Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1989 | 1990 | (Page 1991) | 1992 | 1993 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

  Raia kumi wa Iran na watanzania wawili, leo Oktoba 30, 2017 wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mshtaka matatu ya kukutwa na mchanganyiko wa dawa za kulevya za Heroin Bangi na Kuberi zenye uzito wa zaidi ya kilogram 110.

  Hati ya Mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi imewataja raia hao wa Iran kuwa ni, Nabibakshsh Bibarde ,40, Mohammadhanif Dorzade, 23, Abdallah Sahib,21, Ubeidulla Abdi, Naim Ishaqa, Moslem Golmohamad, Rashid Badfar, Omary Ayoub, Abdulmajid Asqan na Tahir Mubarak.

  Pia watanzania hao ni, Ally Abdallah Ally na Juma Amour Juma.

  Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa imedaiwa kuwa, Oktoba 25 mwaka huu, huko katika Ukanda wa Bahari ya Hindi, upande wa Tanzania washtakiwa walisafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 111.02 aina ya Heroine.

  Aidha, siku na mahali hapo hapo, washtakiwa hao walikutwa wakisafirisha  gramu 235.78 za Bangi.

  Katika shtaka la tatu, watuhumiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha mchanganyiko wa dawa za kulevya aina ya Bangi na Kuberi zenye uzito wa kilo 3.34.

  Hata hivyo, washtakiwa hao ambao walikuwa wakitafsiriwa kwa lugha ya Kiiran kutoka lugha ya kiswahili na mkalimani Meja Ndakeye (45) hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa, mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo ambayo kwa kawaida inasikilizwa mahakama kuu.


  Pia Hakimu Nongwa alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kuwapatia washtakiwa hao dhamana sababu kiwango cha dawa wanazotuhumiwa kusafirisha imezidi kiwango ambacho mahakama hiyo inamlaka ya kutoa dhamana.

  Kwa mujibu wa upande wa Mashtaka. upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Novemba 13,mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

  0 0

  Msanii wa Bongo Fleva nchini IzzoBiznes akiimba na Mashabiki wa Tamasha la Efm Mziki Mnene katika Bar ya Dunda Dunda Bagamoyo.

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MSANII wa muziki wa Hip Pop kutoka mkoa wa Mbeya IzzoBiznes amevunja mwiko kwa wakazi wa mkoa wa pwani kwa kuimba pamoja nao muziki wa Rap.

  Izzo ambaye alipanda katika jukwaa la Mziki Mnene la Efm akiongozwa na RDJ Black ambaye alianza kumpigia wimbo wake unaokwenda kwa jina la Ridhiwani ongea na Mshua jambo lililokonga nyoyo za wakazi hao.

  IzzoBiznes mbali ya wimbo huo aliwapagawisha wakazi hao kwa wimbo wake wa Shemeji ambao uliweza kuinua watu wote ambao walikuwa wamekaa katika viti na kuanza kuimba nae pamoja.

  Baada ya wimbo huo aliongeza kibao chake kinachokwenda kwa jina la Kama Kijana ambao nao uliweza kuinua vijana wote wa Bagamoyo ambao waliimba nae pamoja.Mwisho alimaliza kwa kuimba free Style na kuunganisha wimbo wake wa Tumhoghele.
  Msanii wa Bongo Fleva nchini IzzoBiznes akiimba na Mashabiki wa Tamasha la Efm Mziki Mnene katika Bar ya Dunda Dunda Bagamoyo.
  Msanii wa Bongo Fleva nchini IzzoBiznes akiimba na Mashabiki wa Tamasha la Efm Mziki Mnene katika Bar ya Dunda Dunda Bagamoyo

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema wanafunzi wa elimu ya juu wanatakiwa kupata mikopo kwa  muda mwafaka ili waanze kuhudhuria masoma yao. 
  Nasha ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea bodi ya Mikopo ya Elimu Juu  jijini ambapo amesema  hataki kuona wanafunzi wenye vigezo vya kupata mkopo wanakosa.


