Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1968 | 1969 | (Page 1970) | 1971 | 1972 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Serikali imesema ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu ambapo kwa sasa umefika zaidi ya asilimia Tisini. 

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elius Kwandikwa, mara baada ya kukagua ukarabati wa jengo la kupumzikia abiria na upanuzi wa maegesho ya ndege katika uwanja huo leo mkoani Kilimanjaro.

  "Nimeridhishwa na ukarabati unaoendelea katika uwanja huu na nafikiri mmejionea wenyewe kazi inaendelea vizuri, hivyo naamini kutokana na hali hii kazi itakamilika hivi karibuni, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

  Aidha, Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa ukarabati huo ambao pia umehusisha maboresho ya mfumo wa maji taka unalenga kuleta tija kwa mkoa huo na Taifa kwa ujumla kutokana na kuwepo ongezeko la abiria, huduma za kijamii na kibiashara.

  Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kukarabati na kujenga viwanja vya ndege nchini ili kurahisisha huduma za usafiri wa anga kwa wananchi wake lengo likiwa ni kuchochea fursa za kiuchumi ambazo zitasaidia kulipeleka Taifa katika uchumi wa kati.
  Meneja Miradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mhandisi Mathew Ndossi, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elius Kwandikwa (Mb), (Kushoto), upanuzi wa maegesho ya ndege uliofanyika uwanjani hapo.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elius Kwandikwa (Mb), akikagua maboresho ya mfumo wa majitaka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), alipofika uwanjani hapo kujionea hatua zilizofikiwa za ukarabati wa uwanja huo.
  Muonekano wa Barabara ya Sakina – Tengeru (KM 14.1), mkoani Arusha,ambayo imekamilika kwa kiwango cha lami. Kukamilika kwake kumesaidia kupunguza ajali na msongamano katika eneo hilo.
  Muonekano wa Daraja la Ndurumo lililopo katika barabara ya Sakina – Tengeru (KM 14.1), mkoani Arusha.


  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ametoa pongezi nyingi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) kwa kufanikiwa kutoa huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 100 kwa Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

  Hayo aliyasema alipokuwa akizindua Mradi mkubwa wa Maji wa Manga’na, uliopo Kata ya Uru Kaskazini, utakaohudumia zaidi ya vijiji 11 katika Manispaa ya Moshi na Wilaya ya Moshi Vijijini baada ya kupokea taarifa ya hali ya huduma ya maji katika Mji wa Moshi.

  “Nawapongeza MUWSA kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya, kwa kuwa ndio lengo la Serikali, kuwa ifikapo mwaka 2020 maeneo ya vijijini huduma ya majisafi na salama ifikie asilimia 85 na mijini asilimia 95. Nyinyi leo hii mmeshavuka lengo hilo kwa Manispaa ya Moshi, kwa kweli nimefurahishwa sana na jambo hili na mnastahili pongezi nyingi’’, alisema Mhandisi Kamwelwe.

  Waziri Kamwelwe aliendelea kusema kuwa kwa kufanikiwa lengo hilo, mamlaka hiyo sasa itaongezewa maeneo mengine zaidi, ili kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wengine wa Moshi Vijijini ambao hawajafikiwa na huduma ya maji, na kuahidi kama Waziri mwenye dhamana ya maji atawatafutia fedha kwa ajili ya kufanikisha lengo hilo.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tenki la Maji la Njari.


  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira wakifungua bomba kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Mang’ana.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amkimtua ndoo kichwani mama kutoka Kijiji cha Mang’ana, akiashiria kutimiza lengo la Serikali ‘‘kumtua mama ndoo kichwani’’ baada ya uzinduzi wa Mradi wa Mang’ana.
  Msafara wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe ukielekea kwenye Chanzo cha Maji cha Mang’ana katika uzinduzi wa Mradi wa Mang’ana.
  0 0

   Meneja wa chapa wa Vodacom Tanzania,Yvonne Maruma(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya Tsh.Milioni 1/=mchezaji bora wa mwezi septemba,Shafik Batambuze wa timu ya Singida United inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Katikati ni Afisa Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo,Ibrahim Kaude.
  Mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi Septemba wa Singida United, Shafik Batambuze akiwa ameshikilia hundi yake yenye thamani ya shilingi Milioni 1/- baada ya kukabidhiwa rasmi na wadhamini wakuu wa ligi kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi huo.

  KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC,Ambao ndiyo wadhamini wa ligi kuu Tanzania bara,Jana wamemkabidhi mchezaji bora wa ligi kwa  mwezi septemba wa Singida United,Shafik Batambuze hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 1/- kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi huo.

