Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 196 | 197 | (Page 198) | 199 | 200 | .... | 3278 | newer

  0 0  Airtel na UNESCO kuzindua radio jamii  Karagwe Bukoba

  ·         Mawasiliano ya radio yaboreshwa kufikia vijiji vingi zaida kulinganishwa na awali
  ·         Zaidi ya radio 8 kuzindua chini ya mradi huu

  Jumanne 16 Julai 2013 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO wanatarajia kuzindua radio jamii katika wilaya ya Karagwe mkoani Bukoba mwishoni mwa wiki hii

  Uzinduzi huo unafatia ushirikiano kati ya Airtel na UNESCO katika mradi wa kusadia jamii na kufikisha mawasiliano ya radio sehemu ambazo zina changamoto za huduma za mawasiliano ya radio

  Akiongea kuhusu uzinduzi huo ya Airtel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema  “ Mradi huu wa radio za jamii tunaufanya kwa kushirikiana na UNESCO kwa lengo la kuendeleza na kuboresha huduma za mawasiliano na kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani wa maeneo ya vijijini.

  Tumejipanga kufanya uzinduzi wa ushirikiano wetu na UNESCO na Radio ya FADECO Karagwe utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 19 julai 2013

  Mgeni rasmi atakuwa ni mkuu wa mkoa wa Bukoba LutenFabian Masawe , pamoja na yeye tutakuwa na viongozi mbalimbali wa serikali watakaohuduria sherehe za uzinduzi huo

  TunaamiNi kwa kupitia radio hizi jamii itabadilika na kupata elimu zitakazosaidia kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wananchi wengi wana pata habari mbalimbali zikiwemo za kibiashara, uchumi, kijamii na kisiasa.

  Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin alisema “tunayo miradi mingi ya kusaidia jamii kujikwamua na hali ngumu za uchumi, kupata elimu bora, uongozi bora , kuachana na mila potofu na mengine mengi.  kwa kupitia mradi huu wa Radio tunaoshirikiana na wenzetu wa Airtel tumeshaona matunda na mafanikio mengi mpaka sasa, lengo letu ni kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo za kuwapata wananchi habari za ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha na sehemu nyingine za nchi na Dunia.

  Akiongea kuhusu uzinduzi wa Radio jamii Karagwe Mkurugenzi wa Radio ya FADECO Bw Joseph Sekiku alisema “Mpaka sasa vifaa na mitambo ya mawasiliano ya kisasa imeshafungwa na tuko katika hatua ya majaribio ambapo tumeshuhudia ufanisi mkubwa zaidi kulinganisha na awali kwani tumeweza kutanua wigo na kufikia vijiji vingi zaidi”.

  nawashukuru sana Airtel na UNESCO kwa kutufikia na kuwawezesha kuendesha radio yetu kwa ufanisi zaidi. Radio ya FADECO ilizinduliwa toka mwaka 2007  na kuanza  kurusha matangazo yetu rasmi kwa vijiji vya karibu, changamoto tuliyokuwa nayo ni pamoja na kurusha matangazo yetu katika vijiji vilivyo mbali zaidi kutoka hapa radioni. Kwa kupitia mradi huu tumeweaza kuona mfanikio makubwa tayari, 

  “Tunagemea kuzindua rasmi ushirikiano wetu na UNESCO pamoja na Airtel siku Ijumaa hapa Karagwe. Nachukua fulsa kuwaalika wananchi wadau wa sekta za mawasiliano, viongozi mbalimbali kuhudhuria halfa hii ya uzinduzi na kusherehekea pamoja nasi mafanikio haya” aliongeza Sekiku

  Mradi wa radio jamii umeanzishwa mwaka jana 2012 radio zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi zitafaidika na mradi huu kama ilivyo katika Radio hii ya FADECO iliyopo wilaya ya Karagwe Bukoba

