Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

TRA IKISHIRIKIANA NA MSAMA AUCTION MART YAENDELEZA MSAKO YA KUWABAINI WAKWEPAJI KODI KATIKA KAZI ZA SANAA

$
0
0

Mamalaka ya Mapato nchini (TRA), Msama Auction Mart kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wameendelea na zoezi la kupita Duka kwa Duka, Mlango kwa Mlango kusaka wezi wa kazi za Sanaa na wakwepaji wa Kodi hapa nchini.

Zoezi hilo linaloendelea kwa nchi nzima, hapo jana liliendeshwa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Kamishna wa Kodi za Ndani - TRA, Elijah Mwandumbya amesema wameamua kufanya zoezi hilo ili kujiridhisha katika maduka ambayo yanafanya biashara za kazi za Wasanii.

Mwandumbya amesema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuhakiksha wanaofanya biashara hizo wanalipa Kodi shahiki, na kuhakikisha Stempu za Kodi zimatumika katika kila CD; "Kwa maana Stempu mbili kwa CD moja yaani Stempu moja kwenye Kasha la CD hiyo na nyingine kwenye CD yenyewe", amesema.

Pia kuhakikisha wale wanaofanya biashara za kazi za Wasanii wanavibali vya kufanya biashara hizo, ikiwa sambamba na kuwachukulia hatua stahiki ili kuhakikisha Wasanii hao wanapata haki zao katika kila kazi ambayo inauzwa sokoni.Amesema huo ni muendelezo wa Kampeni ambao unafanywa nchi nzima kutokana na kazi hiyo iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda miezi kadhaa iliyopita.

"Kwa kazi za Wasanii wa kigeni upo utaratibu wakufuata katika Taasisi pamoja na Kampuni mbalimbali ili kuuza kazi za Wasanii hao", amesema Mwandumbya.


Mkurugenzi wa Msama Auction Mart Alex Msama akiwa sambamba na wafanyakazi wake kwa kushirikia na Jeshi la Polisi wakikamata vifaa vinavyotumika kurudufu kazi za wasanii (muziki),jana katika moja ya Mtaa Kariakoo jijini Dar
Kamishna wa Kodi za Ndani - TRA, Elijah Mwandumbya akikagua moja ya CD ya filamu za hapa nchini,kubaini kuwa kama ina stika za TRA ama la,akiwa sambamba na Mkurugenzi wa Msama Auction Mart Alex Msama ambao wamepewa dhamana ya kushirikiana na TRA kupapambana na maharamia wa kazi za wasanii wakiwemo na wale wanaokwepa kodi
Ukaguzi ukiendelea kufanyika katika maduka yanayouza CD za Filamu,kubaini kuwa zinalipiwa ushuru na zina stika kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Baadhi ya Watuhumiwa na mafurushi yao ya CD zinazodaiwa kutolipiwa kodi na kukosa STIKa za TRA wakiwa nchini ya Ulinzi mara baada ya kufikiwa kituo cha polisi kati,jana jioni jijin Dar.

Mitambo ya kuzalisha umeme (System Turbine, no 2) yawasili Kinyerezi II

$
0
0
Mitambo ya kuzalisha umeme (System Turbine, no 2) kwa ajili ya mradi wa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi II iliingia nchini kupitia Bandarini Oktoba 16, 2017 na leo hii Novemba 03, 2017 imetolewa Bandarini na hivi sasa inaelekea kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi Kinyerezi II (MW 240) Jijini Dare es Salaam.

Mradi huu wa Kinyerezi II uliwekwa jiwe la msingi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli achi 16, 2016. Mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 2018. 
Moja ya Gari iliyobeba Mitambo ya kuzalisha umeme (System Turbine, no 2) kwa ajili ya mradi wa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi II ikielekea eneo Kutakapojengwa Mradi huo.

