Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

BIASHARA YA CHUMA CHAKAVU NA TAKA HATARISHI KUUZWA NA WALE WENYE VIBALI TU

$
0
0
Tarehe 20 Mei, 2017 Ofisi ya Makamu wa Rais iliutaarifu umma kuhusu utaratibu wa kufanya shughuli zote zinazohusu ukusanyaji, usafirishaji, biashara na urejeleshaji wa taka hatarishi kama vile vyuma chakavu, "Oil" chafu, matairi yaliyotumika, taka za kieletroniki na za umeme na taka zitokanazo na kemikali. 

Ofisi iliwataka wale wote wanaofanya shughuli hizi hapa nchini kufuata sheria, kanuni na miongozo. Aidha, kuzingatia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira ambayo Tanzania ni mwanachama ikiwa ni pamoja na kuwa na vibali vya biashara husika.

Ofisi inapenda kuukumbusha umma kuwa bado baadhi ya wanaokusanya, kusafirisha na kurejeleza taka hatarishi hawana vibali kama inavyohitajika. Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009, kanuni ya 39 hadi 46 zinatoa muongozo wa hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa ili shughuli husika zifanyike.

Hivyo, Ofisi inawakumbusha tena wale wote wanaofanya shughuli za uuzaji na ununuzi wa taka hizi kuhakikisha wanafanya biashara na wale wenye vibali tu. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009. 

Aidha, Kanuni ya 47 (3) ya Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009 inatoa adhabu kwa mtu ambaye anashindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa, ambapo baada ya kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia anaweza kutozwa faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000.00) au kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja. 

Mhandisi Joseph Kizito Malongo

KATIBU MKUU
OFISI YA MAKAMU WA RAIS

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVENI KATIKA IKULU YA MASAKA NCHINI UGANDA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la mkutano baina ya wajumbe wa nchi mbili za Tanzania na Uganda katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja aliombatana nao katika Mazungumzo na ujumbe wa Uganda uliokuwa ukiongozwa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa pamoja na ujumbe wa Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za Asili cha Cranes Performance mara baada ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Masaka nchini Uganda.
Kikundi Cranes performance kikitumbuiza katika dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Masaka Uganda. PICHA NA IKULU

DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI

$
0
0
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto amewataka watoa huduma na mafunzo kuhusu lishe bora yaanzie ngazi za shule ya msingi ili kuwajenga watoto kuzingatia mlo bora katika kukuza afya za watanzania. Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).

“Walimu wawe sehemu ya afua za kufundishia wanafunzi juu ya lishe bora hasa kuanzia ngazi za shule ya msingi ili kuwajengea mazoea watoto kupenda kula mlo ulio bora hata wanapokuwa majumbani mwao” alisema Dkt. Ulisubisya. Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa baadhi ya watoto walio vijini na mijini wana utapia mlo kwa kukosa chakula kilicho bora hivyo jamii inatakiwa izingatie lishe bora ili kuimarisha afya za watoto nchini.

Mbali na hayo Dkt. Mpoki amesema kuwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawe kipaumbele katika kutoa elimu ya lishe bora ili kuweza kujikinga na Unyafuzi, Kwashakoo na magonjwa yasiombukiza kama vile Kisukari,shinikizo la damu ,magonjwa ya moyo yanayotokana na ulaji kupita kiasi.

Kwa upande wake Meneja wa Magonjwa yasioambukiza ,Usalama wa Chakula na lishe ECSA Bi. Rosemary Mwaisaka amesema kuwa wameamua kuandaa vitini na vitita vya kufundishia lishe bora ili kuweza kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kufikisha elimu hiyo kwa walengwa.

“Tumeamua kuandaa vitini hivi ili viweze kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kuweza kuwafundisha wanajamii juu ya umuhimu wa kula mlo bora na vitatumika Kenya,Uganda na Tanzania” alisema Bi. Mwaisaka. Mbali na hayo Mshiriki wa Mafunzo ya Lishe bora kutoka ECSA ambae pia ni Mtoa huduma Bi. Evelyne Minja amesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kutoa huduma katika jamii kuhusu mlo bora hasa kwa watoto vijijini na mijini.

