Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1987 | 1988 | (Page 1989) | 1990 | 1991 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Lilian Erica Maraure ametwaa taji la Miss Universe Tanzania katika mashindano yaliyofanyika Jumamosi usiku katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni  jijini Dar es Salaam.
  Lilian ambaye ni mtangzaji za TBC International ameshinda taji la 10 la mashindano hayo yalioanza kufanyika nchini mwaka 2007 ambapo mrembo Flaviana Matata alishinda taji hilo na baadaye kumaliza ndani ya 10 bora katika mashindano yaliyofanyika nchini Mexico..
  Mashindano hayo yalikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa warembo wengine hasa mshindi wa pili Anitha Mlay na mshindi wa tatu  Melody Tryphone. Warembo Rogathe Ally na Glory Gideon nao walimaliza katika nafasi ya nne na ya tano. Mashindano hayo yaliandaliwa na kampuni ya  Compass Communications chini ya mkurugenzi, Maria Tsehai Sarungi.
  Liliani alivishwa taji na Miss Universe Tanzania wa mwaka jana,  Jihan Dimachk. Warembo wengine walioshiriki katika mashindano hayo ni Silvia Mkomwa, Prisca Dastan(wote kutoka Dar es Salaam) ambapo kutoka Mwnza ni Maureen Foster na Mary Peter na kutoka Mbeya alikuwa Zahra Abdul.
  Warembo hao waliweza kutoka burudani ya aina yake chini ya mkufunzi, Lilian Loth ambaye alimaliza nafasi ya pili katika mashindano ya mwaka jana na pia ni mshindi wa pili wa shindano la Miss Africa second princess.
  Mashindano hayo yalidhaminiwa na SeaCliff Court Residence, Diana Magese, MnM, Kasakana, Bonuzi  na burudani safi ilitoka kwa  DDI Dance, poetry group (Romantic), na Jeff Mduma ambaye aliimba wimbo wa “A beautiful”.
  Lilian Erica Maraure baada ya kutwaa taji la Miss Universe Tanzania katika mashindano yaliyofanyika Jumamosi usiku katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni  jijini Dar es Salaam.
    Miss Universe Tanzania 2016, Jihan Dimachk (kulia) akimvisha taji mshindi mpya wa shindano hilo mwaka huu  Lilian Erica Maraure mara baada ya kutwaa taji hilo jana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam

   Miss Universe Tanzania 2017, Lilian Erica Maraure (katikati) akipozi katika picha pamoja na mshindi wa pili Anitha Mlay (kushoto) na mshindi wa tatu  Melody Tryphone mara baada ya kutangazwa kushinda katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam
   Majaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania wakifuatilia kwa umakini shindano hilo.
   Jaji Mkuu wa Mashindano hayo yaliandaliwa na kampuni ya  Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi akitangaza warembo watano bora walioingia katika mashindano hayo.
  Jaji Mkuu wa Mashindano hayo yaliandaliwa na kampuni ya  Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi kushoto na Miss Universe Tanzania wa mwaka jana, Jihan Jihan Dimachk wakiwa katika ‘red carpet’.

  0 0

  NA; MWANDISHI MAALUM – KASULU
  Kufuatia zoezi linaloendelea la oparesheni kamata mifugo linaloongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, serikali kwa mara nyingine imetaifisha kiasi cha ng’ombe 171 waliokamatwa katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
  Akiongea katika zoezi hilo Waziri Mpina amesema Wilaya za mipakani mwa Nchi jirani ziko katika tishio kubwa la kuvamiwa na mifugo na kuelekeza mwanasheria wa Wilaya ya Kasulu kuanza kuandaa utaratibu wa mahakama kuzipiga mnada. “Hatua ya kwanza sisi kama Serikali tunataifisha ng’ombe hawa na kufanya utaratibu wa kuzipiga mnada na mwanasheria wetu wa Serikali aanze taratibu ambapo ng’ombe hao tutawapiga mnada kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama No. 17 ya mwaka 2003.” alisema Mpina.
  Mpina aliongeza kusema kuwa, ng’ombe hao kwa sasa wataendelea kuwa chini ya Serikali mpaka taratibu zitakapo kamilika, na kuitaka  kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kasulu  kuelendelea kwa kasi kubwa kukamata mifugo katika mapori na kuhakikisha mifugo yote inapatikana.
  Sambamba na hilo, Waziri Mpina aliwataka wananchi kujiadhari  na kuondoka katika kununua kesi zisizokuwa za kwao kwa kuikubali mifugo kutoka nje ya nchi kuwa ni ya kwao, kwani ni kujitaftia matatizo na kuisadia serikali katika jitahada hizi za kukamata mifugo inayoingia ndani ya nchi kinyume na taratibu.
   “Kwa hiyo wananchi wawe namba moja kuwafichua watu hao, na wale tunaowabaini  kuwa wanaitikia mifugo toka nje ya nchi kuwa ni mali yao lazima wachukuliwe hatua.” alisisitiza Mpina.
  Awali akitoa taarifa ya ng’ombe hao waliokamatwa katika Wilaya hiyo mkuu wa wilaya hiyo Mwanahawa Mrindoko alisema ng’ombe hao ni mali ya  raia wa Rwanda kwani Serikali ya wilaya ilikuwa inawatafuta Raia  wahamiaji haramu  na kuwapata, hivyo sheria itachukua mkondo wake, na aliongeza kwa kusema kuwa kamati ya ulinzi na usalama itaendelea na zoezi la kuwatafuta wafugaji ambao ni wahamiaji haramu.
  Akiwa katika wilaya ya Kakonko Waziri Mpina aliagiza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo  kupitia Mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagalla kuanza mara moja zoezi la oparesheni ya kukamata mifugo toka nje ya nchi kwani tarifa za awali zinasema kuwa Wilaya hiyo ilikuwa haijaanza kabisa kutekeleza agizo hilo na ni moja ya Wilaya ya mpakani mwa nchi jirani ya Burundi.