MSICHANA WA KITANZANIA KUIWAKILISHA NCHI MKUTANO WA DUNIA WA VIJANA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Deusdedit Kaganda akimkabidhi Bendera ya Taifa, Bi Hilda Jacob Mwakatumbula ambaye amechaguliwa na Kamati ya Kimataifa ya Vijana kuiwakilisha Tanzania kwenye Mkutano wa Dunia wa Vijana utakaofanyika Belize, Amerika ya Kati kuanzia tarehe 6 hadi 9 Novemba, 2017. 

Bi. Mwakatumbula ambaye anachukua Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Waseda nchini Japan amepata ufadhili wa kushiriki Mkutano huo kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto). Akimkabidhi Bendera hiyo, Bw. Kaganda alimwomba Bi. Mwakatumbula kuwa Balozi mzuri wa Vijana wa Kitanzania kwenye mkutano huo hususan katika kutekeleza Malengo Endelevu ya Maendeleo. 
Picha ya pamoja 

SPIKA ATANGAZA JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI LIPO WAZI

CWT RUVUMA .WALIMU FANYENI KAZI KWA MAADILI

$
0
0
Mjumbe wa kamati kuu taifa kutoka chama cha walimu Mkoa wa Ruvuma Mwalimu Sabina Lupukila ametoa wito kwa walimu wote nchini kuacha tabia za kutembea na wanafunzi kwani kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya kazi na kulete taswira mbaya kwa jamii kwani mwalimu ni kioo cha jamii,habari kamili hii hapa video yake.

MAKAMPUNI YA BIMA YATAKIWA KUSOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI

$
0
0
Na Oyuke Phostine

Makampuni ya bima nchini yametakiwa kusogeza hudama za bima ya Maisha kwa wanananchi ili kuchangia ukuajia wa uchumi wa nchi hususan katika kipindi hiki cha uchumi wa viwanda. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji alipokuwa akifungua semina ya kimataifa ya Bima ya Maisha inayofanyika jijini Arusha.

Sekta ya bima nchini, kama ilivyo kwa mataifa mengine Afrika, inakumbwa na changamoto nyingi zikiwemo mwamko mdogo wa wananchi kununua bima, huduma kutofikia wananchi, na elimu ndogo ya masuala ya bima kuhusu bidhaa tofauti tofauti za bima.

“Tanzania tuna idadi ya watu takriba ni milioni hamsini, hili ni soko kubwa sana na fursa kwa makampuni ya bima kuwekeza, kwa maana hiyo mna deni la kuwafikia wananchi kwa kuwa na bidhaa za bima zenye ubunifu na zenye kutatua matatizo yao” amesema Dk. Kijaji.

Serikali imejidhatiti katika kuimarisha sekta ya bima kwa kuweka mipango madhubuti ya kuendeleza soko la bima kwa kurejesha imani ya wananchi juu ya huduma za bima zinazotolewa na makampuni yaliyosajiliwa nchini.

“Hili litachangia katika kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania, kwani ni lazima kisheria makampuni ya bima nchini kuwaajiri wazawa na tayari serikali ina vyuo vinavyotoa taaluma hii ya bima. Hivyo nina uhakika kuwa nguvu kazi yenye uweledi wa masuala ya bima inapatikana nchini” amesema Dk. Kijaji.

Pia Dk. Kijaji amitaka Mamlaka ya Bima nchi kupitia Kamishna wa Bima Nchini Dk. Baghayo Saqware kushirikiana na makampuni yenye usajili nchini kuhakikisha biashara ya bima inakuwa imara na yenye kunufaisha watanzania kwa sababu makampuni haya yanakusanya amana kutoka kwa watanzania.

Mkutano huo wenye dhima ya “Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Nini mchango wa bima ya maisha katika kuleta maendeleo endelevu” umewawezesha washiriki wote wa sekta ya bima kutoka Afrika na nje ya Afrika kujadili mada mbalimbali ili kuboresha soko la bima nchini na Afrika kwa ujumla.

