Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

//michuzi2.rssing.com/chan-7007653/article3901-live.html


maalim seif atembelea masoko unguja kujionea bei ya vyakula

0
0
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya maboga katika soko la Mombasa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia mboga mboga katika soko la Mombasa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya samaki katika soko la Mombasa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya nazi katika soko la Mwanakwerekwe, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo. Nazi moja inauzwa kati ya shilingi 200 hadi 400 (bei ya jumla).
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya muhogo katika soko la Mombasa, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo. Fungu la muhogo linapatikana kwa bei ya shilingi 1000 hadi 2000.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihoji bei ya muhogo katika soko la Mwanakwerekwe, wakati wa ziara yake ya kutembelea soko hilo. Fungu la muhogo linapatikana kwa bei ya shilingi 1000 hadi 2000.

Ajali ya Fuso na basi la Metro yaua mmoja na kujeruhi watu zaidi ya sita Moshi

0
0
Picha na habari naa Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii,Moshi 
 MTU mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja amefariki Dunia huku wengine sita wakijeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyotokea juzi usiku majira ya saa moja katika eneo la Kawawa wilayani Moshi. 
 Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC muda mchache baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha magari mawili likiwemo basi la abiria lijulikanalo kwa jina la Metro ambayo yaligongana uso kwa uso na Loli aina ya Fuso lililokuwa likielekea Dar es salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo  ilitokea baada ya dereva wa gari aina ya Fuso kujaribu kulipita Loli jingine aina ya Scania likiwa na trela lake kabla ya kukutana na basi la Metro lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Arusha ndipo magari hayo yakagongana uso kwa uso. 
 Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz alithibitsha kutokea kwa ajali hiyo huku akitaja namba za usajili wa magari yalihusika katika ajali hiyo kuwa ni basi la Metro aina ya Yutong lenye namba za usajili T 129 BQL likiendeshwa na Oscar na Fuso lenye namba za usajili T 615 AWB lililokuwa likiendeshwa na Goodluck Aseri.(45)lilikuwa likitokea Moshi kuelekea Njia panda Himo. 
 Kamanda Boaz alisema Dereva wa basi aliyefahamika kwa jina moja la Oscar alifariki dunia papo hapo huku kondakta na abiria wengie watano katika basi hilo walipata matibabu katika hosptali ya rufaa ya KCMC. 
 Alisema jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Dereva wa Fuso kwa maelezo zaidi na kwamba mara uchunguzi utakapokuwa umekamilika atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za usalama Barabarani.
 Muonekano wa mbele wa gari aina ya Fuso baada ya kugongana uso kwa uso na basi a Metro baada ya kile kilichosemekana kuwa ni kupata hitilafu katika mfumo wa breki.
 Gari aina ya Fuso ikipakia mizigo iliyokuwa katika gari lililopata ajali baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Metro na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
 Sehemu ya mabaki ya gari aina ya Fuso.
Dereva wa Fuso aliyefahamika kwa jina la Goodluck Aseri akiwa amelazwa katika hospitali ya KCMC akiwa na pingu mkononi.

