Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1952 | 1953 | (Page 1954) | 1955 | 1956 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani-kaundasuti) akipewa maelezo ya kilimo cha maharage na mtafiti hifadhi ya mimea Reinfred Maganga (shati nyeupe) katika moja ya bustani ya mifano yaliyopo kwenye viwanja vya taasisi hiyo.KATIKA kujiandaa na msimu wa kilimo Uongozi wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen wamezuru Taasisi ya Utafiti Kilimo (ARI) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) nyanda za juu kusini - Uyole, Mkoani Mbeya ili kushuhudia shughuli zinazofanywa na taasisi hizo na kuchota utaalamu ili kunufaisha maendeleo ya mkoa. 

  Ziara hiyo iliwayobeba Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na makatibu tawala wao walioambatana na viongozi wa vikundi vya wakulima,Wakurugenzi, maafisa kilimo na mifugo wa wilaya, pamoja na wenyeviti wa Halmashauri nne za Mkoa huo, na wataalamu wa kilimo na mifugo kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

  Katika ziara hiyo ya siku moja mada mbalimbali zilitolewa kuhusu aina ya mazao yanayoweza kustawi katika Mkoa wa Rukwa, wadudu wanaoweza kushambulia mazao hayo na namna ya kuwadhibiti ili kuongeza uzalishaji pamoja na utafiti wa udongo.

  Pia viongozi hao waliweza kujifunza umuhimu wa kilimo cha nyasi kwaajili ya mifugo, ufugaji bora kwaajili ya viwanda vya mazao ya mifugo, magonjwa mbalimbali ya mifugo na namna ya kukabiliana nayo

  Mh. Zelote alisema kuwa kwa miongo kadhaa Mkoa wa Rukwa umekuwa katika mikoa inayoongoza kwa kilimo lakini haikuwahi kuwa namba moja hivyo ziara hiyo ndio mwanzo wa kuiendea Rukwa mpya yenye kuzalisha mazao yenye kuleta tija kwa wakulima, mkoa na taifa kwa ujumla.

   “Lengo la kufunga safari kutoka Rukwa hadi hapa ni kwa lengo la kuleta mabadiliko ya Kilimo na mifugo, Rukwa kupitia kilimo ndio litakuwa ni chimbuko la viwanda, kama wataalamu walivyosema kuwa kilimo ndio chimbuko la viwanda,tunahitaji kuboresha kilimo katika Mkoa wa Rukwa ili tuwe na viwanda vya uhakika” Amesema.

  Amesema kuwa ili kuwakomboa wananchi wa hali ya chini ambalo ndio lengo la Rais Dk. John Pombe Magufuli Hakuna budi kuimarisha kilimo na hatimae kuinuka kutoka katika uchumi wa viwanda vidogo kwenda viwanda vya kati na kutoka katika uchumi mdogo kwenda uchumi wa kati.

  Kwa upande wake mratibu wa ziara hiyo Benjamin Kiwozele alimshukuru Mh. Zelote kwa kuona umuhimu wa kuzitumia taasisi hizo kwa malengo yaliyowekwa na serikali.

  Kabla ya Kumkaribisha Mh. Zelote, Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa Kilimo Tulole Bucheyeki alisema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa heshima kubwa walioionyesha kwa kufika kwenye Taasisi hiyo na kuweza kukutana na wataalamu wao kwa nia ya kuboresha uwekezaji na vipato vya wananchi.

   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani-kaundasuti) akiwa katika picha ya pamoja na watafiti mbalimbali katika Taaisi ya Utafiti wa Kilimo – uyole, Mbeya pamoja na baadhi ya wataalamu wa Kilimo na Mifugo kutoka Rukwa.
   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani-kaundasuti) pamoja na uongozi wa Mkoa wa Rukwa wakipewa maelezo ya kilimo cha maparachihci na mtafiti hifadhi ya mimea Reinfred Maganga (shati nyeupe- kushoto) katika moja ya vitalu vilivyopo kwenye viwanja vya taasisi hiyo.
  Uyole4 - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen (wa tatu kutoka kulia) akisikiliza uwasilishaji kutoka kwa mtafiti rasilimali za mifugo Dk. Pius Mwambene (wa kwanza kulia) kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI)

  0 0

  Katika maonesho ya Wiki ya Vijana na Uzimaji wa Mwenge Makamu wa Rais wa pili Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa Maonesho hayo aliupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kutoa Elimu bure kwa wananchi wa Zanzibar kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza kama Shinikizo la Damu (BP), Sukari na uwiano wa Uzito na Urefu, lakini pia kwa upimaji wa magonjwa hayo bure.

