Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1943 | 1944 | (Page 1945) | 1946 | 1947 | .... | 3272 | newer

  0 0

  HAKIMU mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomasi Simba amekwama kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya kwa sababu bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo. 

  Uamuzi huo ulitarajiwa utolewe leo lakini Hakimu Simba amesema bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo ambapo na ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi mwaka huu (2017).

  Mapema Wakili wa Wema, Peter Kibatala aliiomba mahakama isipokee hati hiyo kwa kuwa haikukidhi vigezo.

  Wema anashtakiwa pamoja na wafanyakazi wake wawili,  Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambapo wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

  0 0

  Ofisa elimu msingi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, Doroth Mwandila akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium Vannesa Nada, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (kushoto)  ni Mkurugenzi wa shule hiyo mhandisi Nada Narya.
  Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, wakionyesha mchezo wa kareti wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni kwao.

  ILI kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajili nchini, wanafunzi wametakiwa kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu ambayo yatawajengea uwezo wa kupata ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda. 

  Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, mhandisi Nada Narya aliyasema hayo kwenye mahafali ya pili ya darasa la saba na ya nane ya kumalizika elimu ya awali ya shule hiyo. 

  Mhandisi Narya alisema shule hiyo imewaanda ipasavyo wanafunzi wa shule hiyo kupenda masomo ya sayansi na hesabu ili kukabiliana na tatizo la ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hivyo wanafunzi wengine nchini wapende masomo hayo. 

  Alisema hivi sasa soko la ajira ni dogo na ili kuondokana na hali hiyo inawapasa wanafunzi kuyapenda masomo sayansi na hesabu kwa lengo la kujiandaa kwa nguvu zote katika kuhakikisha wanajipanga ipasavyo hivi sasa ili baadae wachangamkia fursa ya ajili kupitia Tanzania ya viwanda. 

  "Sisi kama Deira tumeanza kuwaandaa wanafunzi wetu wapende masomo ya sayansi na hesabu ili baadaye waweze kuendesha maisha yao kwenye soko la ajira kwani wataalamu mbalimbali watatokea hapa shuleni kwetu," alisema mhandisi Narya. 

  Mgeni rasmi wa mahafali hayo, ofisa elimu ya msingi wa halmashauri ya mji wa Babati, Doroth Mwandila alimpongeza mwanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo, Edson Elias kwa kuongoza kwenye mtihani wa moku katika shule 37 za sekondari za halmashauri ya mji huo. 

  Mwandila alisema ili kumuandaa kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza mwakani, anampa mwanafunzi huyo zawadi ya sh20,000 na atamnunulia vitabu, madaftari na kalamu pindi akianza masomo yake kwa lengo la kumpa motisha ya kusoma kwa bidii zaidi. 

  Aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba kwa mwaka huu, kuwafuatilia watoto wao ipasavyo kwenye mienendo yao ya kila siku wakiwa majumbani ili kuhakikisha wanawaanda vizuri kwa ajili ya kuanza elimu ya sekondari mwakani. 

  Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Daniel Gaitu alisema shule hiyo ilianzishwa rasmi Januari 2010 ikiwa na watoto watano, wavulana wawili na wasichana watatu na hivi sasa ina wanafunzi 253 kati yao wavulana 119 na wasichana 134. 

  Gaitu alisema kwa upande wa taaluma, shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani kwani wanafunzi wa darasa la nne walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye halmashauri ya mji huo katika mtihani wa Taifa wa mwaka 2013, 2014 na nafasi ya pili mwaka 2016. 

  Alisema wanafunzi wa darasa la saba wa mwaka jana walishika nafasi ya kwanza kwa mtihani wa Taifa kwenye halmashauri ya mji huo na darasa la saba wa mwaka huu wameshika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa moku mkoa wa Manyara kwenye shule 37 za halmashauri ya mji wa Babati. 