RC Rukwa awaasa watumishi kutotumia vyeo kuwanyanyasa wananchi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo amewaasa watumishi wa mashirika ya umma na wakala wa serikali mkoani Rukwa kutotumia vyeo vyao kuwanyanyasa wananchi wanaowahudumia na badala yake wawasaidie kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa bila ya kujali, rangi kabila, dini na hali zao kiuchumi.

Amesema kuwa watumishi wa serikali ni watumishi wa wananchi hivyo wanapaswa kujituma bila ya kujali vyeo vyao kwani vyeo hivyo havitakuwa na maana ikiwa wananchi hawapati huduma wanayoitarajia kutoka katika serikali waliyoiweka madarakani.

“Sisi viongozi wa Serikali lazima tufanye kazi kwa kujituma na kujitoa na tukumbuke kuwa sisi ni watumishi tu, sio watu wa kujivuna ama wabinafsi na kujinadi kwa vyeo vyetu kwamba mimi meneja, daktari sijui nani, vyeo vyetu vitakuwa na maana pale tu tunapokwenda kwa wananchi na kuwapa huduma” Alieleza.

Na kuongeza kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kuhakikisha kuwa kila kiongozi anayehudumia wananchi anakuwa mtumishi wa wananchi na kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kuonya vikali watumishi wanaowahudumia wananchi kwa kutumia lugha chafu.   

Ameyasema hayo kwenye kikao cha muda mfupi kilichowajumuisha viongozi kutoka katika mashirika ya umma, wakala na mamlaka mbalimbali za serikali zilizomo Mkoani humo ili kufahamu matatizo wanayokumbana nayo pindi wanapotimiza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi.

Sambamba na hayo Mh. Wangabo amewataka watumishi wote Mkoani humo kuzingatia muda na kutekeleza kwa wakati mipango waliyojiwekea ili kazi zizae matunda na kutoa taarifa sehemu husika bila ya kusubiri kusukumwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akifafanua namna mtumishi anavyotakiwa kuwajibika pindi anapowahudumia wananchi  (aliyekaa) kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa David Kilonzo. 
 Viongozi wa mashirika ya ya umma na mamlaka mbalimbali za seikali Mkoani Rukwa Waliohudhuria kwenye kikao hicho kilichowakutanisha wakuu wa mamlaka na mashirika ya umma. 

SHULE YA MSINGI YA NEW VERSION YANG'ARA MATOKEO YA DARASA LA SABA

$
0
0
Shule ya Msingi ya New Version ya Kibaha kwa Mathiasi imefanikiwa kung'aa katika mtihani wa taifa darasa la saba mwaka huu kwa kushika nafasi ya pili kiwilaya, nafasi ya tano kimkoa huku kitaifa ikishika nafasi ya 96 na kuwa na wastani wa 205. 1765.

Shule hiyo ya New Vision kwa mwaka huu imepanda kutoka nafasi ya sita iliyoshika mwaka jana katika mtihani wa taifa wa darasa la saba na kuwa ya pili kiwilaya huku kimkoa ikishika nafasi ya 22 na kuwa ya 702 kitaifa huku ikiwa na wastani wa 163.0714.

Mkurugenzi wa shule hiyo inayotoa elimu yake kwa lugha ya Kiingereza, Andrea Mfuko alisema siri kubwa ya ufauli kwa watoto katika shule hiyo ni mfumo mzuri wa ufundishaji na mazingira ya watoto kujisomea kwa utulivulisema kwani kila Mwalimu anahakikisha kabla ya kuhama topic moja kwenda nyingine ni lazima mtoto awe ameelewa vema, kile alichofundishwa.

Amesema mbali na masomo, Wanafunzi wa New vision wanafundishwa kujielewa, kujitambua na kujua wajibu walionao kwa jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla.
Wanafunzi waaliomaliza darasa la saba mwaka 2017 wa shule ya msingi ya New Version wakiwa wamembeba mwanafunzi Lawrence Lucian aliyeongoza kwenye matokeo ya Darasa la Saba shuleni hapo.

