti ataenda kinyume na muongozo basi atakumbana na adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kibali cha kufanya tafiti au kuondolewa kabisa kwenye masuala ya utafiti. 

Kwa upande wa Mhadhiri wa chuo cha Ardhi Prof Nancy Marobhe ambaye amefanya tafiti inayohusu masuala ya usafishaji maji kwa njia ya kutumia mbegu ambayo aliifanya mwaka 2008 Singida vijijini. 

Prof Nancy amesema kuwa, aliweza kufanya tafiti hiyo katika vijiji vitano na aliweza kukutana na changamoto kubwa wanazokutana nazo wakina mama wakati wa upatikanaji wa maji safi na salama na kwenda kuishia kuchota maji kwenye marambo (mabwawa) na maji hayo wakiyasafisha kwa kutumia mbegu za asili za mlonge na mkeketa. 

Tayari ameweza kutoa njia nzuri ya kuwasaidia wanawake kuweza kusafisha maji kwa njia ya mbegu na wataweza kufanya hivyo ikiwa ni salama zaidi na watatumia unga wa mlonge na mkeketa kwa kiasi kidogo sana. Changamoto kubwa ni kuwa upatakinaji wa maji kwa vijijini umekuwa mdogo sana kwani visima vingi vinavyojengwa vinakuwa havifanyi kazi kutokana na baadhi ya watu kushindwa kuvitunza na wengine kuviharibu. 
Afisa mwandamizi wa Utafiti (COSTECH) Hildegalda Mushi akielezea muongozo wa sheria utakaosimamia tafiti mbalimbali ambapo utakamilika Januari 2008 ukiwa na matakwa ya kitaifa na kimataifa. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Utafiti (COSTECH) Dr Khadija Malima wakati wa siku ya mwisho ya maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa masuala ya utafiti baina ya Tanzania na Sweden. 
Mhadhiri wa chuo cha Ardhi Prof Nancy Marobhe akizungumzia tafiti yake aliyoifanya mwaka 2008 inayohusu masuala ya usafishaji maji kwa njia ya kutumia mbegu wakati wa siku ya mwisho ya maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa masuala ya utafiti baina ya Tanzania na Sweden.

HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesisitiza kwamba vyombo vya dola vya ndani ya nchi havijashindwa kuchunguza matukio ya kihalifu yaliyotokea nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuwa na subira.

Amesema Serikali hairidhishwi na matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa, ambayo yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini na baadhi yake yamesababisha vifo na wengine kujeruhiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 9, 2017) wakati akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

Bw. Mbowe alitaka apew kauli ya Serikali juu ya hatua zilizochukuliwa kuhusu tukio la kushambuliwa na mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu, ambapo alishauri uchunguzi huo ufanywe na vyombo vya kimataifa, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa na vyombo vya ndani vya dola.

“Vyombo vya ndani vya dola vina uwezo mkubwa wa kusimamia usalama wa nchi na vinaendelea na uchunguzi wa matukio hayo yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa letu. Nawaomba wananchi waendelee kuwa na imani na vyombo vyetu vya dola na mara uchunguzi utakapokamilika taarifa itatolewa.”

KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU APOKELEWA KWA SHANGWE DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola akiteta jambo na Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi mara baada ya kuwasili katika ofisi yake Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo Ofisi hiyo walipokutana kumkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola katika ofisi yake Mjini Dodoma Novemba 9, 2017.
 Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola mara baada ya kumpokea rasmi katika Ofisi hiyo Novemba 9, 2017 Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi akiwatambulisha Wasaidizi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola mara baada ya kuwasili katika ofisi yake Mjini Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE)

$
0
0
Na Mathias Canal, Dodoma.

Serikali inaendelea na mchakato wa kufanikisha uwepo wa Mfumo wa soko la bidhaa (Commodity Exchange) ambapo miongoni mwa kazi za Mfumo huo utalenga kupunguza gharama za uendeshaji wa masoko ya mazao yote ya chakula na biashara ili kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri na yenye tija.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa Bungeni Mjini Dodoma Wakati akijibu swali la Mbunge wa Lulindi Mkoani Mtwara Mhe JEROME DISMAS BWANAUSI aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanzisha mfumo wa “Commodity Exchange” ili kuwasaidia wananchi wanaolima Korosho kupata bei nzuri katika misimu husika.

