Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1995 | 1996 | (Page 1997) | 1998 | 1999 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya ukaguzi wa masuala ya kazi na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.

  Mavunde alianza ziara hiyo katika shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM) ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na kutoa maagizo kwa Menejimenti ya Uongozi wa Shule hiyo kutoa mikataba kwa wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini kinavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kuagiza Taasisi za Serikali kuchunguza malalamiko juu ya unyanyasaji kwa wafanyakazi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa menejimenti.

  Mavunde pia alitembelea Kiwanda cha China Paper Corporation ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na kuiagiza Menejimenti ya Kiwanda hicho kuhakikisha sheria za Kazi zinafuatwa kwa kutoa Mikataba kwa wafanyakazi wote na kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa ikiwemo usalama wa mazingira ya kufanyia kazi.

   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua nyaraka mbalimbali alipotembelea Kiwanda cha China Paper Corporation.

    Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua kiwanda cha China Paper Corporation.

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akizungumza katika kiwanda cha China Paper Corporation.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0


  Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

  TANZANIA imezidi kupata neema kutoka Jumuiya ya Kimataifa ambapo Novemba 2, 2017, Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 50, takriban Shilingi bilioni 130 kwa ajili ya kufadhili Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini unaoendeshwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Mkataba wa Makubaliano hayo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Neven Mimica.

  Msaada huo umelenga kuwasaidia raia wa Tanzania kufikiwa na huduma nafuu ya nishati ya umeme kwa kupanua uwezo wa gridi ya Taifa pamoja na mtandao wa usambazaji umeme.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada huo mkubwa utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa uhakika utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu wake.“Umoja wa ulaya ni wadau wetu muhimu wa maendeleo kutokana na misaada muhimu na mikubwa wanayotupatia, na kusadia agenda yetu ya maendeleo” alisema Bw. James

  Alisema kuwa kiasi cha msaada wa Euro milioni 50 kilichotolewa na Umoja huo bila masharti yoyote si kidogo, na kwamba kitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme utakaochangia kuimarika kwa sekta ya viwanda itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
  Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza kwa makini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akitoa maelezo ya ujio wa ugeni huo kuwa ni neema kwa nchi ya Tanzania kwani Umoja wa Ulaya wametoa msaada wa Euro Milioni 50 utasaidia vijijini 3600 nchini kupata umeme.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) na akimweleza jambo Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Mr. Neven Mimica wakati wa hafla fupi ya Umoja wa Ulaya (EU) kutiliana saini makubaliano ya msaada wa Euro milioni 50 kwa ajili ya kusaidia usambazi wa umeme vijijini kupitia Mradi Kabambe wa Kusambaza umeme Vijijini (REA).
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akiwa pamoja na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Bw. Neven Mimica wakisaini Mkataba wa msaada wa fedha za kusaidia usambazaji wa umeme Vijijini (EURO milioni 50) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Mr. Neven Mimica, wakibadilishana hati za makubaliano ya msaada wa ruzuku ya kiasi cha EURO Milioni 50 katika ukumbi wa wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  Ndugu Wanajumuiya, 

  Kwa masikitiko makubwa Dr. Lindah Mhando wa State College, PA anatangaza kifo cha mdogo wake HAPPY OKOTH kilichotokea Dallas, TX. October 27, 2017.
  Marehemu ameacha :
  Mama yake Mrs Elizabeth Okoth
  Mume wake: Pastor Steven Momoh
  Watoto watatu: Gideon, Desire Na Delight. 
  Kaka: Mike Wilfred
  Dada: Dr. Lindah Mhando 
  Mdogo: Lilian Wilfred

  Mipango y'a mazishi ina endelea kufanyika. Na marehemu anatarijiwa kuzikwa Dallas Texas 
  Tarehe: 10 ( wake keeping) 11 mazishi na tarehe 12. Ibada ya shukran 
  Taarifa zaidi zitafuata baadaye.
  Tafadhali wasiliana na:

  Pastor Steven Momoh 214 830 8459 (husband)
  Prof. Peter Mhando 8144043781
  Jessica Kataraiya 2147736697
  Pastor Absalom 2145547381
  Ben Kazora 12698730937


  0 0
 • 11/02/17--14:32: IN LOVING MEMORY
 • MWL. STEPHEN ZENO MTEMI CHALU 
  (1935 – 2014)

  Daddy, today it is exactly 3 years since you well called by God.

