Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

GAMBO AWATAKA WANANCHI WA MONDULI KUCHANGAMKA KUJILETEA MAENDELEO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameanza ziara ya siku mbili wilayani Monduli mkoani Arusha. Katika ziara hiyo iliyoanza tarehe 20/10 /2017, alitembelea Kata ya Moita vijiji vya Kilimatinde, Moita Bwawani na Moita Kiloriti, pamoja na kutembelea miradi mbalimbali, kuhamasisha wananchi kujiletea maendeleo na kufanya mikutano ya hadhara katika kila kijiji alichotembelea.

Gambo amehamasisha wananchi wa Kata hiyo kujiletea maendeleo yao wenyewe na akawapongeza kwa kujenga ofisi ya kata kwa nguvu zao wenyewe na akamwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli kupeleka kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kumalizia ujenzi huo na akaelekeza jengo hilo liwe limekamilika kabla ya mwezi wa kumi na mbili 2017.

"Kata hii yetu wana Moita na maendeleo yataletwa na sisi wenyewe na sio kumsubiri mzungu atuletee, katika risala yenu mmesema hapo shule ya msingi Kilimatinde kuna upungufu wa darasa moja, tutakwenda kuchanga hapahapa tujenge darasa hilo" alisema Gambo.

Katika harambee ya kuchangua ujenzi wa darasa la shule,  Gambo amewachangia wananchi hao bati 60, wanachi wawili wamechanga tofali 2000 kwa kutoa shilingi milioni 4 na chama cha mapinduzi wilaya kimetoa mifuko thelathini kuchangia ujenzi wa darasa hilo. Ziara hii imezindua darasa moja katika shule ya sekondari Moita Bwawani, darasa lililojengwa kwa mpango wa 'Lipa kwa matokeo (P4R)'.

Mkuu wa mkoa Gambo ameambatana na wataalam kutoka sekta mbalimbali ikiwemo maji,barabara na umeme ambapo kero mbalimbali za wananchi hususan maji ndio iliyoonekana kuwa changamoto katika eneo hilo lakini wataalam wakawakikishia wananchi kwamba serikali inafanyia kazi kilio chao na ndani ya muda mfupi tatizo hilo litakwisha katika sehemu kubwa.

Ziara hii inaendelea leo tarehe 21/10/2017 na Mhe Gambo anatembelea kijiji cha Kipok kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi Kipok ambapo atafanya mikutano miwili ya hadhara na kuzungumza na wanachi wa vijiji vya Kipok na Loolera.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Moita Kiloriti alipokwenda kutembelea mradi wa maji unaohudumia kata hiyo.
Mhandisi Amboka meneja wa TARURA mkoani Arusha akitoa maelezo kwa wananchi namna wakala huo wa barabara za vijijini utakavyotoa huduma katika kata hiyo kwa mwaka huu wa fedha 2017/18
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amezindua darasa moja katika shule ya sekondari Moita Bwawani,mradi huu umetekelezwa na fedha za 'Lipa kwa matokeo' P4R.

