Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2017: PSPF YATEMBELEA WATEJA MAJUMBANI, NIA NI KUWAJULIA HALI NA KUWAHAKIKI

$
0
0



NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

Wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja ikiendelea kote Duniani, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, umeitumia wiki hiyo sio tu kwa kuhudumia wateja ofisini bali pia kutoka nje ya ofisi na kuwatembelea Wanachama na Wastaafu wa Mfuko huo majumbani kwao.

Mmoja wa waiotembelewa ni Mstaafu Bw. Kassim Salehe Mafanya,(63), anayeishi Kipunguni B, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kitendo ambacho kilimfurahisha sana.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu, wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa akifuatana na timu yake, Oktoba 4, 2017 alifika nyumbani kwa Bw. Mafanya, na kufanya mazungumzo naye ikiwa ni pamoja na kumpatia fomu ili aijaze kwa nia ya kumuhakiki kama ambavyo sheria inataka.

Kwa mujibu wa Sheria, Mstaafu anatakia kufika kwenye ofisi za PSPF kuhakikiwa kila mwaka ili kujua uwepo wake, anasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa 

“Kama mnavyofahamu wiki hii ni wiki ya huduma kwa wateja Duniani kote, na sisi PSPF kupitia ofisi zetu nchi nzima tunajitoa na kutembelea wateja wetu ambao ni pamoja na wanachama na wastaafu, na leo tuko hapa eneo la Kipunguni B, tumekuja kumtembelea Bw. Kassim Salehe Mafanya, ambaye ni mstaafu na lengo ni kumjulia hali na kumuhakiki uwepo wake kama ambavyo sheria inataka.” Alisema.

Afisa Uendeshaji wa PSPF ambaye pia alifuatana na Bw. Mkangaa, alimsomea Mstaafu huyo, maelezo yaliyomo kwenye fomu ya uhakiki kabla hajaweka saini kenyefomu hiyo.Aidha kwa upande wake, Mstaafu huyo Bw. Mafanya aliishukuru PSPF kwa kitendo hicho cha kuwatembelea wateja wao yeye akiemo na kwamba ni kitendo kinachofaa kupongezwa.

“Siku ya leo nimefarijika sana, kwanza sikutegemea kama nigepokea ugeni kama huu kutoka PSPF wa kunitembelea mimi Mstaafu hapa nyumbani kwangu,” Alianza kwa kusema Bw. Mafanya wakati akiwakaribishas viongozi hao wa PSPF.“Kitendo cha kuwakumbuka wastaafu kama sisi na kuwatembelea majumbani kwao kimenifurahisha sana na niwapongeze kwa tabia hiyo, Alisema.

Bw. Mafanya alimuhakikishia Kaimu Mkurugenzi Mkuu, kuwa amekuwa akipokea pensheni yake kila mwezi na bila matatizo yoyote na amekuwa akipata ushirikiano mzuri kutoka kwa maafisa wa PSPF kila anapokwenda kufuatilia pensheni yake.

“Nashukuru pensheni yangu inaendelea vizuri, huu ni mwaka wa 14 tangu nistaafu, nachukua vizuri tu pensheni ya kila mwezi na uzuri nikwamba inaboreshwa, na ndio maana mpaka hivi sasa tunaonekana tuna afya nzuri na ninaendelea na shughuli zangu mimi na familia yangu.” Alipongeza.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa, (kushoto), na Mteja wa PSPF, ambaye ni Mstaafu, Bw. Kassim Salehe Mafanya, (63), wakifurahia jambo wakati kiongozi huyo wa alipomtembelea Mstaafu Mafanya nyumbani kwake Kitunda B, nje kidogo ya jiji Oktoba 4, 2017 wakati Dunia ikiadhimisha Wiki ya Huduma Kwa Wateja.
Bw. Mafanya, (kulia), akipokea fomu hiyo 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Andrew Mkangaa, (kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, wakishuhudia Bw. Mafanya akijaza fomu ya uhakiki ya Mstaafu, kutoka PSPF hapo nyumbani kwake. 


ZIJUE SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA SARATANI YA MATITI

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania

Saratani ya matiti ni miongoni mwa saratani inayomkumba zaidi mwanamke duniani na ndiyo inayoongoza kwa vifo vinavyotokana na saratani katika nchi zinazoendelea, ambapo watu takribani milioni 1.7 mwaka 2012 waligundulika kuwa na ugonjwa huo (kwa mujibu wa taarifa zilizopo hivi sasa). Viwango vya saratani duniani kwa ujumla vinatarajiwa kuongezeka kutoka milioni 14 mwaka 2012 na kufikia milioni 20 ndani ya miongo miwili ijayo, na kuifanya saratani kuwa ugonjwa unaotakiwa kuchukuliwa tahadhari zaidi.
Mwezi Oktoba wa kila mwaka dunia huwa imeutenga mahususi katika kukuza uhamasishaji wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya matiti duniani. Kampeni hizo huungwa mkono na serikali, taasisi na mashirika mbalimbali duniani kwa kuangazia umuhimu wa kuhamasisha juu ya saratani ya matiti, kutoa elimu na kufanya tafiti. Miongoni mwa shughuli zinazofanywa katika mwezi huu ni pamoja na kukuza hamasa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo na kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanyia tafiti toauti za ugonjwa huo.