  The years we've shared have been full of joy. The memories we've made will go on and on. We haven’t stopped crying since you went away. You lit up our lives, our hopes, and our dreams. You opened our eyes to see what it all means.

  So now that you're gone how can we forget; No one know how much we miss you, Life has never been the same.  

  Deeply missed and remembered by your wife, sons, daughters, in laws, grandsons, granddaughters, grand grand daughter, relatives, friends and neigbours. (RIP MWL CHALU!)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyo chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya msingi Nguzo mbili. 

  Akizungumza wakati wa ziara yake katika shule hiyo Mheshimiwa Robert Gabriel alisema kuwa ameridhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi wa madarasa kwa ubora wa hali ya juu katika shule hiyo. " Inashangaza sana kuona maeneo mengine wanatumia fedha zote kiasi cha shilingi 20 milioni katika ujenzi wa darasa moja lakini kuna mapungufu mengi hivyo lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha katika miradi ya Serikali"Alisema Lughumbi. 

  Akiwa shuleni hapo Mkuu wa Mkoa ameagiza wakurugenzi kuunda na kutumia vikundi vya ujenzi vilivyo katika maeneo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa pia kuishirikisha jamii ili kupunguza gharama kwa serikali na hatimaye fedha zinazobaki ziwezekufanya mambo mengine katika huduma za jamii. 
   
  Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongozana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Geita na Wilaya ya Geita wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyotekelezwa kwa mpango wa lipa kwa matokeo Halmashauri ya Mji Geita.
   

  Katika hatua nyingine Mhandisi Robert Gabriel aliutaka uongozi wa Shule ya Msingi Nguzo Mbili kusimamia suala la usafi na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha anasimamia uimarishaji wa miundombinu hiyo ambayo mingine imeanza kupasuka. Aidha, ameagiza shule hiyo kupelekewa miundombinu ya maji ili vyoo vilivyojengwa vianze kutumika badala ya kufungwa.

  Pamoja na kutembelea Shule ya Msingi Nguzo Mbili Mkuu wa Mkoa pia ameitembelea shule ya Sekondari na kukagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa matokeo. Shule ya Msingi Nguzo mbili imejenga madarasa nane kwa kutumia shilingi milioni 13 kwa kila darasa, Ofisi 4, kisima cha maji na vyoo vya kisasa pamoja na ukarabati wa madarasa mengine katika shule hiyo kutokana na fedha iliyobaki katika bajeti ya darasa moja. 

  Mkoa wa Geita una upungufu wa vyumba vya madarasa 8600 hivyo serikali imeandaa mpango kabambe wa kutokomeza tatizo hili kwa kushirikiana na jamii na wadau wote wa Mkoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
  Mhandisi Robert Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Mkoa na Wilaya Geita na kamati ya usalama ya Mkoa wakikagua miundombinu ya shule ya Msingi Nguzombili wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa Halmashauri ya Mji Geita.


  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akimkabidhi Cheti cha Shukrani Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, kutoka kwa Shirikisho la Vyama vya wenye ulimavu Tanzania, SHIVYAWATA, wakati wa Tamasha la Sita la Watu wenye Ulemavu, lililofanyika kwenye ukumbi wa LAFP, Makumbusho jijini Dar es Salaam, leo Nov 2, 2017. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, akizungumza wakati wa Tamasha hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Taifa, Ummy Nderiango.
  Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, akizungumza wakati wa Tamasha hilo.
  Meneja wa Kitengo cha Kujenga uwezo wa Asasi, kutoka Taasisi ya The Foundation for Civil Society, Edna Chilimo, akionyesha Cheti alichokabidhiwa katika Tamasha hilo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0

  Leo majira ya saa kumi jioni Mwanariadha Ismail Juma Gallet amepata ajali ya pikipiki kugongana uso kwa uso na Fusso na kufariki papo hapo.

  Ajali hiyo ilitokea Kijijini kwao Gendi Wilaya ya Babati - Mkoa wa Manyara.

  Mwezi uliopita Ismail alivunja rekodi ya taifa kwa kukimbia dakika 59 sekunde 30 katika mbio za Nusu Marathon ambazo ni 21 Kilometres.