MSANII WASTARA AZINDUA FILAMU YAKE MPYA YA KIBWEBWE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MKURUGENZI wa kampuni ya uandaaji filamu ya J Films na muigizaji wa maigizo ya sanaa nchini Bongo Movie Wastara Juma amesema malengo yake ni kuuza filamu zake nje ya nchi na hio linawezekana kama watakuwa wanatengeneza filamu zenye ubora mzuri.
Akizungumza na waandishi wakati wa ufunguzi wa filamu ya KIBWEBWE inayosimamiwa na kampuni yake, Wastara amesema kuwa katika kampuni yao kuna kazi tatu zilizokuwa tayari ila kwa pamoja wakaona ni vizuri wakianza na filamu ya Kibwebwe na itaenda zaidi kimataifa.
Wastara amesema kuwa, filamu hiyo ni ya maisha halisi ya mwanamke wa ktanzania na kiafrika na inaweza kuangaliwa na mtu yoyote mwenye rika lolote pia ina mafunzo yatakayompa mtu elimu ya kimaisha.
"Ni mara yangu ya kwanza kuzindua filamu hii na matarajio yangu ni kwenda kimataifa zaidi, pia nimefurahia kuifanyia nje ya Tanzania nina imani kila mtu ataipenda kwani ni filamu nzuri, sio ndefu na haichoshi sana katika kuangalia na ikizingatia maadili kila rika lina uwezo wa kuiangalia filamu hiyo na kufurahi,"amesema Wastara.
Wastara amesema kuwa filamu hiyo pia itapelekwa katika nchi za Uingereza na Canada na itaanza kuuzwa rasmi nchini baada ya mwezi mmoja.
Mbali na uzinduzi wa filamu ya Kibwebwe, Wastara amemtambulisha msanii wake mpya anayeimba nyimbo kwenye miondoko ya Singeli na wameingia makubaliano ya kumsimamia nyimbo zake, Msanii huyo Charles Fidelis 'Chaz K' ametambulisha nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la Mtaani Kwetu akisema kuwa huo ni mwanzo kwani bado ana nyimbo nyingi na zenye ubora mzuri.

"Nimeamua kuachia nyimbo yangu hii kwa sasa nikiwa chini ya meneja wangu mpya Wastara ambaye atakuwa anasimamia kazi zangu zote, pia bado nina kazi zingine ni nzuri na zitakuja kuingia kwenye soko la ushindani hususani kwenye mziki wa miondoko ya singeli," amesema Chaz K.
Mkurugenzi wa kampuni ya J Films Wastara Juma akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa filamu ya KIbwebwe iliyo chini ya kampuni yake sambamba na kumtambulisha msanii wake mpya wa miondoko ya singeli Charles Fidelis 'Chaz K' (kushoto) 

Msanii wa miondoko ya singeli Charles Fidelis "Chaz K" akimshukuru Meneja wake Wastara Juma kwa kuamua kuamia kazi zake kwa sasa na tayari akiwa ameshatengeneza kazi mbalimbali na kuitambulisha nyimbo yake mpya inayojulikana kama mtaani kwetu.

UKAGUZI RELI YA KISASA USIKU WALETA HAMASA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezungumzia umuhimu kwa wafanyakazi wote waliopata fursa ya kujenga reli ya kisasa (SGR) kufanya kazi kwa moyo na uzalendo mkubwa ili kuandika historia katika maendeleo ya Tanzania.