MAHAFALI YA KUMI NA MBILI (12) YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

MKUTANO MKUU WA KWANZA WA MWAKA WA WADAU WA MFUKO WA WCF KUFANYIKA NOVEMBA 29 - 30 2017 JIJINI ARUSHA

ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU

$
0
0
Askofu “Atallah Hanna’ ambae ni Askofu Mkuu wa Sebastia wa Kanisa la Orthodox la Kigiriki, amesema: "Uwepo wa Ukristo katika nchi hii takatifu (Palestina), ni uwepo wenye historia ya tangu, kwani Ukristo haukuja Palestina kutoka mahali popote duniani, bali umesambaa kutokea hapa katika ardhi takatifu aliyoichagua Mungu,ili iwe ni sehemu ya upendo wake kwa wanadamu".

Askofu “Hanna”ameongeza kusema kuwa, "Tunatoa wito kwa watoto wetu wasome historia ya kanisa lao na waelewe urithi wao wa kiimani, kibinadamu, kiroho na kiuzalendo. Haifai kuwa hawaelewi historia na mizizi yao ya kina (asili yao) iliyo katika udongo wa nchi hii takatifu. Tunaamini kanisa moja ambalo ni chuo kikuu kitakatifu cha kiutume, lakini pia tunajivunia kuwa sisi ni wana wa nchi takatifu ya Palestina. Tunajivunia kuwa sisi ni wa nchi hii, historia yake, urithi wake na utambulisho wake, huku tukitetea haki ya masuala ya wananchi wake."

Aidha amesema "Katika kumbukumbu ya azimio baya la Balfour, upendeleo wetu utabaki daima na wananchi wa Palestina na kwamba kuvamiwa Palestina kumetokana na azimio la Balfour na wala hakukutokana na Mungu. Hatuwezi kuwakubalia wale wanaomnasibisha Mungu na jambo ambalo sio lake, wala kuwakubalia wale wanaofasiri Biblia kama wapendavyo, hatimae wakasema na kuhalalisha alichokiharamisha Mungu.” 

“Tunaamini kwamba Mungu hakuhalalisha mauaji, vurugu, kuhamisha watu kwa nguvu na matendo ya kukiuka Utu na hadhi ya kibinadamu, tunaamini kwamba maadili haya yapo katika dini tatu za kumpwekesha Mungu. Katika imani yetu ya kikristo na kwa mujibu wa maadili yetu ya kiinjili, tunasema haifai kudhulumiwa au kukandamizwa binadamu yeyote, yale yaliyotokea mwaka 1948 ya kuwatoa kwa mabavu Wapalestina katika makazi yao, miji yao na ardhi yao takatifu, sio haki kwa njia yoyote.”

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUZIA BENKI YA DAMU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.
 Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem aliyesimama akiongea na baadhi ya  wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam , katikati waliokaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Lwezimula.
 Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem kulia akimkabidhi zawadi ya mchango mkubwa katika Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu kushoto wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es Salaam akiwa na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MUFINDI YANUNUA MAGARI KWA MAKUSANYO YA NDANI

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imekamilisha mpango wake wa kununua Magari Mawili (2) mapya kwa kutumia sehemu ya mapato yake ya ndani ya mwaka wa fedha 2016-2017 uliyokamilika mwezi juni mwaka huu.

Taarifa ya kitengo cha habari na Mawasiliano cha Halmashauri hiyo, imeyataja Magari hayo kuwa ni Toyota Landcruiser Standard kwa gharama ya Sh. 187,680,373.11na Toyota Hilux –Double Cabin kwa gharama ya Sh. 93,450,713, ambapo Magari yote mawili yamegharimu Sh. 281,131,086.11.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Magari hayo yamenunuliwa ili kukabiliana na changamo ya uchakavu na upungufu mkubwa wa Magari uliyopo na kutanabaisha kuwa kati ya Magari hayo, gari ya kwanza itatumiwa na Ofisi ya utala ambayo wakati wote hutakiwa kufika kila kona ya eneo pana la Halmashauri lenye Majimbo mawili kata 27, Vijiji 121 na Vitongoji 562 kusimamia shughuli za maendeleo, huku gari ya pili ikinunuliwa mahususi kwa shughuli za kukusanya Mapato.

