Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1988 | 1989 | (Page 1990) | 1991 | 1992 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ametoa wito kwa madiwani nchini kuanisha barabara zote zenye kipaumbele katika maeneo yao ili ziweze kuingizwa kwa urahisi kwenye mpango wa matengenezo.

  Kwandikwa ametoa wito huo mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo yenye urefu wa KM 28 ambapo pamoja na mambo mengine amesema mapendekezo yao yawasilishwe katika kamati za maendeleo za wilaya, mikoa na bodi za barabara.

  “Unakuta diwani analalamika kwamba barabara haijatengenezwa ama haifikiliwi kutengenezwa lakini ukija kufuatilia unakuta hakuna mahali popote ambapo taariza za barabara hiyo kutengenezwa zimewasilishwa”, amesema Mhe. Kwandikwa.

  Amesisitiza kuwa umuhimu wa kupeleka mapendekezo hayo kutasaidia barabara hizo kutambulika na kuondoa malalamiko kwa wananchi na baadhi ya viongozi kwa kuwa zitaingizwa katika mipango ya ujenzi kwa wakati.
  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, alipokagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri.
  Mitambo ya ujenzi ikiwa eneo la kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28, mkoani Tabora.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Octoba 30, imeahirisha kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi wa meno ya tembo ya bilioni 13 a raia wa China, Yang Feng Glan 'Malkia wa Tembo' na wenzake wawili sababu, shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi wake leo anaumwa.

  Mwendesha Mashtaka wa serikali, Wankyo Simon amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja leo kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini shahidi anaumwa, akaomba ipangiwe tarehe nyingine.

  Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko alisema hana pingamizi na kesi hiyo imeahirishwa hadi November 7 mwaka huu.

  Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Salvius Matembo na Philemon Manase.

  Washtakiwa hao, wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali.

  Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 5.4 bilioni bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

  0 0

  Serikali imetenga shilingi milioni 700 milioni kwa ajili ya kuanzisha mradi wa maji kwenye Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara utakaopunguza kero ya maji kwenye eneo hilo.

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe ameyasema hayo kwenye ziara yake ya siku moja Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. Waziri Kamwelwe alisema radi huo wa maji utasababisha asilimia 85 ya wananchi wa mji huo kupata maji ya uhakika.

  Alisema mradi huo unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa kwani fedha za mradi huo zimeshatengwa tayari. limuagiza meneja wa mamlaka ya maji safi Babati (Bawasa) mhandisi Idd Msuya kuhakikisha mradi huo wa Mirerani unaanza na kukamilika ndani ya muda wa miezi sita.

  "Baada ya Rais John Magufuli kufanya ziara yake hivi karibuni kwenye mji mdogo wa Mirerani alitoa ahadi ya kupatiwa maji wananchi wa eneo hilo hivyo nikiwa Waziri mwenye dhamana hiyo amehakikisha agizo hilo limetekelezwa," alisema Waziri Kamwelwe. Alisema baada ya Rais Magufuli kuagiza maji ya uhakika yapatikane Mirerani na zoezi la ujenzi wa ukuta wa kuzunguka machimbo ya Tanzanite kuanza, yeye kama Waziri aliamua ashughulikie suala la maji Mirerani. 
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza juu ya utekelezaji wa miradi mitatu ya maji kwenye Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Jackson Leskar Sipitieck. 

   Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary akisoma taarifa ya Wilaya hiyo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji mhandisi Isack Kamwelwe.
   Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula akimshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji mhandisi Isack Kamwelwe kwa utekelezaji wake wa miradi ya maji Simanjiro. 

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Chama cha walimu Tanzania (CWT) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kimewakabidhi walimu 10 wastaafu hundi ya sh3.4 milioni kwa ajili ya ununuzi wa mabati 200. 

  Mwenyekiti wa CWT Wilayani Simanjiro mwalimu Abraham Kisimbi aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mji mdogo wa Orkesumet. Mwalimu Kisimbi alisema lengo la kuwapa mabati hayo ni kuwawezesha walimu hao wastaafu wajenge nyumba zao baada ya kumaliza utumishi wao serikalini. 

