Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1947 | 1948 | (Page 1949) | 1950 | 1951 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Tulizo Kilaga Lindi

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos Silayo amewataka meneja wa misitu nchini kusita kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watendaji wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye vituo vya ukaguzi wa mazao ya misitu.

  Ametoa agizo hilo leo tarehe 04/10/2017, alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa TFS Kanda ya Kusini katika ofisi za Wilaya ya Lindi ya Taasisi hiyo.

  “Kuna tuhuma za hovyo nimesikia, watu wanakamatwa na mazao ya misitu yaliyovunwa ama kusafirishwa kinyume na sheria, wanaombwa kitu kidogo na baadhi ya watumishi wasio waaminifu ili kuhalalisha mizigo hiyo na wakigoma, mizigo yao hukamatwa, nataka kuwaona mnachukua hatua stahiki,”amesema.

  Mtendaji Mkuu ameeleza kuwa licha ya TFS kuwa na changamoto nyingi anaimani na taasisi hiyo na amewataka watendaji wake kufanya kazi kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya na kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu, akiahidi Serikali kufanyia kazi changamoto zinazowakabili.

  Awali, Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini Ebrantino Mgiye alisema miongoni mwa changamoto zinazokabili taasisi hiyo ni pamoja na uhaba wa watendaji.

  Hata hivyo, Mtendaji Mkuu amewataka watendaji wa TFS kujikita katika utendaji wa kimkakati ili kuboresha usimamizi na uhifadhi wa raslimali za misitu na Nyuki kwa ajili ya kuchangia katika mahitaji ya kijamii, kiuchumi, ki-ikolojia, na ki-utamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos Silayo akiwa kwenye mkutano na watendaji wake wa Kanda ya Kusini (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuwataka meneja kuchukukua hatua kwa watendaji wasio waadilifu mapema hivi leo.
  Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini Ebrantino Mgiye (mwenye koti jeusi) akiwasolisha mafanikio na changamoto zinazoikabili kanda huku akifuatiliwa kwa umakini na Meneja Msaidizi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu Bw. Gaudence Kilasi (aliyekaa) mapema hivi leo.
  Baadhi ya Watendaji wa TFS Kanda ya Kusini wakichukua kumbukumbu katika Kikao cha Wafanyakazi kilichoendeshwa na Mtendaji Mkuu wa TFS Prof Dos Santos Silayo kuanza kuzungumza nao mapema hivi leo hii.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos Silayo akimfuatilia kwa umakini Kaimu Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Kusini Ebrantino Mgiye (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mafanikio na changamoto ya miaka mitatu ya kanda hiyo mapema hivi leo.


  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa

  Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji 130 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maarifa, kinyanmbo na zahanati ya Rungemba kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kuel kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini.
  “Nimetoa mifuko 130 ya saruji kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa madarasa katika shule mpya ya Maarifa na zahati ya Rungemba hii ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine ili kulifanya jimbo la Mafinga Mjini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Chumi.
  Chumi alisema kuwa halmashauri ya Mji wa Mafinga imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku mji ukiwa umeshapangiliwa jinsi gani ya kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hii.
  “Ukiangalia miji mingi inakuwa bila kuwa na mpango kabambe kitu kinachokuja kusababisha migogoro ya kugombea ardhi hivyo mpango huu utakuwa namanufaa makubwa kwa jimbo hili la Mafinga Mjini” alisema Chumi.Aidha Chumi alisema kuwa shule zilipata saruji hiyo ni shule mpya ya Maarifa nimekabidhiwa mifuko 50 ya saruji sawa na nyingine ya Kinyanambo lakini pia nimetoa mifuko ya saruji 30 kwa zahanati ya Rungemba lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

  Chumi amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata za ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la mafinga mjini.Naye mwenyekiti kata ya Changalawe Emmanuel Kuzugali ameelezea jinsi wananchi walivyochangia kuwezesha ujenzi wa shule ya msingi utakaoanzishwa katika kata hiyo.