  Amesema fedha iliyoidhinishwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wale wanaostahili kwa sifa na vigezo ni sh. Bilioni 427 na na robo ya fedha hizo ambayo imeshatumwa katika  katika akaunti ya bodi ya mikopo ni sh.milioni 147. 
  Ole Nasha amesema kuwa, kufikia Ijumaa ya Wiki hii mikopo hiyo iwe imeshakwenda kwa walengwa  na rufaa za wale ambao hawajapatiwa huku wana sifa za kupata mikopo hiyo, kufikia Novemba 30 ziwe zimeshakwisha. 

  “Fedha zimetoka kwa wakati hatutaki wanafunzi wacheleweshewe  lengo la serikali ni kuhakikisha wanafunzi hawapati usumbufu” amesema Ole Nasha.

  Amesema ili kuondokana na wanafunzi hewa fedha za wanafunzi wanaorudia mitihani  zipelekwe katika vyuo husika na zile zitazobaki zirudishwe. 
  Aidha, Ole Nasha ameiomba bodi kuwatangaza katika vyombo vya habari wadaiwa sugu ambao wamekuwa wakichelewesha urejeshaji wa mikopo kuweza ili kuwasukma waweze kulipa na baadae bodi iweze kujiendesha.

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru amesema kuwa wamejiwekea mikakati mbalimbali katika bodi ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi

  Amesema moja ya mikakati ni kuboresha mifumo ya Tehama katika kuweza kutunza kumbukumbu mbalimbali itayoweza kurahisisha shughuli za bodi kufanya kazi ya kuwahudumia wanafunzi katika utoaji wa mikopo.

  Aidha amesema bodi inatarajia kuongeza uwigo wa urejeshaji mikopo kwa wale walionufaika na mikopo hiyo.
  Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia , William Ole Nasha akipata maelezo kwa Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Ignatus Oscar wakati alipotembelea bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia , William Ole Nasha akipata maelezo kutoka Kaimu Mkurugenzi wa Upangaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini , Deus Shangala jinsi wanavyopanga mikopo,wakati Naibu Waziri wa Elimu, alipotembelea bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia , William Ole Nasha akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kutembelea Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini, Abdul-Razaq Badru akizungumza juu ya mikakati ya bodi hiyo kwa Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha.

  0 0
 • 10/30/17--21:05: TAARIFA YA SHUKURANI
 •  FAMILIA YA MAREHEMU MZEE MOHAMED NASSOR KISSOKY NA FAMILIA YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI JUMA MOHAMED PONGWE TUNATOA SHUKRANI ZETU ZA DHATI KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI NA WOTE MLIOTUFARIJI NA KUSHIRIKIANA NASI KWA NJIA MOJA AU NYINGINE WAKATI WA MARADHI NA KATIKA MSIBA WA MPENDWA WETU DA BEBBY MARIAM JUMA PONGWE. 

  SI RAHISI KUMSHUKURU KILA MTU MMOJA MMOJA. 

  TUNAOMBA MPOKEE SHUKRANI ZETU ZA UPENDO. NASI HATUNA UWEZO WA KUWALIPA ISIPOKUWA YEYE MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA NDIYE ATAWALIPA KWA KADRI ATAKAVYOONA INAFAA.AMEENA! TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA KUWA HITIMA (DUA) YA KUMUOMBEA MAREHEMU ITAFANYIKA JUMAPILI 05/11/2017 SAA SABA ADHUHURI. 

  MWENGE  MLALAKUWA KUPITIA UWANJA WA NGOME SACCOS KUELEKEA MAKAZI YA RAIA. KUTAKUWA NA MABANGO YA KUELEKEZA. "INNA LILLAH WA INNA ILLAH RAJ'IUN".

  0 0

  Na Dotto Mwaibale, Geita

  MKUU wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi amesema ataanzisha utaratibu wa kuwapima maofisa ugani wa mkoa huo utendaji kazi wao ili kujua uwezo wa kila mmoja wao.

  Hayo ameyasema  wakati Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ilipokuwa ikimkabidhi mbegu bora za mahindi, mihogo na viazi lishe ikiwa ni siku yake ya kwanza kufanya kazi katika mkoa huo tangu ateuliwe na Rais Dk.John Magufuli kushika wadhifa huo.

  "Kilimo ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika uchumi wa kati wa viwanda hivyo nitaweka utaratibu wa kuwapima maofisa ugani wote wa mkoa huu ili niweze kujua utendaji kazi wao" alisema Lughumbi.

