Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1946 | 1947 | (Page 1948) | 1949 | 1950 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetoa ripoti ya robo mwaka tangu ianze kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini ( Hepatitis B) na kutoa tiba ya ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir .

  Akitoa taathimini hiyo leo jijini Dar es salaam,  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo John Rwegasha amesema  muamko ni mkubwa  ambapo katika kipindi cha robo mwaka , Hospitali ya Taifa Muhimbili imesajili wagonjwa  950 .

  Akifanunua amesema  hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi  ya wagonjwa itaongezeka na kufika   1800  .Hata hivyo kati ya hao , wagonjwa 540 ndio wamerudi tena Hospitalini kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa uchunguzi huku wagonjwa wengine wakishindwa kufika kutokana na sababu za mbalimbali hususani za kiuchumi , nakuongeza kwamba waliopo kwenye tiba ni  wagonjwa 40.

  ‘’Idadi ya wagonjwa imeongezeka mara dufu hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watafika wagonjwa 1800  lakini pamoja na changamoto hiyo hatuwezi kusimamisha huduma tutaendelea kutoa huduma kwani kwa upande wa dawa tumejidhatiti kwa miaka mitano , wagonjwa  hawa wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi  ili aanze kutumia dawa lakini  si wote wanaohitaji dawa’’ amesema DK. Rwegasha.
    Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai akisisitiza watu kujitokeza kupima afya ili kuthibiti homa ya ini pamoja na magonjwa mengine.

   Daktari Bingwa wa Magomjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, John Rwegasha wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza katika kongamano jinsi ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya mfumo wa chakula na ini.
   Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakifuatilia kongamano hilo.


  0 0

   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkuranga imekuja na mpango kabambe wa mfumo wa tehama ambao utaweza kusaidia mawasiliano kati ya Wananchi Wadau na Halmashauri zote nchini.


  Hayo yameleezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mhandisi Mshamu Munde alipokuwa akiwasilisha mpango huo kwa wajumbe wa Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(ALAT) unaondelea jijini Dar es Salaam.

  Munde amesema kuwa mfumo huo ambao unafahamika kama ELGA ambao unafanana kabisa na kama mfumo wa E.Gov ambapo mfumo huu utasaidia kufanya kazi kwa uraisi.


  “sisi kama Halmashauri ya Mkuranga tunataka mfumo huu uweze kusambaa nchi nzima hili Halmashauri ziweze kufanya mawasiliano ya kibiashara kwa uraisi na kuwawezesha wananchi wake” amesema Mhandisi Munde


  Munde ameongeza kuwa kama Halmashauri zote zitafanikiwa kutumia mfumo huu zitasaidia katika kuinua uchumi wa Viwanda kama anavyosema Mh Rais.

  Anasema umefika wakati sasa kwa wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia mfumo huu hiliwaweze kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania.
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde  akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(ALAT ) Juu ya mpango wa matumizi ya teknolojia ya huduma kwa njia ya mtandao ELGA.
   Wajumbe wa Mkutano wa 33 wa  Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   Wajumbe wa Mkutano wa 33 wa  Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  IDARA YA UHAMIAJI 
  WAGENI WOTE WENYE VIBALI VYA UKAAZI WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA OFISI ZA UHAMIAJI ZILIZOPO KATIKA MAENEO WANAYOISHI NA KUFANYIA KAZI WAKIWA NA VIBALI VYAO.

  Idara ya Uhamiaji inapenda kuwafahamisha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi mbalimbali na Wageni wote wanaoishi na kufanya kazi nchini kwamba wanatakiwa kuripoti na kuwasilisha taarifa za anuani zao zikiwemo na mabadiliko katika Ofisi za Uhamiaji zilizopo katika maeneo wanayoishi na kufanya kazi katika kipindi cha siku thelathini 30 tangu kutolewa kwa taarifa hii.

  Zoezi hili linafanyika kwa lengo la kuhuisha taarifa na kumbukumbu za Wageni wakaazi ambao baadhi yao wamehama maeneo yao ya awali na kuhamia sehemu nyingine na linafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 29 (1), (2) na 30 za Kanuni za Uhamiaji za Mwaka 1997 na Marekebisho yake ya Mwaka 2016, chini ya Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 Rejeo la Mwaka 2002.

  Aidha, ieleweke kwamba kutokufanya hivyo ni kosa kisheria chini ya Kanuni ya 29 (3) na 37 ya Kanuni za Uhamiaji za Mwaka 1997 na marekebisho yake ya mwaka 2016 chini ya sheria ya uhamiaji sura 54 rejeo la mwaka 2002.