  Kwa upande wake diwani viti maalumu kata ya changalawe Monica Luvanda ameelezea mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi wa shule ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo.
  Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya kuchochea maendeleo na kama unavyo muona akiwa anashusha safuji hiyo kutoka kwenye gari
  Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji akiteta jambo na wananchi waliofika katika eneo hilo alipokuwa akikabidhi saruji hizo.  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate, Bi.Theresia Soka akitoa ufafanuzi katika semina ya Jukwaa la Biashara lililofanyika mkoani Shinyanga jana. Jukwaa hilo lililoandaliwa na  Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kueleza na kuibua fursa mbalimbali za kibiashara na kiuchumi zinazopatikana mkoani humo.
    Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate, Bi.Theresia Soka akiwa na Wadau mbalimbali ktk jukwaa Hilo la biashara wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwa wasilishwa
  Picha ya pamoja ya washiriki wa Jukwaa la biashara  lililoandaliwa na  Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kueleza na kuibua fursa mbalimbali za kibiashara na kiuchumi zinazopatikana mkoani humo.

  0 0

  Mwendelezo wa zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye Matatizo ya Macho linaendelea na sasa ni Huduma ya Matibabu ya Macho kwa Wananchi waliobainika kuwa na Matatizo ya Macho kwenye Kampeni ya RC Makonda ya Upimaji wa Afya Bure.
  Zoezi hilo ni kufuatia ahadi iliyotolewa na *Jumuiya ya Waislamu wa Dhehebu la Khoja Shia Ithnasheri Jamaat K.S.I.J iliyojitolea kumuunga Mkono RC Makonda kwa kujitolea Matibabu ya wagonjwa watakaobainika kuwa na matatizo ya Macho na Mtoto wa jicho kwenye Kampeni ya Upimaji Afya Bure iliyofanyika Mnazi mmoja.
  Zoezi hilo linasimamiwa na *Madaktari bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Muhimbili, Hindumandal na Ebrahim Haji.
  Kutokana na uhitaji kuwa mkubwa RC Makonda ameomba Taasisi hiyo kupima na kufanya matibabu kwa Wagonjwa 1,000 badala ya 500 iliyoahidi ambapo wameridhia ombi hilo.
  Amesema kuwa kwa kawaida *Garama za upasuaji wa Macho ni kati ya Shillingi 900,000 hadi 1,000,000 pamoja na Miwani hivyo kwa Watu 1,000 ni sawa na Kiasi cha Shilling Billion Moja lakini kupitia wadau Wagonjwa hao watapatiwa matibabu na Miwani Bure ili waone Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano kupitia RC Makonda.
  RC Makonda Anawahimiza Wananchi wenye Matatizo ya Macho kufika kwenye kambi ya matibabu ya Macho iliyopo mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili ili wapatiwe Vipimo, Matibabu na Miwani Bure kwa wenye uhitaji.
  Ameshukuru wadau hao kwa kumuunga mkono na kueleza kuwa lengo lake ni kuwawezesha wananchi wasioweza kumudu gharama za matibabu kupata huduma.*

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiongea na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho
   Madaktari bingwa wa macho wakimhudumia mwananchi aliyejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho
  Madaktari bingwa wa macho wakimhudumia mwananchi aliyejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho.

  0 0

  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) anawatangazia wahitimu na wadau wote wa DIT kuwa Mahafali ya Kumi na Moja (11) ya Taasisi yamepangwa kufanyika Jumamosi, tarehe 16 Desemba, 2017.


  Mahafali haya yatatanguliwa na siku ya utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika mwaka wa masomo 2016/2017, sherehe ambazo zitafanyika Ijumaa, tarehe 15 Desemba, 2017.


  Taasisi inapenda kuwataarifu wahitimu wa Shahada ya Uzamili (M.Eng) na Shahada ya Kwanza (B.Eng/BTech), kusoma utaratibu na hatimaye kuthibitisha ushiriki wao katika  Mahafali hayo kupitia tovuti ya Taasisi (www.dit.ac.tz)


  Wahitimu watakaoshiriki wanapaswa kulipia joho la Mahafali Tsh. 50,000/= (kwa wahitimu wa Shahada ya Uzamili) na Tsh. 30,000/=(kwa wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika tawi lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145 na hatimaye kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz)Watakaoruhusiwa kushiriki Mahafali haya ni wale tu watakaokamilisha usajili wao.


