Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 197 | 198 | (Page 199) | 200 | 201 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group iliyokuwa ikijenga majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Bw. Zhang Chengwei akitia saini hati ya makabidhiano kabla ya kukabidhi majengo hayo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria (hayupo pichani).
   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi akitia saini hati ya makabidhiano ya majengo ya Law School of Tanzania wakati wa shughuli ya makabidhiano ya majengo hayo iliyofanyika jana Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam. Wanaoshuhudia ni Bw. Emmanuel Mayeji kutoka Wizara ya Katiba na Sheria (wa kwanza kulia), Mh. Jaji Gerald Ndika Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (wa pili kulia), na wa kwanza kushoto ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji kutoka Co-architecture.
   Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Bw. Zhang Chengwei akimkabidhi hati ya makabidhiano ya majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi jana Julai 16, 2013 jijini  Dar Es Salaam, baada ya ujenzi wa majengo hayo kukamilika. Anayepiga makofi katikati ni Bw. Aloyse P. Mushi Mkurugenzi Mtendaji wa Co-Architecture.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bibi Christina Sonyi akipokea funguo za majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kutoka kwa Naibu Meneja wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Bw. Zhang Chengwei iliyokuwa ikijenga majengo hayo. Makabidhiano hayo yamefanyika Julai 16,2013 jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  MANYARA 2 PICS 252Kushoto Mkurugenzi wa Event Planners na muandaaji wa shindano la Modo wa Utalii Graysson Kijo a.k.a Chinaa akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa shindano hilo Bi.Buya Ernest(19) wa pili ni Simon na Jairos kutoka kampuni ya Megatrade Investment, wadhamini wakuu wa shindano hilo kupitia kinywaji chake cha K-vant gin lililofanyika mjini Babati.
  MANYARA 2 PICS 256Kulia ni mshindi wa pili katika shindano hilo Veronica Christopher(20),Mkurugenzi wa Event Planners Graysson Kijo pamoja na Buya Ernest(19)mshindi wa shindano hilo.
  MANYARA 2 PICS 283Wafanyakazi wa Events Planner wakiwa katika pozi na mshindi Buya Ernrst atakaye wakilisha Mkoa wa Manyara.

  0 0


  MWILI  wa mwandishi mkongwe  David Michael Majebelle.  aliyefariki alfajiri ya Jumapili iliyopita unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam Julai 18

  Kwa  mujibu wa taarifa rasmi ya familia iliyotolewa leo, mwili huo utaletwa  kutoka katika hospilai ya Mwananyamala  ulikohifadhiwa kisha kupelekwa nyumbani kwake eneo la Sinza  jirani na Lion Hotel   ambapo heshima za mwisho zitatolewa majira ya saa sita mchana kisha  kulepekekwa katika kanisa katoliki la Maria Mama wa Mwokozi  lililopo Sinza na baadaye saa tisa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni.

  Marehemu Majebele alizaliwa tarehe 03/05/1941 katika kijiji cha Ibiri, Wilaya ya Tabora Vijijini, Mkoa wa Tabora, akiwa mtoto wa tatu (3) wa familia ya watoto 10 wa Mzee Michael Kanyata Majebelle na Mama Theresia Malwa Majebelle ambao wote kwa sasa ni marehemu.

  SHULE

  Alisoma shule ya Msingi ya Bukene (1950) Puge, Wilaya ya Nzega, Mkoa wa Tabora tangu mwaka 1951, Baadaye katika Shule ya Kati (Middle School) ya Sikonge, Wilaya ya Sikonge, Mkoa wa Tabora, mwaka 1954 mpaka 1957.
  Alijiunga na Tabora Boys School kwa masomo ya sekondari mwaka 1958 mpaka mwaka wa 1961.

  Marehemu alikuwa mpenzi wa mpira wa miguu na aliwahi kushiriki kwenye mashindano ya SUNLIGHT CUP enzi zake.

  KAZI
  David aliajiriwa na kampuni ya Almasi ya Williamson Diamonds Ltd ya Mwadui, Shinyanga mwaka 1962 kama Public Relations Trainee. Mwaka 1963 alipelekwa Uingereza kusomea Stashahada ya Uandishi wa Habari/Upigaji Picha za Uandishi. 