  Imetolewa na

  SAMWEL RHOBBY MAGWEIGA
  KAMISHNA WA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MIPAKA,
  MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI,
  04 OKTOBA, 2017.

  0 0

  HUDUMA ya upasuaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imezidi kuimarika tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 2015 hadi sasa.

  Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa JKCI, Naiz Majani alipozungumza na waandishi wa habari.

  Dk. Naiz alikuwa akizungumza kuhusu upasuaji ulioanza kufanyika hospitalini hapo siku ya jumatatu kwa watoto waliozaliwa na magonjwa mbalimbali ya moyo.

  Alisema JKCI inafanya upasuaji huo ambao unatarajiwa kukamilika kesho (leo) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wenzao kutoka Shirika la Kimarekani la Mending Kids International ambapo jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.

  “Huduma za matibabu ya moyo zilianza rasmi kutolewa nchini mnamo mwaka 2008, hadi kufikia 2015 tuliweza kuwafanyia upasuaji watoto 200 pekee utaona hiyo ni ndani ya miaka saba ya kipindi hicho,” alisema.

  Aliongeza “Lakini mwaka 2015 tuliona vema kuanzisha kitengo maalumu cha upasuaji kwa ajili ya watoto, hadi kufikia mwaka huu tumeweza kuwafanyia upasuaji watoto zaidi ya 500 hiyo ni ndani ya kipindi cha miaka miwili pekee.

  “Kwa hiyo tunaona manufaa makubwa ya kuanzishwa kwa kitengo hiki kwani tumeweza kuokoa maisha ya watoto wengi ambao tungewapoteza, kwa mwaka serikali ilikuwa na uwezo wa kupeleka nje ya nchi watoto 40 hadi 80 kupatiwa matibabu haya,” alisema.

  Alisema pamoja na watoto hao, kuna wengine 145 ambao wanasubiri huduma ya upasuaji.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kozi mbalimbali kwa wanafunzi wa Wizara ya Ulinzi ya Uganda waliokuja kupata mafunzo katika chuo  cha mafunzo cha usafiri wa anga jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga , Dk. Daniel Kerenge akitoa historia ya chuo hicho katika utaoaji mafunzo mbalimbali ya usafiri wa anga jijini Dar es Salaam. 
   Kaimu Mkurugenzi Huduma za Usafiri wa Anga wa TCAA,John Chambo akizungumza juu ya ununuzi wa mitambo mbalimbali ya kisasa watayofunga kwa ajili ya uongozaji ndege , jijini Dar es Salaam.
  kulia ni Meneja wa Usafiri wa Anga uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere wa TCAA, Mwanajumaa Kombo.
  Sehemu mitambo ya kupata taarifa za ndege zinazoingia nchini na zile zinazotumia anga ya Tanzania.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  MAMLAKA ya Usafiri wa Anga (TCAA) kutumia zaidi ya sh.bilioni 70 kwa ajili ya miundombinu ya mitambo ya  kisasa itakayowezesha utekelazaji wa watumiaji wa usafiri anga kutumia miundombinu hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kutembelea miundombinu mbalimbali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ndege wa TCAA, John Chombo amesema miundombinu ya mitambo hiyo ni kwa ajili kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na teknolojia iliyopo kwa sasa katika usafri wa wa anga.

  Amesema mitambo hiyo ikifungwa kazi itarahisha kwenda kisasa katika usalama wa ndege katika viwanja ndege kwa zile zinazoingia na kutoka katika anga ya nchini.

  Chombo amesema miundombinu ya  mitambo mbalimbali  ya kuongozea ndege iliyopo bado inahimiri katika uongozaji wa ndege kinachofanya kununua ni kutokana na teknolojia iliyopo sasa ikiwa ni pamoja na uimarishaji huduma za usafiri wa anga.

  Aidha amesema mitambo katika usafiri wa anga ni miaka 10 hivyo kila baada miaka hiyo inahitaji kubadilisha ili kwenda na mazingira yaliyopo pamoja na teknolojia iliyopo sasa inabadilika wakati kwa kuzingatia ni usalama wa ndege zinazoingia na kutoka.

  Wakati huo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amefungua mafunzo kwa wanafunzi 24 wa Wizara ya Ulinzi ya Ulinzi ya Uganda katika kituo cha mafunzo cha usafiri wa anga cha TCAA.
  Amesema nchi ya Uganda imekuwa ikileta watu wake katika kupata mafunzo mbalimbali ya usafiri wa anga kituo hicho kwani hivi karibuni walihitimu wanafunzi 17 katika kituo hicho wa mamlaka ya usafiri wa anga wa Uganda.