Miongoni mwa mambo ya msingi unayotakiwa kuyafahamu kuhusu saratani ya matiti ni pamoja na: saratani ya matiti huwakumba zaidi wanawake; dalili zake ni pamoja na uvimbe au kuvimba kwa titi, na mabadiliko ya ngozi au chuchu; sababu zinazoweza kupelekea ni pamoja na kurithi, lakini mitindo ya maisha, kama vile unywaji wa pombe, unaweza kusababisha kutokea zaidi; aina mbalimbali za matibabu zinapatikana, zikiwemo upasuaji, tiba ya mionzi na kimotherapi; uvimbe unaotokea kwenye titi sio saratani, lakini mwanamke yeyote ili kuchukua tahadhari kuhusu uvimbe au mabadiliko yoyote inashauriwa kumuona daktari. 
Kwa kuwa mwezi huu umelenga kwenye kujenga hamasa juu ya ugonjwa wa saratani ya matiti duniani, Jumia Travelingependa kukufahamisha juu ya sababu hatarishi zifuatazo zinazoweza kupelekea ugonjwa huo. 

Umri. Hatari ya kuupata ugonjwa huu huongezeka kadri umri nao unavyoongezeka. Katika umri wa miaka 20, uwezekano wa kupata saratani ya matiti ndani ya muongo mmoja ujao huwa ni 0.6%. Lakini katika umri wa miaka 70, takwimu hiyo huongezeka mpaka kufikia 3.84%. Kesi nyingi za ugonjwa wa saratani zimegundulika baada ya umri wa miaka 50.

Kurithi. Endapo ndugu wa karibu anaugua au aliwahi kuugua, saratani ya matiti, hatari ya kuupata ni kubwa zaidi. Wanawake ambao wanabeba jeni aina ya BRCA1 na BRCA2 wanayo hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti, saratani ya ovari au zote kwa pamoja. Jeni hizi zinaweza kurithiwa. TP53 ni jeni nyingine ambayo inahusishwa zaidi na hatari ya kusababisha saratani ya matiti. 

Historia ya kuugua saratani ya matiti kipindi cha nyuma. Wanawake waliowahi kuugua saratani ya matiti kipindi cha nyuma wanao uwezekano wa kuugua tena, ukilinganisha na wale ambao hawana historia na ugonjwa huo.

MSD YAWATAKA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUPELEKA MAHITAJI YA VIFA TIBA NA DAWA MAPEMA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Bohari ya Dawa nchini imewataka Wakurugenzi wa Halmashauri na Wenyeviti kuwasilisha mahitaji ya dawa na vifaa tiba vya Hospitali zao kabla ya tarehe 31 mwezi Januari kila mwaka,ili kuwasaidia kuharakisha hatua za manunuzi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja na Shughuli za Kanda MSD Daud Msasi alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa globu ya Jamii wakati kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (ALAT.

Msasi amesema kuwa Halmashauri zinapaswa kupeleka mahitaji halisi kulingana na bajeti walizonazo kwani kufanya hivyo itasaidia katika kupanga manunuzi ya vitu vinavyohitajika.

“Mahitaji yanatakiwa kuwahi kabla ya tarehe 31 mwezi wa kwanza. hii itasaidia sisi kwenda sokoni kwa wazalishaji na Viwandani hili kuweza kupata dawa kwa haraka” amesema Msasi.

Ameongeza mara baada ya tamko la Rais Dk John Magufuli kuagiza dawa zote ziagizwe na Bohari ya Dawa kwa sasa wameweza kupata dawa kwa bei raisin a zenye ubora unahohitajika.

Amesema kuwa licha ya MSD kuwa na mafanikio makubwa katika usambazaji wa dawa katika Halmashauri na Hospitali za mikoa pia mpango huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuepukana na ubabaishaji uliokuwa ukiletwa na watu wa kati.

