Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

DC SHINYANGA AWATAKA WAFUGAJI KUTII AGIZO LA SERIKALI KUPIGA CHAPA MIFUGO YAO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewataka wafugaji kutii maagizo ya serikali ya kupeleka mifugo yao kuwekewa chapa ya Serikali ili itambulike kisheria na kuwa kinga ya migogoro ya wafugaji. 

Akizungumza jana Jumatatu Oktoba 16,2017 kwenye uzinduzi wa upigaji chapa mifugo wakati akiongea na viongozi wa serikali ya kata ya Pandagichiza,Matiro alisema upigaji chapa mifugo hiyo una faida kubwa kwa wafugaji ikiwemo kuzuia migogoro ya wafugaji.
Alisema upigaji chapa mifupo ni agizo la serikali kutoka kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa na mfugaji ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Nampongeza waziri mkuu kwa agizo la upigaji chapa mifugo na tangu zoezi hili lianze kufanyika hakuna mgogoro wowote wa wafugaji uliotokea",alisema Matiro.

Aidha aliwataka wafugaji kujenga utamaduni wa kufuga kisasa kwa kuvuna mifugo yao na kuwekeza pamoja na kujenga makazi yao kuwa mazuri na siyo kuwa na idadi nyingi ya mifugo halafu waanishi maisha mabaya bila hata ya kuwa na kitanda.

Naye mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi kutoka halmashauri ya Shinyanga Vijijini Omari Kamata, alizitaja Sheria ambazo zitachukuliwa kwa mfugaji atakaye kaidi agizo hilo la upigaji chapa mifugo, kuwa ni faini ya shilingi 300,000/= hadi 600,000/= au kifungo cha Miezi Sita hadi Mwaka mmoja.

Alisema katika halmashauri hiyo kuna jumla ya ng'ombe 344,736 na waliopigwa chapa ni ng'ombe 79,164 tangu zoezi hilo lilipoanza June 20 mwaka huu.

Aidha aliongeza kuwa katika kata hizo mbili za Mwalukwa na Pandagichiza ambalo zoezi hilo la upigaji chapa limezinduliwa leo na mkuu huyo wa wilaya katika kijiji cha Shilabela ambapo ng'ombe 17,117 wanaoanzia umri wa miezi sita wanatarajiwa kupigwa chapa.

Nao baadhi ya wafugaji walisema awali waligomea zoezi hilo kutokana na taarifa za awali kutolewa ndivyo sivyo ,lakini kutokana na maelezo yaliyotolewa na mkuu huyo wa wilaya wameahidi kutii maagizo hayo na kupeleka mifugo yao kupigwa chapa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiongea na viongozi wa serikali ya kata ya Pandagichiza wakiwemo watendaji,Sungusungu,wakulima na Wafugaji, akiwasisitiza kushiriki na kuhamasisha wananchi kuitikia zoezi la upigaji chapa mifugo kwa kuwekwa alama ya serikali-Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog.
Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kata ya Pandagichiza ,wakiwamo Sungusungu, wakulima na wafugaji wakimsikiliza mkuu wa wilaya kwenye uzinduzi wa upigaji chapa mifugo .
Ofisa mifugi wilaya ya Shinyanga William Kidua akipiga chapa mifugo ya Kijiji cha Shilabela Kata ya Pandagichiza baada ya zoezi la upigaji chapakuzinduliwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi kutoka Halmashauri ya Shinyanga Omari Kamata ,akielezea faida za upigaji chapa mifugo.
Daktari wa mifugo kutoka halmashauri ya Shinyanga Vijijini Clement Baksilo ,akielezea faida za upigaji chapa mifugo kuwa endapo mfugo ukiwa hata mnadani ubainika kuwa na ugonjwa itasaidia kubainika unatoka wapi na itakuwa rahisi kuwahi kwenda kutoa tiba mahali hapo na kuokoa mifugo mingine isipate magonjwa.-Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

MAAFISA ARDHI HANNANG WAPEWA SIKU 90 KUJIREKEBISHA KABLA YA KUCHUKULIWA HATUA

$
0
0
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabulla amefanya ziara ya kushtukiza katika idara ya ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Hannang mkoani Manyara na kukuta mfumo mbovu wa uhifadhi wa hati za kumiliki ardhi hali ambayo ni rahisi kwa maafisa hao kudanganya na kumilikisha watu wawiliwawili.

Mheshimiwa Mabulla ameyagundua hayo baada ya kupekua katika makabati ya uhifadhi wa nyaraka hizo katika ofisi ya Idara ya Ardhi na kuona mapungufu makubwa katika mafaili hayo hali inayoweza kupelekea   maafisa hao wa ardhi kufanya
udanganyifu.

