Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1982 | 1983 | (Page 1984) | 1985 | 1986 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Mganula Mbogoni akiweka utepe ikiwa ni ishara ya kulifunga moja ya duka ambalo mmiliki wake hakukidhi masharti ya kisheria ya kufanya biashara ikiwa ni pamoja na kutokuwa na Mkataba hai wa Pango na Leseni ya Biashara.
  Mmoja wa wafanyabiashara akilipa kodi anazodaiwa na Manispaa ya Dodoma wakati wa zoezi la uhakiki linaloendeshwa na Wakuu wa Idara wa Manispaa ya Dodoma.
  Kiongozi wa kikosi kazi cha Wakuu wa Idara Dickson Kimaro (wa pili kushoto ) akimuhoji mmoja wa Wafanyabiashara wa Eneo la 'Mambo Poa' wakati wa zoezi la uhakiki wa nyaraka mbalimbali za kuendesha biashara.
  Mmoja wa wafayabiashara ya chakula maarufu Mama Lishe (kulia) akilipa kodi kwa Maafisa wa Manispaa ya Dodoma wakati wa zoezi la kuhakiki nyaraka za kisheria za kuendesha biashara ikiwemo mikataba hai ya upangishwaji.

  NA RAMADHAI JUMA

  MENEJIMENTI ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imeanza zoezi la uhakiki wa nyaraka mbalimbali kwa wafanyabiashara waliopanga vibanda vya biashara vinavyomilikiwa na Manispaa hiyo, ambapo wakuu wa Idara wanatekeleza zoezi hilo kwa kupita katika vibanda vyote vilivyopangishwa kwa wafanyabiashara.

  Nyaraka zinazohakikiwa ni mikataba ya upangishaji wa chumba cha biashara na leseni za biashara husika, ambapo maeneo mengine kama viwanda vya matofali, maeneo ya kuoshea magari, na maeneo ya kuchomelea vyuma pia yatahusishwa katika uhakiki huo ili kujiridhisha endapo biashara hizo zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria na taratibu kama inavyopaswa.

  Zoezi hilo la siku tatu limeanza vizuri ambapo baadhi ya Wafanyabiashara ambao mikataba yao ya upangishaji ilimalizika wameonesha ushirikiano kwa kulipia huku wengine wakifungiwa maduka kwa kushindwa kufanya hivo.

  0 0

  Siku za hivi karibuni, Serikali imetilia mkazo uwezeshaji wa watanzania kumiliki uchumi wao kwa kuyataka makampuni na mashirika kujiorodhesha katika Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE). Makampuni ya simu na mabenki ni miongoni mwa makampuni yaliyoshika kasi katika kujiorodhesha katika Soko la Hisa.Sambamba na hilo, elimu ya uwekezaji katika eneo hili imekuwa na msukumo mdogo tangu ulipoanza kwenye miaka ya 90. Hii inasemekana kuwa pengine ni uchanga na ugeni wa soko letu lakini pia elimu kutowafikia watanzania wengi kwa wingi.Elimu ya masuala ya hisa inaonyesha kujikita zaidi katika maeneo ya mijini hususani jijini Dar Es Salaam ambapo ni sehemu ndogo tu ya idadi ya wananchi wa Tanzania na hivyo kupelekea umuhimu wa Serikali,wataalamu na wadau wa masoko ya mitaji na dhamana kutoa elimu zaidi katika maeneo yote ya nchi kuanzia mijini, vijijini na hata mashuleni ili kujenga uelewa kwa wananchi ili wawe sehemu ya umiliki wa makampuni na mashirika yanayoingia katika soko la hisa.
  Kazi hii pia imekuwa ikifanywa na Maendeleo Bank ambayo ndiyo benki inayouza hisa zake sasa kupitia matawi yake, matawi ya CRDB nchi nzima, Uchumi Commercial Bank na kupitia njia ya simu.Maendeleo Bank imekuwa ikitoa elimu ya uwekezaji kupitia semina na mikutano mbalimbali na wananchi wa kada mbalimbali na wafanyabiashara ili kuwapatia uelewa wa kutosha kabla ya kuamua kuwekeza.Baada ya kufanya semina jijini Mwanza wiki iliyopita. Mwisho wa Juma lililopita timu ya viongozi wa Maendeleo Bank walitoa elimu hii Shinyanga Mjini na katika wilaya ya Kahama kwa wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha hawabaki nyuma katika elimu hii muhimu hasa wakati ambapo benki hiyo inauza hisa zake.Maendeleo Bank ilianza kuuza hisa zake Septemba 18 na zitakwenda hadi Novemba 3, 2017. Hisa moja ni shilingi 600 tu na kiwango cha chini ni hisa 100 ambazo ni shilingi 60,000