  0 0

  Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu'  wakitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kesi  inayowakabili ya utakatishaji fedha na kugushi kuahirishwa hadi Oktoba 11,2017 kwaajili ya upelelezi kutokukamilika. 

  Evans Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha Dola za kimarekani 300,000.

  0 0

  Na Mwandishi wetu
  Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa nchini.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua wakati wa kufanya tathimini ya mashindano hayo na mashindano ya urembo kwa ujumla.

  Mrembo Jihan Dimachk alishinda taji la Miss Universe mwaka jana  huku Lilian Loth akishinda nafasi ya pili katika mashindano hayo.

  Shalua alisema Basata wamefarijika sana na jinsi mashindano hayo yanavyoendeshwa na hakuna malalamiko yoyote kuhusiana na zawadi na upendeleo.

  Alisema kuwa kutokana na utaratibu mzuri wa mashindano yao, Basata imeridhia waandaaji wa mashindano hayo, kufanya mashindano ya mwaka huu na vile vile kuandaa mashindano ya kutimiza miaka 10 tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2007.

  “Pamoja na kuwa na shindano moja kwa kushirikisha warembo wa mikoa tofauti, bado Basata imefarijika na jinsi mnavyoendesha na utaratibu unaotumia kuwapata warembo, uendeshaji wa mashindano mpaka kumpata mshindi,” 

  “Tunajua kuwa kuna changamoto za wadhamini na kusababisha kufanya mashindano yenye kalenda fupi na kuondoa mlolongo wa matukio, hatua hii ni bora zaidi ili kuondoa malalamiko ya zawadi na mambo mengine, huu ni mfano wa kuigwa,” alisema Shalua.

  Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajihidi kuongeza wigo ili kuona warembo wengi zaidi kutoka mikoa tofauti wanashiriki katika mashindano yao.

  Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini na kufikia malengo yao katika kuendeleza Sanaa hapa nchini.

  “Kwa sasa kuna changamoto kubwa ya wadhamini wa mashindano, kuna haja ya kupata msaada kutoka Basata ambao ni chombo cha serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini kupitia kwenu, tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na mamlaka ya zake kama Tanapa,” alisema Maria.
   Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).Anayesikiliza Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua na Afisa Sanaa, Bona Leon Masenge.
   Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Univerese mwaka jana, Jihan Dimachk (Kulia) na Miss Earth Tanzania, Lilian Loth.
  Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na warembo, waandaaji na maofisa wa Basata mara baada ya kumalizika kikao cha pamoja cha kujadili mashindano hayo.

  0 0

  Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela,Emmanuel Kishosha akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira wakati akimkaribisha kuzungumza na Wateja a Benki hiyo waliojumuika katika Chai ya asubuhi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza na Wateja wa Benki ya NMB wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba Mosi.
  Baadhi ya Wateja wa Benki ya NMB pamoja na viongozi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliotoa wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja katika Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na Wateja wa Benki hiyo na viongozi mbalmbal waliohudhuria kuanza kwa wiki ya Huduma kwa Wateja.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi (katikati),akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo
   Kikosi kazi cha timu ya mauzo ya Nyanza Bottlers katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mchongo chini ya kizibo.
  Msafara wa magari ya kampuni ya Nyanza Bottlers yakipita mitaani katika mji wa Mwanza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.

  Kampuni ya Coca-Cola, imezindua kampeni kubwa ya wiki 10 kwa wateja wake inayojulikana kama ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ ambayo itawawezesha wateja wake wa mikoa ya kanda ya ziwa na jirani kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure. 

   Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi, alisema lengo la promosheni hii ni kuleta msisimko zaidi kwa wateja wanywaji wa soda zote zinazozalishwa na kampuni ya Coca-Cola waliopo mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, na mikoa mingine jirani ya kanda ya ziwa.