  Akimkabidhi hundi hiyo Meneja wa Chapa wa kampuni hiyo,Yvonne Maruma alisema kwa mjibu wa taratibu unaofanywa na kamati ya Tuzo ya VPL iliyopo chini ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Vodacom ikiwa kama mdhamini mkuu haina budi kutekeleza matakwa yote yale yaliyopo katika mkataba na kuweza kutoa kitita cha shilingi milioni 1/-kwa mchezaji bora wa kila mwezi ikiwa na lengo la kuwapa motisha wachezaji wote wanaoshiriki ligi kikuu,Alisema Maruma.

  “Kwa mjibu wa wa kikao cha kamati ya Tuzo ya VPL imeonesha kwamba mchezaji huyu alitoa mchango mkubwa kwa singida united kupata pointi 10 katika michezo mine,ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi huo,matokeo ambayo yaliiwezesha Singida United kutoka nafasi ya 10 katika msimamo na kupanda hadi nafasi ya nne kwa mwezi huo wa Septemba,Singida United ndiyo timu iliyokusanya alama nyingi kwa mwezi huo ukilinganisha na timu nyingine 15 zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara”,Alisema Maruma

  Kwa upande wake Sharif Batambuze,aliishukuru kamati ya tuzo ya ligi na wadhamini wakuu kwa kumpatia fedha hizo na kusema atazitumia vizuri ili iwe kumbukumbu nzuri katika maisha yake kwa msimu wa 2017 Batambuze.

  0 0

   
   Afisa Mkuu wa Masoko, wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akifafanua jambo mapema leo mchana,wakati akieleza namna Supa Mzuka Jackpot inavyofanyika na namna mshindi anavyopatikana.Maganga alisema


  "Kwa Sasa kila wakati ukicheza Tatu Mzuka hadi tarehe 19 Novemba, unapata bure nafasi ya kujishindia Tzs.150 milioni za uhakika kupitia droo ya Supa Mzuka Jackpot" alisema na kuongeza kuwa Wiki iliyopita Juma Othman (pichani kushoto),aliibuka mshindi wa Mzuka Jackpot na kujinyakulia kitita cha Tz.55 milioni. 

  Pichani kulia ni Juma Othman mwenye umri wa miaka 21 tu, akitoa ushuhuda namna alivyoshinda Mzuka Jackpot na kujinyakulia kitita cha Tz.55 milioni. Mshindi huyo ambaye anaishi na mama yake wilayani Bagamoyo, aliishukuru Tatu Mzuka huku akibainisha kuwa ushindi huo umebadilisha maisha yake.
   Afisa Mkuu wa Masoko, wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi Juma Othman aliyeibuka mshindi wa Mzuka Jackpot na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 55 za Kitanzania.

   
  Tatu Mzuka kwa mara nyingine wamevunja rekodi kwa kuwaletea Watanzania jackpot kubwa zaidi kuwahi kutokea nchin. 

  Donge nono la shilingi milioni 150 litatolewa kwa mshindi mmoja atakayebahatika siku ya tarehe 19 Novemba 2017, kupitia droo ya Supa Mzuka Jackpot.

  Kupitia Supa Mzuka Jackpot, Watanzania wanashinda mara 1, si 2 bali nafasi 3 za kushinda kiasi kikubwa cha pesa kwa bei ya soda!

  Njia tatu za kushinda na Tatu Mzuka ni;
  1) Kushinda hadi milioni 6 kila saa, masaa 24 kwa siku

  2) Kushinda Sh100,000,000 kupitia Mzuka Jackpot Jumapili hii, saa 9:30 usiku.

  3) Kushinda Tzs.150,000,000 kupitia Supa Mzuka Jackpot tarehe 19 Novemba
  Sebastian Maganga, Afisa Mkuu wa Masoko, wa Tatu Mzuka alielezea namna Supa Mzuka Jackpot inavyofanyika.

  "Kwa Sasa kila wakati ukicheza Tatu Mzuka hadi tarehe 19 Novemba, unapata bure nafasi ya kujishindia Tzs.150 milioni za uhakika kupitia droo ya Supa Mzuka Jackpot" ilifafanua Maganga.

  Wiki iliyopita Juma Othman, mshindi wa Mzuka Jackpot aliondoka na Tz.55 milioni. Othman mwenye umri wa miaka 21 tu, ambaye anaishi na mama yake wilayani Bagamoyo, aliishukuru Tatu Mzuka kwani ushindi huo umebadilisha maisha yake.

  Tatu Mzuka imebadili maisha ya Watanzania hakika,hadi sasa imetengeneza mamilionea Zaidi ya 70 na kutoa zaidi ya bilioni 3 kwa zaidi ya washindi milioni 1 na laki tatu.