Mabulla aliamua kupekua Hati za mwananchi mmojammoja na kugundua baadhi ya hati hazina vielelezo vya kumbukumbu na baadhi ya nyaraka za umuliki wa ardhi hazina mtiririko mzuri wa uhifadhi wa mafaili.

Mara baada ya kugundua mapungufu hayo makubwa Mheshimiwa Mabulla alimpa muda wa miezi mitatu Afisa Ardhi Mteule Bwana Egidius Kashaga kurekebisha mapungufu hayo pamoja na yeye mwenyewe kubadilika na akishindwa kufanya hivyo atamvua cheo chake na kumuadhibu kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Mabulla amekutana na wananchi wa Kata ya Mogitu, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara na kusikiliza kero zao za ardhi hasa suala la muwekezaji wa Kiwanda cha Manyara Cement Limited ambae ameomba eneo la ujenzi wa kiwanda la ukubwa wa ekari 370.

Mmiliki huyo Bwana James Mtei alipeleka maombi yake kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hannang akiomba ardhi katika kijiji cha
Mogitu ili ihawilishwe na imilikishwe kwa Kampuni yake kwa hati miliki chini ya Sheria ya Ardhi (Sura 113) kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha uzalishaji saruji.

Kwa mujibu wa Sheria hiyo ili mtu au kampuni iweze kumilikishwa ni lazima maombi hayo yaridhiwe na wanakijiji na kumfikia Waziri wa Ardhi na baadae kuidhinishwa na Mheshimiwa Raisi ikiwa ataridhia kutoa kibali chake cha Uhawilishaji.

Mheshimiwa Mabulla alitembelea eneo hilo linalotaraji kujengwa Kiwanda cha uzalishaji saruji ili aweze kujiridhisha kabla ya kummilikisha mwekezaji huyo.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabulla anamalizia ziara yake Mkoani Morogoro ambapo kesho anataraji kutembelea Chuo cha Ardhi cha Morogoro na kutatua changamoto zinazokikabili chuo hicho pamoja kutatua changamoto za walimu, wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabulla akipekua mafaili ya kuhifadhia hatimiliki za ardhi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika idara ya ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Hannang na kukuta mfumo mbovu wa uhifadhi wa hati za kumiliki ardhi hali ambayo ni rahisi kwa maafisa hao kudanganya na kumilikisha watu wawiliwawili.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabulla akikagua eneo lililoombwa na Kampuni ya Manyara Cement Limited kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha uzalishaji saruji katika Kata ya Mogitu, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabulla akiongea na wananchi wa Kata ya Mogitu, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara mara baada ya kusikiliza kero zao za ardhi hasa suala la muwekezaji wa Kiwanda cha Manyara Cement Limited ambacho kimeomba eneo la ujenzi wa kiwanda la ukubwa wa ekari 370.

Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon

$
0
0
SHIRIKA la ndege la Precision Air leo limetangaza udhamini wake wenye thamani ya Sh 20 milioni kwa ajili ya mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 jijini Mwanza.

Kwa udhamini huo, shirika hilo sasa linatambulika rasmi kama shirika maalumu la usafiri wa mbio hizo miongoni mwa wadhamini wengine zikiwemo kampuni za PUMA, Tiper, RedBull, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), New Mwanza Hotel, EF Out door, CF Hospital, KK Security, na kampuni ya uchapishaji ya SDS.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo ,Meneja Masoko na Mahusiano wa Precision Air Bw Hillary Mremi alisema udhamini huo kwa kiasi kikubwa umechagizwa na malengo ya mbio hizo yaliyojikita katika kutangaza utalii wa ndani kupitia mchezo wa riadha.

“Lakini pia kibiashara tunaona kwamba mara nyingi watu wanaopenda kushiriki riadha wamekuwa na ‘hobby’ pia kusafiri sehemu tofauti tofauti ndani na nje ya nchi hivyo ushiriki wetu kwenye mbio hizi utazidi kutukutanisha na kundi hili muhimu,’’ alibainisha.

Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirikala la Ndege la Precision Air Bw Hillary Mremi (wa pilikushoto) akikabidhi mfano wa tiketi ya ndege kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon, Bw Zenno Ngowi ( wa pili kulia) ikiwa ni ishara ya udhamini wenye thamani ya Sh 20 milioni kwa ajili ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe (wa tatu kushoto) pamoja na maofisa wa makampuni hayo mawili.
Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirikala la Ndege la Precision Air Bw Hillary Mremi akizungumza wakati wa makababidhiano hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi pamoja  na Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi (katikati) akizungumzia udhamini huo. Kwa mujibu wa Ngowi udhamini huo unamaanisha kwamba uhusiano wa Precision Air na wateja wake hautaishia  ndani ya ndege bali utaendelea zaidi hadi kwenye mitaa, fukwe, viwanja vya michezo na sehemu zote za utalii katika jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa yote.
Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe (katikati) akizungumzia udhamini huo. Kwa mujibu Lugoe maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba wamejipanga kupokea washiriki zaidi ya 4,000 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo viongozi na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.

