Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Kwa Simu Toka London Na Freddy Macha: Mbio za Nusu Marathon Oktoba 8, 2017


Kwa simu kutoka London na Freddy Macha: Shuhudia Mti wenye umri wa miaka 500

INTRODUCING "NATEMBEA NAE: NEW VIDEO RELEASE FROM ELLISHA JAMES

BENKI YA CRDB YACHANGIA UJENZI WA VYOO WILAYANI CHATO

$
0
0
Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo katika halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita.

Walioketi ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodluck Nkini, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji CRDB.

Na Binagi Media Group.
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, benki ya CRDB imechangia vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita ili kusaidia utatuzi upungufu wa vyoo katika shule za halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus alisema vifaa hivyo vitasaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi za Kalema, Muungano na Katemwa A na kwamba vifaa hivyo vimejumuisha mifuko 150 ya theruji, mabati, sinki za vyoo pamoja na vyombo vya kukusanyia taka na tenki la maji kwa ajili ya halmashauri ya Chato.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas aliishukuru benki hiyo na kubainisha kwamba bado kuna uhaba wa vyoo kwenye shule nyingi na kuiomba kuendelea kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo ili kutoa chachu kwa wadau na benki nyingine kuiga mfano huo.

Zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lilifanya ijumaa Oktoba 06,2017 katika halmashauri ya wilaya ya Chato ikiwa ni muda mfupi baada ya benki ya CRDB kutoa semina kwa wateja wake wilayani humo na pia kutoka maeneo jirani ikiwemo Muleba, Katoro na Biharamulo.
Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.
Zoezi la kukabidhi vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya Chato.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakipokea vifaa hivyo.

SSRA YAWAZINDUA WAJASIRIAMALI KUHUSU KUJIUNGA NA KUJIWEKEA AKIBA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

$
0
0
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akitoa somo kwa wajasiriamali juu ya umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya sasa na baadaye ya familia, wakati wa Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Wajasiriamali wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (hayupo pichani) katika Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
Afisa Uhusiano wa Mamaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Agnes Lubuva (kulia), akigawa vipeperushi vya taasisi hiyo, kwa wajasiriamali waliohudhuria kongamano hilo la Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akijibu maswali ya wajasiriamali katika kongamano hilo.

MATOKEO CHANYA KATIKA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI TANZANIA

MANISPAA YA KINONDONI KUANZA KUREKEBISHA BARABARA KOROFI KATA YA WAZO JIJINI DAR

CHAMA CHA WATAALAMU WA UREMBO NA VIPODOZI TANZANIA (CWUVT) CHAANZISHWA KUENDANA NA SERA ZA AWAMU YA TANO

$
0
0
Chama cha Wataalam wa Urembo na Vipodozi Tanzania (CWUVT) wakutana Jijini Dar es salam kwa lengo la kuwakutanisha  pamoja wataalamu wa ngozi, wataalamu wa urembo, wataalam wa saluni,  wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi. Wanachama waasisi wa chama hicho walikutana chini ya Mwenyekiti Mama Shekha Nasser. Dhira ya Asasi hiyo ni kuinua, kuunganisha na kutumikia sekta ya Urembo na Vipodozi, watabibu wa ngozi na wataalamu wa Saluni ambao huboresha maisha ya watu kila siku. Pia kujenga na kudumisha wanachama ambao uwepo wao ni kukuza na kuunga mkono utaalam katika tasnia ya Urembo na Vipodozi kwa ujumla wake. 

Wajumbe waasisi walioudhuria mkutano huo wameipitisha Katiba ya Chama hicho na kuazimia kujitoa na kushirikiana kwa pamoja katika kuelimisha, kuhudumia na kutetea haki za wataalam wa saluni, wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi katika tasnia ya Urembo na Vipodozi. 

Chama hicho kimeona jinsi tasnia hii inakua kwa kasi, na mabadiliko ya kitechnologia hivyo wameona ni muda muafaka kwa Watanzania kuwa na uelewa zaidi kuhusu tasnia hiyo kubwa yenye Fursa kubwa ya Ajira hapa Nchini na kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi na hata kuingiza mapato ya kigeni.