  Baada ya kuhitimu alibaki nchini humo kwenye Kampuni ya The Anglo American Corporation kupata uzoefu kable ya kurejea Mwadui kuendelea na kazi ya Afisa Uhusiano wa kampuni ya Williamson Diamonds Ltd hadi Septemba 1967 alipojiuzulu na kuajiriwa na Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East African Airways) na kituo chake cha kwanza kikiwa ni Uwanja wa Kimataifa wa Embakasi – Nairobi. Oktoba 1971 alipewa uhamisho na kupelekwa London Uingereza kuwa mwakilishi wa Shirika hilo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa HEATHROW – London.

  Julai 1974 alihamishwa kutoka Uingereza na kuletwa Tanzania kuwa Meneja Mauzo wa Kampuni Tanzu ya Shirika lililojulikana kwa jina la SIMBA AIR. Lilipovunjika Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East African Airways)’

  David Majebelle alijiunga na Shirika jipya la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) kama Meneja Mauzo. Mwaka 1978 aliacha kazi katika Shirika hilo na kujiunga na wamiliki wa magazeti ya AFRICA NEWS na baadaye NEW AFRICA mpaka mwaka wa 1990 kituo chake kikiwa Uingereza. Baada ya pale alianzisha Kampuni yake binafsi kwa jina la MEDIA ADVERTISING CO.Ltd iliyojihusisha na Uhusiano, Matangazo, Upigaji Picha ikiwemo za magazeti mbalimbali kama;

  The Financial Times of London, New Africa African Business, Profit Magazine ,The African Review  na magazeti ya hapa nyumbani
  Kadri umri wake ulivyokwenda aliandamwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu. Ilibidi apunguze kasi ya kushughulikia Kampuni hiyo mpaka alipoifunga.

  FAMILIA

  David Michael Majebelle alifunga ndoa mwaka 1975. ameacha mke na watoto wane (4), wa kiume mmoja na wa kike watatu.

  UMAUTI

  Katika miaka miwili ya mwisho wa maisha yake, marehemu amekuwa akisumbuliwa na kisukari na shinikizo la damu. Jumatano iliyopita alifanyiwa vipimo huko hospitali ya Agha Khan ambako aligundulika kuwa amepata “multiple mild strokes”. Jumamosi kuamkia Jumapili iliyopita alifariki dunia.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.

  Raha ya milele umpe ee Bwana; na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, Amina.

  0 0

   Waziri Mkuu Mizengo kayanza Pinda akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Hospital ya Wilaya ya Namtumbo
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa machinjio ya kisasa katika mji mdogo wa Namtumbo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma
   Baadhi ya Viongozi wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukata utepe
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizundua  mitambo ya kuzalisha umeme katika mji mdogo wa Namtumbo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
  -------------------------------------------------
  WAZIRI Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ameweka jiwe la msingi na kuzindua miradi miwili ya maendeleo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma  yote ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.6.

   Miradi hiyo iliyotembelewa kuwekwa jiwe la msingi  na kuzinduliwa katika siku ya tatu ya ziara ya Waziri mkuu  mkoani Ruvuma ni pamoja na hospitali ya wilaya ya Namtumbo iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 600 kwa ujenzi  uliofikiwa na itakapokamilika itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.4 huku akizindua mradi wa machinjio ya kisasa ya mji wa Namtumbo ambayo yamegharimu kiasi cha shilingili milioni 148.

  Katika hatua nyingine Waziri mkuu amewasha rasmi umeme wa jenereta katika mji huo wa Namtumbo ambao ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 800  na kuwata wananchi wilayani humo kuitumia miradi hiyo yote kujiletea maendeleo ambayo yanapaswa kuibuliwa na wao wenyewe na serikali itatoa ushirikiano mkubwa katika kuifanya wilaya ya Nmtumbo kuwa ya kisasa zaidi.

  Amesema kuwa kuwepo kwa umeme,hospitali na huduma nyingine za muhimu katika maendeleo kutawezekana kwa wananchi wenyewe kujituma katika kufanya kazi zaidi na hsa katika kilimo cha mazao mbali mbali kwa sababu ardhi ya wilaya ya Namtumbo inaruhusu kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

  Amesema kuwa maendeleo  yoyote duniani huletwa na wananchi kwa kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika maeneo yanayowazunguka hivyo amewataka wananchi wilayani Namtumbo na mkoani Ruvuma kwa ujumla kuzitumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo na serikli itaunga mkono kwa dhati jitihada zozote za wananchi katika suala zima la kujiletea maendeleo.
  Aidha amesema kuwa dhamira ya maendeleo huanza kwa mwananchi mmoja mmoja kwa kukubali kutumia fursa mbali mbali zilizopo katika eneo husika na siyo kwa kukaa na kulalamikia serikali kwa kuitaka iwaletee maendeleo bila wao kujishughulisha katika kuyatafuta maendeleo na amewataka wananchi kuitunza miradi yote ya maendeleo iliyopo kwa ajili ya manufaa yao na kizazi kijacho.