  Alisema wamewapa walimu hao wastaafu 10 mabati 200 ambapo kila mmoja atapata mabati 20 yatakayowasaidia kuezeka nyumba zao watakazojenga na kuanza maisha yao ya ustaafu. "Tumeona badala ya kuwapa mabati na kuhangaika kusafirisha kila mmoja tumempa hundi ya sh340,000 ili akanunue mabati 20 kule anapoishi," alisema mwalimu Kisimbi. 

  Aliwataka walimu hao kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyopangwa ili wakafanikishe maisha yao kipindi hiki ambacho watakuwa wamestaafu kazi zao za ualimu na kuanza maisha mengine. 
   Mwalimu mstaafu na Mwenyekiti Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT Peter Toima akizungumza kwenye mkutano mkuu wa walimu wa Simanjiro juu ya mipango na mikakati mbalimbali ya shirika lake ya ujenzi wa baadhi ya shule za wilaya hiyo. 
   Mwenyekiti wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) mwalimu Abraham Kisimbi akizungumza juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu wa wilaya hiyo.
  Mwenyekiti wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara mwalimu Abraham Kisimbi akizungumza juu ya Chama hicho kuwapatia walimu 10 wastaafu hundi ya shilingi milioni 3.4 kwa ajili ya ununuzi wa mabati 200 kwenye mkutano mkuu wa walimu wa wilaya hiyo.   0 0

   Mkurugenzi wa Bidhaa na Huduma wa Kampuni ya simu ya Tigo, David Umoh (kushoto) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya 'TUMEKUSOMA' inayokwenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya huduma za Tigo (*147*00#) itakayowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es sa salaam. Kulia ni Mtaalamu wa Uzoefu wa Wateja wa Kampuni ya simu ya Tigo, Sarah Cyprian.
  Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandhishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya 'TUMEKUSOMA' inayokwenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya huduma za Tigo (*147*00#) itakayowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es sa salaam.

  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania, leo imezindua rasmi kampeni mpya ya Tumekusoma, ambayo ni mkakati mkubwa wa kufikia wateja wake na bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao kwa muda muafaka. Kampeni hii ya Tumekusoma pia inaendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma ya *147*00# itakayowawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi. Wateja wa Tigo watakaotumia namba hiyo mpya pia watapata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hii mpya.

  Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya Tumekusoma jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alisema, ‘Tumesoma hitaji la watumiaji wa mitandao ya simu la menu au namba ya huduma ambayo itarahihisha hatua za kununua vifurushi au kufanya miamala ya fedha. Menu hii mpya inajibu mahitaji hayo yote. Ni rahisi sana kutumia. Pamoja na haya, namba mpya ya *147*00# inawapa wateja ofa kabambe ya nyongeza ya muda wa maongezi, SMS na data kila mara watakaponunua vifurushi kupitia namba hii,’ Umoh alisema.

  Alibainisha faida nyingine kubwa ya menu hiyo mpya ni ofa za Chapchap, zinazowawezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vinavyoendana na mahitaji na tabia zao za kipekee za matumizi ya simu, jambo ambalo linaendana na lengo la Tigo la kuwaongezea thamani wateja wake. ‘Tumesoma mahitaji ya wateja wetu na kuwapa suluhisho muafaka linaloendana na mahitaji yao ya kipekee kupitia menu hii inayorahisisha matumizi yao ya simu kupitia mtandao wetu ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini,’ alisema.

  Tigo inaendelea kuwa mtandao unaoongoza kwa kuzindua bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja. Tigo ndio mtandao ulioleta mageuzi makubwa zaidi katika mifumo ya bei ya mitandao ya simu za mkononi nchini. Tigo pia ndio iliyokuwa mtandao wa kwanza kuzindua huduma za vifurushi vya sauti na data, ndio mtandao wa kwanza kuzindua simu za kisasa zenye mfumo wa lugha ya Kiswahili na pia ndio mtandao wa kwanza nchini kuzindua huduma ya Tigo Pesa iliyowezesha wateja wake kufanya miamala ya fedha nje ya nchi iliyokuwa na uwezo wa kubadili thamani ya fedha kulingana na thamani ya fedha ya nchi husika.

