Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1981 | 1982 | (Page 1983) | 1984 | 1985 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho, Mkuu wa Mkoa aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuliongezea vitendea kazi ili liweze kujidhatiti katika kukabiliana na majanga mbalimbali. 
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akimkabidhi zawadi ya Kalamu yenye ujumbe wa namba ya dharura 114 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kumaliza mazungumzo yao wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho, Mkuu wa Mkoa aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuliongezea vitendea kazi ili liweze kujidhatiti katika kukabiliana na majanga mbalimbali
   Kamishna  Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiagana  na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho, Mkuu wa Mkoa aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuliongezea vitendea kazi ili liweze kujidhatiti katika kukabiliana na majanga mbalimbali.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho, Mkuu wa Mkoa aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuliongezea vitendea kazi 

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Oktoba, 2017 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi watatu waliopangiwa kuziwakilisha nchi za Oman, Uholanzi na China hapa nchini.

  Waliowasilisha hati zao kwa Mhe. Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Mhe. Ali Abdullah Al Mahruqi – Balozi wa Oman hapa nchini, Mhe. Jeroen Verheul – Balozi wa Uholanzi hapa nchini na Mhe. Wang Ke – Balozi wa China hapa nchini.

  Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Serikali yake itafanya kazi nao kwa ukaribu ili kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo na Tanzania hususani katika uchumi.

  “Nimefurahishwa sana na ziara iliyofanywa na Mawaziri wa Oman hapa nchini, naomba ufikishe shukrani zangu kwa Mfalme wa Oman Mtukufu Sayyid Qaboos bin Said Al Said, naamini yote tuliyozungumza ikiwemo kubadilishana uzoefu katika mafuta na gesi, uwekezaji katika viwanda na ujenzi wa miundombinu tutayatekeleza kwa manufaa ya wananchi wa nchi zetu” amesema Mhe. Rais Magufuli alipozungumza na Balozi Ali Abdullah Al Mahruqi wa Oman.

  Mhe. Rais Magufuli amemuambia Balozi Jeroen Verheul wa Uholanzi kuwa Tanzania inayo gesi nyingi na itafurahi kupokea wawekezaji kutoka Uholanzi ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ina uzoefu na teknolojia kubwa katika sekta hiyo.

  Kwa upande wa Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke, Mhe. Rais Magufuli amesema uhusiano wa Tanzania na China ni wa kihistoria na kidugu, hivyo ametoa wito kwa Balozi huyo kuuendeleza na kuhakikisha fursa zenye manufaa kwa nchi zote zinatumiwa ipasavyo ikiwemo kukuza uwekezaji, biashara, utalii na ushirikiano katika usafiri wa anga. 

   Gerson Msigwa 
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, 
  IKULU 
  Dar es Salaam 
  25 Oktoba, 2017.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitazama vitabu alivyokabidhiwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uholanzi hapa nchini  Jeroen Verheul Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Oman hapa nchini Ali Al Mahruqi Ikulu jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua kambi ya uchunguzi wa macho, kisukari na shinikizo la damu.

  Kambi hiyo ya siku tatu imeandaliwa kwa pamoja kwa kushirikiana na Klabu ya Lions ya Dar es Salaam (Host), kwa kushirikiana na Hospitali ya Regency ya jijini hapa.

  Kambi hiyo itakuwa bure kwa wananchi wote watakaojitokeza kuanzia siku ya Ijumaa katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Lions Klabu iliyotolewa na Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Dk. Rajni Kanabar, ufunguzi rasmi wa kambi hiyo utafanyika siku ya Jumamosi na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

  Kambi hiyo itafanyikia kwenye kiwanda cha KNAUF Gypsum Wilaya ya Mkuranga, Kata ya Vikindu kijiji cha Kisemvule Mkoa wa Pwani kuanzia siku ya Ijumaa wiki hii.

  Alisema kambi hiyo ya bure ya siku tatu itaanza tarehe 27 hadi 29 mwezi huu 
  Dk. Rajni Kanabar, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo.