  0 0


  Afisa Muuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Vedastus na Arianna Minghetti wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimnywesha maziwa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo bila ya kufungua kifua (Catheterization) katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.
  Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kufungua kifua na kuziba tundu la moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
  Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la Meding Kids la nchini marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) na kuzibua mishipa ya Moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
  Maafisa Uuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwezao wa Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakijadiliana kuhusu maendeleo ya wagonjwa waliolazwa katika chumba hicho baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.Picha na JKCI

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akifungua Baraza kuu la 47 la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania (Tanesco) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Tanga kulia ni Katibu wa Baraza hilo,Asmaa Myale wa Baraza kuu la wafanyakazi,Asmaa Myale.
  Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella .
  Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakiufuatilia kwa umakini 


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba hii leo amefanya ziara ya kikazi kutembelea Ofisi za Uratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.

  Katika Ziara hiyo Mhe. Makamba amepata fursa ya kuongea na Menejimenti ya Ofisi hiyo na kupata wasaa wa kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano zaidi baina yao.

  Awali, akimkaribisha Waziri Makamba, Mratibu Mkuu Bw. Issa Mlingoti amemshukuru Waziri Makamba kwa kufika na kuahidi kuimarisha ushirikiano katika nyanja za Elimu, ajira na fursa kwa pande zote za Muungano.

  "Sisi tumefarijika sana kwa ujio wako na tunategemea kuwa huu ni mwanzo na mwelekeo mzuri wa kuzidi kuimarisha mashirikiano baina yetu ikiwa sisi ni waratibu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" Alisisitiza Bw.Mlingoti

  Katika ziara hiyo Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wafanyakazi, kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuahidi kuzipatia ufumbuzi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika kikao wa watumishi wa Ofisi ya Uratibu - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Waziri Makamba amepata wasaa wa kuzungumza na Menejimenti na watumishi wa Ofisi hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Luthuli.
  Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Uratibu - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri January Makamba mara baada ya kutembea Ofisi zao zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na: Frank Shija – MAELEZO

  Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimeanzisha huduma ya Dawati la Mhasibu itayaofanyika kwa mara ya kwanza tarehe 07 Oktoba 2017 kuanzia saa 3: 00 asubuhi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaaam.

  Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Fred Msemwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na huduma hiyo leo jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Msemwa amesema kuwa kupitia Dawati hilo wahasibu, wataalam wa kodi, fedha na biashara watajumuika pamoja na kukutana na wananchi wa kawaida, wafanyabiashara wadogo na wakubwa na kuwapatia huduma bure.

  “Kupitia Dawati hili la Mhasibu litatukutanisha na wadau wengine wa masuala ya biashara na ujasiriamali hili kwa pamoja tuweze kutoa huduma za mbalimbali za kijasiriamali zianazohusisha masuala ya mahesabu bila ya malipo” alisema Dkt. Msemwa.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) Dkt. Fred Msemwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya Dawati la Mhasibu itakayofanyika tarehe 07 Oktoba 2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Dyoya James Dyoya na Afisa Mtendaji Mkuu wa TAA Bw. Patrice Sigungu.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) Dyoya James Dyoya (kushoto) akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma ya Dawati la Mhasibu itakayofanyika tarehe 07 Oktoba 2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TAA Bw. Patrice Sigungu na Mweneyekiti wa chama hicho Dkt. Fred Msemwa.


  0 0


  Na Thobias Robert- MAELEZO

  Bodi mpya ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetakiwa kusimamia vyema majukumu yake ya upatikanaji wa rasimali watu wenye weledi, sifa na haiba ambao wataisaidia serikali katika kufikia azma yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025.

  Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Angelah Kairuki alipokuwa akizindua bodi hiyo Jijini Dar es Salaam na kuitaka kuendesha kazi zake kwa uwazi na kwa kuzingatia Sheria kanuni na taratibu.

  “Mmeteuliwa katika kipindi cha miaka michache kabla ya Taifa letu kufikia mwaka 2025 ambapo tunalenga kuingia kwenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda hivyo mnalo jukumu kubwa la kulipatia taifa rasilimali watu yenye uwezo wa kutuwezesha kutimiza malengo hayo,” alifafanua Waziri Kairuki. 