  Lughumbi aliwataka maofisa ugani mkoani humo kuacha kukaa maofisi kwenye viyoyozi badala yake waende walipo wakulima kushirikiana nao kuwapa elimu ya kilimo ili kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo.

  Mkuu huyo wa mkoa ameahidi kununua viatu vya shambani 'gambuti' na koti na kuwa mara moja ataanza kutembelea wakulima katika maeneo yao ili kujua changamoto zao na kusema anapenda kuona mkoa wa Geita unakuwa namba moja kwa kilimo hapa nchini.

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akimkabidhi mbegu bora ya mahindi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi  wakati wa uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu za mahindi, mhogo na viazi lishe uliofanyika nje ya viwanja vya ofisi ya mkoa huo jana. Kushoto ni Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo   (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
   Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa mbegu hizo za mahindi zinazokabiliana na ukame  Wema.
   wananchi wa Kijiji cha Isamilo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
   Mkulima Hernick Elias wa Kijiji cha Isamilo akizungumzia changamoto za kilimo walizonazo
   Watafiti wakifanya vipimo kabla ya uzinduzi wa shamba la mbegu za mahindi katika kijiji cha Isamilo.
   Wakulima wa Kikundi cha Nguvumoja cha Kijiji cha Isamilo wakiwa shambani wakati wa uzinduzi huo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,akiwataka kuwa watulivu wakati suala la mgogoro kati yao na hifadhi likiwa linashughulikiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

  Naibu Waziri Ulega ameeleza hayo jana katika mkutano na wafugaji hao uliofanyika kwenye Kata ya Ololosokwan wilayani humo.

  “Wakati tunamsubiri Waziri Mkuu atoe maelekezo naomba msiharibu hali ya hewa, hii ndiyo rai yetu kama Serikali,ama kama kuna yeyote anayepinga jambo hili? Aliwauliza wafugaji hao na kujibiwa hakuna na wote wapo pamoja na Serikali.

  “Hatua hii itaturahisishia sisi kwa sababu wizara inaliangalia jambo hili kwa ukaribu kutokana na sehemu kubwa ya nchi, wafugaji wamekuwa na malalamiko makubwa sana ikiwemo kufilisi mifugo yao pindi inapoingia hifadhini na kusababishiwa umasikini,”amesema Ulega.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka alimweleza Ulega kwamba ukosefu wa malisho ni mojawapo ya changamoto inayowakabili wafugaji hao kutokana maeneo machache yaliyopo.

  Hata hivyo, Ulega alihaidi kulishughulikia changamoto hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja watatafuta mashirika kwa ajili kuangalia namna ya kuboresha malisho hayo ili kuleta ahueni kwa wafugaji hayo.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisalimiana na wazee wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
   Mmoja wa wafugaji akieleza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

   Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka akizungumza na wananchi wa kata ya Ololosokwan mkoani Arusha.
  Wananchi wa kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo mgogoro wa mpaka na hifadhi. 

  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii,Arusha.


  0 0

   Na Fredy Mgunda,Mufindi

  Chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimemuomba mkurugenzi kuwakopesha viwanja walimu ili kujikwamuamua na mazingira magumu wanayokumbana katika nyumba wanazoishi.

  Hayo yalisemwa na mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale alisema kuwa walimu wamekuwa wakiishi katika nyumba chakavu au mbali na mazingira ya shule kitu kinachosababisha kushuka kwa uwezo wa walimu kufundisha.

  Kimbale alisema kuwa walimu hawana pesa za kununua moja kwa moja viwanja hivyo kwa njia ya kuwakopesha inawezekana kutokana kuwa ni waajiliwa wa serikali na mishahara yao inajulikana na ni rahisi kuresha mkopo huo.

  “Sisi walimu ukitaka kujua mimi nalipwa shilingi ngapi ni rahisi tu kwa kuwa mishahara ya serikali mara nyingi inajulikana hasa pale mtumishi unapoenda kukopa mahali ndio maana tunaiomba serikali itusaidie kukopa viwanja kuwa kuwa tunauwezo wa kulipa kwa awamu tatu” alisema Kimbale
  Aidha Kimbale aliwatupia lawama maafisa elimu na walimu wakuu wa shule kwa kuwanyima ruhusa bila kuwa na sababu maalum. 

