Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAFANYA VIZURI KATIKA NYANJA YA UWEKEZAJI - RIPOTI YA UWEKEZAJI DUNIANI YA MWAKA 2013 YASEMA

$
0
0
IMG_9901
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Uwekezaji ya Dunia ya Mwaka 2013 ambayo imejikita kiundani zaidi kuangalia muunganiko wa Mahusiano ya Kibiashara na Uwekezaji Duniani.
Bi. Kairuki amesema Tanzania imeweza kupata Uwekezaji mara dufu katika maeneo ya Mafuta na Utafiti wa Gesi Asilia katika kusukuma pato la taifa kuongeza ajira na kupambana na umaskini.
Ameongeza Muunganiko wa Biashara na uwekezaji umepata mwamko mkubwa sana kutoka kwenye makampuni makubwa duniani na umeleta fursa kwa nchi maskini na zinazoendelea kama Tanzania kuwa na uhusiano mzuri kiuchumi na nchi zilizoendelea. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO). Picha na Zainul Mzige.
IMG_9892
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali na mabalozi wakifuatilia uzinduzi rasmi wa ripoti hiyo ya Uwekezaji Duniani.
IMG_9876
Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) Manuela TORTORA akizungumzia umuhimu wa sera za nchi za Uwekezaji kuhakikisha zinatoa fursa ya ajira na kupunguza umaskini katika nchini zinazoendelea.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

UGANDA CRANES KUTUA DAR KESHO, KUUMANA NA TAIFA STARS JUMAMOSI

$
0
0
Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Julai 11 mwaka huu) tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
The Cranes itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda ambapo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo. 
Waamuzi wa mechi hiyo ambao wanatoka Burundi nao watawasili kesho saa 9.35 kwa ndege ya Kenya Airways. Naye Kamishna wa mechi hiyo Tesfaye Gebreyesus kutoka Eritrea atatua nchini keshokutwa alfajiri kwa ndege ya EgyptAir. 
Maofisa wote hao wa mechi hiyo watafikia hoteli ya New Africa. Mkutano wa maandalizi ya mechi utafanyika Ijumaa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa, na utakuwa chini ya Gebreyesus.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Introducing DIGNER with her hit single 'Niite'

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MABUNGE WA KUJADILI SERA ZA MISITU BARANI AFRIKA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mabunge wa kujadili Sera za Misitu Barani AFrika, uliofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel (wa pili kushoto) na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela (kulia) wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo kupitia Screen kwa njia ya TV.
Baadhi ya Wabunge wakiwa katika chumba cha mkutano huo, kutoka (kushoto) ni Mbunge wa Kahama James Lembeli, Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wakiwa katika mkutano huo jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (katikati) na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela, baada ya kufungua rasmi mkutano huo jana jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge waliohudhuria Mkutano Mabunge wa kujadili Sera na changamoto za Misitu Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana.