  Waziri mkuu amewataka kutambua kuwa miradi hiyo yote imetumia gharama kubwa ambazozimetokana na kodi zao pamoja na wafadhili ambao nao wanatoa kama msaada kutoka kwenye kodi za wananchi wao hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuithamini miradi hiyo kwa ajili ya maendeleo yao.

  Picha na habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com

  0 0  0 0

   Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma,Fredrick Kriel akitoa mada ya maswala ya Usalama Mgodini wakati wa Semina fupi kwa Baadhi ya Wanahabari waliofanikiwa kutembelea Mradi huo uliopo pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seluu na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Madini hayo ya Uraniuam.
  Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akionyesha moja ya mambo muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu yeyote awapo Mgodini.
  Meneja Mkuu wa Maswala ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Cornelis Van Den Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo wa Madini ya aina ya Uranium wakati wa semina fupi na baadhi ya Wanahabari walioweza kutembelea Mgodi huo leo,na kuweza kujionea na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Mgodi huo.
  Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo akielezea namna Kampuni yake inavyoweza kutoa kipaumbele katika kusaidia jamii inayouzunguka mradi huko.
  Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi huo.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda ambaye ameambatana na wanahabari hao,na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo.
  Wanahabari hao wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi huo.

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bi.Rukia Mtingwa(katikati)akiongea na baadhi ya kinamama wajasiriamali wadogowadogo wanaofanya biashara katika soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI.
  Meneja wa Vodacom Foundation kupitia mradi wa MWEI, Grace Lyon, akiwahakiki baadhi ya kinamama wajasiriamali wadogowadogo wanaofanya biashara katika soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI wakati walipokuwawakikabidhiwa fedha zao za mikopo hiyo.
  Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa( kulia) akishuhudia Karunde Mussa wa Kikundi cha uuzaji wa Mbogamboga katika Soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam, akihesabu fedha kiasi cha shilingi Lakimoja baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi,Nikufya Mbengomwanja( katikati) wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI.wakati walipokuwawakikabidhiwa fedha zao za mikopo hiyo.

  Wanawake 400 katika wilaya ya Temeke wamenufaika na mikopo isiyokuwa na riba,Hii ni katika utekelezaji wake wa azima ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kubadili maisha ya wanawake kwa kuwawezesha kukuza mitaji ya biashara na kuongeza kipato katika familia,kampuni hiyo imepanua wigo wa mpango wake wa kusaidia wanawake wanaojishughulisha na biashara ndogondogo - MWEI ambapo sasa inawafikia wanawake hata wa mijini.

  Meneja wa mpango huo uitwao MWEI Grace Lyon ameyasema hayo wakati wa zoezi la kuwapatia mikopo nafuu isiyo na riba wala dhamana wanawake wajasiriamali zaidi ya 400 wa Wilayani temeke Jijijini Dar es salaam

  Lyona emesema baada ya mpango huo kuleta mafanikio makubwa kwa wanawake wa vijijini pamoja an kuwepo kwa maombi ya kuwafikia wanawake wa mijini kampuni ya Vodacom imekubaliana na mawazo hayo na kwmaba ni Imani yake kuwa wanawake wa mijini watajiweka tayari kutumia fursa ya mikopo ya Mwei kujiinua kiuchumi.

  "Kwa zaidi ya miaka mitatu minne sasa Mwei imekuwa ikielekeza Nguvu zake vijijini ambako tayari tumewafikia wanawake wengi katika mikoa mbalimbali, sasa tumeona ni vema mafanikio yale yawafikie na wanawake wa mijini ambao nao kimsingi wanahitaji kujengewa uwezo wa kumudu maisha."Alisema Lyon.