  ZINGATIA: Malipo yafanyike kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu wa mwaka 2016/17 iliyopo kwenye tovuti ya Taasisi, namba ya usajili na madhumuni ya malipo yaani Mahafali.


  Kwa wanafunzi wa Stashahada (OD) ambao hawatavaa majoho wanatakiwa kuvaa nguo safi, nadhifu na zenye staha.  Na hawa wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia tovuti ya  Taasisi (www.dit.ac.tz) bila kulipia gharama zozote.


  “Rehersal” itafanyika Alhamisi, tarehe 14 Desemba, 2017.


  Mwisho wa kujisajili ni tarehe 15 Novemba, 2017.


  Atakayeona tangazo hili anaombwa kumjulisha mwenzake.


  Tangazo hili limetolewa na:


  Ofisi ya Uhusiano,

  Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,

  S.L.P 2958,


  Dar es Salaam.


  0 0
  0 0

  Wanawake wa halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wametakiwa kutumia jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kama chachu ya maendeleo yao na wanawake wote ndani na nje ya halmashauri hiyo kwa kukaa pamoja ili kujengeana uwezo na kushirikisha fursa za maendeleo. 

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Halmashauri ya Arusha Katibu Tawala wilaya ya Arumeru Timoth Mzava kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru amesema kuwa lengo la serikali kuanzisha majukwaa hayo ni kuwakutanisha wanawake pamoja kutumia fursa ili kuchochea maendeleo ya wanawake kiuchumi kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa na kutoa wito kuwa majukwaa hayo yatumike kwa lengo lililokusudiwa.

  Amesema kuwa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya taifa hili hivyo msiishie kuunda majukwaa tu badala yake mkatumie majukwaa haya kukabiliana na changamoto za kijamii, kiuchumi kwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yenu na zile zinazotolewa na serikali.

  Aidha amewataka wanawake hao licha ya Jukwaa hilo kujikita kwenye masuala ya kiuchumi lakini pia kutumia majukwaa hayo kusimamia malezi bora ya watoto, kupambana na mila na desturi potofu zinzomdhalilisha mtoto wa kike pamoja na kujikita kusimamia maadili ya vijana wetu kwa maendeleo ya taifa letu.

  "Jukwaa hili lisiishie kulianzisha tuu nendeni mbali zaidi tumieni Jukwaa hili kwa kuitumikia jamii yetu kwa kusimamia malezi bora hasa maadili ya vijana wetu, malezi ya watoto na familia kwa maendeleleo ya taifa letu" amesisitiza

  Jukwaa hilo la halmashauri ya Arusha limekutanisha jumla ya majukwaa 27 kutoka kata zote 27 za halmashauri ya Arusha na kuwakilishwa na wajumbe watano kutoka kila kata na kufanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wa Jukwaa la wanawake ngazi ya halmashauri.

  Katika uchaguzi huo jumla ya viongozi 7 walichaguliwa kwa kupigiwa kura na mmoja aliteuliwa, hata hivyo Anna Msuya amechaguliwa kuwa Mwenyekiti,Batuli Juma Makamu Mwenyekiti, Katibu ni Grace Seneu Mollel, Katibu msaidizi Nosimu Kornelo, Mweka Hazina Asha Said na mjube wa kuchaguliwa Chiku Mohamed na mjumbe mmoja wa kuteuliwa mwakilishi walemavu ndugu Jacline Leonard na kupata jumla ya wajumbe 8 amabo watawakilisha Jukwaa hilo ngazi ya mkoa.

  Akizungumza baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti Ana Msuya amewataka wanawake wote kuweka pembeni tofauti zao ikiwemo za kidini, kisiasa hata kiuchumi ili kukabiliana na changamoto nyingi zinazowakabili wanawake wa halmashauri ya Arusha.

  "Tunaposimama kwenye Jukwaa yatupasa kumuweka mwanamke kwanza, mwanamke ndio kila kitu, ili kupambana na changamoto zinazotukabili tunaweka mbali tofauti zetu pembeni kwa maendeleo yetu na taifa letu" amesema Mwenyekiti huyo.

  Aidha amewashukuru kwa kumuamini na kumchagua kuwaongoza na kuwaomba kufanyakazi kwa pamoja kama timu na kusisitiza kuwa hata wale ambao hawakuchaguliwa wanathamani sawa na wanawake wote waliochaguliwa hivyo amewataka kutoa ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa.