  Marehemu Ismail Juma alikuwa kati ya wanariadha ambao majina yao yameshawasilishwa ofisi za TOC tayari kwa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Madola (2018 Gold Coast Commonwealth Games).

  Tunasubiri taratibu zingine kutoka kwa familia ya wafiwa. Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Murara Babati.

  Habari hizi zimethibitishwa na;  

  1) Mzazi wa Marehemu
  2) Uongozi wa Riadha Manyara

  Kwa niaba ya Chama cha Riadha Tanzania natoa pole kwa familia yake, tunakiri kupata pengo ambalo halitazibika.

  Huu ni msiba wa taifa, alikuwa aende kuitetea Tanzania kwa kusaka medali na kupeperusha bendera ya taifa; lakini Mungu amemwita mapema.

  RIP Champ....

  Wilhelm F. Gidabuday,
  Katibu Mkuu,
  Chama cha Riadha Tanzania.

  0 0

  Na Dotto Mwaibale, Bukombe Geita

  WAKULIMA wilayani Bukombe Mkoani Geita wameiomba Serikali na wasambazaji wa mbegu bora za mahindi ya WEMA 2109 yanayostahimli ukame kufikisha mbegu hizo wilayani humo ili kuweza kutatua changamoto ya mavuno kidogo wanayoyapata kila mwaka kutokana na mabadiriko ya tabia nchi na wadudu.

  Ombi hilo limetolewa na wana Kikundi cha Igembensabho kwenye Kijiji cha Kabagole Kata ya Busonzo wilayani Bukombe mkoani Geita wakati wakipokea mbegu bora za mahindi yaliyozalishwa na Mradi wa WEMA kwa ajili ya kupanda kwenye shamba darasa la kikundi hicho ili waweze kuyalinganisha na aina za mahindi wanayolima kila mwaka na mahindi hayo yenye sifa ya kustahimili ukame yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)

  Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi hicho, Adam Kasalamsigwa alisema kuwa kutokana na sifa walizoambiwa na wataalamu kwenye mahindi hayo yatakuwa mkombozi kwa wakulima wengi kutokana na aina zingine za mahindi waliyozoea kupanda kushindwa kutoa matokeo waliyokuwa wakiyatarajia baada ya mvua kukata mapema kabla mahindi hayajazaa.

  “Tunashukuru mmetuletea mbegu hizi ili tufanye majaribio na kuona jinsi mahindi haya yanavyostahimili ukame lakini mmetuambia tayari mmeshayafanyia majaribio kwenye maeneo mengine ya Tanzania na kuonyesha mafanikio makubwa hivyo hatuna sababu ya kusubiri hadi msimu ujao tuleteeni mbegu hizo tununue na kupanda” alisisitiza Kasalamsigwa.
  Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akimkabidhi mbegu ya mahindi ya Wema 2109, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya kwa ajili ya kupanda katika shamba darasa katika Kijiji cha Msasa kilichopo Kata ya Runzewe wilayani humo leo. Wengine kutoka kulia ni Mtafiti wa Mazao ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula na Mtafiti, Dk. Beatrice Lyimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
  Maofisa Ugani wakiandaa shamba darasa la mahindi ya Wema katika Kijiji cha Kabagole kilichopo Kata ya Busonzo litakalosimamiwa na Kikundi cha Igembensabho.
  Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya, akizungumza na wakulima wa Kikundi cha Igembensabho.


  0 0

  NA MWANDISHI MAALUM – KATERERO

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhanga Mpina amewataka wafugaji nchini kutembea kifua mbele kwa kumpata yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Mifugo, Mpina ameyasema hayo leo aliposhiriki katika zoezi la kupiga chapa Mifugo katika Kijiji cha Kyelwa kilichopo katika kata ya Katerero halimashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera, na kuwataka viongozi kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kuepuka hujuma na ubaguzi kwa wafugaji.

  Waziri Mpina alipofika katika kata ya Katerero aliwakuta wafugaji wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi la uwekaji alama katika mifugo yao na kushiriki zoezi hilo kwa kuonyesha msisitizo.