Amemaliza kwa kutoa wito kwa Halmashauri zote nchini kusimamia vizuri vyanzo vyao vya mapato vinavyohusu huduma za afya hili waweze kulipa madeni yao kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za kanda -MSD ,Daudi Msasi akimuonesha mmoja wa Wateja vifaa tiba wakati wa Maonesho ya mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (ALAT)
Afisa Huduma kwa wateja MSD kanda ya Dar es Salaam Florida Siang'a akimuonesha bidha mmoja wa wateja waliotembelea banda lao katika Maonesho ya mkutano wa 33 wa Alat
Wafanyakazi wa Bohari ya dawa ya MSD wakito huduma kwa wageni waliofika katika mkutano wa 33 wa ALAT

RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WAPYA WA TANZANIA NCHINI MISRI NA ZAMBIA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Issa Suleim Nassor kuwa balozi wa Tanzania nchini Misri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Abdulrahman Kaniki Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017 Abdulrhaman Kaniki kuwa balozi wa Tanzania nchini Misri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli balozi mpya wa Tanzania nchini Misri Mhe. Issa suleiman Nassor na Mhe. Abdulrahman Kaniki balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia wakila viapo vya maadili ya viongozi baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
Balozi mpya wa Tanzania nchini Misri Mhe. Issa suleiman Nassor akiongea machache baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017
Blozi mpya wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Abdulrahman Kaniki machache baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA BUNGE LA NCHI ZA KIARABU

$
0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Bunge la Nchi za Kiarabu, Dkt. Feda Yehia Ahmed Alhmoud alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini odoma.
Mjumbe Maalum wa Rais wa Bunge la Nchi za Kiarabu, Dkt. Feda Yehia Ahmed Alhmoud akijadiliana jambo na Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akipokea barua ya ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Bunge lma Nchi za Kiarabu, anayekabibidhi barua hiyo ni Mjumbe Maalum wa Rais huyo, Dkt. Feda Yehia Ahmed Alhmoud wakati alipomtembelea leo Ofisin kwake Mjini Dodoma.
Mjumbe Maalum wa Rais wa Bunge la Nchi za Kiarabu, Dkt. Feda Yehia Ahmed Alhmoud akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai walipokutana na kufanya mazungumzo leo Ofisini kwake Mjini Dodoma

PSPF INAWATAKIA HERI YA SIKU YA WAALIMU DUNIANI

MSHINDI WA TISA WA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA APATIKANA TUNDURU

$
0
0
Mshindi wa droo ya tisa ya Tatu Mzuka amepatikana Jumapili hii ya Oktoba 1, 2017. Mshindi huyu amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 60 na ni Bwana Fulko Hyera, mkazi wa kiuma, wilayani Tunduru 

Ushindi huu wa Bw.Hyera unaonesha namna Tatu Mzuka inavyobadili maisha ya wananchi wa Tanzania sio tu wa mjini bali na vijijini pia. Bw. Hyera ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari ya Kiuma.

Bw Hyera alisema “Katika muda wangu wote, sikuwaza kuwa na hela hizi. Kama familia zetu nina majukumu mengi yakutimiza na sasa nitakuwa na uwezo wa kusaidia familia. Sasa nimeamua kuanza biashara, niajiri wengine na kuongeza fursa za vijana” 

Kumkabidhi cheki Bw Hyera, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Juma Homera alimkabidhi cheki mshindi kwenye tulio lilio andaliwa na Tatu Zuka kijijini Kiuma, Tunduru.

Mheshimiwa Homera alikuwa ana machache ya kusema licha la kumpongeza Bw. Hyera alimuhusia “ Hizi ni hela nyingi sana. Lazima uwe na malengo kamili and pia hii itakupa fursa nyingine ya kusaidia jamii.” Amewapongeza sana Tatu Mzuka kwa kuchangia kubadili maisha ya watu tena ya mwana Tunduru.

 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh Juma Homera (Kushoto) akiwa na MWakilishi wa Tatu Mzuka  Bi Kemi Mutahaba, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kiuma Bw. Joseph Mtuma  Wakimpongeza Mshindi wa 9 wa Tatu Mzuka Jackpot Bw Fulko Hyera, kijijini Kiuma, Tunduru
 Bw. Fulko Hyera  and Mke wake Sigsberta Haule mbele ya duka lao kijijini Kiuma wakisherekea kipato cha Million 60 kutoka Tatu Mzuka.

Tatu Mzuka walizawadia marafiki wa TATU wa Bw. Fulko Hyera  million 1 moja kutokana na promociona ya Tatu Mzuka ya "Cheza na Washkaji na Shinda na Washkaji".  Robert Mbai na Owne Simwanga

JAFO AZIAGIZA HALMASHAURI KUZUIA UVUJAJI MAPATO

$
0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amefanya ziara leo ya kukagua utekeleza wa maagizo ya serikali aliyoyatoa hivi karibuni katika Kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.

Pamoja na maagizo mengine, Jafo aliagiza kuhakikisha kituo hicho kinafunga mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato.