  Alisisitiza NHIF isiishie kwenye Maonesho hayo lakini iwe ikitoa huduma hiyo mara kwa mara pindi Mfuko upatapo fursa ya kufanya hivyo, vilevile Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Mfuko na Fao jipya la TOTO AFYA KADI kwani gharama yake ni nafuu, tofauti na gharama za matibabu ya afya mahospitalini aliuasa Mfuko uhamasishe fao hilo ili watu waweze kujiunga kwa wingi, kwani watoto ni Taifa la kesho, ili waweze kufikia malengo yao wanahitaji uhakika wa Afya zao.

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unaendelea kuwakaribisha wananchi wazidi kujitokeza kwa wingi kuja kupima afya zao bure na vilevile kujiunga fao la Toto Afya Kadi, "Mfuko umejipanga kuhakikisha kila mwananchi anakua na kadi ya Bima ya afya, kwani ili kua na Taifa lenye maendeleo linahitaji wananchi wenye uhakika na huduma za Afya na Mfuko uko kwa ajili ya kuhakikisha hilo" alisema Meneja wa NHIF Zanzibar Bw. Ismail Kangeta.

  Wiki ya Vijana inaadhimishwa kuanzia tarehe 8/10/2017 hadi tarehe 14/10/2017 kama sherehe ya Kumbukumbu ya hayati Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere.
  Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akielezewa jambo na Meneja wa NHIF Zanzibar Bw. Ismail Kangeta pindi alipotembelea banda la NHIF baada ya kufungua Rasmi Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Amaan.
  Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akicheki afya kwenye banda la NHIF, katika Maonesho ya Wiki ya Vijana.
  Afisa wa NHIF Bw. Shabani Muhunzi akielezea jambo kwa mdau alietembelea banda la NHIF kwenye viwanja vya Amaan Zanzibar kwenye Maonesho ya Wiki ya Vijana.
  Afisa Matekelezo wa NHIF Zanzibar Bi.Naima Aboubakar akiwaelezea vijana waliokuja kutembelea banda la NHIF kuhusiana na Huduma zitolewazo na Mfuko huo.

  0 0

   Spika Mstaafu na Mwenyekiti  wa Bodi wa Mfuko  ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda , akizungumza na baadhi ya waumini baada ya kumaliza uzinduzi wa huduma ya “TOTO AFYA KADI” katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.
   Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki  akiendelea kutoa maelezo ya umhimu ya mfuko huo kwa baadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.
  Bbaadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge.

  SPIKA Mstaafu na  Mwenyekiti  wa Bodi ya Mfuko  ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda  azindua huduma ya “TOTO AFYA KADI” kwenye nyumba za ibada.

  Akizungumza na waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe  Mwenge amesema  huduma hiyo itatolewa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kwa  Sh. 50,400 kwa mtoto mmoja kwa mwaka.

  Makinda amesema kampeni hizo ambazo zitaendelea kwenye Madhehebu ya Dini lengo ni kuwa rafiki na huduma hiyo ili kufikia mwaka kesho watanzania asilimia zaidi ya  80 wawe wamejiunga na huduma hiyo.

  Makinda amesema kiasi hicho  cha Sh. 50,400 kitakachochangiwa kwa mwaka kitamuwezesha mwanachama huyo kupata matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

  Naye Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki amesema fao hilo pia hutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu kwa Sh. 50,400.

  Pia amesema NHIF hutoa huduma kwa vikundi vya  wajasiriamali walio kwenye vikundi vya watu kuanzia 10 kwa Sh. 76,800  kwa kila mwanachama mmoja ambaye atachangia fedha hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

  0 0

  Mhe. Mongella aahidi Zawadi Nono

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amewataka wavuvi wa kambi ya fuata Nyayo iliyopo Mwalo wa Mihama na wananchi wa Kata ya Kitangili Wilaya ya Ilemela kuhakikisha wanawabaini wale wote wanaotumia Nyavu haramu na kuendesha Uvuvi haramu katika Mwalo huo,ambapo kwa yeyote atakayetoa taarifa za Siri na zilizo sahihi na kupelekea kukamatwa kwa wahalifu hao atapewa zawadi ya Shilingi Laki Moja tasilimu.