   “Kampuni yetu ya Coca-Cola katika kutoa shukrani kwa wateja wetu wanaotuunga mkono tumekuwa tukifanya promosheni mbalimbali zenye lengo la kuleta furaha na kubadilisha maisha yao kupitia Coca-Cola na promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ tunayoizindua leo. Kwa kunywa soda aina yoyote inayozalishwa na kampuni ya Coca-Cola wataweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, bodabado, televisheni aina ya SONY LED zenye inchi 32, T-shirts , kofia na soda za bure.” Alisema Kisusi. Alisema ili mteja kujishindia zawadi atabandua.

  Iambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 na zaidi ya shilingi milioni 400/- zimetengwa kwa ajili ya kushindaniwa na wateja, ambapo kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele.

   Kisusi aliongeza kuwa pia zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilizvyo zawadi kubwa. “Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia promosheni hii ili waendelee kuburudika na soda zinazotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola sambamba na kunufaika kwa zawadi za kuleta furaha na kuboresha maisha yao, familia zao na wapendwa wao.”

   Kuhusu jinsi ya kupata zawadi alisema kuwa zawadi zote kwa washindi zitatolewa bila urasimu wa aina yoyote kuanzia kwenye maduka ya rejareja, mawakala maalumu wa kusambaza vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola na kwenye kiwanda cha Nyanza Bottlers. Soda za kampuni ya Coca-Cola ambazo zitakuwa na zawadi kwenye ganda la vizibo ni Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida.

  0 0


  0 0

  Mrembo Julitha Kabete (Katikati) mara baada ya kushinda taji la miss Ilala mwaka jana.

  Mrembo Julitha kabete kuiwakilisha Tanzania Miss World 2017 China
  Na Mwandishi wetu
  Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited ambayo inaandaa  mashindano ya urembo ya Miss Tanzania imemteua Julitha Kokumanya Kabete kuwaikilisha Tanzania katka mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika Sanya, nchini China mwezi ujao.

  Afisa Habari wa Lino International Agency Limited, Hidan Ricco amesema kuwa tayari jina la mrembo huyo limekwishwa wasilishwa kwa waandaaji wa mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika  Novemba 18, kwenye ukumbi wa Crown of Beauty Theatre.

  Ricco amesema kuwa  mrembo huyo ambaye ni ambaye ni mshindi wa shindano la Miss Dar Centre,  Miss Ilala na mshindi wa tano wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka jana,  kwa sasa yupo katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mashindano hayo.

  Alisema kuwa uteuzi wa Mrembo Julitha Kabete umezingatia uzoefu wa mashindano ya urembo alionao, uwezo wake katika Tasnia ya urembo, uelewa wa vivutio vya utalii na raslimali tulizonazo hapa nchini, pamoja na nidhamu ya hali ya juu aliyonayo mrembo huyu tangu mwanzo anashiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania katika ngazi ya Kitongoji, Mkoa, Kanda hadi Fainali za Taifa kwa mwaka 2016.

  “Julitha  pia alipata fursa ya kushiriki mashindano ya urembo ya Afrika 2016 (Miss Afrika 2016) yaliyofanyika nchini Nigeria na alituwakilisha vizuri tu, na hivyo kupata uzoefu wa kutosha, jambo ambalo pia litaongeza uwezo wake wa kutuwakilisha vema katika Mashindano ya urembo ya Dunia 2017,” alisema Ricco.

  Mashindano ya Miss Tanzania yanayoendelea katika sehemu mbalimbali ambapo fainali zake zitafanyika hapo baadaye.

  Alisema kuwa mshindi wa mwaka huu atawakilisha nchi yetu katika mashindano ya urembo ya Dunia hapo mwakani 2018, hivyo kupata muda wa kutosha wa matayarisho.

  “Hii sio mara ya kwanza kwa mrembo wa Taifa wa mwaka huu kuwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Dunia mwaka unaofuata, mwaka 2012 Miss Tanzania Brigitte Alfred aliwakilisha nchi yetu katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2013, Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka 2014,” alisema Ricco.

  Mrembo pia atakabidhiwa Bendera ya Taifa na Kiongozi wa Serikali ambaye tutamtambulisha hapo baadae.