Akiwa katika ziara yake leo, Jafo amepongeza ufungaji wa mfumo huo huku akiwataka kuhakikisha wanaziba mianya ya upotevu wa mapato kwa kuwa hali ya ukusanyaji bado hairidhishi.

Amesema kwa mujibu wa taarifa aliyoipata kituo hicho kabla ya mfumo kilikuwa kikikusanya Sh.Milioni nne lakini kwasasa kinakusanya hadi Sh.Milioni 9.9 kwa mwezi jambo ambalo linaonesha bado kuna mianya ya upotevu wa mapato.

“Nawapongeza kwa kutekeleza maagizo ya serikali kwa kufunga huu mfumo lakini sijaridhishwa na ukusanyaji mapato wa kiwango hichi, kuna vituo vinakusanya hadi Sh.Milioni 24 nyie mnakusanya hivi bado haitoshi hakikisheni mnaziba mianya,”amesema Jafo
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisisitiza jambo alipokuwa akikagua mfumo wa kielektroniki katika Kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.
Wagonjwa wakiwa katika dirisha la malipo kwenye kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisalimia wagonjwa alipokuwa akikagua kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.



Tumieni Wataalam wa Utafiti katika Ujenzi-NHBRA

$
0
0

Na. Paschal Dotto- MAELEZO.

Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) imewashauri wananchi kufuata maelekezo katika ujenzi wa nyumba za makazi na majengo mbalimbali ili kupata nyumba bora.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mhandisi Benedict Chila alisema kuwa kuna uhitaji mkubwa sana wa utafiti kwa nyumba za makazi kuhusu matumizi bora ya vifaa vya ujenzi kama matofali, kokoto pomoja na mchanga uliobora katika ujenzi.

“kuna uhitaji mkubwa wa tafiti ambazo zitawawezesha watanzania kupata makazi bora yenye kudumu, kwani katika vifaa na huduma zinazopatikana kwetu zinajikita zaidi katika usanifu majengo pamoja na matumizi ya vifaa, kwa hiyo tafiti hizi ni muhimu kwa wananchi wenye mahitaji ya makazi bora”,.alisema Mhandisi Chila.

Aidha Mhandisi Chila alisema kuwa katika kutambua uhitaji wa wananchi NHBRA imetoa mlango kwa jamiii kupata huduma bora kwa kufanya tafiti katika sanifu ya majengo na vifaa vya kutumia katika ujenzi ili kupata makazi bora.
Mmoja wa wafanyakazi katika Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) akitengeneza vigae vya kuezekea nyumba vilivyofanyiwa utafiti Jijini Dar es Salaam tayari kwa matumizi ya ujenzi wa nyumba.
Ukuta unaofanyiwa utafiti kwa ujenzi wa kutumia tofali mbichi kwa majengo makubwa na nyumba za makazi ulioko katika karakana ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Jijini Dar es Salaam.
Mhandishi na fundi sanifu wa majengo Bw.Hussein Mataka akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu mashine ya kufyatua tofali iliyoko katika karakana la ofisi hizo Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa ofisi za Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) Bw. Benedict Chilla akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma zinazotolewa na ofisi hiyo mapema wiki hii Jiji Dar es Salaam.
Mashine ya kupima ubora na kiwango cha udongo kwa ujenzi wa nyumba ambayo ni moja ya vifaa bora vinavyopatikana Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) kama inavyoonekana kwenye picha.Picha na Paschal Dotto-MAELEZO

Wataalam wa Udhibiti Ubora wa Dawa Afrika Mashariki Wakutana Jijini Dar

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza alipokuwa akifungua kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ambayepia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Udhibiti Dawa Afrika Mashariki Hiiti Sillo akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wataalam toka taasisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati) akifuatilia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Dkt. Hiiti Sillo (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mdhibiti wa Dawa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wizara ya Afya nchini Rwanda Alex Gisagara na Kamishna wa Huduma za Famasi toka Uganda Seru Morries.
Afisa Msajili wa Dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Dk. Shani Maboko akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha wataalam toka Taasisi za Udhibiti wa Dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Frank Shija – MAELEZO

MBUNGE CHUMI AZIPIGA TAFU TIMU ZA JIMBONI KWAKE KWA KUZIPA VIFAA VYA MICHEZO NA FEDHA

$
0
0

Na fredy Mgunda, Mafinga

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amezipiga tafu timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Iringa kwa kuzipatia jozi moja moja ya jezi kwa kila timu lakini pia ameichangia timu ya Mufindi United inayoshiriki lingi daraja la kwanza Tanzania bara kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuisaidia katika harakati zake za kupanda daraja.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa na pesa hizo Chumi alisema kuwa ameguswa kufanya hivyo kwa kuwa anapenda michezo na anacheza mpira wa miguu kufanya hivyo kutaendelea kuzipa morali timu za jimbo la Mafinga Mji kufanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki.