  0 0

  Mahakama nchini imeendelea kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli zake mbalimbali, ambapo kwa siku mbili mfululizo mashauri tofauti yalisikilizwa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video (Video Conference). Katika shauri la kwanza, Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara ilisikikila kesi namba 80 ya mwaka 2015 kwa kutumia teknolojia hii, ambapo shahidi muhimu katika shauri hili aliunganishwa kutoka nchini Kanada. Na katika shauri jingine, Mahakama Kuu ilisikiliza kesi ya madai (Civil Case) namba 225 ya mwaka 2013 ambapo shahidi wa kesi hii alikua nchini Uswisi (Switzerland), na mahakama zilihamia kwa muda kwenye kumbi za mikutano kwa njia ya video za Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA).
  Mawakili wa Pande Zote Kabla ya Kesi Kuanza.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti majaji wanaosikiliza kesi hizi wamesema teknolojia hii itawezesha kusikilizwa kwa mashahidi na hatimae kumalizwa kwa mashauri hayo na mengine ambayo ni ya muda mrefu.
  Mawakili Kutoka NL and Partners Advocates (Mlalamikaji) Kabla ya Kesi Kuanza.

  Teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video, ni teknolojia inayowezesha washiriki kutoka vituo viwili au zaidi kuwasiliana kwa kuonana (video) na kusikilizana. Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) imekua ikitoa huduma hizi tangu mwaka 2000 ambapo teknolojia hii imekua ikitumika kwa shughuli mbalimbali kama mikutano ya kawaida, kusikilizwa kwa kesi mbalimbali, usaili, uwasilisho wa miradi na maandiko, midahalo, mafunzo, kuonana na madakrari bingwa, n.k.

  0 0


  0 0

  Mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam imesababisha adhaa kwa wakazi wa jiji hilo ambapo kwa maeneo ya Mbezi kuelekea Bwaloni/Kwa Msuguli au Malamba Mawili Shule nguzo ya umeme ya shirika la umeme la TANESCO imedondoka eneo la Malamba Mawili msikitini na kusababisha kufunga njia kwa wasafiri wa magari ambapo hakuna magari yanayovuka kwenda upande wa pili. 

  Tanesco tunawaomba msaada tumekwama inasemekana imedondoka saa 9 Usiku kuamkia leo 26.10.2017.


  0 0

   Mpiganaji Danford Mpumilwa ambaye ni Afisa Habari wa Taasisi hiyo akiendesha shughuli za maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na  UNMICT hapo katika makao makuu mapya ya taasisi hiyo sehemu ya mlima Lakilaki, Kisongo, nje kidogo ya Arusha    hayo mbele ya wageni pamoja na maafisa wa UNMICT.
  Mamia ya wanafunzi wa Arusha na wageni mbalimbali wiki hii walihudhuria maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na  UNMICT hapo katika makao makuu mapya ya taasisi hiyo sehemu ya mlima Lakilaki, Kisongo, nje kidogo ya Arusha

  0 0

  Mwigzaji  Elizabeth Michael maarufu kama Lulu akitoka katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

  Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, Novemba 13 mwaka huu inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili msanii maarufu wa filamu nchini,  Elizabeth Michael 'Lulu'.

  Hatua hiyo imekuja baada ya  Wazee wa Baraza kutoa ushauri wao kwa mahakamani hapo na kudai kwamba Lulu ameua bila kukusudia.

  Katika keso hiyo, Lulu anakabiliwa na tuhuma za kumuua bila kukusudia, msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba, Aprili 7 mwaka 2012.

  Mapema kabla ya wazee hao wa Baraza kutoa maoni yao Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo alisoma maelezo ya mashahidi wa pande zote mbili kisha kusikiliza maoni hayo.

  Kabla ya kutolewa maoni hayo, Jaji Rumanyika alisema kimsingi ushahidi wa upande wa mashtaka umejikita kwenye ushahidi wa kimazingira kwa sababu mshtakiwa Lulu ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuwa na Kanumba.

  Jaji rumanyika alisema kuwa ushahidi wa kimazingira sio wa moja kwa moja lakini kama ungekuwa mnyololo basi vipande vyake vikiunganishwa havikatiki.