  Mara Baada ya kushiriki zoezi hilo, Waziri Mpina aliwataka wafugaji hao kuendelea kujitokeza kwa wingi na kuleta mifugo yao kupigwa chapa na kusema kuwa zoezi hilo ni la manufaa na faida kwa wafugaji kwani litaweza kuwasiadia kuhepuka maambukizi ya magonjwa ya wanyama kwa mifugo yao kuto kuchanganyikana na mifugo mingine sambamba na kusaidia upotevu wa mifugo.

  Akiongea katika zoezi hilo diwani wa kata ya Katerero Bw. Nuru Abdul Kabendera alisema kuwa, amefurahishwa na ziara ya Waziri Mpina katika kata ya katerero kwani ni mara ya kwanza kwa kata hiyo kupata ugeni kutoka katika ngazi ya juu ya serikali na kumuomba Mpina kupitia Wizara yake kutatua changamoto inayoikabili kata hiyo la josho la kuoshea ng’ombe ambapo Waziri Mpina amehaidi kuitatua.
  Waziri Mpina na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Bukoba wakielekea katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe katika kata ya katerero kijijini Kyerwa leo.
  Katika picha ikionekana sehemu ya ng’ombe aliyepigwa chapa katika kata ya Katerero kijijini Kyerwa leo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi. Saada Malunde baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamuro, wengine katika picha ni askari wanyamapori wa pori hilo.
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi Saada Malunde wakizungumza baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamuro.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema hatavumulia kuwa na watumishi mizigo ambao hawatimizi majukumu yao kikamilifu na kuleta mabadiliko katika sekta ya barabara ambayo ni nguzo ya uchumi nchini.

  Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wabunge wa Kamati ya kudumu Serikali za mitaa(TAMISEMI) sambamba na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kuhusu majukumu ya Wakala wa barabaraza vijijini na mijini(TARURA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma

  Mhe. Jaffo amesema Serikali ilishatoa muongozo wa malengo ya utendaji kazi katika utumishi wa umma na kuwapima kulingana na malengo yao hivyo watumishi ambao watashindwa kutekeleza na kufikia malengo waliyopangiwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kiutumishi.

  Amesema kuwa Serikali haitavumilia suala zima la ubadhilifu kwa watumishi wa umma, kwa kuwa Serikali haiwezi kumbeba mtu ambaye ni mbadhilifu kwa kuwa Serikali inahitaji kuleta mabadiliko katika utendaji kazi na kuleta maendeleo kwa jamii.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Mhandisi Victor Seif akieleza majukumu ya TARURA kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Bw.Abdul Digaga akiongea kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera amevitaka vyama vya ushirika wilayani hapo kuhakikisha wanatumia mizani yenye lengo la kumsaidia mkulima wa zao la korosho awezekupata matunda mema bala ya kulalamika kila siku hayo ameyasema wakati wa kuzindua mnada wa korosho katika kata ya nakapanya mkoani RUVUMA habari kamili hii hapa VIDEO YAKE.

  0 0

  Na David John Misungwi

  WANANCHI wa Kijiji cha Mwasonge kilichopo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa Daraja linalotenganisha wilaya hiyo na Wilaya ya Nyamagana.

  Wamesema kuwa wananchi wa wilaya hizo hususani wanaoishi mpakani wamekuwa wamekuwa wakipata adha kubwa kutokana na serikali kushindwa kujenga Daraja.

  Akizungumza Wilayani hapa leo Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Mwasonge Masumbuko Reuben alisema Tangu dunia iumbwe Serikali licha ya kutambua umuhimu wa eneo hilo lakini haijawahi kutengeneza Barabara hiyo wala Daraja.

  "Naiomba sana Serikali yangu ifike mahala waone huruma dhidi ya wananchi hawa ambao wengi wao wanakatisha hapa kwenda Buhongwa katika wilaya ya Nyamaga kilometa mbili kuliko kuzunguka Usagala ambako ni zaidi ya kilometa 10."amesema Masumbuko.

  Ameongeza kuwa eneo hilo linakuwa hatari zaidi linapojaaa maji kutokana na Mvua ambazo wakati mwingine zinanyesha mfululizo na kusababisha kutumia mitumbwi kuvusha wananchi hali inayohatarisha usalama.

  Amefafanua kuwa miaka ya hivi karibuni kutokana na eneo hilo kujaa maji pameshawahi kutokea maafa ya raia hivyo kuna kilasababu na haja ya serikali kujenga Daraja katika eneo hilo.