"Leo nimekabidhi jezi kwa timu zinazoshiriki daraja la tatu ngazi ya mkoa na timu hizo ni Bajaji Fc,Mabo Fc (Boda Boda) na Kinyanambo United nimefanya hivyo kuzifanya timu hizi kuzihamasisha kufanya vizuri kwenye ligi hiyo" alisema Chumi
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akitoa maelezo wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano.
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na viongozi wa timu ya Mafinga veterani wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano .




HISA ZA MAENDELEO BANK ZAFANYA VIZURI SOKONI TANGU ZIZINDULIWE NA WAZIRI WA FEDHA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akizungumza na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Hisa za Maendeleo Bank zimeendelea kufanya vizuri sokoni tangu kuzinduliwa kwa mauzo ya hisa hizo rasmi Septemba 18, tukio ambalo lilifanywa na Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango.

Watanzania wengi wameonekana wakiitikia wito wa kuwekeza katika soko la mitaji kwa kufika katika matawi ya Maendeleo Bank ya Luther House, Mwenge na Karikakoo, matawi yote ya CRDB nchini, Uchumi Commercial Bank na Mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) walioidhinishwa kuuza hisa.

Akizungumzia maendeleo ya ununuzi wa hisa hizi, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba alisema “Tumeingia wiki ya tatu sasa katika zoezi letu la uuzaji wa hisa, tumeona watanzania wengi wakijitokeza na kwa kweli sisi kama benki tuna matumaini makubwa ya kufikia lengo ambalo tumekusudia”.Pia tunaendelea kuisaidia Serikali katika kutoa elimu ya uwekezaji katika masoko ya mitaji na faida zake kwa watanzania na nchi kwa ujumla. Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dk. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uuzaji hisa za Maendeleo Bank PLC. Pamoja nae kutoka kushoto ni Askofu Ambele Mwaipopo, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Askofu Dk. Alex Malasusa, Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank Bw. Amulike Ngeliama.

Mwitikio wa watanzania katika kununua hisa, kujitokeza kuuliza maswali ili kuelewa zaidi juu ya mambo haya ni suala la kujivunia kwetu kwani tunafanya mambo makubwa mawili kwa wakati mmoja, moja ni kuuza hisa lakini la pili ni kusaidia juhudi za Serikali juu ya kutoa elimu ya namna gani watanzania wanaweza kuwekeza katika hisa” aliongeza Mwangalaba.

Uwekezaji katika hisa ni mfumo wa uwekezaji unaomuwezesha muwekezaji nafasi ya kumiliki kampuni na kupata gawiwo pale kampuni inapopata faida. Pia hisa ni njia ya ukuzaji wa thamani ya fedha yako pale hisa zinapopanda.Pia hisa zinaweza kutumika kama dhamana ya kujichukulia mkopo katika benki.

Mkurugenzi huyo amewasihi watanzania wengi zaidi kuchangamkia hisa za Maendeleo Bank ili waweze kuwa sehemu ya uchumi wao kwa kumiliki sehemu ya benki hiyo. Hisa za Maendeleo Bank zinaendelea kuuzwa hadi Novemba 3, 2017.

WANAFUNZI WA KIKE MSISHAWISHIKE SOMENI KWA BIDII-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule mbalimbali nchini kusoma kwa bidii na wasikubali kushawishika.

Pia Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka sheria kali kwa wote watakaobainika kukatisha masomo ya watoto wa kike kwa kuwapa ujauzito au kuwaozesha.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Oktoba 04, 2017) wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana na WAMA Sharaf.

Shule ambayo ipo wilayani Lindi inamilikiwa na Taasisi ya WAMA ambapo inasomesha watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira magumu.Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wa kike kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii na hatimaye watimize malengo yao.

Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia vizuri fursa hiyo ya elimu wanayoipata shuleni hapo kwa kusoma kwa bidii na wafuate ratiba itakayokuwa inapangwa.“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikubali kushawishika na kukatisha masomo yenu.”

Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mbunge wa Kuteuliwa alisema shule hiyo inasomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka mikoa yote nchini.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
ALHAMISI, OKTOBA 05, 2017.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na wanafunzi Kike wanaosoma WAMA_SHARIF Sekondari .iliyopo Mkoani Lindi .Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kkikwete (MB) Waziri Mkuu ametembelea shule hiyo jana Oktoba 4,2017 alipokuwa katika ziara ya siku moja katika Mkoa wa Lindi jana
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  ahamasisha utunzaji wa mazingira Nchini kwakupanda Mti jana  Oktoba 4/2017 katika Shule ya WAMA_ SHARIF SEKONDARI.iliyopo Mkoani Lindi ,kushoto mwenye fimbo ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Daktari Hamisi Kigwangala na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)  Mama Salma Kikwete (MB) Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku moja jana Mkoani Lindi .PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

JARIDA LA NCHI YETU MWEZI SEPTEMBA

UNESCO, ILO, UNICEF, UNDP NA EDUCATION INTERNATIONAL YATOA SALAMU KWA WALIMU DUNIANI

$
0
0
Kufundisha Kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu Walimu ni msingi mkuu katika ustawi wa muda mrefu wa kila jamii kwa kuwa hujishughulisha kuwapatia watoto, vijana na watu wazima elimu na ujuzi wanaohitaji ili kufikia uwezo wao. 

