Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1948 | 1949 | (Page 1950) | 1951 | 1952 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwasili uwanja wa ndege wa Njombe, kwa ziara ya kikazi ya siku moja akitokea mkoani Ruvuma, ili kuzungumza na maafisa na askari wa Jeshi hilo pamoja na kuona changamoto wanazokutana nazo wanapotekeleza majukumu yao na namna ya kuwasaidia. 

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoa Njombe, kwa ziara ya kiazi ya siku moja 
  Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, ambaye yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na maafisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto wanazokutananazo wanapotekeleza majukumu yao na namna ya kuwasaidia.
  Picha na Jeshi la Polisi.


  0 0

  Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akimkabidhi kijarida cha Mfuko huo chenye maelezo ya shunguli mbalimbali zinazotekelezwa na PSPF, kwa Mwanachama wa Mfuko amabye ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mstaafu, Mzee Thomas Martin Kiama, (73), nyumabni kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja leo Oktoba 6, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto, ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, na Afisa wa Unedeshaji Bw. Ernest Massay.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambao ni wastaafu, wameupongeza Mfuko huo kwa kupata pensheni za kila mwezi kwa wakati.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya viongozi wa PSPF kutembelea Wanachama wake wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, walisema kimsingi malipo ya pensheni ya kila mwezi yamekuwa yakiingia kwenye akaunti zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.

  “Mimi nashukuru penshni yangu napata bila shida, na inaingia kwenye akaunti yangu kwa wakati, hili napenda kuwapongeza sana.” Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu). Bw. Thomas Martin Kiama wakati alipotembelewa na ujumbe wa PSPF nyumbani kwake Oysterbay jana (Oktoba 6, 2017).
  Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Bibi Mary Logway, ambaye ni mwanachama wa PSPF, akizungumza nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6, 2017, wakati alipotembelewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, kushoto.

  Najua zipo changamoto za hapa na pale, mimi ningependa muwe huru kabisa, ili muweze kutuhudumia vema sisi wanachama, vinginevyo huduma zenu nazifurahia, aliongeza Bw.Kiama, ambaye alistaafu mwaka 2005.

  Kwa upende wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, nchini, Bibi. Mary Hariet Longway, naye aliipongeza PSPF kwa utoaji wa huduma na kwamba yeye anaridhishwa na utedaji kazi wake na kuwapongeza kwa kufika nyumbani kwake ili kupata maoni yake.

  “Ninashukuru sana kwa kunitembelea kwani hii ni ishara ya jinsi mnavyotujali sisi wastaafu, lakini mimi kama Jaji mstaafu kwa utaratibu ulivyokuwa, sisi hatukuwa na bima za afya sasa kama mngetoa elimu ya jinsi ya kupata bima ya afya kupitia kwenu lingekuwa jambo jema.” Alishauri Bibi Longway amabye naye alistaafu mwaka 2005.

  Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wakwanza kushoto), akimsikilzia mteja (mwanachama) wa Mfuko, huku afisa aliye kwenye mafunzo kutoka Chuo Cha Usimamzi wa Fedha, (IFM), Bw. Paschal W. Divaz, (katikati), akifuatilia.

  Alsiema, malipo ya kila mwezi ya Pensheni yake yamekuwa yakiingia kwenye akaunti yake bila shida yoyote.


  0 0

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji jijini Dar es Salaam leo mara baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake yaliyokuwa Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi yake.
  Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa shtaka lake.
   Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa hukumu na kujulikana kuwa upande wa mashtaka hawakuweza kuthibitisha kama kweli alikuwa anatumia dawa za kulevya.
  .
   Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akielekea kwenye gari kwaajili ya kuondoka huku akiwa hana kosa mara baada ya kusomewa hukumu  na kuonekana kuwa hakuwa akitumia dawa za kulevya.

   Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akipanda gari akipanda gari mara baada ya kusomewa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabiri ya kutumia dawa za kulevya ikiwa upande wa mastaka walishindwa kuthibitisha shtaka hilo.
  Wakili wa Manji Bi. Hajra Mungula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya mteja wake kuonekana hana kosa la matumizi ya dawa za kulevya.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0

  BENKI ya CRDB tawi la Mlimani City kutoa mikopo kwa siku saba kwa wateja ambao ni wafanyabiashara wa kati (Small Medium Interpreses) ambao wataenda kukopa katika benki hiyo.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba.

