Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

ajali ya lori yazua foleni kubwa daraja la mto wami leo

0
0
Lorry la mizigo limeanguka karibu na daraja la Mto Wami na kusababisha foleni ndefu sana na usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii ya Dar-Moshi-Arusha
 Kabla ya ajali hiyo


ankal akutana na wadau wa globu ya jamii wa TMA monduli, arusha

0
0
 Ijumaa hii Ankal alitembelea Chuo cha Maafisa wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (Tanzania Military Academy - TMA) huko Monduli, Arusha, na kukutana na baadhi ya wadau wakubwa wa Globu ya Jamii ambao wapo chuoni hapo wakibukua. Ankal alifarijika sana kukuta kuwa hata maafande sio tu ni wafuatiliaji wakubwa wa Libeneke hili bali pia walimshauri aendelee kuheshimu maadili pamoja na sheria na kanuni za taaluma ya habari, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuepuka kujeruhi hisia za mtu ama watu, jambo ambalo wametaja kuwa ni moja ya siri za mafanikio haya kiasi yaliyopatikana.
Ankal akiwakumbusha wadau hao wa TMA kuwa Septemba 8, mwaka huu Globu ya Jamii itasherehekea miaka tisa toka izaliwe kule Helsinki, Finland, na akawakaribishwa kwenye sherehe za kukata na shoka ambazo zinaandaliwa. Stay tuned...Libeneke Oye!

wana paselepa mwenge jazz band bado waendeleza libeneke

0
0
Wakongwe Mwenge Jazz band 'Wana Paselepa' wakitumbuiza katika sherehe za kutunuku kamisheni kwa maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Chuo cha Maafisa wa Kijeshi (TMA) huko Monduli, Arusha, Ijumaa hii. Ankal alifurahi sana kuona kuwa kaka zake wakina Majaliwa (wa tatu kushoto, ambaye ana sauti kama ya TX Moshi William) bado wako juu. Bendi hii ya jeshi ni kiungo muhimu katika kuendeleza uhusiano mwema kati ya rais na askari, na unapowakuta katika kumbi za wananchi wakiwa wamevaa kiraia na kujichanganya huwezi kuamini kwamba walio jukwaani ni askari wa JEYWII.

UZINDUZI WA JARIDA LA ONSPOT MAGAZINE

0
0
 Mgeni rasmi, Mbunge wa Kigamboni, Mh. Dr. Faustine Ndugulile akiongea machache kwenye uzinduzi huo usiku wa kuamkia leo jijijni Dar es salaam. Jarida la Onspot  Magazine zamani ilijulikana kama Teenspot.Magazine
 Mkurugenzi wa Onspot Magazine Nd. Amin Swai akiongea na waandishi
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.
Kwa maelezo zaidi BOFYA HAPA

Rais wa Zanzibar Dr Ali Shein Akutana Kwa Mazungumzo na Waziri wa Uingereza wa masuala ya Afrika

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Waziri wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Bw.Mark Simmonds,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya mazungumzo yao 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Waziri wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Bw.Mark Simmonds,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Waziri wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Bw.Mark Simmonds,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Picha na Ramadhan Othman,ikulu-Zanzibar

wilaya ya Lindi yasitisha mikataba ya ujenzi wa barabara kwa makampuni matatu

0
0
Na Abdulaziz Video,Lindi

Halmashauri ya wilaya ya Lindi imesitisha mikataba ya ujenzi wa barabara kwa makampuni matatu yaliyopewa tenda za kujenga barabara zenye jumla ya urefu wa km 65.2 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011/13.

Hayo yamebainishwa na mhandisi wa ujenzi,Halmashauri ya wilaya Lindi,Aswile Mwasaga alipokuwa akizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea ofisini kwake kufutia kikao cha baraza la madiwani kulalamikia utendaji mbovu wa kazi kwa baadhi ya wakandarasi wanaopewa tenda za Ujenzi katika halmashauri hiyo.

Mwasaga alisema kuwa halmashauri imesitisha mikataba hiyo kwa baadhi ya wakandarasi kwa sababu ya utendaji wao mbovu na kutozingatia muda wa kazi na kusababisha miradi hiyo kuchelewa kukamilika kwa wakati uliopangwa na kujengwa chini ya kiwango kilichokusudiwa.

Aswile Aliyataja makapuni hayo kuwa Mwombe Company Ltd iliyopewa barabara za Rutamba,Mnara,Nyengedi,17.7Milola Kiwawa km12,na Steven Roadwork barabara ya mipingo,Mnyangara,km 8.5, na Mkwajuni, Namkongo Km 19.