  ‘Kupitia Tumekusoma, tunawakaribisha wateja wote wa Tigo wajiunge nasi katika safari hii ya kumbukumbu ya hatua tulizopiga na mafanikio makubwa tuliyopata katika kipindi hiki cha kuwahudumia Watanzania. Tunawakaribisha nyote kuungana nasi katika mageuzi ya kidigitali nchini na kufurahia mtandao wetu wa Tigo ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini Tanzania,’ Umoh alisema. Menu mpya iliyoboreshwa ya *147*00# inaanza kufanya kazi leo na wateja wa Tigo wanaweza kuanza kupata bonasi murwa kwa manunuzi yote wanayoyafanya. Tunawakaribisha wateja wetu wakae mkao wa kupokea ofa zaidi kabambe huku tukiendelea katika safari hii ya kuwahudumia wateja wetu kwa urahisi zaidi na kwa ubora wa hali ya juu.

  0 0

   Abrahamu Too kutoka Kenya ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19

  Kivutio katika mbio hizo ilikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ambae mbali na kuzindua mbio hizo pia alishiriki katika mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.

  Nafasi ya tatu katika mbio hizo pia ilichukuliwa Mkenya George Onyacha aliyetumia muda wa saa 02:23:27, ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.

  Katika mbio hizo zilizoanzia na kuhitimishwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo ilishuhudiwa nafasi ya kwanza hadi ya saba zikishikwa na wakimbiaji kutoka nchini Kenya huku nafasi ya nane ikienda kwa Mtanzania Paschal Mombo alietumia muda wa saa 02:30:43.

  Akizungumzia siri ya ushindi wake, mbali na kusifia uratibu mzuri wa mbio hizo uliomuwezesha kukimbia bila changamoto yoyote Too alisema ni kujituma kufanya zaidi mazoezi na kukaa kambini muda mrefu ili kufanya vizuri katika michuano ya mwaka huu.

  “Maandalizi ya mwaka huu ni mazuri na washiriki wameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka jambo linalotufanya wanariadha kujiwekea mikakati mizuri ili kuweza kukabiliana na ushindani mkali uliopo katika mbio hizi na ninashukuru Mungu nimefanikiwa,” alisema.
   Abrahamu Too kutoka Kenya akimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19.

   Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuzindua mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana  ambapo alikimbia mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali. 
   Mbali na washiriki kutoka ndani ya nchin pia pia washiriki kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo China na Marekani nao hawakuwa nyuma.
   Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka akizungumza kwenye warsha ya kukabidhi zawadi kwa washindi ambapo pamoja na mambo mengine aliwapongeza waandaaji wa mbio hizo kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI). 
   Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mbio za Km 42 (waliosimama nyuma) mara baada ya kuwakabidhi zawadi pamoja na medali. Wengine ni pamoja na Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka(wa tatu kushoto), waandaaji pamoja na viongozi wa mchezo huo. 
   Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza (Kushoto) akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Km 42 kwa upande wa wanawake ambapo washindi wa kwanza hadi watano wote walitoka nchini Kenya.  0 0

  Ms Stephenie Buelna and Carly Brooke enjoying the scenery at Serengeti National Park recently during their visit organized by Tanzania Tourist Board.
  By Geofrey Tengeneza.

  Ms Stephenie Buelna and Carly Brooke the two famous American influencers have successfully concluded their visit in Tanzania following an invitation extended to them by Tanzania Tourist Board to visit and feature Destination Tanzania in their social media networks .

  While in the country the two young ladies who are popular fashion models and bloggers with thousands of followers in their social media networks in the USA had a chance to visit Serengeti National Park, a site of great animal migration in the World and the Spice Island of Zanzibar where they took and posted different photos in their accounts of Facebook, Instagram, You tube, tweet as well as writing in their blogs and tweet.

  “We had a wonderful experience in Serengeti and here in Zanzibar and most of our readers and followers have so far shown a great interest on destination Tanzania, once we are back in the USA we are going to write a lot” says Stephenie The two influencers were in the country as part of the Tanzania Tourist Board (TTB) strategies to engage celebrities and influencers in the massive campaign to promoting Tanzania as a preferred tourist destination by using social media and influencers so that to increase the number of tourists visiting the country and revenues.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella lipo kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI).