  Alisema Lions Klabu ya Lions imeamua kuandaa kambi hiyo ya bure baada ya kubaini kuwa kuna wananchi wengi wanasumbuliwa na maradhi hayo lakini wanakosa uwezo wa kwenda kupima.

  “Hii ni fursa adimu watu wajitokeze kwa wingi kuja kupima afya zao bure, huduma hiii itatolewa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia siku ya Ijumaa hadi Jumapili hivyo wananchi wote wachangamkie hii fursa,” alisema.

  Klabu ya Lions ya Dar es Salaam (Host), imekuwa ikiandaa kambi ya uchunguzi mbalimbali kila mwaka ambapo wananchi hupata fursa ya kwenda kupima bure.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investment Bw. Ally Nchahaga (katikati) akieleza jambo juu ya Tamasha la Magari Tanzania (Autofest) mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Bima ya Britam Insurance Bw. Oscar Ruhasha. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd, Bw. Aluwy Amar. Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu.  
   Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd,  Aluwy Amar ambao ni wadhamini wa Tamasha la Magari Tanzania akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu bidhaa mbalimbali watakazokuwa nazo katika tamasha hilo leo jijini Dar es salaam. Kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investment Bw. Ally Nchahaga. Kushoto ni Meneja Maendeleo kutoka Kampuni ya Jan’s Group Bw. Abdul Wahab. Tamasha hilo litafanyika kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay.
  Meneja Maendeleo kutoka Kampuni ya Jan’s Group, Abdul Wahab akieleza jambo juu ya Tamasha la Tamasha la Magari Tanzania (Autofest) mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd, Bw. Aluwy Amar. Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu.
  (Picha na Thobias Robert- Maelezo) 

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili DR Tumaini Msowoya, katika ukumbi wa Highland Hall Iringa mjini.

  Sambamba na kasesela wageni wengine wa heshima kwenye uzinduzi huo ni Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupita chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdalah, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha Baby Baraka Chuma na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali.

  Akizungumza na blog hii DR Msowoya alisema tayari albamu hiyo yenye nyimbo nane imeshakamilika.“Naenda Iringa kurudisha shukrani zangu kwao, nataka wajue nipo huku sio tu kwa sababu ya kazi bali huduma ya kuimba niliyoanza ”

  Alizitaja nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo kuwa ni Hakuna Matata, Mwamba, Amenitengeneza, Furaha, Mungu Mkuu, Wanawake Jeshi Kubwa, Samehe na Mungu wa Rehema.“Kazi hii nimeifanya chini ya usimamizi wa JB Production ikisimamiwa na Producer Smart Bilionea Baraka. Ndiye meneja anayesimamia kazi zangu kwa sasa,’ alisema Msowoya.

  Lakini Meneja wa Dr Msowoya Smart Bilionea Producer Baraka alisema tayari waimbaji na kwaya mbalimbali kutoka Iringa na Dar es Salaam watamsindikiza kwenye uzinduzihuo.Alizitaja kwaya zizothibitisha kumsindikiza kuwa ni Wakorinto wa Pili kutoka Mufindi, Muhimidini na kwaya ya Vijana kutoka Iringa mjini.

  Baadhi ya waimbaji ni Christopher Mwahangila anayetamba na wimbo wa ‘Mungu ni Mungu tu’, Mchekeshaji na mwanamuziki mpya wa Injili Tumaini Martine maarufu kwa jina la Matumaini wa Kiwewe, Christine Mbilinyi, Moses Simkoko, Ritha Komba na Witness Mbise kutoka Dar es Salaam.

  Wengine ni Rebecca Baraka, Jesca Msigwa, Ester Mgunda, Rebecca Mwalingo, Dennis Lukosi, Wadi Mbelwa, Peter Mgaya, Rehema Chawe, Twaibu Mgogo, Emma Sanga na Victoria Mwenda kutoka Iringa.“Waimbaji watakaomsindikiza ni wengi nab ado tunaendelea kuwasajili wengine. Bado tupo kwenye mazungumzo na Bahati Bukiku ambaye anaangalia ratiba yake, ikiwa sawa tutakuwa pamoja,”alisema.

  Aliwatanzania kupokea kazi ya Msowoya kutokana na ubora wake wa nyimbo zilizobeba ujumbe unaoweza kuisaidia jamii.