  Homa ya Tatu mzuka inapoendelea kupanda, swali linabaki kuwa je? Nani ataondoka na donge kubwa Zaidi katika historia ya Tanzania.

  0 0


  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  BARAZA la Vyama vya hiari na Maendeleo ya Jamii (TACOSODE) limesema wananchi wamekuwa na uelewa kuhamasisha bajeti kuwa na kipaumbele kwa changamoto zinazowakabili.

  Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Miradi wa Tacosode, Theofrida Kapinga wakati akizungumza semina ya kujadilia jinsi gani ya kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya afya iliyofanyika katika ukumbu wa valentine Manispaa ya Iringa.

  “Unajua zamani wananchi hata viongozi wa sekta ya afya walikuwa wagumu kuelezea changamoto zinazowakabili lakini saizi wananchi na viongozi wamekuwa na elimu ya kutosha juu ya kueleza changamoto zilizopo katika sekta hiyo ndio maana vitu vingi vinaibuka muda huu” alisema Kapinga

  Kapinga alisema licha ya serikali kufanya juhudi kutatua changamoto ili kuto huduma ya afya bora lakini bado sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

  “Ukiangalia tafiti nyingi zinaonyesha kuwa serikali imekuwa ikishindwa kuongeza bajeti ya sekta ya afya ili kufikia asilimia 15 ya bajeti yote ya serikali kwa kuzingatia azimio la Abuja” alisema Kapinga
   Mkurugenzi wa Miradi wa Tacosode, Theofrida Kapinga akizungumza jambo wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa valentine mkoani Iringa
  Afisa mchechemzi wa mradi Abrahm Kimuli akiendelea kutoa elimu kwa wanasemina walikuwa wamehudhuria katika ukumbi wa valentine
   Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mijadala ya sekta ya afya na jinsi gani wanaweza kutatua changamoto zinazoweza kuikoa sekta ya afya hapa nchini.


  0 0

  MANISPAA ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imetiliana saini mkataba wa sh.bilioni 5.56 na kampuni ya ukandarasi ya CRJE ya nchini China kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kuwa mbolea aina ya mboji .

  Kiwanda hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchakata takaka tani tano (5) hadi 100 kwa siku kitajengwa katika eneo la Mabwepande.Akizungumza wakati wa hafla ya utilianaji saini, Dar es Salaam, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta amesema kuwa kiwanda hicho ambacho ujenzi wake unaanza rasmi leo kitakuwa na uwezo wa kuchakata taka ngumu na laini kuwa mbolea aina ya mboji.

  Amesema manispaa imekuwa ikitumia kati ya sh.milioni 500 hadi 600 kwa mwezi kugharamia uzoaji wa taka ambazo hizo taka hazizalishi chochote.Sitta amesema Manispaa ya Kinondoni inazalisha tani 22,000 kwa siku hivyo kutumia fedha nyingi kuwalipa makandarasi.

  Amesema zaidi ya wananchi 1000 wanatarajiwa kunufaika na ajira kupitia kiwanda hicho.Aidha amesema hatua hiyo kubwa ya kuitikia sera ya taifa ya kuelekea uchumi wa viwanda na kinondoni tunakuwa kuzalisha mbolea aina ya mboji ambayo haina madhara katika udongo ukilinganisha na mbolea za kemikali,”.

  Meneja wa Kanda wa kampuni ya CRJE, Bai Haochen amesema, ujenzi wa kiwanda hicho unaweza kuchukua muda wa miezi 12 hadi 18.
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta na Meneja wa Kanda  wa kampuni ya CRJE,  Bai Haochen wakitiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na kuwa mbolea leo jijini Dar es Salaam.
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta akizungumza na waandishi wa habari juu ya makubaliano na kampuni ya ukandarasi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kuwa mbolea leo jijini Dar es Salaam.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Banjamin Sitta na Meneja wa Kanda  wa kampuni ya CRJE,  Bai Haochen wakibadilishana hati za makubaliono leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upangaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 leo (Jumatano, Oktoba 18, 2017) katika ofisi za HESLB jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo wa HESLB Dkt. Veronica Nyahende (Picha: HESLB).


   WAOMBAJI wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kuwa, baada ya uchambuzi wa maombi yao, Orodha ya Awamu ya Kwanza yenye wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa kupangiwa mikopo imekamilika.

  hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru wakati akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es Saaam leo amesema kuwa
   Kiasi cha Tshs 34.6 bilioni kimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao 10,196. Kwa ujumla, Tshs 108.8 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi30,000 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
    
  Amesema kuwa "Orodha hiyo ya kwanza inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) na itatumwa kwa vyuo husika. Orodha nyingine (batches) zitafuata kadri taratibu za udahili na uchambuzi zinavyokamilika. Lengo ni kutoa majina ya wote waliofanikiwa kupata mkopo kabla ya vyuo kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba, 2017."