“Mafunzo haya yametufanya tujue jinsi ya kuwahudumia na kutoa ushauri juu ya mlo bora hasa kwa watoto wenye viashiria vya utapia mlo kwa kuwapima na kuwapangia vyakula vinavyostahili” alisema Bi. Minja.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wadau mbalimbali wa maswala ya lishe hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kushoto akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Vincent Assey wa kwanza kulia wakati wa uzinduzi wa hivyo vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia akikata keki kuashiria kuzindua vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Afisa msaidizi wa ECSA Bi. Dorin Marandu.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia akimlisha keki mmoja wa washiriki na mtoa huduma wa lishe ngazi ya jamii Bi. Evelyne Minja wa pili kushoto wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam. PICHA NA ALLY DAUD -WAMJW.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI

$
0
0

Na Mathias Canal, Dodoma

Serikali imesema kuwa Mpango wa Serikali wa kuwapelekea wakulima wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma mbegu mpya za Kahawa ni mahususi kwa ajili ya kuinua uzalishaji kwa kutekeleza Mpango Mkakati wa Kuendeleza Zao la Kahawa katika kipindi cha miaka 10 yaani mwaka (2011 – 2021).

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) amebainisha hayo leo Novemba 10, 2017 Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mhe Martin Mtonda Msuha (Mb) Aliyetaka kufahamu kuhusu kushuka Kwa takwimu katika miaka ya hivi karibuni ya uzalishaji wa Kahawa Wilayani Mbinga kwa mkulima mmoja mmoja (out growers) ambapo alitaja sababu za mojawapo zilizopelekea kushuka kwa uzalishaji huo kuwa ni pamoja na kuzeeka kwa miti ya kahawa.

Mhe Mwanjelwa alisema kuwa Katika mpango huo, utafiti na usambazaji wa miche bora itatolewa ili kuondokana na miche yenye tija duni na iliyozeeka. Ambapo Utekelezaji wake unafanyika kwa kushirikiana na wadau hususani Tanzania Coffee Research Institute (TaCRI).

Alisema, Kituo cha Utafiti na uzalishaji miche cha Ugano kilichopo Wilayani Mbinga, katika mwaka 2016/2017 kilizalisha na kusambaza miche bora ya kahawa 270,869 na kazi mpaka hivi sasa inaendelea.

Aidha, Mfuko wa Maendeleo ya Kahawa (Tanzania Coffee Developemnt Fund (TCDF) umefadhili na kupunguza bei kutoka shilingi 300 kwa mche mmoja hadi shilingi 150 kwa vituo vyote nchini vilivyoko chini ya TaCRI ili miche hiyo isambae kwa kasi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Leo Novemba 10, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akijadili jambo na Mhe Jenista Joakim Mhagama ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.



SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LATOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI SHINYANGA

$
0
0
Shirika la kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa pikipiki kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto la jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 10,2017 wakati wa kukabidhi pikipiki moja kwa jeshi la polisi,Meneja wa shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga Benety Malima alisema pikipiki hiyo itasaidia katika ufuatiliaji wa makosa mbalimbali yakiwemo ya jinai. 

“Shirika letu limekuwa likiendesha mafunzo kuhusu ukusanyaji wa vielelezo kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi kwa ushahidi mahakamani,tumebaini kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo ni usafiri,kutokana na hali hiyo tumeona tuangalie namna ya kuwezesha usafiri ili kukabiliana na vitendo vya ukatili katika jamii”,alieleza Malima. 

Akipokea pikipiki hiyo SSP Lutusyo Mwakyusa aliyemwakilisha kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule,alilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi. 

“Tunalishukuru shirika la Save the Children, huu ni msaada mkubwa sana kwetu kwani utasaidia kuokoa maisha ya watu,na hiki ni kielelezo tosha cha ushirikiano kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia,naomba wadau wengine waige mfano wa shirika hili ili kujenga jeshi letu la polisi”,alieleza Mwakyusa. 