Aidha, Mchakato wa Manunuzi wa Magari hayo ambayo ni moja kati ya nyenzo muhimu za kuharakisha maendeleo katika Halmashauri ya Mufindi, umefanyika kwa kufuata taratibu zote za manunuzi ya Umma, ikiwa ni pamoja na kuomba kibali cha kufanya manunuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakati mchakato mzima wa kuyanunua ukitekelezwa na taasisi za zilizokasimiwa jukumu la manunuzi ya Umma, ambazo ni TEMESA na GPSA.
Afisa manunuzi wa halmashauri Mr. Katunzi akikabidhi funguo za gari pamoja na nyaraka za umiliki kwa Mkurugenzi Mtendaji ambapo naye atakabidhi kwa Mwenyekiti wa Halmashauri.
 Mkurugenzi Mtendaji Prof. Riziki Shemdoe, kulia katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halamshauri Festo Mgina mara baada ya kupokea nyaraka za umiliki wa Magari.

DC KIBAHA AUAGIZA UONGOZI WA KAMPUNI YA YAPI MARKEZI KUTATUA KERO ZA WAFANYAKAZI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akimtambulisha meneja mwajiri wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki kwa vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani wakati akifanya mkutano nao. Mkuu huyo wa wilaya alifanya ziara hiyo kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA - KAJUNASON/MMG - KIBAHA.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akijadiliana machache na meneja mwajiri wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki wakati alipofanya mkutano wake na vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akitolea ufafanuzi wa mambo machache kwa vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani.
Vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Asumpter Mshama.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akaribishwa na uongozi wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki ili aweze kuongea na vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UZALENDO KWANZA WAUNGANA NA MSAMA AUCTION MART KUTOKOMEZA KAZI FEKI ZA WASANII NCHINI.

$
0
0


Kikundi cha Uzalendo Kwanza ikishirikiana na Kampuni ya Msama Auction Mart wameamua kuungana kwa pamoja katika kutokomeza kazi Feki za Wasanii hapa nchini.

Uzalendo Kwanza kupitia kwa Mwenyekiti wake, Steve Nyerere wameungana na Msama Auction Mart pamoja na kushukuru juhudi zinazofanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya yakukamata Walanguzi wa kazi hizo.

Steve Nyerere amesema wafanyabiashara katika Maduka Makubwa ya Filamu vifaa vya Soka wanafanya biashara hizo lakini hawalipi Kodi, hivyo wanawapongeza Msama Auction na TRA kuunga mkono  jitihada zakutokomeza wizi huo.

"Wamejiajiri katika Taifa la Watanzania, wakipata faida kubwa, Kodi na Mapato makubwa yangepatikana", amesema Steve.Ameongeza kusema kuwa "Msama hatoshi, TRA peke yake hatoshi; Mhe. Rais hatoshi kama Wasanii wenyewe hatutounga mkono jitihada hizi".

Pichani kati ni Mwenyekiti wa kikundi cha Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja  na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini,kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart ,Alex Msama.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart ,Alex Msama akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi mapema leo,namna wanavyoshiriki zoezi la kukamata kazi feki za Wasanii,sambamba na wakwepa kodi kupitia kazi wasanii.

Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza,alipokuwa akizunguma nao mapema leo jijini Dar,
,wakiunga mkono kampuni ya Msama Auction Mart pamoja  na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kazi nzito wanayoifanya ya kukamata Walanguzi wa kazi za wasanii hapa nchini.


Baadhi ya Wasanii mbalimbali wa filamu hapa nchin walipokuwa wakifuatilia mkutano huo mapema leo jijini Dar.



