Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI JINSI YA KUTENGENEZA PIPI ZA VIJITI KWA KUTUMIA SUKARI GURU NA SUKARI YA KAWAIDA

$
0
0
Wewe  ni  Mjasiriamali  mdogo  ?  Unataka  kupata  ujuzi  sahihi  utakao  kusaidia  kuongeza  kipato  chako ? Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi  hii ni  HABARI  NJEMA  SANA  KWAKO. 
 Neema  Institute  Of  NGO  Management  wanakutangazia  nafasi  za  kushiriki  katika   mafunzo  ya  ujasiriamali.
Somo  litakalo  fundishwa  ni  namna    ya KUTENGENEZA  PIPI  ZA VIJITI kwa  kutumia  SUKARI  GURU  na  SUKARI  YA  KAWAIDA. 
Mafunzo  haya yatafanyika    siku  ya  JUMAMOSI  ya  tarehe  04  NOVEMBA  2017  kuanzia  SAA  TATU  KAMILI ASUBUHI   katika  madarasa  ya   MBUJI  EDUCATION  CENTER   yaliyopo  mtaa  wa  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO PLAZA  jirani  na  KAGAME  HOTELI. 
ADA  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  ni   NAFUU SANA.

Tunapatikana  mtaa  wa  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.  Kujiandikisha  katika  mafunzo haya, wasiliana  nasi  kwa   SIMU    0787  016  929.
 FAIDA   ZA   KUSHIRIKI   KATIKA  MAFUNZO  HAYA 
Pipi  za  vijiti  zinazo  tengenezwa  kwa  kutumia  SUKARI  GURU  na  SUKARI  YA  KAWAIDA  ni  bidhaa  inayo  pendwa   sana  na  watoto  wa  shule  za  msingi , sekondari  na watoto  wote  kwa  ujumla. Ujuzi  wa  kutengeneza  pipi  hizi  utakusaidia  kuongeza  kipato  chako. 
 Kama  wewe  ni  mjasiriamali  ambae  tayari  una  nafasi  ya  kuuza  biashara  kwenye  eneo la  shule, mafunzo  haya  yatakupa  ujuzi  utakao  kuongezea  kipato. 
CHANGAMKIA  FURSA  HII  MAPEMA.

Wakwepa kodi marufuku jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere - Eng.Nditiye

$
0
0
WAFANYABIASHARA wenye kulipa kodi na kuingizia serikali mapato kwa wakati ndio watakaopata nafasi ya kuwekeza kwenye jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), imeelezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipofanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na kumalizia TBIII.
Mhandisi Nditiye amesema baada ya kukamilika kwa jengo hilo baadaye mwakani, wafanyabiashara watakaopewa kupaumbele hususan waliopo kwenye Jengo la zamani (TBI) na jengo la pili (TBII) ni wale tu wanaozingatia ulipaji wa kodi na mapato yote ya serikali kwa wakati.
“Tunajua wapo wengi waliojitokeza kuomba maeneo ya kufanya biashara, lakini wale ambao watahama kutoka majengo yetu haya mawili la TB I na TBII tunawaambia wazi kabisa kuwa wale waaminifu na waadilifu wenye kulipa kodi ya pango na mapato mengine ya serikali kwa wakati ndio wanafikiriwa kwanza, na wale wasiolipa kwa wakati hawatapewa nafasi kabisa ya kuwekeza kwenye jengo hili,” amesisitiza Mhe. Nditiye.
Hata hivyo, Mhe. Nditiye amesema tayari ameuagiza uongozi wa TAA kuhakikisha wanapitia mikataba yote ya biashara kwenye majengo hayo ya abiria na kutengeneza upya ile yenye matatizo ili iweze kuleta tija kwa taifa, kwani kwa sasa kumekuwa na mikataba ya hovyo.
Amesema TBIII inafursa za biashara ambapo inaeneo kubwa la kujenga hoteli, migahawa na sehemu za kupumzikia watu, hivyo kuwataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza.
“Juzi tu nilikutana na Wajerumani nikawaeleza tunaeneo la uwekezaji hapa TBIII na kule Msalato mnapotarajia kujenga kiwanja cha kimataifa, na wameonesha nia ya kuja kuwekeza, nia ya serikali na tupo pamoja katika uwekezaji wa maeneo yetu mbalimbali, ili kujiimarisha katika uchumi,” amesema Mhandisi Nditiye.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amesema kuwa wanatarajia watoa huduma na wafanyabiashara watakaokidhi vigezo na masharti ya kutoa huduma bora ndio wakaopata nafasi kwenye jengo hilo la tatu.
“Pia tunatarajia watoa huduma na wafanyabiashara ni wale wanaokodhi vigezo kwa hiyo yote yanalenga katika kuhudumia watanzania na kukuza sekta ya usafiri wa anga na kuhudumia vizuri wale wanaopita hapa,” amesema Bw. Mayongela.
Amesema jengo hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria takribani milioni sita (6) kwa mwaka ambalo ni ongezeko kubwa ukilinganisha na jengo la sasa la TBII linauwezo wa kuihudumia kati ya abiria milioni 1.2 hadi 1.5 kwa mwaka.
Hivyo tunaishukuru serikali kwa kutupa ushirikiano katika kuendeleza viwanja vya ndege,  pia kwa upande wa TAA wamekuwa wakifanya matengenezo madogo madogo kwa kutumia fedha za bajeti ya ndani. 
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa ameitaka TAA kuwaondoa wafanyabiashara wote wasiolipa kodi na mapato mengine ya serikali kwa wakati, kutokana na kukwamisha juhudi za serikali za ukusanyaji mapato.

