Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

MADIWANI NA WATENDAJI KATA HALMASHAURI YA HANDENI WASHUARIWA KUHAKIKISHA WANASIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO INAYOFADHILIWA NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOS)

$
0
0
Madiwani na Watendaji wa kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga,wameshauriwa kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi ya maendeleo hususani inayofadhiliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali iliyopo kwenye maeneo yao ili iweze kujengwa kwa kiwango kinachohitajika.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hamlamashuri ya wilaya ya Handeni William Makufwe kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika Oktoba 16 na kueleza kuwa kuna umuhimu wa viongozi wa Kata kuwa karibu na wafadhili wanaojenga miradi kwenye maeneo yao kwani wao ndio wasimamizi.

Makufwe alisema ofisi ya Mkurugenzi inakuwa na imani kwamba Madiwani na Watendaji wa Kata ndio wasimamizi wakuu wa miradi iliyopo kwenye kata zao hivyo ikitokea miradi haina kiwango ina maana viongozi ngazi ya Kata hawakutimiza wajibu wao.

Aliongeza Kuwa ni kweli Serikali inahitaji kufadhiliwa lakini sio kwa kujengewa miradi ambayo ipo chini ya kiwango hali inayopelekea kuharibika Kwa muda mfupi na kutokufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni akizungumza kwenye kikao cha baraza na kutoa ushauri kwa viongozi.
Diwani Kata ya Kwamgwe Mh Sharifa abebe akizungumza kwenye kikao hicho cha baraza
Wataalamu wa Halmashauri na Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza
Mwenyekiti wa Halmashauri MH Ramadhani Diliwa katikati akizungumza na wataalamu na Madiwani, kulia ni kaimu Mkurugenzi kwa Muda Fatuma Kalovya , kushoto ni Makamu mwenyekiti Mh. Abdalla Pendeza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA OPERASHENI NA MAWASILIANO YA DHARURA KWA AJILI YA KUFUATILIA MAAFA NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Maafa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jane Alfred, namna mtambo unavyosaidia kupatikana kwa taarifa za dharura kwa ajili ya kufuatilia maafa nchini, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mchabuzi wa Mifumo ya Kompyuta  Ofisi ya Waziri Mkuu, Alex Ndimbo, namna taarifa zinavyochakatwa na  kupatikana kwa taarifa za dharura kwa ajili ya kufuatilia maafa nchini, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya akieleza umuhimu wa mpango wa uendeshwaji wa kituo Cha Operasheni na Mawasiliano ya Dharura kwa ajili ya kufuatilia maafa nchini kwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kijazi akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na  Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama,jinsi Mradi wa Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali na Mabadiliko ya Tabianchi ulivyoboresha utabiri wa hali ya hewa nchini, alipotembelea mamlaka hiyo, leo tarehe 17 Oktoba, 2017, Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAJERUHI WAONGEZEKA SIMBA, SASA NI BOCCO NA MBONDE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KIKOSI cha Simba kimeanza kuandamwa na majeruhi baada ya John Bocco na Salim Mbonde kuungana na wachezaji wengine baada ya kuumia katika
mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Jumapili iliyopita  dhidi ya Mtibwa Sugar na kushindwa kuendelea mchezo baada ya kupata majeraha.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Hajji Manara amesema kuwa kwa sasa wachezaji wote wapo katika uangalizi wa daktari wa timu.

Amesema beki wa kati Salim Mbonde ambaye ni tegemeo katika safu ya ulinzi ya Simba atakuwa nje kwa wiki nne baada ya kuumia goti katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa mwishoni mwa wiki iliyopita na atakosa michezo takribani minne  ikiwemo Njombe Mji, Yanga, lakini pia anaweza akakosa mechi nyingine mbili dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

Ripoti ya madaktari inasema maumivu yake sio makubwa sana lakini anahitaji kukaa nje kwa ajili ya kutumia dawa lakini kama itakuwa vinginevyo basi tutawataarifu.


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Hajji Manara 


WANAWAKE 28 WAHITIMU KOZI YA UKOCHA TFF

$
0
0
Makocha 28 wanawake kutoka vyuo mbalimbali vya Maendeleo ya Jamii nchini leo Oktoba 17, 2017 wamehitimu kozi fupi ya ukocha katika kozi iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO). 