  Historia

  Hakuna Matata ni albamu ya pili ya Msowoya baada ya ile ya kwanza ya Natembea kwa Imani kutofanya vizuri sokoni.“Bahati mbaya niliitengeneza kutokana na kiwango kidogo hivyo iliishia kabatini, namshukuru Mungu kwa sababu kazi hii ni nzuri na wakazi wa Iringa wameipokea. Naamini itapokelewa kote,”alisema.  0 0

  JENGO la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) linalotarajiwa kukamilika Desemba 2018, litafungwa mfumo wa huduma ya viza kwa njia ya mtandao (e-visa), ambao utarahisha na kuharakisha upatikanaji wake.

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji cha JNIA, Bw. Kaanankira Mbise amemwambia jana Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea eneo la uombeaji viza kwa abiria wa kimataifa wanaowasili, kuwa wanatarajia kutumia huduma hiyo ambayo ni rahisi na haraka.

  “Tayari mkakati umeanza wa kuanzisha huduma hii ya e-visa hivyo tukifanikiwa utafungwa katika jengo hili jipya, ambapo itasaidia kwa abiria kuipata huduma hiyo kwa haraka kwani itatumia mtandao,” amesema Bw. Mbise.Hata hivyo, Bw. Mbise amesema kwa sasa wameboresha huduma hiyo kwa wasafiri wanaowasili katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII) , ambapo tayari wamepatiwa mashine nne za kisasa zinazosaidia kupunguza msongamano wa abiria wenye kuhitaji huduma hiyo, hususan kipindi cha mchana chenye ujio wa ndege nyingi za nje ya nchi.

  “Hizi mashine zimeharakisha upatikanaji wa huduma kwani tumeweza kuhudumia abiria wengi kwa wakati mmoja, na msongamano umepungua kiasi tofauti na awali mashine zilikuwa chache.” amesema Mbise.Naye Mhe. Mhandisi Nditiye amesema baada ya ziara yake amegundua mashine za viza ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa mrefu, na tayari ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwasilisha kwa maandishi mapendekezo yao ya namna ya kuharakisha huduma hiyo, ili serikali iyafanyie kazi kwa kusaidia kuondoa kero hiyo.

  “Nimegundua kuna baadhi ya mashine za viza zimeongezwa lakini pia zilizopo zimechoka kwani ni za muda mrefu na zinahudumia abiria mmoja kwa muda mrefu na hii inaharibu sifa ya kiwanja chetu kwa wageni wanaokuja hapa nchini,” amesema Mhandisi Nditiye.Hata hivyo, amesema wanampango wa kuongeza madirisha ya benki yanayolipia viza hizo ili kuharakisha huduma hiyo, ambapo sasa ni machache kulinganisha na idadi kubwa ya abiria wanaowasili kwa ndege kubwa. Ndege hizo ni Emirates, Etihad, Oman Air, Qatar, South Africa Air na Ethiopia, ambazo zimekuwa zikipishana kwa muda mfupi.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Richard Mayongela amesema tayari wanampango wa kuongeza upana wa eneo hilo la wasafiri wanaowasili wa kimataifa, ambapo sasa kumekuwa na msongamano kutokana na ufinyu wake.“Hili jengo linazaidi ya miaka 30 na ukiangalia abiria waliokuwa wamekadiriwa wakati ule lilikuwa likikidhi mahitaji, lakini sasa abiria wameongezeka na eneo limekuwa dogo, hivyo tayari tumeanza kwa kuondoa baadhi ya ofisi ili kuongeza upana wake, ninaimani litapunguza msongamano uliopo sasa,” amesema Bw. Mayongela. 