MBUNGE KABATI ATOA SH.MILIONI MOJA KWA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE MKOANI IRINGA (TPF)

$
0
0
Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) akiwa sambamba na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi.  
Kabati aliliomba jeshi la polisi mkoani Iringa kuhakikisha wanapeleka dawati la jinsia katika shule za msingi na sekondari ili kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kwa wanafunzi kwa kuwa watakuwa wazi kuzungumza wanachofanyiwa huko mitaani. Mbunge huyo alichangia kiasi cha sh. milioni moja kwa ajili ya kusaidia dawati hilo.
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF)
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi na mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF). 
Hawa ni baadhi ya wanamtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) wakiwa katika maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa kwa mwaka 2007.

DC MSHAMA AMALIZA MGOGORO WA WAFANYABIASHARA SOKO LA LOLIONDO

$
0
0
Na Omary Mngindo, Kibaha

MKUU wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Bi. Assumpter Mshama amemaliza mgongano wa Wafanyabiashara wenye ubao upande wa ndani na wanaouzia kandokando ya Barabara.

Mgongano huo uliokuwepo kwenye soko la Mnalani Maarufu Loliondo kati ya Wafanyabiashara hao ambapo wanaouza ndani kwenye mbao wanadai wateja wanaishia nje hivyo hawapati wateja.

Wafanyabiashara Godruck Mwafrika na Anelista Mbaga kila mmoja amwelezea changamoto iloyopo kwenye soko hilo hali inayoleta mgongano kati yao.Mwafrika alisema kuwa waliowengi wamekimbia meza za ndani na kwenda kupanga nje kwa lengo la kupata wateja kwani wengi wanaishia nje hivyo wao kubaki wakipunga upepo tu.

Kauli hiyo ilipingwa na Bi. Aneliata ambaye alisema wote wanafanyabiashara sawa na kwamba malalamiko hayo hayana msingi huku akisema kwamba wateja wanafika kununua bidhaa sawasawa.

Baada ya kupata malalamiko ya pande mbili, Mshama ameagiza wanaofanyia biashara pembeni mwa soko wote waingie ndani na kwamba meza zote zina upana wa mita 30 hivyo kila moja watakaa watu wawili kwa maana mita 15.

Aidha amevunja aoko la siku za Jumatano akisema hatua hiyo ni ya ujanja wa watu ambapo alisema zuio hilo litaanzia Jumatano ya wiki inayoanzia Oktoba 25 akieleza kwa kiwa agizo hilo limekujanghafla kwani wapomm watu ambao wapo maeneo mbalimbali kutafuta biashara.
 MKUU wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Bi. Assumpter Mshama akizungumza na Wafanyabashara wa soko la Loliondo.
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa soko la Loliondo wakifurahia mara baada ya mgogoro wao kutatuliwa na MKUU wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Bi. Assumpter Mshama.

TAARIFA KWA UMMA:OFISI ZA BAKWATA ZAHAMIA KWA MUDA JENGO LA TIGER TOWER-MTAA WA TOGO

$
0
0
Ndugu zangu Wanahabari,

Assalaamu Alaykum (Amani ya Mwenye ezi Mungu iwe kwenu)

Napenda kuufahamisha umma wa kiislamu kuwa kufuatia kuanza mradi wa ujenzi wa msikiti wa Mohammed VI unaojengwa katika eneo la Bakwata makao Makuu Kinondoni Road.

Hivyo basi napenda kuchukua nafasi hii kuufahamisha umma kuwa ili kupisha mradi huo Bakwata Makao Makuu imehamisha ofisi zake na kuzipeleka katika mtaa wa Togo jengo linalotambulika kama TIGER TOWER na shughuli zote zinaendelea kama kawaida.

Mwisho kabisa tunaomba radhi kwa usmbufu wowote uliojitokeza katika kipindi hiki cha ujenzi.

Wabillahi TTaufiiq

USTAADH TABU KAWAMBWA

MKURUGENZI HABARI NA MAHUSIANO.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25,2016. PICHA NA MAKTABA

MICHUZI TV: TAKUKURU YATOA ONYO KWA NASARI

$
0
0


  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Valentino Mlowola akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati alipokuwa akiwaonya wabunge watatu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema).