MAGAZETI YA JUMATATU LEO OCTOBER 9,2017

KAIMU MKURUGENZI RAHCO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KATIKA MRADI WA RELI YA KISASA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (wa pili kulia) akiongozwa na  Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi (kushoto) pamoja na Meneja mradi huo kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk mara baada ya kufika eneo la Soga - Kibaha jumamosi usiku kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.
 Watanzania waliopata nafasi ya kufanyakazi katika mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge wametakiwa kufanya kazi kwa uweledi na kuacha ubabaishaji. 

Ujumbe huo aliutoa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza usiku wa jumamosi katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali. 

Kadogosa alisema mradi huo unatakiwa kwenda kwa kasi na kukamilika haraka hata kabla ya muda husika hivyo kila mtu atakayefanya kazi katika mradi huo anakikishe anafanya kazi na sio ubabaishaji utakaopelekea mradi huo kuchelewa. 

Aidha Kadogosa alisema wamefikia makubaliano ya kufanya kazi usiku na mchana ili kuharakisha mradii huo na wakandarasi wanafanya haraka na kwa ukubwa wa mradi huu ni lazima tufanye kazi usiku na mchana. “Kama mnakumbuka wakati Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa alipokuja hapa alisema ni lazima twende kasi na wakandarasi wetu wameamua kwenda na kasi na sasa mnaona tuta linaendelea vizuri ni lazima mradi huu ufanywe usiku na mchana kutokana na ukubwa wake,”alisema.
 Shughuli ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga - Pwani ikiendelea.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (wa kwanza kulia) akiongea machache na makandarasi wa mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga -Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.

BENKI YA CRDB YATOA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI WA DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa semina ya iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika mkoani Dodoma, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis, akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei kufungua semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. (Picha na Francis Dande).
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali Benki ya CRDB, Elibariki Masuke (kushoto), akiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika semina hiyo.

DC Hapi aihimiza Vicoba kujitanua zaidi

$
0
0
 MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi ameuomba uongozi wa Vicoba Endelevu hapa nchini kuhakikisha wanatanua mtandao wao uweze kuwafikia wananchi wengi zaidi wakiwemo walimu, wafanyakazi wengine wa serikali pamoja na wafanyabiashara ndogo ndogo ili kuisaidia serikali kufanikisha adhma yake ya kuyakomboa makundi hayo kiuchumi. 


Hapi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu iliyopo Bunju wilayani humo.

“Niwaombe sana viongozi wa Vicoba mtanue zaidi mtandao wenu ili muwafikie maelfu zaidi ya wafanyabiashara ndogo ndogo, wafanyakazi mbalimbali wa serikali wakiwemo walimu na mshirikiane nao katika kuangalia namna bora zaidi ya wao kupata huduma za kifedha ikiwemo mikopo ili waongeze thamani ya mitaji yao,’’ alisisitiza.

Zaidi, alitoa wito kwa wakina baba wahakikishe wanahamasisha wake zao pamoja na mabinti zao waweze kushiriki katika Vicoba ili kuinua vipato vya familia zao.

“Mbali na wakina mama pia hebu tuwahamasishe zaidi wasichana ambao wamekuwa wakitumia muda na pesa zao katika urembo na kujipodoa na badala yake sasa wajenge utamaduni kujijenga kiuchumi zaidi kwa kushiriki katika vikundi hivi vya kijasiliamali pamoja na Vicoba,’’ alisema.

Awali akitoa taarifa ya hali Vicoba endelevu hapa nchini, Rais wa Vicoba Endelevu nchini Bi Devotha Likokola alisema mtandao huo tayari unahusisha vikundi zaidi ya laki moja vikiwa na wanachama zaidi ya milioni mbili na laki mbili huku wakiwa na akiba ya zaidi ya Tsh Trilioni moja na milioni mia mbili.

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akikata utepe wakati akizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Rais wa Vicoba Endelevu nchini Bi Devotha Likokola (alieshika kipaza sauti) na Mkurugenzi wa Taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu Bi Semeni Gama (kulia kwa DC Hapi).

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akikagua baadhi ya bidhaa zinazoandaliwa na wajasiliamali ambao ni wananchama wa Vicoba Endelevu baada ya kizundua taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Bw Ally Hapi (alievaa suti nyeusi) akiongoza maandamano ya wajasiliamali ambao ni wananchama wa Vicoba Endelevu kuelekea kwenye ofisi za taasisi ya BUTA- Vicoba Endelevu yenye maskani yake Bunju wilayani humo jijini Dar es Salaam ambapo alizindua ofisi hizo mwishoni mwa wiki.