NEWS UPDATES: MEYA WA DC KUONGOZA MAELFU KUMUAGA MAREHEMU SYKES, CHUO CHAFUNGUA OMAR SCHOLARSHIP FUND

$
0
0

Na Swahili TV, Washington DC
Chuo Kikuu cha Howard  alichokuwa akisoma mtanzania aliyeuawa  mjini Washington Dc,  marehemu Omary Adam Sykes kinataraji kuuaga mwili wake  leo jioni, viongozi mbalimbali akiwemo meya wa jiji la Washington DC Bwana Gray nao wanatarajiwa kuhudhuria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia Swahili TV shughuli za kumuaga  marehemu zitafanyika katika ukumbi wa Andrew Rankin Memorial Chapel ulio katika kona ya  6th Street  na Howard place na kufuatiwa  sherehe za kukumbuka ya  maisha yake zitakazofanyika katika ukum bi wa Blackburn ambao pia uko katika chuo hicho.
Shughuli za kuuaga mwili huo zimepangwa kuanza saa 12 jioni (takriban muda  wa masaa mawili na nusu toka sasa kwa saa za Tanzania), ambazo habari hizo zinasema Mstahiki meya  Vicent condol Gray atakuwa muongeaji mkuu akishirikia na rais wa chuo hicho  Profesa Sidney A. Ribeau. Sherehe hizi pia zitashirikisha familia ya marehemu Omar ambaye baba yake mzazi mze Adam Sykes  na baba yake mkubwa waliingia jana wakitokea nchini Tanzania.
Si jambo la kawaida kwa Meya wa jiji kubwa la Washington  kuhudhuria sherehe za kuuga mwili, wachambuzi wa mambo ya siasa za Washington Dc  wanasema  hali  hiyo huenda inatokana na umaarufu wa chuo hicho na mstuko mkubwa wa mauaji ya mwanafunzi  huyo ambayo yamelistua jiji la Washington DC,  ambalo licha ya kuwa na matukio ya mauaji ya hapa na pale  lakini eneo la chuo hicho limekuwa salama kwa miaka mingi.
Taarifa ya chuo kwa Swahili TV inasema,Uongozi wa chuo uliamua kuanzisha mfuko maalum utakaosaidia wananchi mbalimbali wasio na uwezo kulipia ada zao, mfuko utatambulika kama Omar Scholarship Fund na tayari watu kadhaa wameshaanza kuchangia.Taarifa za namna ya sifa na uwasilisha wa maombi zitatangazwa baadaye.

Swahili TV itakuwepo katika shughuli za kuuaga mwili ili kukuletea habari za kina na uhakika.

Stay tuned for Exclusive story at www. swahilitv.blogspot.com

ZG FILM "LOVERS ISLAND" SCOOPS THREE AWARDS AT ZIFF (ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL).

$
0
0
Fashion week Zanzibar Founders Film Lovers Island scoops three awards at Zanzibar International Film Festival for Best ZUKU Swahili film, The awards were awarded for Best Acting in Swahili Film, Best Director in Swahili Film and Best Swahili Feature film. Thats the great achievement and congrats to Javed Jafferji for raising the standards of films in Tanzania.
ZG Films , led by renowned photographer and filmmaker Javed Jafferji, aims to not only meet and surpass the current standard of filmmaking in Tanzania, but to raise the bar to such an extent that it re-invents the Tanzanian movie scene and ushers in a new era of worldclass film production in the country. As evidence of achieving this goal, ZG Films presented a rare double billing at this year’s Zanzibar International Film Festival. With Journey to the State House: The Life of Seif Shariff Hamad and Glamour: The Reality Behind Dreams, ZG Films is presenting itself as the leader in Tanzanian film production. Now ZG Films is preparing to release it’s second feature film of 2011.

TANAPA NA WADAU WAFANIKIWA KUDHIBITI MOTO KILIMANJARO

$
0
0
Shirika la Hifadhi za Taifa linashukuru ushirikiano ilioupata na kufanikiwa kudhibiti moto kwa asilimia 100 hadi sasa uliotokea Mlima Kilimanjaro siku ya Jumapili tarehe 7.7.2013. 

Juhudi mbalimbali zilizofanywa na wananchi pamoja na uongozi wa serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa Mkoa Leonidas Gama, zimeweza kudhibiti na kumaliza moto huo uliodumu kwa siku nne sasa.

Leo tarehe 10.7.2013 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alitembelea eneo la Horombo ambalo ni urefu wa mita 3,700 juu ya usawa wa bahari na kujionea jinsi moto ulivyounguza maeneo mbalimbali ya hifadhi.

Mkuu wa Mkoa akiwa eneo la tukio alitoa agizo kwa viongozi wa wilaya za Moshi na Rombo kushirikiana na TANAPA ili kuweza kubaini wale wote waliohusika na uharibifu huu pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha kuwa vitendo kama hivi havijitokezi mara kwa mara.

Taarifa hii inalenga pia kuujulisha umma kuwa shughuli za utalii zinaendelea vizurikama kawaida na hazikuweza kuathirika na moto huu kama ambavyo tumeshatoa katika taarifa zetu za awali kuwa maeneo wanayopita watalii hayakuathirika na moto huu.