  “Wakurugenzi amekuwa ametoa kibali upewe ruhusa lakini viongozi waliochini ya mkurugenzi wanatuwekea vipingamizi ambavyo havieleweki kitu kinachozua utata mkubwa baina ya viongozi na walimu ambao sio viongozi” alisema Kimbale.
  Mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

  mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamuakizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.


  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Inawezekana utakuwa umesikia watu au kusoma kwenye mitandao ya kijamii kuhusu sherehe za Halloween lakini ukawa hauelewi. Mbali na hapo inawezekana pia umekutana na matangazo kadhaa yakikutana kushiriki kwenye sherehe za sikukuu hiyo sehemu kadhaa za starehe hususani vilabu vya usiku hapa nchini.
  Kutokana na utandawazi uliosababisha dunia kuwa kijiji tumejikuta kwa namna moja ama nyingine tukishiriki matukio mbalimbali kwa wakati mmoja. Baadhi ya matukio hayo huwa hatuelewi maana yake kwa undani zaidi. Kwa mfano, Halloween kwa namna inavyosherehekewa ni kama ina uhusiano na sherehe za kishetani.

  Ikiwa sehemu mbalimbali duniani zimeshaanza maandalizi ya sherehe za Halloween ambazo hufanyika kila ifikapo Oktoba 31 ya kila mwaka, Jumia Travel ingependa kukufahamisha juu ya maana halisi ya sherehe hii.  
  Japokuwa umaarufu wa sherehe ya Halloween umetokana na nchi ya Marekani lakini ukweli ni kwamba wanahistoria wanaamini sherehe hii ilianzia nchini Ireland na kusambaa nchi za jirani za Scotland, Uingereza, Ufaransa na baadaye sehemu zingine duniani.

  Na kudhihirisha kwamba Marekani inasherehekea sherehe hii kikamilifu, inaaminika kwamba ni sherehe ya pili kwa ukubwa wa kibiashara ndani ya mwaka. Katika kipindi hiki takwimu zinaonyesha kwamba wamarekani hutumia zaidi ya dola bilioni 5 kuadhimisha sherehe hii. Na kwa kuongezea robo ya mauzo yote ya peremende au pipi ya mwaka hufanyika ndani ya kipindi hiki nchini humo.
  Halloween ina maana gani na kwanini husherehekewa kila ifikapo Oktoba 31 ya mwaka?

  Maana halisi ya neno Halloween ni siku ya mkesha wa siku ya watakatifu wote ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba mosi. Halloween pia ni ufupisho wa neno ‘Allhalloween, All Hallows’ Evening na All Saint’s Eve’ ambapo husherehekewa kila ifikapo Oktoba 31 ya kila mwaka.

  Asili ya Halloween ilitokana na sherehe ya ‘Samhain’ iliyokuwa ikiadhimishwa na watu wa kale wa Ireland au ‘Waseltiki’ kama wanavyojulikana.

  Samhain ni sherehe ya wapagani wa kiseltiki ikimaanisha ‘Mwisho wa Majira ya Joto’ ambayo huadhimishwa mwisho wa msimu wa mavuno.

  Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho walikuwa wakiwasha moto kuuzunguka na kisha kuvalia mavazi yanafanana na ya mashetani ili kuepekana na mizimu inayosemekana huwa inarandaranda usiku huo.

  Katika karne ya nane, Papa Gregory III alisema kwamba Novemba mosi itakuwa ni siku ya kuwakumbuka watakatifu na wafia dini wote. Na hapo ndipo ‘Siku ya Watakatifu Wote’ ilipoanzia na jioni yake ilikuwa ikijulikana kama ‘All Hallows’ Eve’ na baadaye kuwa Halloween.
  Halloween imepata umaarufu mkubwa kadiri muda unavyokwenda na kuwa kipindi cha kufanya biashara kwa wingi ambapo watoto na watu wazima husherehekea kwa kuvalia mavazi ya kuogofya kama mizimu au mashetani na kwenda kuhudhuria sherehe zinazoandaliwa.

  Kwanini watu huvalia mavazi ya kuogofya usiku wa Halloween?