  Aliwaambia wazee hao wa baraza katika kutoa maoni yao waone kuwa mshtakiwa ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu na vile vile ametoa maelezo ya kina yaliyotosheleza juu ya tukio hilo

  Pia alisema, kama wataona mshtakiwa hausiki na mauaji yale wasisite kuieleza mahakama,

  "Kama mtaona kifo cha Kanumba kilitokana na ugomvi  aliwaambia katika mashauri ya mauaji siyo lazima upande qa mashtaka kuthibitisha nia ovu bali kutokea kwa tikio ithibitike kuwa tendo limetendeka.
  "Katika maoni mkumbuke msingi wa sheria wa mashtaka ya mauaji kuthibitishwa kwa nia ya mauaji siyo lazima mara nyingi mauaji ya bila kukusudia yanasababishwa na ugomvi", amesema Jaji.
  " Kama mtaona kifo cha Kanumba kilitokana na ugomvi mtoe maoni yenu na kama mshtakiwa hausiki na tukio hili mtoe pia maoni yenu.

  Katika maoni yake, Mzee wa Baraza Omary Panzi amesema Lulu kutokana na ushahidi uliotolewa imeonyesha wazi kuwa Lulu ameua bila kukusudia.
  Amedai ametoa maoni yake kutokana na ushahidi wa Seth Bosco, mdogo wake Kanumba ambaye alidai ugomvi uliotokea baina ya Lulu na marehemu kaka yake ulitokana na Kanumba.

  Mzee wa baraza, Sarah katika maoni yake amedai Kanumba alikufa kutokana na ugomvi ambapo ushahidi pia umetueleza kulikuwa na Giza hivyo Lulu hakuuwa makusudi bali aliuwa bila kukusudia,

  Mzee wa baraza wa Tatu, Rajabu Mlawa alidai Kanumba alikufa kutokana na ugomvi baina yao kwa kuwa ndani kulikuwa na ugomvi
  "Elizabeth hakuua kwa makusudi, aliua bila kukusudi, kutokana na sababu  ulizosoma sina ubishi,juu ya ushahidi uliotolewa na panda zote mbili, Lulu ameua bila kukusudi ukizingatia Kanumba alikuwa na mwili mkubwa, mnene, mzito mwenye nguvu za kutosha, Lulu hana nguvu katika hekaheka za kujinusuru maana tumesikia kuwa kulikuwa na kupigwa, pengine Lulu alijitetea kwa nguvu zake chache inawezekana alimsukuma Kanumba akaenda kudondokea ukuta na kupata madhara, kwa maoni yangu kosa la kuua bila kukusudia limethibitika".

  Kufuatia hayo, kesi hiyo inatarajiwa kutolewa hukumu November 13 mwaka huu.

  0 0


  Hivi ndivyo  linavyoonekana eneo la Jangwani jijini Dar es salaam mchana
  huu, baada ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi ya jiji hili.
   Barabara ya Morogoro ikiwa imefungwa katika eneo la Fire, kufuatia maji mengi kujaa katika eneo Jangwani baada ya mvua kubwa ilinyeka maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam leo.
   Vikwangua anga vikiwa vimetandwa na wingu la Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar leo.
   Katika hali kama hii, baadhi ya wakazi wa Dar huona ni fursa kwao kutupa uchafu.
   Mkazi wa jiji la Dar akitota maji baada ya kulowa na mvua inayoendelea
  kunyesha wakati akisuburi kuvuka barabara katika eneo la Makutano ya barabara ya Bibi Titi na Morogoro.
  Usiombee gari ikubumie kiwese pindi mvua ikiwa inanyesha, maana unaipiga kibega peke yako labda kwa msaada wa abiria.

  0 0

   Mkurugenzi mkuu wa Sproxil Africa Chinedum Chijioke akizungumza wakati wa uzinduzi wa teknolojia ya simu za mkononi kwa ajili ya kudhibiti bidhaa bandia na kumlinda mteja nchini Tanzania ikiwa na lengo la kutokomeza na kudhibiti wauzaji feki wa bidhaa mbalimbali zinazoingia sokoni.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  KATIKA kudhibiti uuzwaji wa bidhaa bandia nchini, kampuni ya Sproxil Tanzania imezindua teknolojia ya simu za mkononi kwa ajili ya kudhibiti bidhaa bandia na kumlinda mteja nchini Tanzania.

  Sproxil Tanzania imewezeshwa na mfuko wa maendeleo ya ubunifu wa bidhaa za binadamu duniani Human Development Innovation Fund (HDIF) imeweza kuwasilisha rasmi ubunifu bora wa namna ya kudhibiti bidhaa bandia kwa makampuni,taasisi za udhibiti na serikali.