Lakini duniani kote, walimu wengi sana hawana uhuru na msaada wanaohitaji kufanya kazi yao iliyo muhimu sana. Ndiyo maana maudhui ya Siku ya Walimu Duniani kwa mwaka huu – ‘'Kufundisha kwa Uhuru, Kuwawezesha Walimu'’ - inathibitisha thamani ya walimu waliowezeshwa na kutambua changamoto ambazo wengi hukabiliana nazo katika maisha yao ya kitaaluma ulimwenguni kote. 

Kuwa mwalimu aliyewezeshwa ina maana ya kuwa na uwezo wa kupata mafunzo yenye ubora, malipo ya haki, na fursa zisizo na mwisho za kujiendeleza kitaaluma. Pia inamaanisha kuwa na uhuru wa kuunga mkono maendeleo ya mitaala kitaifa – na uhuru wa kitaaluma wa kuchagua njia sahihi na mbinu zinazofaa zaidi kuwezesha utoaji wa elimu yenye ufanisi, jumuishi na ya usawa. Zaidi ya hayo, inamaanisha kuwa na uwezo wa kufundisha kwa usalama wakati wa mabadiliko ya kisiasa, machafuko, na migogoro. 

Lakini katika nchi nyingi, uhuru wa kitaaluma na uhuru wa mwalimu viko chini ya shinikizo. Kwa mfano, katika ngazi za shule za msingi na za sekondari katika baadhi ya nchi, mipango ya uwajibikaji imeweka shinikizo kubwa kwa shule kutoa matokeo kwa vipimo vilivyowekwa, na kupuuza haja ya kuhakikisha mtaala wa msingi unaofaa mahitaji tofauti tofauti ya wanafunzi. 


Serikali yadhamiria kufanikisha utafutaji na upatikanaji wa mafuta katika bonde la Eyasi Wembere na ziwa Tanganyika

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kufanikisha utafutaji na upatikanaji wa mafuta yaliyopo katika bonde la Eyasi Wembere na ziwa  Tanganyika hapa nchini ili Tanzania ianze kunufaika na rasilimali hiyo.

Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo muda mfupi baada kupokea taarifa ya maendeleo ya utafiti wa mafuta katika maeneo ya bonde la ufa ya Eyasi Wembere na ziwa Tanganyika, iliyowasilishwa na timu ya wataalamu wa Tanzania na Uganda.

Timu hiyo imeelezea uwepo wa viashiria vya uhakika vya kijiolojia vinavyothibitisha kuwepo kwa mafuta katika maeneo ya Senkenke, Mwanzugi na Kining’inila katika bonde la Manonga, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani na Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Richard Kabonero, timu ya wataalamu hao imesema miamba, uoto na uwepo wa bonde Eyasi Wembere katika mfumo mmoja wa bonde la Afrika Mashariki unaofanana na maeneo mengine yaliyothibitika kuwa na mafuta ni kiashiria muhimu cha kuwepo mafuta.

Kufuatia taarifa hiyo Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo tayari kutekeleza shughuli zote zitakazowezesha kupatikana kwa mafuta katika bonde la Eyasi Wembere na ziwa Tanganyika na amewaagiza wataalamu wa Tanzania kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wataalamu wa Uganda ambao wana uzoefu wa kupata mafuta katika ziwa Albert nchini humo.


Mhe. Rais Magufuli amewashukuru wataalamu wa Uganda wanaoshirikiana na wataalamu wa Tanzania katika kazi hii na amemuomba Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa Uganda Bw. Robert Kasande kumfikishia shukrani zake kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa ushirikiano anautoa kwa Tanzania katika kufanikisha upatikanaji wa mafuta ya nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Naibu Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika kikao na ujumbe wa wataalamu wa Sekta ya Nishati toka nchini Uganda na Tanzania waliompatia  taarifa ya maendeleo ya utafiti wa mafuta katika bonde la bonde la ufa ya Eyasi Wembere la Ziwa Tanganyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 5, 2017. Picha na IKULU

JUKWAA LA WANAWAKE WAJASILIAMALI TEMEKE LAUNDWA.