  Kuhusu utekelezaji wa azima hiyo, Lyon amesema wameanza na Temeke lakini mipango ni kuzifikia wilaya nyengine za jiji la Dar es salaam huku akiwasihi wanawake hao kutambua kuwa hakuna kikubwa kilichooanza na kingi bali siku zote kikubwa huanza na kidogo Amesema mafanikio makubwa ambyao wanawake wa vijijini wameyapata kupitia Mwei ni matokeo ya kujituma kwao, kuamini katika kidogo kufikia kikubwa na uaminifu katika urejeshaji w amikopo hiyo jambo ambalo limesaidia kuwafikia wanawake wengi zaidi ndani ya muda mfupi.

  "Tunatambua kwua mazingira na hali ya maisha hayafanani kati ya mijini na vijijini unaweza kudhani kuwa mijini kuna changamoto nyingi za kibishara kuliko vijijini lakini nataka kuwaeleza kuwa kwa uzoefu nilionao wa kuwafikia wanawake wa vijijini kila mahali kuna changamoto zake kikubwa ni kuthamini kilicho mbele yako na kutumia ipasavyo kila fusra inayojitokeza.Aliongeza Lyon Mradi huo wa Mwei amabo hutumia teknolojia ay mpesa kuwawezesah wakopaji kufanya marajesho kwa njia ya huduma hiyo jamabo ambalo linafanya gharama za ukopaji na urejeshaji w amikopo kuwa za chini zaidi kwa mkopaji.

  Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara hao wa Temeke wameelezea kufurahishwa na mpango hao hasa katika kipengele cha kutokuwepo kwa riba katika mikopo hiyo.

  Kwa kweli tumekuwa na changamoto ya kupata mikopo lakini hata fursa za ukopeshaji zilizopo zinatukwaza na uwepo wa viwango vya juu vya riba, hapa tunapata kwa gharama nafuu na tunarudisha mkopo bila riba, tunashukuru kwa hilo."Alisema Mfanyabiashara wa Duka katika Soko hilo Tausi Mjape.

  Aidha Nuru Njovu ambaye ni mfanyabiashara wa vitunguu katika soko hilo kwa upande wake ameshauri Vodacom kuwafikia wanawake wengi zaidi kwani itawakomboa wanawake katika lindi la umasikini.

  0 0

  Huu ni Mnara wa Kumbukumbu ya Mahala alipowahi kulala Marehemu Baba wa Taifa,Hayati Mwalim Julius Nyerere wakati akiwa katika harakati za kutafuta uhuru wa nchini yetu hii mnamo mwaka 1955.Mnara huu upo katika Kijiji cha Ruhegu,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma

  0 0

   
  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mtabiri bingwa wa kwanza wa hali ya hewa na mkurugenzi mkuu wa kwanza wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bw. Urban Blass Lifigahani (Pichani). Hayati Lifiga  alizaliwa tarehe 27 Novemba 1936, kifo chake kilichotokea Jumatatu tarehe 15 Julai 2013 mchana katika hospitali ya Bosph Mbezi kwa Msuguli Dar es Salaam.

  Bwana Lifiga alikuwa mtabiri bingwa wa kwanza Tanzania na Mwaafrika wa kwanza kujiunga Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashariki iliyokuwa chini ya Jumuia ya Afrika Mashariki, ambayo kwa wakati huu makao yake makuu yalikuwa Nairobi, Kenya. Bwana Lifaga aliteuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa iliyokuwa Idara Kuu ya Hali ya Hewa, Tanzania. Alishisiriki na kushauri Serikali katika kuanzisha kwa Idara hiyo.

  Pamoja na nafasi ya Mkurugenzi Mkuu pia alichaguliwa kuwa Mjumbe wa kudumu wa Tanzania katika Kamati Kuu ya Shirika la Hali ya Hewa Dunia. Nafasi nyingine aliyeishika wakati wa uhai wake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashiriki.

  Bwana Lifiga atakubumbuka kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sayansi ya hali ya hewa nchini, Afrika na Duniani.

  Ni mmoja kati ya wanasayansi waliokuwa zao la chuo kikuu cha Makerere na alichukua shahada ya udhamili chuo kikuu cha Nairobi. Hapa nchini alipata mafuzo ya Sekondari katika shule za Kwiro Sekondari, Mahenge na Pugu Sekondari, Dar es salaam.

  Mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe 19 Julai 2013  nyumbani kwake Msakuzi.