Kozi hiyo ya siku mbili ambayo ni ya pili kufanyika kwa makocha hao, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume - Makao Makuu ya TFF ilikuwa chini ya mkufunzi wa TFF, Raymond Gweba. 

Akizungumza kwenye ufungaji wa kozi hiyo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo amesema Serikali inafahamu kuwa inatakiwa kuwekeza kwenye soka la wanawake kuanzia upande wa vijana na ndio maana inatengeneza mazingira na sera zitakazowezesha mafanikio hayo. 

Singo amesema nchi mbalimbali wana maendeleo makubwa katika mpira wa miguu kwa wanawake na sasa wakati wa Tanzania kuwekeza katika upande huo kuanzia kwa watoto na makocha. 
Wahitimu wa kozi ya Ukocha kwa wanawake wakiwa katika picha ya pamoja Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (katikati) na viongozi wengine kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na Chama cha Soka la Wanawake Nchini (TWFA) pamoja na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO). 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (kushoto) akiwa anamsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi wakati wa ufungaji wa kozi ya wanawake iliyoendeshwa kwa muda wa siku 2, kulia ni Ulf Kjellstig na Mwenyekiti wa soka la wanawake (TWFA) Amina Karuma. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo akikabidhi cheti na vifaa vya michezo kwa moja ya washiriki wa kozi ya ukocha kwa wanawake leo Jijini Dar es Salaam, sambamba na Mwenyekiti wa Soka la wanawake (TWFA) Amina Karuma Ulf Kjellistig. 

MAHAKAMA YATOA AMRI NG’OMBE WALIOTAIFISHWA KUPIGWA MNADA NA MWANDISHI MAALUM - MWANGA

$
0
0
NG’OMBE waliotaifishwa na serikali katika wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wamatarjiwa kupigwa mnada kufuatia uamuzi wa mahakama.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, wakati alipokwenda kukagua lindo la ng’ombe hao, jana eneo la Mgagao, wilayani Mwanga, walikohifadhiwa.

“Kufuatia uamuzi wa mahakama, ng’ombe hawa watauzwa kwa njia ya mnada siku ya Ijumaa, Oktoba 20, mwaka huu, kutokana na hali za ng’ombe hawa kutokuwa nzuri”, alisema.

Aliongeza, “Tayari mahakama imeridhia ombi la serikali la kutoka kuuzwa kwa ng’mbe hawa na ishamteua dalali wa kufanya mnada huo ambaye ni Marepelanto ya mjini Moshi na kazi hii itafanywa haraka kutokana na ng’ombe wengine kuanza kufa, kama mlivyosikia tayari sita wameshakufa”.

Aidha alisema serikali itaanza operesheni maalum ya kuwakamata ng’ombe walioingizwa nchini kinyume cha sehria kuanzia Jumatatu ijayo.

“Baada ya operesheni ya hapa Kilimanjaro, nilitoa siku saba kwa Mikoa mingine kuiondoa mifugo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria kupitia Mikoa hiyo, muda huo umekwisha, Jumatatu tunaanza ingine itakayochukua siku 15 ili kuhakikisha mifugo hiyo inaondolewa yote”, alisema.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina katikati, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Aaron Mbogho, kushoto kwake katibu tawala wa wilaya ya Mwanga Bw. Yusuph Kasuka wakiangalia ng'ombe waliotaifishwa wakati wakinywa maji katika kijiji cha Mgagau wilayani Mwanga.
Waziri Mpina , Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Maria Mashingo na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Aaron Mbogho wakijadili jambo baada ya kuongea na wanahabari kuhusu amri ya mahakama ya kupiga mnada ngombe walitaifishwa na Serikali.
Ng’ombe walioamriwa na mahakama kupigwa mnada, mnada utapigwa siku ya ijumaa. 