  Hayo yameelezwa leo Octoba 30 na wakili wa Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kesi hiyo kuja kwa ajili ya kutajwa,  

  "Mheshimiwa,  jalada  halisi la kesi hii limetoka ofisi ya upelelezi mkoa wa Temeke (RCO) na sasa lipo kwa DCI." Amesema Mwita.

  Kufuatia Maelezo hayo,, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13, mwaka  huu pia ameusisitiza upande wa Mashtaka wakamilishe mapema upelelezi.

  Katika kesi hiyo namba 5 ya mwaka huu, washtakiwa hao  wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada  wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Aneth Msuya.

  Tukio hilo, linalodaiwa kufanyika Mei 25, mwaka jana maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

  Washtakiwa hao, awali  Februari 23, 2016, waliachiwa huru katika kesi ya mauaji namba 32 ya mwaka 2016 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mwambapa.

  Baada ya kufutwa kwa kesi hiyo iliyokuwa ikifanana na hii walikamatwa  na baadaye kusomewa mashtaka hayo ya mauaji upya.

  0 0

  NA ESTOM SANGA-TASAF.

  Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa Serikali na Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF wanakutana jijini Dar es salaam baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.

  Vikao kazi hivyo vilivyoanza kwenye makao makuu ya TASAF mjini Dar es salaam vitapitia taarifa zilizopatikana kwenye maeneo yaliyotembelewa na wadau hao wa maendeleo na maafisa wa serikali ili kuona Mafanikio na Changamoto za utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini unaohudumia takribani kaya milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote.

  Wakiwa katika maeneo hayo ya utekelezaji wajumbe walipata fursa ya kukutana na baadhi ya walengwa wa Mpango huo na kuona shuhuda mbalimbali za namna Mpango huo unavyoendelea kupunguza adha ya umasikini kwa kutumia fedha wanazozipata kuanzisha shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato.

  Miongoni mwa miradi iliyoanzishwa na walengwa ni pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbuzi,nguruwe na hata ng’ombe wa maziwa na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba za matofali na kuezeka kwa mabati tofauti na hali waliyokuwa wakikabiliwa kabla ya kuingizwa kwenye shughuli za Mpango.

  Vikao kazi hivyo vinavyoambatana na ziara kwenye maeneo ya Utekelezaji wa Mpango hufanywa kila baada ya miezi SITA kwa lengo la kuboresha huduma kwa walengwa na kusaidia nia ya serikali ya kujenga mazingira wezeshi kwa wananchi kukuza mapato yao kwa kuanzisha miradi midogo midogo kulingana na mazingira yao.

  Mikoa ambayo wadau hao wa maendeleo na maafisa wa serikali na TASAF wametemebelea ni pamoja na Tabora, Kigoma,Njombe,Ruvuma,Kilimanjaro, Morogoro, na Zanzibar.Baada ya vikao hivyo taarifa ya maendeleo ya utekelezaji na mapendekezo yakayofikiwa itawasilishwa serikalini. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga (kulia) akiwa na Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika benki ya Dunia Bw. Muderis Mohamed wakiwa katika kikao kazi hicho.
   MMoja wa maafisa wa TASAF Bw. Hamis Kikwape (aliyeshika kipaza sauti) akiwasilisha taarifa baada ya kurejea kutoka Zanzibar na Morogoro akiwa na wadau wa maendeleo.
   Baadhi ya wadau wa maendeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF wakiwa katika kikao cha pamoja cha kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.
   Mmoja wa maafisa wa TASAF Bi. Tumpe Lukonge (aliyeshika kipaza sauti) akiwasilisha taarifa ya ziara kwa wajumbe wa kikao kazi cha wadau wa maewndeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF ,kinachojadili utekelezaji wa  Mpango wa Kunusuru Kaya masikini.
  Baadhi ya wadau wa maendeleo,maafisa wa serikali na watendaji wa TASAF wakiwa katika kikao cha pamoja cha kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini. 