  0 0

  Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni umekabidhi matrekta manne (4) kwa vikundi vya uzalishaji na kuvitaka vikundi hivyo kutumia matrekta hayo kwa lengo la kuchochea kasi ya maendeleo ya kilimo kwenye maeneo yao. 

  Akikabidhi matrekta hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mh. Ramadhani Diliwa amewaeleza vikundi kuwa Halmashauri imeamua kuwapa matrekta hayo kama mtaji kutokana na utayari wa vikundi vyenyewe kwani vikundi vipo vingi ambavyo vingeweza kupewa na hivyo watambue wanao wajibu wa kuyatunza na yasiwe chanzo cha migogoro.

  Amesema kuwa Halmashauri inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya kuhudumia wananchi, matrekta yaliyotolewa wangeweza kutoa hata kwa mtu mmoja mmoja lakini yametolewa kwa vikundi ili kuchochea maendeleo na kurahisisha utunzaji wa mradi huo. 

  “kasaidianeni matrekta haya yakachochee na kuboresha kilimo, kuongeza uzalishaji na tija asitokee mtu mmoja kati yenu akawa ni chanzo cha mafarakano, Halmashauri haitavumilia tutawapokonya na kuwapa wahitaji wengine” alisema

  Ameongeza kuwa matrekta yote matengenezo yake yapo chini ya Suma JKT hivyo iwapo kutatokea hitilafu yoyote wasitumie mafundi wa mitaani kuyatengeneza badala yake yafikishwe kwa walengwa wa matengenezo, na kuwataka wasitumie mradi huo kwa lengo la kujinufaisha mtu binafsi. 
  Mwenyekiti wa Halmashauri MH Ramadhani Diliwa akimkabidhi Kiongozi wa kikundi cha umoja wa marafiki Mkata  nakala za mkataba .

   Mwenyekiti wa Halmashauri MH. Ramadhani Diliwa wa tatu kushoto akizungumza na vikundi juu ya usimamizi bora wa matrekta hayo kwa lengo la kuchochea matumizi ya zana bora zakilimo
   Mwenyekiti wa Halmashauri MH. Ramadhani diliwa akijaribu kuwasha trekta mojawapo Kama ishara ya majaribio baada ya matengenezo.
   Muendeshaji wa trekta aliyeshika usukani wa trekta akitoa ufafanuzi wa vitendo kwa Mkurugenzi Mtendaji William Makufwe mwenye shati jeupe juu ya namna ya uendeshaji wa trekta hilo

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akikagua  ujenzi wa Makao Makuu ya ofisi hiyo unaoendelea mkoani Dodoma. Ujenzi wa ofisi hiyo unatarajia kukamilika mwezi Februari, 2018.  

   Muonekano wa mbele wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma.
   Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma.
  Muonekano wa jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linaloendelea kujengwa mkoani Dodoma. Picha na Veronica Kazimoto.

  0 0
 • 11/03/17--00:39: Mkokoteni wabeba daladala
 •  Daladala likiwa limebebwa kwenye mkokoteni likitoka maeneo ya Dodoma Inn kuelekea barabara ya Dar es salaam mjini Dodoma  Novemba 2, 2017. Licha ya kusababisha mshangao kwa watuomiaji wa barabara pia lilisababisha msongamano wa magari. Picha na Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu


  0 0

  Mjumbe wa kamati kuu taifa kutoka chama cha walimu Mkoa wa Ruvuma Mwalimu Sabina Lupukila ametoa wito kwa walimu wote nchini kuacha tabia za kutembea na wanafunzi kwani kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya kazi na kulete taswira mbaya kwa jamii kwani mwalimu ni kioo cha jamii,habari kamili hii hapa video yake.

  0 0

  Na Robert Hokororo, Kishapu

  Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limekutana kwa ajili ya kuwasilisha na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo ya kata zake mbalimbali.

  Katika kikao hicho cha kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Boniphace Butondo aliipongeza Kishapu kwa kupata hati safi kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu (CAG).  Butondo ambaye pia ni diwani wa kata ya Lagana aliwataka madiwani waendelee kushikamana na kuwahudumia wananchi katika kata zao ili kuleta maendeleo katika halmashauri ya wilaya hiyo.