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inajumuika na familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kuomboleza msiba huu.

  Bwana ametoa, bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe; AMENI  IMETOLEWA NA OFISI YA UHISIANO MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


  0 0

  Ankal akiwa katika sebule ya nyumba aliyokuwa akiishi Mzee Nelson Mandela Mtaa wa Vilakazi namba 8115 huko Orlando ya Magharibi, Soweto, Afrika Kusini. Hii ilikuwa Julai 18, 2010 wakati wa kuadhimisha Hepi Besdei ya miaka 92 ya kuzaliwa kwa Madiba. Leo Globu ya Jamii inaungana na wadau wote duniani kuadhimisha miaka 95 ya shujaa huyu wa Afrika anayependwa na kila mtu.
  Ikumbukwe pia kwamba leo ni siku ya Kimataifa ya Mandela kama ilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2011.
  Tunamtakia aendelee kupata nafuu na aweze kuinuka kitandani huko hospitali alikolazwa kwa mwezi mmoja sasa ili apulize mishumaa yake na kukata keki huku sisi tukimwimbia HAPPY BIRTHDA MADIBA!!!!

  0 0

  HABARI ZA KIJAMII KAMA VILE MISIBA, HARUSI, SHEREHE ZA KUZALIWA NA NYINGINE AINA HIYO HUCHAPISHWA NASI BILA MALIPO. HALI KADHALIKA HABARI NA PICHA KUTOKA SEHEMU YOYOTE ILE HUCHAPISHWA BURE. HII NI KATIKA KUHAKIKISHA TUNADUMISHA SERA YETU YA KUHUDUMIA JAMII BILA MALIPO. KAMA UTADAIWA CHOCHOTE TOKA KWA MTU YEYOTE UJUE HUO NI UTAPELI AMBAO HAUHUSIANI NA GLOBU YA JAMII.

  TUMELAZIMIKA KUTOA UJUMBE HUU KWANI  HABARI ZIMETUFIKIA KWAMBA KUNA WATU WANAPITA HUKU NA KULE WAKIJITAMBULISHA KAMA WAKALA, WAANDISHI AMA WAPIGA PICHA  WA GLOBU YA JAMII NA KUDAI CHOCHOTE KUTOKA KWA WAHUSIKA, KWAMBA PICHA NA HABARI ZAO HAZIWEZI KUTOKA ENDAO HAKUNA MALIPO. JAMBO HILO SI SAHIHI NA SIE TUMEONA HERI TULIWEKE WAZI ILI KUEPUKA USUMBUFU USIO WA LAZIMA.

  KAMA UNA HABARI, TAARIFA AMA PICHA UNAZOTAKA TUCHAPISHE USIHOFU, LETE TU KWANI HAKUNA MALIPO. NI BURE, AKIKUDAI MTU JUA NI TAPELI. NA KAMA UNA SWALI AMA UNAHITAJI MAELEZO ZAIDI TUTUMIE KUPITIA EMAIL YA:
  issamichuzi@gmail.com

  ANKAL

  0 0

  Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba LEO amesema Airtel inafanya zoezi la kuingia mtaani jijini dar es salaam na wafanyakazi wao wote wa ofisi kuu jijini Dar es salaam kwa lengo ka kuhakikisha kuwa kila mteja anafahamu jinsi ya kufaidika na huduma zao zote ikiwemo ya Airtel Yatosha ambapo mteja hujiunga kwa kupiga *149*99# Kisha kuchagua kifurushi nafuu cha SIKU WIKI AU MWEZI ili kuongea kwa gharama nafuu kwenda mtandao wowote nchini Tanzania
   Meneja Uhusioano wa Airtel jackson mmbando akibadilishana mawazo na Maafisa mauzo wa Airtel  wa mkoa wa Dar es Salaam leo wakati wafanyakazi hao wakijipanga kuingia mtaaani kukutana na wateja wao na kuwaelekeza jinsi ya kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha SHINDA NYUMBA 3
   Baadhi ya maofisa na viongozi wa Timu Airtel Yatosha  wakiendelea kupeana maelekezo jinsi ya kwenda kuingia sokoni kwenye kila mtaa jijini Dar es salaam ili kuwapa somo la AIRTEL YATOSHA shinda nyumba tatu
  maofisa na viongozi wa Timu Airtel Yatosha  wakiendelea kupeana maelekezo jinsi ya kwend a kuingia sokoni kwenye kila mtaa jijini Dar es salaam ili kuwapa somo la AIRTEL YATOSHA shinda nyumba tatu
   Mikakati na mipango ikipangwa.