  Kabla ya uzinduzi wa Jukwaa hilo, wanawake hao walipewa mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kutambua na kutumia fursa mbalimbali, majukumu ya Jukwaa la wanawake kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa mpaka taifa pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto.

  Picha za matukio ya siku hiyo.


  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Katikati), Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo (Kulia), Mwingine ni Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor.

  Na Mathias Canal, Singida

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekutana na kufanya kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira kubaini kwa pamoja mbinu bora za kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao ya chakula na biashara kwa wingi.

  Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Maafisa kilimo na Mifugo, Maafisa Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maafisa Ugavi wa Kata sambamba na Maafisa Tarafa, Mhe Mtaturu alisema kuwa bado uzalishaji wa mazao ni mdogo katika Wilaya ya Ikungi ukilinganisha na hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kuwa na ardhi nzuri.

  Aliwataka wataalamu hao wa kilimo kuwasaidia wakulima ili kuiwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kuwa kilimo cha kibiashara kitakachowezesha kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupunguza umasikini kwa watanzania Sambamba na kujitosheleza kwa chakula. 
   Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.

  Mhe Mtaturu alisema Ili kuwe na kilimo kizuri na tija kwa wananchi, Wataalamu mnapaswa kuzingatia uwepo wa Pembejeo za kilimo na mbegu Bora za kisasa ambazo zinazalisha mazao mengi sambamba na kuhuisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuandaa mpango wa kujenga skimu za umwagiliaji ili wananchi waweze kuzalisha chakula cha kutosha mwaka mzima.


  Alisema kuwa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo tayari serikali imetoa tani 20 za mbegu za Pamba katika Wilaya ya Ikungi ambazo zitagawanywa kwa wakulima ili msimu wa kilimo unapoanza tayari ukata wa kucheleweshwa kwa mbegu hizo uwe umetekelezwa.
   Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa, wakati alipotembelea ofisi za Shirika hilo, kuona shughuli mbalimbali zinavyofanywa ikiwa ni muendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja, leo Oktoba 6, 2017. Shirika la Posta ni moja ya Mawakala wakubwa wa Benki ya CRDB wakishirikiana kwa zaidi ya miaka saba sasa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kulia) na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa, kwa pamoja wakikata keki kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kulia) akimkabidhi zawadi Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa, katika muendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kulia) na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji kutoka pande zote mbili.

  0 0

  Muwezeshaji wa Mafunzo kuhusu Mpango wa Matumizi bora ya ardhi kutoka Shirika la PELUM Tanzania, Josent Tesha akifafanua jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Ugesa Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kuhusu manufaa na faida ya mpango huo hivi karibuni. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la Pelum na kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
  Mwezeshaji wa Mafunzo kuhusu Mpango wa Matumizi bora ya ardhi kutoka Shirika la PELUM Tanzania, Simon Mbago akifafanua jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Ugesa Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kuhusu manufaa na faida ya mpango huo hivi karibuni. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la Pelum na kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

  SHIRIKA la PELUM Tanzania kupitia Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika sekta ya kilimo (CEGO) limefanikiwa kutoa elimu ya mafunzo kuhusu Mpango wa Matumizi bora ya ardhi kwa wananchi4,270 kutoka Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Iringa.

  Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwandishi wa Habari hii Mjini Morogoro, Afisa Tathimni na Ufuatiliaji wa Shirika la PELUM Tanzania Frank Maimu alisema katika awamu ya kwanza shirika hilo lilitoa mafunzo kwa wananchi 3,070 na awamu ya pili wananchi 1200 na na tathmini yao ilibaini kuwa kuna uhitaji mkubwa wa wananchi wengine kupatiwa elimu hiyo. Maimu alisema kuwa, kupitia mradi wa CEGO unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID), Shirika hilo lilihakikisha kuwa wananchi wanapatiwa elimu ya masuala ya ardhi kama njia mojawapo ya kuhakikisha mpango huo unakamilika kwa ridhaa ya wananchi wenyewe.