  0 0

  Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  imesema mpango wa utekelezaji uanzishaji wa Anwani za Makazi na Misimbo ya posta itasaidia kurahisisha mawaslimo na kuchochea maendeleo nchini.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Profesa Patrick Makungu aliwambia wanandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam mara baada  ya kufungua semina ya siku moja ya wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa wizara, juu ya kuwajengea uelewa pamoja na kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi na misimbo ya posta..
  “Jambo hili ni muhimu sana katika ulimwengu wa sasa katika kurahishsisha mawasiliano na maendeleo,” na aliongeza kusema kwa jiji la Dar es Salaam ni mhimu zaidi sababu huchangia asilimia 70 ya mapato ya kodi.
  Alisema awamu ya kwanza ya mpango huo kwa jiji la Dar es Salaam ilizinduliwa rasmi na Septemba 14, 2012 na Rais Jakaya Kikwete ambapo utekelezaji wake unahusisha serikali taasisi za serikali, taasisi zisizo za kiserikali na sekta binafsi.
  Alisema mkoa wa Dar es Salaam umeanza kutekeleza mpango huu ambapo tayari baadhi ya wizara na taasisi zimezana kutumia misimbo hiyo ya posta na wananchi wahamasike kuupokea .
  Alisema kamati tendaji kwa kushirikiana na wizara ya mawasiliano ,sayansi na tekonolojia na mamalaka ya mawasiliano Tanzania, Shirika la Posta, Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam na wadau mbalimbali wameandaa mipango ya utekelezaji katika jiji nzima.
  Mkurugenzi Maswala ya Posta Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Bi.Rehema Makubwi alisema program hiyo itasaidia huduma za posta kuimarika ambapo mwananchi atapata barua na vifurushi kwa urahisi zaidi.
  ”Pia inasaidia katika kutambua wananchi walipo, na wakati wa dharura ya majanga kama magonjwa na moto kupata huduma kwa urahisi ,” na hii ndiyo mfumo nzuri zaidi katika kukabili maswala haya.
  Aliongeza kusema pia itawawezesha wafanyabiashara kupata mikopo benki kwa urahisi kutokana anwani ya makazi na misimbo ya posta huruhisisha mawasiliano ya kuwapata.
  Naye, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Uchukuzi, Bw.Issa Nchasi alisema mpango huo katika wizara yake umefika wakati mwafaka kwani ita rahisisha na ni mwongozo wa kitaifa wa uwekezaji wa majina ya mitaa na namba za nyumba.
  “ Hii itaongeza ufanisi katika Mamlaka ya usimamimizi wa  Bandari na Maziwa (TPA) mizigo au bidha kumfikia mmiliki moja kwamoja,” bila ya kubahatisha alipo kutokana na kuwepo kwa anwani za uhakiaka.
  Mpango huo ulitekelezwa kwa majaribio katika kata nane za Manispaa ya Arusha  na Manispaa ya Dodoma kata saba na sasa unateklezwa jijini Dar es Salaam kwa kuanzia na majengo ya Serikali yote ili kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wake.

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) Tawi la Tanzania  Mhe. Mussa Zungu Azzan akifungua kikao cha Kamati tandaji pamoja na  Sekretarieti jijini Dar es Salaam leo kujadili ushiriki wa Tawi la Tanzania katika Mkutano Mkuu wa 44 wa  CPA Kanda ya Afrika utakaofanyika Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17-27 Julai, 2013. Kushoto kwake ni Mratibu wa CPA Bwana Saidi Yakubu na Kaimu Katibu wa CPA Bwana Demetrius Mgalami. Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 45 wa mwaka 2014 ambapo Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ni Mkamu wa Rais wa CPA kwa sasa atachaguliwa kuwa Rais wa CPA Kanda ya Afrika.
   Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti
   Mjumbe wa Kamati na Mbunge wa Kilindi Mhe. Beatrice Matumbo Shelukindo akichangia wakati wa mjadala. 
  Wajumbe wa CPA Tawi la Tanzania (Na Prosper Minja - Bunge)

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Profesa Patrick Makungu akifungua semina ya siku moja ya Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara zote zilizoko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwajengea uelewa pamoja na kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi na misimbo ya posta.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Profesa Patrick Makungu akipongezwa na  Mkurugenzi wa Maswala ya Posta Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Bi. Rehema Makubwi mara baada ya akifungua semina ya siku moja ya Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara zote zilizoko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwajengea uelewa pamoja na kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi na misimbo ya posta.