Aliwataka wadau kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa matukio ya ukatili yanatokomezwa. 
Pikipiki iliyotolewa na shirika la Save The Children kwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ili itumiwea na dawati la jinsia na watoto kufuatilia matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto.

MAFINGA WAO NI KAZI TUU.

$
0
0
Ujenzi wa majengo mbalimbali katika Kituo cha Afya Cha Ihongole umeanza kutokana na fedha za Serikali Tsh. 500m/=. Ujenzi huu unahusisha kujenga Maabara, Chumba cha Upasuaji, Wodi ya Wazazi (Mama na Mtoto), kichomea taka , na nyumba ya Muuguzi/Daktari.


Yote haya ni ushirikiano kati ya Mbunge, Mkuu wa Wilaya, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi na watendaji wa Halmashauri, Serikali na Wananchi. Mafinga Sisi Kazi Tu
 Ujenzi wa Jengp la Mama na Mtoto ukiendelea
 Ujenzi wa Chumba cha upasuaji-Theatre ukiendelea
Jengo la Maabara ujenzi wake ukiendelea pia

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO UGANDA, PIA AZUNGUMZA NA WANAHABARI MBALIMBALI MASAKA NCHINI UGANDA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watanzania waishio nchini Uganda katika eneo la Masaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakizungumza na wanahabari mara baada kumaliza ya kufanya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha umahiri wa kupiga ngoma pamoja na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika eneo la Kyotera nchini Uganda.


PICHA NA IKULU

DC IGUNGA HAITIMISHA ZOEZI LA KUPOKEA MBEGU BORA KUTOKA COSTECH-OFAB

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Igunga Tabora

MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, John Mwaipopo amehitimisha zoezi la ugawaji wa mbegu bora katika mikoa ya Kagera, Geita na Tabora kwa kuipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuwapelekea mbegu bora za mihogo, mahindi na Viazi lishe wilayani humo kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

Pongezi hizo alizitoa jana wakati akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Igogo kilichopo Kata ya Nanga katika uzinduzi na kukabidhiwa mbegu hizo kwa ajili ya mashamba darasa kwa wakulima wa vijiji vinne vya Igogo, Mwanzugi, Sungwizi na Busomeke.

Alisema changamoto kubwa waliyokuwa nayo wakulima katika Halmshauri hiyo ni kukosekana kwa mbegu bora za mihogo na mahindi jambo liliofanya uzalishaji wa mazao kuwa mdogo.

Mwaipopo alisema kuletewa kwa mbegu hizo kutaongeza mori wa kilimo kwa wakulima wa wilaya hiyo na kuondokana na ukosefu wa chakula badala ya kutegemea zaidi zao moja la mpunga.

Alisema kazi kubwa ya serikali ni kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa mradi huo kwa nguvu zote ili kazi kubwa iliyofanywa na watafiti kutoka Vituo vya Ukiliguru Mwanza, Maruku mkoani Tabora na Ilonga mkoani Morogoro isipotee bure.
 Wakulima wa Kijiji cha Igogo wanaunda Kikundi cha Imala Makoye katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wakiwa wameshika mbegu ya mahindi ya Wema 2109 baada ya kukabidhiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika jana wilayani huo. Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa mkuu wa wilaya hiyo, John Mwaipopo.
 Kaimu Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Athumani Mgunya akizungumza kabla ya uzinduzi huo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Igogo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi. Kulia ni Ofisa Ugani wa Kata ya Nanga, Ambele Mwangomo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO NOVEMBA 11,2017

MHANDISI MTIGUMWE ATANGAZA KIAMA KWA MAAFISA UGANI NCHINI

$
0
0
Na Mathias Canal, Arusha

Serikali imekuwa ikiongeza idadi ya wanafunzi katika Vyuo vya Kilimo na kwa sababu hiyo Maafisa Ugani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka ambapo hali hiyo imewezesha Karibu kila Kata hapa nchini kuwa na Afisa Ugani.