  Lakini pia Bw. Mayongela amesema sasa wapo katika mazungumzo na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), ili kuangalia namna bora ya kuzipangia muda ndege zinazopishana muda mdogo kwa wakati wa mchana ili ziachiane muda mrefu, ambapo kutasaidia kupunguza msongamano.Awali eneo hilo linakumbwa na changamoto kubwa ya msongamano wa abiria wanaohitaji huduma ya viza baada ya uchache mashine zinazosimamiwa na Idara ya Uhamiaji zilizokuwepo na kufanya abiria wanaohitaji huduma hiyo kutumia muda mrefu kuipata. 
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akiwaeleza jambo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka katika eneo la kuchukua mizigo baada ya kuwasili.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyenyoosha mkono), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa nne kulia) wakiwa kwenye eneo la abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi.
  Bw. Kaanankira Mbise, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akieleza namna abiria anavyopata huduma ya viza mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), huku Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) akisikiliza kwa makini.


  0 0

  Dear All
  There is a new wave of ransomware attack, #BadRabbit, which launched on October 24th that has hit the market worldwide.The attacks originated in Ukraine and Russia, and have spread and affected critical infrastructures.

  Bitdefender GravityZone Elite Suite detected this at zero hour, as early as July 2017, three months before this ransomware hit prime-time, October 24th.  The Elite suite features tunable machine learning models and this particular model that detected BadRabbit, was created in April 2017. This goes to show the prediction power of Bitdefender's well-crafted machine learning models.


  We all know that ransomware or malware can strike companies well before it becomes widespread.  Ensure your organization is protected at zero hour, Bitdefender Gravityzone Elite Suite is the solution for your organization!
  Interested in learning more about BadRabbit?  Follow us on twitter @Bitdefenderlabs and read the blog for the most up to date analysis https://labs.bitdefender.com/2017/10/bad-rabbit-ransomware-strikes-ukraine-likely-related-to-goldeneye/


  Thank you for trusting Bitdefender,


  INTERCOM SYSTEM (T) LTD
  Bitdefender Cyber Security Country Partner
  Morogoro Road, Old Kisutu Bus Stand
  P.O.Box 8898, Dar Es Salaam, Tanzania
  Telephone +255 22 2121140
  Mobile +255 673 221 933 │+255 689 540 600 │+255 715059801  Description: Description: Description: C:\Users\USER\Downloads\logo (1).png


  0 0

  Eneo la kituo cha mabasi cha Mbagala Rangi tatu likiwa limezingirwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na mikoa ya Pwani
  Eneo la kituo cha mabasi cha Mbagala Rangi tatu likiwa limezingirwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na mikoa ya Pwani. Picha na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii

  0 0

  Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC), imezinduliwa rasmi leo Jumatano Oktoba 25, 2017 kwa droo maalumu kwa timu zitakazofungua dimba kwa mzunguko wa awali.
  Droo hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko Karume, Ilala jijini Dar es Salaam ambako Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi amesema: “Michuano ya msimu huu itaanzia hatua ya awali kabla ya kuja kwa raundi ya kwanza.”
  Amesema kwa ujumla tu, michuano hiyo ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba SC ya Dar es Salaam, itashirikisha timu 91 msimu huu kwa mchanganuo wa timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL); 24 za Ligi Daraja la Pili (SDL) na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa (RCL).
  Kwa kuanzia hatua ya awali, kundi la timu 27 la RCL timu sita zitakazocheza mechi tatu baada ya wachezaji watatu wa zamani wa timu ya taifa Abeid Mziba ‘Tekelo’, Boniface Pawasa na Salum Sued ‘Kusi’ kuchagua vitufe sita ili kupata timu hizo.
  Timu zilizopatikana katika droo hiyo hatua ya awali Buselesele ya Geita itayocheza na Green FC ya Songwe; Kisarawe United ya Pwani itacheza na Silabu ya Mtwara ilihali Usamala ya Simiyu itacheza na Sahale All Stars ya Tanga kati ya Oktoba 31; Novemba mosi au mbili.
  Raundi ya Kwanza ya ASFC itaanza Novemba 7, 8 au 9 ambako timu zilizochaguliwa kwenye droo hiyo ni kama ifuatavyo:
  Mashujaa ya Kigoma itacheza na Mshindi kati ya Buselesele ya Geita na Green FC ya Songwe; wakati mechi nyingine zitakuwa Msange ya Tabora itacheza na Milambo pia ya Tabora ilihali Bulyanhulu ya Shinyanga itacheza na Area C ya Dodoma.
  Kwa mujibu wa droo, Mji Mkuu FC ya Dodoma imeangukia kwa Nyundo ya Kigoma wakati Baruti FC ya Mara itacheza na Ambassodor ya Kahama, Shinyanga huku Eleven Stars ya Kagera ikipangwa kucheza na Ndovu ya Mwanza.
  Changanyikeni ya Dar es Salaam itacheza na Reha FC pia ya Dar es Salaam wakati Mshindi kati ya Kisarawe United na Silabu ya Mtwara atacheza na Kariakoo ya Lindi huku Cosmopolitan ikicheza na Ajabalo wakati Makumba FC itapambana na Green Warriors ya Kinondoni wakati Namungo FC ya Lindi itachuana na Villa Squad ya Dar es Salaam huku Dar City ikicheza na Majimaji Rangers ua Nachingwea.
  Michezo mingine ya hatua ya kwanza itakutanisha timu za Shupavu FC ya Morogoro na Sabasaba pia ya mjini humo wakati Motochini FC ya Katavi dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya wakati The Mighty Elephant ya itacheza na Makanyagio ya Rukwa.
  Timu ya Burkina FC ya Morogoro itacheza na Mbinga United ya Ruvuma wakati Makambako Heroes ya Njombe  itacheza na Mkamba Rangers ya Morogoro wakati Real Moja Moja itapambana na African Wonderers – zote za Iringa. Boma FC ya Mbeya itacheza na African Sports ya Tanga.
  Mechi nyingine za hatua hiyo itakuwa ni kati ya Pepsi ya Arusha ambayo itacheza na Kilimanjaro Heroes ya Kilimanjaro; huku Stand Misuna ya Singida itacheza na Madini FC ya Arusha ilihali AFC ya Arusha itacheza na Nyanza ya Manyara wakati New Generation itacheza na Mshindi kati ya Usamala FC na Sahale ya Tanga. Bodaboda FC itacheza na Kitayose ya Kilimanjaro.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investment Bw. Ally Nchahaga (katikati) akieleza jambo juu ya Tamasha la Magari Tanzania (Autofest) mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mkuu Mauzo kutoka Kampuni ya HYUNDAI Bw. Anthony Nyeupe, wa pili ni Meneja Masoko kutoka Kampuni ya Bima ya Britam Insurance Bw. Oscar Ruhasha. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd, Bw. Aluwy Amar. Tamasha hilo litafanyika kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu katika viwanja vya At The Green Kenyatta Drive, Osterbay, jijini Dar es salaam. 

   Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd, Bw. Aluwy Amar ambao ni wa wadhamini wa Tamasha la Magari Tanzania akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu bidhaa mbalimbali watakazokuwa nazo katika tamasha hilo leo jijini Dar es salaam. Kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investment Bw. Ally Nchahaga. Kushoto ni Meneja Maendeleo kutoka Kampuni ya Jan’s Group Bw. Abdul Wahab. Tamasha hilo litafanyika kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay.  
  Meneja Maendeleo kutoka Kampuni ya Jan’s Group Bw. Abdul Wahab akieleza jambo juu ya Tamasha la Tamasha la Magari Tanzania (Autofest) mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya Lake Oil Ltd, Bw. Aluwy Amar. Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya The Green Kenyatta Drive, Osterbay jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 27 hadi 29 mwaka huu. 
  (Picha na Thobias Robert- Maelezo)

  0 0

   Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (kulia) alipofanya ziara TCRA kuangalia namna taasisi hiyo inavyosimamia maudhui ya vyombo vya habari nchini leo Jijini Dar es Salaam.

  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Posta TCRA Bibi. Cecilia Mkoba (kulia) akimuelezea Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) namna mawasiliano zamani yalivyokuwa yakifikishwa kutoka eneo moja kwenda eneo lingine alipotembelea makumbusho ya mawasiliano leo wakati wa ziara yake TCRA Jijini Dar es Salaam. 
   Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Dkt. James Kilaba (katikati) akizungumza alipomtembeza Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kuangalia gari lililofungwa mtambo wa kusimamia masafa ya redio nchini wakati wa ziara yake TCRA leo Jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akikagua ofisi za Idara ya uhariri na uchapishaji alipotembelea ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kukagua na kuona shughuli zinazofanywa na Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt. Suleiman Sewangi 
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akipokea kamusi kutika kwa mtumishi wa BAKITA Bibi. Wema Msigwa alipofanya ziara katika ofisi za BAKITA leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt. Suleman Sewangi

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Dar es Salaam
  Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe  amezindua msimu wa 16 wa Mbio za Kilimanjaro  Marathon zinazodhaminiwa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro.