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MELI YA MFALME WA OMAN

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia vitabu akiongozana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohammed Bin Hamad Al Rumhy kwenye maonyesho yaliopo ndani ya meli ya Mfalme wa Oman inayojulikana kwa jina la Fulk Al Salamah iliyotia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia akionyeshwa ubani na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohammed Bin Hamad Al Rumhy alipotembelea maonyesho yaliopo ndani ya meli ya Mfalme wa Oman inayojulikana kwa jina la Fulk Al Salamah iliyotia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia machapisho mbalimbali kulia ni Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohammed Bin Hamad Al Rumhy ambaye ameonoza ujumbe maalum uliokuja na  meli ya Mfalme wa Oman inayojulikana kwa jina la Fulk Al Salamah iliyotia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohammed Bin Hamad Al Rumhy pamoja na ujumbe wake mara baada ya kutembelea  meli ya Mfalme wa Oman inayojulikana kwa jina la Fulk Al Salamah iliyotia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

SIDO WATOE MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO ILI WAJIAJIRI: RC NCHIMBI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amelitaka shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) kuandaa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo mbali mbali mkoani hapa ili wakihitimu waweze kujiajiri

Dkt. Nchimbi ametoa wito huo wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo ya SIDO kwa wajasiriamali iliyofanyika kwenye viwanja vya SIDO ambapo amesema mafunzo hayo yatawajengea mazingira mazuri wahitimu kujiajiri.

Amesema Mkoa wa Singida una fursa nyingi za kujiajiri pamoja na kuwa na vijana wengi hasa walipo katika vyuo mbalimbali lakini hawawekezi katika fursa hizo kwa kutokujua au kukosa elimu ya kutosha juu ya ujasiriamali, na hata waliopo vyuoni wakihitimu wanasubiri kuajiriwa badala ya kujiajiri.

Dkt. Nchimbi amesema ili wananchi wakiwemo vijana waweze kuzitambua fursa hizo, SIDO Mkoa na wadau wengine wanapaswa kuongeza juhudi zaidi katika utoaji mafunzo ya ujasiriamali ambapo amewataka wajielekeze kwenye vyuo mbalimbali.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoa hundi ya Mkopo uliotolewa na SIDO kwa mjasiriamali Sarah Isaya kutoka Singida katika hafla fupi ya kukabidhi mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali mkoani hapa.
  Mkurugenzi Mtendaji SIDO Taifa Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji akitoa nasaha zake kwenye hafla ya utoaji wa hundi za mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali mkoani Singida uliofanyika kwenye viwanja vya SIDO mjini hapa. Wa kwanza kushoto (aliyekaa) ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi.


 Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida Shoma Kibende akitoa taarifa ya Viwanda Vidogo vidogo na ujasiriamali Mkoa wa Singida kwenye hafla ya utoaji wa hundi za mikopo kwa wajasiriamali mbalimbali. Wa kwanza kushoto (waliokaa) ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na Mkurugenzi Mtendaji SIDO Taifa Mhandisi Profesa Sylvester Mpanduji.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama ubora wa mafuta ya alizeti  na kupata maelezo ya mafuta hayo yanayosindikwa katika viwanda vya Mkoa wa Singida kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalishaji  Mafuta ya alizeti  ya  Sunshiwe Oil Mill, Salum Khalifan.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


NAIBU WAZIRI MGALU AITAKA TANESCO KUWAJIBIKA IPASAVYO KWA WATEJA

$
0
0
Na Veronica Simba - Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linawajibika ipasavyo kwa wateja wake ili kukuza imani yao kwa shirika hilo.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa shirika hilo wa Mkoa wa Dodoma, leo Oktoba 17, 2017, Naibu Waziri amebainisha kuwa mojawapo ya njia muhimu ya uwajibikaji kwa jamii ni kupitia utoaji taarifa kwa wateja kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu.

“Mathalani, kunapokuwa na katizo la umeme, wateja walioko eneo husika wanapaswa kutaarifiwa kabla ya katizo hilo ili wajipange,” alisisitiza.

Ameeleza njia nyingine ya shirika hilo kuwajibika kwa jamii, kuwa ni kushughulikia matatizo mbalimbali ya wateja wao kwa wakati na kuachana na utaratibu wa kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma (hawapo pichani), alipowatembelea kwa lengo la kujitambulisha kwao na kueleza vipaumbele vyake vya kazi.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (kushoto), akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi yake kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), wakati Naibu Waziri alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na viongozi.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyesimama) akizungumza na viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, alipotembelea Ofisi hizo leo Oktoba 17, 2017.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 17.10.2017

CHAPISHA KITABU KWA SHILINGI ELFU THEMANINI TU!