Profesa Mbarawa amesema hayo alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), inayojengwa usiku na mchana kuanzia Dar es Salaam-Morogoro  yenye urefu wa KM 205 na kuzungumzia kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
“Hii ni fursa kubwa ambayo mmeipata kujenga mradi mkubwa utakaocha historia katika nchi hii hivyo fanyeni kazi kwa bidii, weledi na uzalendo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amewataka viongozi wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO), kuwa katika eneo la mradi wakati wote ili kuhakikisha mkandarasi anapata ushirikiano wa kutosha na hivyo kuwezesha mradi kukamilika kama ilivopangwa.
Aidha amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Edward Malima, kuhakikisha wanafunzi wa uhandisi wanapata nafasi ya kutosha ya kushiriki kwa vitendo katika ujenzi huo ili kuiwezesha nchi kuwa na wataalamu wa kutosha wenye uzoefu kwenye ujenzi na usimamizi wa miradi ya reli.
“Ongezeni wahandisi wanafunzi katika mradi huu, nia yetu ni kupata reli lakini pia na wataalamu wengi katika ujenzi na uendeshaji wa reli”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye  Mhandisi Edward Malima, amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kufanya ziara ya kustukiza usiku ambayo imechochea hamasa kwa wafanyakazi na mkandarasi na kuahidi  kumsimamia mkandarasi kikamilifu ili mradi huo ukamilike kwa wakati na uwiane na thamani ya fedha.
Takribani shilingi trilioni 2.8 zinatarajiwa kutumika kujenga reli ya kisasa (SGR), awamu ya kwaza kati ya Dar es Salaam na Morogoro yenye urefu wa KM 205 itakayowezesha treni ya umeme yenye kasi ya KM 160 kwa saa kupita na hivyo kuhuisha mfumo wa usafiri wa reli hapa nchini.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Yapi Merkezi Abdullah Kilic, anayejenge reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam-Morogoro  yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani. 
 Meneja Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Mhandisi Maizo Mgedzi, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, alipokagua ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga, mkoani Pwani, inayojengwa usiku na mchana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akimpongeza mwanamke anayeendesha mtambo wa kutengeneza tuta la reli ya kisasa (SGR), Bi Miriam Juma alipomkuta saa 4 za usiku akichapa kazi katika eneo la Soga, mkoani Pwani.
Muonekano wa Mitambo ya kisasa inayojenga Reli ya Kisasa (SGR), kutoka Dar es Salaam-Morogoro yenye urefu wa KM 205 eneo la Soga mkoani Pwani, inayojengwa kwa saa 24. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH MKUU WA MKOA WA MOROGORO