   Picha Ng’ombe aina ya nyankole kutoka Rwanda, waliotaifishwa na serikali katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu wakisubiri kukamilika kwa taratibu za mahakama kwa ajili ya kupigwa mnada.
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (kulia) akiongea na kikosi kazi cha  Wilaya ya Kasulu iliyoshiriki katika zoezi la kukamata ng’ombe aina ya nyankole kutoka Rwanda,  waliovamia katika kijiji cha Kakere, kushoto kwake ni kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Mwanahawa Mrindoko.
   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, akiangalia Ng’ombe aina ya nyankole waliopo katika kijiji cha Kakere baada ya kutaifishwa na serikali.
  Waziri Mpina akiongea na wanahabari hawapo katika picha baada ya zoezi la kutaifisha kundi la ng’ombe waliovamia katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu.

  0 0  Naibu waziri wa Mifugo  na Uvuvi, Abdallah  Ulega  amewatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru  wananchi waliotoa taarifa  zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni.
  Naibu waziri huyo ametoa tahadhari hiyo leo wakati akizungumza  na wakazi wa kata za Mgagao na  Kirya  zilizopo wilaya  Mwanga mkoani Kilimanjaro.
  Amesema Serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama  vipo makini na kuhakikisha  usalama wananchi wa eneo.
  Amesema Serikali  ipo makini  na ina macho na masikio  ya kutosha na ipo kila mahali na kwamba kama kuna mpango mbaya dhidi ya wananchi waliotoa taarifa hizo hautafanikiwa.
  "Jambo  limeshapita acheni kutafuta mchawi. Mkae mkijua  kwamba Serikali  ina mkono mrefu atakayethubutu  kutenda mambo ataishia kwenye vyombo vya dola," amesema Ulega.
  Ulega amedai kupata taarifa  za kuwapo kwa baadhi ya wafugaji kuanza vikao  vya kumtafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo
  Mbali na hilo, naibu waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali  ya Rais John  Magufuli  ipo makini na imelenga kuwatetea wanyonge  na kwamba, haina nia ya kuchukua mifugo ya wafugaji  kwenye mchakato wa upigaji wa chapa.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega  akizungumza na wanachi wa  kata za Mgagao na  Kirya  juu ya kuwatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru  wananchi waliotoa taarifa  zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni.
   Mmoja wa wananchi akitoa kero yake mbele ya  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega wilaya  Mwanga mkoani Kilimanjaro.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega akiwasili katika  kata Mgagao na  Kirya  wilaya  Mwanga  ikiwa ni sehemu ya  ziara yake ya kikazi mkoa wa  Kilimanjaro.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya  Mwanga wakiangalia zizi la ng’ombe lilokuwa likihifadhi mifugo iliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni na kukamatwa na Serikali.

  Semu ya wananchi wakimsikiza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega leo  mkoa wa  Kilimanjaro.Picha na Emmanule  Massaka,Glob ,jamii Kilimanjaro.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu aagiza Hospitali na Vituo vya Afya vyote vya Serikali nchini kuanzia kutoa huduma ya uchunguzi wa Saratani kila siku wakati wa kliniki ya mama na mtoto, sambamba na huduma hizi kila mwezi wanatakiwa kuwa na siku moja kwaajili ya kuchunguza na kufanya matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti.
  Ameyasema hayo wakati alipofungua matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, yalifunguliwa katika viwanja vya hospitali ya Ocean Road Jumamosi  jijini Dar es salaam.

  Ummy ameipongeza kazi nzuri inayofanywa na Uongozi wa Hospitali ya Ocean Road katika kutimiza majukumu yake ikiwemo kuongeza vitanda 40 mpaka vitanda 100 kwa gharama zao kwaajili ya wagonjwa wa saratani pindi wanapopata huduma za matibabu ya Chemotherapy.
  “Katika kuwaunga mkono Serikali ya awamu ya tano ya Mh. Magufuli imewapatia Bilioni 5 kwajili yakukamilisha mashine za kisasa za matibabu ya Saratani kwa kutumia mionzi.” alisema.
  Ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Hospitali ya Ocean Road kuwa wanatakiwa kwenda kwenye shule za Msingi na Sekondari ili kuwajengea watoto uelewa kuhusu ugonjwa wa Saratani, lakini ni vipi wataweza kujikinga na magonjwa yasiyo yakuambulizwa ikiwemo ugonjwa wa Saratani.
  Pia ametoa rai kwa wananchi wote hususani wanawake kujitokeza kupima ugonjwa huo kwani unatibika endapo itagunduliwa mapema, Nae Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Grace Maghembe ambae pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Dkt. John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto kwa kazi kubwa wanayoifanya ikiwemo kuongeza kwa bajeti ya Dawa , vifaa tiba vya uchunguzi na matibabu.
  Kwa upande mwingine Dkt. Grace Maghembe kwa niaba ya bodi ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu na bidii kubwa katika kuhakikisha kwamba wanakabiliana na ugonjwa huu wa Saratani kwa wananchi hasa wale wa hali ya chini na kuahidi kuendelea kuboresha huduma hii.

  “Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kwenda kupima Saratani kwani ni bure, usisubiri mpaka kuugua, ukichelewa grarama zinaongezeka lakini pia uwezekano wa kupona unakuwa ni mdogo”, alisema Dkt Maghembe
  Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage amemhakikishia Waziri Ummy kwamba upatikanaji wa dawa katika Hospitali hiyo ni 80% na dawa za wagonjwa wengi zinapatikana kwa 100%, ukilinganisha na 2015/2016 upatikanaji wa dawa ilikuwa 4% tu, jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kubwa na kufanya malalamiko ya dawa kuwa makubwa sana katika hospitali hiyo, hivyo kuishukuru Serikali ya Magufuli kwa niaba ya Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu.