Alisema kampuni nyingine ni Montanga Constraction iliyopewa kazi katika barabara ya Nachunyu,Mmumbu yenye km 8.

Aidha Aliongeza kuwa kuna makampuni mawili ambayo Bhavik constraction na Macroteck yamechelewesha kazi na kupewa adhabu ya kusimashwa kwa muda.

Kufuatia hali hiyo tuliwasiliana na mkurugenzi wa kampuni ya Bhavik Constraction Hitesh Mehta ambae alisema kuwa alisimamisha kazi hiyo kutokana na mvua nyingi zilizokuwa zinanyesha hapo awali lakini baada ya mvua kukatika kazi inaendelea na utekelezaji wake umefikia asilimia 90 ya kazi aliyopewa na kwa kiwango bora kwa mujibu wa mkataba

Vituo vya watoto waishio katika mazingira magumu kunufaika msimu wa ramadhan

0
0
Rais Mstaafu Mh.Ali Hassan Mwinyi,akikabidhi sabuni na vitabu kwa mmoja wa watoto yatima kati ya 700 wa madrasa kisarawe,wakati wa futari ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,walioambatana na Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Foundation Hassan Saleh(kulia)kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi Milion 50 kwa ajili ya kipindi hichi cha Ramadhan.
Rais Mstaafu Mh.Ali Hassan Mwinyi,akikabidhi Mbuzi kwa mmoja wa watoto yatima kati ya 700 wa madrasa kisarawe,wakati wa futari ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi Milion 50 kwa ajili ya kipindi hichi cha Ramadhan.
Rais Mstaafu Mh.Ali Hassan Mwinyi,akimsikiliza Mwenyekiti wa bodi wa Vodacom Foundation Hassana Saleh,akimfafanulia jambo wakati wa futari na baadhi ya watoto yatima kati ya 700 wa madrasa kisarawe,iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi Milion 50 kwa ajili ya kipindi hichi cha Ramadhan.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwapa vyakula baadhi ya watoto wa madrasa wanaoishi katika mazingira magumu kisarawe Pwani wakati wa futari iliyaoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom iliyotenga kiasi cha shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuudhuriwa na Mgeni rasmi Rais Mstaafu Mh.Ali Hassan Mwinyi hayupo pichani.

TAARIFA TOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI


TAHA yafungua rasmi ofisi zake za Zanzibar

0
0
Taasisi kilele ya TAHA inayoundwa na wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha 'horticulture' nchini Tanzania hatimaye imefungua rasmi ofisi zake kuu katika visiwa vyenye marashi ya karafuu Zanzibar. 

Ufunguzi wa ofisi hizo zilizo mtaa wa Kikwajuni kwenye Jengo la mfuko wa barabara ulitanguliwa na ziara fupi ya kutembelea maeneo ambayo Taasisi hiyo imeanzisha mashamba darasa na kusajili vikundi vya wakulima ili waweze kufaidika kwa karibu zaidi na ushauri wa kiufundi katika masuala ya kilimo cha 'horticulture' hali kadhalika masoko ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi wa TAHA akiteta Jambo na Mtaalamu wake kwa upande wa Visiwani Mzee Biwi wakati alipotembelea moja ya mashamba ya tikiti maji ya wakulima ambao ni wanachama wa TAHA.
Wataalamu kutoka Finland ambao ndio wawezeshaji wa shughuli za TAHA Zanzibar wakitazama moja ya shamba la Matikiti maji la moja ya vikundi wanachama wa TAHA.
Hili ni soko la Darajani Zanzibar, ni baadhi tu ya maeneo ambayo bidhaa za wakulima wa horticulture Zanzibar upelekwa na kuuzwa kwa ajili ya kukizi haja za soko la ndani.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Waziri wa habari Utamaduni Utalii na Michezo akutana na wawekezaji toka china

0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya huduma za usafiri ya China (CITS) Zou Wang Sheng (mwenye fulana nyekudu) kushoto ya Sheng ni Balozi mdogo wa China Madam Chen huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya huduma za usafiri ya China (CITS) Zou Wang Sheng baada ya mazungumzo yao huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.PICHA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

anaswa kwa kudaiwa kuuza tiketi feki uwanja wa Taifa.

