Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1975 | 1976 | (Page 1977) | 1978 | 1979 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Gari Maalumu la Benki ya NMB likitoa huduma za kibenki katika maonesho ya wiki ya Usalama yanayoendelea katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.
  Afisa Masoko wa Benki ya NMB tawi la Nelson mandela ,Moshi ,Martha Malisa akizungumza jambo na mteja aliyefika kutembelea Banda la NMB katika maonesho ya wiki ya Usalama yanayofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.
  Afisa Masoko wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Theodosia Manyama akichukua Tasiwra ya mmoa wa wateja aliofika katika Banda la NMB kwa ajili ya kufungua akaunti,aliyeshika kitambaa ni Afisa Masoko wa Benki hiyo Martha Malisa.
  Meneja Huduma kwa wateja tawi la Nelson Mandela Moshi ,Moses Koda akishuka kutoka kwenye gari maalumu ambalo linatoa huduma za kibenki katika maonesho ya wiki ya usalama yanayofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi. 

  Wakala wa Benki ya NMB akipokea pesa kutoka kwa mteja mara baada ya kufungua akaunti papo hapo na kupatiwa ATM kadi katika Banda la NMB wakati wa maonesho ya wiki ya Usalama katika uwanja wa Mashujaa.
  Meneja wa Benki ya NMB ,tawi la Nelson Mandela ,Moshi,Emanuel Kishosha (mwenye tai nyekundu) akiwa katika uwanja wa Mashujaa na wadau wengine kufuatilia maonesho hayo yanayofanyika kitaifa mjini Moshi.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.

  0 0


   Wachezaji wa timu ya Simba wakishangia ushindi wao walioupata dhidi ya Timu ya Njombe Mji, katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam. Simba imetoka na ushindi wa bao 4-0 wafungaji wakiwa ni Emmanuel Okwi, Mzamiru Yassin (magoli mawili) na kumalizia na Laudit Mavugo. 
  Picha zote na Othman Michuzi.
   Beki wa Timu ya Njombe Mji, Laban Kambole akiruka kupiga mpira kwa kichwa huku mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiuzengea.
   Beki wa Simba, Juuko Murshad akimpiga chenga mshambuliaji wa timu ya Njombe Mji.  0 0

  Mbunge mteule Mhe. Janeth Masaburi


  0 0
 • 10/21/17--13:30: TANGAZO LA KUITWA KAZINI TRA


 • 0 0
  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela leo akiongea na baadhi ya viongozi wa Matawi ya Chama cha Wafanyakazi mahala pa kazi (TUGHE), TAA Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
  Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi mahala pa Kazi (TUGHE) matawi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Makao Makuu (TAA HQ) na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jana wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela (kushoto) alipokutana nao leo.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati mstari wa mbele), akinyanyua mikono juu kuashiria mshikamano daima na baadhi ya viongozi wa matawi wa chama cha wafanyakazi mahala pa kazi (TUGHE) matawi ya Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), alipokutana nao leo.

  KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela amewataka viongozi wa wafanyakazi kupitia matawi mawili ya Chama cha Wafanyakazi, TAA Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), kutenda haki kwa kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi wote bila kubagua na kuwasilisha kwa mwajiri ili yaweze kufanyiwa kazi kwa wakati.

  Bw. Mayongela ametoa kauli hiyo leo wakati viongozi wa matawi hayo walipokwenda kujitambulisha ofisi kwake TAA Makao Makuu, ambapo alisisitiza kuwa wafanyakazi wa chini ndio wenye matatizo makubwa lakini wamekuwa hawasikilizwi na kutatuliwa matatizo yao kwa wakati.

  “Ninashukuru uongozi mmekuja kuonana nami, ninahitaji ushirikiano wenu kama chama cha wafanyakazi, muwatumikie wafanyakazi kwa kutenda haki mkisikiliza matatizo ya kila mmoja na kufikisha sehemu husika na ninawaahidi kuwa nanyi bega kwa bega kutatua matatizo ya wafanyakazi kwani wao ndio wanafanya TAA iwepo, endapo wakifanya kazi bila manung’uniko

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

  JUMLA ya shilingi milioni 202 zimetolewa kwa vikundi 89 na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya mikopo ya kuwezesha vijana , wanawake na walemavu. Fedha hizo zimekabidhiwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa sherehe fupi ya uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake na kukabidhi mkopo iliyofanyika mjini Kaliua na kuhudhuria  na wabunge wa majimbo yote mawili ya Wilaya hiyo.