  Dk Mwakyembe amesema Kilimanjaro Marathon imejizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa maandalizi yake ni mazuri na  kuweza kuongeza idadi ya wakimbiaji mwaka hadi mwaka hali iliyofanya upatikanaji wa wakimbiaji wa timu ya taifa kuwa raisi kupitia mashindano hayo ambayo kwa sasa yanatambulika na chama cha riadha cha Dunia.

  “Tunataka kuwaibua kina Felix Simbu wengine kupitia mbio kubwa kama Kilimanjaro Marathon. Nimefahamishwa kuwa Simbu pia alitokana na mbio hizi kwani aliwahi kushiriki kilometa 21 miaka ya nyuma sisi kama serikali tutafanya kila linalowezekana kuyafikia malengo haya kwa kuhakikisha kuwa mazingira yatakuwa  mazuri kwa wakimbiaji wa nadani na wa nje” amesema Mwakyembe.
  Aidha Waziri Mwakyembe alitumia muda huo kuwashukuru wadhamini wengine ambao ni Tigo-21km, Grand Malt 5km na wale wa meza za maji ambao ni pamoja na First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement na KNAUF Gypsum.
  kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis amesema wanajivunia kudhamini mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambazo zinakuwa kwa kasi kubwa mwaka hadi mwaka  na hii inawapa moyo na ari ya kuendelea kuwa wadhamini wa mashindano hayo amabyo uleta mataifa zaidi ya 40 pamoja.
  Amesema udhamini huu katika mbio za kilometa 42 na 5 kupitia Grand Malt, pamoja na mambo mengine unalenga kuibua vipaji zaidi katika riadha na kuwataka washiriki kujiandaa vizuri.
  Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ametoa rai kwa washiriki kuhakikisha wanajiandikisha mapema li kuepuka usumbufu dakika za mwisho na kutoa mfano wa mwaka huu ambapo namba za ushiriki zilikwisha kutokana na watu wengi zaidi kujitokeza mwishoni.  0 0

   
  Ofisa Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akizungumza kuwakaribisha washiriki wa Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha (hawapo pichani) kwenye hafla maalum ya 'cocktail' iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Biashara kati ya Mabenki, Bi. Heidi Toribio akishuhudia.Ofisa Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akinyanyua glasi juu kuashiria uzinduzi wa hafla hiyo pamoja na washiriki wa Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha (hawapo pichani) katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam.
   
  Washiriki wa Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha wakibadilishana mawazo kwenye hafla maalum ya 'cocktail' iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jambo na Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na Wakati wa NMB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam. Katikati ni mmiliki wa mtandao maarufu wa Josephatlukaza.com, Josephat Lukaza akifuatilia mazungumzo hayo. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
  0 0


  Mgeni Rasmi, Waziri wa Madini Angellah Kairuki akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga na waendesha Bodaboda  waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
  Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
    Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azan akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo na waendesha pikipiki waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo na waendesha pikipiki waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
   Mwakilishi wa wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga Bw.Namoto Yusuf Namoto akisoma risala ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
   Mwakilishi wa waendesha Bodaboda Wilaya ya Ilala Bw. Athanas Kitime akitoa salamu zao kwa Mgeni Rasmi, Waziri wa Madini Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga na waendesha pikipiki wakimpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
   Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga Bw. Steven Lusinde (kulia) na Mwakilishi wa waendesha pikipiki maarufu kama waendesha bodaboda Bw. Athanas Kitime wakimkabidhi risala Mgeni Rasmi, Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo na waendesha pikipiki wakimpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
   Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga na waendesha pikipiki maarufu kama waendesha bodaboda waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.
   Msanii Sholo Mwamba akitoa burudani kwa  wafanyabiashara ndogondogo eneo la Kariakoo maarufu wamachinga na waendesha pikipiki waliokusanyika katika viwanja vya Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake.