  Mhe. Mongella amesema hayo katika Mkutano wa hadhara alipokuwa akitoa hotuba wakati wa Uzinduzi wa Zana za Uvuvi endelevu na kusisitiza kuwa kila Mwananchi anatakiwa Kumuunga mkono Rais wetu Dkt.John Pombe Magufuli katika kupambana na uvuvi haramu na kuwataka wananchi kuachana na Uvuvi haramu wa kutumia Nyavu zenye matundu madogo,makorokoro,timba na baruti ambapo kila mmoja anatakiwa kutumia zana na nyenzo salama kama vile nyavu zenye matundu ya inchi 6,7,na 8.

  Hata hivyo Mhe.Mongella amewakabidhi wanakikundi wa Fuata Nyayo jumla ya nyavu mia saba (700 ) na Mitumbwi kuni na nne (14) ambapo kila Mtumbwi una wastani wa nyavu hamsini,zana na Nyenzo jumla zina thamani ya Shilingi Milioni Themanini na nane laki tatu sabini na saba elfu na mia tano tu. (88,377,500) fedha hiyo imetolewa na mfadhili Bwana Vedastus Msizu ambaye ni Mkurugenzi wa Kambi ya Uvuvi ya Fuata nyayo.

  Aidha,Mhe.Mongella amempongeza Bwana Msizu kwa ufadhili huo na kuiagiza Halmashauri kuhakikisha wanasimamia kikamilifi usajili wa kikundi hicho ili kikundi hicho kiolozeshwe kwenye vikundi vinavyopata mikopo kutoka Halmashauri hiyo.


  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (mwenye kofia) akisimamia kurejeshwa kwa maji nyumbani kwa Bi Veronica Mtiro mlemavu wa miguu mkazi wa Nyakato, mara baada ya kumlipia Shilingi Laki moja na elfu arobaini alizokuwa anadaiwa na MWAUWASA baada ya kuugua muda mrefu na kushindwa kulipia deni hilo ambapo amekuwa akiishi kwa kutegemea kuuza maji hayo.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akimsikiliza kwa makini mmoja wa wananchi (aliyeweka mkono begani) wa kata ya Kitangili,Wilaya ya Ilemela mara baada ya Mhe Mkuu wa Mkoa kumaliza kuhutubia wananchi wa kata hiyo na kusikiliza kero zao.


  0 0

   Meneja wa Rasilimali Watu wa Radio Uhuru, Paul Mung’ong’o akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Watoto wenye Kansa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili vyenye thamani zaidi sh. Milioni Mbili leo ambavyo vimetolewa na watu wanaosikiliza radio hiyo kupitia kipindi cha Kugusa Maisha yao.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Radio Uhuru na Mtangazaji wa Kipindi cha Gusa Maisha Yao, Joy Njarabi akizungumza juu ya uendeshaji wa kipindi hicho na kuweza kupata watu ambao wanaguswa moja kwa moja na kutoa msaada ikiwemo kwa kituo cha watoto wenye Kansa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
   Wafanyakazi wa Radio Huru wakiwa na watoto wa kituo hicho wakati wa kukabidhi msaada wa vitu mblimbali katika kituo hicho kupitia kipindi cha Gusa Maisha Yao.
  Picha mbalimbali za wafanyakazi katika kituo cha watoto wenye Kansa

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kushoto), akiwa ameongozana na kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,(ACP) Julius Mjengi (kulia), alipowasili katika mkoa huo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake za kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Picha na Jeshi la Polisi.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Iringa, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. 
   Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa tayari kwa kumpokea Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, ambaye yupo mkoani Iringa, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia.
  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, wakiwa katika kikao kazi na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wakijadiliana namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu mkoani humo, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja.


  0 0

  Jonas Kamaleki-MAELEZO

  Muda mfupi baada ya kula kiapo, Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, ametoa onya kali kwa majingili nchini na kuwataka kuacha mara moja vitendo hivyo.

  Dkt. Kigwangalla ametoa onyo hilo leo Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa mawaziri na naibu mawaziri.“Majangili waanze kukimbia wenyewe pale wanapowaona wanyama kwani tutawashughulikia ipasavyo na kuhakikisha tunakomesha vitendo hivi viovu katika nchi yetu,” alisema Dkt. Kigwangalla.