MOHAMMED DEWJI APONGEZA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KUFUFUA VIWANDA

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji akizungumza katika mkutano wa Global Business Forum 2017 kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika, mkutano huo wa siku mbili umefanyika Dubai, UAE na kuhudhuriwa na watu 5860 wakiwepo viongozi wa serikali za nchi za Afrika na wafanyabiashara. (Picha na Clouds Media)

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amepongeza uamuzi wa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kufufua viwanda ambavyo vilikuwa havifanyi kazi.

Dewji ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa Global Business Forum 2017 (GBF) kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Mfanyabiashara huyo ambaye anamiliki viwanda 41 alisema uamuzi aliochukua Rais Magufuli ni mzuri hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati.

Dewji alisema kampuni yake ya MeTL Group itaendelea kushirikiana na serikali na katika kipindi cha miaka kadhaa ijayo amejipanga kuhakikisha anatoa ajira kwa Watanzania 100,000 jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa nchi na kwa wananchi..

PROFESA MWAKALILA AWAASA WANAFUNZI MWALIMU NYERERE KUACHANA NA SIASA WAKIWA SHULENI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKUU wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo kigamboni,Profesa , Shadrack Mwakalila  ameagiza wanafunzi wa chuo hicho, waliojiunga katika mwaka wa Masomo wa 2017 kutojiusisha na masuala ya siasa pindi wanapokuwa chuo na badala yake wazingatie katika suala zima la taaluma ili waweze kupata kile kilicho wapeleka chuoni hapo.

Profesa Mwakalila amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Mwaka wa kwanza juu ya nini wanatakiwa kufanya wakiwa chuoni hapo na kutambua nini cha msingi kilichowaleta.


"Hapa sio mahali pakufanya Siasa ni sehemu mliyokuja kuchukua taaluma, kamwe msikubali wanasiasa kuwatumia kwa ajili ya maslahi yao kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmepoteza lengo ambalo limewaleta hapa katika kufanikisha malengo yenu ya kitaaluma"amesema Profesa Mwakalila.


Profesa Mwakalila ameongeza kuwa kama wanavyojua chuo hicho kimetokana na Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius .K. Nyerere hivyo wanapaswa kufuata maadili na kuwa waadilifu ili  kumuenzi muasisi Baba wa Taifa ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa sehemu hiyo iweze kupika viongozi wenye maadili mema kwa Taifa hili.


alimaliza kwa kutoa wito kwa wote waweze kukazana katika masomo yao hili waweze kuwa alama ya chuo hicho pindi wanapomaliza masomo yao na kufika hapo kwao isiwe majuto.
 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam,Profesa. Shadrack Mwakalila akizungumza na Wanafunzi wa Chuo hicho wa Mwaka wa kwanza ambao wamechaguliwa katika muhula wa Masomo 2017 kwa ngazi ya Cheti, Astashahada na Shahada juu ya umuhimu wa kufuata Maadili.
 Mshauri  wa Wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akikazia jambo juu ya kuwa na maadili shuleni
 Sehemu ya Wanafunzi wa wapya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila.

TFDA YAPATA CHETI CHA UBORA WA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA 1SO 9001.2015

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imepata cheti cha mfumo wa uhakiki wa Ubora wa Huduma cha Kiwango cha kimataifa cha ISO  9001.2015  na kufanya mamlaka hiyo kuwa ya pili katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema kuwa mafanikio ya TFDA ni kutokana na kazi  wanayofanya katika udhibiti dawa na chakula kwa ajili ya kutumia bidhaa zenye ubora.

Amesema kuwa TFDA ni mamlaka ambayo inagusa masilahi ya kila mtu na hakuna asiyetumia bidhaa zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo ikiwa ni kulinda afya za wananchi ambao wanaweza kufanya kazi na kuiletea taifa maendeleo hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Dk. Ndugulile amesema kuwa TFDA kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa chakula, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ni utekelezaji wa vitendo wa azma ya serikali ya awamu ya tano chini uongozi mahiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha upatikanaji wa wa huduma bora za afya hususani  upatikakanaji wa dawa , vifaa tiba na vitandanishi.