$
0
0
Je !  Wewe  ni  Mwandishi  Chipukizi  ? Una  ndoto  za  kuchapisha  kitabu chako  lakini  unashindwa  kwa  sababu  ya  kutokuwa  na  uwezo  wa  kumudu  gharama  kubwa  za  uchapishaji  ?
Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi   HII  NI  HABARI  NJEMA  SANA  KWAKO,   Mwalu  Marketing  & General  Enterprises   wanakutaarifu  kuwa,  unaweza  kuweka  wazo  lako  kwenye  kitabu  kwa    GHARAMA  YA  SHILINGI  ELFU THEMANINI  TU (TSHS.80,000/=) ZA  KITANZANIA

Kufahamu  zaidi  kuhusu  programu  hii, click :

Tunapatikana   MBEZI  BEACH  jijini  DAR  ES  SALAAM.
Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba   0787   01  69  29.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO OCTOBER 18,2017

DARAJA LA MOMBA KUFUNGUA FURSA MIKOA YA MAGHARIBI

$
0
0
Imeelezwa kuwa kukamilika kwa Daraja la Mto Momba linalounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe kutafufua fursa za kiuchumi katika mikoa ya magharibi na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo leo alipokagua ujenzi wa daraja hilo na kuwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha daraja hilo linakamilika mwezi Agosti mwakani.

“Toeni ushirikiano unaostahili kwa mkandarasi ili Daraja hili la Momba na madaraja madogo saba yanayojengwa katika barabara ya Kasansa-Kilyamatundu yenye urefu wa KM 210.38 yakamilike kwa wakati”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesisitiza nia ya Serikali ya kujenga barabara ya Kasansa-Kilyamatundu KM 210.38 na Stalike-Kilyamatundu-Mloo KM 500 kwa kiwango cha lami ili kuongeza kasi ya uzalishaji na usambazaji wa mazao ya kilimo na mifugo katika Bonde la Mto Rukwa kwenda maeneo mingine ya nchi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa tatu kushoto), wakati alipokagua daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa tatu kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa fulana nyeusi), wakati alipokagua daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Yakabidhi Hundi ya Milioni Hamsini Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda Kuchangia Ujenzi wa Vyumba Vya Walimu wa Shule za Jiji la Dar es Salaam.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayuob Mohammed Mahmoud na Mkurugenzi Masoko wa PBZ Said Ali Mwinyigogo.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonda akizungumza na kutowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo kufanikisha ujenzi wa Ofisi za Walimu wea Shule za Dar es Salaam,kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidhi.

WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA UJENZI NYUMBA ZA POLISI ARUSHA

$
0
0

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba jana Mchana ametembelea jijini Arusha na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za Polisi zinazoendelea kujengwa baada ya ajali ya moto iliyotokea mwishoni mwa mwezi Septemba ambayo ilisababisha familia za askari 13 kuunguliwa vitu mbalimbali na kukosa makazi.

Mh. Mwigulu alitumia fursa hiyo kwa kuishukuru kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ambayo inaoongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Mrisho Gambo lakini pia aliwashukuru wadau ambao wote kwa pamoja walichukua hatua za haraka za kurejesha makazi ya askari ambao walikumbwa na janga la moto huku akisisitiza kwa kusema kwamba hali ilioonyeshwa na wadau hao ni mfano mzuri wa kuigwa na mikoa mingine waone nchi inajengwa na wananchi.

Alisema kwamba suala la makazi ya askari lipo katika kipaumbele cha serikali na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonyesha kwa vitendo katika maeneo tofauti ikiwemo hapa Arusha.

Alisema Serikali ikishamaliza hilo itaendelea na utaratibu mwingine wa kujenga majengo ya kisasa ili askari wapate makazi bora huku akimuagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha awafikishie salamu askari wa Arusha kwamba, Mh. Rais yupo pamoja nao na Wizara ipo pamoja nao.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo mbali na kuendelea kuwashukuru wadau hao kwa kujitolea na kumuunga mkono Mh. Rais ambaye alionyesha njia siku hiyo hiyo usiku kabla hakujapambazuka kwa kutoa mchango wake kama Serikali, lakini pia alisema bado milango ipo wazi kwa watu wengine ambao hawakuwa na taarifa juu ya tukio hilo ili kulisaidia Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha liweze kufanikisha ujenzi wa makazi ya askari hao.

Kamanda Mkumbo aliongeza kwa kusema ujenzi wa makazi bora ya askari mkoani hapa utasaidia kuwaongezea morali zaidi wa kazi askari hao hali ambayo itazidi kuimarisha usalama na shughuli za maendeleo kusonga mbele.