  Amesema kuwa wiki hii ya huduma kwa wateja ni ya kukata keki na kufungua shampeini kwa wateja wa benki ya CRDB karibu kila tawi nchini kote kwaajili ya kuwashukuru wateja wake.

  Pia amewashukuru wafanyakazi wa Tawi lake kwa kufanya kazi kwa juhudi kama kuwajali pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vyeti vya shukrani.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akizungumza na wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam leo wakati alipotembelea katika tawi hilo kwaajili ya kudhimisha wiki ya Huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya Kwanza ya Oktaba kila mwaka. kushoto ni Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango.
   Mteja wa Muda mrefu, FaustaAssenga akikata keki kwaajili ya kushaherekea wiki ya huduma kwa wateja akishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay pamoja na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilango na wateja wa benki hiyo Tawi la CRDB. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay jijini Dar es Salaam leo akimlisha keki Mteja wa Muda mrefu wa Tawila CRDB tawi la Mlimani City, Fausta Assenga ikiwa ni kwaajili ya kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wki ya kwanza ya mwezi Oktaba kila mwaka.
      Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akiwakabidh vyeti vya shukrani wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Kilangowakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa muda mrefu wa Benki ya CRDB tawi la Mlima city.

  0 0


  0 0


   Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kikiendelea na zoezi la uzimaji moto uliozuka kwenye kiwanda cha Matairi cha Superdoll, kilichopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo. Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika. Globu ya Jamii inaendelea kufatilia tukio hilo na tutaendelea kujulishana.
   Harakati za uokozi zikiendelea.


  0 0


  0 0

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imehitimisha zoezi la uhakiki kwa Mashirika Masiyo ya Kiserikali nchini ulioanza Mwezi Agosti mwaka 2017.

  Akizungumza wakati wa kutoa taarifa kwa umma kuhusu kukamilisha zoezi hilo Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa jukumu la Wizara ni kusajili na kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mujibu wa Sera ya kitaifa ya Mashirikka Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001.

  Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kwa kuimarisha mifumo ya uratibu kwa kushirikiana na Halmashauri zote nchini.Bibi Sihaba Nkinga ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni zilizopo katika kuendesha kazi zao katika kuhudumia jamii.

  “Tumekamilisha zoezi hili kwa kipindi tulichokiweka na ninawaomba wadau wetu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo katika utendaji wa shughuli zao la kila siku” alisema Bibi Sihaba.bibi Sihaba mefafanua kuwa Mashirika ambayo hayakuweza kuhakikiwa kwa sababu za msingi katika kipindi chote cha uhakiki, yanatakiwa kufika Ofisi ya Msajili wa NGOs ili kukamilisha zoezi hilo na mara baada ya tarehe hiyo muda wa uhakiki utasitishwa na mashirika hayo hayataruhusiwa kufanya kazi yoyote nchini kwa kushindwa kuzingatia taratibu.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na waandishi wa habari Mjini Morogoro wakati akihitimisha zoezi la uhakiki wa NGOs nchini ulioanza Mwezi Agosti Mwaka 2017 kulia ni Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba.
  Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akiwashukuru wadau wa mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini kwa ushirikiano wao katika zoezi zima la uhakiki wa NGOs nchini kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga.
  Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wadau wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga( hayupo pichani) wakati wa zoezi la kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali nchini.


  0 0

  Jengo la Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa kaskazini Unguja,kwa ufadhili ya Sheikh Saaed Al Buwardy chini ua Usimamizi wa Sheikh Yakob Osmna na mtoto wake Adil Yakob Osman,[Picha na Ikulu.] 06/10/2017. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" kwa ufadhili wa SheikhSaeed Al Bwardy chini ya usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake AdilYakob
  Baadhi ya wananchi na Waislamu waliohudhuria katika uzinduzi wa Msikiti Masjid Saeed Al Buwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa kaskazini Unguja,kwa ufadhili ya Sheikh Saaed Al Buwardy chini ua Usimamizi wa Sheikh Yakob Osmna na mtoto wake Adil Yakob Osman.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa khutba ya uzinduzi wa Msikiti Masjid Saeed Al Bwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" kwa ufadhili wa Sheikh Saeed Al Bwardy chini ya usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake Adil Yakob
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa khutba ya uzinduzi wa Msikiti Masjid Saeed Al Bwardy uliojengwa katika Kijiji cha Kinyasini Bandamaji Wilaya ya Kaskazini "A" kwa ufadhili wa Sheikh Saeed Al Bwardy chini ya usimamizi wa Sheikh Yakob Osman na Mtoto wake Adil Yakob,[Picha na Ikulu.] 06/10/2017.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Kitengo cha Mawasiliano serikalini WAMJW