  0 0

   
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo wakati akitangaza rasmi kuzindua Tamasha la 'Tulia Traditional Dances Festival 2018' linalofanyika kila mwaka Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, pamoja na kuwashukuru wadhamini waliofanikisha Tamasha lililofanyika Mwezi Septemba mwaka huu Tukuyu. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni, Lilly Beleko, aliyemwakilisha Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo (kulia) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Air Tanzania, Ladislaus Matindi. Picha na Muhidin Sufiani

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari na wakazi wa eneo la Tande kwa Mtogole wakati wa ziara ya waziri huyo ya kuzindua operesheni ya miezi miwili ya kusafisha mito nchi nzima.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola akikagua eneo la Mto Ng’ombe eneo la Tandale kwa Mtogole wakati wa ziara ya waziri huyo ya kuzindua operesheni ya miezi miwili ya kusafisha mito nchi nzima.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola akisafisha eneo la Mto Ng’ombe kuashiria uzinduzi wa operesheni maalum ya miezi miwili ya kusafisha mito nchi nzima.
  Eneo la Mto Ng’ombe likiwa limejaa taka ngumu kama zilivyokutwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola wakati wa ziara ya waziri huyo ya kuzindua operesheni ya miezi miwili ya kusafisha mito nchi nzima.


  Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala, Mheshimiwa George Mkuchika akisoma Taarifa ya Maboresho ya Mfumo wa Utumishi na Mshahara Serikalini (MCMIS) wakati Kamati hiyo ilipokutana na Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Laurean Ndumbaro.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa akifuatilia majadiliano ya Wajumbe wa Kamati yake wakati Kamati hiyo ilipokutana na Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala kwa ajili ya kupokea na kujadili Taarifa ya Maboresho ya Mfumo wa Utumishi na Mshahara Serikalini (MCMIS), Kulia kwake ni Katibu wa Kamati hiyo, Eunike Shirima.
  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakiwa katika kikao na Watendaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala ambapo leo walijadili Taarifa ya Maboresho ya Mfumo wa Utumishi na Mshahara Serikalini (MCMIS), Kulia kwake ni Katibu wa Kamati hiyo, Eunike Shirima.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya (CCM), Lazaro Nyalandu muda mfupi uliopita ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama hicho na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia (CCM) kwa madai kwamba hafurahishwi na hali ya kisiasa inayoendelea nchini.

  ifuatayo hapo chini ni taarifa yake aliyoitoa wakati akitangaza uamuzi wake huo.

  NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.

   HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

  AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

  VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

  MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA,  kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

  HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo. 

  VILEVILE, nimemua kujiuzulu KITI Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano  wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na nchi yenye ADILI.

  #MunguIbarikiTanzania.
  Lazaro S. Nyalandu.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bibi. Dorothy Aidan Mwaluko akiagana na Kiongozi wa msafara wa magari yaliyobeba mizigo ya ofisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78. Katikati mwenye miwani Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bibi. Jane Kajiru.
  Gari lililobeba nyaraka na vifaa vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora likijiandaa kuondoka katika viwanja vya ofisi hiyo iliyopo Magogoni leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwapungia mikono ya kwaheri madereva wa magari yaliyobeba mizigo ya ofisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78.

  Picha na: Frank Shija – MAELEZO

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto dkt.Faustine Ndugulile akiongea kwenye mkutano huo wa wataalamu wa magonjwa ya figo nchini.Mkutano huo wa siku mbili unafanyika kwenye Hotel ya Morena Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali nchini,Wadau wa Maendeleo pamoja na wataalamu wengine kutoka nchi za Kenya,Sudan,India pamoja na Norway
  Makamu wa Rais wa Chama cha wataalamu wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT), Dkt.Paschal Ruggajjo akiongea dhima kubwa ya mkutano huo ni teknolojia ya upandikizaji wa viungo nchini ili kuweza kuhudumia wagonjwa takribani milioni 23.
  Baadhi ya Wataalamu wa magonjwa ya figo waliohudhuria mkutano huo.Mkutano huo ni wa siku mbili ambapo watajadili dhana mbalimbali ya ugonjwa wa figo ikiwemo kutoa elimu kwa umma ili kuweza kukabiliana na magonjwa ya figo pamoja na upandikizaji.Tanzania imekua ikipeleka wastani wa wagonjwa thelathini na tano(35) kwa mwaka nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza figo na gharama ya kupandikiza nje ya nchi ikiwemo India ni shilingi milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja ikiwemo kupandikiza,nauli pamoja na malazi
  Makamu wa Rais wa cChama hicho akimpa zawadi mmoja wa wataalamu wa figo ambaye amefanya tafiti na kuwasilisha mada ya katika mkutano huo Profesa Ainory Gesase ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Sayansi ya Tiba.
  Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi wa mkutano huo Dkt.Ndugulile akiwa na wataalamu wa figo nchini pamoja na wadau wengine wa ndani ya nchi na nje ya nchi.
  Naibu Waziri akisalimiana na washiriki wa Mkutano huo mara baada ya ufunguzi.Dkt.Ndugulile alisema Serikali mgonjwa mmoja anahitaji wastani wa shilingi za kitanzania 37,620,504 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama za kusafisha damu nchini
  Mashine za kusafisha figo(Dialysis Machine) ambazo zimefungwa kwenye hospitali nchini.Serikali imefunga mashine katika hospitali nchini ikiwemo UDOM (10),Hospitali ya Muhimbili (42), Hospitali ya Rufaa Mbeya(5), Hospitali ya Rufaa Bugando (10), KCMC(10),Hospitali ya Misheni Serian(10),Hospitali ya NSK Arusha(5),TMK(10),Regency(15),Hurbert Kairuki(5), Aga Khan(10) na Access(10).Mashine hizo zina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 783 kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na 391 kwa huduma ya malipo ya papo kwa papo