  Alisema mkopo huo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya viongozi wa juu ya kutaka kila Halmashauri itenge asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya uwezeshaji wa vikundi vya wanawake asilimia nne, uwezeshaji vijana asilimia nne na uwezeshaji watu wenye ulemavu asilimia mbili.

  Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alitoa wito kwa vikundi vya wanawake vilivyofanikiwa kupata fedha hizo kuzitumia katika malengo waliyoweka ili waweze kuzirejesha kwa ajili ya kuwakopesha wengine. Alisema kuwa ni vema fedha walizokopeshwa wakazitumia kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo na kisha wazirudishe  ili kije kigezo cha siku nyingine kuweza kukopesheka.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama aliwakumbusha vikundi vilivyokeshwa kutambua kuwa fedha hizo sio hisani bali ni mkopo ambao wanapaswa kuufanyia kazi ili waweze kupiga hatua na kisha waurejeshe ili vijana na wanawake wenzao nao wapate fursa ya kukopa.

  Alisema kuwa wanaimani kuwa kundi hilo likitumia vizuri mikopo hiyo jamii yote ya wilaya itakuwa na maendeleo na uchumi wa Wilaya hiyo utaimarika.
  Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua John Pima alisema kuwa wataendelea kuhakikisha kuwa kila mwezi wanatenga fedha kutokana na mapato ya ndani ili baadae wawakopeshe wanawake, vijana na walemavu kwa ajili ya kusaidia kuboresha maisha yao na jamii inayowazunguka.

  Naye Mbunge Jimbo la Ulyankulu John Kadutu alitoa wito kwa wakazi wa Wilaya ya Kaliua kuungana katika shughuli za maendeleo bila kujali tofauti za itikadi zao za vyama.
  Alisema kuwa yeye na mbunge wa Kaliua ambaye anatoka Chama cha waananchi CUF wamekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wote na kuwataka viongozi vingine waige mfano huo.

  Wakati huo huo Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imetoa pikipiki nane zenye thamani ya shilingi milioni 18.9 kwa ajili ya Maafisa Ugani wanne na Watendaji wa Kata wanne ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wakazi wa maneo yao.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Pima , pikipiki hizo zinalenga kuwaondolewa Maafisa Ugani uhaba wa usafiri ili waweze kuwahudumia vizuri wakulima na kuwasaidia ili waweze kupata mazao mengi na bora. Alisema kuwa wakati mwingine ilikuwa vigumu kwa Maafisa Ugani kuwafikia wakulima kwa sababu ya kuwa mbali na hivyo vyombo hivyo wa usafiri vitasaidia kuondoa visingizio kwa watumishi hao.

  Kuhusu watendaji wa Kata kupata usafiri huo alisema kuwa zitawasaidia kuimarisha shughuli za utawala ikiwemo kusikiliza kero na matatizo mbalimbali ya wananchi na kuwaondolea shida ya wananchi  kusafiri umbali mrefu ili kuwafuata viongozi. Akiongea wakati wa kukabidhi pikipiki hizo kwa watumishi hao Mkuu wa Mkoa wa Tabora aliwaonya kutumia vyombo hivyo kuwasaidia wananchi na sio kwa maslahi binafsia kama vile kubeba mizigo na wakati mwingine kuzigeuza bodaboda.

  Alisema kuwa atakayebainika atachukuliwa hatua kali ili ije iwe fundisho kwa wengine. Watendaji walipata pikipiki wanatoka kata za Ilege, Igwisi, Usimba na Nhwande na kwa upande wa Maafisa Ugani watoka kata za Seleli, Zugumlole, Silambo na Ukimbisiganga.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa namba maalumu ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi. Wanaoshuhudia kulia kwake ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo, Godfrey Simbeye. Kushoto kwa Mhagama ni Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Khamis Mwinyimvua.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akifurahia pamoja na viongozi wenzake mara baada ya uzinduzi huo.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 660 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.