  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amewahimiza wanawake nchini kujiunga na vikundi vya kiuchumi katika kujiletea maendeleo.Ameyasema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya majaribio ya kuhamisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika katika wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

  Bibi Sihaba amesema kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi ni moja ya jitihada za utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000; Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/2022); Mpango wa Taifa wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/2021); na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.

  Ameongeza kuwa mwongozo wa uanzishaji wa vikoba utasaidia pia kuwa na takwimu za taarifa sahihi za vikundi kwa ajili ya uchambuzi na kujenga hoja kuhusu maamuzi ya ushiriki na uzingatiaji wa nafasi ya wanawake katika fursa mbalimbali.

  “Nijukumu la kila Mtaalamu wa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha mwongozo huu unatekelezwa ipasavyo na kuleta matokeo yaliyotarajiwa ya kuwawezesha wanawake kiuchumi ikiwemo kuboresha hali ya maisha yao” alisema Bibi Sihaba. Akiongea katika kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi amefafanua kuwa vikundi vingi vimekuwa vikiendeshwa bila kuwa na mwongozo na pia ukosefu wa elimu ya uendeshaji.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi wakimsikiliza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga( hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akifafanua jambo katika mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
  Mwezeshaji kutoka Shirika la Care Tanzania Bi Zenais Matemu akitoa mada katika Mafunzo ya majaribio ya mwongozo wa kuhamasisha wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi yaliyofanyika wilayani Mvomero mkoani Morogoro.


  0 0

  Mhe. Bahame Tom Nyanduga

  MWENYEKITI 

  TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA  0 0

  Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wametoa pongezi kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kutoa huduma bora zinazoendana na viwango vya kimataifa .

  Wakizungumza hii leo katika kilele cha wiki ya huduma kwa wateja, baadhi ya wateja waliofika ofisini hapo kupata huduma mbalimbali wamesema weledi na uharaka wa kupata huduma toka kwa wafanyakazi wa Mfuko huo ni jambo la kuigwa na taasisi nyingine nchini.

  Jessica Mmasy ni miongoni mwa wanachama waliofika kupata huduma hii amesema upotevu wa muda wa kungoja huduma katika ofisi mbalimbali imekuwa kikwazo kikubwa nchini lakini PPF wamepata suluhisho la changamoto hiyo.

  “Nimehudumiwa ndani ya dakika tano tu, kitu ambacho ni sehemu chache unaweza kukuta hivyo wanatoa huduma kwa makini wapo ‘professional’(weledi) na wanajali muda wa mteja,”

  amesema mteja huyo ambae alifika ofisini hapo kupata huduma. Naye Mustafa Adamu ambaye ni mwanachama wa PPF amesema mfumo wa utoaji huduma katika ofisi za PPF unatoa nafasi kwa kila mwanachama kuhudumiwa kwa usawa na bila manungúniko.

  “Hapa ukifika wa kwanza,utakuwa wa kwanza kuondoka pia,kuna mfumo maalumu wa kuhudumiwa kutokana na namba unayopewa hivyo hakuna kugombania kwenda kwenye dirisha la mhudumu,” alifafanua mteja huyo.

  Kwa upande wake meneja wa huduma kwa wateja wa Mfuko huo Michael Christina amesema wameienzi wiki ya huduma kwa wateja kama sehemu ya utendaji wao wa kazi wa kila siku.