Mhandisi Balton Komba wa Tanroads (wan ne kushoto) akimpa maelezo ya jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Ndikiye (wa tatu kushoto), na Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.
 Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (wa pili kulia), Juma Yange akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeshika karatasi) alipotembelea kituo hicho. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), (mbele katikati), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akiongea na Menejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Makao Makuu, kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea majengo matatu ya abiria ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo.

mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini aipiga jeki sekta ya afya zanzibar

$
0
0
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema utamaduni wa watu wa Zanzibar wa kuheshimu dini zote ni nguzo imara iliyosimamisha  amani na utulivu nchini.
Balozi Seif ameyasema hayo afisini kwake Vuga wakati akipokea msaada wa fedha taslim shilingi milioni 10 kwa ajili ya sekta ya afya kutoka kwa mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha nchini.
Amesema tangu zamani waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu wamekuwa wakiishi pamoja na kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kijamii bila ya mikwaruzano. 
Amesema msaada huo wa fedha ambao umekusudiwa kwa hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja umekuja wakati muwafaka ambapo Serikali imo katika mipango ya kuimarisha huduma zote zitolewazo hospitalini hapo.
Akikabidhi msaada huo wa shilingi milioni 10 kwa Makamo wa Pili wa Rais, mchungaji Bariki Urassa amesema madhehebu yao ya Efatha hupeleka misaada yake pale inapohitajika.
Amesema wakati wa ziara ya kiongozi wao Mkuu wa Efatha Duniani mchungaji Josephate Elias Mwingira alipoonana na makamo wa Pili wa Rais aliahidi kuisaidia Hospitali ya Mnazi Mmoja, ahadi ambayo amekuja kuitekeleza kwa niaba yake. 
Sherehe fupi ya makabidhiano ya msaada huo ilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ndugu Asha Ali Abdallah ambaye kwa niaba ya Wizara yake ameahidi kuutumia msaada huo kama ulivyokusudiwa.
Katibu Mkuu huyo amesema Wizara yake itatoa mashirikiano ya karibu kwa wale wote wanaotaka kuchangia na kutoa wito kwa taasisi nyengine  za  ndani na nje kujitokeza kutoa misaada yao kwa Wizara yake ambayo imepewa majukumu makubwa ya kuwahudumia kifya wananchi wote wa Zanzibar. 
 Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akipokea msaada wa fedha taslim shillingi milioni 10 kutoka kwa mchungaji Bariki Urassa wa madhehebu ya Efatha kwa ajili ya hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akionesha msaada huo wa fedha taslimu kwa waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ndugu Asha Ali Abdallah

Bashe akagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Sekondari ya Wasichana jimboni kwake Nzega