Aidha amesema nyenzo zilizofanya mafanikio katika udhibiti ni maamuzi ya menejimenti zaidi ya miaka 10 wa kudhamiria kutekeleza mfumo wa uhakiki ubora wa huduma .Nae Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema kuwa katika kuongeza huduma za udhibiti kwa wananchi wameanzisha ofisi saba za kanda ambazo zitahudumia katika mikoa iliyopo katika kanda hizo.

Sillo amesema kuwa mamlaka imekuwa ikitekeleza mfumo wa uhakiki ubora kuanzia mwaka 2005 baada ya kufanya tathimini ya namna bora ya kufanya shughuli za udhibiti kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa wateja.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo wakiwa wameshishika cheti cha mfumo wa Uhakiki Bora katika Kiwango cha Kimataifa Cha Iso 9001-2015.
Meneja Uchunguzi wa Dawa na Vipodozi Dkt. Yonah Hebron akitoa maelekezo mbele ya Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitembelea maabara katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo (wakatikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya TFDA Dkt Ben Moses.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa kwenye piha ya pamoja wakati akizindua CHETI CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015 tukio lililofanyika katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU AWASILI TOKEA NCHINI CANADA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutokea nchini Canada, Novemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutokea nchini Canada, Novemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TOT PLUS WAJIFUA KUIPUA NYIMBO TATU MPYA UKIWEMO WA KUMUUNGA MKONO JPM KATIKA VITA YA KUTETEA RASILIMALI ZA NCHI

$
0
0
NA BASHIR NKOROMO.

Kundi la Tanzania One Theatre (TOT Plus), limo kambini Wanamuziki wake wakijifua vikali katika mazoezi ya nyimbo tatu ambazo kundi hilo litaziipua hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya nyimbo hizo, Mkurugezi wa TOT Plus inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gasper Tumaini amezitaja nyimbo hizo kuwa ni 'Tumuunge mkono JPM', 'Amani ya Tanzania' na Hongera awamu ya tano'.

Tumaini amsema, wimbo wa 'Tumuunge mkono JPM' ni wa kuwahamasisha Watanzania popote walipo kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika vita ya uchumi anayoongoza kwa kuhakikisha inaziba mianya inayotishia upotevu au matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

"Kama unavyoona Rais tayari ameshaamua kwa dhati kupigana katika vita ya kubana mianya inayotishia upotevu au matumizi mabaya yanayofanya na baadhi ya watu kutumia rasilimali za nchi vibaya kwa kujinufaisha wao huku taifa likiendelea kuwa masikini

Hii siyo vita ndogo, ni kubwa sana inayohitaji ujasiri na ari kubwa ya kujituma, hivyo ni lazima Watanzania wote tumuunge mkono ili asiyumbishwe na waliokuwa wanajinufaisha na rasilimali hizi", alisema Tumaini wakati wa mazoezi ya nyimbo hizo kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM Mwinjuma, Mwananyamala, Dar es Salaam.
Mwanamuziki nguli Juma Abdallah 'Jerry' akikipapasa kinanda kwa mkoni mmoja kuonyesha umahiri wake, Kundi la TOT Plus lilipokuwa katika mazoezi ya nyimbo tatu, leo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala Dar es Salaam
Waimbaji Neca Twalib aliyechukua nafasi iliyoachwa na aliyekuwa mwimbaji nguli na Mkurugenzi wa TOT Plus Marehemu Kampteni John Komba, akiimba na mwenzake Corobian Mkinga wakati wa mazoezi hayo
Mkurugenzi wa TOT Plus Gasper Tumaini (mwenye suti) akizungumza na baadhi ya wadau waliofika kushuhudia mazoezi hayo.
Mwimbaji nguli Hadija Kopa na wenzake wakiimba wakati wa mazoezi hayo.


Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images