Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

SKAUTI MKOA WA MBEYA WANOLEWA NA JESHI LA ZIMA MOTO NA UOKOAJI MKOA WA MBEYA


UWT YAMPONGEZA RAIS DK MAFUGULI KWA KUFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wote katika sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano katika kuwahudumia Watanzania ili kufikia malengo ya Wizara.

Prof. Mbarawa ameyasema hayo jana katika mapokezi ya Manaibu Mawaziri wapya wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ofisini Jijini Dar Es Salaam baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

“Mimi nafurahi sana kufanya kazi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa sababu mimi na wafanyakazi tuko katika timu moja; tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano. Katika kipindi cha miaka miwili tumefanikiwa kufikia malengo mbali mbali ya serikali mfano ujenzi wa reli ya kisasa na barabara “ Mhe. Mbarawa amesema.

 Akiwakaribisha Manaibu Mawaziri hao katika Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema yeye pamoja na wafanyakazi wote wa wizara wamefurahi kupata mawaziri wapya ambao watafanya nao kazi kwa pamoja katika wizara hiyo.
 “Sisi kama viongozi tunapaswa kuwa mfano katika utendaji wetu wa kazi ili kujenga imani na umoja na wafanyakazi wetu. Tunapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano na umoja kwani haya ndio masuala ya msingi katika utendaji kazi,” Prof. Mbarawa amesema .
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akizungumza na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa (Wa tatu kulia), wakati walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), mara baada ya kuapishwa Jijini Dar es Salaam leo. 
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kikao kazi na Makatibu Wakuu wa wizara na baadhi ya Watendaji waliopo jiji Dar es Salaam leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DK.MABODI ATOA NASAHA NZITO KWA MAKADA WA CCM

$
0
0
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar viongozi watakaochaguliwa kupitia Uchaguzi wa ngazi ya Wilaya ya Kaskazini “B” kichama Unguja kuwa mstari wa mbele kukemea vikali tabia ya makundi na safu za uongozi zenye nia ya kuhatarisha uhai wa CCM katika Wilaya hiyo.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya hiyo wa kuwachagua viongozi wa nafasi mbali za ngazi hiyo huko Mahonda katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema matarajio ya CCM ni kuona viongozi wanaochaguliwa katika uchaguzi huo wanachukia kwa vitendo uwepo wa baadhi ya makada wanaoendekeza makundi, Safu na rushwa ndani ya chama hicho.

Dk.Mabodi alieleza kwamba msimamo wa CCM ni kuhakikisha Katiba, kanuni na miongozo inasimamiwa na kufuatwa ipasavyo ili kupata viongozi na makada wenye uwezo wa kuendeleza mafanikio ndani ya chama hicho kwa miaka mitano ijayo.

Aidha aliwambia viongozi watakaopata nafasi ya kuchaguliwa kupitia uchaguzi huo wahakikishe wanajenga ngome imara ya kisiasa katika wilaya hiyo sambamba na kuwashawishi wapinzani waliomo katika Wilaya hiyo kujiunga na CCM kwani ndio chama pekee kinachojali maslahi ya wananchi wote.
-Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akifungua Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" huko Mahonda katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Dk. Mabodi huko Mahonda.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano huo Balozi Seif Ali Idd akipiga kura katika uchaguzi wa CCM ngazi ya Wilaya ya Kaskazini "B" uliofanyika leo huko Mahonda katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika leo.

Tanzania Kushiriki Tamasha la 19 la Vijana na Wanafunzi nchini Urusi

$
0
0
Na. Eliphace Marwa .

JUMLA ya Vijana 31 wanatarajia kuiwakilisha Tanzania katika tamasha la dunia la vijana linalotarajia kufanyika Jijini Sochi nchini Urusi  kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 22 Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na ujumbe wa Vijana hao leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhiwa bendera ya Taifa,  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Erick Shitindi alisema tamasha hilo litakuwa na zaidi ya washiriki ishirini elfu kutoka nchi 150 Duniani kote.