  0 0

   Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga kwenye Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
   Mkurugenzi wa Bw. Mashtaka Biswalo Mganga akifungua Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
   Mkurugenzi wa Mashtaka Biswalo Mganga (wa nne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo).
   Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mashtaka katika Mafunzo ya Uelimishaji kuhusu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  kwa Mawakii wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Saaam, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofayika mkoani Marogoro jana (Leo). (Picha zote na Mpiga picha wetu)

  Na Sebera Fugence – Afisa Uhusiano Mwandamizi (WCF)Morogoro.
  IMEELEZWA kuwa waajiri ambao hawajisajii na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Biswalo Mganga katika mafunzo ya uelemishaji wa Mawakili wa Serikali wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yaliyofanyika Mkoani Morogoro jana. (leo).

  Mheshimiwa Mganga alisema   hatua za kisheria zitachukuliwa kwa waajiri watakaobainika kutenda makosa mengine yakiwemo ya kutowasilisha michango katika Mfuko kwa wakati.

  0 0


  0 0

  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.
  Wataalamu wa Kilimo, Mifugo na Mipango Miji katika Halmashauri ya Itigi na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao Cha kazicha namna ya kuboresha kilimo, Ufugaji na Mipango Miji.
  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji.

  Na Mathias Canal, Singida
  Wataalamu wa Kilimo wametakiwa kuwaunganisha wakulima na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo.

  Akizungumzia katika kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Ufugaji na Mipango miji Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa pamoja na wananchi kujituma katika uzalishaji wa mazao ya chakula na kilimo lakini changamoto Ni kubwa ya namna ya kuongeza ufanisi katika masoko.

  Alisema kuwa endapo wakulima wataunganishwa na Benki ya Kilimo itakuwa Ni njia pekee ya kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akimsikiliza Kmamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya, leo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi alipowasili mkoa wa Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoa wa Mtwara, mara baada ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake. IGP Sirro, yupo mkani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Jairo akiongea machache kabla kumkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa tatu kushoto) kufungua semina ya siku mbili ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. Kutoka (kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi, Rasilimali watu, Dkt. Amos Ibrahim, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Maswala ya Ufundi, Michael Muhoja na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akiongea na wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. Kutoka (kulia) ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi, Taalum, Utafiti na Ushauri, Dkt. Lewis Isemwi, Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Isaya Jairo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo na Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Maswala ya Ufundi, Michael Muhoja. 
  Sehemu ya wahasibu na wakaguzi wa Taasisi za umma wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati wa ufunguzi semina ya siku mbili iliyoanza Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2017. 


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku tabia ya baadhi ya viongozi katika maeneo mbalimbali nchini kuwakamata na kuwaweka ndani watumishi wakiwemo wauguzi bila ya kufuata taratibu.

  Pia amewataka wauguzi nchini kufanya kazi kwa weledi, uaminifu pamoja na kufuata maadili ya taaluma yao kwa kuwa maisha ya wagonjwa yako chini yao.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 04, 2017) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 45 wa Chama cha Wauguzi Tanzania, mkoani Lindi.

  “Naagiza viongozi wote kufuata na kuzingatia sheria. Kama kuna makosa ya kitaaluma, Mabaraza husika yashughulikie jambo hilo na ni marufuku kuwaweka ndani watumishi kwa tuhuma za kitaaluma.”Amesema kwamba katika sekta ya afya bila wauguzi ambao ni kundi kubwa kati ya Wanataaluma wa Afya, Serikali haitaweza kutekeleza ipasavyo mikakati mbalimbali iliyopangwa kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo.

  Katia hatua nyingine Waziri Mkuu amewaasa wauguzi wote nchini kuhakikisha wanazingatia kiapo cha maadili ya kazi yao na kwamba Serikali haitamvumilia yeyote atakae bainika kwenda kinyume.“Nanyi Wauguzi mnao wajibu wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia kiapo na miiko ya taaluma yenu. Tunazo taarifa kuhusu baadhi ya Wauguzi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa, kuomba rushwa na wengine kujihusisha na vitendo vya wizi wa dawa.”

  Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha afya za Watanzania wote zinaimarika ili kuendana na kasi ya utendaji kazi wa Serikali ya kuinua uchumi na kufikia wa kiwango cha kati, hivyo ni lazima watoe huduma bora kwa wananchi.Pia amewaomba waunge mkono kwa nguvu zote jitihada za Serikali katika kuhakikisha miundombinu na vifaa vyote havihujumiwi na watu wachache ili viwe msaada mkubwa hususani kwa akina mama wajawazito ili wajifungue salama.

  Akizungumzia kuhusu upungufu wa wauguzi nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo Wauguzi na Wakunga na kuwapanga katika maeneo yenye upungufu zaidi.
  Awali, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamis Kigwangalla alisema baadhi ya viongozi katika maeneo mbalimbali wamekuwa wakiwakamata na kuwachukulia hatua watumishi wa Sekta ya Afya bila ya kufuata taratibu, jambo ambalo si sahihi.

  Mkutano huo umehudhuriwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Kigwangalla, Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania Bw. Paul Magesa, Mbunge wa Lindi Mjini Bw. Hassan Kaunje, Mbunge wa Kuteuliwa Mama Salma Kikwete(MB) Viti maalum.Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Gustav Moyo, Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bw. Stewart Mbelwa.

  Wengine ni Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Abdallah, Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Uuguzi Bw. Ndementria Vermund, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania Dkt. Obadia Nyongolena wawakilishi wa wauguzi kutoka mikoa yote nchini.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  JUMATANO, OKTOBA 04, 2017.

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akisoma Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) ambao umeanza leo Oktoba 4,2017 Mkoani Lindi. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mwenezi msaidizi wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) Johari Yusuf, baada ya ufunguzi wa Mkutano wa chama cha wauguzi leo Oktoba 4,2017 Mkoani Lindi.katikati  ni mweye beji shigoni ni Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania Bwana Poul Magesa .kulia kwa katibu mwenezi ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania Sebastian Luziga.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya uchapishaji wa Jarida la “TADA Newsletter” Katibu Mtendaji wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Asia Tanzania (TADA) Dinesh Vaishnav leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimwelezea jambo Katibu Mtendaji wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Asia Tanzania (TADA) Dinesh Vaishnav mara baada ya kumkabidhi leseni ya uchapishaji wa Jarida la “TADA Newsletter” leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mtendaji wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Asia Tanzania (TADA) Dinesh Vaishnav akifurahia Jarida la Nchi Yetu linalotolewa na Idara ya Habari (MAELEZO) alipotembelea Ofisi za Idara hiyo leo kwa ajili ya kupokea Leseni ya uchapishaji wa Jarida la “TADA Newsletter”. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.


  Picha na: Frank Shija – MAELEZO

  0 0


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani amesema Wafugaji Nyuki wanayo fursa kubwa ya kujikita katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vya kuchakata, kufungasha na kuongeza thamani mazao ya nyuki na kutengeneza vipodozi kutokana na mazao ya nyuki.

  Mhandisi Makani ameyasema hayo jana wakati alipozungumza na wafugaji wa nyuki na wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, chini ya Kauli Mbiu “UFUGAJI NYUKI KIBIASHARA UNACHANGIA KATIKA UKUAJI WA VIWANDA”

  Amesema Mazao ya Nyuki ni malighafi ya Viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya vyakula vinavyotumia asali, viwanda vya dawa na vipodozi na viwanda vya utengenezaji vinavyotumia nta katika kuzalisha maturubai, dawa za kung’arisha viatu na bidhaa nyingine, hivyo wafugaji wanao wajibu wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki na ujuzi wa kuyaweka katika ubora na kuyaongezea thamani.

