Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1944 | 1945 | (Page 1946) | 1947 | 1948 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Ismail Ngayonga,MAELEZO

  JIJI la Dar es Salaama ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi kubwa duniani, huku ukuaji huo ukiathiri sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo sekta ya usafirishaji.

  Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 inakadiria kuwa jiji la Dar es Salaam lina wakazi milioni 2.4 na kuwa na kiwango cha ongezeko la idadi ya watu cha asilimia 4.4 kwa mwaka huku ongezeko hilo likisababisha kujitokeza kwa mapungufu katika utoaji wa huduma mbalimbali.

  Tangu miaka ya 1990 kumekuwa na mipango mbalimbali ya kuboresha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo kuanzisha barabara za njia moja, kuanzisha maegesho ya magari ya kulipia, na kuhamasisha kujengwa kwa majengo yenye maegesho ya magari.

  Pamoja na jitihada za serikali ya jiji la Dar es Salaam na serikali kuu kuboresha usafiri Jijini humo, bado kuna kero kubwa ya usafiri wa abiria, hasa wakati wa saa za asubuhi na jioni ambapo ambapo ilimlazimu mwananchi kuchukua takribani masaa matatu, kwa mfano, kutoka Mbezi Juu hadi katikati ya jiji.

  Katika kukabiliana na changamoto hiyo, tangu mwaka 2008 Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam imekuwa ikitekeleza miradi maalum ya ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu za Jijini Dar es Salaam.

  Mhandisi Miradi wa Ofisi ya TANROAD Mkoa wa Dar Es Salaam, Julius Ngusa anasema mradi wa ujenzi wa barabara za pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam wa awamu ya tatu ni moja ya mikakati ya Serikali ya kushughulikia tatizo sugu la msongamano wa magari katika Jiji hilo ambapo utekelezaji wake ulianza tangu wa mwaka wa fedha 2008/2009.

  Anasema kupitia mradi huo, Serikali ilichagua barabara tisa kwa ajili ya kujengwa katika kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Ubungo Bus Terminal-Kigogo-Kawawa (6.4 km), barabara ya Jet Corner-Vituka-Davis Corner (km 12), barabara ya Kinyerezi-Kifuru-Msigani-Mbezi mwisho (10 km), Tanki bovu-Goba (9.0 km), Kimara baruti-Msewe-Changanyikeni (2.6 km).

  Anazitaja barabara nyingine kuwa ni pamoja na Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi/Morogoro (km 20) , Kigogo Round about-Jangwani-Twiga katika bonde la msimbazi (km 2.72), Tabata Dampo-Kigogo na Ubungo Maziwa- Mabibo External (Mandela) (2.25 km).

  Mhandisi Ngusa anasema miradi hiyo inajengwa katika awamu tatu za utekelezaji, ambapo hadi sasa awamu ya kwanza ya miradi hiyo iliyohusisha ujenzi wa barabara zenye jumla ya kilometa 19.42 tayari imekwishatekelezwa na kukamilika tangu mwaka 2008.
  Anaitaja miradi iliyokamilika ni pamoja na barabara ya Ubungo-Kigogo-Kawawa iliyokamilika mwaka 2010 kwa gharama ya Tsh. Bilioni 11.44, barabara ya Kigogo-Msimbazi-Jangwani iligharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 7.64 ambayo ilikamilika mwaka 2017 pamoja na barabara ya Jet Corner-Vituka-Devis Corner iliyokamilika mwaka 2011.

  “Kuhusu Awamu ya pili yenye urefu wa kilometa 27.5 na ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40, ujenzi wake ulianza mwaka 2014 ambapo hadi sasa kazi za ujenzi zilizokamilika kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Tangi Bovu (Samaki Wabichi)-Goba km 9 ilikamilika mwaka 2016 kugharimu kiasi Tsh. Bilioni 8.6 ” anasema Ngusa.


  0 0


  MRS CATHERINE SHELUKINDO SAGUTI

  September 1936 - October  2009

  Mama since they day you departed thing are no longer the same. They see us smiling laughing and doing other things but it's just by the grace of our Lord Jesus Christ. 

  You are missed dearly by Baba Mzee Saguti your children's, in-laws, grand children and great grand children's, your only sister, friends and neighbors. Mama Rest in Peace. Will meet when the time comes. Luv you Mama.