UJENZI WA BANDARI BAGAMOYO KUANZA HIVI KARIBUNI

NAIBU WAZIRI SHONZA AFANYA ZIARA BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)

$
0
0
 Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimsikiliza Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (wapili kushoto) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo na kukagua ukumbi wa maonyesho ya sanaa leo Jijini Dar es Salaam
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akizungumza na watendaji wa BASATA (hawapo pichani) alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiangalia moja ya batiki zinazotengenezwa na wajasiriamali wa fani za sanaa alipofanya ziara katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watendaji wa BASATA alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza. Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM



  

MPINA NA WAZIRI WA OMAN WAZUNGUMZIA MASUALA UWEKEZAJI WA VIWANDA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

$
0
0
 Waziri anayeshughlia masuala ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekutana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail na kujadili suala zima la uwekezaji wa viwanda katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi.
Katika Mazungumzo hayo Waziri Mpina amemueleza  Waziri huyo wa uwekezaji wa Oman kuwa Tanzania imekuwa ikizalisha nyama kwa kiasi cha tani 36 kwa siku na imekuwa ikifanya biashara kwa kuuza tani za nyama ambazo hazijakatwa katika nchi za falme za kiarabu ikiwemo Oman, na wakati umefika sasa kwa nchi hizi mbili kushirikiana kwa pamoja katika Sekta hii kwa Oman kuwekeza katika Viwanda vya ndani vya nyama kwa kuendeleza viwanda vilivyopo na hata kujenga Viwanda vipya, akitolea mfano ujenzi wa kiwanda cha nyama cha Ruvu ambao umefikia 51% kukamilika.
“Tunataka viwanda vyote vya nyama vya ndani vikidhi mahitaji na kuweza kuuza nyama nje ya nchi”. Alisema Mpina.
Kwa upande wake Waziri Salim Al Ismail alipoelezwa kuhusu viwango na madaraja mbali mbali ya nyama nchini na mmoja wa mtaalam kutoka wizara hiyo, alisema kuwa Oman ipo tayari kuwekeza katika sekta ya viwanda vya nyama na kuisaidia Tanzania kutafuta soko la Marekani kupitia Oman kwani nchi hiyo ya Falme za kiarabu ina cheti  na kibali kilichothibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa cha Marekani, “Tunaweza kuchukua nyama kutoka Tanzania na kuingiza Marekani bila kulipa Ushuru, tunapaswa kuwa na vyeti halali ili kuweza kupata soko katika nchi nyingine, Alisema Waziri Ismail.”
Waziri Ismail aliendelea kusema kuwa, Makampuni Binafsi kutoka Oman yapo tayari kufanya biashara katika eneo hili hivyo ni wakati wa Tanzania sasa kuonyesha utayari.
“Hizi bidhaa za nyama ni lazima zitoke kwenu sababu sisi hatuna maji wala majani ya kulisha mifugo kama ngombe, mbuzi na kondoo ambao huchinjwa kwa wingi baada ya Hijja. Alisisitiza.”
Kwa Upande wa Sekta ya Uvuvi Waziri Huyo wa Oman alisema Oman imenunua teknolojia ya kisasa ya uwekezaji katika fukwe ya Bahari kutoka Texas Marekani, Teknolojia inayojulikana kitaalam kama Shrim farming inayoruhusu uzalishaji wa chakula cha samaki wavuliwao katika maji marefu bila kuharibu mazingira.
Alisema Tenkolijia hiyo inaweza kutumika katika uwekezaji wa Fukwe ya bahari ya Hindi akitolea mfano eneo la bagamoyo kwa kuzingatia tathmini ya athari ya mazingira na ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuwasaidia wavuvi wadogo.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dkt Yohana Budeba Alisema ni furaha yake kuona wafanya biashara wa Oman wanakuja kuwekeza Tanzania au kushirikiana na wavuvi wa ndani kwani kuna samaki wengi wa kutosha kumudu viwanda vya kuchakata  na kuwezesha biashara kubwa ya samaki.
  Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, akimtembeza Mhe. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika meli ya Oman baada ya mazungumzo yalohusu sekta ya Mifugo na Uvuvi Dar es Salaam leo.
Majadiliano kati ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, na wataalam kutoka pande hizo mbili kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi. (Na Mpiga Picha Maalum.)
 Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, akimtembeza Mhe. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika meli ya Oman baada ya mazungumzo yalohusu sekta ya Mifugo na Uvuvi Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, na wataalam kutoka pande hizo mbili kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya Mifugo na Uvuvi. 