  Amesema kuwa Orodha hiyo ya wanafunzi 10,196 imepatikana baada ya kupokea na kuchambua Awamu ya Kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495waliopata udahili katika chuo kimoja.

  Wanafunzi waliopata udahili katika chuo zaidi ya kimoja na ambao wana sifa za kupata mikopo, watapangiwa mikopo baada ya kuchagua na kuthibitisha chuo watakachojiunga kwa ajili ya masomo.

   Tshs 318 bilioni zatengwa kwa ajili ya wanaoendelea na masomo.

  amesema kuwa wanatarajia kuanza kutuma vyuoni fedha za mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wamefaulu mitihani yao kuanzia leo, Jumatano, Oktoba 18, 2017.

  Kiasi cha Tshs 318.6 bilioni kitatolewa kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018. Tayari Serikali imeshatoa fedha hizo na lengo la Bodi ni kuhakikisha fedha zinafika vyuoni kabla ya kufunguliwa kwa vyuo ili kuwaondoloea wanafunzi usumbufu.

  Bodi ya Mikopo inawasihi waombaji wa mikopo kuwa na subira wakati ikiendelea kukamilisha maandalizi ya orodha zinazofuata za wanafunzi waliopata mikopo. Tutaendelea kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na tovuti ya Bodi mara kwa mara.

  0 0

  ZOEZI la Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoani Kilimanjaro limechukua sura mpya baada ya wananchi kuendelea kuhamasika na kufurika kwa wingi kwenye vituo vya Usajili kujisajili.

  wananchi wa Kata ya Masama Mashariki Wilaya ya Hai ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa katika kituo cha Usajili kilichopo kwenye kijiji cha Mbweera, Mboreny, Sonu, Ngira na Sawe. Zoezi katika Kata hiyo litamalizika Jumatano 18/10/2017 kabla ya kuhamia Kata za Masama Magharibi na Kata ya Kia. 

  Zoezi la Usajili kwa mkoa wa Kilimanjaro linaendelea katika Wilaya zote za mkoa huo ikiwemo Moshi, Rombo, Siha, Mwanga na Same.
   Mmoja wa Wakazi wa Kijiji Mbweera Kata ya Masama Bi Rachel akiweka saini ya kielekektroniki kwenye mashine ya kuchukua taarifa wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika Kata hiyo.
   Afisa Usajili Wilaya ya Hai Bw. Abubakar Karinga akitoa maelekezo ya taratibu za Usajili kwa wananchi waliokusanyika kusajiliwa kutoka vijiji vya Mbweera na Mboreny.
    Wananchi wa Kata ya Masama wakiendelea na hatua za Usajili Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hili likiendelea, ambapo mbali ya na kujaza fomu za maombi pia wanachukuliwa alama za Vidole, picha na saini ya Kielektroniki. 
   Wananchi wa Kata ya Masama wakiendelea na hatua za Usajili Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hili likiendelea, ambapo mbali ya na kujaza fomu za maombi pia wanachukuliwa alama za Vidole, picha na saini ya Kielektroniki. 
  Bi. Anocensia Momburi mmoja wa Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akitabasamu jambo wakati akimhudumia mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mbweera aliyefika kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.

  0 0


  The Minister for Finance and Planning Hon. Dr. Philip Mpango sharing a light moment with the audience while delivering his key note address to 1,000 delegates during the first VICOBA Day launch in Dar es Salaam. NBC was one of the main sponsors of the VICOBA Day.
  The Minister for Finance and Planning Hon. Dr. Philip Mpango presenting a certificate of appreciation to the NBC Retail Banking Director Filbert Mponzi for sponsoring the first VICOBA Day in Dar es Salaam. In between the two is Sihaba Nkinga Permanent Secretary in the ministry of Health, community Development, Gender, Elderly and Children. NBC was one of the main sponsors of the VICOBA Day.
  The Executive Secretary of National Economic Empowerment Council (NEEC) Ben’gi Issa delivering her opening speech during the launch of the first VICOBA Day in Dar es Salaam. The VICOBA day was officially launched by the Minister for Finance and Planning Hon. Dr. Philip Mpango. NBC was one of the main sponsors of the VICOBA Day.
  A cross section view of the 1,000 delegates attending the first VICOBA Day launch celebrations in Dar es Salaam. The VICOBA day was officially launched by the Minister for Finance and Planning Hon. Dr. Philip Mpango. NBC was one of the main sponsors. 