  Picha zote na Wizara ya Afya

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi kuashiria ufunguzi wa wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kufungua daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.
  Sehemu ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ambayo yanalenga kuonyesha namna mashujaa wa Tanganyika walipambana kupata uhuru, maonyesho ambayo yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja katika Makumbusho ya Taifa- Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam. Uzinduzi wa maonyesho hayo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), kwa lengo ya kuendeleza juhudi za Uhifadhi wa Hifadhi ya Urithi Tanzania,hususani ya Ukombozi wa Afrika yanasimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). 

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo, Dkt. Mwakyembe alisema mradi huo wa kuhifadhi historia ya Ukombozi wa bara la Afrika ni muhimu kwa Tanzania kwani unaweza kusaidia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini kuliko ilivyo sasa kwani inawapa nafasi wageni ya kuona mambo tofauti na yaliyozoeleka pindi wanapokuja nchini. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. “Tuna mradi ambao utatupeleka mbali sana Watanzania, Afrika Kusini, Namibia, Angola hata wao wametuambia tusije shangaa sehemu hiyo ikawa inaleta watalii wengi zaidi kuliko wanaokuja kuangalia tembo na simba, urithi wa Afrika tumekabidhiwa na bara la Afrika ni wajibu wetu Watanzania kuusukuma huu mradi maana tumeshachelewa, Watanzania wengi labda hawaelewi mwaka 2011 kwa kushirikiana na UNESCO tulipeleka ombi AU la mradi huu wa bara la Afrika na wakaubariki huu mradi na wakaamua makao makuu yawe Tanzania na sisi tukachagua Dar na hapa kitajengwa kituo kikubwa kitakuwa na historia ya Ukombozi wa Afrika, sisi ndiyo viongozi wa huu mradi,” alisema Dkt. Mwakyembe. 

  Alisema ili kufanikisha mradi huo tayari wameanza kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha pindi watakapojenga kituoambacho kitatumika kuhifadhi vitu mbalimbali ambavyo vilitumika katika kipindi cha ukombozi wa bara la Afrika kuwe na taarifa nyingi kuhusu bara la Afrika. “Tunawatumia wazee walio na historia ya ukombozi wa Afrika tumehoji zaidi ya wazee 100 na tunaendelea na hilo zoezi na tumebaini maeneo zaidi ya 200 Tanzania ambayo yanahitaji kuhifadhiwa, ni wajibu wangu kupeleka muswada bungeni ili tuyahifadhi na kuyalinda kwa kutumia sheria,” alisema Waziri Mwakyembe. Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. Kwa upande wa Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer alisema ni muhimu kwa bara la Afrika kuwa na maonyesho ambayo yanaelezea historia ya bara hilo ili yatumike kuelezea kizazi cha sasa na kijacho namna nchi za Afrika zilipambana kupata uhuru na wao kama EU wataendelea kusaidia miradi mbalimbali yenye lengo ya kutunza urithi wa bara la Afrika. 