  0 0
 • 10/25/17--13:30: Article 3


 • 0 0

   Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi akizungumza wakati wa kufunga warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa uliofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.
   Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja akizungumza wakati wa kufunga warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa uliofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri akizungumza wakati wa kufunga  warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa uliofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.
   Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Richard Kasesela akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.Fabian Daqqaro wakati wa kufunga warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa uliofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma.

  Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya  walioshiriki katika warsha ya kitaifa ya maboresho ya huduma za umma na utoaji Madaraka  kwa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa uliofanyika  katika ukumbi wa Hazina leo Mkoani Dodoma wakifuatilia mada mbaimbali.
  Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO, DODOMA.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kangeme kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa North Ugala na vijiji jirani vya Kangeme, Utenge na Mtakuja katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kangeme wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana. Alisema Wizara yake itakutana na Wizara ya TAMISEMI na Ardhi kwa ajili kutoa uamuzi wa kumaliza mgogoro huo

  NA HAMZA TEMBA- WMU- URAMBO, TABORA

  Naibu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema Wizara yake itashirikiana na Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kutoa uamuzi wa pamoja wa kumaliza mgogoro wa mpaka baina ya Hifadhi ya Msitu wa North Ugala na vijiji jirani vya Kangeme, Utenge na Mtakuja wilayani Urambo .

  Naibu Waziri Hasunga amesema hayo mkoani Tabora jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Akiwa mkoani humo alitembelea eneo lenye mgogoro, akafanya mkutano wa hadhara na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali kwa ajili ya kutafuta majibu ya kutatua mgogoro huo.


  Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kangeme, Mkazi wa Kijiji hicho, Ramadhan Rashid alisema wananchi wa vijiji hivyo wanailalamika Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu kwa kusogeza mpaka wa hifadhi hiyo hadi ndani ya ardhi ya vijiji wakati wa uwekaji wa vigingi vipya vya mpaka. Alisema eneo hilo ni la vijiji hivyo tangu mwaka 1988.


  Naye, Mkuu wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Peter Maiga alisema hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1956 ikiwa na hekta 165,282 huku mipaka yake halisi ikiwa haijabadilishwa. Alisema zoezi la uwekaji wa vigingi vipya vya mpaka lilizingatia mipaka halisi kwa kutumia mfumo wa GPS.

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Urambo, Magreth Sitta akizungumza kwa niaba ya wananchi wa vijiji hivyo kwenye mkutano huo, alisema idadi ya wananchi inaongezeka huku maeneo yakiwa hayaongezeki hivyo akaiomba Serikali ione uwezekano wa kuwaongezea wananchi maeneo ya kulima na kuendeshea maisha yao.


  Akijibu malalamiko na maombi ya wananchi hao wa Urambo, Naibu Waziri Hasunga alisema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutatua kero za wananchi sambamba na kuwaletea maendeleo.


  “Baada ya kukagua eneo hili na kusikiliza pande zote, tunaenda kukaa pamoja na Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Ardhi tuangalie ramani zote zilizopo, Matangazo ya Serikali (GN) na taarifa mbalimbali ili tujiridhishe ni ipi mipaka halali tufikie ufumbuzi wa mwisho, migogoro ya namna hii haiwezi kuisha bila kushirikisha wizara hizi.


  “Nawaagiza watendaji wangu kwenye taasisi mshirikiane na wananchi muwaelimishe na mzuie wasiendelee na uharibifu hadi hapo tutakapopata suluhu ya mgogoro huu”. alisema Naibu Waziri Hasunga.


  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo aliwataka wananchi wa vijiji hivyo kujiepusha na vitendo vya kuingiza mifugo kwenye maeneo ya hifadhi. “Mkiingiza mifugo tukaikuta tutaitaifisha kwa mujibu wa sheria” alisema Naibu Waziri Hasunga.  