madiwani Lindi wacharuka kuhusu gari lililo gereji kwa miaka mitatu

0
0
Na Abdulaziz Video, Lindi
Halmashauri ya wilaya ya Lindi, inaandaa taratibu za kuiburuza Mahakamani  Gereji ya Auto Works Service ya Jijini Dar es salaam,kwa madai ya kuendelea kuishikilia gari yake, huku tayari ikiwa imeshalipwa fedha zote zilizokuwa ni ghalama za matengenezo yake. 
 Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Grace Mbaruku,katika kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani,lililofanyika hivi karibuni . 
 Mbaruku ametoa kauli hiyo,alipokuwa akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa madiwani hao, waliotaka kufahamu hatua iliyofikiwa juu ya gari lao aina ya Toyota Cruser STJ 1826 iliyopelekwa gereji hiyo,kwa matengenezo na kuzuiwa na mzabuni huyo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa akidai alipwe fedha zaidi. 
 Aliwaambia madiwani hao kwamba gari hiyo ilipelekwa gereji hiyo ya Auto Works Service kwa gharama ya Sh,19,446,400/-lakini matengenezo ambayo yamefanyika hadi kutembea yamefikia kiasi cha Sh,7,038,700/-ambacho tayari kimelipwa kupitia LPO Namba 001167. 
 “Kama ni fedha za matengenezo tayari ameshalipwa,lakini bado mzabuni huyu anaendelea kuizuia gari huku akitaka hadi alipwe Sh,19,446,400/-huku tayari fedha halali kwa kazi iliyofanyika ameshalipwa,,,,,,,,,,,sijui jeuri hii anaipata kutoka wapi?”Alisema Mbaruku. 
 Pia,mkurugenzi huyo mtendaji amesema kutokana na mzabuni huyo kuendelea kuishikilia gari hiyo hadi alipwe fedha hizo, Yaonesha anataka kuiibia Halmashauri yake kiasi cha Sh,12,407,700/-ikizingatiwa tayari imeshamlipa kulingana na kazi aliyokuwa ameifanya. Mkurugenzi huyo akasema kinachomsikitisha ni pale mzabuni huyo hataki kuikabidhi gari hilo,kwa madai kuwa bado anaidai fedha Halmashauri hiyo. 
 Akasema kutokana na kitendo cha mzabuni huyo kuendelea kuizuia gari hiyo,uongozi wa Halmashauri umeamua kuwasiliana na mwanasheria wake ili mzabuni huyo aweze kuchukuliwa hatua za kisheria. 
 Baada ya maelezo hayo,madiwani kwa kauli moja wamemtaka mkurugenzi huyo,kuharakisha taratibu za kuwasiliana na mwanasheria ili gari hiyo STJ 1826 likachukuliwe kwa Mwenye gereji hiyo haraka ili kusaidia shughuli za kiutendaji 
 Awali diwani wa kata ya Longa,Abdu Mjenga (CCM) aliitaka halmashauri hiyo kutoa taarifa kwa madiwani kuhusiana na gari hiyo iliyopelekwa kwenye gereji hiyo kwa muda mrefu bila ya wao kutopatiwa maendeleo na mrejesho wake huku wakijua imelipiwa matengenezo yake.
 Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Bi. Grace Mbaruku, akiongea katika kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani,lililofanyika hivi karibuni .
Mmoja wa madiwani akichangia katika baraza hilo

KUMBUKUMBU

0
0
FAMILIA YA DANI MAFURU WA DUBAI LEO TAREHE 15. JULY. 2013.WANAKUMBUKA MSIBA WA MAMA YAO MPENDWA ELIZERBERTH CHILLIKO  LEO IMETIMIA MIAKA MITATU TANGU ALIPOTENGANA NASI KWA MAPENZI YAKE MOLA.
UNAKUKUMBUKWA SANA MAMA NA WANAO, WAJUKUU, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI. WEWE UMETANGILIA MWENYEZI MUNGU AKUREHEM .
AMINA.

MAJAMBAZI YAPORA NA KUJERUHI WILAYANI KILWA

0
0
Na Abdulaziz video,Lindi
Majambazi sita wakiwa na mapanga, nondo na marungu, wamevamia nyumba ya katibu wa Chama cha Ushirika cha Msingi ktk kijiji cha Zinga
kilichoko Tarafa ya Pande wilaya ya Kilwa Mkoani lindi na kupora zaidi
ya shilingi milioni 22 baada ya kumpiga na kumjeruhi vibaya katibu
huyo.

Tukio hilo limetokea wakati katibu huyo akiwa amelala nyumbani kwake
ambako pia alikuwa amezihifadhi fedha hizo mali ya Kampuni binafsi ya
OLAM Ltd alizokabidhiwa kwa ajili ya kununulia ufuta kutoka kwa
wakulima nje ya utaratibu wa stakabadhi ghalani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi Gerge Mwakajinga amethibitisha
tukio hilo na amemtaja katibu huyo aliyejeruhiwa kuwa ni Omari
Kindamba na amelazwa ktk hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje na hali
yake inaendelea vizuri.