  Ni jambo la kujivunia kwa Umoja wa nchi za Ulaya kusaidia kufanikisha mradi huu … EU tumekuwa tukisaidia miradi mingi na hii yote ni kwa ajili ya kutunza utamaduni na urithi wa bara la Afrika, tumesaidia miradi mbalimbali nchini ikiwepo ya Olduvai na Ngorongoro na tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuendeleza maeneo ya kihistoria,” alisema. Afisa Mpango Kitaifa wa UNESCO, Nancy Kaizilege akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. Naye Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco Dar, Ann Therese Ndong- Jatta katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Mpango Kitaifa wa UNESCO, Nancy Kaizilege alisema ni jambo zuri kuwepo na makumbusho ambayo yanaeleza historia ya bara la Afrika na yatawza kuwapa nafasi watu mbalimbali kutoka mataifa ya nje ya bara la Afrika kuona na kujifunza historia ya Afrika. “Makumbusho haya ni muhimu kwasababu ni sehemu ya ukumbusho wetu kwa baadae, kupitia makumbusho haya tutaona historia ya bara la Afrika, historia ya mwanadamu na safari ya kutafuta uhuru ilivyokuwa,” alisema Kaizilege. 


  0 0

  The government has reaffirmed its commitment to support the Small and Medium Enterprises (SMEs), but this time paying particular attention to the mid-size companies whose impact on the economy in terms of job creation and industrialization is immense. Speaking during the Top 100 mid-sized companies awards ceremony yesterday in Dar es salaam, The Minister for Industry, Trade and Investment Hon. Charles Mwijage said the government is committed to creating an environment that will allow the mid-sized companies thrive.

  “SMEs have tremendous ability to create growth and development. And for that, the government is committed to creating an enabling environment for them to excel. We (government), through the establishment of Tanzania Entrepreneurship and competitiveness Centre (TECC), will endevour to deal with challenges that affect the SMEs sector,” he said. Hon Mwijage also advised the mid-size companies to adopt corporate governance practices and improve the quality of their products and services in order to strengthen their market position and remain competitive.

  At the same event, Top 100 mid-sized companies in the country were recognised and awarded after a survey conducted by KPMG, an audit firm showing they meet all the ingredients and financial fitness of a competitive mid-size firm. The survey, which is in its seventh year running, is sponsored by bank M under a joint initiative between KPMG and MCL.

  Speaking on behalf of Bank M, the CEO Ms. Jacqueline Woiso expressed the Bank’s satisfaction to the whole process, “we congratulate KPMG and MCL for this initiative, as well as the winners. Mid-sized companies play a central role in the economic growth of any country. By recognizing their contribution, we believe that they will be encouraged to do even more. By so doing, such companies will prosper increase productivity as well as its contribution to the social welfare of the people by creating more employment opportunities and most importantly boosting our economy.”

  This is the survey which celebrates business success among the country’s Mid-Sized Companies as well as entrepreneurs for contributing to the employment generation and growth of the Tanzanian economy in general. The award is given to companies which rank ahead of their peers in terms of revenue growth, profit growth. A top 100 company has succeeded in progressively growing its market position over time. The event revealed the 2017/18 winners being Dar Ceramica Centre 2001 Ltd , followed by Songoro Marine Transport, Modern Fitting Mart Ltd, Transit Ltd, Meru Spring Water etc.
  Hon. Charles Mwijage, Minister for Industry, Trade & Investments (right) applaud after handling over a trophy to Dar Ceramica Centre 2001 Ltd officials, the company scooped the 1st position of the Top 100 Mid sized companies award for this year during the awards ceremony took place in Dsm over the weekend. Awards are organised by KPMG and MCL in partnership with Bank M. Others in the photo are Bank M CEO Ms. Jacqueline Woiso and KPMG partner Ketan Shah (left).
  Hon. Charles Mwijage, Minister for Industry, Trade & Investments speaking during the Top 100 mid sized companies awards ceremony took place over the weekend.
  Hon. Charles Mwijage, Minister for Industry, Trade & Investments (third right) posing for a photo with the four officials of Dar Cermaica Centre 2001 Ltd (with glasses), the company scooped winners of the Top 100 Mid sized companies award for this year during the awards ceremony held over the weekend in Dsm. Awards are organized by KPMG and MCL in partnership with Bank M. Others in the photo are KPMG partner Ketan Shah (left),Bank M CEO Ms. Jacqueline Woiso (second left)and DSE Business Development manager Mary Kinabo.
  Participants paying attention during the Top 100 Mid sized companies awards ceremony at Mlimani City hall in Dar es salaam took place over the weekend.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Gualbert Mbujilo (katikati) akipata maelezo ya vifaa vya ujifunzaji kutoka kwa mwalimu kwenye chumba cha darasa la kwanza ikionesha hali halisi ya darasa linalozungumza.Kushoto kwake ni Afisa Elimu Msingi Zegeli Shengelo.