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Ndugu Sam Kamanga akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa unaoendelea mjini Arusha 
  Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya NIC wakiwa katika mkutano huo wa mameneja wa NIC unaoendelea jijini Arusha 
  Mwenyekiti wa Bodi ya NIC Ndugu Laston Msongole akizungumza jambo wakati wa mkutano wa mameneja wa Shirika la Bima la Taifa unaoendelea mjini Arusha , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Ndugu Sam Kamanga
  Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi na Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)unaoendela Jijini Arusha


  0 0

  Na Mashirika ya Kimataifa.

  KAMISHNA wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu, siku saba kabla ya Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba  26, 2017


  Akombe ametoa tangazo hilo akiwa jijini New York nchini Marekani, na kusema kuwa hawezi kuendelea kufanya kazi katika Tume hiyo, aliyoielezea kugawanyika.


  Aidha, amedokeza kuwa mazingira ya sasa ya kisiasa hayawezi kuruhusu kufanyika kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.


  “Siwezi kuendelea kufanya kazi, katika mazingira kaa haya, kila dalili zinaonesha wazi kuwa Uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki,” alisema Akombe akiwa Marekani.


  Bi Akombe aliondoka nchini Kenya  siku ya Jumanne, kwenda Dubai kushuhudia uchapishwaji wa karatasi za kupigia kura lakini akaamua kwenda nchini Marekani, ambako pia ni raia wa nchi hiyo.


  Kujiuzulu kwa Bi. Akombe, ni pigo kwa Tume hiyo ambayo ilikuwa inamtegemea kuzungumza kwa niaba yake na kuitetea mara kwa mara.


  "Tume ijitokeze wazi, iwe na ujasiri na kusema kuwa Uchaguzi huu hauwezi kuwa huru na haki katika mazingira haya," aliongeza Akombe.


  Amesema pia alikuwa anapata vitisho kuhusu maisha yake na huenda asirejee nchini Kenya katika siku za hivi karibuni.


  Suba Churchil, kiongozi wa mashirika ya kiraia amesema hali hii inaendelea kuzua wasiwasi kuhusu Uchaguzi huo uliopangwa kufanyika wiki ijayo.


  0 0

   Mtafiti Kutoka REPOA, Dk . Lucas Katera,Akiwasilisha   ripoti ya Nafasi ya nchi katika kufanya Biashara Duniani iliyotolewa na World Economic Forum na Repoa.
   Mkurugenzi wa Repoa nchini, Donald Mmari, akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Nafasi ya Tanzania  katika kufanya Biashara Duniani.
   Mtafiti Kutoka Repoa Prof.Paschal Mihyo akichangia mada  mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Nafasi ya Tanzania  katika kufanya Biashara Duniani.
   Baadhi ya watu walioshiriki katika  uwasilishwaji kwa ripoti ya Nafasi ya Tanzania  katika kufanya Biashara Duniani.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  TIMU ya Taifa ya mpira wa wavu imepanda kwa nafasi 19 kwa timu za wanaume na wanawake na kuanza kufufua matumaini ya mchezo huo kufanya vizuri  kimataifa zaidi baada ya mwanga na kwenda mbali zaidi.


  Tanzania imesogea kwenye viwango hivyo kutoka nafasi ya 137 hadi 118 kwa wanaume huku kwa wanawake ikitoka nafasi ya 115 hadi 97, kwa Afrika Mashariki ni Kenya inayoongoza kwa wanaume ikiwa nafasi ya 33, Uganda 55, Burundi 97, Rwanda 114.

  Nasoro Sharif ambaye ni kocha na mchezaji wa timu ya taifa ya wavu amesema kuwa  jitihada ndizozimewafikisha hapo na hawawezi kuacha kujituma uwanjani na katika michezo ijayo pia   kinachotakiwa kwa sasa ni kuendelea kuupigania mchezo huo ili tusogee zaidi kwenye viwango hivyo sawa na wenzetu wa Kenya.


  “Uongozi mpya unaweza kutusaidia kwa kiasi kikubwa maana unonekana kuja na mambo mengi mazuri, Tanzania imekosa michezo mingi ya kimataifa nadhani itakiwa tuwe na michezo mingi ili itusaidie kupanda," alisema mchezaji huyo.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula na Mbunge wa Ilemela, ameishukuru Kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa kutimiza ahadi yao kwa Mbao kwa kukabidhi gari yenye thamani ya milioni 70 na tayari wakiwa wamelipia gharama zote za ushuru na kufikia jumla ya milioni 100. 

  Mabula amesema kuwa baada ya kuingia mkataba na kampuni hiyo wameanzisha kampeni ya ubingwa ili kulitoa taji kwa timu za Mkoa wa Dar es Salaam na wanaweza kufanikiwa kwa hilo kama wadhamini watajitokeza kwa wingi kwa timu za mikoani.