  0 0  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteremka kwenye ndege GF1 alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam akitokea Nchini Nigeria alikohudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika uliojadili mbinu za kukabiliana na Ukimwi, Malaria na kifua kikuu ambapo aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa Tanzania itafikia malengo ya Umoja wa Afrika iliyojiwekea katika kukabiliana na Magonjwa hayo, mkutano huo ulimalizika jana July 17-2013 mjini Abuja Nchini Nigeria (Picha na OMR)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam akitokea Nchini Nigeria alikohudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika uliojadili mbinu za kukabiliana na Ukimwi, Malaria na kifua kikuu ambapo aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa Tanzania itafikia malengo ya Umoja wa Afrika iliyojiwekea katika kukabiliana na Magonjwa hayo, mkutano huo ulimalizika jana July 17-2013 mjini Abuja Nchini Nigeria (Picha na OMR)  0 0

   Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga,akiwaonesha wakazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam jinsi yakutumia chaji hiyo inayotumia  mionzi ya jua,zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo ,Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
   Mfanyabiashara wa Ubungo jijini Dar es Salaam Rashid Ally(katikati)akimsikiliza Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga(kulia)akimuelimisha namna ya kutumia chaji inayotumia  mionzi ya jua,Chaji hizo zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo hapa nchini,Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
   Mfanyabiashara wa Ubungo jijini Dar es Salaam Rashid Ally(katikati)akionyeshwa jinsi ya kuchaji simu na Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga(kulia)kwa kutumia chaji inayotumia  mionzi ya jua, zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo hapa nchini.Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
  ======   =========   =======

  Ikiwa ni asilimia 18.4% ya Watanzania wanaotumia nishati ya umeme, Watanzania sasa wamebadilika na kuanza kutumia njia mbadala ya vyanzo vya nishati. Takribani asilimia 90 ya Watanzania wanatumia nishati ya kuni, na asilimia 8 wakiwa wanatumia mafuta ya taa.

  Njia mbadala ya vyanzo vya nishati hapa nchini Tanzania zina adhari kubwa kwa jamii husika zikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na afya. Mfano mzuri ni matumizi ya kuni yanayochochea sana ukataji wa miti, na nishati itokanayo na petroli kama mafuta ya taa zikipelekea uchafuzi wa hali ya hewa, kitu kinachopelekea madhara kwa binadamu na mazingira kwa ujumla.

  Kwa kulizungumzia hili, inatakiwa chanzo cha nishati ambacho kitakuwa rafiki wa mazingira na rahisi kupatikana hapa nchini. Makampuni ya kitaifa na kimataifa yanatakiwa kuja na ujuzi mpya na kuweka mawazo pamoja ili kupata ubunifu ambao lengo lake siyo kutoa nishati peke yake, mbali na kupatia Watanzania walioko vijijini na mijini kipato.

  Aidha kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, mwaka huu mwezi wa 4 kwa kushirikiana na Fenix International, walizindua bunifu ambayo lengo lake siyo upatikanaji wa nishati tuu mbali na kupatia Watanzania ajira.
  Makampuni haya mawili alizindua ReadySet, chaja ambayo inatumia nishati ya jua na kuchaji simu na vifaa vingine ambavyo huwa vinachajiwa.

  Katika uzinduzi huo, ilifahamika kuwa takribani watumiaji million 600 wa mitandao ya simu hutumia trillion 16 za Kitanzania kwa mwaka kusafiri kwenda kuchaji simu zao na nishati ya umeme wa betri za magari
  Kwa uanzilishi wa chaja za Readyset, Watanzania wengi wanaoishi vijijini sasa wanaweza kutumia simu kwa ajili ya mawasiliano kuwasiliana na wawapendao bila kusafiri umbali mrefu na kutumia hela nyingi za nauli.