Imetolewa na Idara ya Uhusiano
Hifadhi za Taifa Tanzania
10.07.2013

BREKING NYUUUZZZZZZ: MAMA MZAZI WA PROFESA J AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNGONGWA NA GARI USIKU HUU HUKO MBEZI JUU, DAR ES SALAAM

$
0
0
Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake.  Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'

HABARI ZILIZOPOKEWA USIKU HUU NI KWAMBA MAMA YAKE MZAZI MSANII MAARUFU WA MUZIKI NCHINI, JOSEPH HAULE A.KA. 'PROFESA J' AMEFARIKI DUNIA USIKU HUU BAADA YA KUGONGWA NA GARI  MAENEO YA MBEZI JUU, JIJINI DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA ANAISHI NA MWANAE.

HABARI ZINASEMA MAREHEMU, BI. ROSEMARY MAJANJARA HAULE, ALIGONGWA NA GARI AKIWA ANAVUKA BARABARA KUELEKEA DUKANI KIASI CHA SAA MBILI USIKU, NA KWAMBA BAADA YA KUGONGWA WASAMARIA WEMA WALIMKIBIZA HOSPITALINI TUMBI KWA KUTUMIA BAJAJI AMBAKO ALIFARIKI DUNIA. TAARIFA ZA AWALI HAZIJATAJA AINA YA GARI NA KAMA BAADA YA AJALI HIYO LILISIMAMA AU LA.

PROFESA J AMETHIBITISHA  HILO MUDA MFUPI ULIOPITA, NA KUSEMA INAMUIA VIGUMU KUAMINI IMETOKEA KWANI ANASEMA MAREHEMU MNAMO SAA MBILI HIVI ALIMPIGIA SIMU NA KUMWELEZA KUWA AMEPATA AJALI NA KWAMBA WAKATI HUO YUKO KITUO CHA POLISI, BILA SHAKA KUPATA FOMU YA PF 3 YA KUMUWEZESHA KWENDA KUTIBIWA HOSPITALI.

"MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NA GARI....NJOO NIKO POLISI NAANDIKISHA....MWANANGU NAKUFA....ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU.

ANASEMA WAKATI ANAPIGIWA SIMU NA MAMA YAKE YEYE ALIKUWA KATIKA MGAHAWA WA NYUMBANI LOUNGE, NAMANGA, DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA KATIKA KIKAO NA LADY JAY DEE NA MUMEWE GADNA G. HABASH, AMBAO BAADA YA TAARIFA HIYO WALIMSINDIKIZA HADI HOSPITALI YA TUMBI.

"TULIPOFIKA HOSPITALI SIKUAMINI KUONA BADALA YA KUPELEKWA WODINI AMBAKO NILIDHANI MAMA ATAKUWA AMELAZWA NIKAPELEKWA CHUMBA CHA MAITI AMBAKO NILIMKUTA MAMA AKIWA MAREHEMU", ALISEMA PROFESA J KWA MAJONZI.

GLOBU YA JAMII INATOA MKONO WA POLE KWA PROFESA J KWA MSIBA HUU MZITO NA WA KUSIKITISHA. TUNAMWOMBA MOLA AMPE NGUVU YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. 

TUTAENDELEA KUWAPASHA KINACHOJIRI KADRI HABARI  ZAIDI ZITAPOPATIKANA. KWA SASA PROFESA J NA WADAU WENGINE WAKO NYUMBANI KWAKE MBEZI JUU.

















swali la Mdau kuhusu Mawe Meupe.....

$
0
0
Ankal salaam.

Naomba uniulizie wadau wako, hivi haya mawe meupe yanayoonekana kwa wingi sana pembezoni mwa kipande cha barabara kati ya Segera na Mkata, yana matumizi gani???

 Nauliza hivi kwa kuwa wahusika walianza kidogo kidogo kuyakusanya kwa kutumia "visalfeti" au malboro na kuuza kwa waliojua matumizi yake, lakini kwa sasa ukipita utakuta yamerundikwa kwa kiasi kikubwa sana na zipo semi-trela zinapakia kwa wingi.

 Ni mawe mazuri ajabu, meupe na yenye kumetameta wakati jua likiwa kali sana. Jamani mwenye kujua matumizi yake tafadhali atujuze ili tuyachangamkie mapema kabla "wawekezaji" toka urusi au uchina hawajayavamia.