  Mwisho Dkt. Julius Mwaiselage amemhakikishia waziri kwamba Hospitali ya Ocean Road ipo katika hatua ya Mwisho ya kuweka mashine mpya mbili (Linear accerelators), hivyo zitasaidia kupunguza muda wa kusubiri kwa wagonjwa kusubiri huduma , lakini kubwa kupunguza wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi.


  Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu watatu kutoka kushoto wakati alipofungua matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, kulia kwa Mh. Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage na kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Grace Maghembe.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi cheti moja ya wadau waliofanikisha matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti iliofanyika mapema leo katika viunga vya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu wakirusha Maputo juu kuashiria ufunguzi rasmi wa matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti, iliofanyika katika viunga vya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiambatana na Binti yake katika matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa Saratani ya matiti yaliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
  0 0
 • 10/29/17--11:53: Article 2
 •  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega  akizungumza na wanachi wa  kata za Mgagao na  Kirya  juu ya kuwatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru  wananchi waliotoa taarifa  zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni.

  Naibu waziri wa Mifugo  na Uvuvi, Abdallah  Ulega  amewatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru  wananchi waliotoa taarifa  zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni.


  Naibu waziri huyo ametoa tahadhari hiyo leo wakati akizungumza  na wakazi wa kata za Mgagao na  Kirya  zilizopo wilaya  Mwanga mkoani Kilimanjaro.


  Amesema Serikali haitawavumilia watu wa aina hiyo na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama  vipo makini na kuhakikisha  usalama wananchi wa eneo.


  Amesema Serikali  ipo makini  na ina macho na masikio  ya kutosha na ipo kila mahali na kwamba kama kuna mpango mbaya dhidi ya wananchi waliotoa taarifa hizo hautafanikiwa.


  "Jambo  limeshapita acheni kutafuta mchawi. Mkae mkijua  kwamba Serikali  ina mkono mrefu atakayethubutu  kutenda mambo ataishia kwenye vyombo vya dola," amesema Ulega.


  Ulega amedai kupata taarifa  za kuwapo kwa baadhi ya wafugaji kuanza vikao  vya kumtafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo  Mbali na hilo, naibu waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali  ya Rais John  Magufuli  ipo makini na imelenga kuwatetea wanyonge  na kwamba, haina nia ya kuchukua mifugo ya wafugaji  kwenye mchakato wa upigaji wa chapa.
   Mmoja wa wananchi akitoa kero yake mbele ya  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega wilaya  Mwanga mkoani Kilimanjaro.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega akiwasili katika  kata Mgagao na  Kirya  wilaya  Mwanga  ikiwa ni sehemu ya  ziara yake ya kikazi mkoa wa  Kilimanjaro.
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah  Ulega akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya  Mwanga wakiangalia zizi la ng’ombe lilokuwa likihifadhi mifugo iliyoingia nchini kinyume cha Sheria hivi karibuni na kukamatwa na Serikali.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.Richard Mayongela (wa tatu kulia), jana akiandika mambo mbalimbali katika mkutano na wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Mwanza. Wa pili kushoto ni Meneja wa kiwanja hicho Bi. Esther Madale na wa kwanza kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Agustino Magele.
  Bw. Edger Mwankuga aliyesimama jana akiwasilisha hoja zake mbalimbali mbele ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (hayupo pichani) alipokutana na wafanyakazi wa kiwanja cha ndege cha Mwanza na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.
  Wafanyakazi wa idara mbalimbali za kiwanja cha ndege cha Mwanza na kikosi cha zimamoto na uokoaji, wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela alipokutana nao jana kujadili masuala mbalimbali ya kiuendeshaji.

  Na Mwandishi Wetu

  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wataendelezwa kwa kupata mafunzo mbalimbali, ili kuongeza weledi na tija kazini, imeelezwa. Kauli hiyo ambayo ni moja ya malengo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela jana alipoongea na wafanyakazi wa Kiwanja cha ndege cha Mwanza pamoja na Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi.

  Bw. Mayongela alisema wafanyakazi wakipata mafunzo zaidi ya kazi zao wataisaidia serikari kufanikisha moja ya malengo yake makuu ya kukuza uchumi, ambapo watakuwa na mbinu za kisasa zikiwemo za ukusanyaji wa mapato kwa uaminifu na uadilifu, ambapo viwanja vya ndege ni moja ya vyanzo vya mapato hayo.

  Hata hivyo, alisema atapitia majalada ya wafanyakazi wote ili kubaini waliojiendeleza kwa mafunzo mbalimbali, lakini wanafanyakazi zisizo za kada zao, hivyo ataangalia uwezekano wa kuhamishiwa kwenye kada zao ili waweze kufanya kazi kwa weledi zaidi. “Wapo wafanyakazi wa kada mbalimbali waliojiendeleza, lakini hadi sasa bado wapo kwenye kada walizoajiriwa nazo na zipo tofauti na sasa, nitangalia uwezekano wa kupangiwa kada zao ili waweze kuenda na kasi ya kazi zinazowahusu,” alisema Bw.Mayongela.

  Pia malengo yake mengine alisema atahakikisha anaboresha maslahi ya wafanyakazi wa ngazi ya chini ili kunyanyua ari na tija kazini, ambapo kwa sasa wamekata tamaa kutokana na maslahi duni yasiyolingana na kazi zao.

  Lakini aliwaasa wafanyakazi wenye mamlaka ya kuingia mikataba na wafanyabiashara, kubadilika na kuhakikisha wanatumia vyema sheria zinazowaruhusu kuingia mkataba baina yao na sio kukiuka, kwani inaweza kuwaletea matatizo, endapo itabainika kuwepo kwa udanganyifu uliosababisha upotevu wa mapato ya serikali, kwa kuwa atahakikisha TAA inajitosheleza kimapato na kujiendesha kwa baadhi ya mambo ya ndani bila kutegemea fedha kutoka Serikali Kuu.