  Kuhusu utalii, Dkt. Kigwangalla amesema kuwa watalii wamekuwa wakiongezeka lakini si kwa kiwango cha kuridhisha hivyo Serikali itafanya juhudi za makusudi kutangaza vivutio vya utalii kwa njia za kisasa ndani na nje ya nchi.Amesema kuwa ubunifu katika kujitangaza itabidi utumike ili kuhakikisha Tanzania inavutia watalii wengi kutoka nje hususan soko jipya la China na nchi nyingine ikiwemo Marekani na nchi za Ulaya.

  Kwa kufanya hivyo pato la Taifa kutokana na utalii litaongezeka kuliko ilivyo sasa, alisema Kigwangalla.Aidha, Waziri huyo wa Maliasili na Utalii amesema atashirikiana na wizara nyingine kukomesha migogoro ya wakulima na wafugaji ili lipatikane suluhisho la kudumu.

  Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo, amesema atahakikisha watumishi wa umma katika wizara yake wanafanya kazi kwa kujituma zaidi na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea.

  Kwa mujibu wa Jafo, uadilifu, uwajibika na nidhamu ni mambo ambayo yatatiliwa mkazo katika wizara yake ili kuwa na utumishi wenye tija.Amewataka wakuu wa mikoa, wilaya kufanya kazi kwa mashindano ili kuharakisha upatikanaji wa maendeleo katika sehemu husika na kuchochea ukuaji wa uchumi hasa wa viwanda.

  “Wakuu wa mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri muwe vinara katika utendaji wenu mkiwasimamia walioko chini yenu kwa weledi ili muweze kwenda na spidi ya Serikali ya Awamu ya Tano,” alisema Jafo.Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akizungumza baada ya kuapishwa amesema atahakikisha sekta ya habari inapewa kipaumbele kwani habari ni jambo muhimu katika suala zima la mawasiliano.

  Mhe. Shinza atahakikisha weledi katika sekata ya habari unazidi kuimarishwa ilikuondoa upotoshwaji ambao umekuwa ukijitokeza katika baadhi ya vyombo habari.Kuhusu upatikanaji wa habari kwa sehemu kubwa ya watanzania, Shonza amesema atajitahidi kufanya habari ziwafakie watanzania wengi Zaidi ili kujenga jamii yenye ufahamu wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi yao.

  Katika hafla hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha jumla ya Mawaziri nane na Manaibu Mawaziri 16 ambao wameanza kazi mara baada ya kuapishwa kwa kuhudhuria kikao cha Maalum cha Baraza la Mawaziri.

  Baadhi ya mawaziri waliokula kiapo leo ni Mhe. Angella Kairuki (Madini), Mhe. George Mkuchika (Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Mhe. Hamis Kigwangwalla (Maliasili na Utalii) na Suleiman Jafo (Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa).

  Kwa upande wa Manaibu Mawaziri, Mhe. Rais amewaapisha jumla 16 ambao baadhi yao ni Mhe. Stella Manyanya (Naibu waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji), Mhe. William Ole Nasha (Elimu, Sayansi na Teknolojia), Dkt. Faustine Ndungulile (Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto), Mhe. Stella Ikupa (Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye Ulemeva) na Mhe. Juliana Shonza (Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo).


  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Angela Kairuki kuwa Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Hamisi Kigwangwalla  kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Mhe. Suleiman Saidi Jafo  kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa) Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Kangi Lugola kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
   
  Watu watatu, mchimba makaburi Mohammed Maganga (61)  Khalid Mwinyi (33), anayedaiwa kuwa meneja Wa benki na mfanyabiashara Rahma Almas maarufu baby (37)    wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibi tuhuma za mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter (52).

  Washtakiwa hao wamesomewa shtaka la mauaji.

  Mwendesha Mashtaka wakili wa serikali Adolf Mkini akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amedai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 16 mwaka huu katika makutano ya barabara ya Chole na Haike Selasie Kinondoni Dar es salaam, ambapo wote kwa pamoja wanadaiwa kumuua Lotter.

  Baada ya kusomewa kosa hilo la mauaji, Hakimu Mashauri alisema kosa hilo halina dhamana kesi hiyo ikaahirishwa hadi  Oktoba 23 mwaka huu.

  Wakati huo huo, Maganga, Rahma Mwinyi na mwanafunzi Alma's Sued wamesomewa shtaka lingine la uhujumu uchumi na kukutwa na Bomu la kurusha kwa mkono.