Lighting Africa/Tanzania Imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi ya Taa na Nishati ya Sola

$
0
0
Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC, leo wametangaza uzinduzi wa kampeni ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa.

Nishati inayotumia nguvu ya jua (Sola) na bidhaa za taa zimekuwa zikihitajika zaidi nchini Tanzania, Nchi ambayo familia nyingi za vijijini zinategemea taa za sola zilizo katika viwango duni na bidhaa zingine za umeme kwaajili ya mwanga. Taa ambazo zinaharibika kwa haraka sana na kuwasababishia wateja na watumiaji kupoteza gharama kubwa, jambo ambalo linapunguza uaminifu wao katika uhalali wa bidhaa za sola. 

Kampeni hiyo, iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” ina lengo la kuongeza ufahamu wa watumiaji kuhusu manufaa ya taa za kisasa za sola zenye ubora, ambazo zinasaidia wanajamii kufanya maamuzi yenye uhakika wakati wa manunuzi. Itakuwa inaonyesha aina mbalimbali za taa za sola ambazo zina waranti ambazo zinakidhi viwango vya mwanga ulimwenguni (Lighting Global Quality Standard) kampeni hii vile vile inatoa mbinu za kibunifu za biashara katika nishati ya sola kama vile huduma ya Pay-As-You-Go (PAYGO), huduma ya malipo kwa njia ya simu ambayo inamuwezesha mnunuzi kulipa kidogo kidogo, ambayo inafanya makundi mbalimbali yenye uwezo mdogo kifedha kumudu gharama za bidhaa hizo. 

“Kampeni ya Lighting Africa inataka kuongeza kasi ya matumizi ya bidhaa zenye kiwango bora na zenye gharama nafuu, na inaweza kuboresha kiwango cha maisha ya wanajamii wa vijijini, ambao mara nyingi hutumia bidhaa za mafuta ya taa ambazo sio za uhakika na zina gharama kubwa kama vyanzo vyao vya mwanga.
Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Edward Ishengoma, akiashiria uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” na kampuni ya Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Prof. Egid Mubofu na kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa IFC-Banki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Uganda na Sudan Kusini, Dan Kasirye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga(K) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Edward Ishengoma (Kushoto), akipata maelezo kuhusu bidhaa za sola kutoka kwa Meneja Mkazi wa Kampuni ya Solar Sister, Fatma Muzo,(katikati), pembeni yake ni ANSILA MAKUPA- BUSINESS DEVELOPMENT ASSOCIATE wakati wa uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la ‘‘Ngaa na Sola ndo mpango mzima,” na kampuni ya Lighting Africa, kwa kushirikiana na bank ya Dunia-IFC ya miaka miwili ya kutoa elimu kwa wateja kwaajili ya kuhamasisha taa zasizotumia nishati ya umeme wa kawaida katika jamii za vijijini ambao hawajaunganishwa na gridi ya Taifa katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam mapema iliyopita.
wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo mapema wiki iliyopita.


Polisi Tanzania yaichapa Polisi Dar bao 2-0

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Polisi Tanzania kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi daraja la kwanza ulioikutanisha timu hiyo na Polisi Dar es Salaam katika uwanja wa Ushirika-Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo ulimalizika kwa Polisi Tanzania kupata ushindi wa magoli 2-0.
Mchezaji wa Polisi Tanzania Saimon Fanuel akionyesha umahiri wa kusakata soka wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza ulioikutanisha timu hiyo na Polisi Dar es Salaam katika uwanja wa Ushirika-Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo ulimalizika kwa Polisi Tanzania kupata ushindi wa magoli 2-0.
Wachezaji wa Polisi Tanzania wakishangilia baada ya kujipatia goli la pili katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kundi B ulioikutanisha timu hiyo na Polisi Dar es Salaam katika uwanja wa Ushirika-Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo ulimalizika kwa Polisi Tanzania kupata ushindi wa magoli 2-0.
Wachezaji wa Polisi Tanzania na Polisi Dar es Salaam wakiwania mpira katika lango la Polisi Dar es Salaam katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kundi B uliozikutanisha timu hizo katika uwanja wa Ushirika-Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo ulimalizika kwa Polisi Tanzania kupata ushindi wa magoli 2-0.(Picha na Jeshi la Polisi).