 Shitindi aliwapongeza vijana hao kwa fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika tamasha hilo na kuwaomba kuitumia vyema fursa hiyo kwa ajili ya kuiwakilisha vema na kutangaza uzuri wa nchi viongozi kwa mataifa mbalimbali.

“Tamasha hili litatoa fursa kwenu vijana wa Tanzania na mtakapokuwa huko kuzungumzia mambo mazuri ya Tanzania na hasa kutangaza uzuri wa nchi yetu kwa vijana wa mataifa mengine” alisema Shitindi.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Erick Shitindi (katikati) akimkabidhi bendera mmoja wa vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Venerose Mtenga.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Venerose Mtenga toka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Erick Shitindi juu ya vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la Vijana na Wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi.

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Erick Shitindi (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.


WAZIRI WA NISHATI, WAZIRI WA MADINI NA MANAIBU WAZIRI WAO WARIPOTI RASMI OFISI ZA WIZARA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki, pamoja na Manaibu Waziri wa Wizara hizo wameripoti rasmi katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili katika Ofisi hizo, Mawaziri hao  walifanya kikao cha pamoja ili kufahamishana masuala mbalimbali. Kikao hicho kiliwahusisha pia  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe na Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mhandisi, Juliana Pallangyo.



Aidha,  Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo walifanya  kikao na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe, Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamishna Msaidizi wa Madini, Latifa Mtoro.



Viongozi hao wanaosimamia Sekta ya Madini, wanatarajia kufanya kikao na watumishi wa Wizara husika tarehe 10 Oktoba, 2017.Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu walikutana na Wafanyakazi wa Wizara husika na kutoa maagizo mbalimbali yatakayoboresha Sekta ya Nishati na hasa upatikanaji wa Umeme wa uhakika, unaotabirika na wa bei nafuu.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia), Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki (wa pili kushoto),  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa kwa kushoto) wakiwa katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) wakiwa katika kikao na Watumishi wa Wizara husika katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) wakiwa katika kikao na Watumishi wa Wizara husika (hawapo pichani )katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki (wa kwanza kulia),  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe (wa kwanza kushoto) wakiwa katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamishna Msaidizi wa Madini, Latifa Mtoro.

MAGAZETI YA JUMANNE LEO OCTOBER 10,2017

TAFCA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Na Sixmund Begashe.

Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dr John Pombe Magufuli kwa mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Manaibu wake ambao amewaapisha Ikulu Dar es Salaam jana.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa TAFCA bw Adrian Nyangamalle kupitia mtandao wa shirikisho hili kubwa hapa nchini ambapo pia bw Nyangamalle alichukuwa nafasi hiyo kumpongeza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe (Mb) kwa kubakizwa kwenye wizara yake ya awali pia Mh Juliana Daniel Shonza (Mb) kuwa Naibu Waziri mpya wa wizara hiyo.

“Kwa namna ya pekee tunampongeza Mhe. Juliana Daniel Shonza (Mb) kwa kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na vilele tunampongeza Mhe. Dr Harrison G. Mwakyembe (Mb) kwa kuendelea kuwa Waziri katika Wizara hii, kuendelea kwake kunaonesha namna Mhe. Rais wetu Dr John Joseph Pombe Magufuli alivyo kuwa na imani nae nasi tunatafasiri hivyo kuwa ni ishara ya utumishi wake uliotukuka “ Alisema Bw Adrian.

Bw.Nyangamalle ameongeza kuwa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania ambalo analisimamia litaendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa Mawaziri na viongozi wote wa Wizara hiyo katika kuhakikisha wanatimiza malengo ya kuinua Sanaa na Wasani hususani wale wanao jishughulisha na Sanaa za Ufundi nchini ambao wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.
Pichani ni Rais wa TAFCA Bw Adrian Nyangamale


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MADAKTARI BINGWA 18 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI ZANZIBAR

$
0
0

Na Mwandishi Maalumu, Riyadh- Saudi Arabia

Kundi la madaktari bingwa 18 wa hiyari kutoka nchini Saudi Arabia linatarajiwa kuwasili tarehe 12 Oktoba ambapo wataweka kambi ya tiba (medical camp) kwa muda wa majuma miwili. Madaktari hao wanatarajiwa kufanya matibabu na upasuaji katika hospitali za kisiwa cha Pemba.