Jumla ya nyumba 29 za askari katika moja ya kambi iliyoathirika na ajali ya moto zilianzwa kujengwa toka tarehe 2 mwezi huu jijini hapa na saba ambazo zipo katika ngazi ya msingi zinatarajiwa kujengwa katika kituo kidogo cha Polisi Morombo kata ya Murieti.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba akishiriki ujenzi wa nyumba za Polisi Arusha kwa kuweka tofali na saruji mara baada ya kufanya ukaguzi na kupata maelezo juu ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Naibu kamishna (DCP) Charles Mkumbo akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba juu ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba za askari Polisi walioathirika na janga la moto.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba akikaribishwa akipokelewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo mara baada ya kuwasili kambi ya Polisi iliyopo jijini hapa ambapo ujenzi wa nyumba za waathirika wa ajali ya moto unaendelea.

SERIKALI YA IRELAND YAPONGEZA TASAF KWA KUTEKELEZA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI KWA MAFANIKIO.

$
0
0

NA ESTOM SANGA- MISUNGWI

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa wa Ireland bwana Ciar`an Cannon T.D amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za jamii na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wananchi hususani wanaokabiliwa na umaskini .

Bwana Ciar`an ametoa pongezi hizo alipofanya ziara katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ambako amekutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na kupata ushuhuda wa namna walivyonufaika na Mpango huo.

Baadhi ya Wananchi wanaonufaika na huduma za TASAF wamemweleza waziri huyo kuwa tangu waorodheshwe kwenye Mpango wameboresha maisha yao kwa huku wakijengewa misingi ya kujitegemea kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi,kuboresha na makazi yao .

Aidha baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wameeleza kuwa wamepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na afya katika kaya zao baada ya kujiunga na Mfuko wa Afya Jamii kwa kutumia fedha walizozipata kutoka TASAF na hivyo kuwapungizia mzigo mkubwa wa matibabu katika kipindi cha mwaka mzima,jambo ambalo wamesema limeboresha afya zao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga akitoa maelezo kwa waziri wa Mambo ya nje wa Ireland namna shughuli za kuhawilisha fedha zinavyotekelezwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini.

 Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland akizungumza na Mkurugenzi wa TASAF,Ladislaus Mwamanga  wakati waliposhuhudia zoezi la kulipa ruzuku kwa baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini katika wilaya ya  Misungwi,mkoani Mwanza.

 Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Ciaran akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Misungwi unaotekelezwa na TASAF namna walivyonufaika na huduma za Mpango huo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela (aliyevaa kofia) akiwa na mgeni wake waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland wakiwa na baadhi ya walengwa wa TASAF wakiwa na vyeti vya bima ya afya ya jamii waliyopata baada ya kujiunga na bima hiyo kwa kutumia  sehemu ya ruzuku ya  TASAF.


INTRODUCING BAHATI BEAUTY SHOP @ CHANG'OMBE DAR ES SALAAM

$
0
0
Jipendezeshe! Mpendezeshe umpendae!
Kwa furaha kubwa twawatangazia kufunguliwa duka letu la Vipodozi!
BAHATI BEAUTY ni duka lako jipya la vipodozi vya uhakika, ORIGINAL kutoka Ulaya!
Fika ujipatie lotions, creams, nail varnish, mafuta ya mwili na nywele, lipsticks na wanja. 
Bila kusahau Perfumes Za majina makubwa, handbags, anti perspirants na deodorants za aina mbali mbali na vikorombwezo kedekede. Bei nafuu kwa ubora harusi.
Tuko Chang'ombe Mtaa wa Mganda, jijini Dar.
Ukifika Tameco ni Mtaa wa kwanza kushoto barabara ya Chang'ombe. 
Waweza kuwasiliana nasi kwa Mobile na WhattsApp +255 677 577 119.
Shukran!
Karibuni nyote! 