ujio wa meli ya Sultan Qaboos hapa Zanzibar haihusiani na masuala yoyote ya kisiasa - Waziri Gavu

$
0
0
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                             Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar                      
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imewaeleza wananchi wake kuwa ujio wa meli ya Sultan Qaboos hapa Zanzibar haihusiani na masuala yoyote ya kisiasa bali meli hiyo ilibeba ujumbe wa amani, kukuza ushirikiano na uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Oman.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Ussi Haji Gavu, aliyasema hayo leo huko katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi, Kikwajuni mjini Zanzibar wakati alipofanya mahojiano na waaandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vya Zanzibar na Tanzania Bara.
Katika maelezo yake, Waziri Gavu alieleza kuwa katika kipindi chote cha siku nne cha kuwepo meli hiyo hapa Zanzibar ujumbe huo ulipata nafasi ya kukutana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo masuala mengi yaliyozungumzwa yakiwemo uhusiano uliopo pamoja na mashirikiano katika kuimarisha sekta za utalii, viwanda, elimu,uwekezaji, pamoja na mafuta na gesi.
Waziri Gavu alieleza kuwa katika ziara hiyo miongoni mwa mambo waliyokubaliana kati ya Serikali ya Oman na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni pamoja na matengenezo makubwa ya jengo la Beit-el-Ajab, ukarabati mkubwa wa jengo la ‘People’s palace’, uwekezaji katika kiwanda cha kusindika samaki, uwekezaji katika kiwanda cha kutengenezea ‘juice’. 
Jengine ni kuitangaza Zanzibar kiutalii na kuanzisha safari za moja kwa moja za watalii kati ya Zanzibar na Oman kwa wageni wa Oman wanaopendelea vivutio vya Zanzibar, kutoa msaada wa kiufundi na kisheria katika sekta ya mafuta na gesi kila inapohitajika kufanya hivyo pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu katika masuala ya mafuta na gesi asilia.
Aidha, Waziri Gavu alieleza kuwa wageni hao baada ya kufanya ziara yao hiyo katika visiwa vya Unguja na Pemba walikiri kuwepo maendeleo makubwa yaliofikiwa hapa Zanzibar kwani kati ya miongoni mwa wageni hao yupo alieza liwa katika Hospitali ya Mkoani Pemba na alishangwaza ilivyo hospitali hiyo hivi sasa na jinsi alivyoiacha yeye wakati huo.
Pamoja na hayo, ujumbe huo ulisifu amani, utulivu na mshikamano uliopo kati ya wananchi wa Zanzibar pamoja na kufurahishwa na mapokezi makubwa waliyoyapata kutoka kwa wananchi pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Pia, Waziri gavu alieleza kuwa hakuna Rais duniani anayefanya kazi kwa utashi wa mtu au kikundi cha watu ama kushurutishwa na kueleza kuwa uteuzi anaoufanya Rais Dk. Shein unatokana na azma ya kutaka mabadiliko katika kuiletea nchi maendeleo na anafanya kwa kuafuata sheria, taratibu pamoja na Katiba ya Zanzibar.
Waziri Gavu alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa wananchi kwa ushirikiano, heshima na mapenzi makubwa waliyoyaonesha wakati wa hafla maalum ya kukabidhiwa na kufunguliwa ‘Masjid Jaamiu Zinjibar’ uliojengwa kwa mashirikiano na Serikali ya Oman chini ya uongozi wa Sultan Qaboos bin Said Al Said. 
Sambamba na hayo, Waziri Gavu aliongeza kuwa kutokana na nchi mbali mbali duniani kuendelea kuiunga mkono Zanzibar, Ubalozi wa Saud Arabia unatarajia kufungua Ubalozi wake Mdogo hapa Zanzibar wiki ijayo.
Nae Mshauri wa Rais katika Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Uchumi Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa akijibu baadhi ya masuali yaliyoulizwa na waandishi waliohudhiria katika maojiano hayo, alisema kuwa uvumi wa kisiasa hauzuiliki hapa Zanzibar kwani kabla ya ujio wa meli, wakati meli ipo Zanzibar na baada ya kuondoka mambo mengi yamesemwa na kuzungumzwa na hasa kwa wale wasioipendelea mema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi Ramia aliongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakubaliwa na inaendelea kuungwa mkono na nchi mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na mashirika ya Kimataifa huku Rais wa Zanzibar akiendelea kupata mialiko kutoka sehemu mbali mbali duniani ambapo tayari baadhi yake ameshazitembelea na nyengine anatarajia kuzitembelea kuanzia mwaka ujao.
Hivyo, Balozi Ramia alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya vizuri katika Nyanja za Kidiplomasia huku akisisitiza kuwa Zanzibar ina mahusiano mazuri na nchi za nje hivi sasa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi Gavu (wa pili kushoto) alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbali mbali vya Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar leo. katika mazungumzo hayo yaliyohusu zaidi ushirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Oman (kushoto) Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi Mhe.Mohamed Ramia Abdiwawa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Nd,Hassan Khatibu Hassan na Mshauri wa Rais masuala ya Kisiasa Mhe. Mohamed Haji (wa pili kulia). Picha na Ikulu.     

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 CHART 21ST OCTOBER 2017

Introducing "Sanua Walio Lala" by Gib Carter

$
0
0
Producer: Mswaki & The Wanted Mixing and Mastering by: Tris Video Shot by: Msafiri, Kwetu Studios Ngoma ni style ya ku party hivi. SAWALA inasimama kama kifupi cha maneno haya "Sanua Walio Lala" Ikimaanisha huu ni wakati wa "Kuwaamsha waliolala". "Ni mwendo wa ku Sanua Waliolala mpaka kieleweke"