  Akizungumza wakati wa majadiliano ya wazi kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi mkuu wa Sproxil Africa Chinedum Chijioke amesema bidhaa bandia, batili, haramu na zilizochini ya kiwango ni hatari kwa afya za watumiaji wasio na hatia, upotoshaji wa bidhaa na pia zinateteresha ubora wa mwelekeo wa kiuchumi.

  Chijioke amesema, uwepo wa bidhaa hizo na zisizo na sifa zinaathiri vibaya watumiaji na kuathiri sifa za wazalishaji ndio sababu hii imekuwa wajibu wa serikali za sekta binafsi kuwawezesha watanzania kutumia njia bora za udhibiti zinazoratibiwa na kampuni yao.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini Godfrey Simbeye amesifia teknolojia hiyo na kusema ni nzuri na itasaidia sana katika kudhibiti watengenezaji wa bidhaa bandia kuweza kuingiza bidhaa zao sokoni na kupelekea kwa watumiaji na pia teknolojia hii isiishie tu kwa bidhaa hizi bali ziende mpaka kwenye pembejeo za kilimo ikiwemo Mbolea na dawa za mazao.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini Godfrey Simbeye akielezea namna teknolojia hiyo inavyoweza kuleta mapinduzi hususani kwa upande wa sekta binfasi kwani itasaidia kudhibiti uuzaji wa bidhaa bandia pamoja na kuwashauri kufika sekta ya kilimo hususani kwenye mbolea na dawa za kilimo.

  "Teknolojia hii inatakiwa ifike mpaka kwa wakulima kwani wamekuwa wanapata shida sana kwani wanauziwa sana pembejeo ambazo ni bandia na kusababisha hasara, kwahiyo Proxil Tanzania wameleta njia sahihi sana na mategemeo yangu ni kuona wanakuja kutumia mfumo huo kwa wakulima,"amesema Simbeye.

  Naye mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda Dr Samuel Nyatahe amesema wamiliki wa viwanda walikuwa wanapata tabu sana kupambana na bidhaa feki mtaani kwani wamekuwa wanauza vitu vyao kwa bei nafuu tofauti na wao wanaotengeneza bidhaa nzuri. Amesisitiza kuwa ni kosa la jinai na pia inafanya bidhaa kushuka thamani.

  Licha ya kuzindua huduma ya udhibiti wa bidhaa halali ili kulinda makampuni ya Tanzania, pia wamesema watashirikiana na kutakuwa na zoezi la kuthibtisha ubora wa bidhaa chini ya usimamizi wa bodi ya viwango vya ubora wa bidhaa Tanzania (TBS) na ile ya bodi ya utawala wa bidhaa za chakula na udhibiti wa madawa (TFDA) na jopo la wawakilishi wa sheria na sekta binafsi.
  Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda Dr Samuel Nyatahe akizungumza kwa upande wa sekta ya viwanda na kuelezea namna itakavyowasaidia katika kupambana na wauzaji wa bidhaa bandia ikiwemo kuwaondoa kabisa kwenye soko la ushindani.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Ilala Iddi Azan Zungu akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika eneo la Jangwani lilolokumbwa na mafuriko na kusababisha barabara ya Morogoro kufungwa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha leo Oktoba 26, 2017 Jijini Dar es salaam.
  Kituo cha mabasi ya mwendo kasi cha Fire kikiwa kimesimama kutoa huduma kwa abiria baada kujaa maji kwa  bonde la Jangwani na kufunika barabara kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam leo Oktoba 26, 2017.
  Eneo la bonde la Jangwani likiwa limefurika na kuziba barabara ya Morogoro kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.

   Barabara ya Morogoro ikiwa imefungwa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam.

  Gari za mwendokasi zikiwa zimesitisha huduma kwa sasa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha leo Oktoba 26, 2017 Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
  TANZANIA inataraji kuwa mwenyeji wa Semina ya siku tatu kwa Umoja wa Makampuni ya Bima Afrika kuhusu bima ya Maisha utakaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa AICC Arusha.

  akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mjumbe wa mkutano huo, Phaustine Oyuke amesema Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) kwa kushirikiana na Umoja wa makampuni ya Bima Afrika (AIO),Chama cha watoa huduma za Bima Tanzania(TIBA) Itakuwa Mwenyeji wa mkutano wa biama ya Maisha 2017.