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe amekagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Sekondari ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla. 
 Mafanikio ya ujenzi wa shule hii ni maono ya Mheshimiwa Bashe katika kuhakikisha watoto wa masikini wanapata elimu ili kuweza kujikwamua na umasikini. 
 Mhe. Bashe amesema kuwa  anaamini ya kuwa ..."Elimu ndio njia pekee ya kumkomboa mtoto wa masikini" 
 Aidha Shule hii itakua na uwezo wa kupokea wanafunzi kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Sita huku msisitizo ukiwa ni masomo ya Sayansi. Ujenzi wa shule hii unaendana na ujenzi wa kituo cha Afya ambacho kitahudumia wananchi pamoja na wanafunzi ambao watakua wanasoma katika shule hiyo. 
 Bashe anasema "Tuna vipaumbele vingi lakini kile cha kwanza na msingi kwetu ni Elimu ya watoto wetu""Hivyo nitahakikisha ninaboresha miundombinu ya Elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini na kama sehemu ya urithi kwa watoto wa masikini".
 Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Sekondari ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega ukiendelea
 Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya sekondari ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla.
 Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe akikagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya sekondari ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla.
  Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe akiongea baada ya kukagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla.
 Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe akiongea baada ya kukagua Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Wasichana katika Jimbo la Nzega Mjini na wilaya ya Nzega kwa ujumla.

GAZETI LA TANZANIA DAIMA LAFUNGIWA KWA SIKU 90

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZITAKA BENKI KUFUNGUA MATAWI ZAIDI

$
0
0
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka benki zote zilizopo hapa nchini kuhakikisha zinaanzisha matawi yake katika mikoa mbalimbali ili kuwawezesha wananchi hasa wanawake kupata huduma za kifedha kirahisi.
Samia ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Wanawake na Fedha uliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Women’s World Banking na Benki ya NMB kuwa mshirika mwenza katika mkutano huo.
Mkutano huo ambao kwa mara ya kwanza umefanyika barani Afrika, nchini Tanzania umewakutanisha pamoja wanawake viongozi katika fani mbalimbali zaidi ya 300, zikiwemo mabenki, teknolojia, wafanyabiashara, mashirika ya umma na binafsi.
Mama Samia alisema benki zinapaswa kwenda zaidi kwa wananchi kwa kuanzisha matawi yao huko mikoani kwani baadhi ya watanzania wapo nje kabisa na mifimo ya kibenki kutokana na kutofikiwa.
“Asilimia 70 ya watanzania wanatumia simu za mkononi na kama mnavyojua Tigopesa, Mpesa na zinginezo zimesambaa sana hapa nchini hii inayonyesha huduma za kifedha tumepiga hatua ingawa bado kuna mambo tunapaswa kurekebisha kwa mfano mabenki yetu yaendelee zaidi kwenda huko kwa wananchi kwa kufungua matawi mengi.
Lakini pia benki yetu ya Wanawake ambayo imeundwa kwa madhumuni hayo tunaitaka ijitahidi kusambaza matawi yake huko mikoani, hivyo mkutano huu utaangalia ni jinsi gani jamii inafikiwa zaidi na huduma za kifedha hasa wanawake walioko vijijini ili wapate huduma za fedha ambazo ndizo zinakuza uchumi wan chi,” alisema.
Aidha alisema Shirika la Kimataifa la Women’s World Banking wameamua kuja kufanya kongamano hilo kwa mara ya kwanza hapa nchini ili kuja kuangalia Tanzania inafanyaje katika kusaidia maendeleo ya wanawake.
Naye Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Abdumajid Nsekela alisema mkutano huo uliowakutanisha watu mbalimbali utajikita zaidi kuangalia ni kwa jinsi gani wataweza kumuwezesha mwanamke kupata fursa ili aweze kujikwamua kwenye mitaji na uwekezaji.
Alisema Benki ya NMB imeshirikiana kwa karibu na shirika hilo la Women’s World Banking katika kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo ya kuwawezesha wananchi kwa maana ya mkulima na wafanyakazi hasa wanawake kwa kutengeneza bidhaa ambazo zitawawezesha kupata mikopo nafuu pamoja na kufungua akaunti.
“Zaidi ya wadau 300 ambao wametoka katika nchi mbalimbali duniani wapo katika mkutano huu wanajadiliana ni jinsi gani watumie teknolojia kumfikia mtanzania kwa ukaribu zaidi, wanawake wengi waliopo vijijini ni wakulima na wanahitaji huduma za kifedha hivyo mkutano huu ni mahususi kujadiliana changamoto zinazokwamisha kuwafikia wanawake


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano wa taasisi ya benki ya ulimwengu ya kusaidia maendeleo ya wanawake uliofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya NMB. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemeker, akiongea baada ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano wa Kimataifa la Women’s World Banking uliofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya NMB.


Washiriki a mkutano wa kimataifa wa Women’s World Banking.