Lakini pamoja na kuwepo kwa wataalamu hao wa kilimo bado uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini yakiwemo mazao ya chakula na biashara si wa kuridhisha ambapo wakulima wanalima na kupanda pasina hata kufuata hatua za kitaalamu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi akizungumza na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI TENGERU) kilichopo katika Kijiji cha Tengeru, Kata Patandi, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

Alisema lengo la Serikali kusambaza  Maafisa Ugani kwenye Halmashauri mbali mbali nchini ilikuwa  kuwasaidia  wakulima  waweze kufanya Kilimo kwa Ufanisi na kuongeza mavuno.

Hata hivyo jambo hilo limekuwa kinyume kwani asilimia kubwa ya maafisa ugani ama hawafanyi kazi zao ipasavyo ama wameshindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe akiwasili katika Ofisi za Taasisi ya Horti Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru). Mwingine ni
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Mansoor Hussein

WANAWAKE WATAALAMU WA KILIMO ,UVUVI NA MIFUGO WAZINDUA KITABU CHAO KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA 21 WA CHAMA CHAO

$
0
0
Mgeni rasmi Bi. Butano Philipo wakiwa na Mwenyekiti wakizindua vitabu mbalimbali ikiwemo kitabu cha  Ufugaji wa samaki.

Chama cha wanawake  wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo,Uvuvi na Mazingira, Tanzania association of women leaders in agriculture and environment  ( TAWLAE) wamefungua rasimi mkutano wa mwaka  wa 21 na kuhudhuriwa na Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa raisi bi Butamo Philipo kwa  niaba ya waziri wa  Mazingira  Mhe. January Makamba ambao umefanyika  jana katika viwanja vya wizara ya mifugo na uvuvi.

 Akizungumza katika mkutano huo wenyekiti wa chama cha wanawake kiongozi katika kilimo na mazingira Dkt. Sofia Mlote amesema Lengo kubwa la mkutano huo ni kuunganisha wakulima na tafiti mbalimbali  zilizoandaliwa na wataalamu hao.

 Maadhimisho ambayo yamebeba kaulimbiu isemayo  uchumi wa viwanda Tanzania wanawake tupo tayari,hapa ni kazi tu.

Aidha, Dkt. Sofia Mlote amesema kazi ya TAWLAE ni kuwaunganisha wakulima wadogo au wakubwa na tafiti mbalimbali ambaozo  zimetafitiwa hapa nchini  ili kuongeza uwekezaji na ajira kwa watanzania katika kilimo.

Akizungumza Dkt.Mlote amesema kilimo kilikuwa na faida ndogo kwa sababu utalaam,teknolojia na juhudi zilikuwa bado hazijatumika vizuri katika kilimo
 kuingia na uchumi wa viwanda  ni lazima uzalishaji  wa kilimo uwe na  tija , kuwepo na uboreshaji wa masoko na teknolojia ambapo wataalamu wanawake ndio wanajukumu kubwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo alisema Dkt.Mlote
Getrude Mongela mlezi wa Tawlea ambaye ana PHD ya Philosophy alisema wanawake Uchumi wa viwanda Tanzania wanawake tupo tayari , Hapa kazi tu.

Vile vile amefarijika kuona amelea wanawake toka wakiwa wadogo na sasa wamesoma na wengine wana PHD lengo kubwa hasa alisistiza mpaka kufikia 2020 wanawake wawe wamekua kiuchumi na kuendelea kutoa  wasomi wa kutosha na kufikia malengo.
Kiongozi wa Chama cha Wanawake viongozi katika Kilimo na Mazingira Dkt. Sophia Mlote akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya makamu wa raisi Bi. Butano Philipo katika uzinduzi wa mkutano huo leo.

NAIBU SPIKA TULIA ACKSON AMEWATAKA WANAWAKE NCHI KUJENGA MAZOEA YA KUFAYA MAZOEZI MARA KWA MARA.