  "Mkutano huu unafanyika kila mwaka ambapo mwaka huu nchi yetu imepewa heshima ya kuandaa ambapo mkutano huu utafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 3 mwezi Novemba mwaka huu ambao utajikita katika dhima ya mchango wa sekta Bima katika Mapinduzi ya Viwanda na Maendeleo endelevu kutokana na malengo ya nchi yetu na serikali ya awamu ya tano"amesema Oyuke.

  amesema kwa kuzingatia dhima hii masula mbalimbali yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na misingi ya uendelezaji wa huduma za bima,ubunifu, na malengo endelevu katika sekta ya bima ambapo mada hizi zinalenga kujadili na kutoa ufumbuzi kwa changamoto zinazoikumba sekta ya bima nchini na Afrika kwa ujumla .

  amesema TIRA kama msimamizi na mshauri wa serikali katika sekta ya na soko la bima inachukua fursa hii kuwaalika wadau wote katika sekta hii yaani makampuni ya Bima ,Madalali na Mawakala wa Bima nchini kutumia mkutano huu kama fursa adhimu kujifunza uendeshaji wa biashara ya bima .
  Mjumbe wa mkutano Mkuu wa wadau wa Bima Afrika, Phaustine Oyuke akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya umoja wa makampuni ya Bima Afrika kuhusu Bima ya Maisha.
  Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa umoja wa makampuni ya Bima Afrika kuhusu Bima ya Maisha, Khamis Suleimani akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Mkutano huo.
  Mjumbe wa Mkutano wa umoja wa makampuni ya Bima Afrika kuhusu Bima ya Maisha,Magreth Ikingo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano huo.

  Waandishi wa habari waliohudhulia mkutano juu masuala ya bima Afrika

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango   katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
   Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohamed   (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya  Mzee wakati wa kikao cha siku moja cha  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 cha  Uongozi wa Wizara  hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
   Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango  wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),alipozungumza na Uongozi wa Wizara hiyo leo katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja.
   Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nassor Khamis alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi yake wakati wa kikao cha siku moja cha  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 cha  Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

  0 0

  Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
  WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kuwa viongozi wa siasa waige mfano kwa viongozi dini kujenga tabia ya kukutana mara kwa mara wanapoona matatizo yanapoibuka katika jamii ambayo yanaweza kuvuruga umoja wetu.

  Jaji Warioba ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Amani na Umoja nchini, amesema kuwa viongozi wa dini wakiona mambo hayaendi sawa huwa wanakutana na kujadili lakini viongozi wa siasa hawafanyi hivyo.

  Amesema kuwa viongozi siasa wawe tayari kukutana na kujadili mambo ambayo yanaashiria kuvunja umoja wetu na sio kila mtu kutumia vyombo vya habari kuzungumza juu matatizo yanayotokea.

  "Tuache malumbano kwa mambo ya msingi tofauti za vyama vya siasa vinaweza kuturudisha nyuma , ulinzi wa nchi hii ni jukumu la kila mtanzania tena mzalendo" amesema Jaji Warioba

  Jaji Warioba ameongeza kuwa kuna mauaji ya watu wenye Ualbino , Migogoro ya Wafugaji na Wakulima mkoani Morogoro hayo ni mambo watu lazima wanasiasa wakutane na kujadili mambo hayo.

  Amesisitiza amani ikivurugwa hakuna mtu anaweza kuirudisha kwa wepesi hivyo ni lazima imani ilindwe kwa nguvu zote kwa kuachana na tofauti za kisiasa.
   Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza wakati alipokuwa akifungua Mdahalo wa Mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Kulinda na Kudumisha Amani na Umoja Nchini Tanzania lililoandaliwa Tasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation.
    Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Prof Mwesigwa Baregu.
   Viongozi wa kisiasa na Dini mbalimbali wakifatilia Mdahalo wa Mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Kulinda na Kudumisha Amani na Umoja Nchini Tanzania
   Wajumbe waliohudhuria Mdahalo wa Mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Kulinda na Kudumisha Amani na Umoja Nchini Tanzania
  Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mdahalo wa Mashauriano juu ya Umuhimu wa kuhimiza Kulinda na Kudumisha Amani na Umoja Nchini Tanzania.Picha Zote na Humphrey Shao.

  0 0

  KIKOSI cha timu ya Mbeya City kesho kinashuka dimbani kuvaana na timu ya Azam katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kwa ajili ya mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

  Kuelekea mchezo huo,Meneja wa Mbeya City , Geoffrey Katepa amesema  kwamba wapo hapa tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazoezi yao Uwanja wa Uhuru na wakiwa wameweka kambi katika hostel za wokovu maeneo ya kurasini.