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wamemuonya mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari kuacha kuwashinikiza kufanyia kazi ushahidi wa rushwa aliopeleka katika chombo hicho bali awaache wafanye kazi.

Aidha wamesisitiza kuwa, ushahidi aliopeleka Mbunge Nasari akiongozana na Lema pamoja na Msigwa siyo ushahidi bali ni taarifa ambayo bado wanaifanyia kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Valentino Mlowola amesema suala alilolipeleka Nassari katika Taasisi hiyo siyo suala la kisiasa bali ni la kisheria lakini anachokiona Nasari na wenzie wanataka kulifanya suala hilo kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria.

“Namuonya Mh. Nassari ameishaleta taarifa zake kwetu atuachie tufanye yale tunayopaswa kufanywa kwa mujibu wa sheria na siyo kutushinikiza, kama kauli waliyotoa jana, nitaendelea kuwa natoa series kutokana na  sisi tunavyofanyakazi, hii ni Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote tukiangalia sheria tuko huru kufanya majukumu yetu na hapashwi hata mara moja kutushinikiza”. Amesema Mlowola.

Ameongeza “endapo ataendelea na utaratibu huu sheria itachukua mkondo wake bila kuathiri taarifa zake alizozileta”.

Amesema, katika ushahidi kuna mambo mengi,  wanaangalia matakwa ya kisheria, kwani ushahidi una sifa, kuna swala la relevance na vissibility kwa hiyo na kusisitiza kuwa walichopokea kwa Nasari ni taarifa inayotakiwa kufanyiwa kazi na siyo ushahidi.

Ameongeza kuwa, taasisi hiyo, inapokea taarifa zinazohusiana na rushwa au  makosa ya rushwa kutoka vyanzo mbalimbali vikiwemo vya wazi na vya siri na sheria inataka mtoa taarifa alindwe lakini Nasari yeye aliamua kufanya vikao na waandishi wa habari kwa mara zote tatu alizofika Takukuru na hata kufikia kutoa taarifa juu ya hatua zinazoendelea katika mchakato huo.

Aidha, Mlowola amemshangaa Nassari kuuliza kwa nini hawajaupeleka ushahidi huo mahakamani mpaka sasa na kusema wao wanaongozwa na sheria ya mwenendo wa mashtaka na wakishamaliza uchunguzi watatathimini matokeo waliyoyapata na wakijiridhisha walichopewa kinakidhi vigezo vilivyowekwa na sheria watafikisha katika hatua stahiki ya kupeleka jalada kwa DPP ambaye akiridhika na ushahidi ataandaa mashtaka dhidi ya washtakiwa na kupelekwa mahakamani.

“Kuna matukio yanafanyika na watu wanadhani ni makosa kumbe ni 'moral wrongs' tu amabayo yanahitaji utaratibu mwingine wa kuwashughulikia”

serikali ya Viwanda ni pamoja na ufugaji Kuku na Samaki - Ulega

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu  ya Jamii
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema serikali ya Viwanda inakwenda na ufugaji Kuku pamoja na samaki kwa kutengeneza  Viwanda vya Kuku pamoja na mabwawa ya ufugaji samaki.

Ulega aliyasema hayo wakati wa ziara yake  aliyoifanya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwenye vijiji vinne, ambapo  alisema hakuna sababu ya wananchi wa Mkuranga kuchukua Kuku mikoa mingine  wakati wanaweza kufuga wenyewe na kujipatia kipato na maendeleo yakapatikana na kuwawezesha kuuza hata sehemu nyingine.

Amesema yuko tayari kuwasaidia wananchi wa Mkuranga mbegu za Kuku pamoja na watalaam wa kuwafundisha jinsi ya kufanya ufugaji wa Kuku na samaki wa kisasa. Amesema ajira katika Wilaya hiyo zipo ikiwa ni pamoja na ufugaji Kuku pamoja na samaki ambayo ni ajira ya kudumu na soko ni kubwa kutokana mahitaji ya vitoweo hivyo kuhitajika kwa wingi.

"Sioni sababu wananchi wa Mkuranga kuchukua kuku kutoka mikoa mingine wakati mnaweza kufanya nyinyi wenyewe kutokana na maeneo mlionayo, haitawezekana kama nyinyi hamtaweza  kuonyesha mfano nikiwa ni Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi"alisema Ulega.

Katika ziara yake  alitembelea Ujenzi wa Zahanati za Kibamba, Kimazichana na Mwandege na kuahidi kuwaunga mkono wananchi katika juhudi mbalimbali wanazoonyesha katika maendeleo ya huduma za jamii. Ulega amesema kuwa wakati uliopo ni kufanya kazi za Maendeleo kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya dhamira ya serikali ya Viwanda.

