Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 195 | 196 | (Page 197) | 198 | 199 | .... | 3353 | newer

  0 0  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mfalme Mswati wa Swazland (ii) wakati walipokutana kwenye Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, ulioanza leo Julai 15, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Katikati yao ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, leo Julai 15, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, ulioanza leo Julai 15, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Picha na OMR.

  0 0


   Exhibitions during the Launch of Tanzania Business Enterpreneurs for Women (TBEW) Network  held at Mbezi Garden Hotel
  The launch of TBEW network which was officiated by the Chairwomen, Mrs Haika Lawere
  Vice chair Naomi Kaspar speaking during the event
   Book exhibition
   Domestic appliances
   Vipodozi

  0 0

  Hundreds of UNAMID Sector South HQ staff members led by Head of Office Mr. Imtiaz Hussain today attended a brief ceremony at the Pakistan Level III Hospital in Nyala to pay their final respects to the seven Tanzanian peacekeepers who were killed near Khor Abeche in an ambush by unidentified gunmen on Saturday 13 July 2013. Their bodies were flown today to Khartoum en route to Tanzania.
  Top Sector leadership led by Mr. Hussain (3rd R)

  UNAMID JSR Dr. Mohamed Ibn Chambas along with Acting Force Commander Lt. Gen. Wynjones Kisamba and Police Commissioner Ms. Hester Adriana Paneras visited the other 17 injured peacekeepers at the same Hospital yesterday.
  The Mission leadership and the UNSG Ban Ki-moon have condemned the act and called for the Government of Sudan to bring the perpetrators of the “heinous” act to justice.Meanwhile, according to press reports, Tanzanian President JakayaKikwete expressed his deep shock following the incident and he sent condolences to the Tanzania People’s Defense Forces (TPDF) and the bereaved families.

  Capt. John Kivunge, a Tanzanian Staff Officer with JOC, reads a program of the brief ceremony


  He wished quick recovery for the injured soldiers, saying: “I don’t have a lot of words to express my shock and sadness on the soldiers who died while on a very important mission of United Nations, on keeping peace in an area where thousands of people have been killed…” Mr. Kikwete said in a statement issued by the Directorate of Presidential Communications yesterday, adding; “since the fallen servicemen and women were deployed in Darfur in February this year and since Tanzania  started deploying troops in 2007, they have done a good work and the country is proud of them”. 

  A portion of  staff members at the ceremony


  The TPDF Spokesperson, Lt. Col. KapambalaMgawe, said during a press conference yesterday that a special delegation has been sent to Khartoum and Darfur to talk with the authorities over the incident. Tanzania has a battalion of about 850 peacekeepers in Darfur located at Khor Abeche and Menawashi, South Darfur State.


  Military salute as the 'Last Post'  rings out by Nigbatt in honour of the fallen heroes

  Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers

  Prayers from a chaplain

  Prayers from another  chaplain

  Maj. Elinami Moshi reads brief CVs of the deceased to the top brass

  A section of the top brass
  Last Post
  Start of the last journey home  0 0
 • 07/15/13--21:01: --none--


 • 0 0

  ISUZU JOURNEY BUS  33 SEATER FOR SALE IN EXCELLENT CONDITION IN DAR ES SALAAM!
  CALL KILAMBE: 0755723897; AHMED 0712 022929.  0 0
 • 07/15/13--22:01: --none--


 • 0 0

  Ubalozi wa Tanzania Uingereza, ukishirikiana na Urban Pulse Creative Media pamoja na Freddy Macha wanakuletea ziara fupi ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mh Jakaya Kikwete klabu ya Sunderland kujionea mwenyewe wanavyokumbatia na kuendeleza vipaji vya kucheza mpira kuanzia watoto wenye umri mdogo...

  0 0

  Na Abdulaziz Video,Lindi

  Vijana 38 wa kijiji cha Nyangao B tarafa ya Mtama ktk halmashauri ya wilaya ya Lindi, wamepongezwa kwa kwa uamuzi wao wa kujiunga na kuanzisha kikundi cha bodaboda kwa lengo la kulinda mali zao wenyewe kupitia dhana ya ulinzi shirikishi na polisi jamii.

  Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishina Msaidizi wa Polisi Renatha Mzinga kwenye hafla fupi ya kukabidhi leseni za udereva wa bodaboda na vitambulisho vya polisi jamii kwa vijana 18 iliyofanyika ktk uwanja wa kituo cha polisi kijijini hapo.