  Alisema kwa sasa TAA imekuwa ikinyooshewa kidole kwa kusemwa vibaya na wadau mbalimbali, lakini kupitia umoja na mshikamano wa wafanyakazi atahakikisha anarudisha taswira nzuri iliyokuwepo na kujenga Mamlaka mpya yenye kuaminika. Pia alizungumzia uadilifu na ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi, kuacha mara moja vitendo vinavyoweza kuhujumu jitihada na vipaumbele kwa mwaka huu wa fedha 2017/18 hadi kufikia 2020/21.

  “Mimi ni mgeni katika nafasi hii (ya Ukurugenzi), lakini ninachoomba tufanye kazi kwa bidii, mvunje makundi na tukosoane kwa kujenga na sio kubomoa, na viongozi muache kupendelea mtende haki kwa wafanyakazi wote, tukiwa na lengo la kuijenga TAA yenye mwelekeo mpya,”alisema Bw. Mayongela.

  0 0

  Viongozi mbalimbali na waamini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa utendaji kazi na kuleta maendeleo katika Jimbo hilo.

  Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe.

  Viongozi hao wamempongeza Mbunge Mavunde kwa kugawa vitabu vya Misahafu 50,Juzuu 400 na Kanzu 300 katika misikiti mbalimbali hapa Dodoma Mjini na kwa kusimamia mabadiliko makubwa katika sekta za Afya, Elimu, Miundombinu, Michezo na Uwezeshaji wananchi.

  Akitoa maelezo ya awali,Mwalimu wa Madrasa Ustadhi Omar Salum Itara amemshukuru Mavunde kwa msaada mkubwa alioutoa katika Madrasa hiyo ikiwa pamoja na kuwawekea umeme ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza mpaka usiku.

  Kwa upande wake, Mavunde akizungumza katika Dua hiyo, amewashukuru Viongozi na waamini wa dini ya kiislamu kwa namna wanavyomuunga mkono katika shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo na kuwaomba waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu atimize majukumu yake vyema.

  Mavunde ameipa Misikiti 16 Spika moja kila mmoja zenye thamani ya Tsh 4,000,000 na pia ameahidi kukabidhi Laptop 2 zenye thamani ya Tsh 1,000,000 na milango miwili yenye thamani ya Tsh 500,000 kwa ajili ya madrasa ya Darul Mustafa.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa kwenye picha na viongozi wa dini.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisikiliza mawaidha katika Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu
  Tamasha la nne linalojumuisha muziki wa kiasili na kimataifa nchini, linalojulikana kwa jina la kigeni kama Karibu Music Festival linatarajia kutimua vumbi Ijumaa hii katika viwanja vya Mwanakalenge Bagamoyo Mkoani Pwani, ambapo vikundi zaidi ya 30 vinatarajiwa kutoa burudani bure kwa Wakazi wa Bagamoyo kwa siku tatu mfululizo.
  Mratibu wa Tamasha hilo maarufu duniani Richard Lupia ameiambia Mdimuz Blog kwamba maandalizi ya tamasha hilo lenye lengo la kukutanisha marafiki, kukuza sanaa na utamaduni pamoja na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake yamekamilika, na tayari makundi kutoka nje ya nchi yatakayohusika na utumbuizaji katika tamasha hilo yameanza safari ya kuja Tanzania.
   Lupia ametaja baadhi tu, ya wasanii kutoka nje ya nchi wanaokuja kushiriki tamasha hilo kuwa ni pamoja na Jackie Paladino kutoka Marekani, De Lukes na Selmor Murtukudzi kutoka Zimbabwe, Total Hp Hop Replacement judoka Denmark, Bernice Boikanyo kutoka Afrika ya kusini, Motra Music na Fadhilee Itulya kutoka Kenya na Nigun Yerushalmy kutoka Israel.
  Pamoja na maonesho ya jukwaani, Yamaha pia litaambatana na semina kwa wasanii wa ndani ambapoembat watakuwa wakiongezewa uelewa juu ya sanaa na utamaduni katika ngazi ya kimataifa na pia hapo hapo uwanjani kutakuwa na maonesho ya kazi za sanaa ya mikono.
  Kwa upande wa Tanzania wasanii watakaowakilisha watakuwa ni Laveda, Wamwiduka Band, Safi Theatre, Wahapahapa, GodyKaozya, Jwagwa Music na Dus Top Acoustic.
  Bw Lupia amewahakikishia wakazi wa Bagamoyo burudani iliyotawaliwa na usalama wa hali ya juu huku akisisitizwa kwamba vikundi alivyovtaja kushiriki tamasha ni baadhi tu ya vikundi, kuna zaidi ya burudani katika tamasha la mwaka huu. 
  Tamasha litaanza Ijumaa Novemba 3, 2017  na kumalizika Jumapili  Novemba 5, mwaka huu
  0 0

  Na Greyson Mwase, Simiyu

  Wachimbaji wa madini ya dhahabu katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kufanya utafiti wa madini katika maeneo yao ili waweze kuwa na uhakika wa uchimbaji wa madini na uzalishaji wao kuwa na tija.

  Wameyasema hayo leo tarehe 29 Oktoba, 2017 katika ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu yenye lengo la kukusanya kero za wananchi mbalimbali hususan katika shughuli za uchimbaji madini.

  Akizungumza kwa niaba yao, Sylivester Fundikira alisema kuwa wameunda jumla ya vikundi 30 ambapo kila kikundi kina mashimo yake na kueleza kuwa wamekuwa wakipata changamoto ya upatikanaji wa madini ya uhakika kutokana na maeneo yao kutofanyiwa utafiti kwa muda mrefu.

  Akijibu kero hiyo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alisema kuwa Wizara ya Madini kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) imekuwa ikifanya tafiti sehemu mbalimbali nchini na kusisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo tayari kuwasaidia.

  Alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo wa madini na kuongeza kuwa imeweka mikakati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwapatia vifaa kupitia ruzuku ili uchimbaji wao uwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

  “ Tuna mpango wa kuhakikisha kuwa rasilimali za madini zinakuwa na mchango mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo tutahakikisha tunasimamia ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya uchimbaji madini yanakuwa rafiki,” alieleza Naibu Waziri Nyongo.