$
0
0
Naibu spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson ameendesha arambee ya kuchangia hospitali ya wilaya ya Namtumbo iliyopo mkoaani Ruvuma kwa ajili ya kujenga hodi ya akina mama pamoja na jengo la upasauaji,pia naibu spika alishiriki mbio za kilometa 5 na kuwa mshindi wa mbio hizo habari kamili hii hapa video yake.

YALIYOSEMWA NA DK. HASSAN ABBAS KATIKA KIPINDI CHA VIJANA TZ JUU YA MAFANIKIO /UTENDAJI WA SERIKALI NA CHANGAMOTO KATIKA TASNIA YA HABARI

$
0
0
“Ofisi yangu ina jukumu la kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ya Serikali; Kusajili na kufungua Magazeti; Kusaidia Watu wa mifumo mingine ya Serikali kusema” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Uhuru wa vyombo vya habari upo wa kutosha. Serikali imeruhusu uhuru wa Vyombo vya habari. Kuna Redio zaidi ya 150, tuna redio zaidi ya 30, kuna Magazeti zaidi ya 110 yanayotoka nchini” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Serikali ina simamia Wananchi wapate habari sahihi na si kulishwa habari mbovu. Serikali tunalisimamia hili” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu.“Changamoto iliyopo ni kuhakikisha habari zsahihi zinawafikia Watu wote kwa wakati” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Rais @MagufuliJP amefanikiwa sana kuleta mageuzi ya kifikra. Kujenga hari ya Uzalendo, nidhamu, uwajibikaji kwa Watu wake wakiwemo Watumishi wa Umma na Wananchi” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu.“Rais @MagufuliJP ameleta nidhamu kubwa ya matumizi ya fedha za umma. Mathalani amefanikiwa kudhibiti safari za nje zisizo na tija” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Hapo nyuma zilitumika bilioni zaidi ya 200 kwa safari tu wakati hivi sasa zimetumika bilioni 25 tu kwa safari tumeokoa pesa nyingi”@TZ_MsemajiMkuu

“Rais @MagufuliJP ameleta mageuzi ya kudhibiti Wafanyakazi hewa zaidi ya 20,000 na kuokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 238. Ni mageuzi makubwa” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu

“Tumeondoa wafanyakazi hewa takribani elfu 20 kwa zoezi hilo tumeokoa bilioni 238” @TZ_MsemajiMkuu.“Hawa wanaopiga kelele juu ya mageuzi ya rasilimali za madini. Ipo siku watanyamaza wakiona manufaa ya wazi. Serikali ya @MagufuliJP imeonyesha uzalendo kwenye madini” – Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu.“Zipo nchi kubwa duniani awapati 50/50 kwenye Madini sisi tumeweza @TZ_MsemajiMkuu

WADAU WA MADINI WATAKIWA KUHAKIKISHA MADINI YANANUFAISHA JAMII

$
0
0
Wadau wa madini wametakiwa kuhakikisha sekta hiyo inaakisi maendeleo ya jamii inayozunguka eneo hilo ili waone faida ya kuwepo kwa rasilimali hiyo muhimu. 

Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Luhumbi aliyasema hayo mjini Geita kwenye ufunguzi wa majadiliano ya wachimbaji wadogo Tanzania yaliyowashirikisha wadau wa madini wa nchi mbalimbali duniani. 

Akizungumza kabla ya washiriki hao hawajaanza safari ya kutembelea migodi ya madini ya dhahabu, Luhumbi alisema faida ya uwepo wa madini hayo inapaswa kuonekana dhahiri kwa jamii. Alisema uwepo wa rasilimali ya madini ya dhahabu mkoani Geita bado haujaonekana ipasavyo kwa jamii ya eneo hilo kwani zinapaswa kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara, maji, elimu, afya na mengineyo. 