Hata hivyo Kamanda huyo amewataka wakulima wa ufuta na wafanyabiashara wanaokwenda vijijini na fedha nyingi na kuziacha kienyeji ktk maeneo ya makazi kwa wananchi kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa  fedha hizo pamoja na watu wanaowaachia kwa ajili ya kununulia ufuta

Kwa takriban miaka 3 iliyopita kufuatia ununuzi kufanywa kupitia mfumo
wa stakabadhi ghalani hakukuwepo tatizo la majambazi hali ambayo
ujitokeza nje ya mfumo huo ambapo Bw Said Juma mkazi wa Kilwa alieza
kuwa kwa mawazo yake  huenda wizi/Ujambazi huo utokea kwa kupangwa na makampuni ya wahindi ili waweze kudai Bima huku pesa inayoibiwa ikiwa tofauti na inayodaiwa  Bima

JOSE CHAMELEONE NA ERICA WALIVYOFUNIKA OAKLAND -CALIFORNIA

JK atembelea kambi ya kusaidia walemavu wa kusikia leo

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ametembelea kambi ya kusaidia watu wenye ulemavu wa kusikia katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam asubuhi hii.  Zaidi ya Watanzania 3500 wenye maradhi ya kusikia wanatarajiwa kunufaika kwa huduma ya tiba inayotolewa hiyo Taasisi  hiyo ya Starkey Hearing Foundation yenye makao yake jijini Washington nchini Marekani.
Muasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing foundation Bwana Bill Austin  Starkey amesema tayari huduma hiyo imeshatolewa katika hospitali ya Seliani mjini Arusha baada ya kutoa huduma hiyo katika miji ya Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Nimefurahishwa sana na kutiwa moyo kwa kazi tuliyoifanya ya kuwahudumia watu na kuwawezesha kusikia ambapo wengine ndiyo wameweza kusikia kwa mara ya kwanza tangu walipozaliwa.Furaha yao ni kitu cha kutia moyo sana katika juhudi zetu.
Madaktari wa kitanzania walioshirikiana nao wamefanya kazi kubwa na nzuri” alisema Bwana Starkey ambaye ameambatana na timu ya wataalamu na watu mashuhuri kutoka nchini Marekani ambao wametoa misaada mbalimbali kugharamia kampeni hiyo.
 
 
 
 
 
 
 
 


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda amaliza ziara yake ya kikazi mkoani njombe.

0
0
 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza katika majumuisho ya ziara yake  ziara ya mkoa wa Njombe, Julai  14, 2013.  Kulia  ni  Mkuu wa mkoa wa Njombe, Kapteni Msangi. Na wa wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Deo sanga.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza wakati Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda alipopokea taarifa ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwasili kwenye Ikulu Ndogo ya Songea kwa ziara ya siku nane mkoani humoJulai 14,2013.Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu. 
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza wakati Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda alipopokea taarifa ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwasili kwenye Ikulu Ndogo ya Songea kwa ziara ya siku nane mkoani humoJulai 14,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mkuu wa wilaya ya Njombe, Sarah Dumba baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Njombe Julai 14, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Spika wa Bunge la Korea afanya ziara Nchini Tanzania.

0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Kusini wiki iliyopita alihitimisha  ziara ya siku tatu hapa nchini aliyoianza tarehe 8 hadi 10 Julai 2013 ambapo alikutana na viongozi wakuu wa Taifa. Awali alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda. Spika huyo pia akiambatana na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai aliizuru Zanzibar na kukutana na  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohammed Shein na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho. 