  Utamaduni ambao umekuwepo kwa miaka mingi katika kusherehekea Halloween ni pamoja na kuvalia mavazi ya kutisha kama mizimu au mashetani.
  Washerehekeaji hufanya hivyo kutokana na asili ya sherehe hii ambapo inaamini kwamba katika mkesha wa siku ya Oktoba 31 kuamkia Novemba mosi mashetani, wachawi na mizimu huwa inarandaranda mitaani kusherehekea kuanza kwa msimu wao - kipindi cha majira ya baridi. Inasemekana kwamba huranda mitaani na kuwachezea watu, kuwatisha, kuwadhuru na kuwafanyia hila mbalimbali kadiri wanavyopenda.

  Njia pekee kwa watu waliokuwa wanaogopa kutishwa na mizimu hiyo ni kuwapatia vitu ambavyo walikuwa wanavipendelea, mara nyingi huwa ni vyakula vitamu na zawadi nzuri kama vile peremende kwa kuviacha milangoni.

  Au, njia nyingine iliyokuwa ikitumika, kwa watu ambao walikuwa wanaogopa, ni kwa kuvalia mavazi kama yao na kisha kurandaranda mitaani, lengo ni kwa mizimu hiyo kutowatambua na kuwafananisha binadamu hao na wenzao.
  Je unajiuliza kama usherehekee sikukuu ya Halloween? Kumekuwa na dhana tofauti juu ya sherehe hii ambayo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikihusishwa na ushetani na ushirikina. Hii inategemea namna wewe mwenyewe utakavyosherehekea na kwa malengo gani na kama itaathiri vipi imani yako. Kwa makala haya, Jumia Travel inaamini kwamba utakuwa umefahamu machache kuhusiana na sherehe hii ambayo inazidi kushika kasi kadiri miaka inavyokwenda.

  0 0


  Na Benny Mwaipaja, Dodoma

  MAKAMU wa Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN, amezinduzi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, tukio litakalofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

  Makamu wa Rais ametoa wito kwa watoa huduma ndogo za fedha kupunguza riba za mikopo na tozo mbalimbali ili kufanikisha lengo la Sera hiyo ambalo ni kuimarisha huduma jumuishi za fedha kwa kujenga mazingira wezeshi yatakayoleta ufanisi wa utoaji wa huduma ndogo za fedha nchini kwa wananchi wenye kipato cha chini.

  “Ninawaomba pia muongeze ubunifu katika kutoa huduma zinazohitajika na wananchi wa kipato cha chini pamoja na kupeleka huduma hizo katika maeneo yaliyo karibu na makazi yao au biashara zao” aliongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan

  Alizitaka taasisi za huduma za fedha kuwaelimisha wananchi kabla ya kutoa huduma hizo ili kupunguza athari wanazozipata wananchi.“Ni matarajio yangu kuwa, Wizara ya Fedha na Mipango itashirikiana na wadau katika kutekeleza Sera hii na kuhakikisha malengo ya Sera ambayo ni kukuza uchumi na kupunguza umaskini yanafikiwa” alisisitiza

  Alisema Ripoti ya Finscope ya mwaka 2017 ambayo iilionesha kuwa Tanzania imepiga hatua kwenye suala zima la huduma jumuishi za fedha (financial inclusion) na kufikia asilimia 72 kwa 2017, huku changamoto kuu iliyoainisha ni elimu/uelewa mdogo wa huduma za fedha kwa wananchi.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizundua rasmi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania –TPB Bw. Sabasaba Moshingi baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Akiba na Mikopo-(KIKOBA) cha Mwende Manispaa ya Dodoma, Bi. Bertha Chisawilo, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimpongeza Mwenyekiti wa Kikundi cha Akiba na Mikopo-(KIKOBA) cha Mwende, Manispaa ya Dodoma, Bi. Bertha Chisawilo, baada ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, kumkabidhi Mwenyekiti huyo, Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nyakato nje kidogo ya jiji la Mwanza mara baada ya kufungua kiwandaa cha Sayona Drinks ltd kilichopo Nyakato.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Katikati ya jiji la Mwanza wakati akitokea Nyakato.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati mmiliki wa Kiwanda cha Sayona Drinks Subhas Patel alipokuwa akionesha bidhaa mojawapo ya kiwanda hicho.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wananchi wa Nyakato mara baada ya kuwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuagana na Wananchi wa Nyakato mara baada ya kumaliza kuwahutubia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuagana na Wananchi wa Nyakato mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha Sayona Drinks kilichopo Nyakato jijini Mwanza.