"Hatutaki kuona rasilimali ya madini inaoneka kuwa ni laana kwa jamii badala ya baraka, kwani kupitia tunu hiyo wananchi wanapaswa kunufaika kwa kuona maendeleo yanafanywa kwenye maeneo hayo," alisema Luhumbi. Alisema sekta ya wachimbaji wadogo wa madini inafanywa na idadi ya watu milioni moja hadi milioni moja na nusu nchini hivyo wanapaswa kuwekewa mazingira rafiki yatakayoboeesha maisha yao. 

Mkurugenzi wa asasi ya Haki Madini, Amani Mhinda alisema wameandaa mdahalo huo kwa uwezeshwaji wa taasisi ya kimataifa ya mazingira na maendeleo  (IIED) kituo cha kimataifa cha utafiti wa misitu (CIFOR) na kampuni ya ushauri ya MTL. Mhinda alisema lengo ni kutoa suluhu juu ya changamoto zinazomkumba mchimbaji mdogo nchini na kupendekeza majawabu. Alisema sekta ya uchimbaji madini nchini ni kati ya sekta zinazokua kwa kasi kubwa na yenye mchango mkubwa wa uchumi wa Taifa. 

Alisema ingawa mipango mahususi ya kisera juu ya uchimbaji mdogo imeanzishwa, bado kuna changamoto nyingi hasa katika uelewa, ujasiri, mipango, fedha na taratibu zinazokwamisha utekelezaji wa sera na maboresho. Mchimbaji wa madini wa kampuni ya Nsangano Gold mine, Renatus Nsangano alisema bado wachimbaji wadogo wana changamoto ya kufanya kazi bila kufanya utafiti. Nsangano alisema endapo wangekuwa wanafanya utafiti na kubaini madini yalipo ingekuwa na tija kubwa kwa wachimbaji wengi. 

Hata hivyo, alisema wamesaidia jamii zinazowazunguka kwenye maendeleo mbalimbali ikiwemo ya sekta ya elimu, afya na maji. 
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Luhumbi akizungumza na wadau wa madini juu ya rasilimali hiyo kunufaisha jamii inayozunguka eneo hilo. 
 Mkurugenzi wa kampuni ya Nsangano Gold mine ya Nyarugusu Mkoani Geita Renatus Nsangano (kulia) na Mkurugenzi wa kampuni ya Kadeo, Christopher Kadeo (wa pili kulia) wakiwa na wadau wa madini waliotembelea migodi yao ya dhahabu. 
 Mdau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Joseph Lyimo akivuta udongo kwa kutumia nyenzo katika mgodi wa dhahabu kwenye machimbo ya wachimbaji wadogo wa Nyarugusu Mkoani Geita. 
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wa mgodi wa Nsangano Gold mine ya Nyarugusu Mkoani Geita, wakiendelea na shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kwenye moja kati ya migodi yao. 

KATIBU MKUU NDUMBARO :WATUMISHI WA WIVIVU TUTAPAMBANA NAO

$
0
0
Katibu mkuu ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Dkt. Lauren Ndumbaro amewataka watumishi wote kuwa wazalendo na kuwatumikia wananchi na wafanyakazi ili kuijenga nchi yetu ya Tanzania .Hayo yamesemwa wakati akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kuzungumza na watumishi wa umma wa manispaa ya Songea.

Rais Magufuli amaliza ziara ya siku 3 Uganda, Rais Museveni atoa tamko dhidi ya ICC

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye gwaride la Kimya lililoandaliwa kwa heshma na Jeshi la Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uganda na kurejea nchini. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifurahia ngoma ya asili iliyokuwa ikipigwa na watoto wa nchini Uganda katika eneo la mpakani la Mutukula kabla ya kurejea nchini.   

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mpakani mwa Tanzania na Uganda (Mutukula) kuhusu  ujenzi wa barabara ya Kutoka Miziro hadi Mutukula bila kupitia wilayani Misenyi. Pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi wakuu wa Majeshi ya Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake nchini Uganda.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa mpakani  Mutukula upande wa Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tau nchini Uganda. PICHA NA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa mpakani  Mutukula upande wa Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tau nchini Uganda. PICHA NA IKULU.