  “Leo tumefanya mazoezi yetu ya mwisho hapa Uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo wetu wa kesho dhidi ya wenyeji wetu, Azam, dhamira kuu ikiwa ni kutopoteza tena mechi,”amesema.

  Katepa amesema anafahamu mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu Azam watakuwa wanacheza nyumbani kwao, lakini watapigana kiume kuhakikisha wanawazima hapo hapo Azam Complex.

  “Niseme tu kwamba tunawaheshimu wapinzani wetu, ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri na walimu wazuri. Lakini hata sisi tuna wachezaji wazuri na walimu wazuri na pia ni timu nzuri na ndio maana tupo kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu,”.

  Amesema katika  mchezo huo anaamini utakuwa mgumu sana kwa pande zote na kwa sasaMbeya City inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi saba, ikizidiwa pointi moja na Singida United iliyo nafasi ya tano na inazidiwa pointi mbili na Azam FC iliyo nafasi ya nne.

  Simba, Yanga na Mtibwa Sugar zote zinafungana kileleni mwa Ligi Kuu kwa kila timu kuwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi sana pia.

  Mechi nyingine za Ligi Kuu zinatarajiwa kuchezwa Jumamosi, mabingwa watetezi, Yanga watamenyana na Simba, Uwanja wa Uhuru, Maji Maji wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mtibwa Sugar wataikaribisha Singida United Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro, Lipuli watakuwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa Samora mjini Iringa na Kagera Sugar wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

  0 0

  Na Wankyo Gati, ARUSHA

  Waziri wa maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigangwala amesema kuwa watoa huduma mbalimbali za utalii watatakiwa  kufuzu mtihani kabla ya kupewa leseni mpya kuanzia Januari 2018 ambapo Serikali itaandaa utaratibu mpya katika sekta hiyo.

  Ambapo alisema kuwa Wizara yake iko katoka mchakato wa kuandaa mwongozo kwa ajili ya makampuni ya utalii nchini pamoja na kufunga mashine maalumu ambayo itadhibiti mapato yatokanayo na utalii.

  Aliongeza kuwa wizara yake itarekebisha mfumo wa watoa huduma katika sekta hiyo ambao umekuwa ukilalamikiwa na wadau mbalimbalui hasa watoa huduma za utalii wanaowashawishi watalii kutoka nchi mbalimbali za nje kuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini.

  Dk. Kigangwala aliyasema hayo jana wakati alipokuwa anazungumza na watumishi wa Shirika la hifadhi la Taifa (Tanapa)katika ziara yake ya kutembelea ofisi mbalimbali za shirika hilo.

  Alisema lengo hasa lakuanzisha mchakato huo utakaoanza kutumika mapema mwakani nikuweka vigezo vitakavyotolewa na Serikali kwa makampuni ili kuhakikisha wanakuwa na wahudumu watakaothibitishwa na wizara yake na kutoa cheti maalum kwa kila anaetoa huduma hiyo ya utalii.

  Waziri huyo alisema lengo nikuboresha huduma za utalii ili kuwezesha upatikanaji bora wa huduma za utalii na mapato ambayo yanainua uchumi kwani Tanzania sasa inashindana na nchi mbalimbali katika kuvitangazavivutio vya utalii ili kuhakikisha watalii wenguwanakuja zaidi nchini kwetu.

  Pia aliongeza kuwa watoa huduma za utalii wanapaswa kuzungumza vizuri kutoka nchi mbalimbali ili waweze kuja lakini pia waangalie jinsi ya kuboresha huduma za utalii ikiwemo mapatona mfumo huu mpya wa kukusanya mapatio ua sekta ya utalii kuboreshwa kuongeza mapato kwa mfumo wa kieletronik.

  Aliongeza kuwa maeneo wanayoweka mkazo zaidi ni ukusanyaji wa mapato hiyvyo kutakuwa na dirisha moja litakalounganisha taasisi za utalii kujua mapato yanayoingia nikiasi gani na mtalii anakaa nchini kwa muda gani na hoteli ip na kujua mapato yamnayokusanywa kwa sekta ya utalii yanakuwa kwa kiasi gani.