 Wkend njema.
 Mdau

MOTO MLIMA KILIMANJARO UMEDHIBITIWA

$
0
0
Askari mgambo wakiwa katika eneo la kifunika mlima Kilimanjaro wakiandaa chakula kwa ajili ya watu waliojitokeza kuzima moto katika eneo hilo.
Kundi la asakari mgambo lililopo katika eneo la Kifunika mara baada ya kufanikisha kuzima moto katika eneo hilo.
Sehemu ya eneo lililo athirika na moto mkubwa katika mlima Kilimanjaro.
Maeneo yaliyo athirika na moto mlima kilimanjaro.
Mwakilishi wa globu ya jamii akizungumza na mmoja wa wapagazi katika mlima Kilimanjaro Mathayo Kunkwa kuhusiana na tukio la moto uliozuka mlimani hapo.

Picha na habari na Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii,  Moshi

JUHUDI za makundi mbalimbali yaliyokuwa yakishiriki katika zoezi la moto uliozuka mapema mwishoni mwa wiki iliyopita na kuteketeza zaidi ya ekari 40 katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro zimefanikiwa baada ya kuudhibiti moto huo sasa kwa asilimia 99%.

Hadi kufikia Juzi makundi hayo wakiwemo askari kutoka chuo cha taaluma ya Polisi cha Moshi (MPA),askari Mgambo kutoka wilaya za Rombo ,Moshi vijijini,Mwanga na Same wakiwemo maafisa kutoka hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) walikuwa wamefanikiwa kuzima moto huo huku kukiwa kumebakia na eneo dogo katika sehemu ya Kifunika.

Kwa takribani siku tano sasa eneo la mlima huo mrefu barani Afrika lilikuwa likiteketea kwa moto huku chanzo chake kikidaiwa kuwa ni shughuli za urinaji haramu wa asali uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wananchi katika hifadhi hiyo.

Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)Erastus Lufunguro katika taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alisema hifadhi ya mlima huo inaendeleza doria kudhibiti visiki vinavyotoa moshi ili usiwake tena.

Aidha mhifadhi Lufunguro alirejea kauli yake kwamba tukio la moto huo ulioteketeza zaidi ya Hekari 40 katika hifadhi yam lima huo,haujaathiri shughuli za watalii kupanda na kushuka katika mlima huo wenye urefu wa Futi 5895 kutoka usawa wa Bahari.

alisema pamoja na kuzimwa kwa moto huo,bado kambi za watu zaidi ya 400 zilizoundwa katika wilaya za Rombo na Moshi kuukabili moto huo,zinaendelea kukagua maeneo yote yaliyokuwa na moto na sasa yanafuka moshi ili kuudhibiti usianze upya.

“Kinachofanyika sasa ni doria za mara kwa mara katika maeneo yote ambayo moto ulikuwa ukiwaka ili kudhibiti iwapo utawaka tena kutokana na upepo mkali katika eneo hilo lililotawaliwa na vichaka na misitu mifupi”alisema Lufunguro.

“Baada ya moto kuripotiwa kuanza katika maeneo ya Amboni, Ushiri, Keryo, Kimori na Shimbi wilayani Rombo mnamo Julai 7, tuliunda kambi tano za Kilema, kifunika, Keryo, Maundi na Ujasiri zenye watu 467 ambao wamefanya kazi kubwa kuuzima moto” aliongeza Lufunguro .

Alisema pamoja na kambi za kuzima moto lakini pia hifadhi hiyo imeweka kambi mbili maalum kwa ajili ya kuhudumia wanaoshiriki zoezi la kuzima moto, ambapo moja ipo eneo la Nanjara wilayani Rombo ambapo ilikuwa na sehemu kubwa ya moto.

Lufunguro alisema kambi nyingine ipo katka eneo la Marangu kwa ajili ya kuhudumia eneo la Kilema juu ambapo zote kwa pamoja zilikuwa na askari mgambo 128 kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro sanjari na askari waliopo mafunzoni katika chuo cha polisi CCP.

Katika hatua nyingie mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Moshi,Ibrahimu Msengi pamoja na viongozi mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa walilazimika kupanda mlima Kilimanjaro hadi kituo cha Horombo kujionea hali halisi ya athari iliyotokana na moto huo.