  Aidha aliwataka wananchi hao kujikita kwenye shughuli za ufugaji nyuki kibiashara kwa kutumia mizinga ya kisasa ambayo huongeza uzalishaji. “Asali ina soko zuri duniani kwa sasa, bei yake ni nzuri, kila mtu afuge tuchangie uchumi wa taifa letu” alisema Hasunga.


  Naibu Waziri Hasunga ataendelea na ziara yake ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi katika mikoa wa Katavi, Rukwa na Songwe.
   Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (kulia) akijibu kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kangeme wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa North Ugala na vijiji jirani vya Kangeme, Utenge na Mtakuja Alisema Wizara yake itakutana na Wizara ya TAMISEMI na Ardhi kwa ajili kutoa uamuzi wa kumaliza mgogoro huo.
  Naibu Waziri wa Maliasili, Japhet Hasunga (katikati) akisikiliza maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kigwa (kushoto) kuhusu mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Msitu wa North Ugala na vijiji jirani vya Kangeme, Utenge na Mtakuja baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kangeme wilaya ya Urambo mkoani Tabora jana. Alisema Wizara yake itakutana na Wizara ya TAMISEMI na Ardhi kwa ajili kutoa uamuzi wa kumaliza mgogoro huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akizungumza mbele ya Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara na makampuni mbalimbali wakati wa kufungua Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda lililofanyika jana Oktoba 25,2017 mjini Beijing,nchini China.Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,liliandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies.Picha Ahmad Michuzi-China.

  Balozi Kairuki ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies kwa kuthubutu na kuonesha juhudi kubwa za kutafuta na kuwahamasisha washirika mbalimbali katika suala zima la uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.

  Balozi Kairuki amesema kuwa,yeye yuko tayari kushiriki kwa pamoja kusaidia kuendelea kuwahamasisha Wawekezaji wa nchini China,kuja kuwekeza nchini Tanzania,ili kuhakkisha dhana ya Tanzania ya Viwanda inatimia na hatimaye nchi ya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

  "Kwa kufanya hivyo sote kwa pamoja tutakuwa tunetekeleza kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda",alisema Balozi Kairuki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akizungumza mbele ya Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara na makampuni mbalimbali waliojitokeza kushiriki Kongamano la uwekezaji wa Viwanda lililofanyika jana Oktoba 25,2017 mjini Beijing,nchini China.Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,liliandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akipongezwa mara baada ya kutoa hotuba yake .
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akiwalekeza jambo baadhi ya Wadau wenye nia ya Uwekezaji nchini Tanzania,mara baada ya Kongamano la uwekezaji wa Viwanda kumalizika.Kongamano hilo lilifanyika Oktoba 25,2017 katika moja ya ukumbi wa hotel ya King Wing,mjini Beijing nchini China,ambapo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini humo,Mh Mbelwa Kairuki.
  Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Samataba akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yameulizwa na baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo la Uhamasishaji wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya King Wing mjini Beijing nchini China.Mh Semataba ambaye aliongozana na baddhi ya viongozi waandamizi wa Serikali mkoa wa Pwani,aliwahikikishia mazingira mazuri Washiriki hao wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalibali ikiwemo Viwanda,madini na kilimo na kuwa.
  Kongamano la Uhamasishaji uwekezaji wa Viwanda kwa nchini Tanzania likiendelea mjini Beijing,nchini China.
  Sehemu ya meza kuu na baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akiwasili ukumbini kufungua kongamano la Uwekezaji wa Viwanda akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa (wa pilia kulia) ambao ndio waandaaji wa kongamano hilo ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo la Uwekezaji wa Viwanda,wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakjiri ukumbini humo,pichani kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Mohamed Kiluwa ambao ndio wameandaa kongamano hilo.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo la Uwekezaji wa Viwanda,wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Mohamed Kiluwa akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini,Bi.Tatu Selemani.
  Picha ya pamoja kutoka meza kuu na baadhi ya Wadau wakuu wa Kongamano hilo la Uwekezaji wa Viwanda.

  0 0

older | 1 | .... | 1981 | 1982 | (Page 1983) | 1984 | 1985 | .... | 3284 | newer