Mhe Naibu Waziri alisema kuwa Maandalizi ya Soko la Bidhaa (Commodity Exchange) yalianza tangu mwaka 2011 kwa lengo la kufanya biashara ya mazao kuwa ya wazi na yenye ushindani kulingana na nguvu ya soko. 

Mhe Mwanjelwa alizitaja hatua ambazo zimechukuliwa na serikali mpaka hivi sasa kuwa ni pamoja na kupitishwa kwa Waraka wa Soko hilo, Kuundwa kwa Bodi ya Soko, kutungwa kwa Sheria ya mwaka 2015 ya Soko la Bidhaa pamoja na kanuni zake, Kufanya uzinduzi wa kuanzisha Soko hilo, Kutoa mafunzo kwa Madalali watakaoendesha soko hilo na Kutoa mafunzo kwa baadhi ya viongozi wa Serikali na Sekta Binafsi ili kujenga uelewa wa pamoja. 

OBREY CHIRWA ATWAA TUZO YA MCHEZAJI WA BORA WA MWEZI OKTOBA

$
0
0
Mshambuliaji wa Young Africans ya Dar es Salaam, Obrey Chirwa amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2017/2018.

Chirwa raia wa Zambia alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, beki Erasto Nyoni wa Simba na mshambuliaji Ibrahim Ajibu pia wa Young Africans alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Young Africans mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Septemba hadi ya pili mwishoni mwa Oktoba.

Young Africans iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja, pia Yanga iliifunga Stand United mabao 4-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Kiwango cha mchezaji huyo kilionekana pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliofanyika Oktoba 28, 2017 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Bao la Yanga lilifungwa na Chirwa, hivyo kwa mwezi huo alifanikiwa kuwa na kiwango cha juu katika kila mchezo ikiwa ni pamoja na kufunga.

Kwa upande wa Erasto naye alitoa mchango mkubwa kwa Simba uliowezesha timu hiyo kupata pointi nane katika michezo minne iliyocheza, akitoa pasi za mwisho za mabao nne, ambapo Simba ilishinda michezo miwili na kutoka sare miwili, huku Ajibu akitoa mchango mkubwa kwa Yanga ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba).

Kampuni ya Vodacom, ambao ndiyo wadhamini wa ligi hiyo ina utaratibu wa kuwazadiwa wachezaji bora wa kila mwezi, huku pia mwisho wa msimu kukiwa na tuzo mbalimbali zinazohusu ligi hiyo, ambapo msimu wa mwaka 2016/2017 kulikuwa tuzo 16 zilitolewa kwa washindi wa kada mbalimbali. Chirwa atazawadiwa Sh milioni moja kwa kuibuka Mchezaji Bora wa Oktoba.

BEN POL KUPEWA UBALOZI WA MAÜA ASSOCIATION NCHINI UFARANSA

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol'  (wa pili kushoto) akiwa tayari amewasili katika Jiji la Paris nchini Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalumu ikiweo uzinduzi wa Filamu ya NDOTO na kutambulishwa kuwa balozi wa taasisi ya Maüa association.

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol' ameenda nchinI Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalum ya MAÜA Association pamoja na uzinduzi wa Filamu ya NDOTO utakaofanyika Tarehe Novemba 18, 2017 mjini Paris nchini humo.

Ben Pol alisema kuwa tayari amewasili nchini humo kwa ajili ya hafla hiyo iliyoandiliwa na watanzania wanaoishi nchini Ufaransa na  hafla hiyo itaambatana na utambulisho rasmi wa Msanii huyo kama balozi mpya wa MAÜA association.

"Mimi tayari nimeshafika huku na nina matarajio makubwa katika tamasha hili ambalo ni mara ya kwanza kwangu kushiriki katika nchi hii,"alisema.

Alisema kuwa hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Wana-diaspora, viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Maüa association ni taasisi iliyoundwa na Watanzania waishio ughaibuni (Ufaransa). MAÜA association ilianzishwa na kusajiliwa kwa sheria za mashirika ya kujitolea nchini Ufaransa kwa minajili ya kutoa usaidizi wa kiafya kwa watoto na vijana ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao. 