HOSPITALI YA KIMATAIFA YA MACHO YATOA PUNGUZO LA BEI KWA HUDUMA YA MATIBABU YA MACHO.

$
0
0
KUELEKEA siku ya uoni Duniani Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital) inatoa punguzo la bei za matibabu kwa asilimia 25 kwa watu ambao wataenda kutibiwa katika hospitali iliyop jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital),Adam Mwatima amesema kuwa hospitali ya Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital) inatoa huduma za upasuaji wa macho kwa gharama nafuu sana.

Amesema kuwa kwawatu wenye bima za afya wanaweza kwenda kutibiwa katika hospitali hiyo kwa wale wenye bima za afya waliojiunga na hospitali hiyo hasa wenye bima za Mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) pamoja na mifuko mingine.
Msimamizi wa Hospitali ya kimataifa ya Macho (The International Eye Hospital),Adam Mwatima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa hospitali hiyo ya Kimataifa ya macho inapunguzo la bei kwa watakaoenda kutibiwa watapata punguzo la bei kwa pia kwa wale wenye bima ya afya watatibiwa kuitia bima zao. Kulia ni Meneja Masoko wa Hospitali ya Kimataifa ya Macho(The International Eye Hospital),Ilakoze Bidyanguze. 
Daktari Bingwa wa upasuaji wa Macho wa hospitali ya kimataifa ya macho(The International Eye Hospital), Adyn Buren, Muuguzi wa (The International Eye Hospital), Denis Malanga, na Muuguzi wa hospitali ya Kimataifa ya macho (The International Eye Hospital), Ana Athanas wakimfanyia upasuaji mgonjwa wa macho aliyeenda kutibiwa katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya miwani ambayo hutolewa na Hospitali ya Kimataifa ya Macho (The Intarnationa Eye Hospital)iliyopo jijini Dar es Salaaam wa wale ambao wataenda kutibiwa katika hospitali hiyo.

RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI ALIOWATEUA

$
0
0
 Waziri wa Madini Angellah Jasmine Kairuki akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi. Jumla ya Mawaziri nane na Manaibu 16 wameapishwa pamoja na Katibu wa Bunge. 
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Daniel Shonza akitia saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Justus Nditiye akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Kangi Lugola akipokea hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo hicho leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Said Jafo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo mara baada kumalizika kwa hafla ya kiap oleo Ikulu Jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija - MAELEZO

MAADHIMISHO YA SIKU YA MARADHI YA AKILI DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR.

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Asha Abdulla Juma akielezea machache kuhusiana na maradhi ya Akili katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Mgeni Rasmi ambae ni Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali akitoa hotuba katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Wauguzi wakiwa pamoja na Wananchi wakiungana pamoja na vituo mbalimbali vya afya katika maandamano ya  maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
 aadhi ya Watoto wenye maradhi ya akili waliohudhuria katika maadhimisho ya Kilele cha  Siku ya Afya ya Akili Duniani Kisonge mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BREAKING NEWZZZZZZ:WATU ZAIDI YA NANE WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA KUFUATIA AJALI YA GARI NDOGO (HIACE) KUTUMBUKIA ZIWA VICTORIA

$
0
0

 Juhudi za kuopoa miili ya watu waliokuwemo kwenye gari hiyo ikiendelea.
 Baadhi ya Wananchi mbalimbali wakilishuhudia tukio hilo la kuzama kwa gari ndogo ya abiria (HIACE),ambalo  namba zake za usajili hazikuweza kutambulika mara moja,mara baada ya kuopolewa ziwani.
 Wananchi kutoka maeneo mbali mbali wakilifuatilia tukio hilo mapema leo Kigongo Feri jijini Mwanza
Globu ya Jamii imepokea picha na maelezo kadhaa kutoka kwa mdau aliyeko jijini Mwanza,zikionesha na kueleza kutokea kwa ajali  jijini humo mapema leo,amesema kuwa ajali hiyo ni ya gari ndogo ya abiria Hiace ikiwa na ibiria imepitiliza na kutumbukia ziwa Victoria katika kivuko cha kigongo feri -Busisi,Wilayani Misungwi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 8 na majeruhi wawili,juhudi za kuopoa miili migine bado ikiendelea.