  0 0

  Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt LUGANO WILSON, akiambatana na Timu ya Wafanyakazi wa Shirika hilo kutoka Ofisi ya Uhusiano makao makuu, Kitengo cha udhibiti wa Upotevu Mapato makao makuu na mkoa wa Arusha , na Kitengo cha Usalama pamoja na Wenyeji TANESCO arusha katika Oparesheni Maalum ya Kuwafichua wezi wa Umeme Katika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

  Kwenye Oparesheni hiyo, ambapo Ukaguzi huo umefanikisha Kuwakamata Zaidi ya Watuhumiwa 20 waliobainika Kujihusisha na Wizi wa Umeme Kwenye Wilaya hiyo ya Arumeru.
  Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO ) Dkt LUGANO WILSON, aliyevaa Shati la Pinki akisikiliza kwa umakini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mmoja wa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wakati wa Oparesheni hiyo.
  Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO ) Dkt LUGANO WILSON, aliyevaa shati la Pinki akiwa Kwenye Oparesheni ya Kuwakamata watuhumiwa wa Wizi wa Umeme katika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
  Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO ) Dkt LUGANO WILSON, aliyevaa shati la Pinki akifuatilia namna Oparesheni ya Kuwakamata watuhumiwa wa Wizi wa Umeme katika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
  Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO ) Dkt LUGANO WILSON, aliyevaa shati la Pinki akitoa maelekezo Wakati wa Oparesheni ya Kuwakamata watuhumiwa wa Wizi wa Umeme katika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Gavu (kulia) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tathimini ya ziara ya Ujumbe wa Mfalme wa Oman, Qaboos bin Said Al-Said uliozuru Zanzibar hivi karibuni. Kushoto ni Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika masuala ya Ushirkiano wa Kimataifa, Fedha na Uchumi Mohamed Abdiwawa.
  Baadhi ya Waandishi wa vyombo vya habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Gavu (kulia) akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu tathimini ya ziara ya Ujumbe wa Mfalme wa Oman, Qaboos bin Said Al-Said uliozuru Zanzibar hivi karibuni.

  Na Ismail Ngayonga, MAELEZO - ZANZIBAR

  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetoa hofu wananchi na kuwaeleza kuwa mataifa mbalimbali duniani yanaendelea kuunga mkono na kutoa ushirikiano mkubwa kwa Rais Dkt. Ali Mohamed Shein katika jitihada mbalimbali zake za kuwalelea maendeleo Wazanzibar.

  Hayo yamesemwa leo (Jumamosi Oktoba 21, 2017) Mjini Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Gavu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimni ya ziara ujumbe wa Mfalme wa Oman, Qaboos bin Said Al-Said aliyetembelea Zanzibar tarehe 22 Septemba mwaka huu.

  Gavu alisema katika kudhihirisha kuimarika kwa uhusiano na mataifa mbalimbali duniani, Serikali ya Zanzbar tayari imepokea mialiko tisa ya ziara za nje ya nchi zinazotarajiwa kufanywa na Rais Dkt. Ali Mohamed Shein na Viongozi wa Serikali kuanzia mwishoni mwa mwezi Januari 2018.

  “Serikali inaendelea kupanua wigo wa ushirikiano wa kidiplomasia na mataifa ya kigeni, hakuna haja ya wananchi kuwa na hofu, na tutaendelea kukaribisha ushirikiano na mataifa ya nchi jirani kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya wananchi wetu” alisema Gavu

  Gavu alisema tangu kuingia madarakani kwa Rais Shein, Novemba 2015 uhusiano wa Zanzibar na mataifa mbalimbali ulimwengu umekuwa ukiimarika na kueleza kuwa Kiongozi tayari amesafiri katika mataifa ya Djibout, Morroco na Commoro.

  Aidha Gavu alisema katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na nchi marafiki, nchi ya Saudi Arabia inatarajia kufungua Ofisi ndogo ya Ubalozi Zanzibar na hivyo kuwataka Wananchi wa Zanzibar kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali yao ikiwemo kudumisha amani, umoja na mshikamano.