  PICHA NA IKULU.


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  1.LESENI  YA MAKAZI  NININI.


  Leseni  ya  makazi  ni  leseni/kibali  maalum kinachotolewa  kwa  mmiliki  wa  makazi  ili  kutambua  na  kurasimisha  makazi  hayo.

   Leseni  ya  makazi  ni  nyaraka  ya  umiliki  wa  makazi   kama  ilivyo  nyaraka  nyingine za  umiliki  wa  ardhi.  Leseni  ya  makazi  ni  kwa  ajili  ya  ardhi  makazi  tu  na  si  ardhi  nyingineyo.


  2.  JE  LESENI  ZA  MAKAZI  ZINATAMBULIWA  NA  SHERIA.


  Ndio, leseni  za  makazi  ni  kwa  mujibu  wa  sheria  namba  4/1999 Sheria  ya  Ardhi.  Leseni  za  makazi  zinatambuliwa  na  kifungu  cha  23  cha  sheria  hiyo. 


  Kwahiyo  wanaodhani  kuwa  leseni  za  makazi  ni  mpango  tu  wa  serikali  za  mitaa  na  watendaji  wa  kata  wajue  sio  kweli.  Leseni  za  makazi  ni  nyaraka   iliyo  kisheria  kwa  mujibu  wa  kifungu  hicho  japo  juu.


  3.  TOFAUTI  YA  LESENI  YA  MAKAZI  NA  HATI .


  Hati ni “Right  Of  Occupancy”  kwa  jina  la  kitaalam,  wakati  leseni  ya makazi ni  “Derivative Right” .  Tofauti  za  viwili  hivi  ni  nyingi  ila kubwa  ya  kukufanya  uelewe  ni  kuwa,  leseni  ya makazi  hutolewa kwa  makazi  ya mjini  ambayo  hayajapimwa  na  hayakuwa   rasmi  lakini  yasiyo  hatarishi.


  Wakati hati  hutolewa  katika  makazi  rasmi  na  ambayo  yamepimwa.  Isipokuwa  la  kuzingatia  ni  kuwa   iwe  leseni  ya makazi  ama  hati  vyote  vinatambuliwa  na serikali  kama  nyaraka  rasmi  za  umiliki  na  kila  moja  ina  haki  sawa na  nyingine  katika  umiliki.

                     
   KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com
  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde leo amezindua programu ya Urasimishaji Ujuzi kwa Vijana ambao wana ujuzi lakini hawakupitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya Ufundi(Recognition of Prior Learning).

  Ufunguzi huo wa Program hii ya Urasimishaji Ujuzi ambao unagharamikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu umefanyika leo katika Chuo cha VETA Jijijni Tanga na kujumisha jumla ya Vijana 701 kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara wanatarajiwa kunufaika na mpango huo.

  Akizungumza na Vijana hao, Mh.Mavunde amesema serikali inatekeleza mpango mkubwa wa ukuzaji ujuzi kwa Vijana unaolenga kuwafikia takribani Vijana Milioni 4 nchi nzima kwa lengo la kuwajengea ujuzi stahiki utakaowasaidia kupata Ajira na kujiajiri wenyewe.

  Aidha Naibu Waziri Mavunde amewataka Vijana wote kuchangamkia fursa mbalimbali zitokanazo na ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima,Uganda-Tanga ambapo serikali kuu na serikali ya Mkoa wameendelea kujenga mazingira rafiki ya kuhakikisha Vijana wanafikia malengo yao.

  Wakizungumza baada ya kuzinduliwa program hiyo, Vijana hao wameishukuru Serikali kwa Mpango huu wa urasimishaji ujuzi ambao unawapa fursa ya kupewa cheti cha Ufundi kutoka VETA bila kupitia utaratibu wa kawaida wa masomo ambapo takribani Vijana 3900 watanufaika na Mpango huu nchi nzima.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa programu ya Urasimishaji Ujuzi.
  Mbunge wa Handeni Vijijini Mboni Mhita akizungumza katika uzinduzi wa programu ya urasimishaji ujuzi.

  washiriki wa uzinduzi wa programu ya Urasimishaji Ujuzi.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (Mb), amewataka wananchi wanaopata nafasi za kazi katika miradi ya ujenzi wa barabara kuwa wazalendo katika kulinda vifaa na kuepuka vitendo vya hujuma vinavyoweza kujitokeza ili kuhakikisha miradi hiyo inaenda kwa kasi na kumalizika kwa muda uliopangwa.