  Waziri Kairuki alisema kuwa, katika kutekeleza majukumu yake bodi haina budi kutenda haki ili kuepuka malalamiko ya upendeleo wa aina yoyote, kujuana, ukabila, na ukanda ambavyo vimekuwa vikitolewa dhidi ya bodi ya Sekrtarieti ya Ajira,na kuwataka kuandaa mpango mkakati ambao ukitumika kila mwombaji wa ajira ataridhika.
  Katibu wa sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma Bw. Xavier Daudi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki jinsi ya ufanyaji kazi wa menejimenti hiyo katika uzinduzi wa Bodi mpya uliofanyika leo katika Maktaba Kuu ya Taifa Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki na pili kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro akitoa salama na kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi Sekritarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa ofisi hiyo uliofanyika Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kutoa kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki na pili kushoto ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi.
  Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimentiya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Sekritarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma pamoja na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa ofisi hiyo uliofanyika Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Laurent Ndumbaro.
  Mwenyekti wa Bodi mpya ya Sekritarieti ya Ajira katika utumishi wa umma Bi.Rose Lugembe katika uzinduzi wa tatu wa bodi pamoja na mkataba wa huduma kwa mteja uliofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo Maktaba Kuu ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam kulia ni moja ya wajumbe wa bodi hiyo Bw.Mbaraka Abdul Wakill.Picha na Paschal Dotto-MAELEZO.  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefungua mafunzo ya “Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga ikiwa ni jitihada inayofanywa na shirika la Twaweza kwa lengo la kupima uwezo wa watoto juu ya umahiri wao wa kusoma,kuhesabu na kuandika.  Mafunzo hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga,yameanza leo Alhamis Oktoba 5,2017. 


  Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akisema washiriki wa mafunzo hayo ni waratibu wa wilaya na waratibu wa vijiji kutoka wilaya nane za kanda ya Shinyanga inayojumuisha mikoa ya Dodoma,Singida,Simiyu na Shinyanga.


  “Mafunzo ya tathmini ya Uwezo yanafanyika nchi nzima na kwa upande wa kanda ya Shinyanga,yanafanyika hapa ambapo tunafundisha mbinu na taratibu za kufanya wakati wa kutekeleza zoezi la Tathmini ya Uwezo kwenye wilaya mbalimbali nchini Tanzania na mwaka huu zoezi litafanyika katika wilaya 56”,alieleza Mgoi.

  Alisema washiriki wa mafunzo hayo watafundishwa namna ya kufanya tathmini kuhusu uwezo wa watoto wenye kuanzia miaka 6 hadi 16 katika masomo matatu ya Kiingereza,Kiswahili na Hesabu.
  Aliongeza kuwa Twaweza kupitia tathmini ya uwezo imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuboresha elimu nchini.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo amefungua mafunzo ya “Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga katika ukumbi wa Karena Hotel leo Alhamis Oktoba 5,2017-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akielezea kuhusu Tathmini ya Uwezo
  Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akizungumza ukumbini.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Halmashauri ya Wilaya ya mkuranga imekuja na mpango kabambe wa mfumo wa tehama ambao utasaidia mawasiliano kati ya Wananchi Wadau na Halmashauri zote nchini.

  Hayo yameleezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mhandisi Mshamu Munde alipokuwa akiwasilisha mpango huo kwa wajumbe wa Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(ALAT) unaondelea jijini Dar es Salaam.

  Munde amesema kuwa mfumo huo ambao unafahamika kama ELGA ambao unafanana kabisa na kama mfumo wa E.Gov ambapo mfumo huu utasaidia kufanya kazi kwa uraisi.

  “sisi kama Halmashauri ya Mkuranga tunataka mfumo huu uweze kusambaa nchi nzima hili Halmashauri ziweze kufanya mawasiliano ya kibiashara kwa uraisi na kuwawezesha wananchi wake” amesema Mhandisi Munde
  Munde ameongeza kuwa kama Halmashauri zote zitafanikiwa kutumia mfumo huu zitasaidia katika kuinua uchumi wa Viwanda kama anavyosema Mh Rais.