$
0
0
 Katibu tawala wa Manispaa ya Temeke (DAS), Hashim Komba akizungumza na wanawake wajasiriamali wa wilaya hii katika jukwaa la wanawake jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya watumishi na wanawake wajasiriamali wakisikiliza maada.

KATIBU Tawala Wilaya ya Temeke Bw:Hashimu Komba aunda jukwaa la wanawake wajasiliamali wa wilaya ya Temeke ambao walijitokeza kwa wingi kutoka kata zote za wilaya hiyo. Akiongea na wanawake hao wajasiliamali leo katika ukumbi wa Iddi Nyundo Manispaa ya Temeke. 


Kauli mbiu ya kikao hicho ni “Mwanamke tumia fursa kuimalisha uchumi wa viwanda” ambapo Katibu tawala huyo ameungana na juhudi za Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ikiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa jukwaa la wanawake katika kuinua uchumi wa mwanamke ili kuleta Maendeleo ya taifa kiwilaya.

 Kauli mbiu hiyo ilisemwa na Makamu wa Rais katika siku ya uzinduzi wa Jukwaa la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kimkoa lililofanyika katika viwanja vya Posta,kijtonyama. Ambapo uzinduzi huo ni wa 23,lililoandaliwa na Baraza la uwezeshaji kwa ufadhili wa benki ya CRDB.

Komba amewamwagia sifa wanawake kwa juhudi zao za kujikwamua kiuchumi katika jamii,aliwapongeza akina mama kwanamna wanavyojituma na kuwa waaminifu na kuwa na uwezo wa kusimamia vipato vyao vidogo wanavyopata kwa kujileta maendeleo makubwa. 

Ahadi kuwa jukwaa hilo punde litakopo undwa litakuwa na tija kubwa katika kujitangazia biashara na ubunifu wa kazi zao wanazofanya katika ngazi za kimataifa,kitaifa,kimkoa,kiwilaya mpaka kata. Pia watapata fursa mbalimbali za kupiga hatua kama kushiriki maonesho ya kibiashara ya sabasaba na nanenane. 

Hivyo asisitiza kuchaguliwa kwa viongozi walio na uwezo wakusimamia mawazo,ubunifu na ujuzi wa kazi zao ili kusimamia jukwaa hilo katika kujiletea maendeleo.

Hata hivyo amewapa moyo kuwa kuelekea katika sera ya uchumi wa viwanda kwa kuanzia waendelea kutumia technolojia hizo hizo ndogondogo wanazotumia nyumbani kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni mfano wa viwanda vidogovidogo,wakati wanajiandaa kupata viwanda vikubwa. Kwakufanya hivyo watakuwa wanajiingizia kipato,pia kuinua uchumi wa viwanda katika nchi yetu.

Katika kikao hicho katibu Tawala huyo alipongeza Idara  ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii inayoongozwa na John Bwana kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwatambua wajasiliamali hao ambao wamejitokeza kwa wingi na shauku kubwa kuunda jukwaa hilo.

Jukwaa hilo linatazamiwa kuzinduliwa hivi karibuni ikiwa lengo kuu ni kumwinua mwanamke kufikia katika uchumi wa kati, ambapo inasemekana mwanamke ni mlezi wa familia na jamii, ukimwezesha mwanamke imeliwezesha taifa.

IGP SIRRO AZUNGUMZA NA WANANCHI WA RUVUMA NA KUWATAKA KUENDELEA KUTII SHERIA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa eneo la Lizaboni wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo na kutii sheria za nchi pamoja na kuwafichua wahalifu waliopo kwenye jamii, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa eneo la Lizaboni wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo na kutii sheria za nchi pamoja na kuwafichua wahalifu waliopo kwenye jamii, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja. 
 Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu na wahalifu katika mkoa wa Ruvuma, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, na kuwataka kufanyakazi kwa kuzingatia sheria na taratibu pamoja na kutimiza wajibu wao wa kutenda haki wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (watatu kulia kwenye meza kuu) na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Binilith Mahenge,  wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na Maofisa na askari na kuona changamoto zao ikiwa pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki na kutoa huduma bora kwa wananchi
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (watatu kulia kwenye meza kuu) na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Binilith Mahenge,  wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzungumza na Maofisa na askari na kuona changamoto zao ikiwa pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki na kutoa huduma bora kwa wananchi

BENKI YA DCB WASHEHEREKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUWAHAMASISHA WATEJA KUTUMIA DCB PESA POPOTE.

$
0
0

Wafanyakazi wa tawi la benki ya DCB Magomeni wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo waliohudhuria kusherehekea maadhimisho ya wiki huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam leo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya DCB imesherehea wiki ya huduma kwa wateja kwa kufurahi pamoja na wateja wa benki hiyo huku wakiendelea kuwahamisha kutumia huduma ya DCB Pesa popote nchini.