  Mhe. Kwandikwa ametoa kauli hiyo wilayani Kasulu mkoani Kigoma, alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 inayojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation na kuelezwa kuwa kuna wizi wa mafuta kiasi cha lita elfu 23 zilizoibiwa hivi karibun ambapo amewataka wananchi kuwa na uzalendo kwanza katika miradi yote ya ujenzi katika maeneo yote.

  “Wizi wa namna hii haukubaliki na mtandao ni mkubwa hivyo naagiza vyombo vya usalama vichukue hatua kali mapema ili kuweza kuondoa madhara makubwa zaidi”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

  Amewataka makandarasi na wasimamizi wa miradi kutoa elimu kwa waajiriwa kila siku kabla ya kuanza kazi kukemea tabia za wizi na ubadhilifu wowote utakaowezea kutokea kwani ni moja ya sababu za miradi pia kuchelewa na gharama kuongezeka.

  Kuhusu suala la ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami Mhe. Kwandikwa, ameridhishwa na kasi ya ujenzi ya mkandarasi huyo ambapo mpaka sasa maendeleo ya mradi umefikia asilimia 52.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma wakati akikagua mashine ya kucharangia mawe kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
  Mkandarasi wa Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation Zhu Wan Li akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (wa tatu kushoto), kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kidahwe-Kasulu yenye urefu wa KM 63 inayojengwa kwa kiwango cha lami, ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 52, mkoani Kigoma.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa, akisikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Raphael Ndimbo (kushoto), katika chumba cha maabara ya mkandarasi wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa wa barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 63 kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Kigwangalla “Sasa tutakamata majangili kuliko kukamata nyara” Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla ameweka wazi kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake hiyo ni kuhakikisha wanachukua hatua za haraka katika kulinda rasilimali za Taifa kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili nchini. 
   
  Dkt. Kigwangalla amesema hayoi mapema leo mjini Dodoma wakati wa akielezea namna walivyojipanga kukamata majangili kabla hawajhafanya ujangili. “Tumekusudia kukamata majangili kabla hawajafanya ujangili kuliko kukamata nyara. Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya  biashara haramu ya ujangili nchini.
   
   Ameeleza Dkt.Kigwangalla Aidha, ameendelea kutuma salamu kwa majingili wote kuachana na baishara hiyo kwa kujisalimisha ama kukimbia kwani kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa mtandao mpana wa majingili. “Jana  tumefanikiwa kumkamata Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu, akijipanga kuelekea Moru, ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa malengo ya kuua Faru. 
   
  Amekutwa na risasi 356, magazines 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha. Wizara yangu imejipanga na tutaendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili huu” alimalizia Dkt.Kigwangalla. Dkt.Kigwangalla amebainisha kuwa, tayari vikosi maalum  kwa kushirikiana na Wizara yake wakiwemo wale wa Wanyama pori wanaendelea na uchunguzi wa ndani hasa katika mitandao ya Majangili wakubwa wa ndani na nje ya Nchi. 
  Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu aliyekamatwa akijipanga kuingia Hifadhi ya Serengeti 
  Baadhi ya risasi zilizokamatwa na jangili huyo 
  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla akiwa pamoja na Mhifadhi wa Mkuu wa Serengeti William Mwakilema pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro wakiangalia mpaka unahishia pori tengefu la Loliondo-Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti mwishoni mwa wiki wakati wa kukagua maeneo hayo yenye mgogoro na wafugaji.  0 0
  0 0

  Arusha.Kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini imewatambua kwa kuwapa zawadi wakulima bora watatu waliotangazwa washindi kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji ya Nanenane kanda ya Kaskazini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Themi jijini hapa mwezi Agosti mwaka huu na mkulima mmoja aliyeongoza kwa kuandaa mashamba darasa. 