Tutaendelea kujuzana hapa hapa jamvini kwa kadiri taarifa zitakavyokuwa zikipatikana,ikiwemo na taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi la Jijini Mwanza.Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi -Amen

WAANDISHI WA HABARI WASHAURIWA HABARI ZA VIJIJINI

$
0
0

Na Pamela Mollel,Morogoro

Waandishi hapa nchini wameshauriwa kuongeza muamko katika kuandika na kutangaza habari za vijijini kwa kuwa asilimia 75 ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini, ambako wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali

Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Morogoro na mwenzeshaji Joe Nakajumo katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini iliyowakutanisha wanahabari kutoka mikoa mbalimbali iliyoratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania (UTPC).

Nakajumo alisema kuwa waandishi wa habari wanajukumu kubwa la kuwa karibu na jamii ya vijijini kwa kutambua shughuli zao wanazozifanya na kuzifatilia kwa kuona mafanikio yao pamoja na kuibua kero zinazowakabili

“Asilimia 75 ya wananchi wanaishi vijijini wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli za kilimo,ufugaji ,uvuvi,ujasiriamali hivyo ni muhimu sana  kuwapa kipaumbela wananchi hawa”alisema Nakajumo.Aidha alisema kuwa moja ya majukumu ya msingi ya mwandishi wa habari ni kusaidia na kushiriki katika ujenzi wa taifa hivyo anapaswa kuudhihirishia umma kwa watu wote nchini wanapaswa kupata habari

Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Adam Juma alisema kuwa mafunzo haya yatasaidia kuibua changamoto vijijini ambako panaoneka kusaulika kwa huduma mbalimbali za kijamii.Pia aliwaomba waandaji wa semina hii UTPC kuendeleza mafunzo haya kwa waandishi wa habari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya taaluma hiyo

Umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa waandishi wa habari lengo ikiwa kuwaongezea ujuzi wa kufanya kazi zao kwa kufata misingi ya taaluma .
Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini mkoani Morogoro ,Semina hiyo imeratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC).
Mwezeshaji wa semina Joe Nakajumo akifundisha katika mafunzo hayo leo Mkoani Morogoro.
Kushoto ni Noria Damian ,katikati Editha Carlo pamoja Happines Mtweve wakifatilia mafunzo hayo.
Kushoto ni mwakilishi kutoka Arusha Press club Pamela Mollel,katikati ni Adam Juma kutoka Mtwara Press Club wakifuatilia mafunzo hayo.

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)MKURANGA KIMEPATA VIONGOZI WAPYA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga kimepata viongozi wapya wataongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano katika uchaguzi uliofanyika jana.

Katika nafasi ya Mwenyekiti Wilaya imechukuliwa na Ally Msikamo kwa kura 749 baada ya kuwashinda wagombea wawili , Abdallah Kihato kura 189 na Mbaraka Mahanaka kura 44.

Nafasi ya katibu Mwenezi Wilaya imechuliwa na Ben Mkulia kwa kura 89 na kuwabwaga wagombea wawili , Mchowi aliyepata kula 22 na Ali Ngalema kula Saba (7).

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya Mkuranga , Ali Msikamo amesema kuwa uchaguzi umeisha na kilechobaki ni kufanya kazi katika ya kuendesha chama katika kumsaidia Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Amesema kazi ya chama kazi ya chama wilaya kuishauri serikali katika kusaidia chama kuendelea kushika dola ikiwemo na maandalizi ya uchaguzi mkuu.

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa uteuzi wa Naibu Waziri umetokana na wananchi wa Mkuranga na sio ujanja wake mwenyewe ndio uliomfanya aonekane.

Amesema kuwa maendeleo ya Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuandaliwa mkutano utaohusisha wajumbe wote kuangalia walikotoka na wanako elekea.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega alieapishwa leo kuwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, akizungumza katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa Wilaya ya Mkuranga.

 Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Wilaya  kwa kumpa ridhaa ya kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka miatano.
 Sehemu ya viongozi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi.

Picha mbalimbali za uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images