"MONDULI AMKENI MAENDELEO YATALETWA NA SISI WENYEWE" - RC Gambo.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo yuko katika ziara ya siku mbili wilayani Monduli mkoani Arusha.Katika ziara ziara hiyo iliyoanza tarehe 20/10 /2017  Gambo ametembelea Kata ya Moita vijiji vya Kilimatinde, Moita Bwawani na Moita Kiloriti, pamoja na kutembelea miradi mbalimbali, kuhamasisha wananchi kujiletea maendeleo Mhe Gambo amefanya mikutano ya hadhara katika kila kijiji alichotembelea.
Mhe Gambo amehamasisha wananchi wa Kata hiyo kujiletea maendeleo yao wenyewe na akawapongeza kwa kujenga ofisi ya kata kwa nguvu zao wenyewe na akamwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli kupeleka kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kumalizia ujenzi huo na akaelekeza jengo hilo liwe limekamilika kabla ya mwezi wa kumi na mbili 2017.
"Kata hii yetu wana Moita na maendeleo yataletwa na sisi wenyewe na sio kumsubiri mzungu atuletee, katika risala yenu mmesema hapo shule ya msingi Kilimatinde  kuna upungufu wa darasa moja, tutakwenda kuchanga hapahapa tujenge darasa hilo" alisema Gambo.
Katika harambee hiyo Mhe Gambo amewachangia wananchi hao bati 60, wanachi wawili wamechanga tofali 2000 kwa kutoa shilingi milioni 4 na chama cha mapinduzi wilaya kimetoa mifuko thelathini kuchangia ujenzi wa darasa hilo.
Ziara hii imezindua darasa moja katika shule ya sekondari Moita Bwawani, darasa lililojengwa kwa mpango wa 'Lipa kwa matokeo (P4R)'.
Mkuu wa mkoa Gambo ameambatana na wataalam kutoka sekta mbalimbali ikiwemo maji,barabara na umeme ambapo kero mbalimbali za wananchi hususan maji ndio iliyoonekana kuwa changamoto katika eneo hilo lakini wataalam wakawakikishia wananchi  kwamba serikali inafanyia kazi kilio chao na ndani ya muda mfupi tatizo hilo litakwisha katika sehemu kubwa.
Ziara hii inaendelea leo tarehe 21/10/2017 na Mhe Gambo anatembelea kijiji cha Kipok kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi Kipok ambapo atafanya mikutano miwili ya hadhara na kuzungumza na wanachi wa vijiji vya Kipok na Loolera.
 Mhandisi Amboka meneja wa TARURA mkoani Arusha akitoa maelezo kwa wananchi namna wakala huo wa barabara za vijijini utakavyotoa huduma katika kata hiyo kwa mwaka huu wa fedha 2017/18
 RC Gambo akizindua darasa moja katika shule ya sekondari Moita Bwawani,mradi huu umetekelezwa na fedha za 'Lipa kwa matokeo' P4R


RC Gambo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Moita Kiloriti alipokwenda kutembelea mradi wa maji unaohudumia kata hiyo.

SIMBA , NJOMBE MJI WAENDELEA KUTOANA JASHO UWANJA WA UHURU

$
0
0
Mabeki wa Timu ya Njombe Mji pamoja na Kipa wao, wakijaribu kuuzuia mpira uliokuwa ukiekea langoni mwao baada ya kuligwa vizuri na Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na kuandika goli la kuongoza, katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara unaopigwa kwenye Dimba la Uhuru jijini Dar hivi sasa. Simba inaongoza kwa bao 3-0.
 Mshambuliaji wa Njombe Mji, Jimmy Mwaisondela akipokea mpira kwa ustadi kabisa, katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara unaopigwa kwenye Dimba la Uhuru jijini Dar hivi sasa. Simba inaongoza kwa bao 3-0


VOA Swahili: Yaliyojiri wiki hii kutoka chumba chetu cha habari

Vijana Wamuunga Mkono Rais Magufuli usimamizi wa rasilimali za Taifa

Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Mwanza (UVCCM) wampongeza Rais Magufuli

$
0
0
Baada ya Kampuni ya uchimbaji wa Madini ya African Barrick Gold Mining, kuonyesha nia njema ya kuendelea kuwekeza nchini, Umoja wa vijana wa (CCM) mkoa wa Mwanza (UVCCM), umempongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa jitihada za kusimamia rasilimali za Taifa. 
 Umoja huo umetoa tamko hilo baada ya Kampuni hiyo kuipatia Tanzania shilingi Billion 700, ikiwa ni njia ya kuthamini makubaliano yaliyohafikiwa kati ya Serikali na Kampuni hiyo, ambayo kwa sasa inajipanga kukamilisha deni lake la la zaidi ya shilingi Tririoni mia nne. 
 Viongozi wa Umoja wa vijana wa (CCM mkoa wa Mwanza (UVCCM), wakitoa tamko hilo la pongezi kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli, kwa jitihada za kusimamia rasilimali za Taifa ikiwemo madini.