  0 0

  Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akimkabidhi kipeperushi chenye namba ya dharura 114 ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egird Mubofu (kulia), wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akielekea katika ukumbi wa Mikutano kwa mazungumzo, akiwa ameambatana na mwenyeji wake ambaye ni Afisa habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bi. Neema Mtema (wapili kulia), pamoja na Maafisa wa Jeshi mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Shirika hilo, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jesuald Ikonko, akimuelezea majukumu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mwenyekiti wa Kikao Kaimu Mkuu wa Kitengo cha uhakiki (HCERT), Eng. Agnes Kiweru ambaye hayupo pichani, wakati wa Kikao cha kujadili uingizwaji wa vifaa nchini vya kinga na tahadhali dhidi ya majanga ya moto, visivyo kidhi viwango kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Tarehe 25 mwezi wa tisa msanii wetu wa Pangani Bi Flora Nicholas Mdahila ambaye aliigiza kwenye filamu ya AISHA kama Miriam, mdogo wake wa AISHA aliteuliwa kwa ajili ya TUZO inayoitwa SOTIGUI AWARD, huko Ouagadougou nchi ya Burkina Faso. 

  Flora ni mwenyeji wa Kijiji cha Msaraza, kata ya Bushiri. Kuigiza kwenye filamu ilikuwa ndoto yake tangu alipokuwa mtoto.Kabla ya kuchaguliwa kushiriki kwenye filamu ya AISHA, Flora alicheza kwenye vikundi mbali mbali vya sanaa hapa Pangani kwa ajili ya kuboresha kipaji chake. 

  Juhudi zake hazikuwa bure. Wataalamu wa filamu walikiona kipaji chake. Kwa hiyo aliteuliwa kwa ajili ya kundi la Tuzo ya Sotigui ya Mashariki ya Afrika. Lengo la tuzo hii ni kutangaza na kukuza vipaji vya wasanii wa Kiafrika duniani.

  Filamu ya AISHA ilitengenezwa mwaka 2015 wilayani Pangani kama sehemu ya mradi wa mawasiliano ya shirika la UZIKWASA. Ni filamu ya Wanapangani na wasanii zaidi ya asimilia 90 walioigiza kwenye Filamu ni wenyeji wa Pangani. 

  Filamu hii ilipata sifa kubwa hapa Tanzania na dunia nzima. Ilifanikiwa kupata tuzo mbali mbali ya kimataifa huko Marekani, Ulaya na nchi mbali mbali za kiafrika. 

  Sasa ni zamu ya Flora kupata tuzo. Tutaendelea kuwataarifu kuhusu yatakayotokea. Sisi UZIKWASA tunasikia fahari sana na tunampongeza Flora kwa mafanikio haya makubwa.


  0 0


  Thobias Robert – Maelezo

  Bodi ya ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) imetakiwa kuhakikisha inaimarisha utoaji wa elimu bora na yenye viwango kwa watumishi wa umma ili kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotaka watumishi wenye weledi na wenye maadili katika sekta za umma na binafsi.

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki alipokuwa akizindua Bodi ya washauri wa chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.

  Waziri Kairuki ameeleza kuwa ni wakati sasa kwa chuo hicho kuwa mfano bora wa kutoa watumishi ambao watarejesha nidhamu, utumishi bora na uadilifu wa hali ya juu katika sekta za umma na binafsi ili kumaliza tatizo la watumishi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo viovu kama rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.

  “Chuo cha utumishi wa umma hapa nchini kilianzishwa kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma, hivyo Bodi ya ushauri wa chuo cha utumishi wa umma wa Tanzania inalo jukumu la kuhakikisha kuwa lengo hili linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa,” alisema Waziri Kairuki.
  Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Henry Mambo akitoa taarifa ya chuo hicho wakati wa uzinduzi wa bodi ya ushauri ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Henry Mambo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania pamoja na menejimenti ya chuo hicho wakati wa uzinduzi wa bodi ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Msemaji wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSPF , Msafiri Mugaka akizungumza na Wajumbe wa mkutano wa 33 wa Mamlaka ya Serikali za Mitaaa(ALAT) Juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo na faida zake pindi watakapofikia umri wa kustaafu
   Wajumbe wa Mkutano huo kutoka Mkoa wa Songwe wakiongozwa na Mbunge wa Ileje , Janeth Mbene wakifuatilia mada kutoka kwa msemaji wa PSPF
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Alat wakifatilia mada kutoka kwa Msemaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo

  0 0

  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akisikiliza Maelezo kutoka kwa washiriki tofauti wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Ustawi wa Jamii nchini katika moja ya eneo la maonesho ya masuala yahusuyo Ustawi wa Jamii wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akipokea moja ya kitabu kinachoelezea masuala mbalimbali ya Ustawi wa Jamii kutoka kwa mshiriki wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa TASWO Dkt. Zena Mabeyo akitoa salamu za wananchama wa TASWO kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kulia waliokaa) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa wa Ustawi Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya JSI Dkt.Tuli Tuhuma akitoa maelezo kuhusu kazi za Taasisi yake kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(kulia waliokaa) katika kuleta ufanisi wa kazi za Ustawi wa Jamii nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maafisa Ustawi wa Jamii nchini uliofanyika UDOM Mjini Dodoma.