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA

$
0
0
Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameliagiza jeshi la Polisi nchini, kuendelea kuwapa kipaumbele askari wa kike katika mafunzo mbalimbali ili waweze kukabiliana na vitendo vya uhalifu mpya ambao umeanza kushika hatamu ukiwemo ugaidi, uchochezi, uhafidhina, wizi wa mitandao na matumizi mabaya ya mitandao, utakatishaji wa fedha haramu, ujangili, usafirishaji wa dawa za kulevya na makosa mengine yanayovuka mipaka.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo  jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifunga maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania(TPF NET) katika viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini yaliyokuwa na kauli mbiu ‘Usalama Wetu ni Mtaji wa Maendeleo, Tokomeza Uhalifu Kuwezesha Uchumi wa Viwanda”.

“Tumeona juhudi zenu kwa kudhibiti uhalifu katika maeneo yaliyokuwa korofi, ila ni jukumu lenu pia kuhakikisha kuwa mnakabiliana na vitendo hivyo vya uhalifu,kuhakikisha havivurugi hali ya amani na kuhatarisha usalama wa nchi”amesema .

Ameweka wazi kuwa ni wazi kwamba shughuli za kiuchumi zitafanyika kikamilifu iwapo nchi itakuwa tulivu na yenye amani na kwamba amani na utulivu huo,ndiyo utaleta kuaminiana na kukubaliana miongoni mwa wananchi na wawekezaji, hivyo suala la ulinzi na usalama ni muhimu katika maendeleo na ustawi wa nchi.

Alisema pamoja na kwamba jeshi hilo limejenga madawati ya jinsia ili kukabiliana na tatizo hilo lakini kuna umuhimu wa kuzidisha utoaji wa elimu kwa jamii ili kuwaelewesha kuwa wasiwe waoga wala wasione aibu kuripoti matukio hayo.

Hata hivyo alisema, Serikali inajitahidi kuboresha jeshi la polisi kwa kuendelea kulipatia vitendea kazi na itazidi kufanya hivyo kulingana na bajeti iliyopo sambamba na kushirikiana na wadau wenye nia njema ya kuwasaidiia
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la polisi wanawake kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya umuhimu wa alama za barabarani kutoka kwa Koplo Faustina Nduguru wa Kitengo cha Usalama Barabarani makamo makuu ya polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu kamera kugundua wanaoendesha kwa mwendo mkali kutoka kwa Konstabo Sharifa Ismail wa Kitengo cha Usalama Barabarani makamo makuu ya polisi Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Ali Mussa ambaye alimkaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi  kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka kumi ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yalioyofanyika kwenye Chuo Cha Taaluma ya Polisi,Kurasini, Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SERIKALI YAZINDUA NDEGE MAALUMU ITAKAYOFANYA DORIA ENEO LA BAHARI KUU KUDHIBITI UVUVI HARAMU

$
0
0


Serikali imezindua mkakati unaolenga kutokomeza uvuvi haramu kwa kuanzisha operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua safari ya ndege ya kutoka nchini Mauritius iliyotua hapa nchini, kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kufanya doria ya majini, Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alisema lengo ni kudhibiti uvuvi haramu katika eneo la bahari kuu.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imejipambanua juu ya ulinzi wa rasilimali za nchi, ikiwamo meli ya uhakika ya majini, licha ya kukumbwa na dhoruba kubwa.

Amesema kutokana na hali hiyo ndiyo maana wameunganisha nguvu kwa pamoja kati yao na Ukanda wa nchi za Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi kudhibiti uvuvi haramu kwa njia zote.“Tunaruhusu ndege ya doria leo, ili kuongezea nguvu njia za kudhibiti wavuvi haramu, tulianza kwa njia ya bahari na sasa ni kwa njia ya anga.

“Changamoto ya uvuvi haramu ni kubwa, mtu anapiga bomu kwenye matumbawe anafanya uharibifu ambao kuyatengeneza tena yanachukua zaidi ya miaka 100, huku yeye akiharibu kwa dakika tano, ” alisema Ulega.