0
0
 Mtu mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja akiwa amekamatwa na mmoja wa Polisi waliokuwa nje ya uwanja wa Taifa wakiangalia usalama,kwa kudaiwa kuuza tiketi feki za mechi ya jana iliyozikutanisha timu ya Taifa Stars dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda The Crane's,kwenye mchezo wao wa kuwania kufuzu michuano ya Afrika ya wachezaji wa ndani (CHAN).
 Baadhi ya wateja walionunua tiketi hizo zilizodaiwa kuwa ni feki wakizirejesha na kutaka fedha zao zirudishwe kwa mtuhumiwa huyo aliyewekwa chini ya Ulinzi .Aidha hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari vilieleza kuwa Askari Polisi ndio wanaohujumu mapato ya Uwanja wa Taifa.

NEWS ALERT: Askari 7 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wameuawa huko Darfur,Sudan

0
0
Askari saba wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wameuawa katika shambulizi la kuvizia huko Darfur, magharibi mwa Sudan.

Tukio hilo la Jumamosi limetajwa kuwa baya zaidi katika historia ya miaka mitano ya kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kijulikanacho kama UNAMID. Kaimu Msemaji wa UNAMID Christopher Cycmanic amesema hujuma hiyo ilIjiri katika kituo cha walinda amani cha Manawashi kaskazini mwa Nyala mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini.

Ameongeza kuwa askari wa UNAMID walishambuliwa na kundi la watu wenye silaha ambao hawakuweza kutambulika wakati huo. UNAMID haijatangaza uraia wa maafisa waliouawa lakini wanaosimamia amani katika eneo hilo ni askari kutoka Tanzania.

Kati ya waliopoteza maisha ni wanawake wawili wanaohudumu kama polisi wa kulinda amani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon amelaani vikali shambulizi hilo dhidi ya UNAMID. Ametoa wito kwa serikali ya Sudan kuchukua hatua za haraka kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.

Mji wa Nyala ambao ndio mkubwa zaidi katika eneo la Darfur umekumbwa na tatizo la ukosefu wa usalama katika siku za hivi karibuni.

MWILI WA MAMA MWANAMUZIKI PROF JAY WAAGWA NYUMBANI MBEZI MWISHO,KUZIKWA JIONI HII KINONDONI

BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA WAKE MJINI ZANZIBAR

0
0
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB ya Benki, TullyEsther Mwambapa akizungumza katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake.
 Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Machano Othman Said akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha wateja wa benki ya CRDB iliyofanyika mjini Zanzibar.
 Wadau mbalimbali wakipata futari.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakijumuika pamoja.
Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB katika hafla ya kufuturisha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWASILI ABUJA KUHUDHURIA MKUTANO WA 12 WA AFRIKA WA KUJADILI UGONJWA WA UKIMWI, MALARIA, KIFUA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais wa Nigeria, Isaiah Balat, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikwe, jiji Abuja leo Julai 14, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano Mkuu wa 12 wa Afrika unaojadili Magonjwa ya Ukimwi, Malaria, Kifua Kikuu na Magonjwa mengine ambukizi, unaotarajia kuanza kesho Julai 15 na kumalizika Julai 16. Kushoto ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais wa Nigeria, Isaiah Balat, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikwe, jiji Abuja leo Julai 14, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano Mkuu wa 12 wa Afrika unaojadili Magonjwa ya Ukimwi, Malaria, Kifua Kikuu na Magonjwa mengine ambukizi, unaotarajia kuanza kesho Julai 15 na kumalizika Julai 16. Nyuma yao ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal. Picha na OMR

MWANAFUNZI IFM KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KINONDONI, NI WENDE LWENDO ALIYEKUFA MAJI

0
0
Na Father Kidevu Blog
MAZISHI ya Mwanafunzi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi AIESEC- IFM, Wende Lwendo wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefariki juzi kwa kufa maji baharini yanafanyika kesho.

Wende , alifariki katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni jijini Dar es Salaam akiogelea na wenzake watatu majira ya jioni baada ya kumaliza mitihani yao ya kufunga mwaka wa masomo.

Kaka wa marehemu, Sammy Lwendo ameiambia Father Kidevu Blog leo kuwa marehemu anataraji kuzikwa kesho alasiri katika makaburi ya Kinondoni na mipango yote ya mazishi inaendelea vizuri.

Lwendo amesema kuwa mipango ya mazishi ilikuwa ikisubiri wazazi wa marehu ambao waliwasili juzi usiku wakitoakea mkoani Arusha na kutaarifu ndugu kuwa mazishi yatafanyika Dar es Salaam.
"Marehemu Wende, anataraji kuzikwa Makaburi ya Kinondoni kesho  lakini kabla ya mazishi kutakuwa na ibada itakayofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, "alisema Lwendo.