  

ASKOFU NDIMBO WA MBINGA ANENA KUHUSU KIFO CHA HAYATI ASKOFU CASTOR WA MASASI TUNDURU

$
0
0
Askofu wa jimbo la mbinga ASKOFU JOHN NDIMBO leo ameongoza mapokezi ya kuupokea mwili wa hayati askofu CASTOR MSEMWA aliyefarika dunia tarehe 19.10.2017 saa saba mchana na mazishi yake yatafanika hapo kesho katika jimbo la MASASI TUNDURU mkaoni RUVUMA Askofu CASTOR MSEMWA ALIZALIWA TAREHE 13.02.1955 katika kijiji cha KITULIRA WIALAYANI NJOMBE .

SEKTA BINAFSI YATAKIWA KUPELEKA CHANGAMOTO ZAO SERIKALINI

$
0
0
Sekta Binafsi imetakiwa kuwasiliana moja kwa moja na Serikali ili kutatua changamoto zinazoikabili badala ya kupitia wadau wa nje kwanza, kwa kuwa mlango wa Serikali uko wazi kwa ajili ya majadiliano na kutatua matatizo ya Sekta hiyo.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) katika Mkutano na Sekta Binafsi nchini (TPSF), Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mpango amesema kuwa ni vema Sekta Binafsi ikashirikiana na Sekta ya Umma kwa kuwa zote zinategemeana na hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na Sekta Binafsi ambayo ni imara.
“Sekta Binafsi na Sekta ya Umma hazina budi kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu, tena kwa kuaminiana kwa faida ya Sekta zote mbili na kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla” aliongeza Dkt. Mpango.
Amesema kuwa, lengo la pande zote mbili ni kuharakisha utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuongeza fursa za ajira, kipato cha mwananchi na kuondokana na umasikini uliokithiri kwa kujenga Tanzania inayoongozwa na uchumi wa Viwanda.
Dkt. Mpango alifafanua kuwa Serikali imeendelea kuyafanyia kazi mapendekezo mengi yaliyotolewa na Sekta Binafsi ikiwemo katika kuboresha mazingira ya biashara nchini ikiwemo kuondoa baadhi ya kodi zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara.
Baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Serikali kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kumpa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Fedha mamlaka ya kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani bila kuhusisha utaratibu wa kulipa kwanza Kodi ya Ongezeko la Thamani na baadaye kuomba kurejeshewa (Refund) kwenye miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo (Grants) au mikopo yenye masharti nafuu (Concessional Loans) ambayo mikataba husika ina masharti ya kutoa msamaha wa kodi hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Godfrey Simbeye akifafanua jambo kwa wafanyabiashara waliohudhuria katika Mkutano kati yao na Serikali uliolenga kujadili mafanikio na changamoto za pande hizo mbili, uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti mweza wa mkutano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akielezea kuhusu umuhimu wa majadiliano katika kutatua changamoto za kibiashara nchini, mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza na wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa kupeleka taarifa za changamoto zao Serikalini ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

INTRODUCING " NAONA KIZA" BY BEKA FLAVOUR AND GENTLE MASTER

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA BIASHARA,VIWANDA NA MASOKO

$
0
0
 Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),alipozungumza na Uongozi wa Wizara hiyo leo katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja
 Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Amina Salum Ali (kulia) akiwasilisha taarifa ya  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017  katika  kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara  hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakiwepo na Viongozi wengine wa Wizara hiyo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko  katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja
Katibu Mkuu wa Wizara ya  Biashara,Viwanda na Masoko Nd,Juma Ali Juma akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),akiwepo   Mshauri wa Rais,Ushirikiano wa Kimataifa Fedha na Uchumi Mhe.Mohamed Ramia Abdiwawa  na Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Ndg. Ali Khamis Juma. Picha na IKULU

MAGAZETI YA JUMATANO LEO OKTOBA 25,2017

Elimu juu ya umiliki Ardhi kwa wanawake yaleta Mabadiliko

$
0
0
Wanawake katika Halmashauri za Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma wakishiriki katika zoezi la kuanisha mipaka ya maeneo yao yatakayotumika katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo makazi, kilimo,biashara n.k lililofanyika hivi karibuni Wilayani humo.
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma wakifuatilia mafunzo kuhusu mpango wa matumizi bora ya ardhi yaliyokuwa yakitolewa na Maafisa kutoka Shirika la PELUM Tanzania hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu, Kilolo

WANAWAKE katika Halmashauri za Wilaya ya Kilolo na Mufindi Mkoani Iringa wamepongeza jitihada za Shirika la PELUM Tanzania za kuwapatia elimu ya mafunzo kuhusu Mipango ya Matumizi bora ya Ardhi Vijijini kwa kuwa hatua itawasadia kutambua haki walizonazo katika kumiliki, kutumia na kupata rasilimali ya ardhi.