  Mbele ya Hakimu Mashauri wa mahakam hiyo, Imedaiwa kuwa,Septemba 16 mwaka huu, watuhimiwa hao wakiwa eneo la Upanga DSM walikutwa na silaha moja aina ya Uzigun bila kibali.

  Aidha imedaiwa kati ya September 16 mwaka huu washtakiwa hao walikutwa na risasi 167 bila kibali, vilevile  wanadaiwa kukutwa na Bomu la kurusha kwa mkono (Hand grenade) bila kibali.

  Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo, huku upande wa mashtaka ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

  Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili wa utetezi Mluge Karoli aliomba dhamana kwa washtakiwa kwani shtaka hilo linadhamana,

  Akiwasomea masharti ya dhamana, hakimu Mashauri aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini 2 watakaosaini bondi ya milioni 20 kila mmoja.

  Hata hivyo, ni mshtakiwa Swedi tu ndio aliweza kutimiza masharti ya dhamana huku washtakiwa wengine wakishindwa kutimiza masharti, kesi imeahirishwa hadi October 23 mwaka huu.

  0 0


  :Barclays Bank Tanzania Head of Legal and Company Secretary Dotto Kahabi ( left) presents part of a donation of 60 pairs of kids clothes, 48 pairs of kids shoes, 14 pairs of shoes for parents and clothes to the head of Mwanangu Montessori Centre Jannet Manoni donated by the bank’s Legal and Compliance Department staff as part of the Barclays’ ongoing citizenship activities at a function held at the centre’s premises at Vikindu, Coast Region over the weekend.
  Barclays Bank Tanzania Head of Legal and Company Secretarial, Dotto Kahabi (second left), hands over donation of part of 60 pairs of kids clothes, clothes for parents and guardians, 48 pairs of kids shoes and 14 pairs of parents and guardians shoes to Rukia Selemani, parent of a kid cared for at Mwanangu Montesssori centre, donated by BBT Legal and Compliance department as part of the banks ongoing citizenship activities at a function at the centre premises, Vikindu in Coast Region at the weekend.
  Some staff from Barclays Bank Tanzania Legal and Compliance Department talk to one of the kids cared for at Mwanangu Montessori Centre during their recent visit at the centre.
  Mwanangu Montessori Centre president, Walter Miya (right), talks to on-visit Barclays Legal and Compliance Department staff at the centre’s premises at Vikindu, Coast Region recently. The bank’s staff donated 60 pairs of clothes and 48 pairs of shoes for the children, while parents and guardians were given clothes and 14 pairs of shoes.

  0 0


   Mtaalamu wa dawa za Usingizi na ganzi wakati wa operesheni, Dk. David Chiunga, akimpima mapigo ya moyo mmoja wa wagonjwa waliofika kupata huduma za matibabu bure wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali ya Marie Stopes iliyoboreshwa na kituo cha kupokea simu za wateja, Mwenge jijini Dar es salaam hivi karibuni. 
   Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya Marie Stopes, Neema Mgumba akimpima mapigo ya moyo mmoja wa wagonjwa waliofika kupata huduma za matibabu bure wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali ya Marie Stopes iliyoboreshwa na kituo cha kupokea simu za wateja, Mwenge jijini Dar es salaam hivi karibuni.
  Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya Marie Stopes, Joan Rwechungura akichukua sampuli ya damu kutoka kwa mmoja wa wagonjwa waliofika kupata huduma za matibabu bure wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali ya Marie Stopes iliyoboreshwa na kituo cha kupokea simu za wateja, Mwenge jijini Dar es salaam hivi karibuni.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi (kulia), akimkabidhi kipeperushi cha taasisi hiyo, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea taasisi hiyo, kuwaona wagonjwa na kutoa msaada wa fedha kwa watoto wawili wagonjwa wa moyo, kusaidia kufanyiwa upasuaji, ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani leo Oktoba 10, 2017 jijini Dar es Salaam. 
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (wa tatu kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi (wa tatu kulia), mfano wa hundi ya sh. milioni 4 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wawili wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo, wakati uongozi wa TPC, ulipotembelea taasisi hiyo katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani, Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto, Dkt. Godwin Sharau na wa kwanza ni Meneja Mkuu Usimamizi Biashara wa TPC, Hassan Mwang'ombe.