  0 0

  1Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akijadili masuala ya kiutumishi na utawala bora na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) nchini, Bw. Andrew Karas alipomtembelea ofisini kwake leo.

  2Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) nchini, Bw. Andrew Karas alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala ya kiutumishi na utawala bora.

  0 0

  Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (kushoto) akizungumza kuhusu ushirikiano wa kibiashara na Tanzania alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (kushoto) akizungumza jambo aliokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa tatu kulia) kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na uwekezaji, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), wakimsikiliza kwa makini Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (hayupo pichani) alipokua akizungumzia mazingira bora ya kibiashara kwa maendeleo ya Taifa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akieleza kuhusu uimara wa Serikali katika kusimamia mazingira bora ya biashara ili kusaidia kuinua Sekta binafsi nchini, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Kamisha wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi (kulia) akizungumzia masuala ya kodi katika Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga.
  moja wa wajumbe walioongozana na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza nchini Tanzania, (katikati) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Mwakilishi wa masuala ya biashara wa Uingereza Bw. Lord Clive Hollick (kushoto), mkutano huo umefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa tatu kulia), Mwakilishi wa Biashara wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. Lord Clive Hollick (wa nne kushoto) na Maafisa waandamizi kutoka Uingereza na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano kuhusu Biashara kati ya nchi hizio mbili Jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – WFM)

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Lugimbana akimkaribisha Mjumbe Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa Tanzania katika masula ya Biashara, Lord Clive Hollick mapema leo Ofisini kwake
    Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Lugimbana akizungumza na Mjumbe Maalim wa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa Tanzania katika masula ya Biashara, Lord Clive Hollick mapema leo Ofisini kwake
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Lugimbana akizungumza na Ujumbe alioongozana nao Mjumbe Maalimu wa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa Tanzania katika masula ya Biashara, Lord Clive Hollick mapema leo Ofisini kwake mjini Dodoma.


  0 0
 • 10/04/17--11:12: JPM

 • 0 0


  0 0


  0 0  0 0
  0 0

  Na Mwandhishi Wetu
  Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imeanza kuwatembelea wateja wake katika maeneo yao ya kazi ili kusikiliza kwa ukaribu changamoto wanazokutana nazo zinazohusu  huduma za kibenki, ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa kuwa wateja wake.

  Aidha, katika wiki hii ya huduma kwa wateja, Benki ya Azania imemtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Azania Bank Limited, Ndugu Charles Jackson Itembe, ambaye pia ameongoza msafara wa kutembelea wateja katika maeneo yao ya kazi, ambapo mteja aliyetembelewa leo na Benki hiyo, Ndugu Augustine Nyato amekabidhiwa hati ya kuthaminiwa pamoja na biashara ya mteja huyo kuwa katika biashara watakazozipa kipaumbele.

  Akizungumza na mteja huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe amesema ikiwa Azania Benki inamjali mteja wameamua kuwatembelea wateja wadogo, wa kati na wakubwa ili kuwapa shukrani kwa kuendelea kuwa na wao katika biashara kwa kipindi kirefu na hata kwa kipindi kijacho ili kunafaika na benki hiyo.

  Naye Mteja huyo ambaye ni Mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company Augustine Nyato ameishukuru benki ya Azania kwa kutambua mchango mkubwa wa wateja wao mpaka wakaamua kumtembelea ili kusikiliza changamoto anazozipata katika benki hiyo pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana vyema katika kutoa huduma iliyobora ili kufikia malengo aliyojiwekea.

  Wiki ya huduma kwa wateja imeanza rasmi Jumatatu ya Oktoba 2, 2017 na itamalizika baada ya wiki moja. Ni wakati wa taasisi kuwa karibu zaidi na wateja wake. Ni wakati wa kwenda bega kwa bega katika kuleta maendeleo kwa taifa letu.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akizungumza na mteja wa benki ya Azania ambaye ni mfanyabiashara na mkurugenzi wa  Israel Aaron & Company  Augustine Nyato kuhusu benki hiyo ilivyoamua kuwatembelea wateja wake katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto) akimkabidhi  hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania, Bwana Augustine Nyato leo ofisini kwake katika mtaa wa Survey jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Tawi wa Benki ya Azania  Tawi la Masdo, Benson Msuya.
  Mteja wa Banki ya Azania bwana Augustine Nyato( wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kushoto), Meneja wa Tawi wa Benki ya Azania  Tawi la Masdo, Benson Msuya(wa pili kutoa kulia) na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati (kulia).