 Naibu waziri  aliaahidi kuchagiaji  sh. Milioni moja na mifuko ya saruji kwa ajili ya kikundi cha VICCOBA cha wanawake waliojenga ukumbi wa mikutano na sherehe kilichopo Mwandege.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibamba juu ya maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Zahanati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Kimazichana.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiangalia ufugaji wa Kuku katika eneo la Rabica ,Kibamba.


NAIBU WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA BOHARI YA DAWA (MSD)

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulileleo ametembelea Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pamoja na mambo mengine amepata taarifa yautendaji ya MSD kuhusu usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kusemakuwa bajeti ya dawa inayotolewa na serikali iendane na hali halisi ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye hospitali na vituo vya afya nchini.

Naibu waziri huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea MSD tangu ateuliwe kwenyenafasi hiyo, amesema hatua ya serikali kuongeza bajeti ya dawa kuanzia mwaka wa fedha uliopita na mwaka huu ina lengo la kupunguza gharama ya dawa na kuhakikisha upatikanaji wadawa muhimu kwenye vituo vyote vya Afya vya umma ili kumpunguzia mwananchi gharama zamatibabu.

Kwa upande mwingine Mhe. Ndugulile amewataka watendaji wa MSD kuwa na utaratibu wakuwatembelea wateja wao ili kuboresha huduma zaidi baada ya kusikiliza maoni, malalamiko n ahata ushauri wao. 

Sambambana hilo amewaagiza MSD kitengo cha huduma kwa watejakutembelea wateja wao na kuhakikisha kitengo cha Manununuzi Maalumu (SpecialProcurement) kinaongeza kasi kwenye manunuzi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile, akizungumza na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), alipofanya ziara ya siku moja kutembelea ofisi hizo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu (kulia), akitoa maelezo kwa Mhe. Ndugulile.
Picha ya pamoja.

DK.SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA UGANDA NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Balozi wa Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Richard Mabonero  leo  alipofika Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Richard Mabonero, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Richard Mabonero, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akifuatana  na mgeni wake  Balozi wa Uganda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Richard Mabonero, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo baada ya mazungumzo yao. (Picha na Ikulu).

SERIKALI YAWATAKA WADAU WA SEKTA YA AFYA YA BINADAMU, MIFUGO, WANYAMA PORI NA MAZINGIRA KUONGEZA KASI YA USHIRIKIANO NA MASHAURIANO

$
0
0
Mmoja wa washiriki wa warsha ya wadau wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama pori kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akichangia mada wakati wa warsha ya kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba 16, 2017.
Mwakilishi wa Shirika la DTRA kutoka nchini Marekani Bi. Jean Richard akizungumza na wadau wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama pori wakati wa warsha ya kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21) katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba 16, 2017.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mbazi Msuya (wa pili kushoto)akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na wadau mbalimbali wa warsha wadau wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama pori iliyokuwa ikijadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21) katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba 16, 2017. Wa pili kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Ritha Njau.
Mwakilishi wa Shirika la OIE katika nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw. Moetapele Letshwenyo akizungumza na wadau wa sekta ya afya, mifugo, mazingira na wanyama pori wakati wa warsha ya kujadili Mpango Mkakati wa Usalama wa Afya (2017-21) katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko itokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu iliyofanyika Jumatatu Oktoba 16, 2017.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

RC RUVUMA APOKEA TAARIFA YA KAMATI YA KUCHUNGUZA MIGOGORO YA ARIDHI

$
0
0
Kamati ya kuchunguza migogoro ya ardhi iliyoundwa na ofisi ya katibu tawala mkoa wa Ruvuma imekabidhi ripoti hiyo kupitia Mwenyekiti wa kamati, ambaye pia ni katibu tawala wilaya ya songea,PENDO NDUMBARO amekabizi taarifa hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma dkt bilinith mahenge,baada ya kufanya kazi kwa miezi mitatu,

MAWAZIRI KUANZA KUAINISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

SERIKALI IMEWEKA MAZINGIRA BORA KATIKA UWEKEZAJI-HALOTEL

$
0
0
  Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala.
 Mkuu wa kitengo cha Mawsiliano kampuni ya simu za mkononi ya Halotel, Mhina Semwenda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Kusoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh
Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni
Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh

 KAMPUNI ya Simu ya Mkononi ya Halotel imesema kuwa serikali imeweka mazingira bora kwa wawekezaji kupitia vyombo vyake ambavyo vimefanya Halotel kupata mafanikio katika kutoa huduma ya mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi wa Halotel , Trieu Than Binh amesema Halotel imetimiza miaka miwili tangu ilivyoanzishwa mwaka jana Oktoba 15.
Amesema kuwa katika mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka miwili ni kuwa na wateja zaidi ya milioni 3.5  wanaotumia mtandao  huo katika mawasilino.