Ulega alisema uharibifu huo ndiyo unachangia kuwatia umasikini wavuvi wengi kwa sababu siyo rahisi kupata samaki karibuni na kulazimika kwenda mbali ambako siyo rahisi kufika bila kuwa na vyombo maalumu.

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu, leo jijini Dar es Salaam. Kulia  ni Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akishuka kwenye ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu mara baada ya kuikagua ndani.
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega pamoja na viongozi mbalimbali wakiangalia ndege maalumu ya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu.
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed naNaibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akitoa zawadi kwa marubani wa ndege hiyo. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu yajamii.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA





Article 2

$
0
0
Join us this Sunday for a fun and speedy day of go karting at Ledger plaza bahari beach hotel. Race track opens at 11am & closes at 6pm. Hotel entrance is tzs10,000. and you pay tzs10,000 to ride the go karts for 10laps around the track.

USAMBAZAJI WA VIFAA VYA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI WAENDELEA.

JAFO AZINDUA KAMPENI YA MKOA WETU VIWANDA VYETU

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amezindua kampeni ya “Mkoa wetu, Viwanda vyetu” yenye lengo la kuanzisha viwanda 100 katika kila Mkoa nchini, leo Mjini Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Jafo amesema kuwa ni jambo lililowazi kuwa ili nchi iweze kuendelea inahitaji kufanya mapinduzi makubwa katika viwanda.

“Historia ya Viwanda siyo ngeni katika nchi yetu, tangu tupate Uhuru mwaka 1961 Serikali imekuwa ikilenga katika kujenga Uchumi kupitia Viwanda ambapo tokea wakati huo viwanda vingi vidogo vya kati na vikubwa vilianzishwa na kusimamiwa huku sehemu kubwa ya viwanda hivyo vikisimamiwa na Serikali” ameeleza Mhe. Jafo.

Aidha amesema kuwa ili azma hiyo iweze kufikiwa TAMISEMI itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika kuweka mazingira wezeshi pamoja na kutoa mwongozo wa namna ya kushirikisha Tasisi za Serikali na Sekta Binafsi na wadau wa maendeleo katika kuanzisha, kuendesha na kusimamia Viwanda ili kuikuza sekta hiyo nchini.

“TAMISEMI kupitia Mikoa na Halmashauri imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda, hivyo kila Mkoa uanishe Viwanda vya vipaumbele kwa kuzingatia Malighafi muhimu za Viwanda zinazopatikana kwenye maeneo yao pamoja na mahitaji muhimu ya soko” amefafanua Mhe. Jafo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akizindua Mwongozo wa Kampeni ya uanzishwaji wa Viwanda kwa kila Mkoa hapa nchini ili kuendana na dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisistiza ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo akionesha moja ya viatu vinavyozalishwa hapa nchini katika Viwanda vidogo na vya Kati wakati akikagua mabanda ya wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo za ngozi mara baada ya kuzindua kampeni yenye kauli Mbiu ya “Mkoa Wetu Viwanda vyetu” ili kuhamasisha ujenzi wa Viwanda katika Mikoa yote nchini.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Mikoa(kushoto), kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati katika kila Mkoa.
( Picha zote na Frank Mvungi – Maelezo, Dodoma)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Chama cha Labour cha Uingereza Champongeza Rais Magufuli kwa Utendaji Wake.

$
0
0
Jonas Kamaleki-MAELEZO

Chama cha Labour cha nchini Uingereza kimepongeza juhudi za Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa utendaji mzuri katika kulinda na kugawanya rasilimali kwa watu wake.

Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na Viongozi wa Labour Party katika Mkutano na vyama mbali mbali vya kisiasa vikiwemo vya Kiafrika vya SWAPO, ANC na CCM, uliofanyika Uingereza kama anavyoeleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa kimataifa, Kanali (Mstaafu) Ngemela Lubinga katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

“Chama cha Labour kinataka haki sawa kwa wote, kwa hiyo kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kusimamia rasilimali na kuhakikisha rasilimali zetu zinazoibiwa zisiibiwe tena, kimewapa faraja,” alisema Lubinga.
Lubinga amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inasimamia rasilimali kitendp ambacho kitaleta maandeleo kwani hakuna maendelo yanyowezakupatikana bila usimamizi wa rasilimali.