  0 0
 • 07/16/13--14:10: --none--


 • 0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifafanua jambo wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya China Power Investment ambaye jina lake alikupatikana.
   Balozi wa China hapa nchini Mhe. Lu Youging akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia,kulia ni Rais wa Kampuni ya China Power Investment,  Lu Qizhou

   Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba akiweka saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia, waliosimama kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa China hapa nchini Balozi Lu Youging na  Rais wa Kampuni ya China Power Investment,  Lu Qizhou
  Baadhi ya wajumbe kutoka Kampuni ya China Power Investment wakifuatilia zoezi la uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia. 
  Picha Zote na Frank Shija, MAELEZO


  0 0

   Baadhi ya watoto  yatima wakipakuliwa futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam Jumatatu jioni
  Wtoto  yatima wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam 
  Watoto  yatima wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam 
   Yatima wakipata futari Ikulu
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasabahi baadhi ya watoto  yatima walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watot yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimbeba mmoja ya watoto  yatima walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watot yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo. Picha na Freddy Maro

  0 0


  0 0

  Basi la abiria mali ya Kampuni ya Safari, lenye Nambari za Usajili T 9957 BZT likiwa limelala ubavu baada ya Dereva wake kushindwa maarifa wakati akikata kona kali, katika Kijiji cha Ngumbalu, Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.Katika ajali hiyo ni Dereva peke yake ndie alieumia na kufanikiwa kukimbizwa Hospitali kwa Matibabu
  Askari Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani akiangalia namna Basi hilo kilivyoharibika.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Watanzani ya waishio mjini Abuja, wakati alipokutana nao katika Makazi ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Nigeria, jana Julai 16, 2013 na kufanya nao mazungumzo. Makamu ameondoka leo mjini Abuja kurejea nchini Tanzania, baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa siku mbili wa Afrika uliokuwa ukijadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, Julai 15-16, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Kushoto kwake ni mkewe, Mama Asha Bilal. Picha na OMR
   Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, aliyemaliza muda wake, Siwajibu Baraka Siwajibu, akiwatambulisha baadhi ya Watanzania kwa makamu wa Rais, wakati alipofika kuzungumza nao katika Makazi ya Balozi wa Tanzania, Abuja Nigeria jana Julai 16, 2013. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal, na kutoka (Kulia) ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Fatma Rajabu. 
   Baadhi ya watanzania waishio Abuja, wakimsikiliza Makamu, Dkt. Bilal, (hayupo pichani) wakati akizungumza nao.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Fatma Rajabu, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya watanzania waishio Abuja, baada ya makamu kufanya nao mazungumzo jana.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya watanzania waishio Abuja, baada ya makamu kufanya nao mazungumzo jana.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee, Salu Salatu, ambaye ni raia wa Nigeria aliyefanya kazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria kwa muda wa Miaka 25 hadi sasa, baada ya Makamu kuzungumza na Watanzania waishio Abuja jana Julai 16, 2013. Makamu ameondoka leo mjini Abuja kurejea Tanzania baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa siku mbili wa Afrika uliokuwa ukijadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, Julai 15-16, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.

  0 0

  Fursa ingine kwa watu wote WANUNUZI NA WAUZAJI DUNIANI
  Ni website ya kisasa yenye sifa za kimataifa www.dealmoja.com Yaap ni DEAL MOJA katika wavuti hii kuna mengi waeza fanya bila GHARAMA YOYOTEdealmoja_logogg
  · TANGAZA BIASHARA YAKO KATIKA Category ya Business directory
  · UZA AU NUNUA bidhaa kupitia wavuti hii

  · KWA WALE WENYE BIASHARA AU HUDUMA ZA KUPANGISHA au KUUZA – Unaweza Tangaza kupitia wavuti hii BUREEEEEEE.

  Waweza jiuliza kwanini tunatumia lugha ya KIINGEREZA katika wavuti hii…. Sababu kubwa ni kuwa tunataka kwenda mbali … na hii itasaidia watanzania kufanya biashara na watu wote DUNIANI lugha kuu ikiwa ni KIINGEREZA.

  Ni rahisi sana unajisajili kisha unaanza kurusha bidhaa zako katika website hii ya kisasa naya uhakika kabisa.
  WAWEZA POST BIDHAA/HUDUMA
  KUPITIA SIMU YAKO.

  0 0

  Na Abdulaziz,Lindi.