Than Binh, amesema kuwa katika miaka miwili ya utoaji huduma, wamefanya mapinduzi na mabadiliko makubwa katika sekta hiyo katika nyanja za Mawasiliano ikiwemo kuboresha miundombinu ya Mawasiliano, Mabadiliko katika Elimu, huduma za kifedha pamoja na kupunguza gharama za mawasiliano.

“Tangu tumeanza kutoa huduma kwa mwaka wa pili sasa idadi ya wateja imeendelea kuongezeka kwa kasi. Hii inatokana na huduma ambazo tumekuwa tukizibuni kwa pamoja na kuwekeza zaidi katika kutoa huduma bora na kuboresha miundombinu ya mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini.” Amesema

“Kwanza tunafurahishwa na Serikali kutokana na mazingira bora ya uwekezaji ambayo imeweka hadi sasa,  na pia mazingira mazuri ya ukusanyaji wa kodi kwa uwazi zaidi suala ambalo hata kwetu limeondoa usumbufu kwa kiasi kikubwa, kuzinduliwa kwa kituo cha ukusanyaji kodi kwa njia ya kielectroniki ilikuwa faraja kubwa kwetu na ndio maana tulikuwa miongoni mwa kampuni za kwanza za simu kujiunga na mfumo huo.”

Binh, amesema kuwa wamefurahi pia kuwa kampuni inayoongoza kwa kutoa ajira kwa Maelfu ya Watanzania ikiwa ni ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu moja na mia mbili 1200, na ajira zisizo za moja kwa moija zaidi ya Elfu Ishirini 20000 na kusema kuwa kutokana na uwekezaji ambao kampuni hiyo imeendelea kufanya wanaamini wataendelea kuongeza idadi ya ajira nchini.

Aidha Binh, aliongeza kuwa wanaamini bado wana nafasi kubwa zaidi ya kufanya uwekezaji na kubadili kabisa mfumo wa Mawasiliano nchini kwa kuanzisha njia mpya za mawasiliano kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi na kuwa kampuni itakayo ongoza katika utoaji wa huduma za Mawasiliano kupitia Tehama na Teknolojia ya Mawasiliano.

Amesema wanaelekea kuanzisha mtandao wa 4G LTE kwa wateja wetu wote wa Halotel, hatuta bagua maeneo tutafanya uwekezaji huu katika maeneo yote nchi nzima ili wateja wetu waweze kufurahia huduma bora za mawasiliano na kwa bei rahisi,” alisema na kuongeza, “Pia tunaangazia sekta ya elimu ambayo hadi sasa kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar Es Salaam, tumeweza kuanzisha mfumo wa kujisomea kwa shule za sekondari nchini kwa masomo ya Sayansi Mfumo ambao utapatikana bure kwa shule zote zinazotumia Mtandao wa Intaneti wa Halotel, Tumeanza na masomo ya sayansi na kadri muda unavyokwenda tutaangalia namna ya kuingiza masomo mengine, baada ya kukamilisha kutia saini Mkataba wa Maelewano kati yetu na Wizara ya Utawala bora TAMISEMI.

Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo

$
0
0
Vijana nchini wametakiwa kujiajiri kupitia kilimo badala ya kukimbilia nchi za nje kama njia ya mkato ya kutafuta maisha. Wito huo umetolewa na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi wakati akiyafunga rasmi maonesho ya siku ya chakula duniani yaliyofanyika kitaifa huko Kizimbani, Wilaya ya Magharibi A.

Amesema ni aibu kuona vijana wengi wa Kiafrika wanapoteza maisha baharini Mediterrania kwa safari za kwenda ulaya kutafuta maisha wakati Bara la Afrika lina fulsa nyingi za ajiri kupitia sekta ya kilimo. Akizunzungumzia kuhusu mikopo kwa wakulima wadogo wadogo Balozi Seif amezitaka taasisi za fedha nchini kutoa mikopo nafuu kwa wakulima hao kama hatua ya kuiunga mkono serikali ya kuongeza uzalishaji wa chakula hapa nchini.

Amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuazisha viwanda vidogo vidogo vinavyotumia mali ghafi ya kilimo kutoka hapa nchini jambo ambalo litawasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa wingi na kujiongezea kipato chao.