  “Katika mafunzo hayo tunatoa elimu kupitia mada mbalimbali ikiwemo Mpango wa matumizi ya ardhi kijijini, haki za ardhi kwa wanawake, haki ya kupata, kutumia na kumilikia ardhi Tanzania, utatuzi wa migogoro ya ardhi Tanzania pamoja na utawala wa kidemokrasia katika Jamii” alisema Maimu.

  Aliongeza kuwa kupitia mafunzo hayo ya mipango ya matumizi ya ardhi vijijini, wananchi hao pia waliweza kuelimishwa njia mbalimbali za kutatua migogoro ya ardhi, kufahamu umuhimu na haki wa kumiliki ardhi kwa makundi mbalimbali pamoja na wananchi kuweza kusimamia Serikali zao kuanzia ngazi za vijiji.

  Kwa mujibu wa Maimu alisema mbali na wananchi wa kawaida makundi mengine yaliyopatiwa mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kamati za maamuzi, mabaraza ya ardhi ya kijiji, mabaraza la kata pamoja na Halmshauri za vijiji.

  Kwa upande wake Devota Winga kutoka kijiji cha Nchinila Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma anasema kupitia mafunzo yanayotolewa na Shirika la PELUM Tanzania ameweza kufahamu haki zake za msingi katika masuala ya ardhi ikiwemo sheria ya umiliki wa ardhi jambo ambalo halikuwepo katika jamii zao siku za nyuma

  Naye Kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji cha Iduo Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Bi. Ashura Elianaki anasema idadi ya kesi za migogoro ya ardhi iliyokuwa ikiripotiwa katika Serikali ya Kijiji hicho kwa sasa imepunguakwani kwa sasa wananchi wengi wameweza kuelimika kupitia mafunzo ya Shirika la PELUM Tanzania.

  “Wananchi wengi sasa wameweza kuelewa na kufahamu kwa undani wa sheria zinasemaje na na aina ya kesi zinazopaswa kutafutiwa suluhu na zipi zinapaswa kusuluhishwa na vyombo vingine kwa kuanza kusikilizwa na Baraza la Ardhi la Kijiji na sio Serikali ya kijiji”.alisema Elianaki.

  Mbali na PELUM Tanzania kutoa mafunzo kwa wananchi wananchi 4,270 na kutekeleza Mpango wa matumiz ya Ardhi kwa vijiji vya mradi, Shirika hilo pia linatarajia kutoa hatimiliki za kimila 4883 kwa vijiji 25 vya awali ambavyo vimeshafanyiwa Mpango wa matumizi ya Ardhi.

  0 0

  Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakikata keki kwa pamoja kwa ajili ya kushiriki na Wateja wao ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea.
  Mfanyakazi wa Azania Bank,tawi la Moshi,Diana Ngaiza akimhudumia mmoja wa wateja wa Benki hiyo waliofika kwa ajili ya kupatiwa Huduma za kibenki.
  Baadhi ya Wateja wakipata Huduma katika madirisha ya Huduma ndani ya Benki hiyo.  0 0
 • 10/06/17--02:00: Article 8
 • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
   WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO 


  TAARIFA KWA UMMA.

  Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango inaendelea na juhudi za kusimamia, kudhibiti na kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kifedha ikiwemo mishahara ya watumishi na wastaafu wa Umma. Aidha, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Mashirika ya Bima, Mabenki, Taasisi za Fedha, Saccos na wadau wengine wameendelea kufanikisha utoaji huduma mbalimbali kwa watumishi na wastaafu wa Umma kwa kutumia taarifa za mishahara zikiwa kwenye nakala ngumu. 

  Hata hivyo, bado kuna changamoto mbalimbali katika upatikanaji wa taarifa hizo ikiwemo kuongezeka kwa gharama za uchapishaji na usambazaji wa nakala ngumu nchi nzima, usumbufu na gharama kubwa kwa watumishi na wastaafu kuzitafuta taarifa hizo Hazina na wakati mwingine kughushiwa. 

  Kutokana na changamoto hizo, Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa hati za malipo ya mishahara ya watumishi wa Umma unaojulikana kama “Government Salary Slip Self Service”. Mfumo huu unatumia taarifa sahihi zilizopo kwenye mfumo shirikishi wa taarifa za Kiutumishi na Mishahara (Human Capital Management Information System) wa Serikali ujulikanao kama “Lawson”. Utaratibu wa kujisajili na kutumia huduma hii kwa watumishi wa Umma unatolewa na waajiri wao.