  0 0


  0 0


  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro ameuhakikishia Uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) dhamira waliyonayo ya kuhakikisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea waishio mkoani humo hususani katika Wilaya ya Arusha wanasajiliwa Vitambulisho vya Taifa kwa wakati uliopangwa.

  Kauli hiyo ameitoa leo alipokutana na uongozi wa Mamlaka, kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kuendesha zoezi hilo ambalo litaanza rasmi katika Wilaya hiyo Ijumaa Kata za Sekei, Themi na Sombetini.

  Katika awamu hii ya kwanza takribani wananchi 45,000 watasajiliwa. Ametoa wito kwa wadau wote wakiwemo viongozi wa Dini, wanasiasa na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanasaidia kuhamaisha wananchi kushiriki kikamilifu zoezi hili ambalo lina manufaa makubwa katika maendeleo ya Taifa. Aidha; ameonya zoezi hilo kuhusishwa na siasa.

  Naye Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Viola Lazaro Likindikoki ameahidi ofisi yake kwa kuhusisha wadau muhimu kushiriki kikamilifu kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, na kwamba wakazi wa jiji hilo wanahamasishwa kushiriki.

  Viongozi wengine waliopata fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na uongozi wa NIDA ni Naibu Katibu Tawala wa Mkoa huo na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Arusha Bwana Ali Mohamed. Wilaya zingine za Mkoa wa Arusha tayari zimeanza zoezi la Usajili zikiwemo Monduli, Arumeru na Karatu.
  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akiwa kwenye kikao na Uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kujadili kuanza kwa zoezi la Usajili Wilayani humo.
  Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Viola Lazaro Likindikoki alipokutana na watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kujadili mpango wa Usajili kwenye Halmashauri hiyo.
  Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ndugu David Mwakiposa akizungumza na Viongozi wa NIDA walipotembelea ofisi yake leo kukamilisha mpango wa Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi na wageni wanaoishi mkoani humo.


  Kamishna Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Arusha Bw. Ali Mohamed akisikiliza kwa makini mpango wa utekelezaji zoezi la Usajili wananchi mkoani humo wakati alipokutana na Viongozi NIDA na kukubaliana mpango wa pamoja wa utekelezaji wa zoezi hilo.

  0 0

  Uongozi wa Mkoa wa Rukwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen umeungana na ndugu wa majeruhi 9 na wafiwa wa vifo vya watu 15 vilivyotokea katika ajali ya lori aina ya fuso eneo la Ntembwa, Wilayani Nkasi.

  Katika kuhakikihsa tukio hilo halijirudii Mh. Zelote amepiga marufuku ukiukwaji wa sheria ya kupandisha abiria katika magari ya mizigo na kuonya kuwa yeyote atajayefanya hivyo achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.

  “Nimekataza binadamu kugeuzwa kuwa ni mifuko ya misumari, ni bora tubakie na wananchi wetu salama, watu wasipande kwenye malori, nimefikiria ni vyema tutumie zile chai maharage kuliko kupanda kwenye malori,” Alisisitiza.Mh. Zelote alifika katika eneo la tukio mara tu baada ya kupokea habari hiyo ili kuweza kusaidia na kuhakikisha maiti na majeruhi hao wanapatiwa huduma stahiki na kufanikisha zoezi la uokoaji.


  Ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 425 BFF kuacha njia na kupinduka ilitokana na mwendo kasi wa dereva uliochangiwa na ugeni wa barabara hiyo.

  Lori hiyo mali ya Bakari Ali Kessy iliyokuwa imetokea Kijiji cha Mvimwa kuelekea Kijiji cha Wampembe ilikuwa imepakiwa shehena ya viroba vya mahindi na watu iliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo vya watu 15 kati yao wanawake 10 na wanaume 05.

  Abate wa Pambu Martin Mkolwe Abasia ya Mvimwa akiongoza ibada fupi ya kuwaombea marehemu wa ajali iliyoua watu 15 na kujeruhi 9 iliyofanyika katika kituo cha afya Mvimwa, Wilayani Nkasi.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kaunda Suti ya ugoro) akitoa salamu zake za pole kwa wafiwa, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda na kuliani kwake ni Abate Pambu Mkolwe wa Abasia ya Mvimwa.
   
  Lori aina ya Fuso kama lionekanavyo mara baada ya kupata ajali


  Waliofariki katika ajali hiyo ni BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


older | 1 | .... | 1944 | 1945 | (Page 1946) | 1947 | 1948 | .... | 3285 | newer