Katika maadhimisho ya wiki kwa huduma kwa wateja, Afisa Mikopo wa DCB tawi la Magomeni Miriam Migetto amesema kuwa wanayofuraha ya kujumuika pamoja na wateja wa benki hiyo kusherehekea siku hii muhimu kwao pia na kuwasisitiza kuendelea kutumia huduma za kibenki.

Miriam amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuboresha huduma za kibenki ikiwemo kutumia huduma ya DCB Pesa na DCB Jirani ikiwa ni katika kurahisisha huduma za kipesa kwa wateja wa DCB.

Afisa Mikopo wa DCB tawi la Magomeni Miriam Migetto akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ma kuwataka kuendelea kutumia huduma za kibenki kwa njia ya simu pamoja na kuendelea kuchukua mikopo ya riba nafuu.

Moja ya wateja wa muda mrefu wa benki hiyo, Mama Fatma  Simba amesema kuwa ameanza kutumia benki hiyo tangu mwaka 2005 na amekuwa akipata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi bila usumbufu na hata pia ameweza kupata mkopo wa bei nafuu na riba nafuu.

"Nimekuwa natumia DCB benki kwa zaidi ya miaka 12 na imeweza kunipatia mahitaji yangu kwa wakati ikiwemo mkopo wa bei nafuu na riba nafuu na hata katika utoaji wa huduma za kibenki kupitia DCB Pesa wameweza kutupunguzia wateja wao kwenda benki mara kwa mara, " amesema mama Fatma.

DCB benki wamesherehea wiki ya huduma kwa wateja katika matawi tofauti na kufurahi pamoja na wateja wao na kuahidi kuzidi kuboresha na  kuwapatia huduma wanazostahili na wakati sahihi.
Moja ya wateja wa mda mrefu wa benki ya DCB Mama Fatma Simba akielezea namna benki hiyo ilivyweza kumsaidia katika shughuli zake za ujasiriamali mpaka alipofikia sasa na kuwataka wanawake waache tamaa pindi wanapochukua mikopo na kusifia pia huduma za DCB Pesa katika urahisishaji wa huduma za kipeki kupitia simu ya mkononi.

Baadhi wa wafanyakazi wa Benki ya DCB Tawi la Mabibo External wakiwa katika picha ya pamoja  katika kuazimisha wiki ya huduma kwa wateja.

BENKI YA AZANIA YAENDELEA NA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTEMBELEA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.
Benki ya Azania leo imeendelea na Maadhimisho ya  Wiki ya huduma kwa Wateja kutembelea Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) ambapo imekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James Kilaba.

Akizungumza ofisini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe amesema kuwa wameitembelea TCRA kutokana na kuwa Wateja wao wakubwa wanaowathamini.

Itembe amesema kuwa wanaendelea kutembelea Wateja wao Bega kwa Bega ili kuwahudumia vizuri, pia kusikiliza maoni yao juu ya huduma zinazotolewa na Benki hiyo zikiwemo changamoto pamoja na ushauri.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba ameshukuru kutembelewa na Benki ya Azania, ambapo amesema kuwa wamefurahi kutokana na kuwa Wateja wa Benki hiyo. Mhandisi Kilaba amesema kuwa wao kama TCRA hawajakosa pa kwenda isipokuwa huduma zilizopo kwenye benki hiyo zinawafaa. Pia ameiomba Benki ya Azania kuwekeza kwenye viwanda ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli.

Pia amesema Watumishi wa Malamka hiyo hawajapata vikwazo kupata huduma kama Taasisi katika Tawi hilo lililopo Mawasiliano.

Hata hivyo, Mhandisi Kilaba ameishauri Benki hiyo kuwa na ubunifu zaidi katika sehemu nyingi, kuboresha mambo kama ya Mobile Bank ili kuwafikia wateja wengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akimshukuru mkurugenzi kwa niaba ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuwa wateja wao wa muda mrefu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuwa wateja wa benki hiyo ili kupunguza adha kwa wafanyakazi hao. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba.



 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba(wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(Wa pili kulia), Meneja wa Tawi la Benki la Azania la Mawasiliano, Valentina Chamasa, Meneja Mkuu wa Benki ya Azania, Nyansaho Rhimo( wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Alinanuswe Kabungo(wa tatu kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati(kushoto).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Mitayakingi Kilaba akizungumza kuhusu namna benki ya Azania inavyoweza kujikita kusaidia kukuza viwanda hasa vidogo vidogo na vikubwa ili kuendana na kazi ya Rais Magufili kufikia kwenye malengo waliyojiwekea kama taifa pamoja na kuwashauri kupanua huduma hasa kupitia njia ya simu ili kuwafikia wateja wengi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images