  Walengwa na watumiaji wa mfumo huu ni watumishi wa Umma, Wastaafu, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Mashirika ya Bima, Taasisi za Fedha (Mabenki, Saccos) na wadau wengine wanaotoa huduma  kwa Watumishi wa Umma na wastaafu kwa kutumia hati za malipo ya mishahara (Salary Slip) ikiwa kwenye nakala ngumu.

  Wizara inapenda kuzitangazia Taasisi kuwa, huduma hiyo kwa sasa inapatikana kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia internet kwa masharti ya kusajiliwa kwanza ili ziweze kuondokana na matumizi ya nakala hizo ngumu kwa kutumia namba maalum ya mshahara wa mtumishi kwa mwezi husika (salary slip token) inayotolewa na mwajiri wake.

  Sifa za kusajiliwa kwa taasisi ni kutuma maombi yanayoambatana na namba za makato (Deduction Codes) za taasisi husika pamoja na orodha ya watumiaji wa mfumo wakiwa na taarifa zifuatazo; Namba ya mtumishi (Employee ID), Majina yake matatu, namba ya simu, anuani pepe, namba ya utambulisho iliyoko kwenye kitambulisho chake cha Taifa au namba iliyoko kwenye kitambulisho cha Mpiga Kura au namba ya hati ya kusafiria.

  Taasisi zinazotaka kujiunga na mfumo huu ziwasilishe Maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Barabara ya Jakaya Kikwete,Jengo la ‘Treasury Square’S.L.P 2802 DODOMA.
  Taarifa hii inapatikana pia katika Tovuti ya Wizara (www.mof.go.tz)

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Wizara ya Fedha na Mipango. 

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Yohana Mcharo (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, katikati ni Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo Bi. Imelda Mushi na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.  Mwenyeki wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Bi. Imelda Mushi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika hilo Yohana Mcharo na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

  0 0


  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo amempigia magoti mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuwasaidia kukarabati shule ya msingi Igeleke kwa kuwa miundo mbinu yake imeharibika na sio rafiki kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

  Akizungumza na blog bwana Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule hii kwanza toka mwaka 1978 hadi leo shule hiyo haijawahi kufanyiwa ukarabati wa kueleweka hivyo inahitajika kukarabatiwa haraka iwezekanavyo.

  “Mwandishi ukiangalia majengo ya shule hii unaona jinsi gani yalivyoaribika na ipo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa lakini viongozi wengi hawaingalii kwa jicho la tatu kitu kinachotupa shida sisi viongozi wa eneo hili” alisema Madembo

  Madembo alisema kuwa shule nyingi zilizojengwa miaka ya 1978 na kuendelea zinamiundombinu ilichoka hivyo serikali na viongozi wa kisiasa kuanza kuzitafutia mikakati ya kuzikarabati ili kuboresha taaluma kwa watoto wetu kuendana na karne ya sasa.
   Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakati wa kuzitambua changamoto zinazoikabili shule ya msingi Igeleke iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
   Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakiwa katika picha nawanafunzi wa darasa la saba
   Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua madarasa ambayo miundombinu yake imeharibika.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  1. Saa 4 Mwili wa marehemu kuwasili
   nyumbani. Kinondoni(Shamba) Bakwata Muslim
  2. Dua
  3. Saa 7.30  Chakula
  4. Saa 8.30 Kisomo
  5. Saa 9.30 sala ya maiti
  6. Saa. 9.45 sala ya Alasir
  7. Saa 10 mwili kuelekea makaburini  Kisutu

  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

  WALENGWA wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) wametakiwa kuanzisha vikundi vya ufugaji kuku ili waweze kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kutafuta dawa za chanjo zitakazowasaidia kukabiliana na ugonjwa wa mdodo na kideri(Newcastle diasese) ambao umekuwa ukiwasababishia hasara.

  Kauli hiyo imetolewa jana na Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Richius Bilakwata kwenye mikutano na walengwa wa vijiji vya Itebulanda na Nsenda wilayani Urambo.