DKT. SHEIN AKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA MARK SIMMOBDS

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Waziri wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Bw.Mark Simmonds,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Waziri wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Bw.Mark Simmonds,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Waziri wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Bw.Mark Simmonds,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya mazungumzo yao leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}

Mfuko wa Starkey Hearing watoa huduma za kutibu masikio kwa wakazi wa Dar

$
0
0
Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe Tani Austin(kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto Lilian Vincent (leo) jijini Dar es salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe Tani Austin(kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto Malechela Juma (katikati) leo jijini Dar es salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya huduma ya vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
Baadhi ya wakazi na watoto kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa katika foleni ya kupatiwa matibabu ya huduma ya vifaa vya kuwasaidia kusikia kutoka Mfuko wa Starkey Hearing leo jijini Dar es salaam. Mfuko huo umeweka kambi katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo wanatarajia kutoa huduma hiyo bure kwa watu zaidi ya 2000 kwa kipindi cha nne.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Mtanange wa Taifa Stars na Uganda unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa jijini Dar

$
0
0
 Mshambuliaji Machachari wa timu ya Taifa (Taifa Stars),Amri Kiemba (kushoto) akijaribu kutana kuwatoka mabeki wa timu ya Uganda ( The Cranes) katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN),unaochezwa hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Dakika 45 za mchezo zimemalizika hivi punde huku timu zote zikiwa hazijaliona lango la mwenzake.endelea kufuatilia Libeneke la Globu ya Jamii kwa Matukio mbali mbali ya mtanange huu.

TAIFA STARS YAGEUKA KUWA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU,YAPIGWA BAO 1-0 NA UGANDA THE CRANES

$
0
0
 Mshambuliaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars),John Boko (14) akiwa na mpira mbele ya Beki wa timu ya Uganda ( The Cranes) katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN),uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imekubali kipigo cha Bao 1-0 kutoka kwa Uganda.
 John Boko akiondoka na mpira kuelekea langoni mwa timu ya Uganda.
 hapa hapiti mtu .....
 Mrisho Ngassa akitaka kuwatoka Mabeki wa Uganda wakati wa mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN),uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imekubali kipigo cha Bao 1-0 kutoka kwa Uganda.

PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Hasheem Thabit atinga uwanja wa Taifa jijini Dar kushuhudia mechi kati ya Taifa Stars na Uganda Cranes leo

$
0
0

 Mchezaji wa Kimataifa Mtanzania, anayechezea timu ya kikapu ya Oklahoma City Thunder ya Marekani, Hasheem Thabeet akiwapungia mikono wapenzi wa soka wakati wa mechi ya Taifa Stars na timu ya Uganda 'The Cranes'ya kuwania kufuzu michuano ya Afrika ya wachezaji wa ndani (CHAN), kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
 

Mchezaji wa Kimataifa Mtanzania, anayechezea timu ya kikapu ya Oklahoma City Thunder ya Marekani, Hasheem Thabeet akiwasalimia wapenzi wa soka wakati wa mechi ya Taifa Stars na timu ya Uganda 'The Cranes'ya kuwania kufuzu michuano ya Afrika ya wachezaji wa ndani (CHAN), kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo. Uganda Cranes wameshinda bao 1-0

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JWTZ CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI, LEO

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Ofisa Kadet Ngodoke kwa kuibuka mwanafunzi bora wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Ofisa Kadet D.G.L. Wong- Pool toka Visiwa vya Ushelisheli kwa kuibuka mwanafunzi bora wa kigeni wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa katika Chuo cha Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Meza kuu wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

SHEREHE ZA KUTUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WA JESHI CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI JULY 13, 2013

wanafunzi chuo kikuu cha howard wamkumbuka marehemu omar sykes katika swahili tv

Watu wa aina kumi waliosamehewa kufunga Ramadhani

vikosi vilivyozima moto mlima kilimanjaro vyapongezwa

$
0
0
 Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na wafanyakazi wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro.
  Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na viongozi wa askari mgambo
 Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu akizungumza na viongozi wa askari mgambo ,kushoto kwake ni mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro.
Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images