Akizungumza hivi karibuni katika semina ya mafunzo ya mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa Wananchi Wilayani Kilolo, Afisa Mipango Mji na Vijiji wa Wilaya ya Kilolo, Bernard Kajembe alisema kabla ya utekelezaji wa mradi wa CEGO suala la umiliki ardhi hususani kwa wanawake Wilayani humo ilikuwa ni jambo lisilopewa kipaumbile.

Kajembe alisema kuwa kwa kipindi kirefu mwanamke amekuwa akikosa haki yake ya kumiliki Ardhi kwa kigezo kuwa hana thamani kwenye familia aliyozaliwa na badala yake thamani yake ipo kwenye familia atakayoolewa na hivyo kupelekea mwanamke kuwa na jukumu la kutumia ardhi kwa ajili ya uzalishaji pekee.

“Tunalishukuru Shirika la PELUM Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri kutekeleza mradi huu na kutoa elimu ya awali kuhusiana na masuala ya ardhi ambapo imetoa mwanya kwa wanawake kuanza kumiliki ardhi na hasa kwenye vijiji vya mradi jambo ambalo kwa awali lilionekana ni kama uvunjaji wa mila na desturi” alisema Kajembe.

Kwa upande wake Bi. Maliamusi Mdalingwa mkazi wa kijiji cha Ugesa Wilayani Kilolo alisema katika siku za nyuma ilikuwa jambo gumu kwa wanawake wengi ndani ya ndoa kumiliki hata kama ana haki ya kisheria kumiliki kwa makubaliano yao wawili. Anasema mara baada ya mafunzo kutoka Shirika la PELUM Tanzania kwa sasa hali imekuwa tofauti kwani anathamini hata haki za watoto wake wa kike kuwa nao wanapaswa kumilikishwa rasilimali ya ardhi.

Naye Bi. Agnes Mbamilo toka kijiji cha Isaula wilayani Mufindi alipongeza Shirika la PELUM Tanzania kwa kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani yamesaidia kwa kiasi kikubwa kubadili fikra na mtazamo wa mume wake kwa sasa wana umiliki wa hati ya pamoja katika shamba na kiwanja cha nyumba.

Mbali na elimu ya Haki za ardhi kwa wanawake, mafunzo mengine yanayotolewa na Shirika la PELUM Tanzania ni pamoja na elimu juu ya Mpango wa matumizi ya Ardhi kijijini, Haki ya kupata, kutumia na kumiliki Ardhi Tanzania, Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Tanzania pamoja na Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii.

Mafunzo hayo yanatolewa kupitia mradi wa ushiriki wa wananchi kwenye Sekta ya kilimo (CEGO) na kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) yalitolewa katika vijiji 10 vya Wilaya hizo.

WAREMBO WA VYUO VIKUU WAJIFUA KUWANIA TAJI IJUMAA WIKI HII KING SOLOMON HALL

$
0
0

Warembo wa shindano la kumsaka Miss Vyuo Vikuu 2017, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao ya pamoja katika Ukumbi wa Maisha kujiandaa na shindano lao linalotarajia kufanyika Ijumaa ya wiki hii kwenye Uwambi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO BLOG)
Warembo wa shindano la kumsaka Miss Vyuo Vikuu 2017, wakiwa katika mazoezi ya Shoo yao ya pamoja katika Ukumbi wa Maisha kujiandaa na shindano lao linalotarajia kufanyika Ijumaa ya wiki hii kwenye Uwambi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Itifaki na Nidhamu wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye, akizungumza na warembo wa shindano la Miss Vyuo Vikuu 2017, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi ya kujindaa na shindano hilo linalofanyika Ijumaa wiki hii kwenye Ukumbi wa King Solomon Namanga.
Warembo wa shindano la kumsaka Miss Vyuo Vikuu 2017, wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja katika Ukumbi wa Maisha kujiandaa na shindano lao linalotarajia kufanyika Ijumaa ya wiki hii kwenye Uwambi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA MADAKTARI KUTOKA( WAMY)