  Alisema kuwa ili waweze kuepuka kupata hasara kutokana na kuku zao kushambuliwa na ugonjwa huo ni vema wakawa wananunua chanjo na kuwachanja.“Moja ya chanjo inaweza kuchanja kuku wengi kwa pamoja ni vema mkajiunga pamoja ili muweze kuchangia katika ununuzi wa dawa hiyo kwa urahisi” alisema Bilakwata.

  Aliwashauri walengwa kuwa wakati mpango huu wa kunusuru kaya ukielekea mwishoni ni vema wakajitihidi kutumia kipato kidogo wanachokipata kuwekeza katika miradi midogo kama vile ufugaji wa bata, kuku, mbuzi na mifugo mingine.

  Bilakwata alisema kuwa miradi hiyo itawasaidia wakati mpango huo utakapokuwa umekoma.Nao walengwa wengi walisema kuwa wamekata tama kuendelea na ufugaji wa kuku kwa sababu ya kushambuliwa na magonjwa kama vile mdodo na kideri.

  Hivi sasa kuku moja katika maeneo ya Urambo mjini anauzwa kwa wastani wa shilingi elfu 8 hadi elfu 12.

  0 0  0 0

   Keki ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki ya CRDB tawi la Tegeta Kibo jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mikopo Microfinance wa Benki ya CRDB tawi la Tegeta Kibo, Thadeus Tumaini akimpa zawadi Mteja wa Benki ya CRDB tawi la Tegeta Kibo, William Silawe ikiwa kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka.katikati ni  Meneja Mikopo wa Benki ya CRDB Tawi la Tegeta Kibo, Martha Ngowi.
    Meneja Mikopo wa Benki ya CRDB Tawi la Tegeta Kibo, Martha Ngowi na Meneja Mikopo Microfinance wa Benki ya CRDB tawi la Tegeta Kibo, Thadeus Tumaini wakimpa zawadi mteja wa Benki ya CRDB tawi la Tegeta Kibo na mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi la Eriki Hardware Tegeta jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja.
    Meneja Mikopo Microfinance wa Benki ya CRDB tawi la Tegeta Kibo, Thadeus Tumaini kulia na Meneja Mikopo wa Benki ya CRDB Tawi la Tegeta Kibo, Martha Ngowi.

   Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Tegeta Kibo jijini Dar es Salaam wakiwa katika pcha ya pamoja wakiwa wanasheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila wiki ya kwanza ya Oktoba kila mwaka.a kwa wateja.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0
 • 10/06/17--04:19: SHUKRANI
 • MAREHEMU HARRIS CHARLES MWAKITOSI
  (1941 - 2017)

  Familia ya Marehemu Harris Charles Mwakitosi wa Changanyikeni kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa msaada wa hali, mali na faraja walioutoa kwa familia katika kufanikisha shughuli zote za msiba wa Baba yetu mpendwa Mzee Harris Charles Mwakitosi aliyefariki ghafla tarehe 29 Agosti, 2017 Dar es Salaam na kuzikwa Kijijini kwao Mseke – Iringa tarehe 02 Septemba, 2017. Marehemu Harris Charles Mwakitosi alikuwa Mume wa Bi. Juliana M.E Mwakitosi na Baba wa Laura, Lina, Lilian na Arthur. Pia alikuwa Mkwe wa Gratian, Andrew na Upendo. 

  Kwa namna ya pekee familia inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Uongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge, Uongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Fr. Mvungi - Paroko wa Parokia ya Utatu Mtakatifu - Changanyikeni, Fr. Ngowi, Fr. Eugen Mwanyika, Jumuiya ya Mtakatifu Thomas – Changanyikeni, Majirani – Changanyikeni, Vikundi mbalimbali (social groups) vya marafiki wa watoto wa marehemu, Wana Mseke, Wana Uwemba na Wana Kantare. Asanteni sana kwa sala, maombi, misaada ya hali na mali na kujitokeza kwenu katika kutufariji na kututia nguvu wakati wa majonzi. 

  Aidha, tunapenda kutoa shukrani nyingi kwa majirani, ndugu, jamaa na marafiki kwa misaaada yenu ya hali na mali na pia kushiriki katika shughuli zote za msiba na mazishi. Shukrani kwa wote mliofika nyumbani, mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia mbalimbali kwa lengo la kutufariji na kututia nguvu, tumefarijika sana. Tunawashukuru kwa kutuonyesha upendo wa dhati katika kipindi hiki kigumu kwetu. Ni dhahiri msiba huu haukuwa wetu peke yetu, ulikuwa wetu sote. 

  Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mmoja peke yake, tunaomba mpokee shukrani hizi wote mliohusika kwa namna moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli yote ya msiba wa Baba yetu Mpendwa Charles Mwakitosi. Hatuna cha kuwalipa na itoshe kusema ASANTENI SANA na Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia mahitaji yenu ya kila siku.

  Familia inapenda kuwaalika nyote kwenye Ibada ya Shukrani ya Siku Arobaini (40) tangu kifo chake itakayofanyika katika Kanisa la Parokia ya Utatu Mtakatifu – Changanyikeni Siku ya Jumapili tarehe 08 Oktoba 2017 kuanzia saa 2:00 Asubuhi na baadaye kwenye chakula cha Mchana Nyumbani kwa Marehemu Changanyikeni kuanzia saa 7:00 Mchana.

  2 Timotheo 4:7 “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani  Nimeilinda”

  Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele umuangazie,
   apumzike kwa amani Amina.

  0 0

  MAREHEMU HARRIS CHARLES MWAKITOSI

  (1941 - 2017)

  Familia ya Marehemu Harris Charles Mwakitosi wa Changanyikeni kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa msaada wa hali, mali na faraja walioutoa kwa familia katika kufanikisha shughuli zote za msiba wa Baba yetu mpendwa Mzee Harris Charles Mwakitosi aliyefariki ghafla tarehe 29 Agosti, 2017 Dar es Salaam na kuzikwa Kijijini kwao Mseke – Iringa tarehe 02 Septemba, 2017. Marehemu Harris Charles Mwakitosi alikuwa Mume wa Bi. Juliana M.E Mwakitosi na Baba wa Laura, Lina, Lilian na Arthur. Pia alikuwa Mkwe wa Gratian, Andrew na Upendo.

  Kwa namna ya pekee familia inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Uongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge, Uongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Fr. Mvungi - Paroko wa Parokia ya Utatu Mtakatifu - Changanyikeni, Fr. Ngowi, Fr. Eugen Mwanyika, Jumuiya ya Mtakatifu Thomas – Changanyikeni, Majirani – Changanyikeni, Vikundi mbalimbali (social groups) vya marafiki wa watoto wa marehemu, Wana Mseke, Wana Uwemba na Wana Kantare. Asanteni sana kwa sala, maombi, misaada ya hali na mali na kujitokeza kwenu katika kutufariji na kututia nguvu wakati wa majonzi.

  Aidha, tunapenda kutoa shukrani nyingi kwa majirani, ndugu, jamaa na marafiki kwa misaaada yenu ya hali na mali na pia kushiriki katika shughuli zote za msiba na mazishi. Shukrani kwa wote mliofika nyumbani, mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia mbalimbali kwa lengo la kutufariji na kututia nguvu, tumefarijika sana. Tunawashukuru kwa kutuonyesha upendo wa dhati katika kipindi hiki kigumu kwetu. Ni dhahiri msiba huu haukuwa wetu peke yetu, ulikuwa wetu sote.

  Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mmoja peke yake, tunaomba mpokee shukrani hizi wote mliohusika kwa namna moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli yote ya msiba wa Baba yetu Mpendwa Charles Mwakitosi. Hatuna cha kuwalipa na itoshe kusema ASANTENI SANA na Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia mahitaji yenu ya kila siku.

              Familia inapenda kuwaalika nyote kwenye Ibada ya Shukrani ya Siku Arobaini (40) tangu kifo chake itakayofanyika katika Kanisa la Parokia ya Utatu Mtakatifu – Changanyikeni Siku ya Jumapili tarehe 08 Oktoba 2017 kuanzia saa 2:00 Asubuhi na baadaye kwenye chakula cha Mchana Nyumbani kwa Marehemu Changanyikeni kuanzia saa 7:00 Mchana.

   2 Timotheo 4:7 “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani  Nimeilinda” Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele umuangazie, apumzike kwa amani Amina.

older | 1 | .... | 1947 | 1948 | (Page 1949) | 1950 | 1951 | .... | 3285 | newer