  Mbao FC ya Mwanza imekabidhiwa basi lenye thamani ya Sh70 milioni kwa ajili ya wachezaji.Basi hilo wamekabidhiwa leo Jumatano na wadhamini wao Kampuni ya GF Trucks & Equipments katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Vingunguti, Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Alijawad Karmali alisema basi hilo ni sehemu ya mkataba ambao waliingia na Mbao miezi miwili iliyopita na wameweza kutimiza ahadi hiyo na wanaimani kuwa watalitunza katika kipinci chote..

  Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi amewashukuru Kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa udhamini huo mkubwa waliouweka kwani mpaka basi hilo wanalipokea katika mikono yao limezidi thamani ya Sh70 milioni na litakuwa msaada mkubwa sana kwa timu yao kuhusiana na masuala ya usafiri na pia mpaka sasa udhamini wao umeshazidi milioni 140 

  Mbao inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi sita, huku Simba ikiwa kileleni na pointi 12 ikifuatiwa na Yanga ambayo ndiyo mabingwa watetezi wakiwa na tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula akiwashukuru kampuni ya FT Trucks & Equipments kwa kuipatia udhamini kwa timu ya mkoani kwake Mwanza pamoja na basi sambamba na yeye kuwa mlezi wa timu hiyo leo Jijini Dar es salaam.
  Ofisa Masoko wa Kampuni ya GF Trucks Equipment, Kulwa Bundala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuwakabidhi gari lenye thamani ya milioni 70 kwa timu ya Mbao ikiwa ni moja ya makubaliano yaliyopo katika udhamini wao wa mwaka mmoja kwa timu hiyo. 
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula pamoja na Mkurugenzi wa GF Trucks & Equipments Alijawad Karmal (kulia) na mwenyekiti wa timu ya Mbao Solly Zephania Njashi wakikata keki.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula akikata utepe katika gari ya waliokabidhiwa Mbao na kampuni ya GF Trucks & Equipments lenye thamani ya milioni 70 ikiwa ni katika makubaliano ya mkataba walioingia miezi mitatu iliyopita, juu ni Mkurugenzi wa GF Trucks & Equipmens Alijawad Karmal akimkabidhi mfano wa funguo ya gari mwenyekiti wa timu ya Mbao Solly Zephania Njashi akishuhudiwa na viongozi wengine wa Mbao Fc pamoja na wengine kutoka GF Trucks & Equipments.


  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo ambaye pia ni mlezi wa TPF NET mkoa wa Arusha akikabidhi Mbuzi wawili pamoja na zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi 780,000 na fedha taslimu Shilingi 160,000/= kwa watoto yatima wa kituo cha Christ Hope Orphonage kilichopo jijini hapa.
   Wanachama wa Mtandao wa Polisi Wanawake Arusha pamoja na watoto yatima wa kituo cha Christ Hope Orphonage wakionekana kusikiliza kwa umakini hotuba iliyokuwa inatolewa na mlezi wa Mtandao huo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo.
  Askari wapatao 80 toka wilaya mbalimbali za mkoa wa Arusha ambao ni wanachama wakitembea kwa maandamano umbali wa kilomita 7 huku wakiongozwa na Brass Band ya Polisi. 
  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
  MTANDAO wa Polisi Wanawake mkoa wa Arusha umetakiwa upambane kwa kujitoa na kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu ili kuweza kutokomeza ndoa za utotoni kwa baadhi ya makabila.

  Hayo yameelezwa leo na mlezi wa mtandao huo mkoani hapa ambaye pia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu kamishna (DCP) Charles Mkumbo wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao huo yaliyolifanyika katika kituo cha kulelea watoto yatima kiitwacho CHRIST HOPE ORPHANAGE kilichopo Uswahilini halmashauri ya jiji la Arusha.

  Aliwataka wasimame imara ili kuhakikisha elimu juu ya unyanyasaji na ukatili kwa watoto, akina mama na akina baba inatolewa na kuwafikia walipo hali ambayo itasaidia kuondoa kabisa tatizo hilo.

  Kamanda Mkumbo alisema wakati umefika sasa kwa Madawati ya Jinsia na watoto kutokaa ofisini na badala yake wanatakiwa waifuate jamii ilipo kwani wanaokwenda kutoa taarifa kwenye vituo vya Polisi ni sehemu ndogo tu ya wengi wenye kukosa elimu ya uelewa juu ya ukatili na unyanyasaji waliopo mitaani.

  “Wale wanaokwenda kutoa malalamiko yao katika vituo vya Polisi ni wachache sana ukilinganisha na wale wenye matatizo hayo waliopo mitaani au kwenye taasisi mbalimbali kama vile shule” Alisema kamanda Mkumbo.