  Hyasinta Kissima-Njombe 


  Akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mabatini, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Gualbert Mbujilo aliwataka wazazi kuhakikisha kuwa wanaona umuhimu wa kununua vitabu kwa watoto wao kwani kupitia vitabu hivyo yapo mafundisho ambayo yamekua yakitolewa lakini sambamba na hilo vitabu vinamjengea mtoto uwezo wa kusoma kwa usahihi na kujiamini.

  “Tumeona na tumesikia ni kwa jinsi gani mtoto aliyetusomea hadithi kwenye kitabu licha ya kuathiriwa na Lugha mama lakini amejitahidi kutamka maneno kwa ufasaha, anajiamini vya kutosha na ametuonesha vituo mbalimbali wakati wa kusoma.Hili ndilo Taifa tunalolijenga.

  Wazazi hakikisheni mnawanunulia watoto vitabu vya hadithi na vitabu vya kujifunzia na kuhakikisha tunatenga muda wa kutosha wa kuwa karibu na watoto wetu na kuwaelekeza” Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo Zegeli Shengelo amesema kuwa kueleka kwenye uchumi wa viwanda kutakuwa na mahitaji makubwa sana ya wasomi hivyo ni vyema kufanya maandalizi mazuri kwa watoto wetu kwani msingi mzuri wa mtoto hujengwa kati ngazi za awali za elimu (shule za msingi) na pindi misingi hii inapojengwa vibaya mwendelezo wa mtoto unakua ni wakusuasua na mwisho wa siku mtoto anashindwa kuendelea na masomo kwani msingi wake haukujengwa imara tangu awali.

  Aidha Shengelo amelishukuru shirika la watoto dunia UNICEF ambalo lilitoa mafunzo kwa waalimu katika shule ya Msingi Mabatini ambapo kupitia mafunzo hayo waalimu kwa kushirikiana na wanafunzi waliweza kutengeneza muonekano wa madarasa yanayoongea na kutengeneza zana mbalimbali za kujifunzia kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika maeneo yanayowazunguka.

  “UNICEF imetusaidia sana kwani kupitia madarasa yanayoongea yamesaidia kuboresha mazingira ya watoto kujifunza kwani mtoto mwenyewe anaweza kujifunza pasipo mwalimu na madarasa haya yamekuwa yanawavutia wanafunzi wengi kupenda kusoma” Alisema Shengelo.

  Hafla hiyo pia iliambatana na utoaji wa zawadi kwa Wanafunzi 04 waliofanya vizuri kwenye hatua za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK), pamoja na waalimu 04 washindi wa ufundishaji KKK katika ngazi ya Halmashauri ambapo waalimu walipata fedha taslimu zenye thamani ya shilingi laki moja (100,000/=) na wanafunzi walipewa zawadi ya shilingi elfu hamsini(50,000/=) ,mabegi, kalamu, daftari pamoja na vifaa mbalimbali vya kujifunzia.

  Mwanafunzi Amilton Sanga kutoka shule ya Msingi Ramadhani akikabidhiwa kiasi cha shilingi 50,000/= mara baada ya kuibuka kidedea kwenye ngazi ya Halmashauri katika zoezi la Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
  Wanafunzi walioshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usomaji Vitabu wakiwa wanasoma vitabu vya hadithi mbalimbali kwenye hafla hiyo.
  Sehemu ya wazazi,waalimu na waratibu elimu walioshiriki kwenye kilele cha siku ya usomaji vitabu yaliyofanyika katika shule ya Msingi Mabatini Halmashauri ya Mji Njombe.

older | 1 | .... | 1988 | 1989 | (Page 1990) | 1991 | 1992 | .... | 3283 | newer