  Alisema ni wajibu wao kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo katika kata zao sambamba na kuendelea kuwahamasisha kuhusu kilimo hususan cha mazao yanayostahimili ukame.

  “Waheshimiwa tuwahudumie wananchi katika kata zetu na hasa ukizingatia hivi sasa Serikali inapigania katika kufufua zao la pamba katika wilaya yetu nasi tuwahamasishe kulima,” alisema.

  Aliongeza kuwa katika kikao hicho Baraza linajipima wapi wamefikia katika miradi ya maendeleo na wapi wamekwama hivyo kuweza kutatua changamoto hizo na hatimaye kusonga mbele.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa za kata.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akifungua kikao cha Baraza la Madiwani katika ukumbi wa halmashauri.
  Madiwani wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao hicho.

  0 0

  East African Community Secretariat, Bujumbura, Burundi, November 3, 2017: A two-day workshop on the Integrated Corridor Development Initiative—Lake Tanganyika Transport Programme organized by the East African Community and the Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency in close collaboration with the World Bank is underway at the Le Panoramique Hotel in Bujumbura, Burundi.

  The objectives of the workshop are threefold: to identify and support project packaging to be included in the Programme for matching with available funds and additional fund mobilization; identify the next steps to finalize programme design and move to its implementation, and; identify potential Development Partners and investors to support the programme.

  The workshop will give an opportunity to Partner States and regional organizations to highlight the projects they would like to be considered under the LTTP. In addition, Development Partners will also make presentations on projects they are committed to support.
   
  EAC Director General-Customs and Trade, Mr. Kenneth Bagamuhunda (L), making his remarks. Suiting beside him, is Burundi’s Minister of Transport, Public Works and Equipment, Hon Jean Bosco Ntunzwenimana (M) and the World Bank Country Manager in Burundi, Mr. Nestor Coffi.

  Opening the workshop, Burundi’s Minister for Transport, Public Works and Equipment, Hon Jean Bosco Ntunzwenimana, underscored the importance of infrastructure development in the region and called for more financial support from stakeholders both in public and private sectors to implement all the project under Lake Tanganyika Programme.

  Hon. Ntunzwenimana thanked the World Bank for supporting the Integrated Corridor Development initiative in and its continued commitment in supporting the implementation of the intermodal projects.

  The Minister said improving connective infrastructure and removing policy barriers to trade can help drive economic diversification, the creation of new jobs and poverty reduction. He challenged member states to improve the regional transport network, in sustainable manner because it is essential for competitive and improved integration into the region and global market.
   
  Burundi Minister of Transport, Public Works and Equipment, Hon Jean Bosco Ntunzwenimana (C) makes his official opening remarks. With him are EAC Director General-Customs and Trade Kenneth Bagamuhunda (L) and Mr. Nestor Coffi, World Bank Country Manager in Burundi.

  On his part, the EAC Director General—Customs and Trade, Mr. Kenneth Bagamuhunda, said that the Community recognizes that an integrated and efficient transport system is critical for attaining socio-economic development at the desired pace. Mr. Bagamuhunda noted that the Lake Tanganyika Transport Programme represents yet another coordinated initiative between Partners States, Development Partners and Regional Organizations to deliver an integrated, efficient and cost effective transport system in the regions.

  The Director General (DG) who represented the EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko emphasized the importance of infrastructure and efficient transport systems to the regional economic development in the EAC remains imperative.

  “It is also apparent that required investment to deliver infrastructure projects to bridge the existing infrastructure deficit at a desired pace, cannot be achieved single-handedly by respective Governments,” added the DG.

  Mr. Bagamuhunda commended the World Bank for their commitment to support the Lake Tanganyika Transport Programme. The World Bank, Country Director in Burundi, Mr. Nestor Coffi, said that the Bank recognizes that regional integration plays a critical role in connecting people to markets, both within Africa and the global economy.

  He reaffirmed Bank’s commitment to support the Riparian Countries, EAC, Central Corridor for Transport and Trade Facilitation, as well as Lake Tanganyika Authority, to design and implement infrastructure development programmes.