  Katika hatua nyingine, Nyongo alisema kuwa kazi yake pamoja na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakua kwa kasi na kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Alisema kuwa sekta ya madini imekuwa na changamoto kubwa hususan katika upotevu wa mapato kutokana na wawekezaji wasio waaminifu na kukwamisha juhudi za serikali katika ukusanyaji wa mapato.

  Aliendelea kusema kuwa tangu Rais John Magufuli ameanza kupambana na wezi wa rasilimali za madini kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwa uzalishaji na mapato umebadilika kutokana na Serikali kuhakikisha kiwango sahihi kinapatikana na kulipiwa kodi serikalini.

  Alisema Serikali imeweka Sheria Mpya ya Madini ya mwaka 2017 na kuwataka wachimbaji madini nchini kufuata sheria hiyo pamoja na kanuni zake.
  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, akijibu kero mbalimbali za wakazi wa kitongoji cha Mwanguhi kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Seif Shekalaghe akifafanua jambo mbele ya wakazi wa kitongoji cha Mwanguhi kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
  Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini, Sylivester Fundikira akiwasilisha kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).
  Sehemu ya wakazi wa kitongoji cha Mwanguhi kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara.

  0 0

  WAZIRI wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ameshauri utaratibu unaofanyika katika kusaidia maendeleo ya Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini uendelee katika maeneo mengine ya nchi kwa sababu umeonyesha mafanikio makubwa. Akizindua Kongani ya Mbarali inayojumuisha mikoa miwili ya Mbeya na Songwe mkoani hapa mwishoni mwa wiki/
   Dkt. Tizeba alisema Kituo cha Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT) kimefanya kazi kubwa katika sekta ya kilimo hali inayokifanya kuwa miongoni mwa vituo vinavyohitajika barani Afrika. 
   “Utaalamu upo na uwezo wa kufanya hivyo tunao, kwa kawaida jirani anapofanya vema lazima wengine waone wivu hivyo mpango huu tuupeleke maeneo mengine ya nchi kwa kuwa hatuna sababu za kuona baadhi ya mikoa inaneemeka na mingine inabaki hivihivi,” alisema Dkt. Tizeba. Alibainisha kuwa kituo hicho kinasimamia mambo mengi katika ukanda huo wa nyanda za juu kusini ikiwemo kusimamia miundombinu hasa ya nishati, barabara na maji. Hivyo kuwepo shughuli za SAGCOT katika maeneo mengine ya nchi ni faida kwa watanzania wote. 
   “Kuchaguliwa kwa ukanda huu kulikuwa na sababu nyingi ikiwemo hali ya hewa, sababu hizohizo zitumike kupeleka shughuli hizi maeneo mengine. Kazi yetu serikali ni kuweka mazingira wezeshi na kazi hiyo tunaifanya vema,” alisema Dkt. Tizeba na kugusia changamoto zilizokuwepo kwa kusema: “Zipo changamoto zinazotukabili katika kilimo ikiwemo uduni wa teknolojia, hali inayosababisha kupanda gharama za uzalishaji kwa wakulima wadogo. 
  Vilevile kuna kodi za kero kwa wakulima ambapo mkulima akishavuna anatakiwa kulipa kodi zaidi ya tatu. Haya lazima tuyatafutie ufumbuzi kwa pamoja ikiwa tunataka kusonga mbele kwenye kilimo.” 
   Akizungumza kwa niaba ya wabia wa kituo hicho Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Uingereza (DIFD), Bi. Beth Arthy alisema kinachofanyika katika ukanda huo ni jambo kubwa kwa sababu kilimo ndicho kitu pekee kitakachosaidia kukuza uchumi wa Tanzania. 
   “Mimi ni mgeni katika nafasi hii lakini nilipofika Tanzania nimezunguka maeneo mengi ya nyanda za juu kusini, nimeonana na wakulima wadogo na kujua changamoto zao, nimeona kwa macho yangu umuhimu wa sekta binafsi na sekta ya umma kufanya kazi pamoja. 
   “Bwana Kirenga,Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT na timu yake wamefanya kazi kubwa sana katika ukanda huu kwenye kilimo. Hiki wanachofanya ni wazi wanamsaidia Rais John Magufuli kufikia uchumi wa viwanda kwa sababu malighafi za viwandani zinatoka kwa wakulima,” alisema Bi. Arthy. 
   Akizungumzia safari ya kituo hicho Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Bwana Geoffrey Kirenga alisema majadiliano kati ya sekta binafsi na sekta ya umma katika kusuhirikiana katika kilimo ndiko kulikosababisha kuzaliwa kwa mpango huo. 
   Alisisitiza kuwa kupewa jukumu la kusimamia kilimo katika kongani hizi ni heshima kubwa kwao na wanaahidi kufanya vizuri na kuongeza kuwa safari ya sagcot ilianza kama majadiliano kwa sekta binafsi na sekta ya umma. “Utaona tunataja eneo la ukanda huu lakini tumeligawa ktika kongani, sababu zake ni kuwa hatuwezi kufika kila sehemu kwa wakati mmoja, tunataka hadi ifikapo mwaka 2030 mbali ya mambo mengine tuwaondoe katika umasikini wakulima zaidi ya milioni mbili si jambo dogo. 
   “Vilevile tuongeze makusanyo yatokanayo na kilimo nchini, tutambue pia kufanya kazi katika kilimo changamoto yake ni rasilimali ya asili, hasa hali ya sasa ya mabadiliko ya tabianchi ukikosea unaweza usiendelee kuzalisha,” alisema Bw. Kirenga. SAGCOT ina kongani sita ambazo ni Ihemi inayojumuisha mikoa miwili ya Iringa na Njombe, Mbarali (Mbeya na Songwe), Kilombero (Morogoro), Ludewa (Ruvuma), Sumbawanga (Rukwa) na Rufiji (Pwani), ambapo katika maeneo hayo inaangaziwa ongezeko la mnyororo wa thamani katika mazao ya nyanya, viazi mviringo, chai, mahindi, mchele, soya na maziwa. 
   Wabia wa kituo hicho ni Serikali ya Tanzania, Ubalozi wa Norway, Benki ya Dunia, UKAID, USAID, UNDP na AGRA.
    Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akifurahia baada ya kuzindua kongani ya Mbarali inayojumusiha mikoa ya Songwe na Mbeya chini ya Kituo cha Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT),
  wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Amos Makala na mwakilishi wa wabia wa kituo hicho ambaye ni Mkuu wa DFID Tanzania, Bi. Beth Arthy. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Mbeya
    Sehemu ya wabia wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT), wakiwa katika uzinduzi wa kongani mpya ya Mbarali inayojumuisha mikoa miwili ya Mbeya na Songwe mkoani Mbeya mwishoni
  mwa wiki.
  Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akihutubia wadau wa kilimo waliohudhuria katika ufunguzi wa wa Kongani mpya ya Mbarali inayojumuisha mikoa miwili ya Mbeya na Songwe mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki.