  Katika risala yao,vijana hao wamerishukuru jeshi la polisi ktk tarafa hiyo likiongozwa na Afisa wa polisi jamii wa tarafa ya Mtama Peter Msafiri kwa juhudi kubwa za kupambana na wimbi la wizi wa uvunjaji wa maduka na majumbani na kuahidi kusaidiana kulisambaratisha wimbi hilo.

  Naye mwenyekiti wa kikundi hicho cha bodaboda Ally Manjolo, ametoa wito kwa abiria wanaotumia bodaboda kuanzia sasa kukagua vitambulisho na leseni za madereva waliohitimu mafunzo ya udareva na sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizo na msingi.

  0 0

   Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe.Wilson Masilingi (kushoto) akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati alipomtembea wizarani kujifunza na kupata mwanga wa nini kinatakiwa katika kuendeleza sekta hiyo muhimu, na namna ya kuwaelewesha  wawekezaji nini wategemee watapokuja nchini kuwekeza

  Wataalam kutoka Wizara , Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA ) wakifuatilia mazungumzo kati ya  Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe.Wilson Masilingi (kushoto) akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo. Picha na Teresia X. Mhagama

  0 0

  IMG_9991
  Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu akifafanua umuhimu wa mafunzo hayo ya Ujasiriamali kwa Redio za kijamii kwa washiriki ambayo yatawajengea uwezo wa kuboresha vipindi vyao na kufanikisha kupata wadhamini ili kumudu gharama za uendeshaji wa vituo vyao. Warsha hiyo imeshirikisha radio 9 za jamii zinazotekeleza mradi wa kuziwezesha Redio hizo masuala ya TEKNOHAMA unaoratibiwa na Shirika la UNESCO chini ya udhamini wa SIDA. Warsha hii ni mwendelezo wa mafunzo ya Ujasiriamali katika Redio za jamii chini ya mradi huo.
  IMG_0061
  Mshauri Mwelekezi masuala ya utawala bora Bw. Wilbert Kitima akiendesha mafunzo kwa washiriki wa Redio Jamii yanayofanyika Kayanza, Karagwe Bukoba.
  IMG_0017
  Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki kutoka Redio za jamii 9 ambazo zinazotekeleza mradi wa SIDA unaoratibiwa na Shirika la UNESCO nchini wakichangia mawazo yao namna ya kutengeneza mpango mkakati wa biashara kwa ajili ya kumudu gharama za uendeshaji wa Redio zao.
  IMG_0069
  IMG_0065
  Washiriki wakiendelea kupata mafunzo.

  0 0

  http://4.bp.blogspot.com/-DVJryjhDUnw/UPV2ZHgHQwI/AAAAAAAACtQ/EprgmxP-Q84/s640/DSC_0430.JPG
   Hivi ndivyo hali halisi huwa wakati wa maska barabara ya Tunduru

  Na Steven Augustino, Tunduru
  SERIKALi imewataka wakazi wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kuondoa mashaka juu ya ujenzi wa Miundombinu ya Barabara ya Lami ambayo ilisimama kwa zaidi ya miezi sita ikidai kuwa ujenzi wake utaanza mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

  Kauli hiyo ya matumaini kwa Wananchi hao ilitolewa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo pinda wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha Milonde katika Ukumbi wa AULA uliopo katika taasisi ya KIUMA Wilayani humo.

  Akifafanua taarifa hiyo alisema kuwa Barabara hiyo ambayo ilikuwa chini ya mkandarasi, Kampuni ya Progresvu Co LTD Serikali ilishindwa kuendelea na mkataba wa ujenzi wake baada ya kubaini kuwa ilidanganywa na mkandarasi huyo kwa madai kuwa anao uwezo lakini hali halisi akiwa hana uwezo wa kukamirisha barabara hiyo kwa wakati.

  Alisema pamoja na mambo mengine hivi sasa serikali inakubaliana na ombi la wananchi wa Wilaya hiyo la kuitaka Serikali iiangalie Wilaya ya Tunduru kwa Jicho la huruma ili kuwakwamua wananchi wake ambao uchumi wao umekaliwa na kutofunguka kwa miundombinu hiyo ya barabara.