“Chama cha Labour kinapigana kuhakikisha wananchi wake wanapata makazi bora, hivyo suala la Accacia ambao walikuwa wakifanya vitendo visivyoendana na hali halisi ya rasilimali hasa kwetu sisi walengwa kimewafurahisha sana na kuona kuwa mazungumzo yamekamilika katika mazingira ya kukubaliana namna ya rasilimali hizo zinavyotumika kuwanufaisha watanzania,”alisema Lubinga.

Kuhusu mwelekeo wa uchumi, Kanali (Mstaafu) Lubinga amesema kuwa uchumi wa Tanzania unakua na utakuwa wa kuvutia kwani juhudi za makusudi zinafanyika hivyo amewataka wanachi wawe na subira.

Ameongeza kuwa wazazi wawaandae watoto wao kufanyakazi na wasiwaachie tu kwenda wanavyotaka. Ametoa mfano kuwa mtu akiona mtoto wake amenunua gari la kifahari inabidi amuulize fedha ametoa wapi za kununua gari hilo wakati mshahara wake unajulikana na ni mdogo.Amewataka watanzania wawe wavumilivu kwani mabadiliko huleta kiwewe kwa wat na yakishaleta matokeo chanya, watu hao husahau walioleta maendeleo hayo.

Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza miaka miwili tangu iingie madarakani tarehe 5 Novemba, 2015. Katika kipindi hiki watanzania wameshuhudia miradi mikubwa ya maendeleo ikianzishwa na kutekelezwa, mfano ujenzi wa barabara,madaraja, ununuzi wa ndege sita, ujenzi wa reli ya kisasa, (standard gauge), utengenezaji wa madawati na elimu bure kwa elimu ya msingi na mwisho nidhamu ya kazi imerejea katika utumishi wa umma.

JAMII YATAKIWA KUACHA ITIKADI ZA VYAMA KATIKA KULETA MAENDELEO

$
0
0
NA DENIS MLOWE, IRINGA

MBUNGE Wa viti maalum Mkoa Wa Iringa, Ritta Kabati ametoa wito kwa jamii kuondoka na itikadi za kisiasa pindi linapokuja suala la maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza na wazazi na walezi wa shule ya msingi Igeleke wakati wa ukarabati wa madarasa ya shule hiyo mwishoni mwa wiki ikiwa ni ahadi yake ya kukarabati shule za msingi zenye miundo mbinu mibovu na zamani, Kabati alisema kuwa suala la ujenzi wa madarasa hauna siasa.

Alisema kuwa maamuzi ya kukarabati shule za msingi lengo ni kuyaweka mazingira bora ya kusomea wanafunzi na kuwaepusha na ajali zinazoweza kujitokeza kutokana na uchakavu wa majengo.

Kabati alisema kuwa imekuwa kawaida pindi mtu akitaka kufanya maendeleo mambo ya siasa yanaingizwa ila kwa serikali hii ya hapa kazi lazima tufanye kazi za kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akikabidhi saruji kwa uongozi wa shule kabla ya kuanza ukarabati katika shule ya msingi Igeleke.

MAGAZETI YA IJUMAA LEO NOVEMBA 10,2017


RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA WAWEKA JIWE LA MSINGI LA BOMBA LA MAFUTA GHAFI, WAFUNGUA KITUO CHA PAMOJA CHA HUDUMA ZA MPAKANI MJINI MUTUKULA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakiwa wamesimama wakati nyimbo za Taifa za nchi zao pamoja na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikipigwa kabla ya kuanza kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga pamoja na kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima kabla ya kuanza kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga pamoja na kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Mke wa Rais wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa na Mke wa Rais wa Uganda Mama Janeth Museveni wakati nyimbo za taifa zikipigwa  kabla ya kuanza kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga pamoja na kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitambulisha ujumbe alioongozana nao kwa mwenyeji wake  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga pamoja na kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni huku wake zao wakifurahia baada ya  viongozi hao kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakiongozana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere baada ya kuzindua Kituo cha Pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakisalimiana na viongozi wa kampuni ya Total ya Ufaransa wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta wakiweka  jiwe la msingi la mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika kijiji cha Luzinga Mutukula nchini Uganda Novemba 9, 2017. Picha na IKULU

ZANTEL YAZINDUA PROGRAMU YA 'GRADUATE SALES FORCE PROJECT'

$
0
0
Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel  imezindua programu yake ya 'Graduate Sales Force Project' yenye lengo la kuwapa ujuzi wahitimu wa vyuo vikuuambao bado hawajapata kazi rasmi kabla ya kuingia kwenye Soko la ajira.