  0 0

   ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 26 KUGAWIWA  WANAHISA WA VODACOM 
  Zaidi ya wanahisa 1500 wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC,Walikutana kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki na kufanya mkutano  na Uongozi wa kampuni hiyo na  kuchagua viongozi mbalimbali na kufikia mwaafaka wa gawio la kwanza la Hisa kwa wanachama hao utakaotolewa na kampuni hiyo  kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 26 ifikapo mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu. 
  Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,na Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki alipokuwa akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa gawio hilo kwa wanahisa wake. 
  Mwenyekiti huyo wa bodi alisema kwamba kila mwana hisa atapatiwa gawio hilo la shilingi 12 na senti 74. 
  Aidha alisema kampuni hiyo imeamua kufanya hivyo kutokana na kuimarika vizuri kwa kujiendesha kibiashara hivyo iliona ni vyema kutoa gawio hilo, ili kila mwanahisa aweze kunufaika pale inapobidi. 
  Kampuni hiyo pia iliweza kufanya mkutano wake Mkuu wa mwaka kwa kuwakutanisha wanachama wake kutoka mikoa mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo pamoja na kwenda sambamba na uteuzi wa wajumbe wapya watakaoingia ndani ya bodi ya wakurugenzi. 
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Ian Ferrao  aliwapongeza wajumbe wote walioteuliwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha hisa za vodacom zinaleta manufaa kwa wamiliki wake wote. 
  “Wanahisa watoe shaka kabisa kuhusiana na hisa zao kwani zipo salama na kampuni inaendelea kufanya vizuri sokoni na ninawapongeza wajumbe walioteuliwa na ninaimani nayo  kwani itafanya kazi kwa kushirikiana vizuri  na wanachama ndani nasi tutawapa ushirikiano wakutosha ndani ya kampuni yetu”Alisema Ferrao. 
  Mkutano huo mkuu wa mwaka umefanyika kwa mara ya kwanza kwa wanachama wake tangu kampuni hiyo iuze hisa zake kwa Umma.

   Baadhi ya wanahisa wa Vodacom Tanzania PLC wakifuatilia mada wakati wa mkutano mkuu  wa kwanza  wa wanahisa hao uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Baadhi ya wanahisa wa Vodacom Tanzania PLC wakifuatilia mada wakati wa mkutano mkuu  wa kwanza  wa wanahisa hao uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Mmoja wa wanahisa za Vodacom Tanzania PLC akichangia mada wakati wa mkutano mkuu  wa kwanza wa wanahisa hao  uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
    Baadhi ya wanahisa za Vodacom Tanzania PLC,wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania PLC Ian Ferrao (kulia)wakati wa mkutano mkuu  wa kwanza wa wanahisa hao  uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki (kulia) akisalimiana na mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo, Adella Kaale,wakati wa Mkutano  mkuu wa kwanza wa wanahisa hao uliofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari( hawapo pichani)  juu ya Mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa wa kampuni hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Katikati ni Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo, Ali Mafuruki na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Jacgues Marais.


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja

   Baadhi ya Wakurugenzi katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  wakiwa katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
   Waziri wa  Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  Mhe.Moudline Syrus Castco (katikati) akisoma taarifa yake katika  kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara  hiyo katika Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wengine Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) na Naibu Waziri Mhe. Shadya Mohamed Suleiman
   Katibu Mkuu wa Wizara ya  Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Nd,Fatma Gharib Bilal akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),akiwepo na Mshauri wa Rais masuala  ya Wanawake na Watoto Bi. Zainab Omar Mohamed(kushoto)
  Mshauri wa Rais Ushirkiano wa Kimataifa Fedha na Uchumi Mhe,Mohamed Ramia Abdiwawa (kulia) alipokuwa akitoa mchango wake wakati wa kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 cha  Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),akiwepo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kushoto)
  Picha na IKULU