  Daktari bingwa wa upasuaji moyo watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Godwin Sharau (wa tano kulia), akiwapatia maelezo baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati uongozi wa shirika ulipotembelea moja ya wodi za wagonjwa wa moyo kwenye taasisi hiyo leo jijini. Wa nne kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Deo Kwiyukwa. 
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa, akiwa amembeba mtoto Delphina, ambaye ni mmoja wa watoto waliopatiwa msaada wa sh. milioni 2 kila mmoja na TPC kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa moyo, wakati uongozi wa shirika hilo, ulipotembelea kwenye wodi za wagonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili Dar es Salaam leo katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani. 


  0 0

  Nyuku vikiwa vipo tayari kwenye picnic ya familia na nyama choma iliyoandaliwa na Shield Our Watoto siku ya Jumamosi Oktoba 7, 2017 Westerville, Ohio. SOW ni oganaizesheni iliyoanzishwa na Bhoke Kirigiti akishirikiana na mumewe PeterKirigiti inayotetea watoto kutokana na unyanyasaji hasa watoto wa kike inapowapigania hasa unyanyasaji wa kingono chini ya umri mdogo. Oganaizesheni hii hushirikiana na wazazi wa watoto na watu mbalimbali wakiwemo watoa elimu ya unyanyaswaji wa watoto wakishirikiana na mashirika mbalimbali yasiyokua ya Kiserikali. Shield Our Watoto hutoa elimu ya bure kwa wazazi na watoto kuhusiana na unyanyasaji  wa kijinsia wanaofanyiwa watoto wenye umri ndogo ambao kati ya watoto 3 kati ya 10 wamekua wakiathirika kisaikolojia kutokana unyanyasaji huo
  Peter Kirigiti pamoja na mkewe Bhoke Kirigiti wakielezea Shield Our Watoto (SOW) kwa wadu waliohudhuria family picnic na nyama choma siku ya Jumamosi Oktoba 7, 2017 Westerville, Ohio.

  Wadau mbalimbali waliojumuika kwenye nyama choma hiyo wakiwasikiliza PeterKirigiti na mkeweBhoke Kirigiti.

  Clara James mwandishi wa kitabu cha There's Beauty Inside akielezea unyanyasaji wa watoto hasa kwa mtoto wa kike unawezaje kuathiri saikolojia katika maisha yake

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Na Mwandishi Wetu- Tarime, Mara.

  Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya watoto wa kike hapa nchini wameendesha mafunzo kwa  waendesha bodaboda walioko wilaya ya Tarime mkoani Mara  kuwahamasisha vijana hao  kuunga mkono juhudi za kitaifa za kutokomeza mimba za utotoni kwa wasichana walioko shule ya msingi na sekondari.  

  Akieleza malengo ya mafunzo hayo, Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Jamii Bibi Anna Shengweli amebainisha kuwa madreva wa bodaboda ni kundi mahususi katika ulinzi wa watoto wa kike kwani kutokana na shughuli zao wanakutana mara nyingi na watoto wa kike wakiwa katika mazingira hatarishi. 

  “Wakiwa katika kazi zao za kila siku bodaboda na wanapishana na watoto wa kike wakitekeleza majukumu yao mbalimbali ikiwemo kwenda na kurudi kutoka shule, kuteka maji visimani, kuchunga mifugo porini, sokoni, stendi ya basi na kadhalika’’ alisema Bibi Anna.
    Mwezeshaji kutoka ‘Shirika la Save the Children’ Bw. John Komba akitoa mada kwa madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime katika Semina shirikishi ya jamii katika kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike itakayofanyika kitaifa Oktoba 11, 2017 Wilayani Tarime Mkoani Mara.
   Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la REPSSI Tanzania Bibi. Edwick Mapalala akizungumza na waendesha bodaboda wa wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara katika Semina ya kuelimisha jinsi ya kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni kuelekea maadhimkisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike itakayofanyika kitaifa Oktoba 11, 2017 Wilayani Tarime Mkoani Mara.
  Baadhi ya waendesha bodaboda kutoka Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolea katika Semina ya kuwaelimisha jinsi ya kuwalinda watoto wa kike na mimba za utotoni kuelekea maadhimkisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike itakayofanyika kitaifa Oktoba 11, 2017 Wilayani Tarime Mkoani Mara.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watendaji wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kubadili utendaji wao wa kazi ili kupata matokeo bora katika kutoa huduma kwa wananchi.

  Akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya TAMISEMI mara baada ya kuapishwa amesema biashara ya kufanya kazi kwa mazoea haina nafasi na maemtaka kila mtumishi kubadilika na kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokea tarajiwa.

  Waziri Jafo amesema “ili tuweze kufikia malengo yetu kwa hataka na ufanisi wa hali ya juu naahidi kutoa  ushirikiano kwa kutosha kwa Manaibu Waziri waliochaguliwa na kuapishwa pamojanami leo hii, viongozi wengine wote wa Wizara, manajiment pamoja na watumishi wote.

  Akizungumza wakati wa kikao hicho Naibu Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe. George Joseph kakunda amesema TAMISEMI ni injini ya Nchi na isipofanya vizuri hakuna Wizara nyingine itakayofanya vizuri kwa sababu unapozungumzia tamisemi unagusa wananchi na mengine yote yanayofanyika katika Wizara nyingine ni kwa ajili ya wananchi hawa wa TAMISEMI hivyo ni lazima tuweke mazingira bora na rafiki ili huduma hizo ziwafikie zikiwa na ubora wa hali ya juu.

  “Wizara hii ni muhimu sana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa sababu watekelezaji wa miradi mbalimbali wako katika mamlaka ya serikali za Mitaa hivyo tukifanya kazi kwa bidii na uaminifu hakika mafaniko yatakuja kwa haraka na hilo sisi ndio tunalolihitaji katika Serikali ya awamu ya Tano” alisema Mhe. Kakunda.

  Katika mabadiliko yaliyofanywa juzi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli Wizara ya TAMISEMI itaongozwa na Manaibu Waziri wawili ambao ni Mhe. George Joseph kakunda na Mhe. Josephat Sinkamba Kandege huku Waziri wa Wizaa hii akiwa ni Mhe. Selemani Said Jafo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ndogo ya TAMISEMI – Dar es salaam baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda na kushoto kwake ni Naibu Waziri Mhe. Josephat Kandege
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (aliyesimama katikati) akizungumza na wafanyakazi wa TAMISEMI ofisi ndogo ya dar es salaama mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Katika Picha ya pamoja ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (pili kushoto aliyekaa, Mhe. George Joseph kakunda (kwanza kushoto aliyekaa) Naibu Waziri Mhe. Josephat kandege(Pili Kulia aliyekaa), Naibu katibu Mkuu –Elimu Tixon Nzunda pamoja na watumishi wa TAMISEMI ofisi ndogo ya  Dar es Salaam.


  0 0


  Na; Agness Moshi na Pascal Dotto-MAELEZO.

  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea wataalamu 16 kutoka nchini Cuba kama moja ya mikakati yake ya kuboresha utoaji huduma za Afya ikiwemo kutoa huduma za kibingwa hapa nchini.

  Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Mpoki Ulisubisya alisema kuwa Serikali imepokea madaktari bingwa 6, madaktari bingwa wa usingizi 2, madaktari wa wodi za wagonjwa mahututi 2, Daktari bingwa wa  upasuaji wa macho 1, mtaalamu mmoja wa radiolojia pamoja na wauguzi 10 wa vyumba vya wagonjwa mahututi.

  “Wataalam hawa mamekuja wakati muafaka, kwasababu kwa kipindi hiki hospitali ya Muhimbili inafanya maboresho ya utoaji huduma , hivyo nina amini uwepo wao hapa kwa miaka miwili, hautakuwa kwa ajili ya  kuboresha huduma au kusaidia wagonjwa tu , bali ni nafasi nzuri ya  kuwapa ujuzi na mafunzo  wataalamu wetu “,alisema Dk.Ulisubisya.

  Dk. Ulisubisya amesema kuwa uwepo wa wataalamu hao utaongeza nguvu kazi hususani kwenye utoaji huduma kwa wagonjwa mahututi kwani hospitali hiyo imeongeza vitanda vya wagonjwa mahututi kutoka vitanda 21 hadi 88.
  Katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(katikati) akieleza jambo wakati wa kuwakaribisha wataalamu 16 kutoka nchni Cuba wakiwemo Madaktari Bingwa 6 pamoja na Wauguzi wa Chumba cha uangalizi maalumu kwa wagonjwa mahutiti mapema leo Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam kushoto ni kiongizi mkuu wa matibabu nchini Tanzania Dkt. Maylen Lopezi na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Cuba katika hafla ya kuwakaribisha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Jijini Dar es Salaam.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” wilaya ya Shinyanga ambapo jumla ya wahitimu 238 wamefuzu mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa miezi minne.