  Aidha, ametoa wito kwa wafugaji wa nyuki kuungana katika vikundi vyenye usajili ili waweze kuzalisha asali kwa wingi na yenye kufanana, kwa kuwa ikiwa watazalisha kila mmoja kwa utaratibu wake, asali hiyo haiwezi kuchanganywa na itakuwa na ubora na sifa tofauti, lakini ikiwa wataungana na kuzalisha asali nyingi kwa pamoja wakaipima kwa viwango vya ubora unaotakiwa wataweza kupata soko.

  Sanjali na hilo amesema Serikali itahakikisha inawaunganisha wafugaji nyuki na walaji wa ndani na nje na akabainisha kuwa kwa miaka zaidi ya 11 imekuwa na ushirikiano na soko la Ulaya ambapo sampuli za asali kutoka maeneo mbalimbali zimepelekwa Ulaya na taarifa za maabara zinathibitisha kuwa asali ya Tanzania ni salama kwa afya ya mlaji.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)(kulia)akitundika Mzinga katika Banda la Nyuki la Kikundi cha Wafugaji Nyuki cha Malela wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani (Mb)akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itilima(hawapo pichani ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.
  Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akizungumza na wananchi wa wilayani hiyo (hawapo pichani ) wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Eng. Ramo Makani(Mb) akizindua Manzuki (Shamba la Miti lenye Mizinga ya Nyuki) ya Kikundi cha Wafugaji nyuki cha Malela Wilayani Itilima wakati wa Maadhimisho ya siku ya kutundika Mizinga ya Nyuki Kitaifa yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Isengwa Wilayani humo katika Mkoa Simiyu.  0 0

  Ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajili nchini, wanafunzi wametakiwa kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu ambayo yatawajengea uwezo wa kupata ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda. 

  Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi ya Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, mhandisi Nada Narya aliyasema hayo kwenye mahafali ya pili ya darasa la saba na ya nane ya kumalizika elimu ya awali ya shule hiyo.

   Mhandisi Narya alisema shule hiyo imewaanda ipasavyo wanafunzi wa shule hiyo kupenda masomo ya sayansi na hesabu ili kukabiliana na tatizo la ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hivyo wanafunzi wengine nchini wapende masomo hayo. 

  Alisema hivi sasa soko la ajira ni dogo na ili kuondokana na hali hiyo inawapasa wanafunzi kuyapenda masomo sayansi na hesabu kwa lengo la kujiandaa kwa nguvu zote katika kuhakikisha wanajipanga ipasavyo hivi sasa ili baadae wachangamkia fursa ya ajili kupitia Tanzania ya viwanda. 

  "Sisi kama Deira tumeanza kuwaandaa wanafunzi wetu wapende masomo ya sayansi na hesabu ili baadaye waweze kuendesha maisha yao kwenye soko la ajira kwani wataalamu mbalimbali watatokea hapa shuleni kwetu," alisema mhandisi Narya. 
   Ofisa elimu msingi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, Doroth Mwandila akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium Vannesa Nada, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (kushoto)  ni Mkurugenzi wa shule hiyo mhandisi Nada Narya.
  Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium ya mjini Babati Mkoani Manyara, wakionyesha mchezo wa kareti wakati wa mahafali yao yaliyofanyika shuleni kwao.


  0 0

  Wafanyabiashara wadogo na wakati wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiinua kiuchumi kwa kuchukua mkopo inayotolewa na benki ya CRDB ndani ya siku saba. 

  Akizungumza kwenye sherehe za ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja duniani, meneja wa CRDB tawi la Babati Ronald Paul alisema mkopo huo wa miezi mitatu utawanyanyua kiuchumi wajasiriamali hao. Paul alisema wajasiriamali hao wachangakie fursa hiyo ambayo imeanzishwa wiki hii ya huduma kwa wateja dunia, ambapo pia itaendelea kutolewa na benki hiyo kwa siku zote zinazoendelea kuwepo. 