  “Tumepata cheti cha kutoa huduma kwa kiwango cha kimataifa (ISO 900: 2015 certified) hivyo kutoa huduma bora ni jadi yetu kila siku katika utekelezaji wa majukumu yetu”,amesema meneja huyo.
  Meneja Uhusianao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Lulu Mengele (kushoto) akimwelezea huduma zinatolewa na Mfuko huo mwanachama wa PPF Mustafa Adamu (kulia) alipofika katika ofisi za Mfuko huo kupata huduma.
  Mwanachama wa PPF Wiliam Dagharo (Kushoto) akisisitiza jambo kwa mtoa huduma wa PPF katika ofisi za Mfuko wa PPF Makao Makuu jijini Dar es Salaam hii leo.
  Mwanachama wa Mfuko wa PPF Bi.Mkemwema Said (kulia) akipata huduma katika ofisi za PPF jijini Dar es Salaam hii leo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja duniani.
  Meneja wa huduma kwa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Michael Christian (Kushoto) akitoa huduma kwa mwanachama wa PPF Jessica Mmasy (kulia) aliyefika katika ofisi za PPF Makao Makuu jijini Dar es Salaam tarehe 6/10/2017 katika kilele cha wiki ya huduma wateja.
  Wateja mbalimbali wakipata huduma katika ofisi za Mfuko wa Pensheni za PPF hii leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewakabidhi timu ya African Sports “Wana kimanu manu”fedha milioni 2.1 kwa ajili ya posho za wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la pili Tanzania.Licha ya kukabidhi fedha hizo lakini pia aliwalipia kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF)Laki tano (500,000) kwa ajili ya leseni za wachezaji na ada ya ushiriki wa timu hizo.

  Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Waziri Ummy alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuiwezesha tmu hiyo kuweza kutimiza malengo yake ikiwemo kupanda daraja na kufikia hatua ya kucheza Ligi kuu soka Tanzania Bara.“Kwani iwapo timu hiyo itarejea Ligi kuu soka Tanzania Bara itasaidia kukua kwa fursa mbalimbali za kiuchumi katika Jiji la Tanga.

  “Sambamba na hilo lakini pia tumepokea mchango wa milioni 3 kutoka Kampuni ya GBP Oil ya Tanga ambao umeweza kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano wanayowakabili “Alisema.

  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na wachezaji wa timu ya African Sports kabla ya kuwakabidhi hundi milioni 2.1 leo
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi nahodha wa timu ya African Sports hundi ya milioni 2.1 leo wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hyo na wachezajiWAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya African Sports mapema leo mara baada ya makabidhiano hayo 
  Mmoja kati ya viongozi wa timu ya African Sports wakimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo .  0 0
  0 0


  0 0


  0 0

  Na Mathias canal, Singida

  Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida  Vijijini Mkoani Singida wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.

  Mkutano huo ulifanyika katika Kijiji na Kata ya Ilongelo na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.

  Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Manyoni aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni William Mwang'ima Nyalandu aliyepata kura 440, akifatiwa na FATUMA Ihonde aliyepata kura 189 na nafasi ya tatu ilikamatwa na Alex Mdidi Lissu aliyepata kura 159.

  Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika alisema kuwa uchaguzi huo umekamilika kwa amani na salama kwa kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi zilizoelekezwa na Chama Cha Mapinduzi.
  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
  Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Vijijini ikijihuzuru mbele ya wajumbe muda mchache kabla ya mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema(kushoto) akimsiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe alipokuwa anazungunza kuhusu namna benki ya Azania inavyowajali wateja wao wadogo wadogo, wa kati na wakubwa na kwenda nao bega kwa bega ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea pamoja nakueleza bidhaa walizonazo katika benki hiyo.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema akizungumza kuhusu changamoto na faida anazozipata kupitia benki ya Azania pamoja na kushauri namna nzuri kuwajali wateja wao mara alipotembelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kulia) ofisini kwake.
    Meneja wa benki ya Azania tawi la Tegeta, Geofrey S. Mahona(kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati wakifuatilia mazungumzo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema alipokuwa akisisitiza jambo kuhusu benki ya Azania.

  Mkutano ukiendelea wakati wakati wa maofisa wa benki ya Azania pamoja na Mkurugenzi wao walipomtembelea mteja wao ofisini kwake kwa ajili ya kutaka kujua ni changamoto zipi anazipata kwenye biashiara yake. Kushoto ni uongozi wa Hospitali hiyo na kulia ni viongozi wa benki ya Azania.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kulia) akimkabidhi hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema(wa pili kutoka kushoto).
  Picha ya Pamoja

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications,Francis Nanai(kutoka kushoto),Mhariri mtendaji wa magazeti ya Mwananchi Communications, Bakari Machumu, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka Kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba, Meneja Masoko Azam tv, John Mbele na Meneja Masoko Mwananchi Communications, Sarah Munema wakiwa na baadhi ya zawadi zitakazotolewa katika promosheni ya kuwazawadiwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti katika kipindi maalumu cha Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni ya SportPesa, Tarimba Abbas akizungumza katika hafla ya promosheni ya kuwazawadiwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti katika kipindi maalumu cha Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.
  Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu akizungumza akizungumza katika hafla ya promosheni ya kuwazawadiwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti katika kipindi maalumu cha Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wageni na wafanyakazi wa MCL wakiwa kwenye Kampeni ya Zali la Mwanaspoti iliyozinduliwa leo katika ofisi za Mwananchi Communications jijini Dar es Salaam.