  “Watu wengine mpaka leo hii wanaamini ukeketaji ni moja ya mila yao kitu ambacho sio sahihi hivyo kupitia madawati ya Jinsia na Watoto pamoja na taasisi nyingine zikishirikiana na kutembelea jamii kwa nia ya kuwaelimisha naamini kwamba matatizo haya yataisha”. Aliongeza Kamanda Mkumbo.

  Aliwatake wanachama wa mtandao huo ambao ni Polisi Wanawake kufanya kazi kwa bidii ili kuidhihirishia jamii kwamba wanaweza bila kuwezeshwa. Alimalizia Kamanda Mkumbo.

  Awali akieleza madhumuni ya maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi  Namsemba Mwakatobe, alisema kwamba mtandao huo una wajibu wa kushirikiana na na makundi mbalimbali wakiwemo watoto yatima hali ambayo itasaidia makundi hayo kutambua kwamba, hawapo peke yao bali mtandao huo upo nyuma yao katika kusikiliza matatizo yao na kulinda haki zao.

  Alisema pamoja na kuungana nao siku ya leo lakini pia mtandao huo umejitokeza  kwa ajili ya kuonyesha upendo wao kwao kama askari lakini pia kama wa kike na kuhakikisha kwamba wanakuwa katika mazingira salama na kuepuka vitendo vya uhalifu.

  Akizungumza katika maadhimisha hayo Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Steven Isanja alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2007 kikiwa na watoto 30 lakini hivi sasa kina watoto 64 ambao wanasoma katika ngazi ya Chekechea, Shule ya Msingi na Sekondari.

  Maadhimisho hayo yaliyojumuisha jumla ya askari wanawake 80  kutoka wilaya za mkoa huu yalianzia katika kituo kikuu cha Polisi Arusha ambapo walitembea kwa maandamano umbali wa kilomita 7 kisha kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wa kituo hicho kama vile Mchele kilo 100, Mbuzi wawili, mafuta lita 40, sabuni  vinywaji mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 780,000/= pamoja na fedha taslimu shilingi 160,000/=.

  0 0


  NEC-DODOMA

  Tume ya Taifa ya uchaguzi imesisitiza kuwa Leseni za udereva, Hati za Kusafiria na Vitambulisho vya Taifa vitatumika kwenye uchaguzi mdogo wa Madiwani wa Kata 43, utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Ramadhan Kailima amesema wapiga kura wataruhusiwa kutumia vitambulisho hivyo kwa sharti ya kwamba picha, herufi na majina yaliyopo kwenye Leseni ya Udereva, Hati ya kusafiria na Kitambulisho cha Taifa yawe yanafana na majina na herufi zilizopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

  Kailima amesema kuwa ruhusa hiyo ya Tume ya matumizi ya vitambulisho hivyo imekuja kufuatia maoni ya wadau na baadhi ya wapiga Kura kupoteza kadi zao za kupigia Kura na wengine kadi zao kuharibika kutokana na sababu mbalimbali na hivyo kuwanyima haki na fursa ya kupiga Kura katika uchaguzi huo mdogo.

  Amesema hatua hiyo inazingatia matakwa ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu Namba 61, kifungu kidogo cha 3a na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kifungu Namba 62 (a) ambavyo vinaipa Tume mamlaka ya kuruhusu kutumika kwa utambulisho mwingine wowote utakao msaidia mpiga kura aliyejiandikisha kuweza kupiga kura iwapo hana kadi.


  0 0

  NA HAMZA TEMBA - WMU-DODOMA

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga leo tarehe 18 Oktoba, 2017 ameripoti rasmi Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo Mtaa wa Kilimani, Makao Makuu ya Nchi, Mjini Dodoma.

  Mhe. Hasunga amepokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na kuingia ofisini kwake kwa mara ya kwanza ambapo amesaini kitabu cha wageni na baadaye akapata fursa ya kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo waliopo Dodoma.


  Akizungumza na watumishi hao baada ya kutambulishwa, Mhe. Hasunga aliwaomba ushirikiano katika kufanikisha majukumu ya Wizara ambayo ni kuhifadhi na kusimamia matumizi endelevu ya maliasili na malikale, na kuendeleza ufugaji nyuki na utalii.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akikaribishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati) alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo mtaa wa Kilimani mjini Dodoma leo. Kulia anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Tutubi Mangazeni.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto) akimtambulisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) kwa watumishi wa Wizara hiyo kabla ya kuzungumza nao leo mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na baadhi ya watumishi wa wizara hiyo baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo mtaa wa Kilimani mjini Dodoma leo. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hotel ya Hyatt . Kulia Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga na kushoto ni  Mwakilishi kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby Msammy katika hafla iliyofanyika kwenye Hotel ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
   Mwakilishi kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby Msammy  (kushoto) akimkabidhi bendera Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete (katikati)  katika hafla ya kumuaga iliyofanyika jana kwenye hotel ya Hyatt . Kulia Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
   Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete akiwa katika pozi mara baada ya kukabidhiwa bendera kwenye halfa fupi iliyofanyika kwenye hotel ya Hyatt


   Na Mwandishi Wetu
  MISS World Tanzania, Julitha Kabete (21) ametamba kufanya vyema katika mashindano ya 67 ya kumsaka mrembo ya Dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Sanya, nchini China mwezi ujao.