Kuhusu maonesho Makamo wa Pili wa Rais ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa maandalizi mazuri yaliyopelekea wananchi wengi wa Zanzibar kuhudhuria maonesho hayo. Amesema Serikali imejipanga kuyafanya maonesho ya kilimo hapa nchini kuwa endelevu na kuzitaka taasisi zinazohusika ikiwemo wizara ya Kilimo kuliendeleza eneo hilo la Kizimbani kwa kuweka miundo mbinu ya kudumu. 

Wakati huo huo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametowa zawadi ya kikombe kwa Jeshi la Kujenga Uchumi kwa kuwa mshindi wa Kwanza wa maonesho ya siku ya chakula duniani mwaka huu hapa Zanzibar.

Kutokana na ombi la wananchi wengi maonesho hayo ya kilimo yataendelea kwa siku moja zaidi ili kutoa nafasi kwa wananchi kufaidika na taaluma ya kilimo inayotolewa pamoja na kununua bidhaa mbali mbali za kilimo.

Aidha Serikali imekusudia kutoa fursa kwa wakulima kuuza bidhaa zao kila wiki katika eneo hilo la maonesho ili kutoa fursa kwa wakulima kuwapatia soko la uhakika.
Balozi Seif akiangalia zana za kilimo. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeongeza ununuaji wa zana za kisasa za kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Balozi Seif akipata maelezo kuhusu ufugaji wa mbuzi wa kisasa.

WAKAZI WA MWANZA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA HISA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Rai hiyo imetolewa jana na wataalam wa uwekezaji katika masoko ya dhamana na mitaji walipokuwa wakizungumza na wafanyabiashara, wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma Jijini Mwanza kwenye mjadala ulioandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa ushirikiano na Best Dialogue (Mpango wa Uboreshaji Mazingira ya Biashara nchini).

Mjadala huo ulilenga kuangalia fursa na changamoto za biashara zinazoikumba sekta binafsi na namna ya kuzitatua na kuwezesha ustawi wa biashara jijini Mwanza ili kuweza kufikia uchumi wa kati na viwanda.Mgeni rasmi katika mjadala huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Khadija Nyembo ambaye alisema kuwa Serikali iko tayari kuboresha mazingira ya kibiashara ili kufikia uchumi wa kati pamoja na Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akielezea umuhimu wa kuwekeza kwa njia ya hisa za jana Jijini Mwanza ambapo mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yalifanyika. 

Akizungumza katika mjadala huo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank ,Ibrahim Mwangalaba alitoa rai kwa wadau wa sekta binasfi, sekta ya umma na wakazi wa Mwanza kuwekeza katika ununuaji wa hisa za Maendeleo Bank ambazo zimeanza kuuzwa tangu Septemba 18 hadi Novemba 03 mwaka huu.Mwangalaba amesema hisa za benki hiyo zinauzwa kwa thamani ya shilingi 600 kila moja na kwamba kiwango cha chini ya ununuzi ni hisa 100 zenye thamani ya shilingi 60,000 hivyo wananchi wote wachangamkie fursa hiyo muhimu.
Wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma wakifatilia mkadala wa uboreshaji wa mazingira ya biashara ulioambatana na umuhimu wa kuwekeza kwa njia ya hisa ulioletwa na Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba pamoja na mshauri wa uwekezaji katika masoko ya mitaji Richard Manamba.

Tunauza hisa sokoni sasa na hisa hizi zinauzwa kwenye matawi yote ya benki ya CRDB ambapo tunaunga mkono juhudi za Rais wetu anayesema uchumi wa Tanzania umilikiwe na watanzania wenyewe na njia mojawapo ya kuwajumuisha watanzania wengi ni uuzaji wa hisa sokoni”. 

Amesisitiza Mwangalaba na kuongeza kwamba hisa hizo pia zinapatikana ofisi za TCCIA.Naye Mshauri wa Hisa, Richard Manamba amesema ununuzi wa hisa una faida nyingi ikiwemo wanunuzi kupata gawio la faida ambalo benki hulipata na kwamba hisa hizo huongezeka thamani kulingana na nguvu ya soko.Maendeleo Bank yenye mtaji wa shilingi bilioni 10 sokoni inaendelea kuongeza mtaji wake hadi kufikia shilingi bilioni 17 ambapo inatarajiwa kufungua matawi yake katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza.

AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MABATINI KOMBAINI KESHO JIONI

$
0
0


TIMU ya Azam FC, inatarajiwa kukipiga dhidi ya Mabatini Kombaini katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Alliance kesho Jumatano kuanzia Saa 10.00 jioni.