WANAFUNZI 250 WAPATA MAFUNZO YA GIRL GUIDES TEMEKE

$
0
0
 Baadhi ya  Girl Guides ambao ni wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za Manispaa ya Temeke wakionesha moja ya alama muhimu za Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), baada ya kupata mafunzo ya awali  katika Shule ya Msingi Mbagala, Dar es Salaam leo. Wanafunzi wa kike 250 walishiriki mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke,  Leonida Komba ( wa tatu kushoto waliosimama)

Girl Guides hao walipata mafunzo kuhusu historia ya Girl Guides duniani, kanuni, malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwake.

Pia hufundishwa ujasiri, ukakamavu, mambo ya uongozi, maadili, kujitolea pamoja na uzalendo.(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke, Leonida Komba (kushoto) akiwahamasisha Girl Guides wakati wa mafunzo hayo.
 Girl Guides wakiwa na furaha baada ya kupata mafunzo ya chama hicho kuhusu kanuni, historia ya Girl Guides Duniani, malengo na madhumuni yake.
Kamishna wa TGGA Mkoa wa Temeke, Leonida Komba (wa pili kulia waliosimama) akiwa na walimu ambao ni walezi wa Girl Guides wa shule walikotoka wanafunzi hao.

Kamati Kuu ya AFCON yazinduliwa

$
0
0

Na Anitha Jonas – WHUSM-Dar es Salaam

Serikali yazindua Kamati Kuu ya maandalizi ya Africa Cup of Nation Under 17 (AFCON) yenye wajumbe ishirini na tano kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika nchini mwaka 2019.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe na kueleza kuwa uteuzi wa wajumbe hao wa kamati ulizingatia sekta muhimu zitakazo husika moja kwa moja katika kufanikisha mashindano hayo.

“Nawapongeza wajumbe wote kwa kukubali uteuzi huu maana kazi ya kamati hii si ya kulipwa bali ni kujitolea kwa manufaa ya nchi yetu na ninaimani kubwa kuwa tutafanya kazi nzuri na kwa kufanikisha mashindano haya tutakuwa tumelipa taifa heshima kubwa katika ulimwengu wa soka”,alisema Mhe.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi huo Mhe. Mwakyembe alisema kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo atakuwa yeye mwenyewe, Makamu Mwenyekiti atakuwa Mjumbe wa CAF na Rais wa heshima wa TFF Bw. Leodgar Tenga pamoja na Bw.Hendry Tandau kutoka Kamati ya Olimpiki nchini ambaye atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kamati.

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Leodgar Tenga alitoa angalizo kwa TFF kuzingatia kigezo cha umri kwa watoto hao wanaowaanda kwa ajili ya mashindano hayo ili kuepuka kuvunja sheria kwani mashindao hayo yanalega vijana waliyochini ya umri wa miaka kumi na saba na si zaidi ya hapo.

Pamoja na hayo Kamati hiyo inawajumbe mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Paul Makonda,Mkurugenzi wa ATCL Bw.Ladislaus Matindi,Mohamed Dewji na wengine.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON under 17 mikakati mbalimbali itakayosaidia kufaikisha mashindano ya 2019 yatakayofanyika nchini (kulia) Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw Leodgar Tenga
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON Bw Leodgar Tenga (kulia) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya mashindano yatakayofanyika 2019 nchini katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe na (kushoto ) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw. Wallace Karia.

Mamlaka za Maji Nchini Zatakiwa Kuanzisha Vituo Maalum vya Kupokelea Malalamiko ya Wateja

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo pamoja na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Dawasco Prof. Toli Mbwete (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Meja Jenerali Kitundu, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Hapi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akifafanua jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo akielezea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Shirika hilo mbele ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Issack Aloyce Kamwele (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Tano ya Wakurugenzi wa Dawasco leo Jijini Dar es Salaam.

Viewing all 109984 articles
Browse latest View live


Latest Images