  Akizungumzia kuhusu ziara ya Mfalme Qaboos bin Said Al-Said wa Oman aliyoifanya Zanzibar hivi karibuni, Serikali ya Zanzibar tayari imeunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya mfalme wa Oman na Rais Shein.

  Aliongeza kuwa katika ziara hiyo, Mfalme wa Oman alikubali kutoa ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wanafunzi wa wanafunzi wa Zanzibar katika masuala ya mafuta na gesi pamoja na kujenga viwanda vya kusindika samaki.

  “Tutahakikisha kuwa tunapeleka vijana wenye sifa na weledi katika masomo hayo ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inatumia vyema fursa hiyo, ambapo kwa kuanzia hivi sasa wapo wanafunzi wa masomo hayo katika nchi ya China wakipata ujuzi wa tasnia ya mafuta” alisema Gavu.

  Wakati wa ziara ya ujumbe wa Oman, Waziri Gavu alieleza kuwa katika mazungumzo ya ya ujumbe huo na Rais Shein, Mfalme Qaboos bin Said Al-Said alikubali pia kufanya matengenezo makubwa ya jengo la Beit –el Ajab pamoja na jengo la “People’s palace”, hatua inayolenga kuimarisha ukuaji wa sekta ya utalii Zanzibar.

  Kwa upande wake Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika masuaala ya Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa aliwataka Wazanzibar kuungana pamoja na kuendelea kumuunga mkono Rais Ali Mohamed Shein hususani katika jitihada zake za kuimarisha ushirikiano na mataifa ya kigeni.

  Balozi Ramia alisema katika siku za hivi karibuni kumeibuka hofu isiyo na sababu kuhusu ziara ya Mfalme Qaboos Said Al-Said na kueleza kuwa katika mazungumzo baina ya Viongozi hao wawili hakukuwa na suala la kisiasa lililojadiliwa badala yake ni masuala ya uimarishaji wa ushirikiano wa maendeleo ya wananchi.

  “Kuna minong’ono kuwa Zanzibar ilibanwa na mfalme Qaboos Said Al-Said kuhusu hali ya kisiasa, jambo hilo hakuna na badala yake Viongozi ho walijadili masuala ya ushirikiano na hatua zinazopaswa kuchuliwa ili kuharakisha maendeleo ya wananchi wa pande zote mbili”

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.


  Na Mathias Canal, Singida

  Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka amevuliwa uongozini na Wananchi Wakati wa Mkutano wa hadhara kutokana na tuhuma za kuruhusu na kuingiza wavamizi katika hifadhi ya msitu zinazomkabili huku wananchi hao wakipendekeza Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Ndg Mussa Mkumbo kuendelea Kuhudumu katika nafasi hiyo.

  Mkutano huo uliofanyika katika eneo la Ofisi ya Kijiji Cha Mtavira na kuhudhuriwa na wananchi 353 kutoka Kijiji Cha Makilawa, Mtavira na Mteva Kata ya Makilawa umepelekea pia Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mtavira Ndg Jilala Lutelemula kujiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo tuhuma za kuchukua Rushwa ili kuwaacha wafugaji waendelee kuishi na kuharibu msitu.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.

  Mara Baada ya Mwenyekiti huyo kujiuzulu katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Aliagiza kuitishwa Mkutano wa wananchi haraka iwezekanavyo ili kuchagua Mwenyekiti mpya ambapo pia ameagiza Mwenyekiti huyo kutiwa nguvuni ili kulisaidia Jeshi la polisi kubaini wahujumu wa msitu huo.

  Mhe Mtaturu pia aliliamuru Jeshi la polisi kumtafuta popote alipo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kazizi Ndg Kurwa Maduka kutokana na tuhuma zinazomkabili ikiwemo kuzuia wananchi kuhama katika msitu huo Jambo ambalo Ni kosa kisheria.