  0 0  0 0

  Na Dotto Mwaibale, Muleba, Kagera 
  Imeelezwa kuwa Usambazaji wa mbegu za mazao ya mizizi na Migomba kwa vikundi vya wakulima kwenye Mkoa wa Kagera utasaidia kuwahakikishia wananchi wa mkoa huo usalama wa chakula na mazao mbadala baada ya zao lao kuu la chakula la mgomba kuathiriwa na ugonjwa wa mnyauko. 
  Kauli hiyo imetolewa na Afisa Kilimo Mkoa wa Kagera, Louis Baraka wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa mbegu bora za mazao hayo kwenye wilaya tano za mkoa huo ambazo ni Missenyi, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Muleba. 
   Alisema kuwa wakazi wa mkoa huo wamekuwa na njaa kali kwa misimu miwili iliyopita kutokana na zao lao kuu la chakula la migomba kushambuliwa na ugonjwa hatari wa mnyauko na hivyo kuwafanya wananchi kuhangaika kutafuta chakula na kuomba chakula cha msaada kutoka Serikalini. 
   Baraka alisema kuwa upatikanaji wa mbegu bora za migomba safi iliyozalishwa kwa njia ya chupa itafufua zao hilo ambalo wakulima wengi walishalitelekeza kabisa baada ya kuona zao hilo likikauka na kushindwa kuwapatia chakula walichokizoea kwa miaka mingi. 
   Aidha Baraka ameishukuru Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo OFAB kwa kuwapelekea pia mbegu bora za Mihogo aina ya Mkombozi na Mbegu bora za viazi lishe ili kuwapatia wananchi wa mkoa huo mazao mbadala baada ya kutegemea zao la mgomba pekee. 
   Alisema kuwa kwenye wilaya zote tano za mkoa wa Kagera COSTECH imeweza kuwapatia mbegu za marando ya viazi lishe 30,000, Mihogo mbegu 27,000 na Migomba 1,000, ingawa wameongea na wafadhili hao na kuwaahidi kuwaongeza mingine zaidi ya 500. 
  Kaimu Ofisa Kilimo Wilaya ya Muleba,  Kokushubila Pesha akipanda mbegu ya muhogo katika shamba darasa la kikundi cha Ujamaa  lililopo Kata ya Magata Karutanga wilayani humo. 

  Ofisa Mtendaji wa kata ya Magata Karutanga Joyce Rassia akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa shamba darasa la kikundi hicho.

  Mjumbe wa kikundi cha Ujamaa,  Liberatha Lespicius akisoma risala wakati wa uzinduzi huo mbele ya mgeni rasmi.

  Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku,  Jojianas Kibula akitoa maelekezo kwa wakulima jinsi ya kupanda mbegu hizo bora za mihogo kwa wakulima wa kata ya Magata Karutanga wilayani Muleba.

  Baadhi ya wana kikundi cha Ujamaa wakishirikiana kwenye kupanda mbegu hizo bora baada ya uzinduzi rasmi wa shamba darasa hilo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

  0 0
  0 0
 • 10/29/17--22:53: TANZIA Dallas Texas Marekani
 • Ndugu Wanajumuiya,
  Kwa masikitiko makubwa mwanajumuiya Dr. Lindah Mhando na familia yake wa State College, Pa wanatangaza kifo cha mdogo wake *HAPPY OKOTH* kilichotokea Dallas, TX.
  Happy alipatwa na mauti wakati akisikiliza maombi jioni ya Prayer Line ya Ijumaa October 27, 2017 pale Baylor Hospital Plano, TX  alipokuwa amelazwa. Mama yake mzazi, Mama Elizabeth Okoth, alikuwa pamoja naye.
  Mipango ya Mazishi na taratibu zote zinaendelea na jumuiya itajulishwa yatayojiri.
  Kwa sasa ndugu, jamaa na marafiki wanafika kuhani nyumbani kwa marehemu:
  Advenir at Frankford Springs
  Dallas, TX 75287

  Kwa taarifa zaidi, wasiliana na:
  Ps. Steve Momoh  214-830-8459*(Husband)

  Rosemary Adelaja2147620270
  Michael Nnadi ‭8628497980
  Peter Mhando‭ 8144043781
  Jessica Kataraiya 214773-6697
  Eric Joshua 2145768903
  Mama Mponzi 9174491607

  Taarifa zaidi zitafuata baadae.
  UONGOZI unachukua nafasi hii kutoa pole kwa familia nzima ya marehemu. Tukumike pamoja kuiweka familia katika maombi wakati wa kipindi hiki kigumu. AMEN

  0 0

   Kilimanjaro Regional Commissioner, Ms. Anna Mghwira (centre), cuts a ribbon to officially open a new branch of Barclays Bank Tanzania in Moshi last weekend. Looking on the right is  Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed; on the left,  BBT Moshi Branch Manager, Ibrahim Omari  and Moshi District Commissioner, Kipi Warioba.

   Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed giving his welcoming remarks during the opening ceremony of BBT Moshi branch in Moshi, Kilimanjaro last weekend.
   Kilimanjaro Regional Commissioner, Ms. Anna Mghwira (centre), listens to Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left) during the opening ceremony on BBT Moshi branch. Looking on are Moshi District Commissioner, Kipi Warioba (right), BBT Moshi Branch Manager, Ibrahim Omari (second right),  and Barclays Tanzania Head of Customers Network, John Beja (second left).
  Barclays Bank Tanzania Managing Director, (third left), poses for a memento photograph with some Moshi branch officials after the ceremony. 


  0 0


  Nchini Tanzania Matumizi ya TEHAMA yame endelea kukua katika maeneo mbali mbali. Hii ime endelea kurahisisha upatikananaji wa huduma muhimu na kuwezesha watu kuendelea kuwasiliana kwa urahisi.

  Viwanda na Taasisi mbali mbali zimeendelea kutumia TEHAMA ili kukuza ufanisi na kufikia watu wengi kwa kipindi kifupi. Miamala ya kifedha, ukusanyaji kodi, pamoja na mawasiliano ni baadhi tu ya mambo yanayo wezeshwa na TEHAMA nchini.

  Usalama wa mifumo ya TEHAMA ni moja ya jambo muhimu sana ambapo Tanzania inapaswa kuwekeza ili kujilinda na aina zozote za kialifu mtandao ambazo zinaweza kupelekea huduma muhimu kutopatikana na hatimae uchumi wa Nchi kuyumba.
  -------------------
  STATISTICS: Tanzania installed 27,000 KMS of optic fiber connecting all regions and it has 7 mobile operators – About 94% network coverage, 85% SIM penetration and 40%internet users.
  -------------------
  Mkutano mkuu wa mwaka wa wataalam wa TEHAMA nchini Tanzania ulio fanyika mwishoni mwa wiki iliyopita (26 – 27, Octoba – 2017) jijini Dar-es salaam ulipata kujadili usalama mtandao ambapo mada kadhaa zilizo jikita katika kutoa elimu ya namna bora za kuimarisha usalama wa mifumo yetu zili wasilishwa na kujadiliwa.