  Julitha ambaye anaondoka leo, amesema kuwa amejiandaa vyema ili kuiletea sifa Tanzania katika mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Novemba 18 kwenye ukumbi wa Sanya City Arena in Sanya, China PR.

   Stephanie na kushirikisha jumla ya warembo 120. Julitha anaondoka leo kwenda China chini ya udhamini wa Turkish Airline. Mrembo huyo aliagwa na kukabidhiwa bendera na  Mwakilishi kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby Msammy katika hafla iliyofanyika kwenye Hotel ya Hyatt jijini Dar es Salaam.

  "Nimejiandaa vizuri katika mashindano haya, nina uzoefu mkubwa kwani nilishinda mashindano ya Miss Dar City Center, Miss Ilala na kwenye fainali za miss Tanzania 2016 ambako niliingia tano bora. Pia nilishiriki mashindano ya Afrika na kufanya vyema,” alisema Julitha.

  Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema Julitha ni mrembo wa 23 kuiwakilisha nchi kwenye Miss World.

  "Mwaka huu shindano la Miss Tanzania limechelewa kufanyika, hivyo tukaamua kumtea Julitha akatuwakilishe kwenye Miss World, uteuzi wake umezingatia vigezo vyote na hakuna shaka atafanya vizuri katika fainali hizo ambazo tumekuwa na rekodi ya kutwaa taji la Miss World Afrika na mataji mengine," alisema Lundenga.

  Mrembo huyo aliondoka nchini jana usiku kuelekea katika kambi ya Miss World nchini China ambapo atachuana na warembo wengine kutoka mataifa zaidi ya 120 kusaka mshindi katika fainali itakayofanyika baadae Novemba nchini humo.

  0 0

   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  MKUU wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule ameigiza  Tanesco Same  kuwafata wateja popote walipo hili kuongeza kasi ya huduma kwa kuhakikisha kuwa kila mahali wanapata Umeme.


  Dc Sinyamule amesema hayo alipokuwa akizindua tawi la  Tanesco  Hedaru na Kisiwani katika Wilaya Same na kumbusha kuongeza ofisi maeneo ya milimani.


  Kuhakikisha mkandarasi anayefanya kazi kuzingatia uimara wa nguzo hasa maeneo ya milimani pamoja na Kutengeneza mabango yanayoonyesha wateja tahadhari za kuchukua juu ya umeme ili kupunguza madhara ya vifaa na umeme kukatikakatika”Amesema Dc Sinyamule.


  Amewataka Kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma kwa haraka na Kuanzisha na kuitangaza namba ya simu ya mkononi kwa ajili ya wateja.

  Pia aliwakumbusha wateja kuongeza kasi ya kuweka umeme na  kulipia huduma za umeme pindi watakapohitajika kuunganishiwa.


  Pia aliwakumbusha kuanza kutumia umeme kwa uchumi kwa kuanzisha viwanda vidogo na vya kati kwani serikali imekusudia kumaliza tatizo la umeme ifakapo 2021.


   Kwa Upande wake Meneja wa Tanesco Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Hiza amesema shirika limejipanga kusogeza huduma karibu baada ya ongezeko kubwa la wateja wanaotokana na mpango wa serikali  REA.


  Hivyo aliwaomba wakazi wa Wilaya ya Same na Vitongoji vyake Kulipa bili kwa wakati na kutumia umeme kwa uangalifu ili kusiwepo umeme unaopotea bila sababu.


  Aidha aliwaomba wakazi wa eneo hilo Kuchukua tahadhari za usalama pamoja na kutunza miundombinu na Kutoa taarifa haraka kunapotokea tatizo/ uharibifu
   Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Sinyamule akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Tanesco Hedaru wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro
   Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule  akizungumza na wadau mara baada ya kufungua ofisi ya Tanesco Hedaru
  Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akiwa katika picha ya pamoja Wafanyakazi wa Tanesco Hedaru

older | 1 | .... | 1968 | 1969 | (Page 1970) | 1971 | 1972 | .... | 3284 | newer