$
0
0
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Madaktari kutoka Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu Duniani (WAMY) kuhusiana na Matibabu walioyafanya kisiwani Pemba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
Kiongozi wa Madaktari kutoka Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu Duniani(WAMY) Dk,Sultan Baghdadi akizungumza machache kuhusiana na Matibabu walioyafanya kisiwani Pemba katika mkutano na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
Mkurugenzi Idara ya Huduma za Hospitali Wizara ya Afya Zanzibar Dk,Mohammed Dahoma akitoa neno la shukurani kwa Madaktari kutoka Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu Duniani(WAMY) kuhusiana na Matibabu walioyafanya kisiwani Pemba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Unguja.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kulia akimkabidhi cheti Dk,Ahmed Yasin Abukrecha ambae ni miongoni mwa madaktari kutoka Jumuiya ya Vijana wa Kiislam Duniani(WAMY)waliofanya Matibabu kisiwani Pemba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja Mjini Unguja. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

WALENGWA WA TASAF WAPOKEA BILIONI 20 KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI MKOANI TABORA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, RS-TABORA

JUMLA ya shilingi bilioni 20 zimetolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Halmashhauri zote za Tabora kwa ajili kunusuru kaya maskini katika eneo hilo.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Mratibu wa TASAF Mkoa huo Ngoko Buka wakati  wa kikao cha kutathmini utekelezaji wa TASAF Awamu ya Tatu sehemu ya kwanza kilichowashirikisha Wafadhili ,viongozi kutoka makao Makuu TASAF na wale wa Mkoa na Wilaya ya Uyui.

Alisema kuwa fedha hizo zilitolewa katika kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi Agosti mwaka huu ambapo jumla ya walengwa 45,928 waliwezwa  kunufaika na fedha hizo na hatimaye kubadilisha maisha yao.

Buka alisema kuwa fedha zimesaidia baadhi ya walengwa kuanzisha miradi mbalimbali kama ufugaji wa kuku,bata,mbuzi ,ng’ombe ,ujenzi wa nyumba bora, kusomesha watoto, kuwapa huduma ya kliniki na kuimarisha kilimo.

Alisema kuwa mambo mengine ambayo walengwa wamenufaika nayo ni pamoja na uanzishaji wa biashara mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa imebadilisha maisha ya walengwa.

Naye Mkuu wa Msafara wa TASAF kutoka Makao Makuu Dkt. Jasson Bagonza alisema kuwa wako mkoani Tabora kuangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoratibiwa na Mfuko huo na kujadiliana na wadau mbalimbali ili kuona kama inakwenda  malengo ya uanzishaji wake.

Alisema kuwa baada ya tathmini hiyo watakuja na TASAF awamu ya Tatu sehemu ya pili iliyoboreshwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi wake.

Watumishi wanolewa kudhibiti matumizi mabaya ya Gharama za Uchaguzi, Uchaguzi Mdogo wa Madiwani

$
0
0
Msajili wa vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi akisisitiza jambo kwa watumishi (hawapo pichani) wakati wa Mafunzo ya siku mbili ( jana na leo)kwa watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na wagombea yaliyofanyika katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa Salaam.
Bi Piencia Kiure, Msajili Msaidizi akitoa maada juu ya Elimu ya Maadili ya Vyama vya Siasa wakati wa Mafunzo ya siku mbili ( jana na leo)kwa watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na wagombea yaliyofanyika katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa Salaam.
Bi. Esther Mwanri, Mwanasheria Mwandamizi aktoa mada juu ya matendo yaliyokatazwa kwenye sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati wa Mafunzo ya siku mbili ( jana na leo)kwa watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na wagombea yaliyofanyika katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa Salaam.

Na Monica Laurent, Ofisi ya Msajili wa Vyamavya Siasa

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi amewataka watumishi kutoka ofisi yake kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuleta weledi katika kazi. Hayo ameyazungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Gharamaza Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na wagombea yaliyofanyika Jana na Leo katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa Salaam.

“Chapeni kazi na kuwa vinara wa kusimamia gharama za uchaguzi na maadili ya Vyama vya Siasa ili kubaini wagombea ambao hawafuati matakwa ya sheria ” amesisitiza Jaji Mtungi. Naye Bi Piencia Kiure, Msajili Msaidizi wakati akitoa mada juu Elimu ya maadili ya Vyama vya Siasa ,amewasisitiza watumishi kuendelea na utamaduni wa kufanya kazi kwa weledi.