  Gazeti maarufu la michezo nchini, Mwanaspoti, linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL),  limezindua promosheni maalumu inayofahamika kama Shinda Tiketi na ‘Zali la Mwanaspoti’.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mhariri Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu, alisema kuwa, promosheni hiyo inalenga kuwazawadia wasomaji wake, ambao wengi wao ni wapenzi wa michezo na burudani kujishindia zawadi mbalimbali, lakini pia kupata habari bora zaidi za michezo na burudani.

  Promosheni hii inakuja wakati ambapo, Gazeti la Mwanaspoti ambalo pia huuzwa nchini Kenya, likiwa limefanyiwa maboresho ya kina ikiwamo kubadili mwonekano, kuongeza safu za wachambuzi mahiri, wanamitindo maarufu na wasifu wa wanamichezo maarufu  kutoka nje na ndani ya Tanzania. 

  Kwa mujibu wa Machumu, lengo la MCL ni kuhakikisha kuwa wasomaji wa gazeti la Mwanaspoti wanapata habari zilizo bora na zinazokwenda na wakati na pia zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi wa kina.

  Alisema Machumu, katika promosheni hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na zawadi za kila siku, wiki na  za mwisho wa promosheni.

  Zawadi za kila siku ni pamoja na fulana na mipira ya miguu, jezi za timu mbalimbali za ligi kuu ya Uingereza. Wakati  zawadi wiki ni ving’amuzi vya Azam TV ambavyo vimeunganishwa na vifurushi vya bure kwa muda wa mwezi mmoja pamoja na pikipiki, simu za mkononi pamoja na bodaboda pamoja na washindi 8 watakaopatikana katika droo ya kila wiki, ambao watapata fursa ya kwenda Uingereza kushuhudia mechi mojawapo dhidi ya timu kubwa katika ligi kuu nchini humo.

  Kati ya washindi hao nane , mshindi wa droo kubwa ya mwisho wa promosheni  atapata nafasi ya kuchagua rafiki yake atakayetaka kusafiri naye kushuhudia mechi hizo kabambe.

  Droo za kila wiki zitakuwa zinarushwa kupitia televisheni ya Azam kwenye kipindi cha michezo cha Mshike Mshike kila Jumatano.

  Promosheni hii inadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa, ambapo Mkurugenzi wake, Abbas Tarimba, alisema kuwa lengo la kudhamini safari hiyo ni kuongeza hamasa ya watanzania kupenda michezo.

  Mdhamini wa pili ni Azam ambapo, Mwakilishi wake, John Mbelle ambaye ni Meneja Mauzo, alisema kuwa wameamua kudhamini promosheni hiyo kama wadau wa michezo nchini na pia kutoa ving’amuzi ili watanzania wapate fursa ya kushuhudia michezo mbalimbali kupitia Azam TV.

  Machumu aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kusisitiza kuwa, droo ya kwanza itafanyika baada ya wiki mbuili. “Hii ni fursa pekee na sisi tutafanya droo zetu kuanzia Mwezi Oktoba chini ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha,” alisema

  Machumu alimaliza kwa kutaja gharama za kampeni nzima hii ya “Zali la Mwanaspoti kuwa itagharimu shilingi milioni mia tatu (300,000 000/=).

  0 0
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa akizungumza kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, yatakayofanyika Oktoba 9, nchini, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akizungumza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kumkaribisha Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Deo Kwiyukwa (kushoto), kuzungumza nao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, yatakayoadhimishwa Oktoba 9, 2017. 

  Baadhi ya Wakurugenzi na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo, wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Postamasta Mkuu, Deo Kwiyukwa.

  Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kazini, wakichukua picha wakati Kaimu Postamasta Mkuu, Deo Kwiyukwa akizungumza katika mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1948 | 1949 | (Page 1950) | 1951 | 1952 | .... | 3285 | newer