  Anasema umefika wakati sasa kwa wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia mfumo huu hiliwaweze kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(ALAT ) Juu ya mpango wa matumizi ya teknolojia ya huduma kwa njia ya mtandao ELGA.
  Wajumbe wa Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa uliofanyika jijini Dar es Salaam
  Wajumbe wa Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa uliofanyika jijini Dar es Salaam--

  0 0

  Mkuu wa jeshi la polisi nchini TANZANIA, IGP SIMON SIRRO amesema wahalifu wote watafute sehemu ya kukimbilia ,amesema hayo wakati wa ziara yake mkaoni ruvuma wakati akizungumza na waandishi wa habari ,akitoa mkoani mtwara

  0 0

    Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) ofisi kwake Karimjee,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen.
   Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen akizungumza wandishi wa habari leo mara baada ya kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita aliyesimama katikati, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko. 
   Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaa Isaya Mwita ,kushoto Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen. 
  Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati akiwa pamoja na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko.Picha zote na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya wa jiji.

  0 0

   Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali, akikabidhi msada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa Msimamizi Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Hassani Hamis, Wafanyakazi wa Uhuru FM walipofika kituoni hapo, Sinza Jijini Dar es Salaam, leo, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere. kulia ni Mtangazaji wa Uhuru FM Aggrey Manzi na wanne kulia ni Meja Rasilimali Watu na Utumishi wa Uhuru FM Paul Mng'ong'o. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
   Watangazaji wa Uhuru FM Steven Mhina na Sheila Simba wakiwa tayari kutangaza Mbashara tukio hilo la  utoaji msaada
   Msimamizi Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Hassani Hamis (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhiwa msaana huo
   Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akikabidhi msada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa Msimamizi Mkuu wa Kituo cha kulelea Watoto yatima na wasio chini ya malezi ya wazazi wao cha CHAKUWAMA, Hassani Hamis, Wafanyakazi wa Uhuru FM walipofika kituoni hapo, Sinza Jijini Dar es Salaam, leo, kutoa msaada katika kampeni ya "Gusa maisha yake" iliyoanzishwa na kituo hicho cha radio ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere. kulia ni Mtangazaji wa Uhuru FM Aggrey Manzi. 
   uongozi wa Uhuru FM ukikabidhi Watoto wa kituo hicho baadhi ya vitu vya msaada
   Watoto wa kituo hicho wakienda kuhifadhi baadhi ya vitu ambavyo Uhuru Fm ilikabidhi


  0 0

  Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu limeendelea leo mkoani Songwe, ambapo zaidi ya Kata 5 tayari zimekamilisha Usajili huo uliolenga kukusanya taarifa sahihi za watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wakiwemo wageni wanaoishi kihalali mkoani humo.

  Wakazi wa Songwe na Mbozi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kunufaika na manufaa mapana ya Kitambulisho hicho na pia kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora zaidi.
  Afisa Usajili Wilaya ya Mbozi Ndugu Eckson Mwakyembe akiwa na Mtendaji wa Kijiji cha Mlowo Bi. Judith Mtega wakikamilisha fomu za maombi ya Usajili za wananchi wa vijiji vya Shuleni, Mtakuja, Mlowo na Kiwandani kata ya Mlowo wakati zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa likiendelea wilayani humo.
  Meneja Mifumo ya Komputa wa ndugu Francis Saliboko akifanyia matengenezo ya kiufundi moja ya kifaa kinachotumika wakati wa usajili katika zoezi linaloendelea Kata ya Mlowo – Mbozi mkoani Songwe. 
  Maafisa Usajili wa NIDA wakifanya kazi ya kupiga picha na kuchukua alama za kibaiolojia katika zoezi linaloendelea kata ya Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe. 
  Afisa Usajili Bi. Coletha Peter na Bi. Magreth Moshi wakisaidia taratibu za kuchambua na kuhakiki fomu za maombi ya Vitambulisho za wananchi wa kata ya Mlowo kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kupiga picha, kuchuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki.
  Mwananchi wa kata ya Mlowo akichukuliwa alama za vidole, picha na kuweka saini ya kielektroniki wakati wa Usajili Vitambulisho vya Taifa. kushoto ni Afisa Usajili Ndugu Baraka Haonga.

  0 0


  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo mjini Bagamoyo. Kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bi. Fransisca Muindi na Mkurugenzi wa Utumishi, Bi. Ediltruda Maseko.
  Maafisa Rasilimali Watu wa TPA wakiwa katika semina hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amefungua semina ya siku tatu (3) kwa Maafisa Rasilimali Watu wa TPA ambao wanafanyakazi katika maeneo mbalimbali ya Bandari hapa nchini. 

  Semina hiyo inayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Wauguzi Bagamoyo inaenga kuwajengea uwezo Maafisa hao kuhusiana na masuala mazima ya Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002.

  0 0


older | 1 | .... | 1946 | 1947 | (Page 1948) | 1949 | 1950 | .... | 3286 | newer