Akizungumza katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh wakati wa hafla ya kuagana na madaktari hao, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, alisema kambi tiba hii ni ya pili kufanyika Zanzibar. Mwezi Novemba mwaka 2016 madaktari hao walifika Zanzibar na kuweka kambi ya kwanza katika kisiwa cha Pemba kwa mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa.

Mwaka jana madaktari hao walipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar na madaktari wenyeji, ndio maana wamependelea kurejea tena mwaka huu.

Pamoja na kutoa huduma za matibabu, madaktari hao watakwenda na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo Mwisho wa kambi watavitoa kama msaada kwenye hospitali hizo.
Katika picha ni viongozi wa Madaktari wakiwa na Balozi Hemedi Mgaza na Afisa wa Ubalozi Bw. Ahmada Sufiani walipofika Ubalozi mjini Riyadh kujitambulisha.

MAMLAKA ZAZUZUNGUMZIA AJALI YA DALADALA KUZAMA ZIWA VICTORIA.

$
0
0
Watu 12 wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria, kutumbukia katika fukwe za Ziwa Victoria katika eneo la Kingo Feri wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa tano asubuhi baada ya daladala hiyo yenye nambari za usajili T.229 DDW Toyota Hiace iliyokuwa ikitokea Buhongwa Jijini Mwanza kwenda kivukoni hapo kudaiwa kukatika breki ikiwa kwenye mwendo kasi.

KLABU YA NDANDA KUNG'OA MABANGO YA WADHAMINI

$
0
0
Bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Ndanda FC yenye maskani yake manispaa ya Mtwara Mikindani imeukana udhamini wa kampuni ya Maxcom Limited na Kiboko ambapo awali ulitangaza kutoa udhamini kwa klabu hiyo hivyo kuleta mvutano wa pande mbili kati ya wanachama na uongozi ambapo wanachama wandai kuwa na wadhamini wanne na huku timu ikiendelea kulalama ukata wa fedha

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA

$
0
0
Wananchi wa Halmashauri ya mji Geita, mkoani Geita wameendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la usajili na utambuzi linaloendeshwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. Zoezi hili ambalo kwa sasa linaendelea mikoa yote ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini limekuwa ni fursa nzuri na muhimu kwa wananchi kusajiliwa na kuwezeshwa kushiriki katika shughuli za maendeleo kutokana na umuhimu wa taarifa zinazokusanywa.

Pindi mfumo huu utakapokamilika wananchi watawezeshwa kupata huduma mbalimbali kwa urahisi pamoja na kusaidia Serikali kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi kwani Kitambulisho hiki kitakuwa ufunguo kwa mifumo mingine ya Serikali kubadilishana taarifa.
Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita katika foleni wakisubiri kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa, wakati wa zoezi la usajili linaloendelea mkoani humo.
Wananchi kata ya Bulela Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Mkoani Geita.
Wananchi kata ya Bulela Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Mkoani Geita.
Afisa Msajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, akiendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa kwa Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita.
Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiendelea na zoezi la uingizaji wa taarifa za wananchi katika zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika Halmashauri ya Mji Geita Mkoani Geita.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uratibu Ofisi za wilaya Bi. Rehema Kionaumela akitoa maelekeza kwa Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoani Geita kuhusu taratibu mbalimbali wakati wa maandalizi ya zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Geita.

DC Mkuranga kuwa mgeni rasmi kugawa nyumba Jumamosi

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani,Gilberto Sanga amekubali kuwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa,Julius Nyerere yatakayofanyika Oktoba 14,2017 katika kijiji cha wasanii Mwanzega wilayani hapa.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib alisema jana kuwa katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya atagawa nyumba 18 zilizojengwa na wanachama wa mtandao kwa njia ya kuchangiana na atakabidhi alama 55 kwa wanachama.