  Usiku wa kuamkia Octoba 17, 2017 Mhe Mtaturu aliongoza Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Ikungi kuwasaka na kuwakamata wavamizi wa msitu wa Minyughe wanaoendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo Makazi, kilimo na Ufugaji kinyume na Tangazo la serikali (GN) ya kuanzisha hifadhi ya msitu wa Minyughe ya Mwaka 2007.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtavira, Makilawa na Mteva wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Ofisi za serikali za kijiji cha Mtavira.

  Katika Oparesheni hiyo Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mambo mengine pia iliyobaini ukiukwaji wa taratibu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Vijiji na Vitongoji ikiwemo kuwauzia mavamizi maeneo kwa kutoa Rushwa ya fedha au Mifugo.


  0 0

   Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Pwani wakipatiwa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huateng Metalluargical Co.Ltd, Chunsheng Jiang (wa tatu kulia) kuhusiana na michoro waliyopewa kama zawadi, ikionyesha mandhari ya maeneo mbalimbali ya jiji la Beijinga pamoja na shughuli zao nchini China. Viongozi hao ni Mkurugenzi wa halmashauri Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani (kofia nyekundu), Mansouly Ally ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha, Afisa Biashara (M) Pwani Suleiman Sirindwa, Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga (koti jekundu) pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Mhina. Viongozi hao wamekuja jijini Beijing nchini China kwa ziara iliyoratibiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa (mwenye koti la njano). Malengo ya ziara hiyo ni kuja kuangalia fursa za viwanda zilizopo Beijing kwa kushirikiana na wadau wakubwa waliopo mjini humo na hatimaye fursa hizo kuzileta nyumbani nchini Tanzania kuendeleza na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kujenga uchumi wa viwanda
  Aidha baada ya kukutana leo viongozi hao pamoja na wadau wakuu wa mambo ya viwanda nchini China, kesho wanatarajia kushiriki kwa pamoja mkutano utakaohusu masula ya viwanda,utakaojumuisha wadau zaidi ya 160 kutoka maeneo mbalimbali nchini humo.


  0 0

  Barrick Gold Corporation yenye makao yake jijini Toronto, Canada, litaunda kampuni mpya (sio Acacia) kuendesha migodi yake ya Bulyanhuru, Buzwagi na North Mara nchini Tanzania.
  Katika taarifa yake juu ya makubaliano na serikali ya Tanzania yaliyofikiwa juzi jijini Dar es salaam, Shirika hilo limesema msimamo wa uwazi ulioafikiwa baina ya washirika (Tanzania na Barrick) ndio utaoainisha namna kampuni hiyo mpya itafanya shughuli zake.
  "Kwa mfano Serikali ya Tanzania itashiriki katika maamuzi yahusuyo shughuli, uwekezaji, mipango, manunuzi na masoko (ya kampuni hiyo mpya itapoanzishwa)", sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Makamu wa Rais Mwandamizi  wa Barrick Gold anayeshughulikia Shughuli za Uwekezaji na utawala Bw. Daniel Oh na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Barrick anayeshughulikia Mawasiliano Bw. Andy Lloyd.
  Taarifa imesema kampuni hiyo mpya itaajili Watanzania, itawajengea uwezo wazawa  katika ngazi zote, kuanzia uanachama wa bodi hadi shughuli zote, na kwamba itaongeza ununuzi wa bidhaa na huduma ndani ya Tanzania katika kuhakikisha faida  ya dhahabu inaifaidisha nchi.
  Taarifa hiyo imethibitisha kwamba faida ya kiuchumi kutoka katika migodi hiyo mitatu itagawanwa nusu-kwa-nusu ama 50-kwa-50 baina ya kampuni hiyo mpya na serikali ya Tanzania,  faida yake  ya kiuchumi ikitokana na mirahaba na kodi huku asilimia 16 ikibakia pale pale.
  Kupata chanzo na habari kamili BOFYA HAPA

  Makubaliano Barrick: JPM awa gumzo duniani
  *New York Times wasema ni mageuzi tupu
  *Mining Quartz: Ana msimamo usioyumba

  SIKU chache tu baada ya Rais John Pombe Magufuli kufanikisha kukamilika kwa ufanisi sehemu ya kwanza majadiliano na kampuni ya Barrick Gold kuhusu biashara ya madini hayo nchini, majarida na magazeti mbalimbali maarufu duniani yamemzungia kwa staili tofauti.