Akizungumzia programu hiyo katika Makao makuu ya Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Zantel, Haidari Chamshama alisema "Programu hii ni ya mwezi mmoja na ina lengo la kuwanufaisha wahitimu wa vyuo mbalimbali ambao bado hawana ajira rasmi kwa kufanya kazi kwenye vitengo mbalimbali katika Kampuni ya Zantel".

Kwa sasa programu hiyo itajikita kwenye Masuala ya Mauzo na wataangalia jinsi ambavyo wahitimu hao wanavyojituma kazini na hatimae kuajiri wachache kati yao.

Kwa Upande wake Meneja wa Chapa na Mawasiliano Zantel, Rukia Mtingwa alisema Soko la ajira limekua gumu kwa hivi sasa hivyo, Zantel wameona ni vyema kuwapa ujuzi wanahitimu wa vyuo mbalimbali ili kuwajengea ujuzi kabla ya kuingia ya kujipatia ajira.

Jumla ya wahitimu ni 95 kutoka vyuo 15 vya Tanzania wa fani tofauti wamechukuliwa kwa mwezi huu na Zantel kwa ajili ya mafunzo hayo kwa vitendo.
Meneja Mauzo na Usambazaji Zantel, Haidari Chamshama akizungumza na Wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini ambao wanafanyakazi kama Wauzaji wa huduma na bidhaa za Zantel leo katika makao Makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam kabla ya kutawanyika na kuelekea katika sehemu mbalimbali za kazi zao. Wahitimu hao wa vyuo vikuu wapo chini ya Programu ya Zantel iliyopewa jina la ‘Graduate Sales Force Project’ yenye lengo la kuwawezesha na kuwafundisha kwa vitendo ili kuwapatia ujuzi kabla ya kuingia kwenye Soko la ajira.

LUSINDE AUWASHA MOTO KOROGWE MKOANI TANGA WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde kushoto akimnadi mgombea udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduizi (CCM) Mustapha Shengwatu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba sokoni wilayani humo .
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi wa Kata ya Majengo kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kushirikiana naye kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kasi zaidi.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Majengo katika Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mustapha Shengwatu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni .
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi katikati akifuatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda na kushoto ni Mgombea Udiwani wa CCM Mustapha Shengwatu.

DC NZEGA ASEMA SAYANSI NA TEKNOLOJIA HAIKWEPEKI KATIKA KILIMO

$
0
0

Na Dotto Mwaibale, Nzega Tabora

MKUU wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Godfrey Ngapula amesema Sayansi na Teknolojia haiwezi kuepukika katika kilimo nchini.

Ngapula ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na Viazi lishe kwa ajili ya kuanzisha mashamba darasa katika vijiji vya Shila, Iyombo, Upungu, Lububu na Kapanga wilayani humo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ili kufanya kilimo chenye tija sayansi na teknolojia haiwezi kuepukika kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo.Alisema kilimo cha kisayansi kina tija kwani mkulima anaweza kulima eneo dogo na kupata mavuno mengi kuliko kilimo cha mazoea ambacho mkulima hulima shamba kubwa mazo kidogo.

Ngapula aliipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuwapelekea mbegu hizo kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) 

Akizungumzia matumizi ya mbegu zilizozalishwa kwa teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) alisema hayakwepeki kwa kuwa mbegu hizo zinasifa ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukame na wadudu waharibifu wa mazao.
Wanawake wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo Kata ya Utwigu wakiwa wamebeba mbegu ya Viazi lishe wakielekea kupanda katika shamba darasa.
Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wanakikundi hicho jinsi ya kupanda mbegu hiyo.
Wanawake wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo Kata ya Utwigu wakipanda mbegu hiyokatika shamba lao.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images