  “Tulikatisha mkataba na kampuni hiyo baada ya kubaini kuwa mkandarasi huyo aliidanganya Serikali yetu" alisema Pinda na kuongeza kuwa kwavile fedha za ujenzi wa mradi huo wa kilometa 1992 zipo serikali imejipanga upya na kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati ili kuwaondolea wananchi adha ambayo wamekuwa wakiipata kwa muda mrefu.

  Awali akisoma taarifa ya taasisi hiyo Mkurugenzi wa KIUMA Dkt. Matomora Matomora alimweleza waziri Mkuu kuwa kitendo cha kutofunguliwa kwa barabara za Tunduru / Namtumbo na Tunduru/ Mangaka kunaonekana kuwa ni kikwazo kikubwakinacho watia umasikini wananchi wanaoishio katika Wilaya hizo zilizopo maeneo ya kusini kati.

   Dkt. Matomora aliendelea kueleza kuwa kutoka na kutofunguka kwa barabara hizo Wilaya zote za Kusini kati zimekuwa zikiachwa nyuma na Wilaya zilizofunguka katika maendeleo ya Elimu,afya na kilimo ambavyo ili huduma zake ziweze kukamilika zinahitaji wataalamu na vifaa kutoka katika maeneo mengine ya nchi.

  0 0

   Mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete akizindua huduma mpya ya Benki ya Posta iitwayo TPB POPOTE mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.
  Rais Jakaya Kikwete akijaza fomu yake ya huduma hiyo mpya ya TPB POPOTE iliyozinduliwa na Benki ya Posta mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Pichani kulia ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kushto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.

   Rais Kikwete akipewa maelezo mafupi namna ya kuitumia huduma hiyo ya TPB POPOTE kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Posta.
    Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa kadi yake mpya ya huduma mpya TPB POPOTE  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki  ya Posta Bw.Moshingi ,mara baada ya huduma hiyo kuzinduliwa rasmi mapema leo .
    Mgeni rasmi,Rais Kikwete akikabidhiwa zawadi kut0ka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya .

  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe, wakati walipokutana katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe, baada ya mazungumzo yao walipokutana katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan na baadhi ya Marais wengine baada ya kufunguliwa mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.Picha na OMR .

  0 0

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenelle Mukangara kulia akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bibi Liz Lloyd alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao walijikita katika kuangalia namna ambavyo benki ya Standard Charterd Tanzania inaweza kushirikiana na Serikali kuwawezesha Vijana kukabiliana na changamoto za maisha. 
   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenelle Mukangara kulia akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bibi Liz Lloyd alipomtembelea afisini kwake leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia kuhusu benki uwezeshaji wa Vijana kupitia Standard Chartered Bank Tanzania Limited.

  0 0

  Na. James Katubuka


  Serikali kupitia Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imesaini mkataba  kwa ajili ya kuunda mfumo wa kutoa huduma za kitabibu kwa njia ya elektroniki ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora kwa wakati.


  Akisaini mkataba huo leo,Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi alisema mkataba huo utawezesha kuboresha huduma katika sekta ya afya nchini. “Mfumo huu unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika huduma za kitabibu zitolewazo na Sekta ya Afya” alifafanua Bw. Yambesi.

  Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Marina Njelekela alisema, kupitia mfumo huu huduma za kitabibu zinaweza kutolewa na Daktari Bingwa aliyepo Muhimbili kwa wagonjwa walio katika hospitali zilizo katika maeneo mengine bila ya wagonjwa hao kupewa rufaa ya kuja kupata huduma hiyo Muhimbili.


  “Mfumo huu utawawezesha madaktari kubadilishana ujuzi wa kitabibu kwa urahisi zaidi hivyo kuboresha huduma za afya nchini” alifafanua Dkt. Njelekela.


  Akizungumza kwa niaba ya Kampuni ya kutoa ushauri elekezi, Meneja  Mradi  wa Swiss Tropical and Public Health Institute Bw. Reinhold Werlein aliitaka Serikali kutoa ushirikiano ili kufanikisha matumizi ya mfumo huo.“Mshauri mwelekelezi pekee hawezi kuuwezesha mfumo huu kufanya kazi kwa ufanisi hivyo ametoa wito kwa Serikali kutoa ushirikiano wa kutosha ili mfumo huu uweze kuwa na manufaa kwa watanzania” alisisitiza Bw. Werlein.


  Uwepo wa mkataba huu kwa ajili ya kuunda mfumo wa kutoa huduma za kitabibu kwa njia ya electroniki ni mojawapo ya jitihada za Serikali katika kuboresha huduma katika sekta ya afya nchini.