  Kwa upande wake Mkurugeni wa Tanapa Allan Kijazi alisema kuwa utaratibu huo utakuiwa mzuri na kpia wako katika mchakato wa kufungua ofifi katika mkoa wa dodoma ili kuweza kusogeza huduma mbalimbali zinazotoklewa nashirika huilo ili kuboresha sekta ya utalii na kuongeza pato la nchi kupitia sekta hiyo.

  0 0

  Matangazo haya yanahusu uteuzi wa viongozi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

  Matangazo haya yatarushwa kupitia Televisheni ya Taifa - TBC1, Redio - TBC Taifa na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

  0 0

  Fainesy Matiholo akishangilia ushindi wake wa kitita cha Milioni 65 akiwa baba na Mama yake Tabora Mjini.

  Fainesy Matiholo, mkazi wa Tabora Mjini ambaye amekuwa akicheza Tatu Mzuka huku akiwaa kuwa itatokea siku aibuke msndini basi, siku hiyo ikawa ni Jumapili iliyopita ambapo akaibuka kuwa mshindi wa 12 wa droo kubwa ya Tatu Mzuka na kujinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania Milioni 65.

  Bi. Matiholo amekabidhiwa zawadi yake ya ushindi na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mheshimiwa Queen Mlozi ambaye alitoa zawadi hiyo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Aggrey Mwanri. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Tabora.

  “Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kila juma lakini lengo langu kubwa lilikuwa kupata ushindi wa kila saa. Sikutarajia kabisa kuwa nitaibuka mshindi wa droo kubwa ya Tatu Mzuka,” anasema.

  Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi. Mlozi alizungumza kuwa; “tumefurahi sana kuona kuwa juma hili mshindi wa Tatu Mzuka katika katika Mkoa wetu. Ushindi huu umetusaidia kuamini kuwa mchezo huu unatoa fursa sawa kwa watu wote. Naamini sasa wananchi wa Tabora watahamasika zaidi kushiriki katika mchezo huu.”

  Katika ushindi huu wa Bi. Matiholo pia rafiki zake watatu ambao hushiriki kucheza Tatu Mzuka nao wamefanikiwa kujishindia kiasi cha Shilingi milioni 1 kila mmoja kupitia kipengele cha Tatu Mzuka “cheza na washkaji na washikaji promosheni.” Walioshinda kipengele hiki ni Jacqueline Samuel, Sande Kabaye na Lilian Tegete.

  “Tatu Mzuka imebadili maisha yangu,” Bi. Matiholo anasema na kuongeza kuwa; “naweza sasa kuanza kupanga namna ya kuishi maisha bora zaidi, nitaweza kumpatia mwanangu elimu bora zaidi na pia kuboresha biashara yangu,“ alieleza.

  Hata wewe unaweza kuwa mshindi ajaye wa Tatu Mzuka na safari hii mshindi anatarajiwa kupata kitita kinachofikia milioni 110. Hadi sasa kumekuwepo na washindi zaidi ya milioni 1.7 waliojishindia zawadi mbalimbali kutoka Tatu Mzuka. Pia kuna zaidi ya shilingi milioni 500 zinazosubiriwa kushindaniwa kadri siku zinavyoenda. Unaweza kuwa mshindi lakini jambno la kufanya ni kushiriki mchezo huu mara nyingi zaidi uwezavyo.
  Fainesy Matiholo mshindi wa 12 wa droo kubwa ya Tatu Mzuka na kujinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania Milioni 65.

  Mheshimiwa Queen Mlozi Mkuu wa Wilaya wa Tabora akitoa zawadi kwa Fainesy Matiholo akimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Aggrey Mwanri.Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Mkoa wa Tabora.

  0 0


  0 0

  Serikali inatumia mikopo inayoipata kutoka kwa wadau wa Maendeleo kwenye miradi ya uzalishaji na Miundombinu ili iweze kuwa na tija kwa Jamii na Serikali. Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt, Jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa, Serikali imejipanga kulipa madeni kwa wadau mbalimbali baada ya madeni hayo kuhakikiwa, hata hivyo amesema kuwa hatua za kukopa zitaangaliwa kwa umakini mkubwa ili kuzuia kuwa na madeni ambayo hayana tija kwa wananchi na Serikali. Tayari baadhi ya madeni yameanza kulipwa na Serikali imeendelea kutimiza ahadi zake ilizozitoa kwa wananchi kwa kuangalia vipaumbele vyenye kuleta matokeo chanya na ya haraka kwa wananchi, utekelezaji wake unazingatia weledi mkubwa ili kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa kwa wakati.