Sheria namba 6 ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015 kupitia Amri ya Gharama ya uchaguzi inaweka wazi viwango vya juu vya matumizi kwa wagombea, kudhibiti matumizi ya fedha zinazotumika wakati wa uchaguzi kuanzia katika mchakato wa uteuzi, kampeni na kupiga kura ili kuweka uwanja sawa wa kisiasa na kudhibiti vitendo vya rushwa.

Sheria hii hubainisha wajibu wa Mgombea na Chama cha Siasa kujaza fomu maalumu za gharama za uchaguzi ili kubainisha bajeti yake ambayo ni mapato na vyanzo vya mapato na kurejesha katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndani ya siku saba baada ya uteuzi wa wagombea unaofanywa na Tume ya uchaguzi .

Fomu maalumu ya kubainisha marejesho ya matumizi ya uchaguzi inayoambatana na kumbukumbu na stakabadhi za malipo hujazwa na mgombea na kurejeshwa kwenye chama chake ndani ya siku sitini baada ya uchaguzi, chama cha siasa kina wajibu wa kuiwasilisha fomu hiyo kwenye ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndani ya siku 180 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Hata hivyo ukiukwaji wa sheria hii unaambatana na adhabu kali ambayo hutolewa kwa chama ambacho kitashindwa kuwasilisha mapato na matumizi ya kila mgombea ambayo ni pamoja na kufutiwa kushiriki uchaguzi endapo kitashindwa kutoa maelezo ya kuridhisha.

Usimamizi wa Sheria ya gharama za Uchaguzi katika uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe Novemba 26 mwaka huu ni mwendelezo wa usimamizi wa sheria hii ambao hufanywa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa uchaguzi wa Urais, Wabunge na Madiwani. Kwa mara ya kwanza sheria hii ilianza kutumika katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010

RC Rukwa aagiza kufuata utaratibu uingizwaji wa mahindi kutoka nchi za jirani

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameziagiza Halmashauri zote Mkoani kwake kuhakikisha wanakuwa na magulio rasmi ya kuuzia mahindi ili wakulima na wafanyabiashara waweze kufuata utaratibu.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutakuwa na usimamizi thabiti na taratibu za uingizwaji wa bidhaa kutoka katika nchi za jirani utafuatwa pamoja na mamlaka husika kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na halmashauri kupata mapato na nchi kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kufanya ziara ya ghafla katika Kijiji cha Safu, kilichopo mpakani mwa Tanzania na Zambia na kujionea malori yenye shehena za mahindi yakiingizwa kiholela kutoka katika nchi ya Zambia bila ya kuwepo kwa mamlaka husika zinazosimamia uingizwaji wa bidhaa kutoka katika nchi za jirani.
“Ni mategemeo yangu kuwa wakurugenzi wataanzisha vituo ili wakulima waweze kupeleka mazao yao hapo na kuweza kuyauza na ndipo nao halmashauri waweze kukusanya ushuru unaotakiwa, lakini hizi biashara zinazofanywa kupitia njia za panya, nasema si kitu cha kuachiwa, hivyo basi nisingependa kuona malori yanaruhusiwa kwenda maeneo ambayo siyo mipaka rasmi kuchukua mizigo na kuingiza nchini,” Amesema.

Na kuongeza kuwa hakuna tatizo kufanya biashara na nchi za jirani isipokuwa biashara hizo zifanywe kihalali kwa kufuata sheria zilizowekwa.
Halikadhalika Mh. Zelote Alisema kuwa Mkoa wa Rukwa una mahindi ya kutosha na wafanyabiashara wa mikoa mingine wafike kununua na sio kuvuka mipaka kwa njia za kupanya kufanya biashara hiyo.

Kwa upande wao wafanyabiashara waliohojiwa na Mh. Zelote katika ziara yake hiyo walidai kuwa mahindi yanayotoka Zambia bei yake ni nafuu zaidi kuliko ya Tanzania lakini pia wakulima wa Tanzania huficha mahindi yao wakisubiri kupanda kwa bei jambo ambalo ni hasara kwa wafanyabiashara wanaotoka nje ya Mkoa wa Rukwa.

“Wakulima wa Mkoa wa Rukwa huficha mazao yao wakisubiri kupanda kwa bei, sasa kama mimi mfanyabiashar natokea Mwanza nakuja kwa mahesabu ya kuchukua mzigo na kuondoka, nikisema nimsubiri huyu mkulima aliyeficha mazao yake hadi yaapande mimi nakula hasara,” Amiri Giti mfanyabiashara kutoka Mwanza alisema.