Lwendo amesema ibada hiyo itaanza majira ya saa 8:00 mchana ambapo pia ndugu jamaa na marafiki watapata wasaa wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Wende.

Mmmoja wa wanafunzi wa IFM, Ester Boswell, ambaye walikuwa wakishi chumba kimoja na marehremu huko Kigamboni ameelezea msiba huo kuwa ni pigo chuoni kwao na kwake kwani Marehemu alikuwa ni rafiki yake mkubwa si chuoni lakini hata kabla hawaja jiunga na chuo hicho.

Boswell amesema kuwa Marehemu alikuwa ni Rais wa taaasisi ya Wanafunzi wa IFM ijulikanayo kama AIESEC na alikuwa mhim,ili mkubwa wa taasisi hiyo.

Aidha amesema kuwa hadi sasa binafsi haamini kifo cha Wendi, huku akielezea kuwa Marehemu alikuwa ni mtu mcheshi na kuogelea ilikuwa ni moja ya vitu vikubwa anavyo vipenda.

"Marehemu alikuwa mpenzi kumbwa sana wa kuogelea na siku zote alikuwa anapenda kwqenda kuogelea na hata anapokuwa mpweke hosteli huamua kwenda Beach kuogelea na siku ya tukio aliniaga kuwa anaenda kuogelea na wanafunzi wengine wakiwapo wazungu ambao wapo katika kubadilishana uzoefu wa kimasomo," alisema Boswell.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam ukisubiri maziko.

Askari traffic na mwendesha vespa zenji: nani mwenye makosa?

0
0
Mambo vipi Ankal, 
naomba hii video uiweke kwenye blog yako kwani imenisikitisha sana kuona polisi anavyochukua hatua mikononi mwake na kutumia kazi yake kunyanyasa raia. Video hii nimetumiwa na ndugu yangu ambaye aliirikodi kwa simu yake na kunirushia mimi huku nilipo na mimi nikaamua kuitia katika YouTube , lakini nikaona kwa kuwa blog yako inatembelewa na watu wengi duniani nikaona itakuwa vizuri kwani watu wataona ni jinsi gani traffic wanavyotumia nguvu na kuwaonea raia. Shukrani
Mdau Zenji

NYUMBA INAPANGISHWA MBEZI BEACH

0
0
Nyumba ipo MBEZI GOIG, mita chache kutoka Barabara Kuu (Bagamoyo Road), upande wa kushoto kama unatokea Mbezi Tangi Bovu. Ina vyumba 3 vikubwa vinavyojitosheleza (3 Master Bedrooms), Two kitchens, Two Sitting Rooms, Garage ya kuweka magari na Fencing.
HAKUNA DALALI. KUJUA BEI NA MALEZO MENGINE, TAFADHALI PIGA SIMU NAMBA: +255 0657 803 139

HOUSE FOR SALE AT MBWENI JKT

0
0

A brand new house is now available for sale at Mbweni JKT near Ndege Beach Club. The house is located at a prime area with facilities such as school (opposite the house), paved roads, approx. 2 km from tarmac road (Bagamoyo Road), and approx.1 km from the beach.


The house has a Master bedroom with Jacuzzi, AC and walk in closet (to be fixed). Three bedrooms, one study room/office, dinning room, seating room with AC, two public toilets and bathrooms with shower cubicle. In addition, the house has a modern kitchen equipped with gas cooker and/or electricity and oven, kitchen store, outside toilet and bathroom, water (well), electricity (3 phase), security fence and three water heaters.

If you are interested please call 0713 337 368, 0755 779 933 or 0784 444 200.






NEWS ALERT: HATIMAYE PESA ZA RESEARCH KWA WANAFUNZI WA MWAKA WA 3 CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI (TEKU) KULIPWA PESA ZAO KUANZIA KESHO.

0
0
  Vice Chancellor wa TEKU Prof. Dr. Tuli Kassimoto
 Huu ni uthbitisho wa kupokea Fedha hizo leo na sio kama walivyo kuwa wakidai wanafunzi kuwa Chuo kilitunza Fedha zao katika (Fixed deposit)
Huu ni uthibitisho kutoka Bodi ya Mikopo wakati walipoanza kufanya malipo kwa ajili ya wanafunzi .

IMETOLEWA NA 
UTAWALA 
CHUO KIKUU CHA TEOFILO KISANJI
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images