  “Aidha katika kuhakikisha Serikali inaendelea kuwahudumia wananchi ipasavyo, kumekuwa na mikakati ya kuwaongezea watumishi ujuzi ili kuendana na kasi ya maendeleo kuelekea uchumi wa kati kwa kuwa tuna uhaba wa watu wenye ujuzi wa kutosha, hivyo ni vyema wadau wa maendeleo wakalitazama hilo ili kusaidia katika kuharakisha ukuaji wa uchumi”, alieleza Dkt. Mpango.

  Kwa upande wake Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt amesema kuwa nchi yake inania ya kusaidia kukuza Sekta ya nishati na tayari mazungumzo na Wizara husika yameanza. Alielezea umuhimu wa Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa nchi ambapo amesema nchini mwake wafanyabiashara wanachangia pato la ndani kwa asilimia 50 kwa kuwa kuna biashara huria.

  Waziri Mpango amesema kuwa Serikali inafanyajitihada za dhati kuhakikisha kuna mazingira bora ya biashara na ili kufikia huko kumekuwa na majadiliano ya mara kwa mara na wafanyabiashara nchini ambapo kero zao nyingi zimetatuliwa ikiwemo kupungua kwa uwingi wa kodi.

  “Siwezi kuwa Waziri wa Fedha ikiwa sitakuwa na wafanyabiashara, kwa kuwa wao ndio wanaolipa kodi zinasosaidia kuendesha nchi”, aliongeza Dkt. Mpango.

  Kuhusu utekelezaji wa Demokrasia na Haki za Binadamu, Dkt Mpango amesema kuwa mambo hayo yapo kikatiba na Tanzania inafuata katiba na kuiheshimu hivyo haki za binadamu zinafuatwa kwa mujibu wa sheria na hakuna yeyote anayependa haki zake zivunjwe. Hata hivyo ameeleza kuwa ni vema tamaduni za Mtanzania zikaendelea kuheshimiwa wakati wa utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano wa maendeleo. Alitoa wito kwa jamii kuendelea kutangaza yale mazuri yanayojitokeza nchini yakiwemo ya kukua kwa uchumi kwa kuwa Tanzania itajengwa na watanzania.

   “Inashangaza kuona baadhi ya watu wakieleza mabaya tu ili hali kuna mafanikio mengi yaliyopatikana, tunakaribisha ukosoaji lakini wenye tija” alifafanua Dkt. Mpango.

  Pia, alisema Serikali inadhamira ya dhati ya kulinda wawekezaji wa ndani lakini amewataka wawekezaji hao kuungana kwa lengo la kuongeza nguvu na nyenzo bora ili watakapopata fursa ya kujenga miundombinu na mambo mengine, wafanye kwa ubora unaokubalika na wenye tija.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kulia) na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt (wa pili kulia) pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka pande hizo mbili wakiwa katika mkutano ulioangazia ushirikiano wa maendeleo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) akizungumzia umuhimu wa kufuata utamaduni wa mtanzania katika kustawisha ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden wakati wa mkutano na Balozi wa Sweden Nchini, Bi. Katarina Rangnitt, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt (kushoto) akielezea Sekta ya biashara katika nchi yake inavyofanikisha kuchangia takribani asilimia 50 ya pato la ndani wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, kulia ni Naibu Balozi wa Sweden Bw. Ulf Kallstig ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Balozi wa Sweden nchini Bi. Katarina Rangnitt wakijadili jambo baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya pande hizo mbili katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo Mjini Dodoma ambapo walikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Hawa Ghasia akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Mjini Dodoma ambapo leo imekutana na Taasisi ya Sekta Binafsi kujadili kuhusu vyanzo vya mapato ya Serikali na mapendekezo ya hatua za kupunguza utegemezi wa kibajeti kwa mwaka 2018/19
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Hawa Ghasia akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Mjini Dodoma ambapo leo imekutana na Taasisi ya Sekta Binafsi kujadili kuhusu vyanzo vya mapato ya Serikali na mapendekezo ya hatua za kupunguza utegemezi wa kibajeti kwa mwaka 2018/19
  Mjumbe wa Kamati ya Bajeti, Mheshimiwa Janeth Mbene akichangia jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Mjini Dodoma, Kamati Bajeti 3 ambapo leo imekutana na Taasisi ya Sekta Binafsi kujadili kuhusu vyanzo vya mapato ya Serikali na mapendekezo ya hatua za kupunguza utegemezi wa kibajeti kwa mwaka 2018/19.

older | 1 | .... | 1982 | 1983 | (Page 1984) | 1985 | 1986 | .... | 3283 | newer