  Wajumbe kutoka kata 21 za wilaya kilwa  mkoani Lindi waliounda baraza
  la katiba la wilaya nusura wazipige kufuatia mvutano kuhusu nafsi ya
  waziri mkuu kwenye serikali ya shirikisho katika katiba ijayo.

  Tukio hilo lilitokea baada ya mwenyekiti wa kundi la sita la tume prof
   Palamagamba Kabudi lilipokuwa wilayani kilwa ambapo walichangia
  kutokana na makundi yalioanishwa.

  Katika makundi hayo yalipewa hoja  kujadili ambapo kundi na moja
  lilipewa hoja ya maadili lingine mihimili ya dola pamoja na , haki za
  binadamu na  suala la uwepo wa Muungano,

  Akichangia maoni yake kwenye kundi lilokuwa likijadili suala la
  Maadili,bw Shaibu mohamedi Nginji alieleza kuwa uwepo   wa serikali ya
  shirikisho hakuna umuhimu wa kuwa na waziri mkuu kwa kuwa majukumu
  yake yatafanywa na makamu wa rais.

  “hakuna haja ya kuwa na waziri mkuu kwani kufanya hivyo ni sawa na
  kurudi kwenye  muungano wa serikali mbili,jambo ambalo aliwezi
  kukubalika kwa kuwa hakuna sababu ya kuogopa muundo wa serikali tatu
  na ndio utakuwa ukombozi wetu watu wa bara.

  Hoja hiyo ilipingwa na wajumbe wengine wa kundi liloongozwa na Haji
  Ibrahimu na kusababisha kurushiana maneno  na wajumbe wengine kususia
  mjadala  na kuwaachia wachache wakiendelea kujadili .

  Mvutano  huo ulipata ufumbuzi baada ya mwenyekiti wa kundi la sita la
  tume Prof Paramaganda Kabudi kuwataka wajumbe hao kutambua kuwa kila mjumbe aliekuwepo kwenye kikao hicho ana haki ya kuchangia mawazo yake ili mradi havunji sheria  za Nchi na kufanya hivyo ndio maana ya
  kuunda katiba ya Wananchi baada ya kutoa maoni yao

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akionyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) jinsi droo ya Airtel Yatosha inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya   promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya ashindi 7 ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.
  Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wa promosheni ya Airtel yatosha mara baada ya kuibuka mshindi katika droo ya wiki ya kwanza inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya   promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya ashindi 7 ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa ya benki hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mikopo, Andrew Lyimo, Mkuu wa Huduma za Rejareja, Raymond Mutagahywa, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale na Kaimu Mkuu wa Hazina, Ivan Tarimo.   
   Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NBC Tanzania, Andrew Lyimo (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa  jijini Dar es Salaam leo. Wengine kulia kwake ni Mkuu wa Huduma za Rejareja, Raymond Mutagahywa, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale. 
   Mkuu wa Huduma za Rejareja wa Benki ya NBC Tanzania, Raymond Mutagahywa (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa jijini Dar es Salaam leo. Wengine kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu,  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi. Mwinda Kiula Mfugale na  Kaimu Mkuu wa Hazina wa NBC, Ivan Tarimo. 
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya waandishi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo kwa Wafanyakazi Waajiriwa ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0


   Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Rorya Bi. Pendo Bernard, akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Wilayani hapo Julai 14, 2013.
  Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Bi. Faustina Vallery akitoa kuhusu maadili katika Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani hapo juzi (Julai 14, 2013).
   Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Muheza wakijadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani hapo jana (Julai 16, 2013).
   Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Njombe wakijadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wilayani hapo jana (Julai 16, 2013).
   Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Rorya katika ukumbi wa mkutano wilayani humo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili na kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo uliitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Julai 14, 2013.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei  akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDBEsther Kitoka. 
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), kutoka Wizara ya Kazi na Ajira Dk. Akwilina Kayumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa upimaji afya kwa wafanyakazi wa benki ya CRDB. Kulia ni 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akipimwa afya yake.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), kutoka Wizara ya Kazi na Ajira Dk. Akwilina Kayumba akimpima afya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.