WAZIRI JENISTA MHAGAMA AFANYA ZIARA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Walemavu Jenista Mhagama akiambatana na Makamishna, Maafisa na Askari kuelekea Ofisi za Kituo cha Zimamoto Mkoa wa Ilala mara baada ya kuwasili Kituoni hapo kwa ajili ya kukagua Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali (DARMAERT) Jumanne tarehe 17/10/2017.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage akitoa taarifa fupi juu ya utendaji wa Jeshi hilo mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Walemavu Jenista Mhagama kuwasili Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, kwa ajili ya kukagua Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali (DARMAERT), Jumanne tarehe 17/10/2017.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akizungumza na Makamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Uongozi wa Darmaert, mara baada ya kuwasili Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, kwa ajili ya kukagua Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali (DARMAERT),  Jumanne tarehe 17/10/2017.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi La Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (kulia), akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya (aliyevaa suti), na Mratibu wa Darmaert Dkt. Christopher Mzava (kushoto), mara baada ya kuwasili Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala, kwa ajili ya kukagua Mradi wa Uboreshaji wa Taarifa za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali (DARMAERT), Jumanne tarehe 17/10/2017.

SERIKALI YALIPA MADENI YA NDANI BILIONI 190 KATIKA KIPINDI KIFUPI

$
0
0
Benny Mwaipaja, KAGERA
Serikali imelipa madeni ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi yanayofikia kiasi cha shilingi bilioni 190 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu baada ya kufanya uhakiki wa madeni halali inayodaiwa na wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali.
Hayo yamesemwa Mjini Bukoba mkoani Kagera na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Ashatu Kijaji (Mb), wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
Dokta Kijaji alisema kuwa wazabuni wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 67.2, wakandarasi wamelipwa shilingi bililioni 24.2, watoa huduma mbalimbali wamelipwa Shilingi bilioni 38, watumishi wa umma wamelipwa Shilingi bilioni 37, huku wadai wengine wakilipwa shilingi bilioni 24.
Alisema kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017, Serikali imetenga zaidi ya Shilingi trilioni 1 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali na kwamba itaendelea kulipa madeni yote yaliyohakikiwa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na badhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera alipowasili katika Ofisi hiyo ili kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera, alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa huo ambapo amewaasa kuwa waadilifu katika kazi zao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera kuhusu masuala ya kiutendaji alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Kagera, Bw. Adam Ntoga, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Kagera.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

PUBLIC NOTICE- ANNUAL ICT PROFESSIONALS CONFERENCE

$
0
0
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF WORKS, TRANSPORT AND COMMUNICATION
 INFORMATION AND COMMUNICATIONS TECHNOLOGY COMMISSION

 PUBLIC NOTICE

ANNUAL ICT PROFESSIONALS CONFERENCE, 2017 (AIPC-17)
         
1.INTRODUCTION
The Annual Conference for ICT Professionals 2017 (AIPC-17) is a platform for discussion, networking and raising awareness to ICT professionals and stakeholders on the global ICT affairs and skills needed by Tanzanians to cope with the dynamic digital economy. This year’s conference is the commencement of a series of annually held ICT Professionals Conference to be organised by the ICT Commission to discuss on topical developments in ICT especially on how to transform the dynamic growth of ICT into an opportunity for digital industrial development in Tanzania.The theme of this year’s conference is “Building the Tanzania Digital Industrial Economy”.
2.CONFERENCE TOPICAL ISSUESAIPC-17 seeks to strengthen the synergy between the Tanzanian ICT Professionals and other ICT stakeholders towards the advancement of professional competency and business development in the Tanzanian ICT Industry.  The conference will be a two days event held on 26th -27th October 2017 in Dar es Salaam at the Julius Nyerere International Conference Centre. The conference among other issues will discuss the following issues:
a.    Principals of profession accreditation in ICT: An introduction on the ICT Professionals Accreditation Framework outlining the recognition procedures and continuous skills development plan for ICT Professionals in Tanzania will be presented for discussion and adoption by participants.

b.    Trust and confidence in digital industrial economy: The conference will also examine the emerging global trends in the context of Cyber security and digital forensics and what further needs to be done to strengthen cyber security ecosystem in Tanzania and skills set needed towards achieving a truly secure and trustworthy cyberspace.
c.    Challenges and opportunities with evolving technologies: how can Internet of Things (IoT) can shape the future organizations and socio-economic development of Tanzania. The impact of IoT to individuals and businesses, and arising opportunities will be outlined. The future of Cloud and Big Data in Tanzania; the opportunities and challenges to the ICT industry, looking into Data Analytics in Cloud, Public Key Infrastructure, Artificial intelligence, and how the ICT industry can leverage open and big data will be topical discussions.

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images