Katika mazungumzo waliyofanya, jambo lililojikeza na kupokelewa kwa mtizamo chanya ni lile la Tanzania kufungua Ubalozi nchini Korea. Pichani Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda wa nne kushoto na Spika wa Bunge la Korea Mhe. Kang Chang-Hee wa nne kulia wakiendesha mkutano baina yao na wabunge wa nchi zote mbili ulifanyika jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa mkutano kwa upande wa Tanzania
 Picha ya pamoja ya viongozi hao baada ya mkutano ambao baadhi ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na Korea kuuwekeza hapa nchini katika Nyanja ya TEHAMA.
 Spika Makinda akimkabidhi mgeni wake zawadi mara baada ya chakula cha jioni.
 Spika Kang akipokelewa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. A.P. Kificho mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein (kulia) akiwa na mazungumzo na Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee (kushoto). Katikati ni mkalimani.
 Picha ya pamoja kwenye Ikulu ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) wakati wa ziara ya Spika wa Korea visiwani Zanzibar.
Spika wa Bunge la Korea Kusini Mhe. Kang Chang-Hee akiushukuru ujumbe wa Tanzania kwa heshima kubwa mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini. (Na Prosper Minja - Bunge).

DRFA yaipongeza Friends Rangers

0
0
 Viongozi wa Friends Rangers wakimhudumia mchezaji wao aliyefunga bao la kwanza jana, Robert Katabi aliyeumia baada ya kufunga bao hilo jana katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Polisi Jamii kwenye Uwanja wa Azam Complex.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya (wa kwanza kushoto), akifuatilia mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam dhidi ya Polisi Jamii ya Mara iliyochezwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex. Rangers walishinda mabao 3-1 na kufuzu Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
========  =====  =======
DRFA yaipongeza Friends Rangers
 
CHAMA ya Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimeipongeza timu ya Friends Rangers kwa kufuzu kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao baada ya jana Jumapili kuifunga Polisi Jamii ya mkoani Mara mabao 3-1.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 6 kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma, Polisi waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Katika mechi ya marudiano iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam na kuchezeshwa na mwamuzi Hans Mabena kutoka Tanga, Rangers walipata mabao yao kupitia kwa Robert Katabi katika dakika ya 53, Bakari Bakari dakika ya 67 na Mick Castro dakika ya 87.
 
Bao la Polisi lilifungwa na Faustine Faru katika dakika ya 68 na hivyo kuipa tiketi ya Friends Rangers kufuzu kucheza Daraja la Kwanza kwa jumla ya mabao 3-2.

Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, amesema ni faraja kwao kuona Friends Rangers imetinga Ligi Daraja la Kwanza na kuuwakilisha vyema Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kwa niaba ya DRFA nachukua fursa hii kuwapongeza wachezaji, viongozi na mashabiki wa Friends Rangers kwa uvumilivu na subra waliyokuwa nayo katika kipindi chote cha ushiriki wa Ligi ya Mabingwa wa Mkoa, bado tupo pamoja nao katika kufanikisha timu hiyo inafanya vizuri zaidi na hatimaye kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema Mharizo.

Friends Rangers inaungana na Kimondo FC ya Mbeya na Stand United ya Shinyanga kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

Wawakilishi wengine kutoka Mkoa wa Dar es Salaam katika Ligi ya Mabingwa wa Mikoa walikuwa Red Coast na Abajalo ambazo ziliaga michuano katika hatua za awali.

RAIS KIKWETE KATIKA SHUGHULI YA UTOAJI VIFAA VYA KUONGEZA USIKIVU KWA WALEMAVU WA KUSIKIA JIJINI DAR LEO

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mmoja wa wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni akiwa na  mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni baada ya kupatiwa vifaa na  mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni  alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Sholloh Challi, katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa mstaafu,  alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013.PICHA NA IKULU. 