DAS IRINGA AWATAKA WALIMU KUTUMIA KINGA

$
0
0

Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo.
Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.

Na Fredy Mgunda, Iringa. 

Walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kinga (kondomu) ili kujikinga na magonjwa ya zinaa ambayo yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa. Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa.

Chintinka alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia kondomu.



“Jamani hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi” alisema Chintinka

Chintinka alisema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya kinga

“Naombeni tuwakinge hawa watoto wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto wengine maana bila hivyo tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema Chintinka

Aidha Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za lishe.

“Jamani walimu fungu la lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni walimu mjitokeze ili mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi ndio tunaotenga naombeni fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao hawajafika hapa” alisema Chintinka

Chintinka aliwataka watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha tabia hiyo mara moja ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze kujitokeza na wapate lishe iliyotengwa na wilaya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

"Kwa kweli mgeni rasmi umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri nje kitu kinachowafanya walimu waathirika kujificha na maradhi yao” alisema Mgongolwa

Naye Katibu wa Chama cha Walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla atembelea Ngorongoro

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara maalum kukagua masuala mbalimbali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro sambamba na kuzungumza na viongozi wa Mamlaka hiyo kwenye eneo la makao makuu yake yaliyopo ndani ya hifadhi. 

Katika ziara hiyo, Waziri Dkt. Kigwangalla ameweza kupokea kupokea maoni na masuala mengine ya kuendeleza Mamlaka hiyo ya Ngorongoro. Waziri yupo Ngorongoro kwa muda wa siku mbili ambapo pia amepata kutembelea maeneo ya hifadhi yenye migogoro na wafugaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokelewa na viongozi wa Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25, 2017.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa hifadhi hiyo wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25, 2017.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa mhifadhi wa Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25,2017
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza maoni kutoka kwa viongozi wa hifadhi ya Ngorongoro wakati alipowasili kwenye makao makuu ya hifadhi ya Ngorongoro leo Oktoba 25,2017.
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri wa Maliasili Dkt.Kigwangalla alipowasili hapo mapema leo kwa ajili ya kupata maelezo na ya kina namna ya uendeshaji na masuala mbalimbali.

KESI YA LULU: USHAHIDI WA MUSHUMBUS WASOMWA MAHAKAMANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii.


MAHAKAMA Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kwa kushirikiana na wazee wa baraza wa mahakama hiyo kesho wanatarajia kutoa muhtasari wa kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayedaiwa kumuua msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Jaji Sam Rumanyika amesema kuwa muhtasari huo utasaidia wazee wa baraza kupitia shauri hilo na kuamua kama Lulu anahatia ama la. Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wao kwa Stafu Sajenti, E 103  Nyagea (53) kusoma maelezo ya ushahidi ya Josephine Mushumbus ambayo aliyarekodi.

Maelezo hayo yalisomwa baada ya wakili wa utetezi, Peter Kibatala kumueleza Jaji Rumanyika kuwa wanaomba askari huyo ayasome maelezo ya Mshumbus ambaye ni shahidi wao pili kwa sababu yeye ndiye aliyemuandikia na yuko mbali hawezi kupatikana kwa urahisi. 

Akisoma maelezo hayo, amesema kuwa anamfahamu Mushumbus na ndiye aliyeandika maelezo yake ya ushahidi. Amesema kuwa katika maelezo hayo Mushumbus alijitambulisha kuwa ni Daktari, ana miaka (46) Mkazi wa Bunju National Housing na aliyaandika maelezo hayo April 23, 2012.

Akimnukuu Mushumbus, askari huyo alisoma kuwa;MShumbusi alimwambia kuwa yeye ni mmiliki ya clinic ya precious inayotoa tiba mbadala iliyopo katika jengo la Mawasiliano barabara ya Sam Nujoma.

Katika clinik yake alikuwa akitibu wateja wa aina mbali mbali akiwemo marehemu Steven Kanumba ambaye alimfahamu tangia Agosti mwaka 2011 alipofika katika clinic yake hiyo kwa Mara ya kwanza kwa ajili ya kutoa sumu mwilini, na kuanzia hapo akawa na mazoea ya kwenda hapo clinic kwa ajili ya huduma hiyo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images