  Katika makubaliano hayo, huku Mwenyekiti wa Barrick Gold, Prof. John Thornton, akilazimika kusafiri kwa ndege binafsi kuja mara 2 nchini Tanzania, Tanzania imefikia kile ambacho nchi chache sana duniani zimeweza kufanikisha katika kunufaika na sekta ya madini.

  Pamoja na kupewa hisa zinazofikia asilimia 16 katika migodi yote ya Barrick nchini, makubaliano hayo pia yanaruhusu Tanzania kuchukua madini yote yanayopatikana baada ya makinikia kuuzwa na itapata faida ya nusu kwa nusu na Barrick baada ya dhahabu ya kawaida kuuzwa.

  Aidha, kampuni ya Barrick itaweka ofisi zake mpya katika jiji la Mwanza Tanzania na kwamba idadi ya watanzania wanaoshiriki katika Bodi na menejimenti ya Shirika hilo itaongezeka ili kulinda maslahi ya pande zote mbili.

  Ndio maana katika makala yake iliyoitwa “Tanzania’s squeeze on mining firms seems to be working as it gets $300 million in back taxes” Jarida mashuhuri la masuala ya madini Quartz lilimueleza Rais Magufuli kama kiongozi aliyefanikiwa kuyabana makampuni makubwa kwa maslahi ya wananchi wake na hayumbishwi.

  “Rais wa Tanzania mwenye msimamo usioyumba katika madini, Dkt. John Pombe Magufuli anaongoza vita inayohakikisha kuwa makampuni makubwa yanapata haki yao lakini wananchi wa Tanzania nao wanapata faida katika sekta ya madini,” anaandika Abdi Latif Dadir mwandishi wa jarida hilo lenye makao yake makuu Marekani.

  Kwa upande wake mtandao wa habari za uchumi na biashara wa Bloomberg ulisema kuwa Rais Magufuli ni kiongozi ambaye “anaifanyia mageuzi makubwa sekta ya madini ili kuwafaidisha wananchi.”

  Mtandao huo pia umeongeza kuwa licha ya azma hiyo, Serikali ya Magufuli pia ina mikakati mipana zaidi katika “kutekeleza sera ya viwanda na miradi ya kiuchumi katika nchi ya Tanzania ambayo ni ya sita kuwa na uchumi mkubwa katika Ukanda wa Afrika Kusini mwa Sahara.”

  Gazeti mashuhuri la New York Times lilianza kwa kusema Serikali nyingi katika nchi za Afrika na Asia-kutoka Afrika Kusini hadi Indonesia zimeanzisha harakati za kuhakikisha zinafaidika zaidi na madai yao.


  Gazeti hilo limeeleza hatua mbalimbali alizozichua Rais Magufuli ikiwemo kuzuia usafirishaji wa mchango wa madini maarufu kama makinikia. “Rais wa Tanzania hata hivyo hakusema iwapo uuzaji nje wa madini hayo utaruhusiwa tena ama la,” limeripoti New York Times.
  0 0
  0 0  0 0

  Kesi ya kuuwa bila kukusudia inayomkabili, Msanii wa filamu hapa nchini, Elizabert Michael "Lulu" inaendelea kusikilizwa leo katika Mahakama kuu Dar es salaam, ambapo shahidi wa nne atatoa ushahidi wake Mahakamani hapo. Pichani ni Wakili wa Lulu, Peter Kibatala akijadiliana jambo na mteja wake aliyeambatana na wazazi wake Mahakamani hapo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo. Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Msanii mwenzake, Marehemu Steven Kanumba miaka sita iliyopita. 

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba leo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi za Muungano zilizopo Zanzibar. Katika kikao hicho kilichofanyika katika Jengo la Uhamiaji Waziri Makamba alitoa fursa ya viongozi hao kuwasilisha maoni na changamoto zinazojitokeza katika utendaji wao wa kazi na kuweka mikakati ya kukabiliana nazo.


older | 1 | .... | 1975 | 1976 | (Page 1977) | 1978 | 1979 | .... | 3348 | newer