JK ATETA NA UONGOZI WA BENKI YA MAENDELEO YA TIB

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya TIB uliofika
Ikulu kumwelezea Rais Kikwete mipango na mikakati kabambe ya kuijenga upya benki hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Tanzania Investment Bank (Benki ya Rasilimali Tanzania) ikiwa ni pamoja na vitega uchumi. miundo mbinu na upanuzi wa wigo wa biashara.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Peter Noni, Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 13, 2013. Bw. Noni na ujumbe wake walifika Ikulu kumwelezea Rais Kikwete mipango na mikakati kabambe ya kuijenga upya benki hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Tanzania Investment Bank (Benki ya Rasilimali Tanzania) ikiwa ni pamoja na miundo mbinu na upanuzi wa wigo wa biashara.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Peter Noni, Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 13, 2013. Bw. Noni na ujumbe wake walifika Ikulu kumwelezea Rais Kikwete mipango na mikakati kabambe ya kuijenga upya benki hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Tanzania Investment Bank (Benki ya Rasilimali Tanzania) ikiwa ni pamoja na miundo mbinu na upanuzi wa wigo wa biashara.


JK ashukuru taasisi ya Starkey Hearing Foundation kwa kusaidia walemavu wa kusikia

0
0
Rais Jakaya Kikwete akiishukuru taasisi ya Starkey Hearing Foundation kwa kusaidia vifaa vya kusaidia usikivu kwa walemavu wa kusikia leo July 15, 2013 jijini Dar es salaam

KIJIWE CHA UGHAIBUNI KUWA HEWANI JUMANNE JULY 23, 2013

0
0
 Kipindi chako ukipendacho cha Kijiwe cha Ughaibuni kitaanza kurushwa tena kuanzia Jumanne wiki ijayo July 23, 2013 kipindi hiki kilisimama kutokana na pilikapilika ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani. Vijimambo inaomba radhi kwa wadau na masahabiki wa kijiwe cha ughaibuni kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa kutorusha kipindi hiki.
 Juu na chini ni kruu nzima ya kijiwe ikitafakari jambo

Article 2

KIJIWE CHA UGHAIBUNI KUWA HEWANI JUMANNE JULY 23, 2013

0
0
 Kipindi chako ukipendacho cha Kijiwe cha Ughaibuni kitaanza kurushwa tena kuanzia Jumanne wiki ijayo July 23, 2013 kipindi hiki kilisimama kutokana na pilikapilika ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa Kiswahili Marekani. Vijimambo inaomba radhi kwa wadau na masahabiki wa kijiwe cha ughaibuni kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa kutorusha kipindi hiki.
 Juu na chini ni kruu nzima ya kijiwe ikitafakari jambo

Video za Ramadhan:Matengenezo ya Msikiti wa Makkah

0
0
Asalaam Alaikum & Ramadan Rakeem.

Katika mwendelezo wa video za Ramadhani. Hii video inaonyesha matengenezo yanayoendelea kwenye Mzunguko wa Kaaba, ndani ya msikiti mkuu wa Makka ambao unaendelea ili kukidhi ongezeko la mahujaji (milioni 6 huzunguka hapo at a time)

Historia fupi ni kuwa hiyo Kaaba ndiko waislam wote duniani huelekea wakisali na ilijengwa na Nabii Adam na kisha kuendelezwa na Nabii Abraham (Ibrahim) kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu.

Kutokana na ongezeko la watu sehem ya kufanya Tawaf (Kuzunguka mara 7) kama alivyofanya Adam, kuna matengenezo/renovation inafanywa kukidhi idadi ya watu na ndio moja kati ya sababu idadi ya mahujaji imepunguzwa mwaka huu

Pia ndani ya huo msikiti ipo sehem ambao Mke wa Nabii Ibrahim, Hajar (Hagar) alikuwa anakimbia kati ya milima miwili (Safa & Marwa) wakati alipokuwa anamtafutia maji mwanae hivyo hiyo milima imekuwa icorporated ndani ya msikiti mkuu na inabidi nayo kuzuka mara 7 kama alivyofanya Hajar.

Mwenye maelezo zaidi anaweza kutoa kwenye comments.

 Nakutakieni Saum njema na yenye subra na utulivu.