Alisema katika maadhimisho hayo ambayo SHIWATA huadhimisha siku hiyo kila mwaka kwa matukio mbalimbali mwaka jana walikabidhi fedha kwa watu waliopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoa wa Kagera.

Taalib alisema SHIWATA ambayo mpaka sasa imekwisha kabidhi nyumba 268 zilizojengwa kwa njia ya kuchangiana pia imekuwa ikiendesha matamasha ya wasanii mbalimbali kuonesha vipaji vyao.

Alisema Julai mwaka huu SHIWATA iliendesha tamasha la wasanii wote na Desemba mwaka huu kutakuwa na mashindano ya soka ambayo yalianza mwaka jana na timu ya maveterani ya Kitunda iliibuka kuwa mabingwa kati ya timu sita zilizoshindana.

Katika hatua nyingine wanachama wa SHIWATA ambao mashamba yao yanachukuliwa na serikali kwa ajili ya kujenga viwanda wameazimia kutafuta mashamba mengine kando kando ya reli ya Kati.

INTRODUCING NEW SINGLE "NAMPAGA" BY BARNABA CLASSIC


MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFURAHIA HUDUMA ZA NHIF KATIKA MAONESHO YA WIKI YA VIJANA NA UZIMAJI WA MWENGE YANAYOENDELEA KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA AMAAN - ZANZIBAR.A

$
0
0
Katika maonesho ya Wiki ya Vijana na Uzimaji wa Mwenge Makamu wa Rais wa pili Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa Maonesho hayo aliupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kutoa Elimu bure kwa wananchi wa Zanzibar kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza kama Shinikizo la Damu (BP), Sukari na uwiano wa Uzito na Urefu, lakini pia kwa upimaji wa magonjwa hayo bure.

Alisisitiza NHIF isiishie kwenye Maonesho hayo lakini iwe ikitoa huduma hiyo mara kwa mara pindi Mfuko upatapo fursa ya kufanya hivyo, vilevile Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Mfuko na Fao jipya la TOTO AFYA KADI kwani gharama yake ni nafuu, tofauti na gharama za matibabu ya afya mahospitalini aliuasa Mfuko uhamasishe fao hilo ili watu waweze kujiunga kwa wingi, kwani watoto ni Taifa la kesho, ili waweze kufikia malengo yao wanahitaji uhakika wa Afya zao.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unaendelea kuwakaribisha wananchi wazidi kujitokeza kwa wingi kuja kupima afya zao bure na vilevile kujiunga fao la Toto Afya Kadi, "Mfuko umejipanga kuhakikisha kila mwananchi anakua na kadi ya Bima ya afya, kwani ili kua na Taifa lenye maendeleo linahitaji wananchi wenye uhakika na huduma za Afya na Mfuko uko kwa ajili ya kuhakikisha hilo" alisema Meneja wa NHIF Zanzibar Bw. Ismail Kangeta.

Wiki ya Vijana inaadhimishwa kuanzia tarehe 8/10/2017 hadi tarehe 14/10/2017 kama sherehe ya Kumbukumbu ya hayati Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere.
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akielezewa jambo na Meneja wa NHIF Zanzibar Bw. Ismail Kangeta pindi alipotembelea banda la NHIF baada ya kufungua Rasmi Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Amaan.
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akicheki afya kwenye banda la NHIF, katika Maonesho ya Wiki ya Vijana.
Afisa wa NHIF Bw. Shabani Muhunzi akielezea jambo kwa mdau alietembelea banda la NHIF kwenye viwanja vya Amaan Zanzibar kwenye Maonesho ya Wiki ya Vijana.
Afisa Matekelezo wa NHIF Zanzibar Bi.Naima Aboubakar akiwaelezea vijana waliokuja kutembelea banda la NHIF kuhusiana na Huduma zitolewazo na Mfuko huo.

INTRODUCING "Kacheze Unapochezaga" by Z Anto

INTRODUCING "USINGOJE" BY MADADA SITA

TIPS TO ADHERE TO FOR YOUR SAFETY AT FUEL STATION IN TANZANIA.

new Art new Audiences (nAnA) projects announcements

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images