Meya Mwita ashauri Vijana wasichague kazi za kufanya

$
0
0
Na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya Dar 
 MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka vijana kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya, kutegemea ajira serikalini badala yake wawe wabunifu na kuwa tayari kufanya shughuli yoyote isipokuwa ya kiuhalifu. 
 Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa leo wakati akizungumza na wanafunzi wanaohitimu elimu ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Minazini iliyopo Kata ya Vijibweni ,Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Meya Mwita ameeleza kuwa vijana wengi wanachagua kazi kwa malengo ya kusubiri ajira kutoka serikalini jambo ambalo alisema sio sawa na kwamba wanapaswa kufanya shughuli yoyote ambayo itawaingizia kipato na kuweza kuendesha maisha yao.
 “ Vijana wangu tufanyeni kazi, tuache habari za kuchagua kazi ipi unataka kuifanya, kazi ni kazi tu ilimradi inakuingizia kipato cha kuendesha maisha yako, lakini msifanye zile ambazo mnajua sio halali mana vyombo vya dola vitawashugulikia” amesema Meya Mwita. 
 Mbali na hilo, Meya Mwita amewapongeza walimu kutokana na kujitoa kwao kuwafundisha wanafunzi licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo. Amesema walimu wamekuwa na changamoto kadha wa kadha lakini bado wamekuwa wavumilivu ikiwemo kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao ambapo alitumia nafasi hiyo kuwataka wazazi, kamati za shule kutoa ushirikiano wa kutosha ili waweze kutimiza majukumu yao. 
 “ Naelewa kwamba zipo changamoto nyingi zinazo wakabili, lakini bado mnafanya kazi kwa moyo mmoja, kutokana na juhudi hizo nawapongeza sana, zile changamoto ambazo ninauwezo wakuzitatua tutashirikiana” amesema. 
 Katika hatua nyingine Meya Mwita ameahidi kuwachimbia kisima cha maji shuleni hapo ili kuondokana na changamoto ya kutumia gharama kubwa ya kununua maji jambo ambalo alielezwa wakati wa risala iliyosomwa na wanafunzi washule hilo. 
 Hata hivyo Mkuu wa shule hiyo Maria Abihudi amesema kuwa shule hiyo inachangamoto ya Umeme ambapo kwasasa upo katika jingo moja la walimu hivyo bado kusambazwa kwenye madarasa mengine ambapo Meya Mwita aliahidi kulishughulikia jambo hilo.

 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akishiriki zoezi la upandaji miti katika shuleni ya Sekondari Minazini iliyopo  Kata ya Vijibweni Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kabla ya kuanza kwa  sherehe za mahafali ya shule hiyo.
 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na walimu hawapo pichani wa shule ya Sekondari Minazini iliyopo  Kata ya Vijibweni Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali ya shule hiyo.
 Wahitimu wa kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Minazini iliyopo Kata ya Vijibweni Halmashauri ya Manspaa ya Kigamboni wakimsikiliza Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipokuwa akihutubia shuleni hapo.
 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimkabidhi cheti ya tuzo mwanafunzi anayemaliza elimu ya kidato cha nne Mwajabu Ibrahimu aliyefanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi waanzilishi wa shule ya Minazini waliojumuika pamoja kwenye mahafali hayo. Aliyevaa suti nyekundu ni Mkuu wa shule hiyo Maria Abihudi.