  Sherehe za kufunga mafunzo hayo zimefanyika leo Jumatatu Oktoba 9,2017 katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.Akizungumza katika sherehe hizo,Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo waliyoyapata huku akiwaasa kufanya shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchumi.

  Matiro aliwataka wahitimu hao kuunda vikundi vya ujasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia. “Mmejifunza mambo mengi,naomba muzingatie mlichojifunza,muwe wazalendo wa nchi yetu,kuweni mstari wa mbele kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuwafichua wahalifu na wale wote wanaoleta uvunjifu wa amani katika jamii”,aliongeza Matiro.
  Katika hatua nyingine alizitaka kampuni za ulinzi kutumia walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua gwaride

  Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Meza kuwa wakiwa wamesimama wakati wahitimu wakipita kwa mwendo wa polepole

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao kifupi na baadhi ya Watendaji wa Ofisi yake mara baada ya kuapishwa IKULU jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiongoza kikao chake cha kwanza mara baada ya kuapishwa mapema leo IKULU jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao na Watendaji wa Ofisi yake  mara baada ya kuapishwa IKULU jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kuongea na baadhi ya Watendaji wa ofisi yake jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Timu ya kata ya Ihembe imeibuka mabingwa wa Bashungwa Karagwe Cup 2017 baada ya kuifunga Nyaishozi mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Changarawe huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba uliteka hisia za mamia ya wakazi wa jimbo la Karagwe waliojitokeza kwa wingi.

  Ihembe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 25 kupitia kwa Athumani Chuji aliepiga shuti kali la mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Nyaishozi na kuingia wavuni. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Nyaishozi ambao walionyesha kutoelewana katika eneo la ulinzi na kujikuta wakiruhusu bao la pili katika dakika ya 35 lililofungwa na Mshauri Kato aliewatoka walinzi wa Nyaishozi na kufunga goli la kiustadi. 

   Kipindi cha pili Nyaishozi waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 78 lililofungwa na mshambuliaji MC, hata hivyo jitihada za kusawazisha matokeo zilikwamishwa na mlinda mlango wa Ihembe alieokoa michomo mingi.
  Mgeni rasmi akiwasili katika uwanja wa changarawe ilipofanyika fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
  Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akikagua vikosi vya Ihembe na Nyaishozi
  Mchezaji wa Ihembe akipiga mpira wa kona
  Uwanja wa Changarawe ulihosheheni mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu.


  0 0

   NI MIEZI MITATU TANGU ULIPOTANGULIA MBELE ZA HAKI MPENDWAWETU MZEE GALLUS CHOGIMEMBE NYAKUNGA HAPO TAREHE 12 JULY 2017 KIHESA IRINGA.

  HATUTASAHAU UPENDO, UCHESHI, NA BUSARA ZAKO DAIMA, KIUKWELI PENGO LAKO HALIWEZI KUZIBIKA KAMWE.


  UNAKUMBUKWA SANA NA MKE WAKO MPENDWA YASINTA KIBIKI, WATOTO WAKO, WAKWE NA WAKAMWANA WAKO, WAJUKUU, VITUKUU, KAKA, DADA NA SHEMEJI ZAKO, NDUGU, JAMAA, MAJIRANI NA MARAFIKI ZAKO.


  TULIKUPENDA LAKINI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI, PUMZIKA KWA AMANI.


  MKESHA WA KUMALIZA MSIBA NI TAREHE 13/10/2017, MISA TAREHE 14/10/2017  SAA 12.30 ASUBUHI KANISA LA KIHESA IKIFUATIWA NA KUSIMIKA MSALABA KIJIJINI NDULI.


  TUNAWASHUKURU WOTE KWA KUTUFARIJI KIPINDI HIKI KIGUMU, MUNGU AWABARIKI.  TUNAWAKARIBISHA KUUNGANA NASI KATIKA KUHITIMISHA MSIBA HUO NYUMBANI KWAKE KIHESA IRINGA.


older | 1 | .... | 1952 | 1953 | (Page 1954) | 1955 | 1956 | .... | 3278 | newer