  Akiongea huku akionyesha kifaa hicho jijni Dar es Salaam wiki hii, meneja wa kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom, Nicholus Kizenga, alielezea kuwa Watanzania wamekuwa wakisubiria jambo hili kwa mda mrefu.
  "Chaja hizi zimezinduliwa wakati muafaka kabisa hapa nchini kwasababu zitaleta msaada mkubwa sana kwa Watanzania walio wengi kwa kuwa zitawasaidia kutunza mali kama pesa na muda," alisema Kizenga.
  Pia, Kizenga aliendelea kusema kuwa chaja hizi zimeleta suluhisho la kupunguza gharama na nishati kwakuwa zinaweza kuchaji simu kumi kwa wakati mmoja, taa za ndani, radio, na kompyuta.

  Kifaa hicho kinagharimu laki tatu na ishirini (320,000) na kinaweza kikamuingizia mtu anayefanya biashara ya kuchajisha simu shilingi 64,000 kwa mwezi. Hili litawasaidia kujiwekea takribani dola kumi za kimarekani kwa kutokutumia mafuta ya taa.

  Alihimiza Watanzania wasiogope kutumia kifaa hicho kwasababu kinaendana na mazingira ya Kitanzania na kinapopata shida kuna mafundi wa kuvitengeneza kwasababu kina warantii  Maneno Mashaka, mmoja wa watu waliokuwepo wakati wa maonyesho hayo, alisema ana matumaini kwamba kwa maendeleo haya, Tanzania inakuwa kiuchumi bila kuwa na gharama kubwa kama za kufungiwa umeme, na kuingiza mafuta yatokanayo na petroli nchini.

  "Huu ni uzinduzi mkubwa sana, na wengi wetu ambao tulikuwa hatuna umeme majumbani mwetu tumelazimika kutumia mkaa na mafuta ya taa. Haya yametuletea athari kubwa sana za kiafya. Kwa  kutumia chaja hizi tunaweza kuingiza kipato na wakati huo huo kupata nishati ya umeme,"alisema Mashaka

  0 0

   Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa kushoto akiwa na Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea  wakionyesha mkataba wa mkopo wenye thamani ya shilingi billioni 87 za kitanzania,waliosaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.
   Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa kushoto akiwa na Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea  wakionyesha mkataba wa mkopo wenye thamani ya shilingi billioni 87 za kitanzania,waliosaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.
   Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa (kushoto)akimpa mkono wa shukrani Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea baada ya  kusaini  mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dickson Maimu (wa tatu kushoto ) na Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import Korea  Yong Hwan Kim(wa pili kulia)wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo baada ya halfa ya kusaini Mkataba wa Mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhia vitambulisho vya Taifa, leo jijini Dar Es Salaam.
   Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa (wa pili kushoto),Balozi wa Korea nchini Chung Il(wa kwanza kulia),Mwenyekiti na Raisi wa Benki ya Export and Import Korea Yong Hwan Kim(wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Saada Salum(kushoto), wakiwa  katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kusaini mkataba wa mkopo wa Kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa kutoka Benki ya Export and Import Korea.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import ya Korea baada ya hafla ya kusaini iliyofanyika Wizara ya Fedha leo jijini Dar Es Salaam. 
   Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa  akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania  kwa Mwenyekiti na  Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea baada ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import ya Korea baada ya hafla ya kusaini iliyofanyika Wizara ya Fedha leo jijini Dar Es Salaam.picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo).

  0 0

  Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile, Freddie Manento akifafanua jambo katika wakati wa uzinduzi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi. kulia ni Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.
  ======  ==========

  NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki amezindua huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi.

  Katika huduma hiyo, wananchi wataweza kupata huduma zote zinazotolwa na RITA kwa kuchagua kipengele anachotaka baada ya kutuma neno RITA kwenda namba 15584 na kupokea muongozo utakaomwezesha kujua utaratibu wa kusajili kizazi au kifo kilichotokea hospitali na kwengine.

  Pia wanaweza kupata taraifa zao mbali mali kwa kutembelea tovuti ya wakala hao, www.rita.go.tz, kwa kujiunga na mtandao wa kijamii wa www.facebook.com/ritatanzania na www.twitter.com/ritatanzania.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Kairuki alisema kuwa huduma hiyo itapunguza msongamano wa wananchi kujua taarifa mbali mbali za vizazi na vifo na nyinginezo zinaztotolwa na wakala hao.

  Waziri Kairuki alisema kuwa huduma hiyo ni kwa nchi nzima na kuipongeza RITA kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Media Mobile kwa kutengeneza huduma hiyo yenye ubora wa hali ya juu.