  Zoezi la upimaji afya likiendelea.
  Baadhi ya Madkatari wa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), wakiwa katika ofisi za benki ya CRDB tayari kwa kuanza zoezi la upimaji afya za wafanyakazi wa benki hiyo.
  Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDBEsther Kitoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0

       Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, akimkabidhi zawadi yenye nembo ya Jeshi Polisi Tanzania, Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo la Darfur, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku sita hapa nchini. (Picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi Dar es salaam.)
     Naibu Kamishina wa UNAMID Dkt. Syed Kaleem Imam, kutoka nchini Sudan, jimbo la Darfur (wapili kutoka kulia), akitoa mada katika kikao cha kubadilishana uzoefu kilichowashirikisha makamishina na maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi Nchini. Kutoka kulia ni Kamishina wa utawala na fedha wa jeshi la polisi, CP Clodwig Mtweve, Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Paul Chagonja, Mkuu wa tathmini na ufuatiliaji Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Omar Rashid pamoja na Mkuu wa Utawala na rasilimali wa jeshi la Polisi (DCP)Thobias Andengenye.( Picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi Dar es salaam.)

  0 0

  Mahmoud Ahmad Arusha.
   
  Magavana kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi majirani zao wamekutana jijini hapa katika mkutano wao wa 13 pamoja na mengine kujadili mtangamano wa kuwa na sarafu moja ya bara la Afrika kwa kuanzia na kuwa na mtangamano wa sarafu za kikanda.

  Akizungumza kwenye mkutano huo Gavana wa Tanzania Beno Ndulu alisema kuwa kuna chama cha mkutano huu ujulikanao kama (CENTRAL BANK OF AFRICA SUMMIT) na kuwa mkutano huo ni wa 13 unaowakutanisha magavana na manaibu gavana kutoka kwenye wanachama wa chama hicho.

  Akazitaja nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuwa  ni nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na majirani zao nchi za congo drc,Ethiopia, Sudan, Komoro,Mauritius,na Ghana mada kuu ya mkutano huo ikiwa ni kujenga mtangamano wa sarafu ya pamoja kwa kuanzia na ukanda na baadae Afrika nzima.

  Gavana Ndulu alisema kuwa baada ya mawazo ya wakuu wa nchi wanachama wa AU kupitisha maadhimio yao ya kutaka kuwa na sarafu za pamoja hivyo wao kama wadau wa sekta ya fedha wanakutana kujadili mtangamano huo.

  “Tunajiangalia tutafikaje huko na je tumejiandaaje kufika huko hili ndio lengo la kukutana hapa leo kwani timu hii ndiyo inadhamana ya kutufikisha huko”alisema ndulu

  Mkutano huo wa siku tatu unaowashirikisha wadau wa fedha kutoka kwenye nchi za afrika  ulinza tangia juzi na kufunguliwa leo jijini hapa na Gavana Ndulu

  0 0

  IMG_0073

  Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira alipomtembelea ofisini kwake mjini Kayanga mkoani Kagera kutambulisha mradi wa Amani na Demokrasia wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani nchini Tanzania. Mradi huo utakuwa unaratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNDP.
  IMG_0085
  Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akifafanua jambo kuhusiana na mradi wa Amani kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira (wa tatu kulia) namna utakavyoendeshwa kwa wakazi wa Wilaya yake. Kushoto ni Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya Karagwe Joseph Sekiku na wa pili kulia ni Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu.
  IMG_0221
  Picha juu na chini ni Bw. Omary Hassan akikusanya maoni ya vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (KDVTC) kilichopo kitongoji cha Kayanza wilayani Karagwe mkoa wa Kagera. picha zaidi bofya hapa.


  0 0

   MAREHEMU JAJI (MSTAAFU) BUXTON DAVID CHIPETA.

  Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA anasikitika kuufahamisha umma kuwa aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SUMATRA Jaji (Mstaafu) Buxton David Chipeta amefariki dunia tarehe 16 Julai, 2013 katika Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam.

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Marehemu, Oysterbay Mtaa wa Chole/Lincon, Plot No. 580.

  Tunaomba tuungane na Familia ya Marehemu Jaji (Mstaafu) Chipeta katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya msiba huu mkubwa.

  Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu
  SUMATRA
  17 Julai, 2013.

older | 1 | .... | 196 | 197 | (Page 198) | 199 | 200 | .... | 3278 | newer