UZINDUZI WA UPIMAJI AFYA MAKAO MAKUU YA BENKI YA CRDB, DAR ES SALAAM

0
0
  Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei akizungumza wakati wa uzinduzi wa upimaji wa Afya , zoezi litakalo endeshwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA), kwenye matawi ya benki hiyo nchi nzima.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA) Dr. Akwilina Kayumba akielezea jinsi zoezi hilo litakalofanyika kwa wafanyakazi wa benki ya CRDB kwenye matawi yake yote nchi nzima, ikiwa ni mpango wa kuhakikisha wafanyakazi wanafanyakazi katika mazingira salama.
 Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB Dkt Charles Kimei akifanyiwa vipimo wakati wa zoezi la uzinduzi wa upimaji Afya kwa wafanyakazi wa benki ya CRDB, kwenye ofisi za makao makuu ya benki hiyo Jijini Dar es salaam
Madaktari toka OSHA wakichukua maelezo toka kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB, ikiwa ni mwanzo wa zoezi la upimaji Afya kwa wafanyakazi zaidi ya 2000 wa Benki ya CRDB ambao wanatarajiwa kupimwa Afya zao( Fitness to work) hivi karibuni kwenye matawi yote.

BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA LAANI VIKALI SHAMBULIO DHIDI YA WALINZI WA AMANI HUKO DARFUR

0
0
Na Mwandishi Maalum
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  limelaani vikali shambulio lililofanywa dhidi ya walinda Amani wa Tanzania katika  UNAMID, na limetaka uchunguzi wa kina ufanyike.
Taarifa ya Baraza hilo ambalo ndilo lenye dhamana Kuu ya usimamizi wa Amani ya kimataifa na  jukumu la  kuidhinisha  Misheni zote za ulinzi  wa Amani za Umoja wa Mataifa, imetolewa kwa niaba ya  Baraza  na Marekani ambaye ni Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa  Julai.
Taarifa inasema, Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama  wanalaani  kwa nguvu zao   zote mashambulizi yaliyofanyika Julai 13  na  watu wasiojulikana dhidi ya  walinzi wa Amani wa  UNAMID huko Darfur,  waliokuwa katika  doria  katika  eneo la Magharibi ya Nyala Kusini mwa Darfur   na kusababisha vifo vya walinzi  wa Amani  Saba , majeruhi 17, akiwamo  Polisi  huku hali za    majeruhi wawili kati yao ikielezwa kuwa ni  mbaya.
Wajumbe wa Baraza la Usalama Kuu wanatoa salamu zao za rambirambi kwa familia za walinzi hao wa Amani waliopoteza  maisha katika shambuli hilo, na pia  kwa Serikali ya Tanzania na kwa  UNAMID.
Baraza Kuu  la Usalama  limeitaka Serikali ya Sudan kufanya uchunguzi wa kina  juu na tukio hilo na kuwafikisha  mbele ya mkono wa sheria wale wote waliohusika.
Taarifa hiyo inaeleza zaidi kwamba. Baraza Kuu la Usalama ,  limeonyesha  wasiwasi wake  kuhusu mazingira ya shambulio hilo, moja ya   shambulio baya  kuwahi   kufanyika  dhidi ya walinzi wa UNAMID tangu kuanzishwa kwake.
Baraza Kuu la Usalama katika taarifa yake hiyo limesisitiza kwamba shambulio au vitisho vya aina yoyote dhidi ya  UNAMID havikubaliki. Na limetaka kutojirudia tena kwa  tukio kama hilo.
Vile vile Baraza Kuu la Usalama  limerejea  msimamo wake  kwamba linaunga mkono kwa kauli moja Misheni ya kulinda Amani ya UNAMID na  limetoa wito kwa pande zote huko Darfur  kushirikiana na   Misheni hiyo.
Wakati huo huo, kufuatia tukio hilo la kusikitisha, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa  Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, amekuwa akipokea kwa niaba ya serikali na familia, salamu za pole   kutoka kwa Mabalozi wenzake.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images