  Meneja Kiongozi wa kampuni hiyo nchini,Frank Wenga alisema wameamua kutoa zawadi za baiskeli zenye boksi maalumu la kubebea pembejeo wakati wa kilele cha Jukwaa la Wakulima Meru (Juwame) baada ya kutambua uwezo wao katika kilimo cha kisasa kinachozingatia kanuni za matumizi ya mbegu bora.

  "Kampuni yetu inawapongeza kwa kuonesha mfano wa kuigwa katika mikoa yenu,naamini wakulima wengine wataiga mbinu sahihi za kilimo mnazotumia kufikia malengo hadi kutambuliwa kwenye maonesho ya kanda ya kaskazini kama wakulima bora nasi tukiwa wadau tunawapongeza,"alisema Wenga

  Walionufaika na baiskeli hizo zenye thamani ya Sh 1.2 milioni ni mkulima bora kutoka mkoa wa Kilimanjaro ni Ebenezeri Shao,Kaanael Kitomari kutoka mkoa wa Arusha, Boay Tlem mkoa wa Manyara na Letayo Nnko mkulima kutoka halmashauri ya Meru ambaye ameandaa mashamba darasa mengi zaidi kwaajili ya kutoa elimu kwa wakulima wenzake.
  Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha wakimsikiliza Mkuu wa idara ya Kilimo ya halmashauri ya Meru,Grace Solomon kwenye kilele cha siku tatu za maonesho ya Jukwaa la Wakulima Meru(Juwame) eneo la Leganga. 
  Meneja kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kushoto) na Mkuu Idara ya Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Grace Solomon(katikati) wakimkabidhi zawadi ya baiskeli yenye boksi maalumu la kubebea pembejeo mkulima bora kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane mwaka huu kutoka mkoa wa Kilimanjaro,Ebenezer Shao .  
  Meneja kiongozi wa kampuni ya mbegu ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kushoto) na Mkuu Idara ya Kilimo katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Grace Solomon(katikati) wakimkabidhi zawadi ya baiskeli yenye boksi maalumu la kubebea pembejeo mkulima bora kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya Nanenane mwaka huu kutoka mkoa wa Arusha,Kaanael Kitomary . 


  0 0

  Na.Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Serikali imetoa onyo kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe juu ya taarifa za upotoshaji wa takwimu za Pato la Taifa alizozitoa hivi karibuni.

  Taarifa hizo za Mh. Zitto zimeripoti kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017 kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7 ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017.

  Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Bw. Daniel Masolwa Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa za Takwimu (NBS),kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS,pamoja na  Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Johnson Nyella wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari.

  Masolwa amesema kuwa upotoshaji huo uliofanywa na Mh. Zitto ni wa makusudi na unalenga kuonesha kuwa juhudi znazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano hazina manufaa kwa Wananchi.

  “Napenda kukanusha kauli ya Mh. Zitto kuhusu taarifa zake zinazodai kuwa takwimu za Pato la Taifa zimepikwa, Mh. Zitto anatakiwa kujua kwamba kazi ya kukokotoa takwimu za Pato la Taifa ni ya kitaalam na inafuata miongozo inayotolewa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Takwimu na Shirika la Fedha Duniani (IMF)”,alisema Masolwa.
  Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo ichani) wakati akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za pato la taifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Tafiti toka Benki Kuu Johnson Nyella
  Mkurugenzi wa Sera na Tafiti toka Benki Kuu Johnson Nyella (kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo ichani) wakati akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za pato lataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge (kushoto) akipokea taarifa ya Makabidhiano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Jordan Rugimbana Oktoba 30, 2017.
  Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge (kushoto) na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Jordan Rugimbana wakitiliana saini taarifa ya Makabidhiano ya ofisi Oktoba 30, 2017.
  Picha ya pamoja kati ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Jordan Rugimbana na Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge mara baada ya kukamilika kwa tukio la Makabidhiano ya ofisi baina yao Oktoba 30, 2017
  Picha ya pamoja kati ya Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Jordan Rugimbana pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma mara baada ya kukamilika kwa tukio la Makabidhiano ya ofisi baina ya Ndg. Rugimbana na Dr. Mahenge Oktoba 30, 2017.

  0 0


older | 1 | .... | 1989 | 1990 | (Page 1991) | 1992 | 1993 | .... | 3284 | newer