  Alisema wamejipanga kuboresha zaidi huduma kwa wateja wa benki yao, hivyo wajasiriamali wa mjini Babati, wilaya za Kiteto, Mbulu, Simanjiro, Hanang' na miji midogo ya Mirerani, Magugu, Galapo, Haydom na Dareda, wachangakie fursa hiyo.

  Alisema wiki ya huduma kwa wateja dunia, itafikia kileleni jumamosi ijayo mjini Babati, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera ambaye atazungumza na wadau wa benki ya CRDB."Siku hiyo kutakuwa na shamrashamra za kutosha kwani wadau wenye ushawishi kwa jamii watakuwepo kwenye tawi hili la CRDB Babati, ambapo watatueleza mambo mawili matatu yatakayowanufaisha wajasiriamali wetu," alisema Paul. 

  Aliwaahidi wateja wa benki hiyo kuwa huduma zimeboreshwa zaidi hivyo wafike na kujionea wenyewe kwa kuweka fedha, kufungua akaunti au kuchukua mikopo, kwani hata riba zao ni nafuu tofauti na taasisi nyingine za fedha. Mmoja kati ya wajasiriamali wa mji mdogo wa Magugu wilayani Babati, Elizabeth Seluhinga alisema huu ndiyo wakati wa kuchangamkia fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kiuchumi kupitia mikopo inayotolewa na benki hiyo. 

  Seluhinga alisema yeye ni mjasiriamali wa nyanya kwenye mji mdogo wa Magugu na anatarajia kuchukua mkopo kwenye benki ya CRDB ambapo ameambiwa ndani ya siku saba atakuwa ameshapatiwa fedha za mkopo. 

  Alisema wajasiriamali wasiogope kuchukua mikopo ili kuboresha biashara zao kwani hata wafanyabiashara maarufu nchini, wengi wao wamenyanyuka kimaisha kwa kuchukua mikopo na siyo vinginevyo. 
   Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, wakiwa kwenye viwanja vya benki yao tayari kabisa kwa kutoa huduma kwa wateja wao kwenye wiki ya huduma kwa wateja dunia ambayo itafikia kilele jumamosi ijayo.
  Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Ronald Paul, akizungumza jana na waandishi wa habari juu ya wiki ya huduma kwa wateja dunia ambayo itafikia kilele jumamosi Ijayo. 


  0 0


  0 0

  Jumla ya wananchi 600 wameshiriki katika zoezi la upimaji wa magonjwa ya Moyo ambao ulienda sambamba na utoaji wa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani iliyofanyika tarehe 29/09/2017 katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

  Wananchi walioshiriki katika zoezi hilo walipimwa urefu, uzito, shinikizo la damu (BP), sukari na kupewa ushauri. Asilimia 80 ya wananchi waliopimwa siku hiyo walikutwa na matatizo ya shinikizo la juu la damu na wengine walikutwa na matatizo mengine ya Moyo.

  Aidha wagonjwa 400 waliokutwa na matatizo ya moyo walipewa dawa na baadhi yao walianzishiwa kliniki ili wataalamu wetu waweze kufuatilia maendeleo ya afya zao kwa ukaribu na kuweza kupata huduma ya matibabu kwa ukaribu zaidi.

  Kwa namna ya kipekee tunazishukuru sana kampuni zinazotengeneza dawa za binadamu za Tata Africa Holdings (T) LTD, Reddy’s, na Phillips ambazo ziligawa dawa bure kwa wananchi waliokutwa na matatizo ya Moyo.

  Tunawaomba wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la na hivyo kuanza matibabu mapema. Asilimia kubwa ya wagonjwa tunaowapokea katika kliniki zetu baada ya kuwafanyiwa vipimo tunawakuta mioyo yao haiko katika hali nzuri. Hii inaonyesha kuwa wana matatizo ya Moyo pasipo kujifahamu.


  Imetolewa na :

  Kitengo cha Uhusiano na Masoko
  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

  04/10/2017

older | 1 | .... | 1943 | 1944 | (Page 1945) | 1946 | 1947 | .... | 3272 | newer