  Binafsi, Nilizungumza na washiriki kuhusiana na namna bora ya kulinda taarifa zinazo patikana kwenye simu zetu na komputa mpakato (Protecting Mobile devises Data) ambapo vifaa hivi vimekua vikitumika katika utendaji wa shughuli za kiofisi na kufanya miamala ambapo taarifa hizo zimekua muhimu kulindwa dhidi yawahalifu mtandao.


  0 0

  Na. Sarah Reuben.

  Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese limehitimisha Wiki ya Kutambua Huduma ya Mchungaji Elitabu Kajiru wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese. 

  Akizungumza wakati wa Ibada Kuu Mch. Aston Mmamba amelipongeza kanisa la waadventista wasabato Manzese kufanikisha tukio hilo muhimu linaloleta upendo na umoja kanisani. "Ninawapongeza sana washiriki wa mtaa wa Manzese kwa kuthamini kazi ya utume inayofanywa na mchungaji wenu Elitabu Kajiru", alisema.

  Mch. Mmamba amewataka washiriki wa kanisa kuwasikiliza viongozi wao kwani wanajukumu kubwa la kuwalea kiroho. Alifafanua kuwa mchungaji mara nyingi hana muda maalum wa kutenda kazi kwa sababu muda wowote anapohitajika kutoa huduma kwa washiriki wake analazimika kufanya hivyo. Aidha, Mch. Mmamba aliwakumbusha kisa cha Musa alivyowaongoza wana wa Israeli kutoka utumwani Misri kwenda Kaanani ambapo kutokana na majaribu mengi, wanawaisraeli walisababisha Musa asifike Kanaan na kufia njiani.

  Mch. Mmamba pia alimpongeza Mch. Elitabu Kajiru kwa kukubali kuacha kazi serikalini na kuamua kujiunga na kazi hii ya uchungaji anayoitumikia hadi sasa. Alifafanua kuwa, "Sio kitu rahisi kuacha ajira yenye mshahara mzuri na kuja kwenye uchungaji, inahitaji nguvu ya uweza wa roho mtakatifu kuweza kufanya maamuzi ya namna hii, alisisitiza Mch. Mmamba.

  Naye Mch. Elitabu Kajiru na Mke wake waliwashukuru washiriki wa kanisa la Wasabato Manzese na Tandale kwa kutambua huduma yake na kuendelea kumtia moyo katika kazi hii ya utume.

  Kilele cha Wiki ya Kutambua Huduma ya Mchungaji Elitabu Kajiru wa Kanisa la Waadventista Manzese kilihitimishwa na Mch. Aston Mmamba aliyeambatana na mkewe kwa hafla fupi ya waumini wote kushiriki chakula cha mchana pamoja na kuwepo kwa kwaya ya Angaza, Mbiu, Vijana, Dorcas na vikundi mbalimbali vya uimbaji. Wiki hii ilianza tarehe 21 Oktoba, 2017 na kuhitimishwa tarehe 28 Oktoba, 2017 hapa jijini Dar es Salaam.
   Mchungaji Elitabu Kajiru(wa kwanza kushoto) akiongozana na mkewe wakikaribishwa rasmi kanisani kwa program maalum ya kutambua huduma ya mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.
   Mchungaji Aston Mmamba akitoa neno wakati wa ibada maalum ya kutambua huduma ya mchungaji wa kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.

  Kwaya ya Angaza ya Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese ikimtukuza Mungu kwa Wimbo wakati wa hafla ya kutambua huduma ya Mchungaji Kajiru

  0 0

  Na Hamza Temba - WMU

  SERIKALI imesema imedhamiria kufungua utalii wa Kanda ya Kusini ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini na hatimaye kuongeza idadi ya watalii na kipato kwa Serikali na jamii kwa ujumla.


  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga katika kijiji cha Kapozwa Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea Maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika baada ya Maporomoko ya Tugela yaiyopo nchini Afrika ya Kusini.


  Alisema kwa sasa vivutio vingi vinavyotumika kwa utalii nchini ni vile vya ukanda wa Kaskazini hususan vya wanyamapori ambavyo vimeanza kuelemewa kutokana na watalii wengi kutembelea ukanda huo zaidi kuliko Kanda ya Kusini ambayo pia ina vivutio mbalimbali vya asili.


  Alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo benki ya Dunia kupitia mradi wa REGROW imepanga kuboresha miundombinu ya vivutio vya utalii vya Kanda ya Kusini na kuvitangaza ili kuimarisha sekta hiyo muhimu ambayo inachangia asilimia 25 ya mapato yote ya kigeni na asilimia 17.5 ya pato la taifa.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya Greens Construction Limited, Hamimu Bakari wakati akishuka kwenye ngazi maalum zinazojengwa na mkandarasi huyo kwa ajili ya kuwawezesha watalii kushuka hadi kwenye kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo wakati wa ziara yake mkoani Rukwa. Maporomoko hayo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika baada ya TUGELA yaliyopo Afrika ya Kusini yana kina cha mita 235 na upana kati ya mita 3.6 hadi 18. 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akiteta jambo na Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Frank Schalwe wakati akishuka kwenye ngazi maalum zinazojengwa kwa ajili ya kuwawezesha watalii kushuka hadi kwenye kina cha Maporomoko ya Mto Kalambo wakati wa ziara yake mkoani Rukwa. Maporomoko hayo ambayo ni ya pili kwa kina kirefu barani Afrika baada ya TUGELA yaliyopo Afrika ya Kusini yana kina cha mita 235 na upana kati ya mita 3.6 hadi 18. 
   Muonekano wa ngazi hizo kuelekea kwenye Maporomoko ya Mto Kalambo.
  Sehemu ya juu ya Maporomoko ya Mto Kalambo.
  Taswira ya maporomoko ya mto Kalambo kutokea angani (Picha hii ni kwa hisani ya Mtandao)

older | 1 | .... | 1987 | 1988 | (Page 1989) | 1990 | 1991 | .... | 3284 | newer