  0 0

   Waziri wa Ujenzi Dr.John Magufuli (kushoto) akisikiliza maelezo ya ujenzi wa barabara kutoka  Ndundu-Somanga (km 60) mkoani Pwani jana kutoka kwa Mhandisi  Mkazi kutoka kampuni ya ESG (Mouchel Parkman )alipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi huo ambapo hadi sasa wameshalipwa  kiasi cha shilingi 59 bilioni.


   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(mwenye pama katikati)   akitoa maagizo kwa meneja wa mradi wa ujenzi pamoja na Mhandisi mkazi wa mradi huo hawapo pichani  jana alipotembelea mradi huo jana,ambapo Waziri Magufuli mna  mwenedo wa kususua wa ujenzi huo. (kushoto) Ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Herbet Mrango.(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Dsm Mecky Sadick.Picha na Mwanakombo Jumaa.
   Baadhi ya shughuli za ujenzi mbalimbali za barabara zikiendelea.
   .Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akiongea na baadhi ya wanakijiji wa Malendego jana wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa mradi ya barabara ya Ndundu- Somanga(km 60).
   Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Malendego mkoani Pwani wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli  (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi

  0 0

  Pamoja na mambo aliyozungumzia waziri mkuu mstaafu aliwaasa Diaspora Marekani, kuungana mkono katika shughuli zao , kupendana na kutakiana mema. Amesema kama wananchi waishio Marekani wakipendana itakuwa rahisi zaidi kuleta maendeleo katika nchi ya Tanzania. Pia aliongelea maswala ya elimu, mchakato wa katiba unaoendelea na muelekeo wa kisiasa wa nchi nzima ya Tanzania.

  Mahojiano yake yatafuata hapo baadae.


  0 0

  Mahmoud Ahmad Arusha.

  Meya wa jiji la Arusha Afyatuka awataka wanasiasa kuwapelekea wananchi maendeleo na kuachana na kauli za kumuondoa meya huyo na malumbano yasiyo na tija kwa wakazi wa jiji hili kwani utaratibu wa kanuni na sheria zipo wazi na hazihitaji malumbano  kwani yupo kisheria.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha Meya huyo Gaudency Lyimo alikuwa akijibu swali aliloulizwa kumekuwepo na malumbano ya muda mrefu kiasi cha kupachikwa majina kuwa meya wa kichina huku wanasiasa wakijinadi kuwa ataondoka kwenye kiti hicho baada ya uchaguzi mdogo uliopita mjadala wa meya hauna tija kwa wakazi wa jiji hili.

  Meya Lyimo alisema kuwa wakati huu si wa kulumbana bali ni wakati wa kuwaletea wananchi maendeleo kwani siku hazirudi nyuma na wanaofikiri mawazo hayo wanakosea kwani kila nchi inasheria na kanuni walizojiwekea na hata halmshauri inaongozwa kwa mujibu wa sheria hivyo suala hilo lipo kisheria .

  Lyimo Akawataka wanasiasa  wanaopita kuhoji uhalali wa meya huyo  kuwa ataondoka wanandoto za mchana kwani yeye yupo kisheria na kanuni zinazoendesha halmashauri hapa nchini huku akiwataka madiwani waliochaguliwa kuweka mbele maslahi ya wakazi wa jiji hili na kuwaletea maendeleo.

  “Hapa suala si meya suala ni kuwaletea maendeleo wale waliokuchagua hapa utakuwa umetimiza majukumu yako kama diwani au mwanasiasa utakuta watu wanashindwa kuwatetea wananchi na kuanza kuilumbana hilo silo wananchi wanalihitaji bali wanahitaji maendeleo wao hawaangalii vyama bali watakudai maendeleo tu”alisema Meya.

  Malumbano hayo yalianzishwa baada ya uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye jimbo la Arusha kwa chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA)kudai kuwa muda wa meya huyo unahesabika kwani idadi yao au koramu inatosha kumuondoa meya huyo.

  Huku vyombo mbali mbali vya habari vikiripoti kuwa meya akalia kuti kavu ndipo waandishi walipoamua kumuhoji mmeya huyo kupata msimamo wake kwenye suala hilo.

older | 1 | .... | 195 | 196 | (Page 197) | 198 | 199 | .... | 3353 | newer