  “Huduma hii ni muhimu sana kwa wananchi na itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu ili kupata taarifa hizo, sasa taarifa utazipata kiganjani, tena kwa kutumia simu yako ya mkononi, ni jambo la faraja na la kujivunia,” alisema Waziri Kairuki.

  Alisema kuwa Wizara yao ina mpango wa kuanzisha utaratibu ambao utaongeza kasi ya usajili wa wananchi kwa wakala hao ambapo mwananchi hataweza kupata kazi mpaka awe na cheti cha kuzaliwa. Pia hata kwa watu wanaotaka kupata leseni za biashara, kujiunga na shule na shughuli nyingine mbali mbali watalazima kuwa na cheti cha kuzaliwa.

  Afisa Mtendaji Kuu wa RITA, Phillip Saliboko alisema kuwa wameamua kujiunga digitali ili kwenda na wakati na mpango wao mkubwa ni kupanua wigo wa huduma zao kwa kaya zote.

  “Tunataka kuwa karibu zaidi na kushirikiana na umma, kwa kutumia tovuti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi kama njia ya kuwasiliana na kusambaza taarifa muhimu kwa wananchi, hii itaturahisishia hata sisi kujua ufanisi wa shughuli zetu na kukabiliana na changamoto mbali mbali,” alisema Saliboko.

  Saliboko alisema kuwa kutokana na ongezeko la watumiaji wa intaneti, mitandao ya kijamii na simu za mkononi, RITA iko tayari kwenda sambamba na mabadiliko hayo na kutoa jukwaa la mawasiliano baina yao na wananchi.

  0 0

  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha mada wakati wa mkutano maalumu wa kuangalia changamoto na hatua mbalimbali za kimaendeleo katika sekta ya TEHAMA kwa nchi zilizo katika ukanda wa Bonde la Ufa jijini Dar es Salaam jana.
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano maalumu wa kuangalia changamoto na hatua mbalimbali za kimaendeleo katika sekta ya TEHAMA kwa nchi zilizo katika ukanda wa Bonde la Ufa jijini Dar es Salaam jana. Wengine katikati ni Commissioner wa Umoja wa Afrika (AU) anayeshughulikia Miundo Mbinu na Nishati,Dkt.Elham Mahmoud Ibrahim na kushoto ni Waziri wa Habari na Technolojia ya Mawasiliano wa Uganda, Bw.John Wasasira.

  0 0
  1. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ina jukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

  1. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa dawa aina ya Diclofenac kupitia mitandao ya simu na vyombo vya habari. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

  a.      Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs”(NSAIDs). Dawa hizi hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi na maumivu ya kichwa.  

  b.      Mamlaka imesajili dawa ya Diclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika. Kwa baadhi ya wagonjwa Diclofenac inaweza kusababisha vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.
     
  c.        Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, hivi karibuni imetolewa taarifa na Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya (European Medicines Agency) kwamba watu wenye matatizo  ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.

  1. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inaendelea kufuatilia madhara yatokanayo na dawa hii kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kitaalam ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO). Aidha, tunawakumbusha watoa huduma za afya kutoa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika vituo vyote vya afya nchini.
  2. Mamlaka inasha+uri watoa huduma za afya nchini na wagonjwa kuchukua tahadhari za madhara haya hasa kwa watu wenye magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari, wenye lehemu nyingi kwenye damu na wanaovuta sigara ikiwa ni pamoja na kutumia dawa mbadala.

  1. Vilevile wananchi wanashauriwa kuepuka matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri wa kitaalam ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

  Imetolewa na:

  Mkurugenzi Mkuu
  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) – Makao Makuu
  S. L. P 77150
  Dar-es-Salaam
  Tanzania
  Simu: +255 22 2450751
  +255 22 2450512
  Barua pepe: info@tfda.or.tz
  0 0

  USAID/Tanzania Mission Director Sharon L. Cromer delivers remarks about the nutritious and economic benefits of Orange Fleshed Sweet Potatoes during the Orange Fleshed Sweet Potato Harvest held in Mikocheni on Wednesday, July 17th.
  A member of the Tanzania Agriculture Productivity Program, sponsored by USAID through the Feed the Future Initiative explains appropriate planting and harvesting techniques of the nutritious Orange Fleshed Sweet Potato.

older | 1 | .... | 197 | 198 | (Page 199) | 200 | 201 | .... | 3270 | newer