MCHEKI BINGWA WA DUNIA WA NDONDI WA SASA ANTHONY JOSHUA WA UINGEREZA

TAFUTENI ENEO LA KUJENGA BWAWA LA KIMATAIFA LA KUOGELEA – WAZIRI JAFO

$
0
0
 Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinonondoni Mhe. Ally Happy sambamba na uongozi wa Manispaa hiyo kutafuta eneo maalumu litakalofaa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuogelea lenye viwango vya kimataifa litakalotumika kufundishia vijana wa Kitanzania jinsi ya kuogelela. 
Mhe. Jaffo ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuangalia eneo la shule litakalofaa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuoegelea litakalofadhiliwa na chama cha kuogelea Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe alisema kwa kipindi kirefu watanzania tumekuwa tukiungaunga kwenye mashindano mengi ya kimataifa kitu ambacho kimesababisha ushindi wetu kuwa wa kusua sua kila wakati lakini sasa tunataka tuweke miundombinu katika mashule ambayo itatoa fursa ya watoto kujifunza kuogelea kuanzia ngazi za chini.
“Tuna vipaji vingi sana katik Nchi yetu lakini haviendelezwi mfano katika hili la kuogelea kule kwetu Mbeya watu wanaogelea kwenye mito na wanajua vizuri  lakini ukiwaleta kwenye mabwawa ya kimataifa wataishia kushindwa kwa sababu hawana mbinu za kitaalamu za kushiriki kwenye mchezo huo” Alisema Mhe. Makyembe.
Akipokea maombi ya kujenga bwawa la kuogelea katika shule ya msingi Osterbay Waziri wa Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amesema amepokea na kukubali ombi la kujenga bwawa la kuogelea lakini eneo la shule ya Osterbay  ni dogo halitakidhi mahitaji na viwango vya bwawa la kimataifa la kuogelea hivyo uongozi wa Manispaa utafute eneo lingine kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Aliongeza kuwa anawashkuru wafadhili kutoka Chama cha kuogelea Tanzania kwa kuamua kutoa msaada wa ujenzi wa bwawa la kuogelea ili kukuza vipaji wa watanzania wengi ambao wamekosa fursa hiyo kutokana na ukosefu wa mabwawa ya kuogelea(Swimming Pools) katika maeneo mengi.
Pia amewaomba wafadhili hao kuendeleza kutoa msaada huo Nje ya Mikoa ya Dar es Salaam na kufika mpaka Dodoma katika chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambapo pana eneo la kutosha kwa ujenzi wa bwawa la kimataifa na uhitaji ni mkubwa kwa kuwa wanafunzi wanaosoma hapo ni muhimu wakapatiwa burudani (entertainment) mbalimbali baada ya kutoka masomoni.
 Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapy, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Osterbay wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuogelea.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(aliyesimama)akizungumza wakati wa hafla ya kuangalia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la Kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla ya kuangalia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la Kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Happy (kushoto) wakati wa wa hafla ya kuangalia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la Kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(katikati) akiwa na Waziri wa habari, Sanaa na  Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe(tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Happy( nne kulia) na walimu wa shule ya Msingi Osterbay wakati wa hafla ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la kuogelea.

MICHUZI TV: SIMBA SC YAOMBA KUTUMIA UWANJA MKUU WA TAIFA MCHEZO WAKE DHIDI YA YANGA OKTOBA 28

WATU WATANO WAHOFIWA KUFA KATIKA AJALI YA HELIKOPTA ZIWA NAKURU NCHINI KENYA

$
0
0

Helikopta iliyoanguka Ziwa Nakuru mara baada ya kuruka kutoka katika hoteli jirani na ziwa hilo Jumamosi hii asubuhi imepatikana lakini habari zinasema miili ya abiria watano waliokuwamo bado haijapatikana.

Habari zinazidi kueleza kwamba helikopta hiyo ilikuwa ikielekea kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha Jubilee katika county ya Narok.
Ajali hiyo ilithibitishwa na kitengo cha Taifa cha maafa cha Kenya (NDMU). "Taarifa toka chanzo cha kuaminika ni kwamba kwa bahati mbaya helikopta binafsi imezama katika ziwa Nakuru, na inadhaniwa kwamba abiria na nahodha wake bado wangali wamenasa ndani yake.
"Juhudi za uokoaji zinaendelea na NDMU imeleta helikopta kusaidia zoezi hilo", Naibu Mkurugenzi wa NDMU Mwachi Pius amenukuliwa akisema.
Polisi bado haijatoa majina ya watu watano walikuwemo kwenye ajali hiyo hadi baada ya ndugu wao wa karibu kujulishwa.
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images