Kikosi cha Azam FC kipo hapa mkoani Mwanza tokea juzi, kikifanya maandalizi ya kuikabili Mbao, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.



Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu uliopita wanaodhaminiwa na Maji Safi ya Uhai Drinking Water, Benki Bora ya NMB na Tradegents, wanatarajia kuutumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wao na Mbao.

Hadi hivi wachezaji wote wa Azam FC wako fiti, isipokuwa kipa Razak Abalora, anayesumbuliwa na Malaria, ambaye leo ameanza mazoezi mapesi wakati kikosi hicho kilipofanya mazoezi ya asubuhi katika Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa Mwanza.


Kueleka mchezo wa Mbao, Azam FC imeonekana kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa ni miongoni mwa timu nne zilizokaa kileleni zote zikiwa na pointi 12, zingine zilizojuu yake zikiwa ni Simba, Yanga na Mtibwa Sugar, ambazo ziko juu yake kwa idadi ya mabao ya kufunga.

KIKAO CHA BARAZA KUU LA UWT TAIFA LEO DODOMA

$
0
0
  Katibu Mkuu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi akizungumza wakati wa Kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyi Taifa, kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017. Kulia ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Pereila Silima na katikati ni Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho Diana Chilolo. (Picha na Bashir Nkoromo)
 Mwenyekiti wa muda wa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo Taifa, Diana Chilolo, akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017.  Kushoto ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Pereila Silima na kulia ni Katibu Mkuu wa 
UWT Amina Makilagi. 
 Wajumbe wakishangilia wakati wa kikao wa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya ya wanawake Taizania (UWT) kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017
 Maofisa wa UWT wakiandaa makabrasha kabla ya kuanza kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyi Taifa, kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma akisalimia alipotambulishwa katika kikaocha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya ya wanawake Taizania (UWT) kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, (Picha na Bashir Nkoromo).

NAIBU WAZIRI SHONZA AHIDI KUSIMAMIA MAADILI YA MTANZANIA

$
0
0

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameahidi kushirikiana na Watendaji wa Wizara, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kusimamia maadili ya Mtanzania ili kuendelea kuwa na taifa bora.

Mhe. Shonza ameyasema hayo alipowasili katika ofisi za Wizara leo mjini Dodoma ambapo alipokelewa na Waziri mwenye dhamana Dkt. Harrison Mwakyembe, viongozi wa Wizara pamoja na  watumishi.

“Wizara hii ni muhimu sana kwa kuwa inajenga taswira ya taifa kupitia sekta zake ambazo ni Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo hivyo ntahakikisha tunashirikiana kwa karibu katika kuwatumikia wananchi “alisema Naibu Waziri Shonza.

Aliongeza kwa kueleza kuwa atahakikisha suala la maadili bora kwa jamii  linazingatiwa ili kuendelea kujenga taifa imara kwa kuzingatia mavazi yenye heshima na  nyimbo zenye kujenga.

Aidha, Naibu Waziri Shonza amesema ni wajibu wetu kama watumishi wa umma kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya chama tawala ambacho kiliahidi kuwatumikia watanzania ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa kwa wakati.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) baada ya kuwasili ofisini leo mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizra hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Millao.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili ofisini mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TATIZO LA UMEME MTWARA NA LINDI: MAFUNDI WA TANESCO WAFANIKIWA KUWASHA MASHINE MOJA

$
0
0

NA K-VIS BLOG, MTWARA

SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco), limefanikiwa kukarabati mashine namba 6 iliyokuwa imeharibika na kuiwasha kwa ajili ya kutoa huduma ya umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.

Hatua ya kuwashwa kwa mtambo huo ni juhudi za shirika hilo za kuimarisha hali ya upatikanaji umeme kwa wananchi kusini huku ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alipotembelea Kituo cha kufua umeme kwa gesi .

Akizungumza leo mjini hapa, Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Mhandisi Dk. Tito Mwinuka ambaye amepiga kambi mkoani humo pamoja na watalaamu wengine, alisema kuwa mitambo iliyokuwa ikifanya kazi ilikuwa minne lakini baada ya juhudi kubwa za wataalamu wa Tanesco hadi kufikia jana jioni wamefanikiwa kuwasha mashine hizo zenye uwezo wa kuzalisha Megawati 16.
Mafundi wakiratibu zoezi la ukarabati wa mshine .
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Tito Mwinuka, (wakwanza kushoto), na viongozi wengine wa Shirika hilo, wakifuatilia maendeleo ya ukarabati wa mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara leo Oktoba 17, 2017.
Mafundi wa TANESCO wakiendelea na ukarabati wa mshine.

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images