  0 0

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuanzisha chombo cha kuendesha na kudhibiti sekta ndogo ya usafiri majini, usalama wa meli na mazingira ya bahari ili kulinda maslahi mapana ya taifa.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wakati akijibu hoja ya Serikali kuhusu Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli wa Taifa mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma.

  Prof. Mbarawa amesema kuwa Serikali ipo kwenye mchakato wa kupeleka Muswada Bungeni wa kutunga sheria ambayo itaanzisha Shirika la Wakala wa Meli wa Taifa (NASAC) ambao utasimamia usalama wa meli na bahari zetu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa bandari zetu kama mnavyojua bandarini kumekuwa na changamoto nyingi. “Hivi karibuni tumeshuhudia upotevu wa mali na vitu vingi pale bandarini kama vile madini na vitu vingine vinaingia bila utaratibu,” amefafanua Prof. Mbarawa.

  Ameongeza kuwa Serikali imeona ibadilishe mtazamo uliokuwepo zamani kupitia SUMATRA ambayo inasimamia masuala ya nchi kavu na majini, “Serikali imeona ianzishe chombo kingine ili kiweze kujikita kusamimia masuala ya usafiri wa majini pekee na masuala nyeti hasa ya uchumi wetu kama vile madini”. Chombo kimoja cha kutoa huduma na kudhibiti sio jambo geni.

  Hapa nchini tunayo taasisi ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ambayo inatoa huduma ya anga na kudhibiti anga, hivyo Serikali inataka kufanya hivyo pia kwenye sekta ya usafiri wa majini. Hili si jambo geni kwa kuwa linafanyika kwenye nchi nyingine kama vile ya bandari ya Singapore na nchi nyingine ya India.

  Aidha, Prof. Mbarawa ametoa wito kwa wadau kushirikiana na Serikali kuanzisha chombo hiki. Pia amefafanua kuwa SUMATRA haitapokonywa majukumu yake bali nia ya Serikali ni kuitaka SUMATRA isimamie sekta ya nchi kavu tu kwa maana ya barabara, reli, magari ambayo ni sehemu kubwa na ina changamoto ambayo inahitajika kutatuliwa hivyo ijikite huko na sekta hii ndogo ya usafiri wa majini iwe na chombo kingine tofauti ili sheria iweze kutusaidia kukuza uchumi wa baharini na wa nchi kavu.

  Ni imani ya Serikali kuwa, kwa kuwa na chombo cha udhabiti cha sekta ya nchi kavu ambapo NASAC itaanzishwa kwa ajili ya sekta ya usafiri wa majini, utaziwezesha sekta hizi za majini na nchi kavu kukua vizuri hivyo kukuza uchumi wetu, watanzania watapata ajira na kampuni nyingi za meli zitaingia nchini na kufanya kazi kwa kuwa mahali ambapo hakuna udhibiti sekta haiwezi kukua, “angalieni sekta nyingine kama ya mawasiliano ambako kuna udhibiti mzuri na sekta inakua vizuri” amesema Prof. Mbarawa. Kwa mantiki hiyo, Serikali itawasilisha sheria ya SUMATRA Bungeni ili kufanyiwa maboresho ili iweze kuchangia vizuri ukuaji wa sekta ya nchi kavu na iende na wakati.

  Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigalla King amesema kuwa azma ya Serikali ni nzuri katika muendelezo wa kuhakikisha kuwa taasisi zinazoanzishwa zina mgusa mlaji na kwa manufaa ya Serikali kwa ujumla. Serikali imejibu hoja zote za wadau na Kamati yetu inaendelea kuchambua hoja hizo ili kuhakikisha kuwa inasimamia na kuishauri Serikali kwenye Muswada huu.

  Ni dhamira ya Kamati kuona kuwa biashara bandarini inaendelea kuimarishwa na kudhibitiwa; na nchi yetu sio pekee yenye bandari kwenye ukanda huu hivyo ni lengo la Kamati kuhakikisha kuwa Muswada huu unaopendekezwa unaboreshwa ili kuhakikisha una akisi ushindani. Ameongeza kuwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameelekeza udhibiti kwenye bandari yetu, hivyo huu ni mlolongo wa kusimamia na kudhibiti shughuli za uendeshaji wa bandari.

older | 1 | .... | 1995 | 1996 | (Page 1997) | 1998 | 1999 | .... | 3285 | newer